Kwanini haya yanafanyika Zanzibar?

Emanueli misalaba

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
1,111
1,658
Wana Jf bila shaka mpo salama,
Hongereni kwa majukumu ya kutwa zima ya ujenzi wa uchumi mtu mmoja mmoja, Familia na Taifa,

Bila kuwachosha nijielekeze kwenye hoja yangu,

Kwa Zanzibar unakuta kuna malalamiko sana chini kwa chini hasa linapokuja swala la kuajiliwa kwenye taasisi za serikali na hata kwenye vikosi mbali mbali za majeshi, Jku, Kmkm, Valatia nk.

1. Unakuta vijana wana sifa zote za kuajiliwa, elimu wako vizuri.

2. Ni raia halali wa nchi.

3. Vipimo vya afya vinaonyesha wako fit.

4. Vitambulisho vyote wanavyo nk.

Lakini tu kwa sababu yeye si mwanachama wa chama Fulani, hana kadi ya umoja wa vijana wa chama na kwenye system ya chama jina lake halionekani basi kijana huyu au vijana hawa majina yao yanaenguliwa kuweza kuendelea na michakato inayofua.
Je mlio madarakani kwa nini mnafanya hivi?

Hawa mnaowaweka kando kisa tu si wanachama mnakuwa mpo sahihi kwa kiasi gani?

Hawa vijana ni raia wa nchi yenu wanazo haki zote za kikatiba juu ya nchi yao ikiwemo kulitumikia taifa lao kwenye nyanja mbali mbali.

Leo hii kwenye baadhi ya taasisi mfano Hospital ya Mnazi Mmoja, baadhi yao wameajiliwa hawana vigenzo lakini tu kwa sababu ni wanachama wa chama chenu wametumika kupiga kura 2015 au 2020 wanapata upendeleo wa kuajiliwa, mwisho wa siku ukienda Mnazi Mmoja hospital unakutana na baadhi ya watoa huduma wenye kauli mbovu kwa wateja, wavivu wa kazi, watoro wachelewaji hawana weledi na kazi zao, hawana ubunifu, wenye sifa wengi wao mnawatupa nje ya mfumo.

Je, mnajenga taifa la namna gani?

Je, Tanzania bara nako haya hayapo maana chama ni hicho hicho?

Watanzania wengi tunajinasibu wacha Mungu kupitia dini zetu, Uislamu, Ukristo nk je dini zetu zinaruhusu ubaguzi?

Kubangua watu kwa sababu ya chama kwenye ucha Mungu ruksa?

Ikifika Kwaresima, Ramadhani full kufunga, swala tano, je dhamiri zenu zinawashuhudiaje juu ya hili na Mungu mnayemwabudu anawaangalije juu ya hili?
 
ala tano, je dhamiri zenu zinawashuhudiaje juu ya hili na Mungu mnayemwabudu anawaangalije juu ya hili?
Ukichunguza ki undani wengi wanaofunga Kwaresma au Ramadhani, wanafunga ni kama wanajishindisha njaa tu, maana matendo yao hayaendani na wanachokifanya., Ubaguzi, unafiki, u chawa, uzinzi, ufirauni n.k yote haya huwa wanasitisha kwa muda tu baada ya mwezi kuisha wanarudia yale yale.
 
Mkuu Citizen_37 je na nchi za wenzetu mfano za ulaya hasa Waliotutawala nao wana ubanguzi kama huu kwa raia wao ambao yamkini hawana vyama wako neutral?
 
Kama ungelikuwa unajua Zanzibar hawaitaki hiyo CCM hata Mwinyi usingeongea ,kuwepo kwa CCM zenji ni swa na ukoloni mamboleo yaani chama cha bara kitawale zenji..

Haya yote ni laana ya CCM.
Mkuu Accumen Mo nadhani hujaelewa maswali yangu kiongozokiongozi, hao hao ccm ili uajiliwe inaonyesha uwe upo kwenye system ya uvccm au kwenye system ya chama Kisiwadui.
 
Baadhi ya vijana wengine wala hawana vyama, wala hawaichukii Ccm wala Act Wazalendo, bali hawana vyama,
Na kwenye jamii huwezi kuwalazimisha watu watu wote wafanane, watakuwepo wenye vyama na wasio na vyama, wapenda haki na amani, je unawatengaje hawa kwenye kuijenga nchi?

Je makoloni waliotutawala Waingereza nk nao raia wao huwabangua kwenye ajira hata km wana kidhi vigezo vya ajira ila tu kwa sababu si wa chama tawala unawaweka kando?

Wale wazenji japo wachache kuna jamaa hawapati ajira ng'o kwa sababu hawataki CCM
 
Wana Jf bila shaka mpo salama,
Hongereni kwa majukumu ya kutwa zima ya ujenzi wa uchumi mtu mmoja mmoja, Familia na Taifa,

Bila kuwachosha nijielekeze kwenye hoja yangu,

Kwa Zanzibar unakuta kuna malalamiko sana chini kwa chini hasa linapokuja swala la kuajiliwa kwenye taasisi za serikali na hata kwenye vikosi mbali mbali za majeshi, Jku, Kmkm, Valatia nk.

1. Unakuta vijana wana sifa zote za kuajiliwa, elimu wako vizuri.

2. Ni raia halali wa nchi.

3. Vipimo vya afya vinaonyesha wako fit.

4. Vitambulisho vyote wanavyo nk.

Lakini tu kwa sababu yeye si mwanachama wa chama Fulani, hana kadi ya umoja wa vijana wa chama na kwenye system ya chama jina lake halionekani basi kijana huyu au vijana hawa majina yao yanaenguliwa kuweza kuendelea na michakato inayofua.
Je mlio madarakani kwa nini mnafanya hivi?

Hawa mnaowaweka kando kisa tu si wanachama mnakuwa mpo sahihi kwa kiasi gani?

Hawa vijana ni raia wa nchi yenu wanazo haki zote za kikatiba juu ya nchi yao ikiwemo kulitumikia taifa lao kwenye nyanja mbali mbali.

Leo hii kwenye baadhi ya taasisi mfano Hospital ya Mnazi Mmoja, baadhi yao wameajiliwa hawana vigenzo lakini tu kwa sababu ni wanachama wa chama chenu wametumika kupiga kura 2015 au 2020 wanapata upendeleo wa kuajiliwa, mwisho wa siku ukienda Mnazi Mmoja hospital unakutana na baadhi ya watoa huduma wenye kauli mbovu kwa wateja, wavivu wa kazi, watoro wachelewaji hawana weledi na kazi zao, hawana ubunifu, wenye sifa wengi wao mnawatupa nje ya mfumo.

Je, mnajenga taifa la namna gani?

Je, Tanzania bara nako haya hayapo maana chama ni hicho hicho?

Watanzania wengi tunajinasibu wacha Mungu kupitia dini zetu, Uislamu, Ukristo nk je dini zetu zinaruhusu ubaguzi?

Kubangua watu kwa sababu ya chama kwenye ucha Mungu ruksa?

Ikifika Kwaresima, Ramadhani full kufunga, swala tano, je dhamiri zenu zinawashuhudiaje juu ya hili na Mungu mnayemwabudu anawaangalije juu ya hili?
Zanzibar itakombolewa tu
 
Back
Top Bottom