Swali Gomvi: Ni nani Unayemwamini na Kwanini?

Swali Gomvi: Ni nani Unayemwamini na Kwanini?

Kuhusu sakata la mchanga wenye madini; ni nani unayemwamini kuwa anasema kweli?


  • Total voters
    90
  • Poll closed .
kwenye mambo ya trust, the most trusted ni the most experienced! .
Paskali


Trust is irrational. Watu wameshalishwa sumu kwamba haya makampuni yapo nchini kutuibia, wanaiamini serikali ambayo haitaki kuonyesha hiyo mikataba iliyoingia na haya makampuni hata kwa wabunge. To be fair to both serikali (Magufuli) and ACACIA, hili suala lipimwe kwa mizani ya kisheria tu.
 
Binafsi simuamini yeyote.........ACACIA kama wafanyabiashara sio wa kuamini 100%, sababu maono yao yote ni kutengeneza faida, tena faida kubwa, so kwa vyovyote wanaweza kudanganya. lkn pia Serikali, Serikali yetu kwa miaka mingi imekuwa ikipigiwa kelele kuwa tunaibiwa, wapinzani wameongea sana, lkn wakaonekana wanafiki na wenyewe wivu wa kike, Leo mh.Magufuli anayafanya haya, naamini ni kwa nia njema, kama ni kwa nia njema, nilitamani aliposomewa ile ripoti basi angetoa agizo mikataba yote ya madini iangaliwe upya, ama ipelekwe bungeni au ile tume aliyoiunda iipitie upya hiyo mikataba, hapo ndio tuanze kucheza ngoma na nao ACACIA, kama ni kutulipa au kuwatimua kwa kukiuka mikataba.
 
Binafsi simuamini yeyote.........ACACIA kama wafanyabiashara sio wa kuamini 100%, sababu maono yao yote ni kutengeneza faida, tena faida kubwa, so kwa vyovyote wanaweza kudanganya. lkn pia Serikali, Serikali yetu kwa miaka mingi imekuwa ikipigiwa kelele kuwa tunaibiwa, wapinzani wameongea sana, lkn wakaonekana wanafiki na wenyewe wivu wa kike, Leo mh.Magufuli anayafanya haya, naamini ni kwa nia njema, kama ni kwa nia njema, nilitamani aliposomewa ile ripoti basi angetoa agizo mikataba yote ya madini iangaliwe upya, ama ipelekwe bungeni au ile tume aliyoiunda iipitie upya hiyo mikataba, hapo ndio tuanze kucheza ngoma na nao ACACIA, kama ni kutulipa au kuwatimua kwa kukiuka mikataba.
 
1. ACACIA's too little, too enclosed, too much NDA-ish. Too much questionable, too much 'we didnt' than this is what has been done
2. Committee's bloated, too much (ultra-)resource nationalistic. Sentimental, attention seeking of sorts, ugly we-couldve-done-it-ourselves attitude that works not in these times.

None of which makes any bloody sense!
Samahani mimi, Deo Sanga na Msukuma tunaomba tafsiri
 
Ubishi wa kipimo chochote kile huamuliwa na MTU wa tatu(Third Party).Ilipaswa hiyo tume pamoja na Acacia wachukue containers tatu randomly wapeleke maabara na smelters tatu tofauti wakiwa pamoja katika upimaji huo waone kitakachotokea.Tume imetumia maabara jee imefanya smelting halisia?Upimaji ufanywe pamoja sii upande mmoja

Mzee Mwanakijiji
 
Tukiweka uzalendo pembeni CCM niwaongo awajawai kutokea Afrika mashriki na kati
 
Hapa ngoja na mimi kwa elimu yangu ndogo yauchimbaji mdogomdogo ni seme kitu.kiwango cha dhahabu kilicho tolewa na Mruma katika kila kontena ni kikubwa sana kiasi cha mtu ana jua prosses ya dhahabu ata staajabu. Nasema hivyo kwa sababu kiwango kama hiki nikikubwa kiasi kwamba body ore(mkanda wa dhahabu) kule underground lazima dhahabu znge onekana kwa macho,hapa na maanisha visible gold yaani jiwe likiwa na dhahabu nyingi lazima uzione kwa macho najiweka lisilo na dhahabu nyingi huwezi kuziona. Nasema haya kwa sababu nishafanya kazi bulyanhulu underground nautalamu wangu wakujua dhabu mpaka naacha kazi sijawahi ona jiwe lina dhahabu zaidi ya kuona mashaba mengi. Ilifikia kipindi ikabidi niwafate jiolojisti niwaulize niwapi ambapo pana ore gredi ya juu?
Wale jamaa wakanieleza maeneo fulani wakaniambia pana gm500/tn.hapa ndobado naitafakari taarifa ya Mruma je kunaukweli?

