Taarab kwa wanaume

Taarab kwa wanaume

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,952
Reaction score
25,327
Ukimuona mwanaume yeyote mwenye akili zilizo timia na bila kushurutishwa na mtu yeyote, anashabikia na kucheza muziki wa taarab ujue kwamba kuna hitilafu kichwani mwake.

Hili suala nimekuwa nikilitafakari kwa muda mrefu, hasa ikizingatiwa kwamba taarab ni muziki wa kike, nimekuja kugundua kwamba wanaume wanaoshobokea taarab wana walakini kwenye mbongo zao. Tena utakuta wanaume hao wapo kwenye mduara na wanakata mauno kisawasawa huku wakinyoosha vidole vyao juu! Lahaulah!
 
...ngoja waje wa vidole juu,ingawa mimi hata nikimuona mtu anasikiliza taarab najua nimuweke kundi gani huyo mtu...
 
inawezekana kuna tatizo, kwanini useme .ni muziki wa kike tu,Jesus .ni kwa miaka hii au tangu .zamani !?
 
Ukimuona mwanaume yeyote mwenye akili zilizo timia na bila kushurutishwa na mtu yeyote, anashabikia na kucheza muziki wa taarab ujue kwamba kuna hitilafu kichwani mwake.

Hili suala nimekuwa nikilitafakari kwa muda mrefu, hasa ikizingatiwa kwamba taarab ni muziki wa kike, nimekuja kugundua kwamba wanaume wanaoshobokea taarab wana walakini kwenye mbongo zao. Tena utakuta wanaume hao wapo kwenye mduara na wanakata mauno kisawasawa huku wakinyoosha vidole vyao juu! Lahaulah!
Hata kwa mwanamme kuiba Taarabu,kuna waswas kuwa si riziki.
 
Ukimuona mwanaume yeyote mwenye akili zilizo timia na bila kushurutishwa na mtu yeyote, anashabikia na kucheza muziki wa taarab ujue kwamba kuna hitilafu kichwani mwake.

Hili suala nimekuwa nikilitafakari kwa muda mrefu, hasa ikizingatiwa kwamba taarab ni muziki wa kike, nimekuja kugundua kwamba wanaume wanaoshobokea taarab wana walakini kwenye mbongo zao. Tena utakuta wanaume hao wapo kwenye mduara na wanakata mauno kisawasawa huku wakinyoosha vidole vyao juu! Lahaulah!

Kwa hiyo Mze Yusuph ana hitilafu au?
 
? hebu tuorozeshee miziki ya kike na kiume??? yaan watu wengine cjui mnaposting Uzi mkiwa bar mnapata viroba au kijiwen mnakula mabange!!!!kma hukopend kitu kwa akili zako za kimfumo dume co kila mtu yako ivo.taharabu inapenda pwani hadi bara na jinsia zote wanaburudika.so acha kupost utumbo na kukandia mtu na burudan zake.
 
Ni ngumu kuhukumu hilo jambo ingawa nami nimekuwa nikiona majority ya wahusika wa mziki huo wakiwa wa jinsia ya Ke lakini sidhani kuwa ni sahihi sana kuwahukumu hivyo.

Kuna mziki fulani ambayo wapenzi na waimbaji wake wengi ni Me mfano Hip Hop nk, lakini kuna waimbaji na wapenzi wake wengine ni wa jinsia ya Ke, so sijui kama napo itakuwa right kutoa the same judgment.

