Swali Gomvi: Ni nani Unayemwamini na Kwanini?

Kuhusu sakata la mchanga wenye madini; ni nani unayemwamini kuwa anasema kweli?


  • Total voters
    90
  • Poll closed .

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,742
40,873
Ni nani unayemwamini? Wawekezaji wanaosema "hatukudanganya" au Serikali inayosema "Wamedanganya" na kwanini? Yule usiye mwamini ungependa afanye nini ili umuamini kuwa anachosema ni kweli?

Unaweza kupiga kura hapo juu lakini hapa chini unaweza ukadadavua sababu zako ili tuzidi kubadilishana mawazo na mitazamano na kushawishiana kwa hoja na si vihoja.
 
1. ACACIA's too little, too enclosed, too much NDA-ish. Too much questionable, too much 'we didnt' than this is what has been done
2. Committee's bloated, too much (ultra-)resource nationalistic. Sentimental, attention seeking of sorts, ugly we-couldve-done-it-ourselves attitude that works not in these times.

None of which makes any bloody sense!
 
Acacia wanadanganya hao. Walivyo waona wale wenzetu tuliowaweka pale kuwa angalia wasituibie, wakaziona njaa zao, Tizama, waliwalambisha muwa wakajisahau kutazama kazi zao, wakabaki kuguguna muwa. Mali si zikapita?? Ndo maana JPM kasema, wachunguzwe, wakibainika wapelekwe mahakamani. Tunmatizamia watu wafilisiwe.
Serekali, imechukua maamuzi ya haraka mno. Wangekaa chini, wajadiliane jambo hili ndani ya ukumbi maalum uliosheheni wanasheria. Kwa kuwa hili jambo ni la kisheria. Wakiona tutashinda ndio wamshauri JPM akamate makontena husika.
Lakini, kama kweli uchunguzi uliofanywa utaonesha hata robo kilo ya madini ambayo hayaku be declared na ACACIA, nasema, B/up sana JPM.
 

Hakuna shaka kwa hapa tulipofikia Lazima kuiamini serekali KIKAMILIFU!


Hao ACACIA sio wakuamini kabisa anyway kwanini wasijitetee ..! Kwa uharamia wa wazi kabisa wanaofanya.

Watanzania lazima kuwa wamoja na kushikana kwenye hii vita sio vita ndogo. Inabidi kuweka tofauti zetu zote kando na kuja pamoja kwenye hili kama Taifa.
 
Nawaamini acacia kwa sababu procedure za kuchukua sampuli, kukokotoa 'grade, tonnage, metal content & recovery' ni za uwazi na zinakubalika kimataifa tena hizo parameters zote zinapatikana kwa kuzishirikisha idara za serikali kama TRA, TMAA, mineral residential officers etc baada ya kuchukua sampuli na kuzipeleka kwenye maabara za nje na ndani!
Nina uhakika kabisa nikimuuliza Mruma amepata vipi hizo data kutoka kwenye makontena zaidi ya 200 alizo mkabidhi muheshimiwa na kuutangazia umma wa watanzania anaweza kujikojolea kama si kuji***a kabisa!
 
Naiamini serikali kwasababu imeundwa tume makini iliyokuja na issues zilizolalamikiwa miaka mingi. Statement ya ACACIA ilikuwa na lengo la kutuliza upepo huko kwenye stock exchange while trying to solve the issue ....
 
ACACIA Wana hoja ya msingi. Ila huwezi amua nani wa kumwamini mpaka ipatikane ripoti kamili inayoonyesha "among other things", methodologies, who and where the samples were analyzed, credibility(international) of the analyzer and other things. Tatizo la watanzania walio wengi wanachukulia haya mambo kiurahisi-rahisi. Kwenye mambo haya kama tukiangukia pua tutaomba ardhi ipasuke tujifiche na haitapasuka. Tunatakiwa kuwa na proper legal standing na sio siasa.
 
Naiamini serikali inaposema tulidanganywa sana na kwa muda mrefu tumeibiwa sana. Tatizo ni kwamba kwa sababu ya uongozi mbovu katika sekta ya madini tumeibiwa huku tunaona tena huku sheria ikionekana kuwa na uwezo wa kuwalinda wawekezaji "majizi" sababu ya mikataba mibovu tuliosaini.

Nashauri kuwa namna nzuri ya kushughulika na majizi haya ni kuvunja mikataba kisheria na hata kwa gharama itumike ili kujitoa kwenye makubaliano mbali mbali yanayolinda majizi, bila kuvunja sheria.
 
