Suala la mzee Mwinyi kuzikiwa Zanzibar wala lisifanywe la kisiasa, pitieni hapa msome muelewe sababu

...Ila umewahi kuipangia familia ya viongozi wa kitaifa na serikali kujua wapi walipolazwa viongozi wa nchi.

Huu ndio msimamo wako naufahamu, nina kumbukumbu nao, sio mjinga kuandika nisichokijua kukuhusu, kazi ya kutafuta thread huku ifanye mwenyewe majibu yako utayapata.

Kuujua msimamo wa mtu kwenye jambo fulani sio ajabu, usitake kuletewa ushahidi hapa ili kupotezeana muda, prove me wrong if you can.

Tena uje na ushahidi wako toka kwenye ule uzi wa ugonjwa wa Makamu wa Rais alipoenda kutibiwa hivi karibuni, nimeshakupa na point of reference kazi kwako.

Unasumbuliwa na egoism, matokeo yake umegeuka kama popo, jambo moja unataka upewe ushahidi wa kifamilia ili kulijadili, jambo lingine unakimbilia kutaka kujua kulikoni bila ushahidi wa ugonjwa!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Nimekutaka uweke maneno yangu mwenyewe kwenye hiyo thread tuyachambue, umeshindwa.

Inawezekana nimeandika A, ila kichwa chako kidogo hakielewi A, kimeelewa B.

Wewe acha uvivu, point unaitoa wewe halafu ushahidi unataka nitoe mimi?

Siwezi kushangaa unavyopenda uzushi, hiyo ni tabia ya watu wavivu kama wewe wasiopenda kufanya kazi ya kuthibitisha mambo kwa ushahidi.
 
Watanzania tupeane pole kwa msiba huu mzito katika taifa letu.

Kuna watu wanashangazwa na hili swala la kuamua kuhamisishia msiba wa mzee Mwinyi Zanzibar, wakidai kuwa mzee huyo alikuwa asha usia kuwa akifariki akazikiwe kwao Mkuranga walipozikiwa na kulazwa wazazi wake na babu zake.

Wengi wanalaumu bila kujua ni nini kilichojadiliwa kati ya mzee Mwinyi na familia yake kabla ya umauti kumkuta. Je, kama walijadiliana nae na mzee kuridhia kuzikiwa Zanzibar alipokulia, kuoa, na kuzaa watoto wake huko?

Ni kweli mzee Mwinyi ana asili ya kwetu bara, lakini ukiangalia muda alioondoka bara kwenda Zanzibar mpaka sasa ni almost miaka 90 ambayo ni sawa na karne nzima. Sasa mtu ambae aliondoka bara miaka 90 iliyopita inamaana kwa sasa wale watu waliokuwa wanamfahamu na kumjua kupitia wazazi wake kama vile mashangazi, wajomba, baba wadogo, mama wadogo nk wameshafariki muda mrefu sana. Hakuna anaemfahamu kiundani zaidi ya wale walioko Zanzibar.

Ni kweli wakati alipokuwa raisi na hata baada ya uraisi huenda alikuwa anakwenda kwao mara moja moja, lakini sasa wale watu wake wa muhimu ambao wangemfanya kuvutiwa na kwao wameshafariki hivyo alikuwa ni kama vile mtu mpya au muhamiaji asiefahamika kijijini kwao. Familia nzima mke na watoto ni wenyeji wa Zanzibar, sasa kuna ubaya gani watoto kuongea na mzee wao ili kumsihi azikiwe kule alipoanzia kujenga familia yake ambapo ana watu wengi wanaomfahamu zaidi ya huku alipotokea.

Binafsi nafikiri hili swala la kuzikiwa Zanzibar lina baraka zake baada ya watoto na mke / wake zake kukaa na kumuelewesha hadi mzee kubadili gia angani na kuridhia kuzikwa Zanzibar ila imekuwa siri tu ya kifamilia. Wao sio wajinga wa kukurupuka kupishana na usia wa baba yao, na wakati ni watu wazima wenye elimu zao lakini pia wanafahamu vizuri madhara ya kupishana na usia wa marehemu, hivyo naona wanabaraka zake wala hawakukurupuka yaje yawakute yaliowakuta wengine waliopishana na usia wa ndugu zao.
wewe kwenu ni bara?
 
Nimeshakuonesha umuhimu wa unachoita uzushi, ajabu unajidai kichwa ngumu usiyetaka kuelewa, badala yake unakuja na majibu kuonesha kichwa chako ndio "computer" inayojua kila kitu, ujuaji tu, ukiulizwa umepima kwa uthibitisho wa kifaa kipi huna jibu.

Niambie; hivi mvivu ni nani kati yetu kama kweli una akili unazoamini unazo..

