Tabia ya Sekretarieti ya Ajira kupanga usaili Jumamosi ni kama ubaguzi kwa Wasabato

Unajisumbua kuleta hoja hii hapa, majibu ya watu wanaosnesha hakuna anaejali sana sana wanajibu kwa kejeli, lakini siyo haki kuwatendea hivyo kutokana imani yao. Serikali inapaswa kuheshimu imani ya kila Mtanzania hata wanaoamini usabato ni watanzania kama wengine na wanahaki kama nyie mnao kejeli hapa. Usaili ni sehemu ya kazi hivyo ni bora ufanyika siku za kazi na zisiwe za ibada za watu na hata ijumaa hakuna haja ya kufanya hivyo kuna jumatatu mpaka alhamis haiingiliani na imani ya mtu. Kazi inayofanyika ni sehemu ya kazi na kuwaumizia wengine siyo haki.
Mimi nakushauri iwe wewe ushauri hizo interview zifanyike siku ya ijumaa, kwa maana hawa Waislamu hawalalamiki kwa nini ijumaa ni siku ya majumuhisho ya ibada zao za wiki nzima lakini na ni siku ya kazi pia ...?

Lakini pia hilo wazo wewe sio mtu wa kwanza, nakumbuka Magufuli alibadilisha siku ya uchaguzi kutoka siku ya jumapili ambayo ulikuwa unafanyika kila mwaka wa uchaguzi kabla ya yeye kuwa Rais, mwaka 2020 akasema uchaguzi ufanyike siku ya jumatano ili jumapili wakristo waende kanisani.

Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, BW Mkapa hata Dr. Kikwete hili hawakuliona, na watu walikaa kimya na kumpongeza Dr. Magufuli kwa alichokifanya cha kubadili siku ya uchaguzi, ila wasiwasi jambo kama lile lingefanywa na mtu kama Kikwete la kwasema siku ya ijumaa ni siku kuu ya ibada kwa Waislamu, watu waende makazini hadi saa 11 : 45 am kisha waende misikitini na saa 01 : 15 pm warudi maofisini ingekuwa ajenda kubwa sana sana.
 
Understanding yako iko chini sana siwezi hata ku argue na wewe tena! just think out side the box, hivi muislam safi anaweza kula nguruwe eti kwasababu wakatoliki na waluteli wanakula? usitoe majibu mepesi hivyo wakati kuna watu wengine wanaumia let us be realistic tuache chuki na majibu ya dharau kwa imani za watu tukijidai wataalamu sana wa hoja nyepesi
Yani understanding yangu iwe ndogo kwa hoja yako yako ya jumamosi ...
 
Yani understanding yangu iwe ndogo kwa hoja yako yako ya jumamosi ...
No the way ulivyo argue ndiyo nimekudharau kabisaaaa siyo sababu ya jumamosi na hata sasa huelewi nilicho andika you are in a very sorry condition🤣🤣 kweli wewe ni Mr. Njaa, it seems ni njaa ya uelewa wa maswala
 
Mtoa mada umeleta hoja nzuri sana lakini sasa shida ipo kwenye kuiweka kwenye uhalisia, waliondaa usaili uwe jmosi wana sababu zao mfao suala Zima la maslai coz j3 adi ijimaa watakwambia kuna ugumu wa kuweka usaili watasema jmoc kwanza suala zima la maslai wanapata overtime kingine kumbi nyingi ni za vyuoni so kupata nafasi siku za kawaida coz wanafunzi wanatumia mda wingi kwa iyo wakaona jmc imekaa vyema kwa zoezi kwa ujumla alafu kitu kingine kwa wasailiwa sasa asilimia kubwa wengi wanaofanya interview ni wafanyakz so wengi upenda siku ya jmoc coz inakuwa rahisi ata kwa kusafir kwa iyo kuweka siku tofaut na jmoc sjui embu ngoja tuone labda utumishi wataona watafanyia kazi
 
