SoC01 Suluhisho la Ukosefu wa Ajira Tanzania: Jinsi ninavyoweza kupunguza ukosefu wa Ajira kwa 10% Ndani ya siku moja

Stories of Change - 2021 Competition

Gwamanga

Member
Jun 25, 2021
66
138
Nawasalimu ndugu zangu wanajukwaa.
Kutokana na changamoto za upatikanaji wa Ajira Tanzania na Duniani kwa ujumla wake kama Taifa tunatakiwa tuwe na Mawazo, mipango na ubunifu mbalimbali ili kutatua changamoto hii, tuweke mapendekezo mbalimbali yafanyiwe kazi. Miongoni mwa mapendekezo hayo ni, Badala ya Mfumo wa kielimu kutilia mkazo sana kwenye vyuo vya kati na vyuo vikuu sasa elimu yetu ianze kutilia mkazo vyuo vya ufundi na vyuo hivyo viunganishwe moja kwa moja na vyuo vya kati na vyuo vikuu, Vipaji vinavyoanzia mtaani vipewe thamani sawa na vipaji vinavyovumbuliwa shuleni vipaji hivyo viingizwe kwenye mfumo rasmi wa malezi na kupewa dhamana, tubadilike badala ya kuwa Walaji (consumers) tuwe wazalishaji ( producers ) ukilinganisha Tanzania tuna Rasilimali nyingi, Kilimo, Madini, Bahari, Mbuga za wanyama na Udongo wenye rutuba, Kikubwa kuliko vyote Tanzania tuna rasilimali watu kubwa tena walio wazalishaji.
......................................................
......................................................

Binafsi nimetoa pendekezo moja ambalo kwa utafiti wangu linaweza tatua changamoto hiyo kwa asilimia kumi, pendekezo langu ni kama ifuatavyo.

Kuna sehemu nyingi nimepita mikoani kuna majengo mengi yametelekezwa, Mfano majengo ya wachina wakati wanafanya ujenzi wa barabara za lami mengi yametelekezwa( Mfano wa hayo majengo yapo kigoma), Majengo ya Jeshi yametelekezwa( Mfano wa hayo majengo yapo Tabora, Brigedi ya FARU) Nini kifanyike Kuhusu Hayo Majengo HASA WAKATI HUU WA UHABA WA AJIRA???

Mosi, Kuna wahitimu wengi wa vyuo vya Ualimu kwanini wasipewe mkakati wa kuyatumia Majengo hayo kama madarasa.

Pili, Majengo hayo yanaweza tumika kama vituo vya Afya hivyo vijana wahitimu wa kada hiyo wakipewa majengo na mikakati ya kuanzisha vituo vya Afya inakuwa imepunguza uhaba wa Ajira kwa Asilimia Angalau 10% kulingana na utafiti wangu mdogo kwani kalibia kila mkoa yapo majengo hayo.

Tatu, Majengo hayo yanaweza kutumika na vijana MaIT waliohitimu pale UDOM au UDSM wakatengeneza maduka ya mitandaoni, Ukufunzi, Ufundi, na kuuza ujuzi wao juu ya mambo ya mitandao.

Nne, Sehemu hizo wapewe vijana kimkakati waanzishe, Maktaba za jamii na vyanzo vya Taarifa( Data resources Center) Watu wangapi watanufaika hapa?

Tano, Vijana waliohitimu ufundi wapewe maeneo hayo ili waanzishe ufundi wao ili wauze thamani na ujuzi wao ndani na nje ya nchi kuna mwaka nilikuwa naangalia Televisheni nikaona Nchi kama za Azbaijan wanaishi kwa kutegemea ufundi tu Fikilia tanzania tuna rasilimali ngapi ambazo zinatuwezesha kulipiku soko, Kumbuka baadhi ya miti wanayotengenezea huko ulaya, huitoa Tanzania.

MIKAKATI WANAYOPASWA KUJA NAYO SERIKALI ILI KUWAFANYA VIJANA WANUFAIKE NA MAJENGO HAYO.

