Kwanini nawahusisha Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi kwenye kifo cha mtoto wangu...

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Kuanza nianze kwa kuwashukuru wana Jamii Forums mlio nitafuta PM kwa kunipa pole katika msiba ule mzito. Nawashukuru pia wale mlio kuja PM kunikebehi yakuwa nilikuwa nawasinzigizia nilio wataja kwa kuwahusisha na Mauaji ya mtoto wangu.

Ilianzia hapa: Mh. Rais, Mkuu wa Wilaya na OCD Lindi 'wamemuua' ANGEL KESSY Mwanafunzi wa PCB

Naomba nieleze kilichojitekeza na ili niweze eleweka vizuri. Kisa kilikuwa hivi:
Mtoto aliripoti shule ya Lindi girls akiwa mzima wa afya pasi na shida yoyote kiafya akitoka shule aliyokuwa amepangiwa Iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani kombi ya PCB.

Baada ya kuripoti amesoma pale wiki mbili akielekea wiki ya 3 tunapewa taarifa yakuwa mtoto amezidiwa tarehe 16 saa nne kamili kupitia simu ya Mama yake. Tarehe hiyo hiyo 16/11/2023 kwa simu ya mtu aliyejitambulisha ya kuwa ni mwalimu, mama mzazi wa marehemu alitokea Mbagala kuelekea shule majira ya saa tano kamili na alifika shule pale saa kumi na mbili kamili.

Mama mzazi alipofika cha kwanza alikutana na watu wafatao;-
1. Mkuu wa Wilaya ya Lindi.
2 OCD kituo cha polisi Lindi.
3. Mganga Mfawidhi wa Wilaya.
4. Walimu wawili.

Kutokana na uwepo wa watu hao kwenye eneo ilo kulipelekea Mama mzazi wa Marehemu kuingia na hofu kubwa kuwa yawezekana mtoto wake ameishaFARIKI. Ili mambo yaweze kwenda sawa, jopo ilo hapo likiongozwa na DC liliona ni busara kwanza kumnyang'anya simu ya Mkononi Mama yule kitendo kile kilimtia hofu zaidi.

Baada ya kumnyang'anya simu walimwingiza ndani na kumwonesha mtoto wake akiwa TAYARI KWENYE JENEZA. Mama mzazi wa marehemu kiukweli alipatwa na mshutuko mkubwa sana watu wale wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya na OCD walimtaka mama yule ataje no za simu za ndugu wa karibu.

Mama wa marehemu alitaja no ya kwanza ni ya Dada yake mkubwa ya pili alitaja no za simu za mme wake na mtoto wa Dada yake.

Ili kutimiza kile walichokuwa wamekipanga yafatayo yalifanyika:
Kwanza DC kupitia simu ya OCD alipiga simu kwa Dada mkubwa wa mzazi wa marehemu kumpatia taarifa yule dada mtu alipokea taarifa na kuanza safari kutoka Bukoba kuja DSM.

Aliyepigiwa akiwa wa Pili ni Baba wa Marehemu huyu alipigiwa simu ya kupewa taarifa lakini pia akubali mwili uletwe usiku usiku kwa gari la serikali na JENEZA tayari liliishanunuliwa.

Simu nyingine ilikwenda kwa Kaka wa Marehemu; yeye alipewa taarifa ya msiba na kuombwa pia akubali mwili uletwe DSM usiku usiku. Kwa upande wa Kaka wa marehemu yeye alipinga mwili usiletwe DSM mpaka ufanyiwe uchunguzi.

Kwa kuwa mama wa marehemu alikuwa kazingirwa na kundi hilo likiongozwa na DC huku akiwa amenyang'anywa simu, kila tulipopiga simu yake, ilipokelewa na Mwalimu aliyedai kuwa MAMA WA MAREHEMU AMEZIMIA.

Kwa maana hii, aliyeridhia pasipo kufikiria kwa kina mwili uletwe alikuwa mtu mmoja tu. Kweli majira ya Saa TISA usiku mwili ulifikishwa nyumbani kwao Kongowe Mzinga DSM. Baada kufikishwa mwili waliingia ndani wanawake wawili na wanaume wawili wakajitambulisha vizuri. Wakiwa ndani ukatokea mzozo kidogo ndugu wa marehemu wakataka kujua nini kilichomuua mtoto wao.

