Tabia ya kutopokea namba ngeni/namba mpya

Tabia ya kutopokea namba ngeni/namba mpya

Mimi hii ndio principle yangu namba ngeni huwa sipokei kabisa.
Huu utaratibu naupenda na siuachi kamwe.

Najiambiaga kama una la muhimu sana kuniambia utanitumia message.
Na kama hujatuma message najua huyu hakuwa na jambo la msingi ndio maana hajanitumia message.

Ila kwa ujumla kabisa sipendi kupokea simu kabisa, kuna siku ntapokea na tutaongea vizuri ila kuna siku sipendi kupokea kabisa hata kama naijua namba yako.

Cha ajabu ukituma texts tutachati kabisa na nitaanza kutunga sababu za kukwambia kwanini sikupokea simu yako.

Japo ni tabia ya ajabu kabisa yaani unaona kabisa simu inaita na jina unaliona lakini badala ya kupokea unaanza kutunga uongo wa kudanganya kwanini hukupokea.
Na ikinilazimu sana nitakupigia huku nikiomba kimoyomoyo usipokeee yaani ikiita tu mara 2 nakata, kuweka ushahidi kuwa hata mimi nilikupigia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1].

Ila kuna watu wanaudhi sana wanaweza kukupigia simu saa 12 asubuhi alafu hawana hata cha maana kukwambia.
Mimi naanza kupokea simu kuanzia saa tatu asubuhi (9:00AM) kwa siku za kazi na saa tano(11:00AM)siku za WeekEnd na Public Holiday.

Sio dharau wala kiburi ila ndio Principle yangu tu japo najua kuna wakati nakosea sana kufanya hivi, ila kwenye maisha lazima uwe na Principle zako na uweze kuzisimamia.
Una tabia za like na bila Shaka utakuwa ni sshoga
 
Kwa kweli tunatofautiana, mimi naweza nisipokee mtu ninayemfahahamu ila hakuna namba napokea haraka kama namba mpya. Huwa nakuwa na shauku sana nijue ni nani?? Kapiga kwa sababu gani?

Dalili ya umaskini!
 
Huo ni ushamba
ni utaratibu binafsi tu kila mtu anawake
hata angepokea mwanzoni kaka asingepona

mimi simu ya mawasiliano nawasha saa 4 asubuhi nazima saa 2

watu wangu wote washazoea.
 
[emoji122][emoji122]
A wise man

Sent using Jamii Forums mobile app
Thanks Dr.

Unajua humu tunakutana na watu wengi wenye malezi na makuzi tofauti tofauti.

Kuna wengine wao kutukana hadharani ni sawa tu.
Lazima tujifunze kuishi na watu tofauti tofauti na kuwaelewa hali zao.
Siku zote huwa nawaambia watu unapomuona mtu na tabia fulani basi inatokana na makuzi na malezi yake.
Nawaambia wazazi mara zote wawe makini sana na malezi ya watoto wao kwa kuwa malezi yao yanaathiri mtoto iwe kwa ubaya ama kwa uzuri hadi atakapokuwa mtu mzima na tabia hiyo ataendelea nayo hadi siku anaingia kaburini.

Kwa malezi yangu na heshima yangu kwa watu siwezi kumtusi mtu hata kama atakuwa ameanza kunitusi mimi.

Pamoja na kutokumjua huyu bwana siwezi kumvunjia heshima yake hapa kwa kumtusi kama alivyofanya kwangu.
 
Kwenye maisha kila mtu kajiwekea principles zake na utaratibu wa Maisha.. Ni sahihi sana lakini Kuna vingine vinahitaji Utashi wa kibinadamu kung'amua Hasara na Faida zake.

Kuna watu wamejiwekea utaratibu kwamba Hata iweje, Basi Namba ngeni itapiga sana na kamwe hatopokea.. Sijui ni madeni au basi tu hataki lakini ndo alivyoniwekea.. Hii iko pande zote kwa Baadhi ya wanaume na Wanawake.. Wanawake wengi wanasema wao huepuka Usumbufu kwani mara nyingi huwa ni wanaume wakware wanaotaka penzi lao.

Dhana hii kwa upande mmoja ni sahihi.. Lakini Je, huoni haja ya kumsikia anayekupigia ni nani kabla huja ignore? Na unakuta wewe ni mfanyabishara, mfanyakazi na pengine Mtafutaji wa kazi ume apply huko na huko.. Sasa umepigiwa simu ya interview na hupokei unataka uje kumlaum nani?

Juzi Mtu wangu wa karibu Kapigiwa sana simu Kwa namba mpya na hakuipokea maksudi kabisa zaidi ya mara nne.. Huku akibetua mdomo "Wanaume bana huyu nae anataka kunisumbua tu" Lakini baadae kupitia Namba hyo hiyo akatumiwa Msg Kwamba Kaka yake kafariki kwa Ajali.. Ndo akaanza kutoa vilio kama punda mwenye Njaa

Wakati mwingine tuangalie misimamo yetu kama ina tija kwenye Maisha.
Mimi napenda sana kupokea namba mpya mara nyingi huwa za madili/mishiko!! Nikikuta missed call ya namba mpya kwanza lazima niangalie imesajiliwa jina gani ndio napiga kama namjua ni mzushi naachana nae kama jina silijui nampigia.

Kuna wengine unajua kabisa anaomba michango ya harusi au huwa ni mtu wa story zisizo na mshiko(tantalila).
 
Hivi hii huduma ya Voicemail imekaaje kibongo bongo?

Kuongea Ongea kunachosha, sio namba ngeni tu sometimes hata phonebook yangu naikaushia.
 
Thanks Dr.

Unajua humu tunakutana na watu wengi wenye malezi na makuzi tofauti tofauti.

Kuna wengine wao kutukana hadharani ni sawa tu.
Lazima tujifunze kuishi na watu tofauti tofauti na kuwaelewa hali zao.
Siku zote huwa nawaambia watu unapomuona mtu na tabia fulani basi inatokana na makuzi na malezi yake.
Nawaambia wazazi mara zote wawe makini sana na malezi ya watoto wao kwa kuwa malezi yao yanaathiri mtoto iwe kwa ubaya ama kwa uzuri hadi atakapokuwa mtu mzima na tabia hiyo ataendelea nayo hadi siku anaingia kaburini.

Kwa malezi yangu na heshima yangu kwa watu siwezi kumtusi mtu hata kama atakuwa ameanza kunitusi mimi.

Pamoja na kutokumjua huyu bwana siwezi kumvunjia heshima yake hapa kwa kumtusi kama alivyofanya kwangu.
That is why I love you [emoji4][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
You're too humble regardless of your status [emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi napenda sana kupokea namba mpya mara nyingi huwa za madili/mishiko!! Nikikuta missed call ya namba mpya kwanza lazima niangalie imesajiliwa jina gani ndio napiga kama namjua ni mzushi naachana nae kama jina silijui nampigia.

Kuna wengine unajua kabisa anaomba michango ya harusi au huwa ni mtu wa story zisizo na mshiko(tantalila).
We uko kama mimi
 
Back
Top Bottom