Yule anayekaa kusubiri ushahidi wa jambo ili aanze kulizungumzia? au huyu anayechukua tetesi/uzushi kisha anaanza connect dots ili apate majibu sahihi?

- Ukiulizwa kwanini majibu yasiwe sahihi, umetumia kipimo gani kuthibitisha hilo, huna jibu, ukiulizwa kwani fikra zako ziko sahihi kila wakati, kimya tena, unabaki kuzunguka tu na logical fallacy kama vile wewe pekee ndie mwalimu wa logic hapa duniani.

Huo ushahidi unaousubiri utaletewa na nani? Umekaa tu hapo umelaza kitumbo na uzungu wako wa uswahilin, huu ndio uvivu, nakwambia tena tafuta glass ya maji unywe utulize hicho kichwa.

Hata kwenye uzushi, kuna uzushi ubaoweza kutetewa kwa logical consistency. Ukiendekeza uzushi huo, nawwza kusema labda hapa kuna ukweli haujajulikana, unaanza kwa kuonekana kama uzushi.

Lakini, uzushi wako hauendani na logical consistency yoyote, hakuna sababu yoyote ya kumfanya Mwinyi asitake kuzikwa Zanzibar. Sababu mzizozitoa ni za uzushi pure ambao umekuwa based kwenye wosia wa Mwinyi, ambao ni wa hadithi za uzushi tu.

Yani sababu zako ni sawa na mimi niseme denoo JG anashikia bango hiki suala Mwinyi azikwe Mkuranga kwa sababu yeye ni mla nyama za watu anayeishi Mkuranga, anataka Mwinyi azikwe Mkuranga iki apate urahisi wa kufujua kaburi amle nyama Mwinyi wa watu.

Si unataka tuendekeze uzushi?

Bisha sasa.
 
Mwinyi ameishi maisha yake zaidi Bara kuliko huko visiwani. Ndiyo maana hata baada ya kufa ameendelea kuishi bara na si visiwani.

Na nyumba yake ya kustaafu akajengewa na Magufuli Dar kwa nini hawakumjengea kwao Zanzibar.

Hata Mwanaye pia maisha yake ameishi zaidi bara, wanamzika kule kimkakati!!
Angezikwa Mkuranga, Dr. Mwinyi urais wake Zenji ungekoma 2025.

Mkakati ni mkakati....
 
Unarudi kulekule kwenye maneno ya kuungaunga nilikokukataa mimi.

Unasema desturi zetu hivi na vile, desturi za nani? Unajua unapotulundika wote katika "zetu" unakosea? Hapo kuna makabila tofauti, dini tofauti, misimamo ya kifalsafa tofauti, unaelewa neno "zetu" linaweza kukosa maana?

Mlikubaliana wapi hizo desturi? This is a logical fallacy, argument from tradition, problem of induction.

Ali Hassan Mwinyi ndiye mtu wa kwanza kuzaliwa bara, kwenda kuwa rais wa Zanzibar, na kuwa rais wa Tanzania. Hakuna precedent ya mtu mwingine yeyote mwenye historia hiyo, sasa utatumia vipi desturi kumzika mtu ambaye maisha yake hayako defined na desturi, mpaka leo watu wanabishana kama Mwinyi ni Mzanzibari au mtu wa bara?

Unatumia vipi desturi kumzika mtu ambaye maisha yake hayako easily defined ki desturi?

Habari yoyote ya "ingekuwa mtoto wake si rais wa Zanzibar asingezikwa huko" ndiyo hizo ninazosema habari za kuunga unga. Hujui Mwinyi alifikiri nini, aliienzi Zanzibar vipi, una speculate tu.

Mimi si rais wala nini, nimeishi tu Marekani, nimepapenda, nimesema nikifa nisirudishwe Tanzania. Mazishi yangu yafanyike Marekani. Sasa ikiwa mtu kama mimi nimeamua hivyo, kwa nini iwe ajabu Mwinyi kuzikwa Zanzibar sehemu ambayo bado ni ndani ya Tanzania na huhitaji hata passport kwenda?

Huna ushahidi kwamba politics ndiyo imeamua wapi Mwinyi azikwe, hizo ni simple stories za kijiweni tu.

Manapenda sana conspiracy theories.
🤝🆒
 
Usihofu, mtoto wa mzee MWINYI akiitwa HASSAN nae amezikwa Zanzibar, kwa hiyo hatakua mpweke.
Na kama kuna ulazima wa kupeleka udongo Mkuranga utapelekwa.
Kijana unatuchekesha wafiwa 😂😂😂😂
 
Watanzania tupeane pole kwa msiba huu mzito katika taifa letu.

