Suala la mzee Mwinyi kuzikiwa Zanzibar wala lisifanywe la kisiasa, pitieni hapa msome muelewe sababu

Familia yake ndiyo wana maamuzi
Azikiwe wapi!

Ova
Wabongo wengi suala la kusema "naheshimu maamuzi yako katika jambo hili ambalo una uhuru wote wa kuamua wewe binafsi, hata kama mimi nisingeamua hivyo" ni suala gumu sana.

Yani hata ukimwambia mtu mimi napenda nyekundu sipwndi bkuu, hawezi juelewa juwa huo nibuamuzi wa binafsi na una uhuru huo.

Atataka kukusema "wewe utapenda vipi nyekundu wewe?".

Wengi masuala ya faragha ya binafsi, uhuru wa binafsi, ni masuala magumu sana kuyaelewa.

Kwa sababu wamezoea kuswagwa kama ng'ombe na kuishi kwa kukariri formula na kwenda kwa amri kutoka juu.

Hawajui uhuru ni nini.
 
Ukichota mchanga bara ukaenda kuumwaga zanzibar kuna shida gani.
A dead body is nothing, ukifa we sii kitu, unaliwa na wadudu iwe bara iwe znz
Imagine watu wanaiingilia familia ya wenzao kwenye suala la mazishi.

Unailazimisha vipi familia ya watu wasiokujua wapi wamzike baba yao?
 
Mwinyi hata nyumba Zanzibar Hana, Sasa alikuwa anaishi Kwa nani, AU kwenye Yale maflat ya pale unguja ?
Mkuu,

Tuseme Mwinyi hakuwa na nyumba Zanzibar, just for the sake of argument.

Hao watu wote wanaoishi Dar wana nyumba zao Dar?
 
Unarudi kulekule kwenye maneno ya kuungaunga nilikokukataa mimi.

Unasema desturi zetu hivi na vile, desturi za nani? Unajua unapotulundika wote katika "zetu" unakosea? Hapo kuna makabila tofauti, dini tofauti, misimamo ya kifalsafa tofauti, unaelewa neno "zetu" linaweza kukosa maana?

Mlikubaliana wapi hizo desturi? This is a logical fallacy, argument from tradition, problem of induction.

Ali Hassan Mwinyi ndiye mtu wa kwanza kuzaliwa bara, kwenda kuwa rais wa Zanzibar, na kuwa rais wa Tanzania. Hakuna precedent ya mtu mwingine yeyote mwenye historia hiyo, sasa utatumia vipi desturi kumzika mtu ambaye maisha yake hayako defined na desturi, mpaka leo watu wanabishana kama Mwinyi ni Mzanzibari au mtu wa bara?

Unatumia vipi desturi kumzika mtu ambaye maisha yake hayako easily defined ki desturi?

Habari yoyote ya "ingekuwa mtoto wake si rais wa Zanzibar asingezikwa huko" ndiyo hizo ninazosema habari za kuunga unga. Hujui Mwinyi alifikiri nini, aliienzi Zanzibar vipi, una speculate tu.

Mimi si rais wala nini, nimeishi tu Marekani, nimepapenda, nimesema nikifa nisirudishwe Tanzania. Mazishi yangu yafanyike Marekani. Sasa ikiwa mtu kama mimi nimeamua hivyo, kwa nini iwe ajabu Mwinyi kuzikwa Zanzibar sehemu ambayo bado ni ndani ya Tanzania na huhitaji hata passport kwenda?

Huna ushahidi kwamba politics ndiyo imeamua wapi Mwinyi azikwe, hizo ni simple stories za kijiweni tu.

Manapenda sana conspiracy theories.
Hapo juu nilimjibu nikamwambia kwamba binadamu akishakufa amekufa, sasa ukimzika kiembe samaki, mwanalumango, Ujerumani, UK nk haiwezi kubadilisha kitu.

Hawa hawa wanaopinga Mwinyi kuzikwa Zanzibar wakienda kanisani au misikitini utasikia wanasema kuwa binadam wote tulitoka udongoni, na tutarudi udongoni. Hivyo mtu akizikwa popote haina tatizo ilimradi mzikwaji awe amezikwa udongoni kule alipotokea. Sasa hapo tatizo liko wapi!
 
