6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 1,826
- 4,074
Watanzania tupeane pole kwa msiba huu mzito katika taifa letu.
Kuna watu wanashangazwa na hili swala la kuamua kuhamisishia msiba wa mzee Mwinyi Zanzibar, wakidai kuwa mzee huyo alikuwa asha usia kuwa akifariki akazikiwe kwao Mkuranga walipozikiwa na kulazwa wazazi wake na babu zake.
Wengi wanalaumu bila kujua ni nini kilichojadiliwa kati ya mzee Mwinyi na familia yake kabla ya umauti kumkuta. Je, kama walijadiliana nae na mzee kuridhia kuzikiwa Zanzibar alipokulia, kuoa, na kuzaa watoto wake huko?
Ni kweli mzee Mwinyi ana asili ya kwetu bara, lakini ukiangalia muda alioondoka bara kwenda Zanzibar mpaka sasa ni almost miaka 90 ambayo ni sawa na karne nzima. Sasa mtu ambae aliondoka bara miaka 90 iliyopita inamaana kwa sasa wale watu waliokuwa wanamfahamu na kumjua kupitia wazazi wake kama vile mashangazi, wajomba, baba wadogo, mama wadogo nk wameshafariki muda mrefu sana. Hakuna anaemfahamu kiundani zaidi ya wale walioko Zanzibar.
Ni kweli wakati alipokuwa raisi na hata baada ya uraisi huenda alikuwa anakwenda kwao mara moja moja, lakini sasa wale watu wake wa muhimu ambao wangemfanya kuvutiwa na kwao wameshafariki hivyo alikuwa ni kama vile mtu mpya au muhamiaji asiefahamika kijijini kwao. Familia nzima mke na watoto ni wenyeji wa Zanzibar, sasa kuna ubaya gani watoto kuongea na mzee wao ili kumsihi azikiwe kule alipoanzia kujenga familia yake ambapo ana watu wengi wanaomfahamu zaidi ya huku alipotokea.
Binafsi nafikiri hili swala la kuzikiwa Zanzibar lina baraka zake baada ya watoto na mke / wake zake kukaa na kumuelewesha hadi mzee kubadili gia angani na kuridhia kuzikwa Zanzibar ila imekuwa siri tu ya kifamilia. Wao sio wajinga wa kukurupuka kupishana na usia wa baba yao, na wakati ni watu wazima wenye elimu zao lakini pia wanafahamu vizuri madhara ya kupishana na usia wa marehemu, hivyo naona wanabaraka zake wala hawakukurupuka yaje yawakute yaliowakuta wengine waliopishana na usia wa ndugu zao.