Ila nimekaa nikatafakali nikaona inawezekana kabisa hicho kiwango cha dhahabu kikawepo tena ata na zaidi ujue kivipi?

Hapa muelewe wa tz kama acacia kweli alikuwa anakwepa mapato huenda alikuwa anafanya prosses ya ku tikisa mchanga,hapa unapofanya hii prosses kiwango kikubwa cha dhahabu kinakimbilia chini.

Huenda hapa ndipo acacia huchukua ule mchanga wa dhahabu ulio na dhahabu nyingi tayari kwa kusafirisha.

Nahii ieleweke kwamba hapa kuna mashne inaitwa shaking mashine hii ndo ina lahisisha hii kazi.nje na hapo hakuna ore body inayo soma kiwango cha juu cha zahabu kiasi cha tarifa ya Mruma. Haya ni mawazo yangu.



l
 
..suluhisho ni serikali kuchukua jukumu la kusafirisha, kutafuta smelter ya kuchambua mchanga, na baadaye kuuza kilichomo ktk mchanga huo.
Baada ya hapo wawakatie acacia kiasi chao, na sisi tusepe na kilicho chetu.

..halafu naona tumebeba bango kuhusu mchanga. Je dhahabu inayochimbwa tumejiridhisha kwamba hawatupunji? Nguruvi3[/USER]
Nadhani serikali inapaswa kuwa na data za uhakika kwa kuchambua mchanga. Hoja ya 'extrapolation' kwamba container A lina kiasi X hivyo container 600 zina kiasi Z, inakuwa defeated kirahisi,siyo scientific kwa mtizamo wa vipimo

Acacia wana nguvu za kueleza uonevu wakitimka, madhara yatakuwa ya muda mrefu

Kuhusu dhahabu hiyo nayo ni hoja. Zile ndege zinazotua tunajua zinaondoka na nini?

Swali la Mzee Mwanakijiji . Nani anaaminika naweza kusema ni Acacia

Kabla ya kueleza sababu, nisema pia Acacia hawakudanganya.
Wangesafirisha mafuta wakati mkataba ni uchimbaji madini tungesema wamedanganya.

Hapana! wanachimba tulichokubaliana wafanye , hawajadanganya

Kuna mkataba tuliosaini , tuna Watanzania katika bodi, ipo wizara na taasisi ya TMAA

Kwa miongo takribani miwili hakuna aliyesema kuna udanganyifu. Kwanini tuamini upo!!!

Zitto alipoibua hoja ya udanganyifu, Bunge lilimuadhibu na si kutafuta ukweli.
Acacia wamedanganya wapi!. Serikali ikaunda tume ya Bomani na kukabidhi taarifa

Hakuna anayejua nini kilikuwemo serikali haikuta wananchi wajue. Acacia wamedanganyaje?

Tume ilitoa taarifa na Acacia wakaendelea kuruhusiwa kusafirisha mchanga mchana kweupe.
Kwanini tudhani walitudanganya ikiwa kontena zinapita bandarini. Hawakudanganya

Tunawazeaje kusema wamedanganya ikiwa hakuna miongoni mwetu aliyeona mkataba!

Wako wapi waliotia saini mkataba watueleze kama Acacia wamedanganya!

Prof Mruma alipaswa atuonyeshe mkataba na jinsi ulivyokiukwa hata kupelekea kuibiwa

Alichotuonyesha ni kuibiwa, je, tuamini tu tunaibiwa hata kama mkataba unasema wasombe mchanga?
 
La msingi mikataba inasemaje? Wakati miswada ya sheria za madini inaletwa kwa hati ya dharura na serikali (baraza la mawaziri) Magufuli alikuwa Senior minister ndani yake, na wapinzani walipohoji waliitwa majina mengi ya hovyo na kukebehiwa. Leo tunapongeza nini hapo? Utapeli mtupu!
 
Nadhani serikali inapaswa kuwa na data za uhakika kwa kuchambua mchanga. Hoja ya 'extrapolation' kwamba container A lina kiasi X hivyo container 600 zitakuwa na kiasi Z, inakuwa defeated kirahisi kwasababu siyo scientific katika mtizamo wa vipimo

Acacia watakuwa na nguvu za kueleza uonevu hata kama watatimka, madhara yatakuwa ya muda mrefu

Kuhusu dhahabu hiyo nayo ni hoja. Zile ndege zinazotua tunajua zinaondoka na nini?