Unajisumbua kuleta hoja hii hapa, majibu ya watu wanaosnesha hakuna anaejali sana sana wanajibu kwa kejeli, lakini siyo haki kuwatendea hivyo kutokana imani yao. Serikali inapaswa kuheshimu imani ya kila Mtanzania hata wanaoamini usabato ni watanzania kama wengine na wanahaki kama nyie mnao kejeli hapa. Usaili ni sehemu ya kazi hivyo ni bora ufanyika siku za kazi na zisiwe za ibada za watu na hata ijumaa hakuna haja ya kufanya hivyo kuna jumatatu mpaka alhamis haiingiliani na imani ya mtu. Kazi inayofanyika ni sehemu ya kazi na kuwaumizia wengine siyo haki.
Utumishi hawana venue binafsi kwa ajili ya kufanyisha watu interview hasa watu wanapokua wengi ndo maana siku za weekend zinatumika maana wanaomba madarasa kutoka sehemu mbalimbali hasa vyuoni ambapo madarasa hutumiwa na wanafunzi Siku za kazi
 
Weekdays watumishi wanakua kwenye majukumu yao ya kiofisi so jmosi ndio siku sahihi
Watumishi wanaoendesha usahili ni kazi yao weekdays na watahiniwa wengi wanaotafuta siyo watumishi
 
Kumezuka tabia ya baadhi ya Waajiri ikiwemo Sekretarieti ya Ajira kupanga usaili siku za Jumamosi ( hususani Usaili wa Mchujo).

Kitendo hiki ni Kinatafsiriwa kama Ubaguzi (Discrimination) kwa waumini wa Kanisa la Waadvetista Wasabato ambao Jumamosi ni siku ya Ibada therefore, by doing so, their opportunity in employment is nullified and impaired. Naomba nieleze kidogo swala ya ubaguzi katika ajira katika tafsiri ya Kisheria kwa ufahamu wangu mdogo nilionao.

Article Na.1 of the Decrimination (Employment and Occupation) Conventions, 1958 which then rectified by Tanzania ni 2002, this practice can be termed as Employment/ occupational Discrimination so “Any distintion, exclusion on preference made on basis of race, sex, colour, religion, political opinion, national extraction or social origin, which has the effect of nullifying or impairing equality of opportunity or treatment in employment or occupation”. Meanwhile, discrimination employment and occupation is not allowed under Section 7 (4) of Employment and Labour Relation Act No.6 /2004 as follows

“No employer shall discriminate, direct or indirectly against an employee in any employment policy or practice or any of the following grounds; colour, nationality, tribe or place of origin, race, natural extraction, social origin, political opinion or region, sex ,gender, pregnancy, marital status or family responsibility, disability, HIV/AIDS, Age or station of Life”

According to Section 7(9) of of Employment and Labour Relation Act No.6 /2004

“An “employment policy or practice “ includes any policy or practice relating to recruitment procedures, advertising and selection criteria appointment and appointment process, job classification and grading, renumeration, employment benefits and terms and conditions of employment, job assignments, the working environment and facilities, training and development, performance evaluation systems, promotion, transfer, demotion, termination of employment and disciplinary measures”

Kwa msingi wa maelezo hayo ya Kisheria, kwa heshima kubwa, naomba Sekretarieti ya Ajira ifikirie upya na kusitisha mara moja tabia ya kupanga usali siku za mapumziko ya mwisho wa juma (Weekends) ikijumuisha Jumamosi ili kuwa na mchakato wa ajira usiokuwa na ubaguzi. Aidha, nawashauri wafanye utafiti kwa njia ya maoni wa sababu zinazofanya baadhi ya Waombaji wa kazi kutohuduria Interview wanaweza kupata sababu nzuri za kuboresha mchakato huo.

Nina imani ombi litaapokelewa ili kuwapa Haki sawa wale ambao Jumamosi ni siku yao rasmi ya Ibada.

Nawasilisha kwa ajili ya maoni na ushauri
JUmamosi ni rahis kupta kumbi mbali mbali za kuendeshea usaili. Katikat ya wiki uite intervuu watu 1000 utapta wapi ukumbi wa dizajn hyo, so kma untafuta Kazi nenda kama untafuta ufalme wa mbingun pekee endelea. Hata mungu anajua Kuwa unatafuta nini.
 