A) Kuwakopesha vijana kimakundi kadri vijana watakavyokubaliana kwa umoja wao.
Tuchukulie Mfano wa kada yangu, Tunakubaliana walimu kadhaa humo atoke, Mkuu wa Shule, Mkuu Msaidizi, Taaluma na wengine Halafu tunaandika proposal kwa serikali inatukopesha pasipo riba, inawezekana Jiulize Ni wahitimu wangapi currently wanaolipa bodi ya mikopo??( Wachache), ni vikundi vingapi vya akina mama wanaorejesha mikopo yao Halimashauli??( Sina Jibu sahihi lakini naweza sema wachache) Kwanini Tusiwakopeshe watu Tuliowagharamia Shahada ya kwanza kwa zaidi ya Mamilioni?? Serikali ikiamua inawezekana, pia itachangia Upatikanaji wa Elimu Bora kwa gharama Nafua.

B)Serikali Kutoa Msaada kwa Masharti nafuu kwa Vijana wahitimu ili kuyaendeleza Majengo hayo.

C) Wakandalasi kuyatunza Na kuyakabidhi majengo hayo baada ya ujenzi au matumizi husika.
Binafsi Nimeshuhudia Majengo ya Wachina yakibomolewa nina ushahidi wakutosha hapa, kuna sehemu moja mkoani kigoma panajulikana kwa jina la mkongoro, Barabara ya Mwandiga kwenda Mnanira baada ya wachina kumaliza ujenzi wa barabara hiyo Majengo yao yalibomolewa eneo hilo lipo karibu na mkongoro sekondari au karibu na mto ujulikanao kama Kaseke, Hivyo serikali iwape mashariti hayo wakandarasi.

D) Serikali ifikishe Huduma za kijamii haswa maji na umeme kwani kuna baadhi ya sehemu za majengo hayo huduma hizo hazifiki.

NAFASI YA VIJANA.

Vijana sisi wenyewe tunatakiwa kuishawishi na kuishauri serikali, vijana kuunda vikundi ili iwe rahisi kuandika mpango kazi, Vijana wengi si waaminifu haswa linapokuja swala la hela, Japo nimeshuhudia baadhi ya vijana wamefanikiwa kwa kutengeneza muungano wakaanzisha kituo cha kujifunzia ama kwa kokidi eneo au kwa kuomba kwa serikali, wamefanikiwa kufika mbali, ni mfano wa kuiga.
Mwisho ni lai yangu kwa Serikali na vijana hasa wahitimu tufikilie namna ya kupunguza uhaba wa Ajira, kwa utafiti wangu tu kama vijana watapewa Majengo yaliyotelekezwa wakaanzisha vitu vinavyoendana na ujuzi wao tatizo la Ajira litapungua kwa Asilimia 10% .

ASANTE KWA KUSOMA ANDIKO HILI UBALIKIWE👏
 
Huwa nafikilia serikali ina wexa kutukopesha zaidi ya mil12 ili tusome vyuo kwanni isiweke utaratibu wa kuwapatia vijana mikopo hasa wanapohitimu vyuo vikuu sio case basi kwenye hizo mil12 watenge hata mil1 au 2.
vijana wakielimishwa wanaweza
 
Huwa nafikilia serikali ina wexa kutukopesha zaidi ya mil12 ili tusome vyuo kwanni isiweke utaratibu wa kuwapatia vijana mikopo hasa wanapohitimu vyuo vikuu sio case basi kwenye hizo mil12 watenge hata mil1 au 2.
Mimi na vijana wenzangu tumekopeshwa ml 20 na serikali ya Magufuli na kuanzisha Kiwanda
 
Karibu, nilipotea kidogo hewani, kuvote unabonyeza kitufe cha kupanda kilicho mwishoni mwa andiko hili ukiona kula zimeongezeka na umeambiwa upvoted unakuwa tayari umepiga kura kinyume cheke kura hupungua Asante usisite kunipa mrejesho, na
Sijui kama nimevote, please niambie
 
Karibu, nilipotea kidogo hewani, kuvote unabonyeza kitufe cha kupanda kilicho mwishoni mwa andiko hili ukiona kula zimeongezeka na umeambiwa upvoted unakuwa tayari umepiga kura kinyume cheke kura hupungua Asante usisite kunipa mrejesho, na
Naomba kura yako nimhimu kwangu. pia nina andiko langu jingine usisite kulitembelea!
 