Swali la Mzee Mwanakijiji . Nani anaaminika kuhusu suala naweza kusema ni Acacia
Kabla ya kueleza sababu, nisema pia Acacia hawakudanganya.

Kama wangesafirisha mafuta wakati mkataba unasema ni uchimbaji madini tungesema wamedanganya.
Hapana, wanachimba tulichokubaliana wafanye , hawajadanganya

Kuna mkataba tuliosaini nao, tuna Watanzania katika bodi, ipo wizara na taasisi ya TMAA zinazosimamia Kwa miongo takribani miwili hakuna aliyesema kuna udanganyifu. Kwanini basi tuamini upo!!!

Zitto alipoibua hoja ya udanganyifu, Bunge liliamua kumuadhibu na si kutafuta ukweli. Acacia wamedanganya wapi!. Serikali ikaunda tume ya Bomani na kumkabidhi Rais taarifa

Hakuna anayejua nini kilikuwemo kwasababu serikali haikuta wananchi wajue. Acacia wamedanganyaje?

Tume ilitoa taarifa na Acacia wakaendelea kuruhusiwa kusafirisha mchanga mchana kweupe.
Kwanini tudahni walitudanganya ikiwa kontena zilikuwa zinapita nadnarini bila shaka. Hawakudanganya

Tunawazeaje kusema wamedanganya ikiwa hakuna miongoni mwetu aliyewahi kuona mkataba!

Wakowapi waliotia saini mktaba watueleze kama Acacia wamedanganya!

Prof Mruma alipaswa atuonyeshe mkataba na jinsi ulivyokiukwa hata kupelekea kuibiwa
Alichotuonyesha ni kuibiwa, je, tuamini tu tunaibiwa hata kama mkataba unasema wasombe mchanga?
Mzee wewe ni mfalme wa twist za kisiasa ...nakusoma mpaka nachoka sana ....yaani Mruma athibitishe wizi kimkataba while unajua hata mikataba yenyewe ni wizi tu? ...hivi hapa tunataka kumchoresha JPM au taifa? ...yaani kwavile tulishakosea kwenye mikataba tusiwe na sehemu ya kuanzia kujadili mikataba yenyewe? .....Walau wanao argue takwimu zilizotolewa na tume unaweza kuona hoja mahali lakini si kwa hoja Kama hizi kutoka kwa moja wa wachambuzi nguli kama wewe humu JF ....
 
Mzee wewe ni mfalme wa twist za kisiasa ...nakusoma mpaka nachoka sana ....yaani Mruma athibitishe wizi kimkataba while unajua hata mikataba yenyewe ni wizi tu? ...hivi hapa tunataka kumchoresha JPM au taifa? ...yaani kwavile tulishakosea kwenye mikataba tusiwe na sehemu ya kuanzia kujadili mikataba yenyewe? .....Walau wanao argue takwimu zilizotolewa na tume unaweza kuona hoja mahali lakini si kwa hoja Kama hizi kutoka kwa moja wa wachambuzi nguli kama wewe humu JF ....
Mkuu usichoke, tujadiliane.
Umejuaje mikataba ni wizi? Huu wa Acacia umewahi kuuona?

Nauliza hivyo kwasababu IPTL walishinda kesi kwasababu ya mkataba unavyosema

Nimeeleza hoja, kama hatujui mkataba unawaruhusu wafanye nini, tunawezaje kuamini tu taarifa ya kwamba tunaibiwa? Mkuu huoni mantiki hapo.

Nitakuwa nimekuibia kama nitaingia shambani kuchukua mananasi yako kienyeji.
Nikiingia kwasababu kuna mkataba wa biashara sijakuibia isipokuwa kama mkataba ni wa mananasi nikachimba mihogo na mlenda na kuweka katika gunia, nitakuwa nimekuibia

Haitoshi tu kusema hivyo, ninapaswa kuonyesha kuwa mkataba hauruhusu kuchukua mihogo na mlenda

Hoja ya pili, wale walioandika mkataba wako wapi watueleze, naam kilichoonekana ni kweli kwasababu siku wanasaini hakuna kipengele cha mchanga ubebwe!

Tatu, tulikuwa na wizara, tukawa na taasisi ya TMAA, na bahati nzuri wapo Watanzania katika bodi.
Ilikuwaje hawakuona tunaibiwa wakati wote hadi Mruma atoke nje na kutueleza tunaibiwa?

