Swali Gomvi: Ni nani Unayemwamini na Kwanini?

Kuhusu sakata la mchanga wenye madini; ni nani unayemwamini kuwa anasema kweli?


  • Total voters
    90
  • Poll closed .
Ni nani unayemwamini? Wawekezaji wanaosema "hatukudanganya" au Serikali inayosema "Wamedanganya" na kwanini? Yule usiye mwamini ungependa afanye nini ili umuamini kuwa anachosema ni kweli?

Unaweza kupiga kura hapo juu lakini hapa chini unaweza ukadadavua sababu zako ili tuzidi kubadilishana mawazo na mitazamano na kushawishiana kwa hoja na si vihoja.
Kwa sasa nchi hii mtu aliyebaki kuaminika ni Tundu Lissu, ndo pekee amekuwa consistent tangu nyie mnasainiana mikataba, let's start preparing him for Tz presidency come 2020
 
wallahi natamani kweli niamini tume kwa uzalendo wangu ila tatizo taarifa za tume zimekuwa nzuri kupindukia kwa mtu anaefikiri vizuri kuaminiwa kwasasa nipo 50/50 waswahili wanasema shilingi imesimama
 
Nawaamini acacia kwa sababu procedure za kuchukua sampuli, kukokotoa 'grade, tonnage, metal content & recovery' ni za uwazi na zinakubalika kimataifa tena hizo parameters zote zinapatikana kwa kuzishirikisha idara za serikali kama TRA, TMAA, mineral residential officers etc baada ya kuchukua sampuli na kuzipeleka kwenye maabara za nje na ndani!
Nina uhakika kabisa nikimuuliza Mruma amepata vipi hizo data kutoka kwenye makontena zaidi ya 200 alizo mkabidhi muheshimiwa na kuutangazia umma wa watanzania anaweza kujikojolea kama si kuji***a kabisa!
we nahc sio mtanzania wewe
 
Najali kuchangia hapa.

Najali kujibu swali la kura aliyoanzisha Mwanakijiji.

Zaidi ya hapo sijali na ndo maana sijaandika zaidi ya nilichoandika.
Ndo unajali-hujali sasa.

Kuna wengine hawajali kabisa hata wakichungulia wanaona huyu Mwanakijiji mzushi tu wanapotezea.

Hao hawajali-hawajali.
 
Tume haikuwa huru. Imeundwa na Magufuli wakati ambapo Magufuli alishasema wazi msimamo wake hasi dhidi ya haya makampuni. Wajumbe waliounda tume iliyochunguza hili sakata walionekana wazi wakati wa kuwasilisha kwamba walikuwa na shauku ya kumpa Magufuli matokeo aliyoyatarajia (kwamba ACACIA ni wezi). Kwa kifupi, ilihitajika tume huru, siyo tume ya kuteuliwa na upande mmoja.

ACACIA. Sina sababu ya kuwaamini. Sina sababu ya kuwatilia mashaka pia. Sijaona ushahidi wa kimahakama wa ACACIA kuwa wezi. Ninachosikia ni tuhuma tu dhidi yao.

The whole thing smells like a political stunt by the accuser.
yani wewe akili yako imekaa kisiasa siasa tuuu
do u really think that the whole thing is just politics ??
https://jamii.app/JFUserGuide off
 
Ndo unajali-hujali sasa.

Kuna wengine hawajali kabisa hata wakichungulia wanaona huyu Mwanakijiji mzushi tu wanapotezea.

Hao hawajali-hawajali.

Hahaha naona unacheza tu na maneno hapo!

Maswali ya kura ya Mwanakijiji umeyaona lakini?

Vyovyote iwavyo, sijali.

Waibe, sawa. Wasiibe, sawa tu.

Wachimbe, sawa. Wasichimbe, sawa tu.

Wabaki, sawa. Waondoke, sawa tu.

Vyovyote vile, sawa tu.
 
Hahaha naona unacheza tu na maneno hapo!

Maswali ya kura ya Mwanakijiji umeyaona lakini?

Vyovyote iwavyo, sijali.

Waibe, sawa. Wasiibe, sawa tu.

Wachimbe, sawa. Wasichimbe, sawa tu.

Wabaki, sawa. Waondoke, sawa tu.

