Tabia ya kutopokea namba ngeni/namba mpya

Tabia ya kutopokea namba ngeni/namba mpya

Dawa ya mdeni sio kutokupokea simu ila ni kuwa mstaarabu na kumpanga kwa kumpa matumaini ili msifikie ugomvi usio na sababu... Ukipata unampa pesa yake
Mimi voda wananidai nlikuwa sipokei cm ya voda.no mpya ikipiga.kwa sasa.
Nimejitoa tu muhanga.ntapokea cm zote.kama ni wao ntawajibu tu ya kwamba ntawalipa.no namna
 
Tanzania imejaa mafal* wa aina hii. Hata ukisoma huu uzi utagundua hivyo. Sisi tunaokaa nje ya nchi ni shida tupu. Mtu akiona namba ya nje ndio basi kabisa. Hapokei hata ukipiga mara ngapi. Ili apokee, inabidi kwanza nitume ujumbe wa maandishi nikijitambulisha. Kuna nchi ambazo hilo haliwezekani kwa vile mitandao ya simu hairuhusu SMS. Hii tabia ya Watanzania walio wengi, inakera sana. Katika kukaa kwangu nje, sijawahi kuonana na tabia hii. Ni tabia ya Watanzania tu.
 
Mpo wengi sana. Tabia zenu zinakera. Siyo wote wanaokupigia, wana njaa. Wengine wanapiga kwa faida yako wewe.
Nadhani badala ya kumpigia tu mtu na namba mpya, mtumie ujumbe jitambulishe. Sasa mtu unapiga kama vile hasira
 
Technology zipo why mtu uhangaike?
Caller id app inasaidia kujua Nani anakupigia..
Utajua Tu hii nipokee au hii sipokei
Lazima niwe nayo hii maana nami maana nina tabia kama alizozitaja mtoa mada
 
Kwangu Mimi nimekuwa nikilalamikiwa mara kwa mara na ndugu na jamaa..."sipendi kuongea kwenye simu sijui ni kwann japo kiasili sio muongeaji sana pia, napenda kutumia sms kwa mawasiliano"

Nadhani hii ndo asili yangu, japo walio wengi wanahc vinginevyo.
Tupo njia moja nikipigiwa simu naona kero sana (sipendi pia kupiga simu) sijui nina tatizo gani ila SMS natoa ushirikiano vizuri
 
Huwa nashangaa sana Mkuu, Mtu mwingine unampigia kwa nia njema kabisa pengine kuna fursa ya kazi unataka kumpa.. Ama hata kumtumia taarifa nzuri lakini Hataki kupokea anataka sjui ukampigie magoti ndo apokee.. Huu ni ushamba tu
Mpo wengi sana. Tabia zenu zinakera. Siyo wote wanaokupigia, wana njaa. Wengine wanapiga kwa faida yako wewe.
 
Mimi ndo tabia yangu namba ngeni sipokei,hata nazo sijua ambazo zitakuwa usumbufu tu sipokei..

Sipendi usumbufu,mtu anapiga simu kila siku anakusalimia tu.
Unahisi kila simu Mpya ni usumbufu wa kusalimiwa au umejiwekea hivyo tu? Iko siku litatokea jambo serious utajutia sana
 
Unahisi kila simu Mpya ni usumbufu wa kusalimiwa au umejiwekea hivyo tu? Iko siku litatokea jambo serious utajutia sana
Wengi wao ni usumbufu tu,sometimes mtu uko busy unapigiwa mtu anataka mpige story tu.

Au daily unapigwa vizinga,inachosha.
Sikatai kweli sometimes zipo kweli simu za muhimu.
 
Binafsi sipokei namba mpya, kuna wapiga mizinga wengi wanajuaga wakitumia namba zao sipokei, walibuni njia ya kutumia namba ngeni. Na Mimi nimejiongeza piga hata Mara mia sitapokea.
 
Mimi bana baada ya kugraduate kuna siku nilipigiwa simu na namba ngeni kama mara mbili nkapotezea.. baada ya hapo nikatumiwa message inayosema "This is UDSM calling.."

kila nkipiga ile namba haipokelewi kila nikipiga waapiii.. dah tumbo lilichafuka ghafla mana nilishaona nimebugi.
sasa sijui walikua wanataka waniajiri au wamenitaftia muajiri. siwezi kusahau ile siku.
 
Endeleeni kutopokea Simu kisa namba ngeni mtapishana na magari ya mishahara.

Kwani MTU ukishapokea Simu yake akianza mazinguzi si unakata kwani lazim umsikilize kila mtu???

Na kama je ni tatizo ambalo unahitajika wewe kulisolve???

Mimi naona ni ushamba,kujiona,dharau,kiburii,,acheni viburiii ipo siku mtarudi udongoni mkawe msosi wa finye finye!!
 
Ulipishana na gari ya helaa aiseh pole

Back
Top Bottom