Nne, tatizo la madini si limeelezwa bungeni. Taarifa ya Tume ya Bomani uliwahi kuiona?
Kama hukuiona, tume iliundwa kwa ajili gani na Taifa lilinufaika vipi kiasi cha kudhani tunaibiwa?

Tano, tunazungumzia mchanga 'zile Cesna' tunajua zinaondoka na nini? Huhitaji 747 !

Tusishangilie tu mambo lazima tuyaangalie kutoka kona zote.

Ujinga wetu si excuse hata kidogo unless tuhalalishe ujinga kama ndio weledi wetu.
 
...hivi hapa tunataka kumchoresha JPM au taifa? ...yaani kwavile tulishakosea kwenye mikataba tusiwe na sehemu ya kuanzia kujadili mikataba yenyewe?
Vema, wala sijakataa suala zima la mchanga lilivyo. Ninachokataa ni kudhani hili limetokea kwa bahati mbaya. Ninachokataa ni kuwahukumu Acacia bila kuona upande wa pili wa shilingi.

Kama tumekosea ni uzembe wetu, tunaposahihisha makosa si ushujaa ni sehemu ya kujirudi
Waliotufikisha hapa si walikuwepo wakati mikataba inapelekwa kwa 'Fedex' Bungeni

Si hao ndio walikuwa 'ndiyoo' bila kujua mfanyabiashara Acacia ameandika nini
Si tulikuwa na wanasheria kama ilivyokuwa mikataba mingine

Unakumbuka kiongozi mmoja aliyetuingiza mkataba mbovu ni mwenyekiti wa vikao vya Bunge
Kwamba ana oversee shughuli za Bunge ikiwemo mikataba.

Yaani umkabidhi fisi ulinzi wa bucha ya nyama, kesho useme nyama imeliwa bila idhini yako!

Tunajichoresha wenyewe hilo lazima tukiri ili tuweze kwenda mbele.

Upo msemo' tatizo si tatizo tena ikiwa unajua chanzo'' hapo ndipo tusimame na kuweka 'kauzalendo pembeni'

Wazalendo Bungeni hawataki kujadili mikataba, seuse wewe na mimi. Nani mkatoliki zaidi ya Pope

Tukubali makosa ,tukae chini na kuiuliza akina walitenda, nani walihalalisha na nini kifanyike

Si suala la ku score political points kwasababu imefanyika tukiwa ahatuna uhakika kama ni vema
 
Magufuli simuamini sababu alikurupuka ishu ya meli ya uvuvi na kuipa hasara serikali. Kuhusu ishu ya dhahabu anajua wazi hatuna uwezo wa kuichimba, anagombana na wawekezaji ili iweje? Kilichotakiwa ni kuipitia mikataba upya au awalipe wasepe.
 
Mtu akisema Acacia wamekula njama na serikali kuwahujumu Watanzania wakati Magufuli akionekana kinara wa kupigania haki za Watanzania siwezi kukataa.

Kwa sababu.

1. Magufuli alishiriki kupitisha mikataba mibovu. Hakuipinga wala kujiuzulu. Imepitishwa maana yake aliipitisha. Collective Responsibility applies.

2. Hata kama alitakakuwa rais, kawa rais mwakammoja na nusu. Alikuwa anasubiri nini kuvunja mkataba sasa?

3. Kama atasema alikuwa anajipanga,kujipanga kungehusisha kuitoa Tanzania katika international conventions zinazo govern mikataba hii ili arbitration isifnyike London ningeelewa.Tundu Lissu kaandikajinsi Evo Morales alivyofanya hivyo. Alijitoa katika conventions kisha akavunja mikataba. Ukivunja mkataba kiholela unawapa wawekezaji uwezo wa ku sue na kulipwa damages.

4. Inaonekana kama Magufuli na genge lake walikubali mikataba mibaya. Wawekezaji wamechimba madini mpaka wanaona yanakaribia kuisha, wamepanga mpango na serikali ili serikali ivunje mkataba kiholela na kuonekana inapigania haki za Watanzania, halafu kesi ikienda Londoan, wawekezaji washinde na kula bingompya ya IPTL. Kwa hivyo mtu akiuliza "why now and not earlier?" jibu linaweza kuwa wawekezaji wameona sasa wanamaliza kuchimba madini, wamesuka mchezo na serikali waanzishiwe kesi halafu washinde kesi halafu walipwe fidia bila kuchimba madini.

Mtu akisema hivyo, kwa jinsi Magufuli anavyofanya maamuzi kwa pupa kama hana ujuzi na mambo ya mikataba, nani anaweza kubishia hii theory?
 
Back
Top Bottom