Kuna watu wanashangazwa na hili swala la kuamua kuhamisishia msiba wa mzee Mwinyi Zanzibar, wakidai kuwa mzee huyo alikuwa asha usia kuwa akifariki akazikiwe kwao Mkuranga walipozikiwa na kulazwa wazazi wake na babu zake.

Wengi wanalaumu bila kujua ni nini kilichojadiliwa kati ya mzee Mwinyi na familia yake kabla ya umauti kumkuta. Je, kama walijadiliana nae na mzee kuridhia kuzikiwa Zanzibar alipokulia, kuoa, na kuzaa watoto wake huko?

Ni kweli mzee Mwinyi ana asili ya kwetu bara, lakini ukiangalia muda alioondoka bara kwenda Zanzibar mpaka sasa ni almost miaka 90 ambayo ni sawa na karne nzima. Sasa mtu ambae aliondoka bara miaka 90 iliyopita inamaana kwa sasa wale watu waliokuwa wanamfahamu na kumjua kupitia wazazi wake kama vile mashangazi, wajomba, baba wadogo, mama wadogo nk wameshafariki muda mrefu sana. Hakuna anaemfahamu kiundani zaidi ya wale walioko Zanzibar.

Ni kweli wakati alipokuwa raisi na hata baada ya uraisi huenda alikuwa anakwenda kwao mara moja moja, lakini sasa wale watu wake wa muhimu ambao wangemfanya kuvutiwa na kwao wameshafariki hivyo alikuwa ni kama vile mtu mpya au muhamiaji asiefahamika kijijini kwao. Familia nzima mke na watoto ni wenyeji wa Zanzibar, sasa kuna ubaya gani watoto kuongea na mzee wao ili kumsihi azikiwe kule alipoanzia kujenga familia yake ambapo ana watu wengi wanaomfahamu zaidi ya huku alipotokea.

Binafsi nafikiri hili swala la kuzikiwa Zanzibar lina baraka zake baada ya watoto na mke / wake zake kukaa na kumuelewesha hadi mzee kubadili gia angani na kuridhia kuzikwa Zanzibar ila imekuwa siri tu ya kifamilia. Wao sio wajinga wa kukurupuka kupishana na usia wa baba yao, na wakati ni watu wazima wenye elimu zao lakini pia wanafahamu vizuri madhara ya kupishana na usia wa marehemu, hivyo naona wanabaraka zake wala hawakukurupuka yaje yawakute yaliowakuta wengine waliopishana na usia wa ndugu zao.
Azikwe Zanzibar au Bara, udongo ndo huu huu Tu.
 
Hivi aliyekuwa mbunge wa Mkuranga ni Mwinyi baba au mtoto?
Mimi nafahamu Mwinyi mtoto alikuwa mbunge wa mkuranga kwa takriban miaka 20, lakini waliokuwepo enzi za ubunge na uwaziri wa mzee Mwinyi wanasema na baba alianza kwanza kuwa mbunge wa mkuranga na kushika nyadhifa mbali mbali za uwaziri, kisha baadae akaenda kuwa raisi wa Zanzibar na wa Jamhuri ya Muungano.
 
Naona hautaki kulundikwa kwenye desturi zetu, mindset ya kimarekani imekuingia unaanza kuzikataa mila na desturi zako, hata kama huzitaki, wazazi wako na ndugu zako wengine wanazifuata, hiyo ndio sababu iliyonifanya nikachagua kutumia neno "zetu" nikimaanisha waswahili, sio wakina wewe "swahili-zungu".

Hapa pia kuna angle ya pili niiite social status.

Mzee Mwinyi alikuwa mtu mzito hapa Tanzania -Rais Mstaafu, hivyo kwangu sioni ubaya yeye kujadiliwa, hata nawe huwa unakuwa kwenye upande wa kuunga mkono mtu mwenye nafasi kwenye jamii kuzungumziwa, nikikumbuka umekuwa ukilaumu taarifa za viongozi wagonjwa kwenda nje kutibiwa kufanywa siri na serikali.

Sasa sijui kwanini hapa kwa marehemu Mzee Mwinyi umeamua kugeuka kuwa mtu wa kutaka "ushahidi wa vikao vya kifamilia", kwanini wakati ule wa ugonjwa wa viongozi huwa huulizii ushahidi wa ugonjwa wa kiongozi toka kwa familia yake kwanza, badala yake huishia tu kuitaka serikali isitufiche habari zao kwenda kutibiwa nje?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
🙄
 
Kuhusudu mila na desturi sio ujinga, na wala sio kweli wanaofuata mila na desturi huishia kufulia, naona wewe ndie unaishi kwa kukariri.

Kuhusu Mzee Mwinyi kujadliwa ni kujadiliwa tu, iwe kwa story zenye ushahidi au zisizo na ushahidi, hiyo yote ndio mijadala yenyewe, usitufunge midomo.