Acha roho ya kishetani. Halafu sema "mimi" sio "sisi".... usitujumuishe kwenye upumbavu wako
Umemjibu vizuri huyo mpumbavu mwenye roho ya kichawi. Siku ya kifo cha Lowasa kila uzi aliingia kumsifu na kuisikitikia familia yake kama vile na yeye ni mmoja wa wanafamilia.

Leo ameondoka mtu ambae leo hii kaifanya nchi ijue maendeleo ni kitu gani anakuja hapa kutapika mapombe yake aliyonywehwa na rafiki zake usiku.
 
Hapo juu nilimjibu nikamwambia kwamba binadamu akishakufa amekufa, sasa ukimzika kiembe samaki, mwanalumango, Ujerumani, UK nk haiwezi kubadilisha kitu.

Hawa hawa wanaopinga Mwinyi kuzikwa Zanzibar wakienda kanisani au misikitini utasikia wanasema kuwa binadam wote tulitoka udongoni, na tutarudi udongoni. Hivyo mtu akizikwa popote haina tatizo ilimradi mzikwaji awe amezikwa udongoni kule alipotokea. Sasa hapo tatizo liko wapi!
Kwani unafikiri tatizo lao ni Mwinyi anazikwa wapi?

Tatizo lao ni kwamba Mwinyi anazikwa huko "kinyume na wosia wake, ambao alisema anataka kuzikwa Mkuranga".

Na wanasema anazikwa huko kwa sababu za kisiasa.

Tatizo, huo wosia wake hawana ushahidi kwamba upo, ni wa hadithi tu.
 
MBONA UBUNGE ALIGOMBEA MKURANGA KWANI HAKUGOMBEA ALIKOKULIA na KUOA?
Rudi tena kusoma mada yangu mkuu, naona umekimbilia ku comment bila kusoma au kama ulisoma basi haukuelewa. Mimi sipingi mzee Mwinyi kuzikwa Mkuranga wala Zanzibar mkuu.

Nafikiri umenisoma vibaya!
 
Kwani unafikiri tatizo lao ni Mwinyi anazikwa wapi?

Tatizo lao ni kwamba Mwinyi anazikwa huko "kinyume na wosia wake, ambao alisema anataka kuzikwa Mkuranga".

Na wanasema anazikwa huko kwa sababu za kisiasa.

Tatizo, huo wosia wake hawana ushahidi kwamba upo, ni wa hadithi tu.
Mswahili ukimuanzishia jambo tu basi atalimalizia yeye hata kama hatojua sababu ya kulianzisha hilo jambo.

Mimi nilitambalia mlemle walipopataka. Nikawambia sawa mzee Mwinyi tufanye alitaka azikiwe kwao, lakini baadae pengine watoto wake walikaa nae wakamshauri akifa wakamzike Zanzibar na yeye akakubali.

Sasa kama amekubaliana na familia yake kuwa azikiwe Zanzibar, hawa wanaopinga au kulaumu wanatumia kigezo gani kulaumu familia ya muhusika na wakati walipokaa kumshauri mzee wao hawa wanaolaumu hawakuwepo!

Badala ya kupewa jibu nikaishia kushambuliwa tu mwanzo mwisho bila kujibiwa.
 
Halafu watu hawa hawa wasiotaka kuipa familia ya Mwinyi uhuru wa kuamua baba yao azikwe wapi, watakuja hapa kudai uhuru kutoka serikalini, kudai haki zao za kikatiba.

Wakati wao wenyewr wameshindwa kuipa familia ya Mwinyi faragha ya kifamilia tu, tena katika msiba.

Hivi hata huo uhuru wanauelewa kweli?
 
Hayo mambo yaliyojadiliwa kwenye familia ya Mwinyi kama kweli yalijadiliwa, ni siri yao.

Lakini kimsingi, siku zote mtoto lazima azikwe pale walipozikwa wazazi wake, huu ndio utamaduni wetu, unalazwa pale walipolazwa ndugu zako wengine.

