Suala la ardhi halimo kwenye Muungano, Zanzibar wapo makini kulinda ardhi yao lakini wametuzidi akili kuimiliki ardhi ya bara

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
3,222
2,000
Kwenye katiba ya Tanzania hakuna sehemu iliyohusisha ardhi kwenye muungano, Ardhi ya Tanzania bara ni kwajili ya raia wake na ardhi ya Zanzibar ni ya raia wake.

Hatuna budi kuwapongeza wazanzibari maana hawana mchezo kwenye kulitekeleza hili kwa kulinda ardhi yao iwe kwajili yao, Lakini sasa huku bara ni kama vile tuna upofu katika kusimamia haki yetu kwasababu katiba imeshaweka wazi hii ardhi ni ya raia wa bara pekee lakini cha ajabu wazanzibari wanapewa umiliki wa ardhi, ndugu zangu hivi hatuna uchungu na ardhi yetu kama ilivyo kwa wazanzibari wenye uchungu na ardhi yao ?

Mtu wa bara ukienda huko Zanzibar hata uwe na pesa vipi utapigwa stop, ukiona unamilikishwa kirahisbi rahisi jua ya kwamba umekutana na wajanja wa kipemba, watakufojia hadi hati za ardhi feki ilimradi uingie kingi, utatapeliwa pesa zako mchana kweupe, siku unaanza shughuli zako ndipo unakuja kugundua umetapeliwa.

Ajabu ni kwamba Kigamboni karibu yote, Temeke, Buguruni, Wazanzibar wanamiliki ardhi bila bugudha. Msingi wa hoja yangu ni kwanini Wazanzibari wanamiliki ardhi Bara licha ya kwamba katiba hata ya sasa ipo wazi haiwaruhusu ?

Kimsingi Tanganyika imekuwa kama shamba la bibi au yatima, haina mwenyewe wala mtetezi.

Kuna kila sababu ya kuona kwamba Zanzibar "wametuzidi akili", Sizungumzii akili za kukariri darasani what is physics, ni akili ya kawaida kabisa ambayo mtu inabidi awe nayo, kwa kiingereza huitwa "common sense"

1639340797167.png
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
3,222
2,000
Ardhi ya huku (bara) ni kubwa mno, acha tu tutumie sote. Watu wenyewe wako milioni moja na nusu, hawawezi kutumalizia "hiyo ardhi yetu".

Khaa, nchi hii...
Wapo wanaotumia kisingizio kwamba Zanizbar ina eneo dogo kwahiyo wabara wasipewe umiliki wa ardhi ila huku bara wazanzibar wapewe umiliki wa maeneo kwasababu bara ni eneo kubwa.

Sioni mantiki ya hizi sababu, sisi tunachokitaka kama wao wanaweza kumiliki popote basi na mtu wa bara aweze kuwe na Uhuru wa kumliki ardhi sehemu yoyote either Tanganyika or Zanzibar, bila kuuangalia idadi ya watu na eneo la sehemu, ndio matunda ya Muungano au wewe unataka Muungano iwe faida kwao lakini kwa Mtanganyika ni hasara.

Sifa ya kumliki ardhi iwe tu wewe ni Mtanzania na unaruhusiwa kumliki sehemu yoyote ndani ya Tanzania bila kikwazo. kuhusu bei ni swala la eneo husika mfano Masaki /Osterbay kiwanja ni Bei kubwa kuliko kigamboni lakini mfuko ikiwa inasoma unanunua. Tofauti na Zanzibar ambako hairusiwi Mtanganyika kisheria kumliki ardhi.
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
3,222
2,000
Zanzibar kisiwa
Ardhi yao ndogo
Wangeruhusu wabara wamiliki ardhi
Mpaka sasa kungekwisha

Ova
Sheria huwa ni msumeno, hukata kuwili. Iweje hiyo marufuku iwe kwa Zanzibar pekee na isiwe kwa bara kupiga marufuku waZanzibari kumiliki aridhi?

Kisingizio cha ...'wataimaliza ardhi yote'..! ni Tafakuri za kijinga sana hizi.

Maana ya uhuru ni nini na lini ulisikia kila mTanganyika ana nia ya kwenda kununua aridhi na kuishi Zanzibar?