Kabla niliwaamini acacia kwa sababu data zao zilifanana kwa karibu na watu wa TMAA na watu waliowahi kutumwa na serikali kutafiti makinikia 2011 Ila sasa naiamini tume ya Magufuli Bila Shaka, ntabadilika ikitokea wamekuwa challenged kwa tafiti na takwimu za kisomi huku wao wakishindwa kutetea walichokigundua.
 
..suluhisho ni serikali kuchukua jukumu la kusafirisha, kutafuta smelter ya kuchambua mchanga, na baadaye kuuza kilichomo ktk mchanga huo. Baada ya hapo wawakatie acacia kiasi chao, na sisi tusepe na kilicho chetu.

..halafu naona tumebeba bango kuhusu mchanga. Je dhahabu inayochimbwa tumejiridhisha kwamba hawatupunji?

Cc Nguruvi3
 
Nawaamini acacia kwa sababu procedure za kuchukua sampuli, kukokotoa 'grade, tonnage, metal content & recovery' ni za uwazi na zinakubalika kimataifa tena hizo parameters zote zinapatikana kwa kuzishirikisha idara za serikali kama TRA, TMAA, mineral residential officers etc baada ya kuchukua sampuli na kuzipeleka kwenye maabara za nje na ndani!
Nina uhakika kabisa nikimuuliza Mruma amepata vipi hizo data kutoka kwenye makontena zaidi ya 200 alizo mkabidhi muheshimiwa na kuutangazia umma wa watanzania anaweza kujikojolea kama si kuji***a kabisa!
Mie nafikiria wewe unajitoa ufahamu
Unaongelea Sampuli, kukokotoa, grade, tonnage, metal content and recovery...........
Wakati sampuli iliyochukuliwa na tume imeleta matokeo tofauti...
Tonnage wamekuta container lina mpaka tons 23 over
Tume imekuta madini aina chungu nzima ambayo hayakuonyeshwa kwenye document tangu wameanza kuchimba,
Mbona bado wenye migodi lazima wajambe cheche.
Wakitoka kwenye dhahabu wanahamia kwenye Tanzanite
 
Tume haikuwa huru. Imeundwa na Magufuli wakati ambapo Magufuli alishasema wazi msimamo wake hasi dhidi ya haya makampuni. Wajumbe waliounda tume iliyochunguza hili sakata walionekana wazi wakati wa kuwasilisha kwamba walikuwa na shauku ya kumpa Magufuli matokeo aliyoyatarajia (kwamba ACACIA ni wezi). Kwa kifupi, ilihitajika tume huru, siyo tume ya kuteuliwa na upande mmoja.

ACACIA. Sina sababu ya kuwaamini. Sina sababu ya kuwatilia mashaka pia. Sijaona ushahidi wa kimahakama wa ACACIA kuwa wezi. Ninachosikia ni tuhuma tu dhidi yao.

The whole thing smells like a political stunt by the accuser.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ni nani unayemwamini? Wawekezaji wanaosema "hatukudanganya" au Serikali inayosema "Wamedanganya" na kwanini? Yule usiye mwamini ungependa afanye nini ili umuamini kuwa anachosema ni kweli?

Unaweza kupiga kura hapo juu lakini hapa chini unaweza ukadadavua sababu zako ili tuzidi kubadilishana mawazo na mitazamano na kushawishiana kwa hoja na si vihoja.
kwenye mambo ya trust, the most trusted ni the most experienced! .

Hii iliwahi kutokea hapa
Kauli tata za Mkulu
I believe in "better be sure than sorry!", kuna haraka gani?!. Hilo la milioni 7 au 8 kwa dakika, japo ni kweli, ila limegeuka kichekesho!, kama rais anaweza kusema vitu ambavyo haviaminiki, then nani wa kuaminika?!.

Milioni 7 au 8 kwa dakika ni shocking!, watu wameingia shock, mwisho wa siku hata bilioni 100 !, hazijafika, watu wikihesabia ni matrilioni!. Hizi mimi naziita ni comedies!, comedy awaachie ma comediana kina Joti na Masanja , but not him with full info facts at his finger tips!, we expect hard facts na sio guess work ya sijui hivi, au sijui vile!, hizo ni zetu sisi huku jf na sio pale mahali patakatifu petu!, urais ni taasisi ya presidential, sasa mtu anapokuwa president, hata kama hapo kabla haukuwa a presidential material, lakini unapochaguliwa wewe kuwa president unapaswa lazima ubadilike na kuivaa hiyo taasisi ya presidential kwa kujitahidi kuwa presidential material kws kufikiri, kusema na kutenda ki presidential!.

Kwa baadhi yetu sisi ma conservatives kiukweli tunatatizwa sana na hizi kauli za paying "lip services", just for political capitalization na nyingine ndio hizi sasa zinakuja kugeuka ze comedy!.

Paskali
Wakuu MsemajiUkweli na jingalao, kiukweli tunatofautiana sana humu jf katika uwezo wa kusoma bandiko la mtu, kila anayejua kusoma na kuandika, anaweza kusoma chochote na kuandika chochote, tatizo ni kuandika kitu cha maana na kiwango cha uwezo wa uelewa wa kuelewa kilichoandikwa kwenye bandiko fulani na kubaini lengo na maana halisi ya bandiko husika lina maana gani na lengo lake ni nini, yaani "the motive behind".

Sasa kama mmeshindwa kuelewa kitu simple na straight forward kilichoandikwa humu na BAK, mtaweza kweli kusoma mabandiko kama yetu tunaokuja na vitu complex na vigumu kuelewa kama we were hutafikirisha ability yako?!.

Rais ndio mkuu wa nchi, with all info tips from "his" reliable "sources" ziko at his finger tips!, hivyo he is expected to be the one and only who should have known better than anybody else!, sasa inapotokea mkuu wa nchi anajitokeza kwenye public ya watu au kadamnasi ya watu na kuanza kutoa kauli za guess work, kama hizi,
hamuoni kuwa ni tatizo?!. If rais wa nchi is unsure about allegations fulani ya ufisadi kwenye taasisi nyeti kama jeshi la polisi!, then who will be sure?!, kiukweli we have a serious problem here!, ambayo saa hizi haiwezi kuonekana kwa sababu bado ni mapema mno kumfanyia assessment lakini akiendelea hivi, for sure, taifa litakuwa in deep trouble!, nyie endeleeni tuu kumuimbia nyimbo za sifa na mapambio ila mwisho wa siku wakati wa suffering utakapowadia, tuta suffer wote, nyie mnaoshangilia na sisi tunaopinga, na ndipo mtakapogundua kumbe he is not only just a real dictator, but also a comedian!, stabbing you while making look like a joje!, kama Tanzania kama nchi tunachotaka ni comedy, then, tutapata na rais tumempata!.

Tangu mwanzo kuna kina sisi ambao we don't believe in one man show za hizi shows za comedy kama ziara za kushtukiza, tunataka a real and serious changes in systems!, tukitaraji rais wetu kama mkuu wa nchi to be perfect kuongoza mabadiliko haya!, akipata tip ya ufisadi popote, kabla hajatamka chochote, kwanza ajiridhishe kwa kutumia vyombo vyake, ajue for sure what is it exactly!, watu wameiba bilioni 20, 40 au 60, ni kina nani, na ni kiasi gani?!, hii ya "eti nimesikia, kuna watu!, wamekwapua eti sijui ni bilioni 20, 40, 60, etc", atuachie sisi watu wa kawaida tukiwemo wana jf tusio na source, lakini yeye mwenye all the sources hana haja ya kuharakisha!, anaharakishia nini kama hii
Magufuli: Kuna mtu alikuwa anahamisha kati ya Tsh milioni 7-8 kila dakika...
ikaja kutokezea jumla ya fedha zote kwa miaka yote hazifiki hata bilioni 100!. Alipokwenda pale BOT aliingia kwa mkwala kumtetemesha Gavana na kuongea kwa confidence kuwa ana taarifa na anakijua anacho zungumza! , hadi leo kiko wapi? ,hizi ziara siku hizi zimeishia wapi? ,ukisikia nguvu ya soda utatofautishaje na hii. Tunataka mrejesho wa kila anachokifanya rais sio kuvamia tuu mahali au kutoa tuhuma then nothing!.

Hapa kazi tuu, tunataka kazi kweli kwenye changing the systems, mifumo, changing the mindset za watendaji, mabadiliko ya how we do things yaonekane na tuambiwe matokeo chanya ya mabadiliko hayo kwa maeneo yote na sio hizi shows za ze comedy za one man show zinazoebdelea!.

Paskali
Kwenye hili la mchanga wa madini, the gap ya 10X ni too big and too good to be true. Let's wait and see, na ikitokea hesabu hiyo ikawa ni kweli, then hawa Acacia they can just pack and go!. Na tutahakikisha hawaondoki na kitu hadi wa bring back our money!.

Paskali
 
ACACIA hawawezi kuaminika
Walianza na kukwepa kodi kwa kutoa taarifa ya uongo TRA,wakajisahau wakapeleka taarifa sahihi London stock exchange ili kupata bei nzuri ya hisa.TRA wakapiga kodi kwa kutumia hesabu walizopeleka LSE.
Kama wanaweza kuwa na taarifa mbili za kodi utawaamini vipi watu kama hawa.
Kwa hili tunapaswa kuwa na Magufuli
 
Back
Top Bottom