Sasa leo Mwinyi badala ya kuzikwa Mkuranga anaenda kuzikwa Zanzibar, kisa alisoma huko, hebu tuambie, kwa uamuzi wenu huo, hivi hamuoni kama mmemtenga na ndugu zake wengine waliozikwa huku Bara?

Ndugu yake yupi tena atakaekwenda kuzikwa nae Zanzibar, kama ni Rais Dr. Mwinyi, hamuoni pia hawa wawili mtakuwa mmewatenga na ndugu zao wengine waliozikwa huku Bara?

Hapo ndipo unapopata picha kwamba, huu uamuzi wa kumzika Mzee Mwinyi Zanzibar, ni purely political motivated.

Ndio maana kwasababu hizo za kisiasa, watajikuta ni wao wawili pekee, baba mtu na mwanae [kama nae atataka kuzikwa huko, sababu wanasema anaogopa baba yake kuzikwa bara sababu naye ataonekana sio mzanzibar na maadui zake kisiasa, sijui akiondoka madarakani hiyo hofu itabaki au ataondoka nayo] kama itabaki, ndio wawili pekee watakaozikwa Zanzibar, huku ndugu zao wengine wote wakizikwa Bara.

I never thought kama siasa ina nguvu kiasi hiki, au ni uoga tu wa mwanasiasa mwenyewe anayeamua kuchukua maamuzi yatakayokwenda kinyume na mila na desturi zetu, kwa maslahi yake ya kisiasa, hiki kilichofanyika kwa Mzee Mwinyi, binafsi sijakipenda, tunatakiwa siku yetu ya mwisho sote tulazwe pale walipolazwa ndugu zetu kama nafasi ipo.

Na ndio maana pia, wengine wetu ambao hawana uwezo wa kusafirisha ndugu zao, hupeleka udongo wa pale alipozikwa ndugu yao nyumbani kwao uende kuzikwa huko, yote hii ni ili kuonesha umuhimu wa kumzika marehemu pale alipozaliwa, nashangaa na kusikitika kwanini wamemuondolea Mzee Mwinyi haki yake hii, ikiwa uwezo wa kumsafirisha na kumzika nyumbani kwao Mkuranga upo, sio fair.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hukufurihia kwasababu tu znz ila dar wp wng kwao mikoani lkn wanazikwa dar jua ya kwamba wk wengi wny asili ya bara na znz lkn hawakubali familia kuzikwa bara

mzee mwinyi haikufk mwezi mmoja km yupo tz lzm znz aje uhae wk wte sio km nnahadithiwa tulimuona wa znz mpk wtu wanashangaa kuambiwa sio mzanzibar lkn aliwathmin wznz kwa hali zte changa mote na misukosuko yte mzee mwinyi hakuwa nyuma zidi ya wznz

familia kukubaliana hawajakosea namna mzee alivokaa na wa znz

Wznz wanamsemo huu,sehm unapolelewa na ww nikwenu ukisoma historia yk tu huewz kulalamikia maamuzi ya familia
 
Hayo mambo yaliyojadiliwa kwenye familia ya Mwinyi kama kweli yalijadiliwa, ni siri yao.

Lakini kimsingi, siku zote mtoto lazima azikwe pale walipozikwa wazazi wake, huu ndio utamaduni wetu, unalazwa pale walipolazwa ndugu zako wengine.

Sasa leo Mwinyi badala ya kuzikwa Mkuranga anaenda kuzikwa Zanzibar, kisa alisoma huko, hebu tuambie, kwa uamuzi wenu huo, hivi hamuoni kama mmemtenga na ndugu zake wengine waliozikwa huku Bara?

Ndugu yake yupi tena atakaekwenda kuzikwa nae Zanzibar, kama ni Rais Dr. Mwinyi, hamuoni pia hawa wawili mtakuwa mmewatenga na ndugu zao wengine waliozikwa huku Bara?

Hapo ndipo unapopata picha kwamba, huu uamuzi wa kumzika Mzee Mwinyi Zanzibar, ni purely political motivated.

Ndio maana kwasababu hizo za kisiasa, watajikuta ni wao wawili pekee, baba mtu na mwanae [kama nae atataka kuzikwa huko, sababu wanasema anaogopa baba yake kuzikwa bara sababu naye ataonekana sio mzanzibar na maadui zake kisiasa, sijui akiondoka madarakani hiyo hofu itabaki au ataondoka nayo] kama itabaki, ndio wawili pekee watakaozikwa Zanzibar, huku ndugu zao wengine wote wakizikwa Bara.

