Taarifa ya msiba wa mama yangu mpendwa.

Taarifa ya msiba wa mama yangu mpendwa.

Last edited by a moderator:
Pole Sana !kufiwa Na Mzazi Kunauma Jamani Maana Wazazi Ni Marafiki Zetu Wa Ukweli Na Ni Washauri Wetu Wakuu Waukweli Wa Maisha . pole Sana Na Mungu Amlaze Mama Pema Peponi!
 
Pleni sana mkuu. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu.
 
Pole sana mkuuKitomai, mungu amlaze mama mahala pema na pia awape nguvu katika kipindi hiki kigumu maishani.
 
ninayo masikitiko makubwa kuwatangazia kifo cha mama yangu mpendwa, telinala mtambo kilichotokea ghafla asubuhi ya siku ya leo tarehe 12/03/13 jijini mbeya. Mazishi yanategemea kufanyika siku ya ijumaa tarehe 15/03/2012, kwa hapa dar-es-salaam ndugu, jamaa na marafiki wanakusanyikia nyumbani kwangu kimara kwa ajili ya mipango ya mazishi. Safari ya kwenda msibani jijini mbeya itakua kesho tarehe 14/03/13. Rambi rambi zinakaribishwa.
Kwa maelezo zaidi tunaweza kuwasiliana katika namba za simu zifuatazo: 0717114409/0755312233/0784225000. Amen.

Nani kama mama? U will miss her LOVE nad CARE. pole sana comred, tuko pamoja.
 
Naendelea kujifunza namna ya kukabiliana vema na matatizo kila siku ya kimaisha ambayo hakuna mtu anayeweza kuyazuia kama ili kufiwa na mtu wa karibu. Katika kipindi hiki kigumu kwangu nina jaribu sana kuruhusu fikira zenye kunipa furaha kuingia katika mfumo wangu mkuu wa kufikiri maana taarifa ya msiba wa niliyekua nampenda sana imeutikisa mwili wangu wa hisia.
Mama hakuugua kwa muda mrefu au kakuwa na magonjwa ya hatari, Baba akanipigia simu na kunijulisha kuwa tulipokua katika kusali asubuhi kama ilivyo kwaida yetu, mama yako akaniambia ''Nakwenda nyumbani''. Kisha akayafumba macho yake, baada ya kupelekwa Hospitali, daktari wa zamu baada ya kumpima akatoa ripoti ya kuwa amefariki.
Asubuhi ninasafiri na watu wa familia yangu wasiopungua 7, ''All eyes on me''. Taarifa hizi za msiba zimenijia kipindi ambacho nina tatizo la kifedha ndiyo maana nikasema ''michango inakaribishwa''.
Pia napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wale wote ambao wamenitumia jumbe za kunitia moyo na watakao fanya hivyo baadaye.

Pole sana Mkuu!
 
Poleni sana wafiwa. Mungu awatie nguvu na kuwapatia faraja!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Pole sana jombaa..Bwana alitoa na Bwana ametwaa,jina la Bwana libarikiwe ....
 
Pole sana kitomai,kifo cha mzazi,mwanzo wa wewe kuitwa yatima na mzee,si mtoto wa mama tena bali ni baba wa watoto wako...ndo ukubwa be strong...ay her soul RIP.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Mungu wa rehema amlaze salama. Poleni. Shida haziji wakati tumepanga tofauti na harusi na sherehe. Nawaalika wana JF tumchangie kwa maombi, fedha na maneno ya faraja.

Tunawaombea heri wote.
 
Pole Muheshimiwa,may the almighty God bless you at this critical moment.
 
Pole sana, Mungu akutie nguvu kipindi hiki na mkampunzishe vyema mama yetu mpendwa.













Ninayo masikitiko makubwa kuwatangazia kifo cha mama yangu mpendwa, Telinala Mtambo kilichotokea ghafla asubuhi ya siku ya leo tarehe 12/03/13 jijini Mbeya.

Mazishi yanategemea kufanyika siku ya ijumaa tarehe 15/03/2012, kwa hapa Dar-es-salaam ndugu, jamaa na marafiki wanakusanyikia nyumbani kwangu Kimara kwa ajili ya mipango ya mazishi.

Safari ya kwenda msibani jijini Mbeya itakua kesho tarehe 14/03/13.

Rambi rambi zinakaribishwa.

Kwa maelezo zaidi tunaweza kuwasiliana katika namba za simu zifuatazo: 0717114409/0755312233/0784225000. Amen.

attachment.php

Picha ya baba na mama yangu wiki mbili zilizopita.
 
Back
Top Bottom