Ndipo alipojitokeza Askari Polisi aliyevalia kiraia, akajitambulisha kuwa yeye ni Afande Kyaruzi, akatoa maneno yalikuwa na vitisho ndani yake. Mwisho magari yale mawili yaliwabeba Baba wakubwa wa marehemu baadhi ya ndugu mpaka hospatli ya Temeke kwa ajili kuhifadhi mwili.

Mwili ulihifadhiwa pale, hakuna nyaraka yoyote iliyotolewa kutoka shuleni na hospitali ya Lindi iliyoonesha mtoto aliumwa nini? Na walimpa dawa gani?

Zaidi, wale walimu na afande Kyaruzi waliacha stakabadhi inayoonesha Mkuu wa Wilaya na jopo lake walilipa shiilingi Laki moja ya kumuhifadhi mtoto hosptalini tu na walilipa mwili uhifadhiwe saa 24, jambo lililoonesha kuwa hata malipo yalifanyika tarehe 15/11/2023.

Ila sisi wanafamilia tulipewa taarifa tarehe 16.

Kilichotushangaza zaidi:

Ndugu wa marehemu walipoenda kuosha mwili walikuta mwili wa marehemu ukiwa na kovu kubwa sana maeneo ya miguuni na lilikuwa limeshonwa na nyuzi kumi na mbili. Kovu lile liliashiria marehemu alikuwa amegongwa.

Changamoto walioosha mwili hawakuwa tayari kutoa taarifa kuwa wamekuta mwili una kovu jambo hilo lilipelekea kuendelea na ratiba ya mazishi na tulimzika mtoto wetu tarehe 18/11/2023.

Marehemu (mtoto wangu) alikuwa anaitwa ANGEL NINSIMA KESSY na alikuwa MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO (PCB) LINDI GIRLS.

KWANINI TUNAMTUHUMU MKUU WA WILAYA, OCD NA MGANGA MFAWIDHI?

1. Kwanini msiba ule haukutolewa taarifa ya kifo na Uongozi wa Shule badala yake awe DC kupitia simu ya OCD?

2. Kwanini Mkuu wa Wilaya na jopo lake hawakutoa taarifa ya mtoto aliumwa nini? Je, alipokelewa hosptali na kupimwa na kupewa dawa gani?

3. Kwanini Mkuu wa Wilaya alikuwa akipiga simu na kuomba sana mwili upokelewe Usiku ule ule pasipo kukubali ifanyike postmotamu?

4. Kwanini DC alipofikisha mwili Temeke hosptali hawakuteua mtu hata mmoja kufika hapo msibani kuleta hata salamu za shule kwa niaba ya shule na wanafunzi wenzie na marehemu?

5. Kama mtoto alikufa kifo cha kawaida, Polisi walisindikiza Mwili wa marehemu kwa cheo gani alichokuwa nacho marehemu?

6. Kwanini DC baada ya kufikisha mwili Dar alizuia mawasiliano baina yake na ndugu wa marehemu akaelekeza mawasiliano yote yafanyike kati ya ndugu wa marehemu na OCD tu?

Tunahoji mengi katika hili.

Nimalizie kwa kufikisha masikitiko yangu makubwa kwa waandishi wa habari hasa ITV NA VYOMBO VINGINE Maana tuliwatafuta tukihitaji msaada wao ili taarifa hii iweze fika mbali kwa ajili ya kufichua uovu wa namna hii lakini hawakuwa tayari.

Ombi langu nalipeleka kwa Mawaziri wa Afya na TAMISEMI, jambo hili lichunguzwe,

Napeleka ombi kwa mkuu wa Odara ya Usalama wa Taifa, tafadhali fanya jambo hapa.

Napeleka ombi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) tafadhali OCD na Afande Kyaruzi wawajibishwe.

