KERO Maafisa wa Taasisi ya Moyo wanachezea mifumo ya Bima ionekane baadhi ya Dawa hazipo katika Bima ya NHIF

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna tabia imeibuka au yawezekana ipo kwa muda mrefu, nasema hivyo kwa kuwa sikuwahi kuelewa kuhusu hilo siku za nyuma lakini baada ya hili nitakalozungumza hapa kutokea nikishuhudia, nimepata hisia kuwa inawezekana kuna watu wengi wameumzwa na katabia ka aina hii hasa katika Hospitali kubwa.

Kumekuwa na mchezo wa kuchezea mifumo ya Taasisi zao kwa ajili ya kuondoa baadhi ya dawa ambazo zipo kwenye Bima ili zionekane hazipo katika listi ya dawa ambazo zinatakiwa kuwemo.

Mfano kuna tukio limetokea kwa ndugu pale Muhimbili kwenye ile Taasisi ya Moyo, waliamua kutoa baadhi ya dawa kwenye orodha ya NHIF kisha wakamwambia mgonjwa alipie kwa madai dawa hizo hazipo katika listi ya NHIF.

Mgonjwa huyo amekuwa akienda kupata matibabu hapo, juzi akiwa hapo akaambiwa vilevile kuwa kuna dawa hazipo kwenye listi na kwamba alipie cash.

Akaamua kuwatafuta NHIF makao makuu ambao walipofanya mawasiliano na taasisi hiyo ikagundulika kuwa kilichofanyika ni mfumo kuchezewa ili hata ukiuliza uoneshwe kwenye kompyuta zao uone hiyo dawa au hizo dawa hazipo.

Baada ya mgonjwa kuonekana anajua anachokifanya na anazijua taratibu za NHIF kukaibuka mvutano wa hapa na pale na mwisho ikabainika ni kweli kuna hiyo changamoto.

Baada ya mkutano huo wahusika wakakiri kweli kuna changamoto ya aina hiyo, wakamalizana na yule mgonjwa na kuamua kumpa zile dawa anazohitaji.

Swali la kujiulia kama huyu mgonjwa mwenye uelewa kaweza kulibaini hilo katika Hospitali kuwa kama hiyo, je, kuna Watanzania wangapi wameathiriwa na tabia ya ina hiyo inayowalazimu watu kutumia fedha licha ya uwepo wa bima, au ni wangapi wameshindwa kulipia kwa kuwa tu hospitali zimecheza na mifumo yao?

Majibu ya JKCI - Taasisi ya Moyo (JKCI) yafafanuzi madai ya kuchezea mifumo ya NHIF ili baadhi ya Dawa ionekane hazipo
 
Ukiona hivyo ujue kuna mazingira ya Rushwa yalikuwa yakitengenezwa, sio sahihi kuchekecha mfumo wa kompyuta ili kumnyima mgonjwa dawa, it is unethical
 
Kitafute kitita kipya cha NHIF.
Huenda hizo dawa zipo ila bima wanalipa pesa ndogo kuliko ya manunuzi na hivyo inakjuwa ni hasara kuwa na dawa hiyo
 
Habari,

Ni suala ambalo mpaka ujue undani wake na kikao kilihusiana na nini, yapi yaliongelewa kwa kesi husika.

Pia:
1: Kwa Hospitali ya Serikali si rahisi sana kuwa na lengo hasi kwani hata hayo mauzo ya dawa, pesa inaingia serikalini labda vinginevyo.

2: Kwa upande wa private, suala la bei linaweza kuwa na mashiko. Na hakuna anaependa kutoa dawa kwa hasara.

3: Kuna wakati mabadiliko yanaweza kushinikizwa na aina ya mteja au taasisi inayotoa pesa za bima hasa bima kubwa (SUPPLEMENTARY), kwa sababu wanakuwa na wigo mkubwa zaidi wa dawa na vifaa tiba.

4: Ingawa kuna hili, ambalo linaweza kubeba uhalisia:

Kumekuwa na changamoto kwenye mfumo wa bima upande wa MADAI/CLAIM. Ambapo baadhi ya dawa zimeondoka kwa bahati mbaya na nyingine ni kwa kufuata mabadiliko.

Unapopewa dawa mgonjwa, huitajika dawa husika kuingizwa kwenye mfumo.
Unapoingiza dawa LAZIMA bima wawe wameiweka ili uweze kuichagua/ACCESS.
Kama haionekani upande wa bima basi wewe kama mtoa huduma ukitoa dawa wakati kwenye mfumo haipo, maana yake hutaweza kuidai dawa husika kulipwa.

Suala la msingi ni pale bima wanapopewa taarifa ya kutokuonekana kwa dawa husika na labda kuirejesha au kutoa maelezo husika/sahihi. Hii pia hutegemeana na ukubwa wa bima husika kama maelezo yaliyotangulia.


Ni mchakato unaohitaji masikilizano ya pande mbili hasa baada ya mabadiliko.
 
Suala la msingi ni pale bima wanapopewa taarifa ya kutokuonekana kwa dawa husika na labda kuirejesha au kutoa maelezo husika/sahihi. Hii pia hutegemeana na ukubwa wa bima husika kama maelezo yaliyotangulia.
Hapa ndio pa kufikiri kwa kina.

Turejee, sasahivi kuna mvutano wa hiki KITITA na baadhi ya dawa zishaondolewa kwenye kitita.

Hospital za Umma hawajakikataa hiki kitita jambo ambalo hawawezi kukataa kumhudumia mgonjwa kwa huduma iliyopo kwenye kitita.

Mdau anasema mgonjwa aliwasiliana na NHIF ndipo Hospital ikapewa melekezo baada ya tatizo kurekebishwa. Hapa huenda ni kweli hizo dawa ziliondolewa ila baada ya mgonjwa kulalamika na kuwauliza ndipo wakaamua kuirejesha, jambo ambalo ndio Hospital ikakiri kulikuwa na changamoto ila imetatuliwa.

Sasa tungejua hizo dawa alizotaka kunyimwa ni zipi ili tuangalie kwenye kitita kama kweli zipo au la..
 
Back
Top Bottom