Swali chokonozi: Lengo la vitambulisho vya wamachinga ni nini na kwanini linafanywa na Serikali kuu?

Kweli shilingi elfu 20 hizi utakusanya kiasi gani; isipokuwa kama unawalipisha watu kila mwezi au kila wiki... wakinunua wajasirimali 5,000,000 utakachopata ni milioni 100 tu! Utafanya nazo nini na hizi ni kwa nchi nzima? Kama chanzo cha mapato sidhani kama ni lengo sahihi... labda itabidi nirejee ile hotuba ya rais alipotangaza hili na kugawa pale Ikulu; labda kuna kitu nimemiss.
Wewe nawe, hesabu zimekupita kushoto. Ebu rudia tena.
5,000,000 × 20,000 = ?
 
Sion kama Machinga ananyonywa kwenye issue hii..! Hapa Lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mfanybiashara anatambulika hiki kinacho endelea ni kuwaingiza kwenye system na naamini kuanzia mwaka wa fedha ujao kuna utaratibu rasmi utakuja chini ya sheria..!

unazungumzia unyonyaji ambao 20,000/= per year sawa na Tsh ngapi kwa siku? yani kama inakushinda kupata 20,000 kwa mwaka mzima hiyo ni biashara ama kitu gani?
Uko serious?
 
Unajua kodi inakusanywa na nani?
 
Nafikiri lengo kuu ni kukusanya pesa, na litatimia.

Mh Rais alisema "ole wake atakayethubutu kuwabugudhi wenye hivyo vitambulisho". Akikusudia wasisumbuliwe kutozawa kodi na tozo zingine wala mahali pa kufanyia biashara. Sifa ni uwe mtanzania na uwe na shughuli yenye mtaji usiozidi milioni 4.

Nani anapima hiyo mitaji na kwa namna gani, ni Mungu pekee anayejua!

Politicians!

"Rais wa wanyonge" ....ndio napigiwa mstari hivyo!
 
Kweli shilingi elfu 20 hizi utakusanya kiasi gani; isipokuwa kama unawalipisha watu kila mwezi au kila wiki... wakinunua wajasirimali 5,000,000 utakachopata ni milioni 100 tu! Utafanya nazo nini na hizi ni kwa nchi nzima? Kama chanzo cha mapato sidhani kama ni lengo sahihi... labda itabidi nirejee ile hotuba ya rais alipotangaza hili na kugawa pale Ikulu; labda kuna kitu nimemiss.
Mzee wangu hapo jibu ni Bilioni 100.
 
Kapu la hazina Hakuna kitu ndio ,ubunifu wa PhD holder ,ili kujaza kapu maana hata Sikh za kupokea mshahara zinahesabika muda si mrefu mishahara itasanda ,jiwe keshaharibu kila kitu .
 
View attachment 1029451
(Picha kutoka Ahmad Michuzi)

Sijafuatilia sana suala hili la vitambulisho na sijapata nafasi ya kusoma uchambuzi yakinifu ya kwanini linafanyika sasa na jinsi linavyofanyika. Kwa kufuatilia tu habari kama wengine ningependa kujua zaidi ili kuweza kutoa mchango wa mawazo ipasavyo. Inawezekana kabisa kuwa hili ni wazo zuri sana (brilliant idea) lakini uzuri wake unahitaji kuangaliwa kwa macho ya darubini kuona uwezekano wa matatizo na hata matumizi mabaya ya mpango wenyewe.

1. Lengo la kuwa na hivi vitambulisho ni nini hasa? Ni kutaka kujua nani anafanya biashara, wapi, na gani? au ni kwa ajili ya kuona ni wapi serikali inaweza kupata mapato zaidi?

2. Kwanini vitambulisho hivi vimeanzia Ikulu badala ya wizara fulani kwa mfano TAMISEMI? (naelewa TAMISEMI iko chini ya Ikulu). Kwa maana ya kwamba, Ikulu inataka kutatua tatizo gani hasa?

3. Imeonekana kuna ulazima kuwa wafanyabiashara hawa wadogo wadogo - hadi wabangua kokoto - watatakiwa kuwa na vitambulisho hivi. Ulazima huu ni kwa ajili gani hasa? Wao watapata faida gani ya kuwa na vitambulisho hivi? Je, mtu asiponunua vitambulisho hivi atapata adhabu gani na kwa kosa la kuvunja sheria gani?

4. Je, vitambulisho hivi vinaingizwa kwenye database gani ambayo inakusanya na kuchanganua taarifa za wafanyabiashara hawa? Au watu wananunua vitambulisho na kusema wanavyo?

5. Je, ni kwanini viuzwe au kutolewa kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa/Wilaya badala ya Halmashauri ambapo watu wanafanya shughuli zao? Mapato haya ya vitambulisho - sijui vinauzwaje yanaenda wapi? Mkoani, Halmashauri au Hazina Kuu?