Napeleka ombi langu kwa Waziri wa Elimu shule ya Lindi Girls ni ya Serikali; uzembe uliojitokeza hasa kwa watumishi wa shule ni mkubwa mpaka mwanangu anaaga dunia.

Mwisho kwa Mh Rais, kwa mamlaka yake jamani ni huzuni kumpoteza mtoto wa kidato cha tano mkondo PCB, tuliisha invest vingi jamani.

Naomba niliowataja wawajibishwe kwa manufaa ya Umma.

Ujumbe huu umfikie pia Joyce Mhavile: ITV kuna changamoto kubwa wanahabari wako wana-cover stori inayowapa bahasha.

WASI WASI

JE, KAMA MTOTO HAKUGONGWA NA WAKUBWA KWANINI ALIYEMGONGA HAKUKAMATWA?

JE, MTOTO ALIGONGWA AKITOKEA WAPI KWENDA WAPI?

NANI ARIRUHUSU MTOTO ATOKE NJE YA SHULE MPAKA AKAGONGWA?

KUNA UHUSIANO GANI KATI YA “MARELIA” ILIYOTAJWA NA DC NA KOVU LIRE LA AJALI?
 
Hiki nini tena huko Lindi?

Mleta mada weka wazi habari yote kama ilivyo ili umma wote ujue nini hasa kimetokea, na ili upate msaada au ushauri unaostahili.

Hakuna sababu ya kuficha ficha mambo ktk vifo au mauaji.

Habari yako hii inatia mashaka sana kupita kiasi, inaacha maswali mengi zaidi kuliko majibu.

Nina maswali mengi najiuliza bila kupata majibu, maswali yapo kwa upande wako wewe mleta mada na hata kwa upande wa hawa watu unaowatuhumu kwamba wamemuua mtoto wako.

Wewe mzazi ulipopata taarifa ya msiba, Je, ulijaribu kuwasiliana na Uongozi wa Shule ya Sekondari Lindi ambako mwanao alikuwa anasoma?

Je, huyo DC, OCD, Bwana Afya wa Wilaya, n.k majina yao halisi ni yapi?Kwa nini unaficha utambulisho wao endapo kama kweli habari yako ina ukweli?

Je, maiti tayari imezikwa? Kama tayari mmezika, kwanini mliamua kuzika haraka bila kufanya uchunguzi wa kina wa awali Kwanza wakati kifo cha mtu huyo kimegubikwa na utata mkubwa?

Wakati maiti ilipoletwa nyumbani kwako na ulikuwa unajua wazi kwamba kifo hicho kina utata, Je, kwa nini hamkuchukua hatua za haraka za kufungua jeneza na kukagua mwili wa marehemu kabla ya watu waliosindikiza msiba kutoka Lindi hawajaondoka?

Kutokana na utata huo uliojitokeza, na mara tu mlipopata taarifa ya msiba, kwa nini kwa haraka hamkuunda kamati ya wanandugu haraka ili kuwakabili kwa kuwadodosa kwa kina hao waliosindikiza msiba kutoka huko Lindi?

Kwenye msafara wa kuleta maiti kwa wazazi wa marehemu, Je, wawakilishi/walimu kutoka Shuleni alikosoma mwanao walikuwepo kwenye msafara?Je, Walitoa neno gani kama salamu za rambirambi?
 
Msiba ulikuwa WA kulazimisha sana. Inaonekana Kuna vitu nyuma ya pazia. Ila kwa kilichotokea lazima ukweli utajulikana siku sio nyingi mana hakuna Siri ikafichwa na watu zaidi ya mmoja.

Lazima Kuna mwanafunzi atakuja kuropoka kilichotokea.na huyo ocd Bora angenyoosha maelezo ili mambo yasiwe mengi KULIKO kuficha ficha ishu kama hii mana ikija kubumburuka ishu inaweza kuwa kubwa.

Mwisho ya yote nitoe pole kwa mfiwa kuwa kubali yaliyotokea mana mtoto alishafariki na hawezi tena kurudi kuwa mzima.!

Innalilah wainna ilaih rajiuna.
 
Back
Top Bottom