KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Vladmir Putini

JF-Expert Member
Mar 22, 2022
777
1,442
Huenda ni mimi nilifanya makosa kwa kutopitia terms & conditions vizuri ila hawa jamaa walicho nifanyia ni uzalilishaji mkubwa sana.

Kuna app moja mtandaoni (play store) inaitwa "PESA M FINANCE".

Hawa jamaa walinikopesha elfu 42 mtandaoni kwa muda wa siku 7.

Siku jana nilitakiwa ndiyo nilipe, na jana hiyo nilikuwa kazini nikitegemea nitoke kazini jioni niwalipe pesa yao.

Lakini nashangaa jana mida ya mchana saa saba, watu wanaanza kunitumia kunipigia simu na kunifoadia sms kuwa nadaiwa.

Kumbe hii kampuni ilichofanya baada ya kunikosa hewani jana mda flani, wakatuma sms kwa watu wote walioko kwenye phone book yangu (watu zaidi ya 200) kuwajuza kuwa wananidai na nataka kuwatapeli.

Nikawa napata simu ngingi sana kutoka kwa hao watu waliotumiwa hiyo sms.

Aisee niliona ni udhalilishaji sana hii kampuni imenifanyia.

Sasa nikajiuliza walipataje majina yaliyopo kwenye simu yangu, hapo ndipo nilipokumbuka kwenye app yao ukiwa unafungua kuna sehemu itaandika "allow access to your contacts, messeges n.k" hapo ndipo walipopata majina ya phone book yangu.

Sasa tangu jana hiyo nimekosa raha kabisa baada ya kuzalilishwa na mimi nimeamua kutowalipa mpaka sasa.

Nimepata wazo la kutafta mwanasheria nikawafungulie kesi ya kunidhadhalisha wanilipe fidia, kwanini wanidhalilishe wakati dead line ya malipo ilikuwa bado haijapita.

Screenshot_20240220_200408_Magic SMS~2_1.jpg
Screenshot_20240221_115816_Apex Launcher Classic~2.jpg

Pia soma malalamiko mengine: Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Iwashughulikie Wakopeshaji wa Mtandaoni Wanaodhalilisha Wateja Wao Kwa Kusambaza Taarifa Binafsi Kwa Wasiohusika
 
Hiyo access uliwapa wewe mwenyewe....
Mara ya kwanza ulipoanza kutumia hiyo app ilikutaka uruhusu matumizi kama location,storage na some authority options ndio maana yamekutokea hayo....

Hao dawa yao simu inakua rooted,Una remove acces ya contact unawaomba mkopo,wanakupa....
Unafungua lucky patcher unaedit custom firmware za app halafu unafuta na application
 
Imenishangaza kidogo kwamba simu ina majina zaidi ya 200 lakini hukumuona hata mmoja ktk hao angeweza kuku-save 50K ili umalize shida zako mpaka ukaenda kudhalilika mtandaoni.

Hao walipe tu hela yao but pamoja na hayo upo umuhimu wa wewe kuboresha mahusiano yako na jamaa zako (sisemi unahusiana nao vibaya ila ongeza umakini)
 
Wachana nao
kwani wakitumia watu sms kama hiyo we unapungukiwa nini, songa mbele usirudishe pesa
Wanakupunguzia heshima!

Wapo watu wanakuheshimu na ni muda hawajasikia kutoka kwako so wakiona sms dizain hiyo wanasema huyu jamaa alivyokuwa smart siku hizi amekuwa tapeli anatapeli mpaka mitandaoni?basi siyo wa kumuamini tena na hata siku ukiwatafuta kwa ishu serious hawakusikilizi.
 
Wanakupunguzia heshima!

Wapo watu wanakuheshimu na ni muda hawajasikia kutoka kwako so wakiona sms dizain hiyo wanasema huyu jamaa alivyokuwa smart siku hizi amekuwa tapeli anatapeli mpaka mitandaoni?basi siyo wa kumuamini tena.
na haohao ukiwacheki , aisee nimekwamba wanaweza kukupa link ya playstore udownload loan app 🤣 🤣 🤣
 
Hii adha alikutana nayo PS wa ofisini kwetu, tulimshauri atafute mwanasheria akaogopa akaishia kulalamika. ila yeye case yake ni tofauti kidogo, walimdhalilisha akiwa ameshafanya malipo tayari na wao ndio walichelewa kuconfirm malipo.
Wamenifanyia udhalilishaji sana hawa jamaa.

Mpaka saivi kuna baadhi ya watu wakinipigia simu naogopa hata kupokea.
 
Hiyo access uliwapa wewe mwenyewe....
Mara ya kwanza ulipoanza kutumia hiyo app ilikutaka uruhusu matumizi kama location,storage na some authority options ndio maana yamekutokea hayo....

Hao dawa yao simu inakua rooted,Una remove acces ya contact unawaomba mkopo,wanakupa....
Unafungua lucky patcher unaedit custom firmware za app halafu unafuta na application
Haya maujuzi kwangu kidogo sikuwa nayo mkuu.

Ila nimedhalilika pakubwa sana, hadi kuna demu naona ni kama ananiacha hivi kwa sababu ya sms aliyotumiwa
 
Huenda ni mimi nilifanya makosa kwa kutopitia terms & conditions vizuri ila hawa jamaa walicho nifanyia ni uzalilishaji mkubwa sana.

Kuna app moja mtandaoni (play store) inaitwa "PESA M FINANCE".

Hawa jamaa walinikopesha elfu 42 mtandaoni kwa muda wa siku 7.

Siku jana nilitakiwa ndiyo nilipe, na jana hiyo nilikuwa kazini nikitegemea nitoke kazini jioni niwalipe pesa yao.

Lakini nashangaa jana mida ya mchana saa saba, watu wanaanza kunitumia kunipigia simu na kunifoadia sms kuwa nadaiwa.

Kumbe hii kampuni ilichofanya baada ya kunikosa hewani jana mda flani, wakatuma sms kwa watu wote walioko kwenye phone book yangu (watu zaidi ya 200) kuwajuza kuwa wananidai na nataka kuwatapeli.

Nikawa napata simu ngingi sana kutoka kwa hao watu waliotumiwa hiyo sms.

Aisee niliona ni udhalilishaji sana hii kampuni imenifanyia.

Sasa nikajiuliza walipataje majina yaliyopo kwenye simu yangu, hapo ndipo nilipokumbuka kwenye app yao ukiwa unafungua kuna sehemu itaandika "allow access to your contacts, messeges n.k" hapo ndipo walipopata majina ya phone book yangu.

Sasa tangu jana hiyo nimekosa raha kabisa baada ya kuzalilishwa na mimi nimeamua kutowalipa mpaka sasa.

Nimepata wazo la kutafta mwanasheria nikawafungulie kesi ya kunidhadhalisha wanilipe fidia, kwanini wanidhalilishe wakati dead line ya malipo ilikuwa bado haijapita
View attachment 2910966View attachment 2910967
Hizi kampuni hazina muda mrefu zitafilisika kwa kesi mahakamani,maana Mimi wamenipigia kwamba wananidai wakati hata kumi mbovu haijaingia!
 
Back
Top Bottom