@Kifupi hakuna kipya alichozungumza waziri zaidi amerudia tu baadhi aliyosema waziri mkuu Pinda. @Jambo baya kuliko yote ni kuamua kuupotosha umma kwa makusudi juu ya hali halisi ya huduma za afya zilivyo kwa sasa na madai halisi ya madaktari. @Kwa mwendo huu mgogoro wa madaktari na serikali ndio kwanza umeanza na kuutatua utahitaji muda mrefu na gharama kubwa sana.