Kwa mtazamo wangu,(naomba nisamehewe Kama nitawakwaza baadhi ya watu) Kuna Hawa waislamu na wasabato Ni watu wabaya sana, ni Kama watoto wa kambo, wanapenda kulinganisha Kila kitu!! .
Waislam wameingiaje hapa??
 
Hao utumishi waangalie namna ya kurekebisha hili maana hoja sijui za venue sijui kitu gani ni hoja dhaifu sana ukilinganisha na madhara yake. Wapange siku neutral ambayo haitaathiri kundi lolote
 
Hao utumishi waangalie namna ya kurekebisha hili maana hoja sijui za venue sijui kitu gani ni hoja dhaifu sana ukilinganisha na madhara yake. Wapange siku neutral ambayo haitaathiri kundi lolote
Haipo siku neutral...watakuja wengine watasema jumatatu, au alhamisi ni siku zao za kuabudu.
Wengine watasema muda wa asubuhi ni muda wa kusali. Tusifungue Pandora Box...Hakuna namna.
 
Haipo siku neutral...watakuja wengine watasema jumatatu, au alhamisi ni siku zao za kuabudu.
Wengine watasema muda wa asubuhi ni muda wa kusali. Tusifungue Pandora Box...Hakuna namna.
Hao watu unaowasemea hawapo kwa hiyo hatujadili vitu vya kufikirika hapa, hebu toa mfano wa watu kama unawafahamu
 
Hao utumishi waangalie namna ya kurekebisha hili maana hoja sijui za venue sijui kitu gani ni hoja dhaifu sana ukilinganisha na madhara yake. Wapange siku neutral ambayo haitaathiri kundi lolote
Mkuu kibongo bongo bado sana kama utaona kufanya usaili hakuna maana yoyote basi nakushaur jikite kutafuta ufalme wa mungu si lazima kuajiliwa unaweza anzisha ata biashara yako ili jmoc siku ya sabato uende ukashinde uko sabato mpk kesho yake ukeshe na kuomba
 
Interview za utumishi kwa mchujo mara nyingi hufanyika kwenye vyuo mbalimbali, wanaoitwa interview ni wengi hivyo miundombinu ya vyuo inaweza kuwatosha hawa wote.

Wanapanga jumamosi na jumapili sababu ili kupata ile nafasi wanachuo wanakua off.

Inatakiwa uwe tayari kufata ratiba mana hiyo nayo ni sehem ya interview, kama huezi kuhudhuria interview jumamosi ukipangiwa majukumu ya kazi jumamosi utaweza?

Wengine wanaenda interview siku ya jumapili na wengi hawa hawalalamiki, huoni kuwa hoja yako ya uchache wa wasabato inakua ni ubaguzi wa kidini?

Umeona siku ya jumamosi tu na siku ya jumapili wanaohusika hawa siyo watu? Au hawana dini wewe tu unajua dini?
Yesu mwenyewe alifanya kazi hiyo siku ya sabato Yohane 5:16-40.
Mkuu amejibiwa vizuri kabisa hapa
 
Mkuu kibongo bongo bado sana kama utaona kufanya usaili hakuna maana yoyote basi nakushaur jikite kutafuta ufalme wa mungu si lazima kuajiliwa unaweza anzisha ata biashara yako ili jmoc siku ya sabato uende ukashinde uko sabato mpk kesho yake ukeshe na kuomba
Unajibu hivi kwa sababu hili halikugusi kwa namna yoyote ile ingekuwa linakugusa usingejibu hivi. Nyie ndiyo aina ya watu mwenzako anapitia shida mnamuacha kisa haikuhusu ikifika kwako unataka watu wote wakusaidie na lawama kuu.

Haki ya mtu ikivunjwa msaidie hata kama wewe haikuhusu
 
Kwasababu ni wachache ( minority) ni ngumu kuona athari zake. Haipendezi kila Interview inapangwa Jumamosi kwanini hazipangwi siku nyingine kwa kurududia. Kwanini mara zote na mara nyingi ni Jumamosi, hata kama hatujali kwakuwa ni wachache hawana sauti lakini wanaumia sana.
Kwani lazima waende? Wachague moja, hiyo siku dhambi nyingine wanafanya ila kwenda kwenye interview wanaona nongwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom