Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,329
- 24,211
Kati ya tabia ambazo nitamkumbuka sana mzee Ally Hassan Mwinyi, ni humility, yaani uvumilivu.
Moyo wa uvumilivu umembeba sana na kumvusha katika mazingira ya utatanishi.
-humility ilimfanya ajiuuzuly uwazi wa mambo ya ndani kulipotokea mtafaruku wa watendaji kuua watu waliotuhumiwa ushirikina humko mikoa ya kanda ya ziwa.
-humility, wakati alipojiuzulu uwaziri, katika nyumba aliyokaa , waziri mwingine mzanzibari hamkumruhusu kuchukua mali zake zote ikiwemo mabati yake. Mwinyi hakubisha wala kukasirika. Baadaye waziri huyo mzanzibari akaona soni sana Mwinyi alipoteuliwa kuwa rais wa Zanzibar.
-humility,tumesikia akisema rais Kikwete, kuwa wakati wa kumpendekeza ris ajaye wa Zanzibar, kuna waziri alimbania chumba chake ple Dodoma naye bila hiana akaenda kukaa bwenini CBE.
-humility, alipokuwa rais, kuna wakati Mwalimu Nyerere alimpinga wazi wazi hadharani. Mapashkuna waandishi wa habari, kwa kutaka kuwachonganisha walimuuliza mzee Mwinyi, mbona Nyerere amakupinga rais hadharani ilhali wewe ndiye mwenye madaraka makubwa nchini? Mzee Mwinyi akawajibu, "mimi ni kichuguu, wakati mwalimu Nyerere ni mlima Kilimanjaro". Jamaa wakapigwa butwaa lakini lilikuwa jibu tosha la kuondoa ukakasi wowote.
Humility, RIP mzee Mwinyi, umeondoka nayo.
-