Songwe: Ghala Bubu lakutwa na Dawa zilizo 'Expire', nyingine zina Nembo ya Serikali

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1695533903149.png

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imakamata shehena za Dawa na Vifaa Tiba zilizohifadhiwa na mmiliki wa Duka la Dawa Muhimu la Miranaco Kata ya Vwawa, vyote vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 13.2.

Kuhusu Dawa zenye Nembo ya Serikali, Kaimu Meneja wa Kanda, Dkt. Sylvester Mwidunda amesema Dawa hizo bado zinaendelea kusambazwa maeneo mbalimbali mkoani humo na kuuzwa kwa mteja mmoja mmoja lakini hawajajua Mfanyabiashara huyo alizipataje.

Ameongeza kuwa Mfanyabiashara huyo alifanikiwa kutoroka wakati zoezi la ukaguzi likianza na atachukuliwa hatua kwasababu kutunza Dawa na Vifaa Tiba kinyume na utaratibu ni kosa linakiuka Sheria ya Dawa na Vipodozi.

Kwa mujibu wa Tafiti za Afya, Dawa zilizokwisha muda wa Matumizi zinamweka Mtumiaji katika hatari ya Kuongeza Vimelea vya Magonjwa Sugu kwasababu Vijuasumu vyake vinakosa nguvu na kushindwa kutibu Maambukizo.

================

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imakamata shehena za dawa na vifaa tiba zilizohifadhiwa kwenye ghala' bubu' la mmiliki wa duka la Dawa muhimu la Miranaco Kata ya Vwawa Mkoa wa Songwe vyenye thamani ya Sh13.2 milioni.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Septemba 23, 2023 Kaimu Meneja wa Kanda, Dk Sylvester Mwidunda amesema miongoni mwa dawa zilizokamatwa ni ambazo zimeisha muda na nyingine zina nembo ya Serikali ambazo zilikuwa zikiendelea kusambazwa maeneo mbalimbali mkoani humo na kuuzwa kwa mteja mmoja mmoja.

“Katika ukaguzi wetu wa kitaalamu sehemu ya shehena hiyo dawa nyingi zimekwisha muda sambamba na nyingine ambazo ni mali ya serikali ambapo bado hatujajua mfanyabishara huyo alizitapa kwa njia gani na kitendo ni kinyume cha sheria ya kifungu namba 75 ya dawa na vifaa tiba sura namba 2019,”amesema.

Dk Mwidunda amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kufichua wafanyabishara wa maduka ya dawa muhimu ambao wanauza dawa zilizokwisha muda ili hatua ziweze kuchukuliwa kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha afya za watumiaji sambamba na kutoa taarifa za kufanikisha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo ambaye alitoweka mara baada ya kuanza ukaguzi.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe, Rajab Kambangwa ameitaka mamlaka hiyo kufanya oparesheni za mara kwa mara ili kuokoa maisha ya watanzania kwani shehena hiyo ya dawa zilizokamatwa zingeleta madhara makubwa kwa binadamu hususan watoto.

“Kimsingi hiyo ni hatari kwa watumiaji tuombe tu muendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wenye lengo la kuwabaini wafanyabishara wa maduka ya dawa muhimu wasiokuwa waaminifu na kuwachukulia hatua,”amesema.

MWANANCHI
 
Niliwahi sikia kuna utaratibu serikali inaingia mkataba na watu/taasisi binafsi/kampuni kwa lengo la kusaidia kataka uteketezaji/kuharibu wa bidhaa/shehena feki ama zilizoisha muda wake. Isijekuwa jamaa alitumia mwanya huo kuzirejesha kwenye mzunguko
 
Eti hawajui dawa zenye nembo ya serikali amezipataje!! Yani mnajifanya hamjui kama zimeibwa serikalini akauziwa huyo mfanya biashara

Hi nchi kungekuwa na sheria ya kunyonga mafisadi wangenyongwa watu wengi sana
 
View attachment 2760379
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imakamata shehena za Dawa na Vifaa Tiba zilizohifadhiwa na mmiliki wa Duka la Dawa Muhimu la Miranaco Kata ya Vwawa, vyote vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 13.2.

Kuhusu Dawa zenye Nembo ya Serikali, Kaimu Meneja wa Kanda, Dkt. Sylvester Mwidunda amesema Dawa hizo bado zinaendelea kusambazwa maeneo mbalimbali mkoani humo na kuuzwa kwa mteja mmoja mmoja lakini hawajajua Mfanyabiashara huyo alizipataje.

Ameongeza kuwa Mfanyabiashara huyo alifanikiwa kutoroka wakati zoezi la ukaguzi likianza na atachukuliwa hatua kwasababu kutunza Dawa na Vifaa Tiba kinyume na utaratibu ni kosa linakiuka Sheria ya Dawa na Vipodozi.

Kwa mujibu wa Tafiti za Afya, Dawa zilizokwisha muda wa Matumizi zinamweka Mtumiaji katika hatari ya Kuongeza Vimelea vya Magonjwa Sugu kwasababu Vijuasumu vyake vinakosa nguvu na kushindwa kutibu Maambukizo.

================

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imakamata shehena za dawa na vifaa tiba zilizohifadhiwa kwenye ghala' bubu' la mmiliki wa duka la Dawa muhimu la Miranaco Kata ya Vwawa Mkoa wa Songwe vyenye thamani ya Sh13.2 milioni.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Septemba 23, 2023 Kaimu Meneja wa Kanda, Dk Sylvester Mwidunda amesema miongoni mwa dawa zilizokamatwa ni ambazo zimeisha muda na nyingine zina nembo ya Serikali ambazo zilikuwa zikiendelea kusambazwa maeneo mbalimbali mkoani humo na kuuzwa kwa mteja mmoja mmoja.

“Katika ukaguzi wetu wa kitaalamu sehemu ya shehena hiyo dawa nyingi zimekwisha muda sambamba na nyingine ambazo ni mali ya serikali ambapo bado hatujajua mfanyabishara huyo alizitapa kwa njia gani na kitendo ni kinyume cha sheria ya kifungu namba 75 ya dawa na vifaa tiba sura namba 2019,”amesema.

Dk Mwidunda amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kufichua wafanyabishara wa maduka ya dawa muhimu ambao wanauza dawa zilizokwisha muda ili hatua ziweze kuchukuliwa kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha afya za watumiaji sambamba na kutoa taarifa za kufanikisha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo ambaye alitoweka mara baada ya kuanza ukaguzi.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe, Rajab Kambangwa ameitaka mamlaka hiyo kufanya oparesheni za mara kwa mara ili kuokoa maisha ya watanzania kwani shehena hiyo ya dawa zilizokamatwa zingeleta madhara makubwa kwa binadamu hususan watoto.

“Kimsingi hiyo ni hatari kwa watumiaji tuombe tu muendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wenye lengo la kuwabaini wafanyabishara wa maduka ya dawa muhimu wasiokuwa waaminifu na kuwachukulia hatua,”amesema.

MWANANCHI
Halafu ua kuta hizo dawa wananchi wanauziwa na wanatumia bila kujua
 
Back
Top Bottom