Suala la Utawala Bora Serikalini, Rais Samia na Hayati Magufuli lao moja tu wanaangalia siasa zaidi kulipo productivity

JPM aliondoka akiwa amevuruga kabisa mambo ya good governance Serikalini na hasa kwenye Taasisi zake. Enzi za Mkapa mpaka JK, nafasi za nyeti Serikalini angalau watu walishindanishwa.

Sheria nyingi za Taassis zinaonesha utaratibu wa kupatikana kwa viongozi wa Taasisi na nafasi za juuu.

Mfano kumpata DG wa TCRA, EWURA, FCC, OSHA, TIC, ATCL, nk. kunaelekezwa kabisa kuwe na ushindani.

JPM aliachana kabisa na utaratibu huo na kwanza ilifkia hatua hata wajumbe wa Bodi mbalimbali kuteuliwa tu alivyotaka yeye.

JPM ameacha Taasisi nyingi zikiwa hazina Bodi na watendaji wakubwa ambao ama wanakaimu ama aliwapachika wake bila kufuata taratibu.

Angalia yule CEO wa Benki ya Kilimo alivyokuwa hafai lakni ndiyo akampa hivyo hivyo (Heko Samia kumtumbua huyu mtu).

Ilidhaniwa Samia sasa atakuwa kurekebisha lakini na yeye imekuwa vile vile. Taasisi nyingi zina nafasi za wazi za watendaji wakuu na maaofisa waandamizi.

HAzijazwi hizi nafasi ila tu anapopatikana mtu wao kutoka CCM wanamweka pale mara moja. Ni Ofisi ngapi hazina watendaji wakuu?

Ni Ofisi ngapi ambazo siku hizi watumishi hawashindanishwi kushika nafasi za juu?

Eti Erio kapelekwa na kupachikwa tu FCC wakati huyu bwana maisha yake yote yalikuwa kwenye Mifuko ya Pensheni.

Minafasi ya wajumbe wa Bodi ipo mingi haizibwi na kufanya Taasisi hizi zishindwe kufanya kazi zake.

Samia achana na mambo ya kikale ya kazi iendelee. Ni bora kusema "Achana na ya kale, tufanye kwa ujuzi Zaidi".

Kusema kazi iendelee ni sawa kusema manyanyaso yaendelee!
MAGUFULEGACY
 
Back
Top Bottom