Mapokezi ya ndege, Rais Magufuli: Wasiofurahia ujio wa ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner, watapata tabu sana

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009

Ni nderemo na vifijo hapa uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalim Julius Nyerere ambapo rais Magufuli anapokea ndege ya wananchi wa Tanzania aina ya Boeng 787 dreamliner inayobeba abiria 262. Hakika Magufuli na serikali yake amethubutu na ameweza.

Fuatilia uzi huu kwa updates.

UPDATES:
5.jpg

Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali ikiwasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Updates. Viongozi mbalimbali wa kitaifa wanazidi kuingia apa. Mawaziri waandamizi akiwemo Makame Mbarawa waziri wa maji, Alois Mbwelwe waziri wa ujenzi na uchukuzi, seleman Jaffo waziri wa TAMISEMI pamoja na naibu mawaziri, wabunge, wenyeviti wa bodi za taasisi mbalimbali za umma, makatibu wakuu wa wizara na mashirika pamoja viongozi wa vyama siasa. Wananchi ndio usiseme

Makam wa rais samia suluhu Hassan anaingia hapa

John Momose Cheyo asema lazima tutumie barabara zetu za angani. Hivyo tununue ndege nyingi sana

Mrema: Tanzania ya viwanda inawezekana kwa kuwa na usafiri wa uhakika na pia biashara inakuwa rahisi kukiwa na usafiri wa uhakika. Tumuuge mkono rais

Rais Magufuli ameingia sasa uwanjani apa kuongoza rasmi mapokezi haya

Hii ni mubashara kupitia vyombo vya habari hususan tbc1

Updatesss!!!!
Rais wa Tanzania Dr Magufuli ameingia ktk viwanja hivi tayari kuongoza mapokezi haya makubwa na tayari wimbo wa taifa umeimbwa na sasa ni dua maalum kutoka kwa viongozi wetu wa dini

Ameomba dua mufti wa tanzania kisha kiongozi wa makanisa ya kkkt na sasa ni mwenyekiti wa kamati ya amani alhad musa ambaye pia ni sheikh wa mkoa wa dar es salaam

Katibu mkuu wizara ya ujenzi anatambusha viongozi mbalimbali waliohudhuria apa. Mawaziri, kamati ya kudumu ya bunge ya miindombinu, makatibu wakuu wizara mbalimbali, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wenyeviti wa bodi mbalimbali nk

Updatessssss!!!!
Hapa mbele ya rais linafanyika zoezi la kusaini mkataba wa makabidhiano wa ndege hii kati ya serikali ya Tanzania na shirika la ndege la tanzania la ATCL

Masainiano haya yamefanyika kati ya katibu mkuu kiongozi na katibu mkuu wizara ya uchukuzi na wasiliano nchini. Hivi sasa waziri wa ujenzi na mawasiliano anaelezea hatua mbalimbali muhimu za maendeleo katika wizara hii

Rais anamkaribisha kaimu balozi wa Marekani nchini ambapo ndege hii imetoka, ambaye anatoa maneno kidogo kwa kutumia lugha ya kiswahili

Upsatesss!!!
Sasa rais anaendelea.
Rais anasema ndege hii imetoka moja kwa moja marekani haijapita sehemu yyte ile. Anasema mfumo wa mawasiliano wa ndege hii ni mzuri mno kiasi kwamba amekuwa akiwasiliana nao wakati wote wakiwa angani.
Anasema ana imani kuwa watz wote tumefrahi sana kwa ujio wa ndege hii. Ambao hawajafurahi watapata tabu saaaanaa

Rais anasema ndege yetu nyingine kama hii itatua januari 2018 na amemuomba balozi wa marekani kuhakikisha ndege hiyo inafika kwa wakati uliopangwa bila kukosa. Anaeleza changamoto alizozikuta zilizokuwa zinalikabili shirika la ndege ambapo tz ilikuwa na ndege moja tu halafu ilikuwa mbovu. Sasa tunazo Nne mkononi na zinakuja zingine tatu . Na tumenunua kwa fedha zetu wenyewe sio mkopo

Rais JPM anasema "kama kuna mtu ambaye hafurahii ujio wa ndege hii basi atapata tabu sana"!