Mtoa maada sijui kama ulichoandika ni matokeo ya utafiti ama ni mtazamo binafsi.

cc[MENTION]tpaul[/MENTION]
 
Binafsi nilikuwa naamini hivyo na hasa ile taarab asili kwani ililenga kupeleka ujumbe wa maneno ambayo huonekana tu kuwa kama ya kike kike zaidi.Modern taarab inakitu tofauti kidogo.Unajua baada ya ujio wa hizi fm radio hasa clouds,walitumia nguvu nyingi sana kuua muziki wa dansi na hasa bolingo.Ikaonekana kama ushamba fulani kupenda nyimbo zisizo za wabana pua.Hii yote ni katika kutukuza uzungu.Pamoja na hayo bado sebene lilikuwa ndio aina ya muziki unaokuna hisia za mwafrika(mtanzania) na ndio sababu ikaingizwa kinyemela kwenye muziki wa taarab wao wakaita modern taarab.Tangu hapo wapenzi wengi walianza kuipenda sana na kujipatia mashabiki wa kila jinsi na rika,bara mpaka pwani,na hata nje ya nchi.Hata hivyo inaonekana muziki wa kizazi kipya'wabana pua'wanashika kasi sana na kuheshimiwa sana kuliko wanamuziki wenyewe ambao wengi wako katika bendi za dansi na taarab.Ukisikiliza vituo vya utangazaji karibu asilimia 95 ya muziki wanaopiga ni huu wa usanii wa kutengezewa na mtaalamu wa kompyuta na sio wa vyombo asili.Hii inahitimisha tu ujinga wetu wa kutokujitambua na kujifanya black americans ambao tunadhani wako grade ya juu kidogo kuliko sisi!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Sidhani kama mtoa mada yupo sahihi juu ya hilo. Jaribu kwanza kuitafuta asili ya huo muziki ndipo utajuwa!
 
Ukimuona mwanaume yeyote mwenye akili zilizo timia na bila kushurutishwa na mtu yeyote, anashabikia na kucheza muziki wa taarab ujue kwamba kuna hitilafu kichwani mwake.

Hili suala nimekuwa nikilitafakari kwa muda mrefu, hasa ikizingatiwa kwamba taarab ni muziki wa kike, nimekuja kugundua kwamba wanaume wanaoshobokea taarab wana walakini kwenye mbongo zao. Tena utakuta wanaume hao wapo kwenye mduara na wanakata mauno kisawasawa huku wakinyoosha vidole vyao juu! Lahaulah!

Kila mtu anapenda la kwake, kama wewe hupendi unakaa kimyaa sio kutokupenda kwako kufanye na wengine wasipende na hujatoa sababu za msingi
 
Ukimuona mwanaume yeyote mwenye akili zilizo timia na bila kushurutishwa na mtu yeyote, anashabikia na kucheza muziki wa taarab ujue kwamba kuna hitilafu kichwani mwake.

Hili suala nimekuwa nikilitafakari kwa muda mrefu, hasa ikizingatiwa kwamba taarab ni muziki wa kike, nimekuja kugundua kwamba wanaume wanaoshobokea taarab wana walakini kwenye mbongo zao. Tena utakuta wanaume hao wapo kwenye mduara na wanakata mauno kisawasawa huku wakinyoosha vidole vyao juu! Lahaulah!

Taarab haichezwi hiyo ni rusha roho uisemayo. Taarab mtu anakaa anasikiliza ala na mashairi mwanana.

Upo hapo ulipo?

Pata kitu hiki:

[video=youtube_share;Kvx1nkRi2mA]http://youtu.be/Kvx1nkRi2mA[/video]
 
We jamaa umeongea point tupu. Sasa vidole juu na mwanaume wapi na wapi. Nyimbo zao ni kupondana tu. Uksikilza taarabu lazma uwe mbea na mwanaume hutakiwi kuwa hvyo. Na mashoga wengi wanapenda taarabu.
Hutaki unaacha!
 
Binafsi ni mziki usionivutia kwangu mimi na siupendi kabisa na nikimuona mwenzangu anasikiliza wa kiume simuelewi ingawa kila mtu na starehe zake na kuna watu wakinikuta nasikiliza hip hop nao awanielewi kwahiyo nachukulia kawaida ila ni mziki unaopendwa na mashoga na wanawake ila sio kila wanaume wanaopenda taarabu ni mashoga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom