Swali chokonozi: Lengo la vitambulisho vya wamachinga ni nini na kwanini linafanywa na Serikali kuu?

Kweli shilingi elfu 20 hizi utakusanya kiasi gani; isipokuwa kama unawalipisha watu kila mwezi au kila wiki... wakinunua wajasirimali 5,000,000 utakachopata ni milioni 100 tu! Utafanya nazo nini na hizi ni kwa nchi nzima? Kama chanzo cha mapato sidhani kama ni lengo sahihi... labda itabidi nirejee ile hotuba ya rais alipotangaza hili na kugawa pale Ikulu; labda kuna kitu nimemiss.

Hela nyingi Sana zinakusanywa aisee.

Awamu ya kwanza tu kwa dar zimekusanywa 500M Sasa kwa mikoa yote?? Vikaletwa awamu ya pili, vimeletwa awamu ya tatu Mara 5 ya awamu kwa kwanza.

Zinakusanywa B za kutosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna lengo jingine la maana zaidi ya "kuuza" vitambulisho.

Lengo kuu ni kukusanya fedha.


Lengo ni ili viishe hakuna la zaidi hivyo kila Mkuu wa Mkoa na Wilaya ana parangana kivyake ili kumaliza mgao wake aliopewa.

Ukivisoma Vitambulisho utaona vimeandikwa "Vimetolewa na TAMISEMI" hivyo Kwa Kua Wizara hiyo ipo ofisini kwake hivyo ni yeye ndiye Mhusika Mkuu.
 
Jamani hivi vtu vinahtaji utaalamu ujue wengine wanalipia kodi bado wanaongezewa mzigo, hafu biashara ngumu ka nini. Mimi nawahurumia hao wapaka rangi, wachoma mahindi, I think aliyekuja na hili wazo alitaka had wauza kahawa watoe kodi sasa wazo lake hakuliboresha vzuri, so wakipata hicho what next ka hawajaandikwa majina?

Sent using Jamii Forums mobile app

Wale waliokuwa wakilipa Kodi Halmashauri ama TRA hawastahili kununua vitambulisho hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1029451
(Picha kutoka Ahmad Michuzi)

Sijafuatilia sana suala hili la vitambulisho na sijapata nafasi ya kusoma uchambuzi yakinifu ya kwanini linafanyika sasa na jinsi linavyofanyika. Kwa kufuatilia tu habari kama wengine ningependa kujua zaidi ili kuweza kutoa mchango wa mawazo ipasavyo. Inawezekana kabisa kuwa hili ni wazo zuri sana (brilliant idea) lakini uzuri wake unahitaji kuangaliwa kwa macho ya darubini kuona uwezekano wa matatizo na hata matumizi mabaya ya mpango wenyewe.

1. Lengo la kuwa na hivi vitambulisho ni nini hasa? Ni kutaka kujua nani anafanya biashara, wapi, na gani? au ni kwa ajili ya kuona ni wapi serikali inaweza kupata mapato zaidi?

2. Kwanini vitambulisho hivi vimeanzia Ikulu badala ya wizara fulani kwa mfano TAMISEMI? (naelewa TAMISEMI iko chini ya Ikulu). Kwa maana ya kwamba, Ikulu inataka kutatua tatizo gani hasa?

3. Imeonekana kuna ulazima kuwa wafanyabiashara hawa wadogo wadogo - hadi wabangua kokoto - watatakiwa kuwa na vitambulisho hivi. Ulazima huu ni kwa ajili gani hasa? Wao watapata faida gani ya kuwa na vitambulisho hivi? Je, mtu asiponunua vitambulisho hivi atapata adhabu gani na kwa kosa la kuvunja sheria gani?

4. Je, vitambulisho hivi vinaingizwa kwenye database gani ambayo inakusanya na kuchanganua taarifa za wafanyabiashara hawa? Au watu wananunua vitambulisho na kusema wanavyo?

5. Je, ni kwanini viuzwe au kutolewa kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa/Wilaya badala ya Halmashauri ambapo watu wanafanya shughuli zao? Mapato haya ya vitambulisho - sijui vinauzwaje yanaenda wapi? Mkoani, Halmashauri au Hazina Kuu?

6. Ni kwa vili itakuwa vigumu watu ku counterfeit vitambulisho hivi? Yaani, kuna teknolojia gani iko (embedded) kwenye hivi vitambulisho kuzuia kuigwa?