Updatesss!

Tufuatilie hotuba ya rais.
Rais anasema ndege nyingine tatu aina ya bombadier zitafika nchini desemba mwaka huu. Rais anasema mafanikio haya ni matokeo ya uchapaji kazi wa watanzania wote. Anawapongeza watanzania wote na anawaomba walipe kodi ili kuweza kununua ndege zingine zaidi. Anawapongeza sana watz wote

Rais anaeleza sababu za kuamua kulifufua shirika la ndege la Tanzania. Kuwa ni kurahisisha mawasiliano na usafiri na kuondoa aibu ya nchi yetu ambayo ina rasilimali nyingi na vivutio vingi lakini havimnufaishi mwananchi wa kawaida.

Usafiri wa uhakika wa ndege utawezesha wananchi kufikia kirahisi masoko yaliyopo nje ya nchi ikiwemo kuuza samaki nje ya nchi, maua yaliopo arusha na mbeya, pia lengo lingine ni kupunguza gharama za usafiri wa anga.

Leo hii kwenda bukoba ni shilingi laki 4 badala ya milioni moja

Lengo lingine la kufufua shirika letu la ndege ni kupanua wigo kwny sekta ya utalii nchini ambapo sekta hiyo haituingizii fedha za kutosha za kigeni kwa sababu ya kukosekana usafiri wa uhakika

Rais anaelezea miradi mbalimbali ambayo serikali inatekeleza ikiwamo kujenga madaraja ya juu nchini hususan katika jiji la Dsm ili kurahisisha usafiri wa jiji hilo, miradi mikubwa ya umeme nchini ikiwamo stiglers gorge, kinyerezi one na two, kuboresha barabara korofi nchini pamoja kujenga hoslitali 67 za wilaya nchini

Updatesss!!!
Ndege yetu inajiandaa kutua .....ipo kwenye anga la tanzania. Tanzania hoyeee. Ndege hiyooooo inashuka jamani hiyoooo

======

Baada ya sala ya Madhehebu yote yalioandaliwa, anayeanza kuongea na kutoa salamu na utambulisho ni Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda.

Makonda anasema;

Mhe. Rais si kwamba wananchi hawa ni wanyonge, bali ni mshangao wa umewezaje kufanya mambo haya kwa muda mfupi.

Kwakuwa leo ni jumapili, naomba uniruhusu nikupitishe kwenye maandiko matakatifu. Amesoma Waefeso 4:11
"11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;.

Nlipotazama watumishi wote watano, nikamuona ambaye hapendwi ambaye ni nabii. Nabii husema ukweli na kutabili. Rais Magufuli umedhihilika wewe ni nabii tuliyekuwa tunamsubiri kwenye taifa hili. Wewe ni sawa na nabii Ezekiel. Umetamka kwenye bandari, umetamka kwenye ndege, reli, ttcl. Yote uliyoyatamka yanatendeka. Rais Usiumie na anayekusema, akusemaye amsema nabii wa bwana. Taifa letu lina amani na kila aina ya wageni wanakuja.

Rais umetupa heshima, wananchi wote hawa wanakuombea kwa Mungu. Kila anayesema neno kinyume na mafanikio haya, hakupingi wewd bali anapinga mafanikio. Ukisikia mtu akisema Magufuli hajafanya kitu, mwambie kama huwezi kuona tega masikio yako utasikia.

Leo ninao ndugu zangu wameamua kuungana na wewe, Sekta binafsi wakiongizwa na Mengi, watu wa mabenki na watu wa makampuni wote wamekuja kukuunga mkono. Wapo wasanii, JB na Steve Nyerere walikuwa wanapigana nani awe wa kwanza kuingia kwenye ndege. Wapo wabunge wa Dar Es Salaam. Yupo mtulia, mhe. Rais matokeo yale ya kinondoni, ni shukrani zako kwa kazi unayoifanya. Hapa wapo Makada wa CCM, Machinga na shirikisho la vyuo vikuu. Hapa wamekuja kamati ya Amani, Kamati ya ulinzi na usalama wote wa Dar. Wapo wazee wa Dar zaidi ya 50. Yupo Meya wa Jiji mhe. Isaya. Wenzake walitaka kuja wakaona aibu sababu walisema ndege hakuna.

