Watu 60 wajiua kwa kuaibishwa na mikopo ya mtandaoni India. Ni kama utapeli unaofanywa Tanzania

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,066
40,725
Uchunguzi wa kijasusi uliofanywa na BBC umegundua yafuatayo.

1) Mteja mtarajiwa hutumiwa meseji akiambiwa kwamba amechaguliwa kupata mkopo wa kiasi flani, hivyo afuate link ya ‘playstore’ ili ku-‘download’ na ku-‘install’ app ya kampuni husika.

2) Wakati wa ku-‘install’, ile app inakuomba ruhusa ya kuingia kwenye ‘contact list’ yako yote, ‘Photo gallery’ yote, ‘Messages’ zote, ‘call log’ yote! Halafu ndani ya dakika chache mkopo wako unaingia.

3) Riba za kampuni husika zinaenda kinyume na matakwa ya kisheria ya nchi husika, mfano ukikopa elfu 40, unaweza kuja kuambiwa ulipe laki 2 kama jumla ya mkopo na riba, hii ni mara 5 ya pesa uliyokopa, na ni kinyume cha sheria za mikopo za BOT.

4) Kampuni husika huwa hazina ofisi popote zaidi ya kuwepo mtandaoni tu, ila huwa inaajiri recovery unit huko vichochoroni na kuwapa training jinsi ya kufanya unyanyasaji/harassment kwa watu waliopitiliza kulipa.

- Hapa wanapitia contact zako zote na kuwatumia meseji kwamba wewe ni tapeli na kukuaibisha na kukufanya usiaminike tena kwao.

- Pia wanapitia meseji zako na kutafuta zile unazotumiana na mchepuko wako, kisha wanatishia kutuma namba ya mchepuko wako kwa mke wako, ambapo hutishia kuharibu na kusambaratisha maisha yako na kuvuruga familia yako. Hapa wanaweza kukublack mail uwalipe hata milioni 2 badala ya laki 2, ni ‘Extortion’ na ‘Intimidation’. Na hakuna kitu BOT wanaweza kufanya, ni TCRA ndio anaweza kufungua App hizo, ila nahisi wana mgao, kwahiyo wanagawana hizi ‘Extortions’.

- Wanapitia picha zako zote za Photo gallery yako na kutafuta zile ulizopiga ukiwa uchi, ukiwa na michepuko, au kama ni shoga unafanya kwa siri na wakakuta picha zako ukiliwa ndio umekwisha kabisa, maana watatuma hizo picha kwenye whatsapp ya baba mkwe, mama mkwe, baba, mama, dada, ndugu, marafiki nk. Huko India watu 60 wameshajiua, hapa Tanzania sijui, mwenye takwimu azilete. Ukitaka wasizitume picha unaweza ukaambiwa lipa milioni 10, wengi wamelipa kunusuru kuaibishwa. Imagine unalipa milioni 10 kwa mkopo wa elfu 20.

Uchunguzi umebaini kwamba muhusika mkuu yupo Hongkong, ambapo ofisi yake inajina lingine kabisa, na hupokea mapato ya ‘unyonyaji’ ambayo hugawana na mamlaka ya usimamizi wa nchi husika, mfano kwa hapo bongo kuna TCRA.

MWISHO.

- Wote mliokopa kaeni kwa akili sana, usije ukapiga picha ya ajabu hata baada ya kuwa umekopa wakati hiyo app bado ipo, au ukatuma meseji kwa mchepuko, au ukaweka simu karibu wakati wa tendo, maana wana hadi live access ya Camera yako bila wewe kujua, wanakusikiliza na wanakurekodi mwanzo mwisho.

- Hizi kampuni hazina uwezo wala eligibility ya kukupeleka mahakamani au popote pale endapo hutolipa, bali wanatumia tu tactics za kukuaibisha na kukudhalilisha hadi ulipe, usipo lipa ndio basi, hawana cha kufanya zaidi ya kuharass ndugu na marafiki zako.

KAMWE USIKOPE KWA HAWA MATAPELI.

————————————————————-

32D8FE55-5F68-4057-A519-D9A42018182E.jpeg

==========================

Uchunguzi wa kijasusi uliofanywa na BBC umegundua yafuatayo.

1.) Mteja mtarajiwa hutumiwa meseji akiambiwa kwamba amechaguliwa kupata mkopo wa kiasi flani, hivyo afuate link ya ‘playstore’ ili ku-‘download’ na ku-‘install’ app ya kampuni husika.

2.) Wakati wa ku-‘install’, ile app inakuomba ruhusa ya kuingia kwenye ‘contact list’ yako yote, ‘Photo gallery’ yote, ‘Messages’ zote, ‘call log’ yote! Halafu ndani ya dakika chache mkopo wako unaingia.

3.) Riba za kampuni husika zinaenda kinyume na matakwa ya kisheria ya nchi husika, mfano ukikopa elfu 40, unaweza kuja kuambiwa ulipe laki 2 kama jumla ya mkopo na riba, hii ni mara 5 ya pesa uliyokopa, na ni kinyume cha sheria za mikopo za BOT.

4.) Kampuni husika huwa hazina ofisi popote zaidi ya kuwepo mtandaoni tu, ila huwa inaajiri recovery unit huko vichochoroni na kuwapa training jisi ya kufanya ‘harassment’ kwa watu waliopitiliza kulipa.
- Hapa wanapitia contact zako zote na kuwatumia meseji kwamba wewe ni tapeli na kukuaibisha na kukufanya usiaminike tena kwao

- Pia wanapitia meseji zako na kutafuta zile unazotumiana na mchepuko wako, kisha wanatishia kutuma namba ya mchepuko wako kwa mke wako, ambapo hutishia kuharibu na kusambaratisha maisha yako na kuvuruga familia yako. Hapa wanaweza kukublack mail uwalipe hata milioni 2 badala ya laki 2, ni ‘Extortion’ na ‘Intimidation’. Na hakuna kitu BOT wanaweza kifanya, ni TCRA ndio anaweza kufungua App hizo, ila nahisi wana mgao, kwahiyo wanagawana hizi ‘Extortions’.

- Wanapitia picha zako zote za Photo gallery yako na kutafuta zile ulizopiga ukiwa uchi, ukiwa na michepuko, au kama ni shoga unafanya kwa siri na wakakuta picha zako ukiliwa ndio umekwisha kabisa, maana watatuma hizo picha kwenye whatsapp ya baba mkwe, mama mkwe, baba, mama, dada, ndugu, marafiki nk. Huko India watu 60 wameshajiua, hapa Tanzania sijui, mwenye takwimu azilete. Ukitaka wasizitume picha unaweza ukaambiwa lipa milioni 10, wengi wamelipa kunusuru kuaibishwa. Imagine unalipa milioni 10 kwa mkopo wa elfu 20.

Uchunguzi umebaini kwamba muhusika mkuu yupo Hongkong, ambapo ofisi yake inajina lingine kabisa, na hupokea mapato ya ‘unyonyaji’ ambayo hugawana na mamlaka ya usimamizi wa nchi husika, mfano kwa hapo bongo kuna TCRA.

MWISHO.

-Wote mliokopa kaeni kwa akili sana, usije ukapiga picha ya ajabu hata baada ya kuwa umekopa wakati hiyo app bado ipo, au ukatuma meseji kwa mchepuko, au ukaweka siku karibu wakati wa tendo, maana wana hadi live access ya Camera yako bila wewe kujua, wanakusikiliza na wanakurekodi mwanzo mwisho.

- Hizi kampuni hazina uwezo wala eligibility ya kukupeleka mahakamani au popote pale endapo hutolipa, bali wanatumia tu tactics za kukuaibisha na kukudhalilisha hadi ulipe, usipo lipa ndio basi, hawana cha kufanya zaidi ya kuharass ndugu na marafiki zako.

KAMWE USIKOPE KWA HAWA MATAPELI.

————————————————————-

View attachment 2911948
Hakuna Nchi Duniani iliwahi fanikiwa kutokomeza Utapeli na wizi,magendo au dawa za kulevya.

Serikali zinachofanya ni kupunguza hali isiwe at alarming rate au kuwa in excess
 
Back
Top Bottom