Mimi na vijana wenzangu tumekopeshwa ml 20 na serikali ya Magufuli na kuanzisha Kiwanda
Mimi na vijana wenzangu tumekopeshwa ml 20 na serikali ya Magufuli na kuanzisha Kiwanda
🙏🏾 Big up mkuu, Hongereni sana mimi nimegraduate mwaka jana sasa hivi nipo mtaani ndo najitafta ila mtaani ushindi upo, Vijana tupeane michongo.
 
Mkuu big up sana, upo vizuri nyuzi zote zako mbili zinafika kwenye suluhisho moja kwangu mimi nimelielewa kuwa tunatakiwa kuwa wabunifu pia kutumia kila rasilimali tuliyopo nayo, Asante umenifunza vingi!✍🏽✍🏽
 
Asante karibu, pia naomba kura yako!
Mkuu big up sana, upo vizuri nyuzi zote zako mbili zinafika kwenye suluhisho moja kwangu mimi nimelielewa kuwa tunatakiwa kuwa wabunifu pia kutumia kila rasilimali tuliyopo nayo, Asante umenifunza vingi!✍🏽✍🏽
 
Nilichokipenda ume-address sulusheni moja kwa moja hongera!

Yaeh Ni kweli Ameeleza suluhisho moja kwa moja ni kweli pia hayo majengo yapo, ni kweli pia uwezekano wa kuyatumia kwa namna hiyo upo, nampa kura yangu, andiko hili nitasaidia kushea lifike kwa wahusika.
 
Serikali ikiacha ubize wa kukimbizana na Mbowe inaweza maliza tatizo la ajira nchini na sio kuwatgemea wachumi Jamii ya mwigulu
 
Njia pekee ya kumaliza tatizo la ajira nchini ni kuwekeza kwa vijana wapewe maarifa ya kuzalisha,milango ya uchumi ifunguliwe,vyuo vya maendeleo, ufundi,kilimo vijengwe kila kata vijana wapate maarifa namna ya kuzitambua fursa zinazowazunguka.
Watu ni masikini sababu ya upofu ukosefu wa maarifa ya kuona fursa zinazowazunguka kuwa mtaji
 
Serikali ikiacha ubize wa kukimbizana na Mbowe inaweza maliza tatizo la ajira nchini na sio kuwatgemea wachumi Jamii ya mwigulu
Sawa sawa, kama sijakosea unamanisha kama taifa lazima tuwe na vitu msingi vya kuvitilia mkazo, tuwe na standard moja inayotakiwa kutuvusha, kama taifa tuwe na vipaumbele vyenye kuleta ukombozi kwa vijana, kismsingi tatizo la ajira limekuwa kubwa sana.
 
Njia pekee ya kumaliza tatizo la ajira nchini ni kuwekeza kwa vijana wapewe maarifa ya kuzalisha,milango ya uchumi ifunguliwe,vyuo vya maendeleo, ufundi,kilimo vijengwe kila kata vijana wapate maarifa namna ya kuzitambua fursa zinazowazunguka.
Watu ni masikini sababu ya upofu ukosefu wa maarifa ya kuona fursa zinazowazunguka kuwa mtaji
Upo sahihi💯 % Na nikwambie tena kwa tanzania upofu upo wa aina nyingi!
 
Sisi nyumbani kuna msemo usemao " Umwana wuwundi ahanzula ahomba" ukiwa unamanisha kwamba mtoto wa mwengine asipate wakati wa kutafta, mfano huo ni sawa sawa na serikali yetu haitaki watoto wawengine wapate, wasichokijua kuwa mtu mmoja anapofanikiwa ni rahisi kwa wengine kupanda juu.
Watu ni masikini sababu hawana maarifa sababu ya ukosefu wa serikali makini.
 
Sisi nyumbani kuna msemo usemao " Umwana wuwundi ahanzula ahomba" ukiwa unamanisha kwamba mtoto wa mwengine asipate wakati wa kutafta, mfano huo ni sawa sawa na serikali yetu haitaki watoto wawengine wapate, wasichokijua kuwa mtu mmoja anapofanikiwa ni rahisi kwa wengine kupanda juu.
Ubinafsi ni sumu ya maendeleo. Umasikini wetu chanzo ni ubinafsi
 
Back
Top Bottom