Tunao viongozi wa vyama mbalimbali akiwemo Dovutwa, Mrema, Cheyo na Lipumba yupo njiani. Tupo na Viongozi wa dini. Tunaye Mufti mkuu Abubakari Zuberi kwa niaba ya wenzetu Waislam, tunaye kiongozi wa KKKT Baba Askofu Alex Malasusa akiongoza Viongozi wa Kikristo na wengine wengi.

Rais umetufanyia mengi katika jiji letu. Tunakuomba usichoke, mafanikio yako ndio mafanikio yetu, anguko lako ndio anguko letu sisi viongozi wa chini.

Leo nakuomba mbele ya watanzania hawa, uniruhusu au nikuombe kwa lugha nyingine, usichukue hata dakika moja kumfikiria mtu anayesema kinyume na mafanikio haya. Niachie hilo jukumu mimi ni mtaalam wa kujibu na ntajibu kwa niaba yako. Nakubembeleza Mhe. Rais mimi ntajibu kwa niaba yako. Acha tukuache mahala patakatifu Ikulu, uendelee kutafakari kazi ya Watanzania kwa utimizaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi. Ili sisi tuhangaike na hawa wanaotukanatukana na kuongeaongea kwenye mitandao, huo uwezo tunao. Kama kuna mtu ataanza kuiponda hii ndege, ntajibu kwa niaba yako

Sasa anaongea katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamuriho.

Dkt. Leonard Chamuriho anasema;

Mheshimiwa Dr. Magufuli, napenda kuchukua fursa hii kutambulisha viongozi wachache waliokuja kuungana nawe. Tunaye makamu wa rais Samia, tunaye Waziri mkuu Majaliwa, Katibu Mkuu wa CCM bashiru Ali. Rais tunao Mawaziri wakiongozwa na Kamwele. Wapo pia manaibu waziri. Tunaye katibu mkuu kiongozi Kijazi. Tunayo kamati ya kudumu ya miondombinu ya Bunge.


Kuna wageni watakaotoka Marekani watakuja na ndege kutoka Marekani. Wapo wa kampuni tatu. Ndege kubwa hutengenezwa na kampuni tofauti.

1. Kampuni ya kwanza Boeing wao walitengeneza Bodi ya ndege. Boeing wametuma wageni wanne.

2. Kampuni ya pili ni ya Kampuni iliyotengeneza Injini. Kampuni hiyo ni Rolls-Royce ambayo imetuma wageni wawili.

3. Kampuni ya tatu ni Panasonic iliyotengeneza Mifumo ya ndani ikiwemo simu, video, na Viburudisho. Wameleta mgeni mmoja.

Naomba niongelee kuhusu hii kampuni ya ndege ya Tanzania ambayo itaendesha hii ndege kwa kukodi kutoka kwa taasisi ya serikali ambayo imekaimishwa kuzinunua na kuzihudumia. Shirika letu hili serikali imeendelea kulliboresha na kuboresha mifumo kama tehema ya kisasa, tumegaramia vipuri vya awali na kutoa mafunzo kwa marubani na wahandisi wazalendo ikiwemo kuboresha kalakana.

Ndege tatu tulizonazo ambazo zimeshawasiri Q 400,kwa sasa zinatoa huduma katika miji 12 ambavyo ni; Bukoba, Dar Es Salaam, Arusha, Mtwara, Songea na Zanzibar na kituo cha hayaya cha Comoro.

Kwa hii ndege mpya ambayo tunaipokea leo, tutaanza kuitumia kwa safari wa anga kwa safari za ndani za nchi katika vituo vya Dar, Kilimanjaro na Mwanza. Marubani wetu watafanya route training hapa nchi.

Baada ya hapo kuanzia mwezi Septemba mwaka huu ndege hii itaanza kwenda nje ya nchi miji ya bombay, Guan zhong, na Bangkok Thailand. Tumeanzisha utaratibu ambao umetuwezesha kwenda katika nchi za Uingeleza na katika soko la anga. Na tutaendelea kupanua huduma hizi katika siku zijazo.