I never thought kama siasa ina nguvu kiasi hiki, au ni uoga tu wa mwanasiasa mwenyewe anayeamua kuchukua maamuzi yatakayokwenda kinyume na mila na desturi zetu, kwa maslahi yake ya kisiasa, hiki kilichofanyika kwa Mzee Mwinyi, binafsi sijakipenda, tunatakiwa siku yetu ya mwisho sote tulazwe pale walipolazwa ndugu zetu kama nafasi ipo.

Na ndio maana pia, wengine wetu ambao hawana uwezo wa kusafirisha ndugu zao, hupeleka udongo wa pale alipozikwa ndugu yao nyumbani kwao uende kuzikwa huko, yote hii ni ili kuonesha umuhimu wa kumzika marehemu pale alipozaliwa, nashangaa na kusikitika kwanini wamemuondolea Mzee Mwinyi haki yake hii, ikiwa uwezo wa kumsafirisha na kumzika nyumbani kwao Mkuranga upo, sio fair.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Karume Babu zake walizikwa Malawi, yeye kazikwa Kisiwandui, na hakuna nongwa
 
Mwinyi hata nyumba Zanzibar Hana, Sasa alikuwa anaishi Kwa nani, AU kwenye Yale maflat ya pale unguja ?
Soma historia yk vzr utajifunza kitu usipoteshe fanya utafit kumbuka alikua mwalim mkuu skuli ya makadara mjni znz miaka ming kabla ya hapo alikua mwalim wa kawaida miaka mingi tu na nyumba yk ipo hadi leo na kipindi anaishi mikwechen km yupo tz hawez kufk mwez mmoja lazima aje znz akipenda kutumia usafir wa boti nenda bandarin dar utapata uhalisia na km hufahm anashamba lake sehm inoitwa kitopo mara nyingi akija anaenda wng hamfaham mnaongea kumba
 
Unaishi njombe huko ndani ndani hujui mwinyi tangu kastaafu anaishi mikocheni !

Tuma ndugu zako walioko dar waende sehemu inaitwa mikocheni Kwa mwinyi
 
Eti kaishi Zanzibar miaka 90,pale mikocheni Zanzibar?

Wamekataa kumpeleka mkuranga kwao, makazi duni ni aibu ingepata
 
Hata kwenye uzushi, kuna uzushi ubaoweza kutetewa kwa logical consistency. Ukiendekeza uzushi huo, nawwza kusema labda hapa kuna ukweli haujajulikana, unaanza kwa kuonekana kama uzushi.

Lakini, uzushi wako hauendani na logical consistency yoyote, hakuna sababu yoyote ya kumfanya Mwinyi asitake kuzikwa Zanzibar. Sababu mzizozitoa ni za uzushi pure ambao umekuwa based kwenye wosia wa Mwinyi, ambao ni wa hadithi za uzushi tu.

Yani sababu zako ni sawa na mimi niseme denoo JG anashikia bango hiki suala Mwinyi azikwe Mkuranga kwa sababu yeye ni mla nyama za watu anayeishi Mkuranga, anataka Mwinyi azikwe Mkuranga iki apate urahisi wa kufujua kaburi amle nyama Mwinyi wa watu.

Si unataka tuendekeze uzushi?

Bisha sasa.
Maswali nimekuuliza pale juu naona umeshindwa kujibu ili tujue mvivu kati yetu ni nani, naamini umepata jibu ukaamua kupotezea usijali kiutu uzima nimekuelewa, naona umerukia sehemu nyingine kama kawaida yako....

Unaposema: " hakuna sababu yoyote ya kumfanya Mwinyi asitake kuzikwa Zanzibar" kwani ulikuwa unaingia ndani ya kichwa chake kuona nini alichokuwa akifikiria wakati akiwa hai? huoni kama huu nao ni "uzushi" wako!, ajabu one minute unajidai hupendi uzushi, next unaleta uzushi wako!.

