BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,840
Hiii ndio Sura (ufunuo) pekee katika Qur'an iliyopewa jina la mwanamke maalumu anayejulikana, ingawa ndani ya sura hii kumetajwa manabii wakubwa wakubwa kama vile Nabii Yahya, Zakaria, Ibrahim, Is-haq, Yaquub, Idriss, Ismail, n.k. Wote wametajwa ndani ya sura hii.
Kisa cha Bi Maryam katika kumzaa Nabii Issa, ilikua si tukio la kawaida ni miujiza ambayo ilistahiki kubakishwa na ndipo Mwenyezi MUNGU akalitumia jina la Marym katika sura hii.
Sura hii imeitwa kwa jina la mwanamke msafi, ambaye aliishi maisha yake yote katika hali ya kiimani kuanzia utoto wake hadi katika ujana wake.
Malaika walimwambia, 'Ewe Maryam, hakika Mwenyezi MUNGU amekuchagua wewe na akakutakasa, na akakuteua kuliko wanawake wa ulimwengu wote.
Sifa za Maryam
-Aliweza kulinda uke wake, hakufanya machafu ya aina yoyote, aliudhibiti uchi wake, hakufanya uchafu wowote wa zinaa, ni mwanamke ambaye alilinda nafsi yake. Lakini Mwenyezi MUNGU alimtia roho Maryam, yaani Nabii Issa.
Sura hii imeitwa Maryam kwa lengo la kubakisha historia ya mazazi ya kimiujiza,
Suratu Mariam ni sura ya 19 katika sura 114 za Quran, pia ipo juzu la 16 katika majuzu 30 ya Qur'an. Sura hii imechukua aya 98 katika aya 6666 za Qur'ani Tukufu.
Suratu Marym imeshuka katika mji wa Makka, ispokua aya mbili tu ndio zimeshuka Madina. Aya 96 zimeteremka Maka. Aya mbili zimeshuka madina ambazo ni aya ya 58 na aya ya 71.