TLS yadaiwa kugawanyika makundi mawili, Rais Sungusia apingwa na kundi moja

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1695473390579.png

Mpasuko mkubwa unafukuta ndani ya Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ukihusisha baadhi ya viongozi wanaounda Baraza la uongozi la chama hicho, Jambo Media inaripoti.

Taarifa za mpasuko huo zimebainishwa na chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TLS, zikionyesha wazi kama hali itaendelea hivyo huenda Rais wa TLS, Harold Sungusia akaondoshwa katika nafasi yake kabla ya kumaliza muda wake.

Mpasuko huo unaelezwa kugawanya wajumbe wa baraza la uongozi ambapo nusu inamuunga mkono na nusu nyingine haimuungi mkono, jambo ambalo litachangia kumkwamisha kufanya vikao vya baraza la uongozi.

Wajumbe wa baraza la uongozi ambao hawamuungi wanaelezea sababu za kufanya hivyo inatokana na kumlalamikia Sungusia kuongoza taasisi kama mali yake banafsi ikiwemo na kutotekeleza maelekezo yanayomuliwa na Baraza la uongozi.

Tayari Sungusia ameshaanza kuonja joto lililochangia kuahirisha kikao kimoja kutokana na kukosa akidi ya wajumbe wa baraza la uongozi.

Taratibu za TLS zinaeleza kuwa ili mkutano wa baraza la uongozi ufanyike kuwe na akidi ya wajumbe wasiopungua Sita.

Mpashaji wetu anasema, "Rais Sungusia alijikuta akiwa na wajumbe watano pekee hivyo ilimbidi kuahirisha kikao hicho kwa kukosa akidi,jambo linalotoa tafsiri kwamba kama ikiendelea hivyo atakosa sifa ya kuendelea kuwa kiongozi wa taasisi."

Mambo mengine yanayolezwa kufanywa kinyume na taratibu na Sungusia ni kile kinachodaiwa kuruhusu ajira kutolewa kinyume na taratibu pasipo kuchukua hatua yoyote.

Mtoa taarifa wetu anaongeza kuwa sababu nyingine ni wajumbe kutopewa nyaraka za taarifa za fedha kabla ya kwenda kwenye vikao, hali iliyowasababisha kushindwa kusimamia uwazi wa kifedha kwa ufanisi.

Pia ni kudharau utekelezaji wa azimio la Baraza la Uongozi lililotaka kutolewa kwa barua ya onyo kwa Mkurugenzi Mtendaji kutokana na makosa aliyokuwa amefanya.

Rais wa Chama hicho, Sungusia alipotafutwa kuzungumzia malalamiko yaliyoelekezwa kwake ambapo alikana kuwepo mpasuko .

Pamoja na kukana uwepo wa mpasuko ila alikiri kutofanyika kwa kikao kilichopita cha Baraza la Uongozi kutokana na kukosekana kwa akidi ya wajumbe wa baraza.

Alisema "kwenye taasisi yoyote wakati wowote linaweza kutokea jambo lolote hivyo kukosekana akidi kwenye kikao ni jambo la kawaida.

Aliongeza, "Niwe mkweli kikao kiliahirishwa kutokana na kukosekana kwa akidi, sababu zilizochangia ni kwamba yupo mmoja wa viongoni wetu ameteuliwa kuwa jaji huku wengine walikuwa na majukumu mengine mahakamani, ila nakuhakikishia kuwa kikao kijacho kitafanyika kama kilivyopangwa na tutafanya maazimio yetu,"

Jambo TV ilipowatafuta baadhi ya wanachama wa @TanganyikaLaw kueleza mtazamo wao juu ya uongozi wa Sungusia wamesema taasisi yao inakabiliwa na changamoto za kiuongozi ikiwemo baadhi ya maazimio ya taasisi hiyo kutokufanyiwa kazi na uongozi huku wengine wakimnyooshea kidole Sungusia kuwa ameshindwa kutekeleza matamanio ya wapiga kura waliomchagua kwa yeye kuwa mzito kutokuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha taasisi hiyo inakuwa sauti ya umma hususan katika maswala yanayogusa wananchi katika nyanja ya kisheria
 
Back
Top Bottom