Afya ya Umma inaweza kudhoofishwa na uwepo wa Taarifa Potofu

JamiiCheck

Member
Nov 3, 2023
54
41
JC AFYA.jpg


Taarifa potofu kwenye afya zinaweza kuwa na athari mbaya kwa watu binafsi na jamii kwa ujumla. Watu wanaweza kufanya maamuzi mabaya ya kiafya ikiwa wanapata taarifa potofu. Wanaweza kujitibu kwa njia isiyo sahihi au kuepuka matibabu ya kisasa kwa kuzingatia habari isiyo sahihi.

Mathlanani, tangu mwaka 1988, idadi ya watoto walioathiriwa na polio imepungua kwa asilimia 99. Ingawa mwisho wa polio unaweza kufikiwa, juhudi za chanjo zimekuwa zinarudishwa nyuma kutokana na uwepo wa taarifa potofu za chanjo, na kuwaweka watoto walio katika hatari kubwa katika hatari.

Pakistani na Afghanistan ni nchi mbili ambazo polio imesalia kuwa janga, ambapo video bandia za watoto wakiugua baada ya kupokea chanjo ya polio zilienea. Taarifa hizo potofu zilisababisha hofu kubwa na kuharibu juhudi zilizopigangwa kwa muda mrefu za kuchanja mamilioni ya watoto kote nchini.

Thabo Mbeki, aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini kuanzia mwaka 1999 hadi 2008, yupo kwenye mjadala mkali kuhusu jinsi serikali yake ilivyoshughulikia janga la UKIMWI kwa kukataa kuwa VVU haikuwa na uhusiano wowote na UKIMWI Pamoja na kukataa mpango wa kuruhusu dawa za kufubaza virusi zitumike nchini kwake kusaidia jitihada za kulikabili janga hili.

Kwa mujibu wa Chuo cha Harvard, zaidi ya watu 330,000 walipoteza Maisha kwa ugonjwa huo huku Watoto zaidi ya 35,000 wakizaliwa na Maambukizi ambayo yangeepukika ikiwa wazazi wao wangekuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi (ARV’s).

Si hapo tu, kuibuka kwa Janga la virusi vya Corona mwishoni mwa mwaka 2019 lilikuza Janga la usambazaji wa taarifa Potofu. Madai ya Chanjo kusababisha mtu kuwa zombi, kuwa na sumaku, kuwa na ugumba au utasa au hata kubadilika kwa vinasaba vya urithi yalirusisha nyuma juhudi za kupambana na janga hili kwa kufanya watu wazikatae chanjo. Madai haya yote yalikanushwa na Shirika la Afya Duniani.

Taarifa Potofu kwenye afya inaweza kuwa na madhara makubwa, ikiathiri maamuzi ya kiafya na huduma za matibabu. Watu wakipokea taarifa potofu, wanaweza kuchukua hatua zisizo sahihi kama vile kutotii miongozo ya kuzuia magonjwa, kukataa chanjo muhimu, au hata kutumia tiba zisizo na msingi wa kisayansi. Hii inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa, kuongezeka kwa matukio ya magonjwa yanayozuilika, na kudhoofisha juhudi za afya ya umma.

Aidha, zinaweza kusababisha hofu isiyo na msingi, kutokuwa na imani kwa wataalamu wa afya, na kuchangia kuchanganyikiwa miongoni mwa jamii, yote yakichangia kwa jumla katika athari mbaya za afya ya umma.

Zaidi, tembelea Jukwaa la JamiiCheck kwa kubofya HAPA.
 
Back
Top Bottom