Unadai tena: "hakuna logical consistency yoyote.." unaweza vipi kuipata consistency kwa jambo lililoanza kuzungumzwa juzi baada ya kifo chake? Hujioni ulivyo mweupe hata usiyejua maana ya consistency!.

- Usilazimishe kuufunga mjadala because of your lazy mind - kusubiri ushahidi, wacha tunaofikirisha bongo zetu tuendelee kutafakari mbele tutaipata hiyo logical consistency yako.

Unaita tena sababu nazotoa ni "uzushi pure" sijui unatumia kipimo gani kudhani hivyo, narudia tena kama ni fikra zako, basi uko wrong, kwasababu wewe sio kipimo cha usahihi hapa duniani, kujua uzushi upi ni pure, na upi sio pure, hata kama unatumia "logic" yako, kwangu huo ni ujuaji wako tu.

Lastly, huo mfano uliotoa wa .... mimi kuwa sawa na kula nyama za watu, hapo ndio naona kabisa umechoka akili ndugu, pumzika, maana hata mambo unayozungumzia hayaendani tena na mada iliyoko mezani, umegeuka ndege anayerukia kila tawi la mti, bahati mbaya kwake miti yote huteleza!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Watanzania tupeane pole kwa msiba huu mzito katika taifa letu.

Kuna watu wanashangazwa na hili swala la kuamua kuhamisishia msiba wa mzee Mwinyi Zanzibar, wakidai kuwa mzee huyo alikuwa asha usia kuwa akifariki akazikiwe kwao Mkuranga walipozikiwa na kulazwa wazazi wake na babu zake.

Wengi wanalaumu bila kujua ni nini kilichojadiliwa kati ya mzee Mwinyi na familia yake kabla ya umauti kumkuta. Je, kama walijadiliana nae na mzee kuridhia kuzikiwa Zanzibar alipokulia, kuoa, na kuzaa watoto wake huko?

Ni kweli mzee Mwinyi ana asili ya kwetu bara, lakini ukiangalia muda alioondoka bara kwenda Zanzibar mpaka sasa ni almost miaka 90 ambayo ni sawa na karne nzima. Sasa mtu ambae aliondoka bara miaka 90 iliyopita inamaana kwa sasa wale watu waliokuwa wanamfahamu na kumjua kupitia wazazi wake kama vile mashangazi, wajomba, baba wadogo, mama wadogo nk wameshafariki muda mrefu sana. Hakuna anaemfahamu kiundani zaidi ya wale walioko Zanzibar.

Ni kweli wakati alipokuwa raisi na hata baada ya uraisi huenda alikuwa anakwenda kwao mara moja moja, lakini sasa wale watu wake wa muhimu ambao wangemfanya kuvutiwa na kwao wameshafariki hivyo alikuwa ni kama vile mtu mpya au muhamiaji asiefahamika kijijini kwao. Familia nzima mke na watoto ni wenyeji wa Zanzibar, sasa kuna ubaya gani watoto kuongea na mzee wao ili kumsihi azikiwe kule alipoanzia kujenga familia yake ambapo ana watu wengi wanaomfahamu zaidi ya huku alipotokea.

Binafsi nafikiri hili swala la kuzikiwa Zanzibar lina baraka zake baada ya watoto na mke / wake zake kukaa na kumuelewesha hadi mzee kubadili gia angani na kuridhia kuzikwa Zanzibar ila imekuwa siri tu ya kifamilia. Wao sio wajinga wa kukurupuka kupishana na usia wa baba yao, na wakati ni watu wazima wenye elimu zao lakini pia wanafahamu vizuri madhara ya kupishana na usia wa marehemu, hivyo naona wanabaraka zake wala hawakukurupuka yaje yawakute yaliowakuta wengine waliopishana na usia wa ndugu zao.
Nikajua unajua kumbe unahisi. Hao unaowasema watoto wake ikiwa ni pamoja na Rais wa Zanzibar Dr. Mwinyi, aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga mbona hakutengwa kwa vile ni Mzanzibar? Mkuranga ndo kwao hayo mengine ya Mzee Ruksa kuzikwa Zanzibar ni ya kutafuta uhalali wa kisiasa wa Dr. Mwinyi.
 
Back
Top Bottom