Mheshimiwa rais, Usafiri wa anga unapitia katika changamoto hasa wakati huu wenye ushindani mkubwa. Baadhi ya changamoto ni Uchache wa Marubani na wahandisi wa ndege. Msimamo wetu ni kufundisha Marubani na wahandisi wazawa. Dkt. Leonard Chamuriho amemaliza.

Sasa ni zamu ya katibu mkuu kiongozi Mhandisi John William Kijazi.

John Kijazi anasema;

Kwa mara ya tatu katika kipindi kisichozidi miaka miwili, leo tumekusanyika hapa ili kuhushukudia nchi yetu ikiendelea kuandika historia katika usafiri wa anga 18 septemba 2016 tulishuhudia mapokezi ya ndege mpya 2 na kwama huu ulizindua nyingine tena. Na leo unazindua ndege ya nne Boeing 787-8 Dreamliner kati ya saba serikali ilizozinunua.

Uwamuzi uliofanya na serikali wa kununua ndege una manufaa makubwa kwa nchi yetu.

Itaongeza ushindani na kuleta unafuu wa gharama za usafiri wa anga, Shughuli za biashara, ukwezaji na utalii zitaongezeka. Ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 262 wakati nyingie zinabeba 76.

Ni mara ya kwanza kwa nchi yetu kuwa na ndege kubwa na ubira wa namna hii

Ndege hizi saba ni mali ya Serikali. Zinakabidhiwa kwa shirika la ndege la taifa ATCL kwa njia ya kuwakodisha ili wazisimamie. Wito wangu kwa ATCL ni wazitunze ndege hizi ili wazalishe na kuilipa Serikali kwa Mujibu wa Mikataba iliyopo.

Sasa ni nafasi ya Mhandisi Isack Kamwelwe kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Waziri Kamwelwe anasema;

Kwanza nakushukuru kwa kuniteua katika wizara inayoongoza kwa shuguli za kiuchumi.

Mheshimiwa rais nikuponeze, hizi ndege ni juhudi zako mwenyewe, juhudi binafsi.

Leo tunapokea ndege yenye kubeba abilia 262 na mwezi kumi na moja 2018 tutapokea ndege nyingine mbili za CS 300 yenye kubeba abiria 132 kila ndege. Tumelipia ndenge nyingine kama hii tunayoipokea leo ambayo tutaipokea January 2020.

Sasa ni zamu ya Rais Magufuli

Rais Magufuli anasema;

Kabla sijasema lolote, naomba nimkaribishe kaimu balozi wa marekani ambayo ndo ndege imetoka., halafu baadae nitaendelea.

Kaimu Balozi wa Marekani anasema;

Leo ni siku ya furaha kwa Tanzania na Marekani kwa hatua kubwa kwa sekta ya usafiri wa anga ya nchi ya Tanzania, Najivunia kwamba kampuni ya Marekani inatoa mchango muhimu, Nashukuru rais Magufuli, tupo hapa kujenga pamoja Tanzania yenye neema na usitawi, Asanteni.

Rais Magufuli: Itifaki imezingatiwa. Ndugu zangu, nmepata taarifa ndege imeshapita maeneo ya Mwanza, kwahiyo kwenye saa kumi na moja na dakika kumi itakuwa imeshatua hapa. Na imetoka moja kwa moja Marekani bila kutua, Wamenipigia simu wakiwa Ureno, wakapita maeneo ya Chad, wakapita Kongo, Uganda na wananyosha maoja kwa moja kuja hapa. tumshukuru wmenyezi Mungu kwa kuifika ndege yetu salama hapa nchini, Ndo maana nmeona nizungumze nmalize ili ikishafika iwe ni shughuli za ndege, Nmeona nmalize hotuba yangu.

Ninaimani kubwa kuwa watanzania wote tumefurahia ujio wa ndege yetu hii, kama kuna ambao hawajafurahia, basi watapata tabu sana.

