Taarifa ya msiba wa mama yangu mpendwa.

Kitomai

JF-Expert Member
May 21, 2009
1,061
281
Ninayo masikitiko makubwa kuwatangazia kifo cha mama yangu mpendwa, Telinala Mtambo kilichotokea ghafla asubuhi ya siku ya leo tarehe 12/03/13 jijini Mbeya.

Mazishi yanategemea kufanyika siku ya ijumaa tarehe 15/03/2012, kwa hapa Dar-es-salaam ndugu, jamaa na marafiki wanakusanyikia nyumbani kwangu Kimara kwa ajili ya mipango ya mazishi.

Safari ya kwenda msibani jijini Mbeya itakua kesho tarehe 14/03/13.

Rambi rambi zinakaribishwa.

Kwa maelezo zaidi tunaweza kuwasiliana katika namba za simu zifuatazo: 0717114409/0755312233/0784225000. Amen.

attachment.php

Picha ya baba na mama yangu wiki mbili zilizopita.
 
Mungu apate kukufariji kiongozi. May the great Woman Rest in Peace. Amen.
 
Pole sana mkuu Kitomai, MUNGU akupe nguvu na ujasiri ktk kipindi hiki kigumu na ampumzishe kwa amani mama yetu mpendwa!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu Kitomai, MUNGU akupe nguvu na ujasiri ktk kipindi hiki kigumu na ampumzishe kwa amani mama yetu mpendwa!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Kitomai, tunamwombea mama apumzike kwa amani. Amen.
 
pole sana ndugu hyo ni kaz ya mungu haina makosa mwenyez mungu akupe uvmiliv kwenye kpnd hki kigumu.pole
 
Pole kiongoz . Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana mkuu, niko mbali nasikitika sitaweza kuwa karibu nawqe katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa mama yako mpendwa...
Je Dr. John na wadau wa FAJI wanazo taarifa?
 
Naendelea kujifunza namna ya kukabiliana vema na matatizo kila siku ya kimaisha ambayo hakuna mtu anayeweza kuyazuia kama ili kufiwa na mtu wa karibu. Katika kipindi hiki kigumu kwangu nina jaribu sana kuruhusu fikira zenye kunipa furaha kuingia katika mfumo wangu mkuu wa kufikiri maana taarifa ya msiba wa niliyekua nampenda sana imeutikisa mwili wangu wa hisia.
Mama hakuugua kwa muda mrefu au kakuwa na magonjwa ya hatari, Baba akanipigia simu na kunijulisha kuwa tulipokua katika kusali asubuhi kama ilivyo kwaida yetu, mama yako akaniambia ''Nakwenda nyumbani''. Kisha akayafumba macho yake, baada ya kupelekwa Hospitali, daktari wa zamu baada ya kumpima akatoa ripoti ya kuwa amefariki.
Asubuhi ninasafiri na watu wa familia yangu wasiopungua 7, ''All eyes on me''. Taarifa hizi za msiba zimenijia kipindi ambacho nina tatizo la kifedha ndiyo maana nikasema ''michango inakaribishwa''.
Pia napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wale wote ambao wamenitumia jumbe za kunitia moyo na watakao fanya hivyo baadaye.
 
Mama ameacha watoto 10, wasichana 6 na wavulana 4, wajukuu 23, na vitukuu vitatu.
Tuchangie kiasi cha Pesa ili kuweza kufanikisha Mazishi ya Mama Yetu, Ndugu Yetu na JAMAA Yetu TELINALA MTAMBO kwa kupitia namba 0755312233 kwa njia ya M-Pesa AU 0717114409 Tigo Pesa.
Tunatanguliza shukrani zetu kwa kushiriki kwako.
 
Pole sana kwa kondokewa na mama. M/Mungu akupe ujasiri ktk kipindi hiki kigumu. RIP Mama.
 
Back
Top Bottom