Taarifa Muhimu - Tafadhali Soma Hapa

Hilo nalo ni neno, topic moja inawekwa jamvini mara kibao, kila la kheri bana.
 
Mmengoja bujibuji hayuko ndio mkaleta hii kanuni> maana yeye ndio huwa anaingia na visa vya mikasa.
 
Kutokana na hali ambayo imekuwa ikiendelea humu kwenye Jukwaa la MMU kwa muda mrefu napenda kuwafahamisha members wote kuwa kuanzia sasa thread zote ambazo zitakuwa posted hapa MMU zitakuwa under MODERATION kabla hazijawa approved tumeamua kufanya hivi kwa sababu kumekuwa na mlolongo wa TOPIC zisizokuwa na maana yoyote au TOPIC ambazo kimsingi hazina mantiki yoyote ndani ya Jukwaa hili.

Halikuwa lengo letu kufanya hivi ila kwasababu hali hii imeendelea kwa muda mrefu bila watu kujirekebisha hivyo basi tumeona itakuwa ni busara tukaliweka Jukwaa hili under MODERATION kama tulivyofanya kwenye Jukwaa la Siasa, topic ambazo tunaona zinafaa kukaa hapa zitawekwa hapa na ambazo tutaona hapa sio mahala pake zitahamishwa na kupelekwa Jukwaa husika. Lengo hasa ni kufanya maboresho kwenye Jukwaa hili na kuiweka JF katika hatua nyingine tofauti na sasa hivyo tunaomba sana ushirikiano wenu.

Poleni kwa usumbufu, na wale ambao watakwazika tunawataka radhi.



Asante sana, ningekuwa wewe zile topic zote za kijinga ningezifuta huna haja kuzipeleka kwingine. Poe na kazi kubwa.
 
mkuu nahitaji kujua, sina nia mbaya!
Sitaki kuwa kenge kwenye msafara wa mamba bana!

Mkuu jaribu kushughulisha kichwa kidogo.Hili jukwaa linaitwaje? Naomba uandike jibu then kila herufi ya mwanzo ya neno anza na herufi kubwa na uibold utapata jibu.
 
Uamuzi mzuri ingawa thread yako na yenyewe haikutakiwa kuwa hapa.
I thought hapa ndio MMU -( mahusiano mapenzi urafiki) kwenyewe, sasa post ilitakiwa ikawekwe wapi tena na tungeionaje huko ambako ingewekwa??? kama nakosea nisahihishwe tafadhali
 
hata kama zina nini huwezi post post nyingi hivo kwa siku watu watachangia vp banaa ?maana post zikiwa nyingi watu wanashindwa kuchangia mwishowe jf litakuwa jukwaa la kupost tu sasa
Akachangie kule fesikibuku!
Na mapicha akabandike!
 
Back
Top Bottom