Nawashukuru Wizara wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano kwa kunialika na nina shukuru kwa kujitokeza kwenu kwa wingi kwenye hafla hii. Naishukuru Kampuni ya Boeing ya Marekani iliyokubali kututengenezea ndege hii. Waziri wa Marekani atufikishie shukurani zetu kwenye kampuni ya Boeing na uwaombe ile ndege nyingine waikamilishe mapema na fedha za kununua zipo na tumeshatanguliza za mwanzo,

Moja ya ahadi katika uchaguzi wa 2015 ilikuwa ni ya kufufua ATCL ambayo ilikuwa na ndege moja inayobeba watu 51 na ilikuwa inahudumia Dar, Arusha na Mwanza. Nayo ilikuwa ikishinda kwenye kalakana.

Mafanikio haya hayajileta yenyewe, nawapongeza watanzania kwa kuchapa kazi, hongereni sana. Kuwa na ndege 7 katika kipindi cha miaka miwili na nusu ilikuwa ni ndoto, Huu ni uthibitisho kwamba watanzania tukiamua tunaweza.

Serikali iliamua kufufua Shirika la ATCL kwa sababu tatu

1. Kujijengea heshima. Nchi kubwa yenye almas dhahabu watu hamsini miliono lakini hawana ndege

2. Tumefufua ili kuboresha usafiri wa anga nchini, Hakuna nchi isiyohitaji usafiri wa ndege. Watanzania wanahitaji usafiri wa ndege. Watu walikuwa hawatumii ndege kwa sababu ya kutokuwepo kwa safari za uhakika nchini. safari zilikuwa ni Dar, Arusha na Mwanza watu watapandaje ndege?, gharama zilikuwa kubwa. Mfano dar to Bukoba ilikuwa ni Milioni moja kwenda na kurudi, hii ilikuwa gharama kubwa. Sasa hivi gharama zimepungua. Sasa hivi kwenda bukobana kurudi ni shilingi lakini nne. Zamani kwa mwezi wasafiri wa ATCL walikuwa 4,000 kwa mwezi, sasa ni 21,000 kwa mwezi. Gharama zimepungua.

3. tuliamua kufufua ili kukuza sekta ya Utalii. Mwaka jana tulipokea watalii 1.3 tu. Sehemu yenye mashirika imara wanapokea watalii wengi. Mfano Misiri wanapokea watalii Mil. 10 kwa mwaka. Mwaka jana watu Bil 4 walisafiri kwa ndege, Watalii waliosafiri ni Bil 1.3 na 70% ya hao watalii walitumia ndege. Hii ndege itatusaidia.

Adhima na dhamira ya Serikali ya CCM ni kuleta maendeleo katika nchi yetu. Mbali na kuimalisha Sekta ya anga, tumeimalisha pia usafiri wa maji, tunapanua bandari ya Dar, Mtwara na Tanga. Tunaboresha utendaji wa kazi. Wakati tunachukua hatua kwenye Bandari ya Dar, kuna watabiri walikuwa wanasema tunafukuza wateja, sasa watabiri wameanza kuaibika.

Tunaendelea na uimarishaji na Usafiri wa Ardhini ikiwemo reli. Tunakarabati reli ya Arusha hadi tanga, Tumekarabati Meli ya Ummoja maarumu kwa kubeba Makontena kwenda Uganda, Tunajenga flyover ya Tazara ambayo tutaiita MFUGALE. barabara nyingi zinajengwa na madaraja Wakazi wa Mwenge, Sinza Tandale, Kijitonya na kwa Mtogole Dar Es Salaam mtakuwa mnaona kazi inayofanyika. Tunatekeleza miradi ya Umeme Kinyelezi natupo mbioni kutekeleza mradi ya Bwawa la Kidunda kwa ajili ya Maji kwa jiji la Dar na stiegler's gorge kwaajili ya Umeme. Ujenzi wa hospital za Wilaya 67 kwa gharama ya Bil. 104.

Nilipokuwa nyumbani, nmeona comment mlizokuwa mkizoa kuhusu ndege hii, nawashukuru sana. Kujitokeza kwenu kwa wingi namna hii ni kwamba mnatambua umuhimu wa ndege hii kwa nchi yetu.

