Mageuzi ya kiuchumi ya Zanzibar yalisaidia sana Watanzania kutamania Alhaj Ali Hassan Mwinyi aongoze Tanzania

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,461
1,445
kiukweli Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliongoza vizuri sana Zanzibar na baadaye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kilichochangia Watanzania wawe na imani naye sana ni mageuzi ya kiuchumi na kijamii aliyoyafanya Zanzibar kwa kipindi kifupi wakati wa awamu yake na hivyo wananchi wengi hususani kutoka Tanzania Bara kutamania huyu mzee aongoze Jamhuri yote kutokana na alivyoifungua zanzibar kwa wakati huo.Hili halisemwi sana na wanasiasa.

Hili lilimpandisha chati sana na kupendwa na watu wote mimi nikiwa mmoja wapo, bidhaa km sabuni za lifeboy,sunlight, Rexona,Lux, colgate zilizokuwa zimepotea awamu ya kwanza nk.

Zilianzia kuonekana huko Zanzibar kipindi chake. Na hapo ndipo walipo mpa credit Rais Mwinyi na kumhusudu kwa kusimamia sera za liberari za uchumi huria
 
kiukweli Mzee Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliongoza vizuri sana Zanzibar na baadaye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,lakini kilichochangia watanzania wawe...
Ni sawa na makubwa anayoyafanya mwanae kule Zanzibar, tunamuhitaji kuwa Raisi wa Muungano.Hawa kina February wanaoutaka huu uraisi wakae pembeni kwanza na genge lao.
 
Back
Top Bottom