Swali chokonozi: Lengo la vitambulisho vya wamachinga ni nini na kwanini linafanywa na Serikali kuu?

View attachment 1029451
(Picha kutoka Ahmad Michuzi)

Sijafuatilia sana suala hili la vitambulisho na sijapata nafasi ya kusoma uchambuzi yakinifu ya kwanini linafanyika sasa na jinsi linavyofanyika. Kwa kufuatilia tu habari kama wengine ningependa kujua zaidi ili kuweza kutoa mchango wa mawazo ipasavyo. Inawezekana kabisa kuwa hili ni wazo zuri sana (brilliant idea) lakini uzuri wake unahitaji kuangaliwa kwa macho ya darubini kuona uwezekano wa matatizo na hata matumizi mabaya ya mpango wenyewe.

1. Lengo la kuwa na hivi vitambulisho ni nini hasa? Ni kutaka kujua nani anafanya biashara, wapi, na gani? au ni kwa ajili ya kuona ni wapi serikali inaweza kupata mapato zaidi?

2. Kwanini vitambulisho hivi vimeanzia Ikulu badala ya wizara fulani kwa mfano TAMISEMI? (naelewa TAMISEMI iko chini ya Ikulu). Kwa maana ya kwamba, Ikulu inataka kutatua tatizo gani hasa?

3. Imeonekana kuna ulazima kuwa wafanyabiashara hawa wadogo wadogo - hadi wabangua kokoto - watatakiwa kuwa na vitambulisho hivi. Ulazima huu ni kwa ajili gani hasa? Wao watapata faida gani ya kuwa na vitambulisho hivi? Je, mtu asiponunua vitambulisho hivi atapata adhabu gani na kwa kosa la kuvunja sheria gani?

4. Je, vitambulisho hivi vinaingizwa kwenye database gani ambayo inakusanya na kuchanganua taarifa za wafanyabiashara hawa? Au watu wananunua vitambulisho na kusema wanavyo?

5. Je, ni kwanini viuzwe au kutolewa kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa/Wilaya badala ya Halmashauri ambapo watu wanafanya shughuli zao? Mapato haya ya vitambulisho - sijui vinauzwaje yanaenda wapi? Mkoani, Halmashauri au Hazina Kuu?

6. Ni kwa vili itakuwa vigumu watu ku counterfeit vitambulisho hivi? Yaani, kuna teknolojia gani iko (embedded) kwenye hivi vitambulisho kuzuia kuigwa?

7. Kuna ulazima kweli wa kuwa na vitambulisho hivi? Watu wana leseni za biashara, wana vitambulisho mbalimbali kwanini ulazima wa kuwa na hivi; hivi vinamuongezea mtu kitu gani ambacho angeshindwa kukipata au kuvifanya kwa kutumia vitambulisho alivyo navyo tayari?

Naomba kusaidiwa kwa taarifa sahihi (facts) kuliko kukisia au kunuia. Kama mwenzangu na wewe uko kama mimi basi tuendelee kuuliza maswali; wenye majibu watatusaidia kujibu.

Maswali yako yote jibu lake ni, huo ni utapeli kama utapeli mwingine.
 
1 Lengo Ni kukusanya pesa

Sent using Jamii Forums mobile app

Kweli shilingi elfu 20 hizi utakusanya kiasi gani; isipokuwa kama unawalipisha watu kila mwezi au kila wiki... wakinunua wajasirimali 5,000,000 utakachopata ni milioni 100 tu! Utafanya nazo nini na hizi ni kwa nchi nzima? Kama chanzo cha mapato sidhani kama ni lengo sahihi... labda itabidi nirejee ile hotuba ya rais alipotangaza hili na kugawa pale Ikulu; labda kuna kitu nimemiss.
 
Jamani hivi vtu vinahtaji utaalamu ujue wengine wanalipia kodi bado wanaongezewa mzigo, hafu biashara ngumu ka nini. Mimi nawahurumia hao wapaka rangi, wachoma mahindi, I think aliyekuja na hili wazo alitaka had wauza kahawa watoe kodi sasa wazo lake hakuliboresha vzuri, so wakipata hicho what next ka hawajaandikwa majina?
UKIWAONA WANAOVIUZA UTAWAONEA HURUMA. WAFANYEJE SASA WAKATI NI LAZIMA VIUZIKE!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom