Swali chokonozi: Lengo la vitambulisho vya wamachinga ni nini na kwanini linafanywa na Serikali kuu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,989
2,000
1550858939163.png

(Picha kutoka Ahmad Michuzi)

Sijafuatilia sana suala hili la vitambulisho na sijapata nafasi ya kusoma uchambuzi yakinifu ya kwanini linafanyika sasa na jinsi linavyofanyika. Kwa kufuatilia tu habari kama wengine ningependa kujua zaidi ili kuweza kutoa mchango wa mawazo ipasavyo. Inawezekana kabisa kuwa hili ni wazo zuri sana (brilliant idea) lakini uzuri wake unahitaji kuangaliwa kwa macho ya darubini kuona uwezekano wa matatizo na hata matumizi mabaya ya mpango wenyewe.

1. Lengo la kuwa na hivi vitambulisho ni nini hasa? Ni kutaka kujua nani anafanya biashara, wapi, na gani? au ni kwa ajili ya kuona ni wapi serikali inaweza kupata mapato zaidi?

2. Kwanini vitambulisho hivi vimeanzia Ikulu badala ya wizara fulani kwa mfano TAMISEMI? (naelewa TAMISEMI iko chini ya Ikulu). Kwa maana ya kwamba, Ikulu inataka kutatua tatizo gani hasa?

3. Imeonekana kuna ulazima kuwa wafanyabiashara hawa wadogo wadogo - hadi wabangua kokoto - watatakiwa kuwa na vitambulisho hivi. Ulazima huu ni kwa ajili gani hasa? Wao watapata faida gani ya kuwa na vitambulisho hivi? Je, mtu asiponunua vitambulisho hivi atapata adhabu gani na kwa kosa la kuvunja sheria gani?

4. Je, vitambulisho hivi vinaingizwa kwenye database gani ambayo inakusanya na kuchanganua taarifa za wafanyabiashara hawa? Au watu wananunua vitambulisho na kusema wanavyo?

5. Je, ni kwanini viuzwe au kutolewa kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa/Wilaya badala ya Halmashauri ambapo watu wanafanya shughuli zao? Mapato haya ya vitambulisho - sijui vinauzwaje yanaenda wapi? Mkoani, Halmashauri au Hazina Kuu?

6. Ni kwa vili itakuwa vigumu watu ku counterfeit vitambulisho hivi? Yaani, kuna teknolojia gani iko (embedded) kwenye hivi vitambulisho kuzuia kuigwa?

7. Kuna ulazima kweli wa kuwa na vitambulisho hivi? Watu wana leseni za biashara, wana vitambulisho mbalimbali kwanini ulazima wa kuwa na hivi; hivi vinamuongezea mtu kitu gani ambacho angeshindwa kukipata au kuvifanya kwa kutumia vitambulisho alivyo navyo tayari?

Naomba kusaidiwa kwa taarifa sahihi (facts) kuliko kukisia au kunuia. Kama mwenzangu na wewe uko kama mimi basi tuendelee kuuliza maswali; wenye majibu watatusaidia kujibu.
 

lukesam

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
10,690
2,000

Wakati awamu hii inaanza,kule mwanzoni kabisa nilitoa maoni yangu nikasema, kama tulifikiri serikali zilizopita zina makandokando basi tuchukue kalamu na daftari tukae chini tuandike.

Ukali wa kupitiliza na kuzimwa kwa bunge live ni kiashiria tosha cha kuwepo makandokando yasiyo na kifani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom