Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Wakuu,
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi imeanza kufanya kazi toka Mei 1, mwaka huu 2023 na Tume ipo kuhakikisha huumizwi na watu au taasisi wanaotaka kutumia vibaya taarifa zako kwa maslahi yao.
Ikiwa una malalamiko ya taarifa zako kutumiwa vibaya mfano mtu katumia picha zako kwenye matangazo wakati hilo halikuwa lengo, mtu kavujisha picha au jumbe ili akukomoe unatakiwa kupeleka malalamiko yako katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Kazi ya Tume hii ni kupokea, kuchunguza na kushungulikia malalamiko kuhusu Madai ya Ukiukwaji wa Ulinzi wa Taarifa binafsi na Faragha za watu.
Pia ili mtu au kampuni iwe na ruhusa ya kukusanya au kuchakata taarifa binafsi inatakiwa kupata usajili kutoka katika tume hii, ambayo inaongozwa na Mkurugenzi anayeteuliwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Usajili huo ni wa miaka mitano, baada ya kipindi hicho kuisha Muhusika anatakiwa kuhuisha Usajili wake kama Kanuni zinavyoelekeza.
Swali ni je, tume hii ipo wapi mpaka sasa wakati sheria imeshanza kutumika?