Swali la Kizushi. Wanaume Vs Wanawake

hapa sina ushahidi...na katika hiyo idadi kubwa unayosema,mm simo...
nawaheshimu wanawake sana nikijua wazi nina mama mpenzi alienilea kwa upendo mpaka leo hii...

Wee ushasifiwa msimamo wako hapo juu na bi Amyner ni dhahiri huwezi badili msimamo lolz
 
Naona wengi mnakubali kua twategemeana. Kama kweli mwaamini hivo ni kwa nini siku zoote idadi kubwa ya wanaume wanakua na dharau saana dhidi ya wanawake?

Si wanaume wote wenye dharau na ukimwona mwanaume anamdharau mwanamke basi ujue anahitilafu katika fikra zake.

Nasema hivyo kwa maana hii:
mwanaume kazaliwa na mama yake ambaye ni mwanamke,
kama mwanaume huyu atamdharau mwanamke basi moja kwa moja atakua amemdharau pia na mama yake kwa kua hata mama yake ni mwanamke.

Kwa ujumla watu wote wanapaswa kuheshimiana kwa kua hakuna aliye mkamilifu kwa maana kua tunategemeana.
 
Neiwa, umenifanya niingie hapa japokuwa nilikuwa nifungue uzi maalumu kwa ajili ya kesho.

Ikiwa kuna mtu anahisi kuwa kuna jinsia inajihisi iko bora kuliko nyengine, huyo hafai hata kuwekwa zoo. Na kuhusu kudharauliana, ingawaje wanaume ndio wanaonekana kuwadharau sana wanawake, tukubali pia wanawake wenyewe nao wanadharauliana na kuwekeana vikwazo katika maendeleo. Mfano mdogo tu, kwa nini asilimia kubwa ya wanawake Tanzania ni wanawake, lakini ikiwa kuna mwanamke jimboni kagombea nafasi, inapofika wakati wa kumpigia kura wanawake wanamchagua mwanamme?

Sababu ya juu juu inawezekana ama wanawake hawaamini uwezo wa mwanamke mwenzao au wanadanganywa kirahisi na wanaume, au pengine yote mawili. Lakini sababu ya msingi nahisi ni mwamko wa jamii juu ya nafasi ya mwanamke katika jamii. Imefika wakati, wanawake muamke, msisubiri "kuwezeshwa" ndio muweze kwani ninaamini mnaweza. Kwa nini muweze kutulea baadae mshindwe kutudhibiti na hata kututawala mkitaka?

HONGERA WANAWAKE WOTE!!!
 
Well said skype!
 
Unayoongea ni kweli tupu. ila wadhani ni kwanini wanaume wengi hawana msimamo huu ulioweka kwenye post hii?
 
Wee ushasifiwa msimamo wako hapo juu na bi Amyner ni dhahiri huwezi badili msimamo lolz

hahahahaaaa...neiwa unataka kubadili MSIMAMO wangu?
unataka kuchoma mahindi kwenye jiko la mchina?
Amy ananisifia mpaka kwenye PM mbona...lolest!
 
Unayoongea ni kweli tupu. ila wadhani ni kwanini wanaume wengi hawana msimamo huu ulioweka kwenye post hii?

Nionavyo mimi ni kua huenda hawatambui majukumu binafsi na majukumu mtegemeano.
Kwa mantiki hii wanaume wengi huchukulia majukumu binafsi kua sawa na majukumu mtegemeano.
Nini namaanisha? Soma hapa chini:

Majukumu binafsi ni yale ayafanyayo mtu kwa manufaa yake kwa mfano kuoga, kushiriki michezo, kupumzika, nk.

Majukumu mtegemeano ni yale wayafanyayo watu kwa manufaa ya wote mfano kusomesha watoto, kufanya kazi kwa bidii, kushauriana, nk.

Aghalabu watu huchanganya majukumu na kujiona wao ndiyo kila kitu kumbe wanatenda isivyotakiwa.

Hayo ndiyo mawazo yangu mkuu sijui wewe wasemaje?
 
Neiwa, umenifanya niingie hapa japokuwa nilikuwa nifungue uzi maalumu kwa ajili ya kesho.

Ikiwa kuna mtu anahisi kuwa kuna jinsia inajihisi iko bora kuliko nyengine, huyo hafai hata kuwekwa zoo. Na kuhusu kudharauliana, ingawaje wanaume ndio wanaonekana kuwadharau sana wanawake, tukubali pia wanawake wenyewe nao wanadharauliana na kuwekeana vikwazo katika maendeleo. Mfano mdogo tu, kwa nini asilimia kubwa ya wanawake Tanzania ni wanawake, lakini ikiwa kuna mwanamke jimboni kagombea nafasi, inapofika wakati wa kumpigia kura wanawake wanamchagua mwanamme?

Sababu ya juu juu inawezekana ama wanawake hawaamini uwezo wa mwanamke mwenzao au wanadanganywa kirahisi na wanaume, au pengine yote mawili. Lakini sababu ya msingi nahisi ni mwamko wa jamii juu ya nafasi ya mwanamke katika jamii. Imefika wakati, wanawake muamke, msisubiri "kuwezeshwa" ndio muweze kwani ninaamini mnaweza. Kwa nini muweze kutulea baadae mshindwe kutudhibiti na hata kututawala mkitaka?

HONGERA WANAWAKE WOTE!!!

Mammamia asante sana kwa kutambua umuhimu wetu na role tunayo play katika jamii..
Tatizo ni kwamba kuna mambo mengi ambayo toka enzi hizo yameonesha kutudidimiza wanawake. Mifumo ya kidini, kitamaduni n.k. Mentality ambayo imeharibu vizazi na vizazi. Taratibu tutajikomboa. Ila WANAWAKE TUPENDANE NA TUPEANE NAFASI YA KUONESHA UWEZO WETU jamani!
 
Nahisi dini na utamaduni vinaweza kutubadilisha mitizamo. Kuna watu waliuliwa kwa kusema tu kuwa dunia ni duara.Mara ya kwanza binadamu alipokwenda mwezi wengine walisema kufanya hivyo ni kukufuru.Tatizo ni kubadilika "mentality"; na mara nyingi kwa makusudi jamii zinashikilia misimamo yao kwa kulinda maslahi yao. Lakini yote yanawezekana ikiwa wanawake wenyewe mtapambana kwa nia na kauli na juhudi moja.
 
Katika Maisha yetu ya kila siku kuna wanawake na wanaume ambao wana interact kwa namna tofauti katika nyanja mbali mbali za maisha. Swali; Ni kundi gani linategemea kundi lenzie kiasi kwamba bila uwepo wa hilo kundi lingine waweza hata potea kabisa?
Hkuna kundi linalomtegemea mwenzie,makundi yote yanategemeana,
Na km moja litatoweka basi na hilo lingine pia litatoweka kwani haliwezi kuishi bila kuwa na kundi lenzake.
 
Back
Top Bottom