Si bora mmepata hizo mbovu? Je mngekosa kabisa?
Kimsingi mjadala stahiki hapa si Magufuli au makandarasi bali ni kwa jinsi gani Tanzania inatakiwa kuimarisha usafiri wa reli ili kupunguza kutumia njia ya barabara kusafirisha mizigo mizito. Hata hizo barabara zijengweje hazitamudu uzito wa mizigo kwa muda mrefu. Ni wakati wa nchi kuimarisha usafirushaji kwa njia ya reli na mabomba. Hakuna haja ya malori ya mafuta kutoka dar kwenda tunduma. Kwa nini tusijenge bomba la kusafirisha mafuta?Magufuli anajua kucheza na vyombo vya habari na waandishi wetu vilaza barabara nyingi zinazojengwa sasa wakati wake hazidumu kuna barabara nyingine zinaumuka sijui kuna tatizo gani ni kweli zamani tulikuwa na barabara chache lakini zilikuwa za ubora wa hali ya juu
si bora mmepata hizo mbovu? Je mngekosa kabisa?
Sugu angeiweka hii vizuri. Mwenzake Kafulila kasema vema asubuhi bila kuwa na reli bora nchini hizo barabara mtalaumiana tu. Link ya Makambako-Songea ina low traffic volume kulinganisha na maeneo mengi ya nchi na infact ujenzi ule wa lami ilikuwa na kuchochea maendeleo ya mkoa wa Ruvuma. Vinginevyo mkoa ungetengwa sana ule. Hata hivyo kwa sasa barabara imechoka kiasi kwamba serikali inatakiwa kuachana na type of maintenance inayofanyika ili kuokoa link hiyo. Kwa uchache nawasilisha.
Unasema sugu amekutelekeza si uende ustawi wa jamii
Kwa kweli inasikitisha sana barabara zote walizojenga awamu hii ni majanga nyingine kabla ya makabidhiano wanaweka viraka.
Hivi mbeya jiji zima mliona huyu ndo m2 wa kuwasilisha mawazo yenu bungeni? ok any way ndo demokrasia hiyo.
NB: Magufuli ni vema huyu usimjibu endelea na shughuli zako, hapa Nyamirembe na Kazunguti mpaka kachwamba jimboni chato maji hayafiki kutokea ziwani tafadhali jitahidi kutatua na Mungu akubaliki sana kazi yako tunaiona na kukuombea sana Maana Magufuli vs Sugu..... ni almas vs kinyesi.
Natangaza dau kwa mwanajamvi atakayetaja barabara mpya yenye kipande cha urefu wa zaidi ya km 3 ambacho hakina kasoro ya kuhitaji marekebisho
Hoja ya uimara wa Makambako- Njombe-Songea ni ya kweli na ya msingi, lakini kwa mtu mwenye FIKRA HURU, anaefuata mkumbo hawezi kuliona hilo na kujiuliza!
Si bora mmepata hizo mbovu? Je mngekosa kabisa?
itakua labda kamlipua kwenye verse za huipu hopu, lakini hana credentials za kuhoji utendaji wa magufuli. waliomchagua walikosa mbadala wake ila 2015 hawatakosea tena kumrudisha bungeni