Jimbo la Kiteto - Taarifa Maalum kwa Wananchi Kuhusu Miradi ya Huduma za Mawasiliano

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

JIMBO LA KITETO - TAARIFA MAALUM KWA WANANCHI KUHUSU MIRADI YA HUDUMA ZA MAWASILIANO

Ndugu wananchi wenzangu wa Jimbo la Kiteto natambua kuwa wakati natafuta kura tulipata changamoto nyingi sana za huduma ya mawasiliano ya simu katika Vijiji zaidi ya 30 ambavyo mitandao ya simu ni changamoto kubwa sana na wakati mwingine hakuna kabisa mawasiliano ya simu.

Ndugu Wananchi wenzangu swala la mawasiliano ni muhimu mno kwa maendeleo ya watu na Jimbo letu hususan katika zama hizi za kidigitali.

Mtakumbuka nimezungumza mara kadhaa Bungeni kufikisha kilio chetu cha kukosena kwa mtandao wa simu na mawasiliano lakini mtakumbuka wakati nachangia katika Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Technologia ya Habari 2022-2023 nilimpongeza kwa dhati Mhe. Waziri, Mhe. Nape Moses Nauye ( Mb) kwa kuweka katika mpango wa Bajeti zaidi ya Vijiji 25 vya Kiteto katika mpango wa Vijiji vilivyotengewa fedha kwaajili ya huduma ya Mawasiliano ( Yaani Kujengewa Minara)

Ndugu wananchi wenzangu kwa unyenyekevu mkubwa napenda kuwafahamisha kuwa leo tarehe 13. 5. 2023 hapa Dodoma nipo katika hafla ya Kitaifa ya Kutia Saini Mikataba ya Kupeleka Huduma ya Mawasiliano Vijijini iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Technologia ya Habari hapa Dodoma na Mgeni Rasmi ni Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika Hafla hii nimezungumza na Mhe. Waziri, rafiki yangu Nape Moses Nauye (Mb) na amenihakikisha kuwa Jimbo letu la Kiteto ndio wanufaika wakubwa katika Miradi hii. Tumepata bahati kubwa kuwa Kata 12 na Vijiji 23 zitanufaika katika Miradi hii ya Huduma ya Mawasiliano inayozinduliwa leo kama ifuatavyo;

1. Kijiji Cha Esuguta kata ya Dosidosi
2. Vijiji (3) vya Laiseri, Ndotoi na Enguserosidan vya Kata ya Laiseri
3. Vijiji vya (2) Orkitikiti na Engangongare vya Kata ya Lengatei
4. Vijiji ( 3) vya Amei, Loolera na Lembapuli vya Kata ya Loolera
5. Vijiji ( 3) vya Nahti, Emarti na Magungu vya Kata ya Magungu
6. Kijiji cha Kinua Kata ya Namelock
7. Vijiji ( 3) vya Ndirigish, Taigo na Krash vya Kata ya Ndirigish
8. Vijiji ( 2) vya Ndaleta na Orpopongi vya Kata ya Njoro
9. Vijiji ( 2) vya Mwitikira na Kiperesa vya Kata ya Kiperesa
10. Kijiji cha Kimana Kata ya Partimbo
11. Kijiji cha Songambele Kata ya Songambele
12. Kijiji cha Loltepesi Kata ya Sunya

Aidha ndugu wananchi wenzangu nafahamu kuwa kwa Radio Tanzania hasikiki kabisa Kiteto. Nachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Technologia ya Habari kwa mwaka wa fedha 2022-2023 pia imeweka katika mipango yake kuhakikisha kuwa Radio Tanzania inasikika katika Jimbo letu la Kiteto.

Nawaomba tuendelea kuwombea Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa moyo wa kuendelea kutufuta pesa kwaajili ya miradi ya kuboresha Miundombinu ya Mawasiliano na Habari kwaajili ya kushughulia changamoto za wananchi katika wilaya yetu. Ahadi za CCM zinaendelea kutekelezwa kwa ufanisi na kasi kubwa zaidi.

Kiteto yetu inaendelea Kung'ara !
Mungu Ibariki Kiteto !
Mungu Ibariki Tanzania !
Mungu ambariki Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge
Edward Ole Lekaita Kisau (Mbunge wa Jimbo la Kiteto)
Leo tarehe 13. 5. 2023
Kazi Iendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-13 at 16.16.44.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-13 at 16.16.44.jpeg
    58.5 KB · Views: 5
  • FwAo_0eWwAgeImK.jpg
    FwAo_0eWwAgeImK.jpg
    113.3 KB · Views: 5
  • FwArSoMaYAI0tBp.jpg
    FwArSoMaYAI0tBp.jpg
    86.3 KB · Views: 4
  • FwABKMKX0AAN6Jp.jpg
    FwABKMKX0AAN6Jp.jpg
    165.9 KB · Views: 4
Back
Top Bottom