Nahitimisha kwa kutoa wito kwa Bodi na menejimenti ya ATCL kuendelea kufanya kazi kwa bidii. Tumetumia fedha nyingi, hivyo msiwaangushe Watanzania.

Watu wachache wa kukosoa huwa hawakosi. Nawaomba watanzania tushikamane, tumefanikiwa hili, tutafanikiwa na mengine.

Asante.

Habari zaidia...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 08 Julai, 2018 ameongoza mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliimarisha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL).

Mapokezi ya ndege hiyo yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Wabunge, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Wakuu wa Mikoa, viongozi wa Dini, viongozi wa vyama vya siasa, wadau wa usafiri wa anga wakiwemo wafanyabiashara na wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

Ndege hiyo imewasili majira ya saa 11:10 jioni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kisha kupewa heshima ya kumwagiwa maji (Water Salute) na baadaye Mhe. Rais Magufuli akiwa na viongozi wakuu walioambatana nae akaizindua rasmi na kuikagua kwa kuingia ndani ya ndege ili kujionea mandhari ya ndani.

Akizungumza kabla ya kuwasili kwa ndege hiyo Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Watanzania kwa kuchapa kazi na kulipa kodi, na hivyo kuiwezesha Serikali kupata fedha za kutekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ununuzi wa ndege kwa ajili ya kuimarisha ATCL ambayo ilikuwa na hali mbaya.

“Shirika letu la ndege lilikuwa na hali mbaya sana, lilikuwa na ndege moja tu tena ilikuwa inafanyiwa matengenezo mara kwa mara, soko la ATCL lilishuka sana hadi kufikia asilimia 2.5, lakini sasa tumenunua ndege 7, hii ni ndege ya 4 na nyingine mbili zitakuja kabla ya mwaka huu kuisha, na nyingine kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner itakuja mwaka 2020.

“Tangu tumeongeza ndege 3 mpya aina ya Bombardier Q400 biashara ya ATCL imeongezeka, Shirika letu lilikuwa linasafirisha abiria 4,000 tu kwa mwezi lakini sasa linasafirisha abiria 21,000 na ndege zinatua katika vituo 12” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amebainisha kuwa Serikali iliamua kuchukua hatua ya kulinusuru Shirika la Ndege la Taifa ili kujenga heshima na kulinda hadhi ya Taifa, kuimarisha na kuboresha huduma za usafiri wa anga na kukuza utalii.

Mapema akitoa taarifa ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyowasili hapa nchini leo, Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege hiyo yenye uwezo wa kuchukua abiria 262, itaanza kutoa huduma kwa safari za ndani katika vituo vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza, mwezi Septemba itaanza safari zake kwenda Bombay nchini India, Guangzhou nchini China na Bangkok nchini Thailand na kwamba utaratibu umeanza ili ifanye safari za kwenda Uingereza na miji mingine duniani.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Inmi Petterson amewapongeza Watanzania kwa mafanikio makubwa ya kununua ndege hiyo kutoka nchini Marekani na amesema hiyo ni hatua muhimu ya Tanzania kujenga uchumi wake.

Viongozi wa Dini waliohudhuria katika tukio hili wameongoza dua ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mafanikio haya makubwa na kuliombea Taifa pamoja na Mhe. Rais Magufuli katika majukumu yake ya kuongoza juhudi za kuleta maendeleo.

Katika sherehe hizo Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi amekabidhi ndege hiyo ya Serikali kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho kwa ajili ya kuikodisha ATCL ili kuanza kuitumia.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

08 Julai, 2018
1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali.
2.jpg
4.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege hiyo mpya na yakisasa aina ya Boeng 787-8 Dreamliner ambayo imenunuliwa na Serikali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 
Ratiba ya mapokezi ya ndege yetu ya Nne aina ya boeing 787 inayobeba abiria 262
IMG-20180708-WA0079.jpg
 
Ndege haina utofauti na baiskeli maendeleo take yanapotea kama upepo
 
Waziri wa mambo ya ndani anaingia pamoja na waziri wa ulinzi Dr Hussein Mwinyi
 
Hongera Rais , hakika IPO siku utakumbukwa na wanaokupiga mawe
 
Back
Top Bottom