6. Ni kwa vili itakuwa vigumu watu ku counterfeit vitambulisho hivi? Yaani, kuna teknolojia gani iko (embedded) kwenye hivi vitambulisho kuzuia kuigwa?

7. Kuna ulazima kweli wa kuwa na vitambulisho hivi? Watu wana leseni za biashara, wana vitambulisho mbalimbali kwanini ulazima wa kuwa na hivi; hivi vinamuongezea mtu kitu gani ambacho angeshindwa kukipata au kuvifanya kwa kutumia vitambulisho alivyo navyo tayari?

Naomba kusaidiwa kwa taarifa sahihi (facts) kuliko kukisia au kunuia. Kama mwenzangu na wewe uko kama mimi basi tuendelee kuuliza maswali; wenye majibu watatusaidia kujibu.

MM,
Siasa pembeni, kulikua na zoezi nyeti linaendelea la kutaka kujua the actual size ya informal sector ya TZ na lengo kubwa ni kurasimisha hiyo informal sector half baada ya hapo ukubwa wa uchumi (GDP) unakua re-based kwan kuzingatia jumuisho hilo la informal sector.

Kwa hilo usishangae wiki ijayo ukiambiwa kuwa uchumi wetu sasa ni USD 80 bilion.
 
Kweli shilingi elfu 20 hizi utakusanya kiasi gani; isipokuwa kama unawalipisha watu kila mwezi au kila wiki... wakinunua wajasirimali 5,000,000 utakachopata ni milioni 100 tu! Utafanya nazo nini na hizi ni kwa nchi nzima? Kama chanzo cha mapato sidhani kama ni lengo sahihi... labda itabidi nirejee ile hotuba ya rais alipotangaza hili na kugawa pale Ikulu; labda kuna kitu nimemiss.
Rudia hesabu zako Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1029451
(Picha kutoka Ahmad Michuzi)

Sijafuatilia sana suala hili la vitambulisho na sijapata nafasi ya kusoma uchambuzi yakinifu ya kwanini linafanyika sasa na jinsi linavyofanyika. Kwa kufuatilia tu habari kama wengine ningependa kujua zaidi ili kuweza kutoa mchango wa mawazo ipasavyo. Inawezekana kabisa kuwa hili ni wazo zuri sana (brilliant idea) lakini uzuri wake unahitaji kuangaliwa kwa macho ya darubini kuona uwezekano wa matatizo na hata matumizi mabaya ya mpango wenyewe.

1. Lengo la kuwa na hivi vitambulisho ni nini hasa? Ni kutaka kujua nani anafanya biashara, wapi, na gani? au ni kwa ajili ya kuona ni wapi serikali inaweza kupata mapato zaidi?

2. Kwanini vitambulisho hivi vimeanzia Ikulu badala ya wizara fulani kwa mfano TAMISEMI? (naelewa TAMISEMI iko chini ya Ikulu). Kwa maana ya kwamba, Ikulu inataka kutatua tatizo gani hasa?

3. Imeonekana kuna ulazima kuwa wafanyabiashara hawa wadogo wadogo - hadi wabangua kokoto - watatakiwa kuwa na vitambulisho hivi. Ulazima huu ni kwa ajili gani hasa? Wao watapata faida gani ya kuwa na vitambulisho hivi? Je, mtu asiponunua vitambulisho hivi atapata adhabu gani na kwa kosa la kuvunja sheria gani?

4. Je, vitambulisho hivi vinaingizwa kwenye database gani ambayo inakusanya na kuchanganua taarifa za wafanyabiashara hawa? Au watu wananunua vitambulisho na kusema wanavyo?

5. Je, ni kwanini viuzwe au kutolewa kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa/Wilaya badala ya Halmashauri ambapo watu wanafanya shughuli zao? Mapato haya ya vitambulisho - sijui vinauzwaje yanaenda wapi? Mkoani, Halmashauri au Hazina Kuu?

6. Ni kwa vili itakuwa vigumu watu ku counterfeit vitambulisho hivi? Yaani, kuna teknolojia gani iko (embedded) kwenye hivi vitambulisho kuzuia kuigwa?

7. Kuna ulazima kweli wa kuwa na vitambulisho hivi? Watu wana leseni za biashara, wana vitambulisho mbalimbali kwanini ulazima wa kuwa na hivi; hivi vinamuongezea mtu kitu gani ambacho angeshindwa kukipata au kuvifanya kwa kutumia vitambulisho alivyo navyo tayari?

Naomba kusaidiwa kwa taarifa sahihi (facts) kuliko kukisia au kunuia. Kama mwenzangu na wewe uko kama mimi basi tuendelee kuuliza maswali; wenye majibu watatusaidia kujibu.
Tatizo ni kwamba siyo wazo shirikishi kuna kitu kinaitwa mjasiliamali na mabo yanayo mzunguka '' An Entrepreneur and his Environments '' kuna mambo mengi yanayo mzunguka mfanya biashara huanzia nyumbani hadi kimataifa Majukumu ya Serikali 3
 
Back
Top Bottom