Kama hupendi story za uzushi kwanini wewe huitaka serikali ikwambie wapi walipolazwa viongozi wetu, ikiwa wewe hujui lini waliondoka nchini na ugonjwa upi unaowasumbua?

Kwanini usiitake serikali kwanza ikupe ushahidi wa ugonjwa wao, ili uanze kutaka kujua wapi walipoenda kulazwa viongozi wetu?

Hujioni nawe kutaka kujua wapi walipolazwa viongozi wetu, bila kujua kwanza ugonjwa wao nawe ni miongoni mwetu wanaopenda uzushi wa vijiweni?

Kaa chini tafakari.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Mkuu usihamishe magoli! Tetea hoja yako kama Kiranga!
 
Hivi aliyekuwa mbunge wa Mkuranga ni Mwinyi baba au mtoto?
Mwinyi baba hajawahi kuwa Mbunge wa Mkuranga.

Wakati Mwinyi baba waziri miaka ya sabini alitokea Zanzibar, na Mkuranga hata halikuwa jimbo la ubunge.

Hapa hadithi za kuungaunga ni nyingi sana.

Mara nyingine mtu unashindwa hata uanzie kusahihisha wapi.
 
Mkuu usihamishe magoli! Tetea hoja yako kama Kiranga!
Kutetea hoja inabidi uwe na fact, uwe na logic.

Huyu anatetea uzushi, anatetea habari zisizo na ushahidi, anatetea hisia zake, anatetea hadithi anazozitaka yeye.

Hawezi kutetea hoja.

Katoa habari ya wosia wa Mwinyi, wosia wenyewe uzushi mtupu.

Kanibandika maneno anasema nimeandika hapa, nimemuuliza anipe thread na bandiko twende kwa ushahidi na muktadha vizuri, kashindwa.

Ni mtu wa vimaneno vya kuungaunga kimbeambea kizushizushi tu.
 
Watanzania tupeane pole kwa msiba huu mzito katika taifa letu.

Kuna watu wanashangazwa na hili swala la kuamua kuhamisishia msiba wa mzee Mwinyi Zanzibar, wakidai kuwa mzee huyo alikuwa asha usia kuwa akifariki akazikiwe kwao Mkuranga walipozikiwa na kulazwa wazazi wake na babu zake.

Wengi wanalaumu bila kujua ni nini kilichojadiliwa kati ya mzee Mwinyi na familia yake kabla ya umauti kumkuta. Je, kama walijadiliana nae na mzee kuridhia kuzikiwa Zanzibar alipokulia, kuoa, na kuzaa watoto wake huko?

Ni kweli mzee Mwinyi ana asili ya kwetu bara, lakini ukiangalia muda alioondoka bara kwenda Zanzibar mpaka sasa ni almost miaka 90 ambayo ni sawa na karne nzima. Sasa mtu ambae aliondoka bara miaka 90 iliyopita inamaana kwa sasa wale watu waliokuwa wanamfahamu na kumjua kupitia wazazi wake kama vile mashangazi, wajomba, baba wadogo, mama wadogo nk wameshafariki muda mrefu sana. Hakuna anaemfahamu kiundani zaidi ya wale walioko Zanzibar.

Ni kweli wakati alipokuwa raisi na hata baada ya uraisi huenda alikuwa anakwenda kwao mara moja moja, lakini sasa wale watu wake wa muhimu ambao wangemfanya kuvutiwa na kwao wameshafariki hivyo alikuwa ni kama vile mtu mpya au muhamiaji asiefahamika kijijini kwao. Familia nzima mke na watoto ni wenyeji wa Zanzibar, sasa kuna ubaya gani watoto kuongea na mzee wao ili kumsihi azikiwe kule alipoanzia kujenga familia yake ambapo ana watu wengi wanaomfahamu zaidi ya huku alipotokea.

Binafsi nafikiri hili swala la kuzikiwa Zanzibar lina baraka zake baada ya watoto na mke / wake zake kukaa na kumuelewesha hadi mzee kubadili gia angani na kuridhia kuzikwa Zanzibar ila imekuwa siri tu ya kifamilia. Wao sio wajinga wa kukurupuka kupishana na usia wa baba yao, na wakati ni watu wazima wenye elimu zao lakini pia wanafahamu vizuri madhara ya kupishana na usia wa marehemu, hivyo naona wanabaraka zake wala hawakukurupuka yaje yawakute yaliowakuta wengine waliopishana na usia wa ndugu zao.
Ukichota mchanga bara ukaenda kuumwaga zanzibar kuna shida gani.
A dead body is nothing, ukifa we sii kitu, unaliwa na wadudu iwe bara iwe znz
 
Back
Top Bottom