Vyovyote vile, sawa tu.
The dark nihilistic tendencies of a fashionable anarchist is the grotesque nonchalant fueling tethered to the unpatriotic arson of our dear motherland.
 
..suluhisho ni serikali kuchukua jukumu la kusafirisha, kutafuta smelter ya kuchambua mchanga, na baadaye kuuza kilichomo ktk mchanga huo. Baada ya hapo wawakatie acacia kiasi chao, na sisi tusepe na kilicho chetu.

..halafu naona tumebeba bango kuhusu mchanga. Je dhahabu inayochimbwa tumejiridhisha kwamba hawatupunji?

Cc Nguruvi3
Hivi unaweza kuyasafirisha tu hayo makontena kama mzururaji huku ukitafuta hizo smelter au kuna utaratibu wowote?
 
Hivi unaweza kuyasafirisha tu hayo makontena kama mzururaji huku ukitafuta hizo smelter au kuna utaratibu wowote?

..LOL!!

..wafuate utaratibu.

..ama serikali ijenge smelter hapa nchini ,au ipeleke mchanga huo nje ya nchi ukachambuliwe.
 
Naamini ripoti ya tume na Raisi Magufuri,lakini sina imani na serikali kwa maana ya watumishi ipo at crossroad.Pia kuna influence kubwa ya waovu (king makers)wanaimiliki serikali kana kwamba ni gang la Mafia.
Lakini Raisi Magu akianzisha kampaini ya kuswaga mafisadi papa walioibia matrioni ya migodi nitaiunga serikali mkono.
 
Hivi tuliibiwaje wakati TMAA wapo!, Wizara ya madini ipo!, STAMICO ipo!.
Kama taasisi hizi zote zina data za kutosha kuhusu kiwango cha madini na hata projections za expected percentage ya madini kwenye concentrates basi lawama ni yetu sisi wenyewe!.

Kiufupi tukabane mashati sisi wenyewe, maana wawekezaji it seems tulikuwa na roho nzuri sana kwao kuwaacha eti " watudanganye",

Kiufupi hata dhana yenyewe ya kwamba tulidanganywa inatutia aibu, yaani mmedanganywa kwa miaka yote hiyo 15 mliyoanza uzalishaji!. Je vipi kuhusu data zetu wenyewe kuanzia tulipoanza utafiti wa madini nchini toka miaka ya 1970s enzi za mwalimu, tuna data zinazoshabihiana na tume au za ACACIA kwenye michanga?
 

Hakuna shaka kwa hapa tulipofikia Lazima kuiamini serekali KIKAMILIFU!


Hao ACACIA sio wakuamini kabisa anyway kwanini wasijitetee ..! Kwa uharamia wa wazi kabisa wanaofanya.

Watanzania lazima kuwa wamoja na kushikana kwenye hii vita sio vita ndogo. Inabidi kuweka tofauti zetu zote kando na kuja pamoja kwenye hili kama Taifa.
Unadhani hatatukiwa wamoja kama sharia za mikataba zimekiukwa tutazibadili zisoma tutakavyo sisi?
Mda wakuwa pamoja tayali rais ameuruka kwamaana alipaswa kuwakusanya wataalamu wa sheria na mikataba na uchumi wakayajenga kabla ya hatua aliyochukuwa.
Tusubili vyombo vya haki tu
 
Nawaamini Acacia
Ila vita ya madawa ya kulevya haijawahi kumuacha mtu salama
 
Kutokuwepo kwa independence ya kamati imepunguza credibility ya ripoti yao. Mh Rais tayari alikuwa na conclusion yake kuhusu huo mchanga na aliweka wazi. Je kamati ilikuwa na uthubutu wa kiasi gani kutoa matokeo ambayo yangeonesha Mh Rais alisema/alituhumu vya uongo?

Hata hivyo kuwepo au kutokuwepo kwa independence ya kamati peke yake hakuondoi ukweli (kama ni kweli) wa findings zao. Kinachoathirika ni kiwango gani ukweli huo utaaminiwa na watu wengine wenye maslahi na jambo hilo?

Wengine tumeshauri serikali inunue kwa thamani ambayo acacia wanaiamini au kupiga mnada mchanga huo ili kupata thamani halisi.
 
Back
Top Bottom