FUTURE HUNTER
JF-Expert Member
- Apr 30, 2018
- 2,022
- 2,591
Yaani ni wizi wa wazi waziInategemea na malengo yake. Naskia ni vijiplastic tu wanagawa. Na kakipotea imekula kwako!
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani ni wizi wa wazi waziInategemea na malengo yake. Naskia ni vijiplastic tu wanagawa. Na kakipotea imekula kwako!
Unatekeleza mauzo ya Vitambulisho kwa niaba yao, then unawatumia fedha kupitia account maalum iliyotolewa ambayo kimsingi iko chini ya "tra ya magogoni" then ndio unajiuliza hilo swali "who is auditing"?
Wana fosiwa kununua hivo vtambulisho, maana eti havihusiki na vya TRANi kiherehere Chao kukwepa Kodi.
Halmashauri na TRA wataendelea kuwabana tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Swali la Mzee Mwanakijiji umelisoma na kulielewa? Hivi inashindikana kuwaambia mgambo wasinyanyase wamachinga mpaka kuwe na vitambulisho?na serikari imekuwa wazi ukiwa nacho asije mtu kukutoa katika makazi yako ya biashara au mgambo kukunyang'anya mzigo wako. Fair enough na hela yenyewe ndogo tu.
Unatekeleza mauzo ya Vitambulisho kwa niaba yao, then unawatumia fedha kupitia account maalum iliyotolewa ambayo kimsingi iko chini ya "tra ya magogoni" then ndio unajiuliza hilo swali "who is auditing"?
Ask yourself je hili jambo limebainishwa kwenye bajeti kama chanzo cha mapato ya serikali kuu?
Je inatekelezwa chini ya sheria Ipi?
Unajuwa kipindi cha nyuma niliona habari kuwa serikali imekula pesa za rambi rambi sikuamini. Nikasema ni fake news tu. Lakini nikawa bado naiona tu na serikali haipingi. Kufuatilia nikakuta ni kweli kule Kagera pesa zao za rambi rambi serikali ilikamata ikazitumia kwingine.
Asisumbuliwe kuhusu nini?asisumbuliwe tena ndani ya mwaka?
Kwa nilivyomuelewa, wao wanakusanya kisha wanaweka kwenye akaunti ya magogoni. Labda wao ndiyo wakatiwe kwa kufanya shughuli hiyo.Sijaelewa hapo kidogo; wenye vitambulisho wakiuza wanaikatia hela serikali?
Kama hataelewa kwa lugha hiyo nyepesi na ya moja kwa moja kamwe hataelewa Tena.Ni agizo la mzee baba ili akusanye pesa...ila hutaki kuamini...ila ndio ukweli huu.
Tukisema kuwatambua walahi hakuna data base....wanachukuliwa tu particulars zao kwenye makaratasi tu..
Na ukizingatia vitambulisho vyenyewe havina chochote zaidi ya zile namba zao..
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkakati wa ccm kuelekea uchaguzi serikali za mitaaaView attachment 1029451
(Picha kutoka Ahmad Michuzi)
Sijafuatilia sana suala hili la vitambulisho na sijapata nafasi ya kusoma uchambuzi yakinifu ya kwanini linafanyika sasa na jinsi linavyofanyika. Kwa kufuatilia tu habari kama wengine ningependa kujua zaidi ili kuweza kutoa mchango wa mawazo ipasavyo. Inawezekana kabisa kuwa hili ni wazo zuri sana (brilliant idea) lakini uzuri wake unahitaji kuangaliwa kwa macho ya darubini kuona uwezekano wa matatizo na hata matumizi mabaya ya mpango wenyewe.
1. Lengo la kuwa na hivi vitambulisho ni nini hasa? Ni kutaka kujua nani anafanya biashara, wapi, na gani? au ni kwa ajili ya kuona ni wapi serikali inaweza kupata mapato zaidi?
2. Kwanini vitambulisho hivi vimeanzia Ikulu badala ya wizara fulani kwa mfano TAMISEMI? (naelewa TAMISEMI iko chini ya Ikulu). Kwa maana ya kwamba, Ikulu inataka kutatua tatizo gani hasa?
3. Imeonekana kuna ulazima kuwa wafanyabiashara hawa wadogo wadogo - hadi wabangua kokoto - watatakiwa kuwa na vitambulisho hivi. Ulazima huu ni kwa ajili gani hasa? Wao watapata faida gani ya kuwa na vitambulisho hivi? Je, mtu asiponunua vitambulisho hivi atapata adhabu gani na kwa kosa la kuvunja sheria gani?
4. Je, vitambulisho hivi vinaingizwa kwenye database gani ambayo inakusanya na kuchanganua taarifa za wafanyabiashara hawa? Au watu wananunua vitambulisho na kusema wanavyo?
5. Je, ni kwanini viuzwe au kutolewa kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa/Wilaya badala ya Halmashauri ambapo watu wanafanya shughuli zao? Mapato haya ya vitambulisho - sijui vinauzwaje yanaenda wapi? Mkoani, Halmashauri au Hazina Kuu?
6. Ni kwa vili itakuwa vigumu watu ku counterfeit vitambulisho hivi? Yaani, kuna teknolojia gani iko (embedded) kwenye hivi vitambulisho kuzuia kuigwa?
7. Kuna ulazima kweli wa kuwa na vitambulisho hivi? Watu wana leseni za biashara, wana vitambulisho mbalimbali kwanini ulazima wa kuwa na hivi; hivi vinamuongezea mtu kitu gani ambacho angeshindwa kukipata au kuvifanya kwa kutumia vitambulisho alivyo navyo tayari?
Naomba kusaidiwa kwa taarifa sahihi (facts) kuliko kukisia au kunuia. Kama mwenzangu na wewe uko kama mimi basi tuendelee kuuliza maswali; wenye majibu watatusaidia kujibu.
Mchuuzi na mama ntilie, mgambo na wengine wote wenye tabia za kuwapora bidhaa waacheAsisumbuliwe kuhusu nini?
Wenye kipato chini ya 500000Swali la Mzee Mwanakijiji umelisoma na kulielewa? Hivi inashindikana kuwaambia mgambo wasinyanyase wamachinga mpaka kuwe na vitambulisho?
Unajua wanaotakiwa kuwa navyo ni wale tu wenye mauzo kwa siku ya Shilingi 10.958? Yaani hata mama ntilie yule anayeuza chakula sahani 1,500 akiuza sahani 10 tu naye hastahili kupewa hicho kitambulisho.
Iko hivi Rais Wa Wanyonge kaanzisha vitambulisho na kuvigawa kupitia Wizara ya TAMISEMI as you know kwamba ipo chini ya ofisi yake.Sijaelewa hapo kidogo; wenye vitambulisho wakiuza wanaikatia hela serikali?
Hata mimi nimejiuliza, kwani fungu la uchaguzi huwa lina toka wapi? Miaka ya nyuma ndo tulisikia EPA nk. Labda ni pesa ya uchaguzi. Kwasababu wafanyabiashara sidhani kama wanahamu na hii maneno. Wafadhili wa ccm sijui ndo kina nani? Labda ndo njia ya wanyonge kuchangia na wenyewe.Mkakati wa ccm kuelekea uchaguzi serikali za mitaaa