7. Kuna ulazima kweli wa kuwa na vitambulisho hivi? Watu wana leseni za biashara, wana vitambulisho mbalimbali kwanini ulazima wa kuwa na hivi; hivi vinamuongezea mtu kitu gani ambacho angeshindwa kukipata au kuvifanya kwa kutumia vitambulisho alivyo navyo tayari?

Naomba kusaidiwa kwa taarifa sahihi (facts) kuliko kukisia au kunuia. Kama mwenzangu na wewe uko kama mimi basi tuendelee kuuliza maswali; wenye majibu watatusaidia kujibu.
Unaambiwa hadi hawa ni lazima wawe na vitambulisho , hii ni kwa mujibu wa RC wa Ruvuma
FB_IMG_1549369100113.jpeg
 
Kweli shilingi elfu 20 hizi utakusanya kiasi gani; isipokuwa kama unawalipisha watu kila mwezi au kila wiki... wakinunua wajasirimali 5,000,000 utakachopata ni milioni 100 tu! Utafanya nazo nini na hizi ni kwa nchi nzima? Kama chanzo cha mapato sidhani kama ni lengo sahihi... labda itabidi nirejee ile hotuba ya rais alipotangaza hili na kugawa pale Ikulu; labda kuna kitu nimemiss.

Mzee rudi shule ukajifunze hesabu, 20,000x5,000,000 ni milioni 100!? Huna hoja ni bora ukae kimya maana hujui unaongea nini.
 
Kweli shilingi elfu 20 hizi utakusanya kiasi gani; isipokuwa kama unawalipisha watu kila mwezi au kila wiki... wakinunua wajasirimali 5,000,000 utakachopata ni milioni 100 tu! Utafanya nazo nini na hizi ni kwa nchi nzima? Kama chanzo cha mapato sidhani kama ni lengo sahihi... labda itabidi nirejee ile hotuba ya rais alipotangaza hili na kugawa pale Ikulu; labda kuna kitu nimemiss.[/QUOTE)
Mkuu cheki hesabu vizuri
 
Wale waliokuwa wakilipa Kodi Halmashauri ama TRA hawastahili kununua vitambulisho hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
"Ganja" wangu amini kwamba kuna maeneo wapo hao wenye leseni za Biashara kutoka Halmashauri and yet wamelazimika kununua vitambulisho.

Nimeshuhudia kwa macho yangu, kuna maeneo kwa sasa kitambulisho hicho kimegeuzwa kuwa lazima sio hiyari Tena.

Kuna maeneo hadi madereza wa Boda Boda wametakiwa kununua vitambulisho hivyo.

Lengo ni kuuza vitambulisho na ni ili kila "muuzaji" amalize mgao Wake.
 
Kweli shilingi elfu 20 hizi utakusanya kiasi gani; isipokuwa kama unawalipisha watu kila mwezi au kila wiki... wakinunua wajasirimali 5,000,000 utakachopata ni milioni 100 tu! Utafanya nazo nini na hizi ni kwa nchi nzima? Kama chanzo cha mapato sidhani kama ni lengo sahihi... labda itabidi nirejee ile hotuba ya rais alipotangaza hili na kugawa pale Ikulu; labda kuna kitu nimemiss.
We Mzee Vitambulisho vilivyozalishwa toka Ikulu/TAMISEMI ni around 1.5M Kila kitambulisho kinauzwa Shilingi 20,000/= na hela hiyo ni kwa mwaka mmoja tu hivyo mwaka ujao kila anayepewa Kitambulisho atatakiwa kukilipia Tena.


Huu ni ukusanyaji wa mapato kupitia "tra ya magogoni".
 
Ukiona hivyo ujue serikali iko taabani ki pesa ndio inakimbizana na wanyonge ,serikali haina kitu kabisa mbwembwe za akiba tunayo ya miezi mitano ni uongo mtupu Jiwe yuko taabani kiuchumi soon itajulikana tu .
 
Watanzania wanapenda kulalamika ovyo vitambulisho ni kama usajili rasmi kwa wafanyabiashara wenye kipato cha chini; na serikari imekuwa wazi ukiwa nacho asije mtu kukutoa katika makazi yako ya biashara au mgambo kukunyang'anya mzigo wako. Fair enough na hela yenyewe ndogo tu.

Kuna watu wanapenda kulalamika tu, na kila kitu kwao ni fursa ya kuchonganisha kundi fulani na serikari.
 
Back
Top Bottom