Huu ni ubaguzi, haya mambo yanazostahili kuangaliwa upya na kufumuliwa.
 

mkokoriko

Member
Oct 8, 2020
42
125
Hao Wazanzibari wenyewe hawamiliki ardhi wanapewa hati ya matumizi ya ardhi tu. Serikali ikiitaka hiyo ardhi inaichukuwa tu bali unalipwa fidia ya mazao na majengo ikiwa hujaiendeleza inachukuliwa bila yakulipwa hata senti.
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
8,151
2,000
Bila kuwepo Katiba mpya, kuwepo serikali ya Tanganyika na kuitoa CCM madarakani, hizi mambo hazitaisha milele.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
18,329
2,000
Mkuu hilo mama kesha litolea ufafanuzi:Nguvu yako tu kote kwenu kama Chatto tu.
 

mkokoriko

Member
Oct 8, 2020
42
125
Kuna nini kwani naona suala la ardhi ya Zanzibar imekuwa issue. Kimsingi Zanzibar hakuna mtu anaemiliki ardhi, ardhi yote ni mali ya Serikali raia wanapewa hati za matumizi, wageni wanaotaka kuwekeza au raia wanakodishwa ardhi kwa muda maalum na wanatakiwa kulipa kila mwaka.
 

Akhi

JF-Expert Member
Jul 12, 2021
1,099
2,000
Hii n katiba yetu, na hakuna sehemu iliyohusisha ardhi kwenye muungano,

View attachment 2041944

Mtu wa bara ukienda huko Zanzibar hata uwe na pesa vipi utapigwa stop, ukilazimisha kuimiliki kijanja janja basi utakuwa umevunja Sheria kwa kujua au kutojua , wakienda mahakamani huna haki ya kumiliki hio ardhi na hutolipwa fidia yoyote

Ajabu ni kwamba Kigamboni karibu yote, Temeke, buguruni, wazanzibar wanamiliki ardhi bila bugudha.

Kimsingi Tanganyika imekuwa kama shamba la bibi au yatima, haina mwenyewe wala mtetezi..

Kwa katiba ya jamhuri mzanzibar akiwa bara anahaki sawa na mtanganyika. Ila Kwa katiba ya Zanzibar mtanganyika akiwa Zanzibar hana haki sawa na Mzanzibar.

kuna kila sababu ya kuona kwamba Zanzibar "wametuzidi akili", Sizungumzii akili za kukariri darasani what is physics, ni akili ya kawaida kabisa ambayo mtu inabidi awe nayo, kwa kiingereza huitwa "common sense"
Naona wiki hii watu wengi wamekua wakipiga kelele kuhusu Ardhi ya Zanzibar

Mimi najua fika na hili jambo lipo kwenye katiba ya Zanzibar kuhusu umiliki Ardhi

Hata ukiuziwa Ardhi ww ambae si mzanzibari ukienda kuihaulisha ardhi yko utapewa kibali cha kukodi Ardhi na sio kununua Ardhi na hili jambo linasimamiwa na sheria na litasimamiwa na sheria za Zanzibar mpk mwisho.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
18,329
2,000
Kuna nini kwani naona suala la ardhi ya Zanzibar imekuwa issue. Kimsingi Zanzibar hakuna mtu anaemiliki ardhi, ardhi yote ni mali ya Serikali raia wanapewa hati za matumizi, wageni wanaotaka kuwekeza au raia wanakodishwa ardhi kwa muda maalum na wanatakiwa kulipa kila mwaka.

Yaonesha pamoja na maneno matamu ya mama:Kungali kuna tashwishi ya kuchezana shere kiaina. Kumbuka kuna wahuni na viroboto wanaorushiana makombora pia.

Usisahau mama amesisitiza zaidi maridhiano kwao si bara:

IMG_20211106_200104_587.jpg


Mtu wa kawaida anayaona haya:

IMG_20211211_115457_124.jpg


Mama angejikita zaidi kimaridhiano
 

Sirdirashy

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
2,874
2,000
Sheria huwa ni msumeno, hukata kuwili. Iweje hiyo marufuku iwe kwa Zanzibar pekee na isiwe kwa bara kupiga marufuku waZanzibari kumiliki aridhi?

kisingizio cha ...'wataimaliza ardhi yote'..! ni Tafakuri za kijinga sana hizi.

Maana ya uhuru ni nini na lini ulisikia kila mTanganyika ana nia ya kwenda kununua aridhi na kuishi Zanzibar?

huu ni ubaguzi, haya mambo yanazostahili kuangaliwa upya na kufumuliwa.

yasje yakaanza mambo ya xenophobia hii nchi
Mkuu Sheria hazifatwi na naamini hujataka Ardhi Zanzibar we Nunua Tu sifikiri kama kuna shida sio kila kilichopo kwenye Sheria kinafatwa.

Muungano huu unamatatizo mengi Ila tushazoea na inabidi uzoee Kumbuka Zanzibar ni kisiwa na nisehemu muhimu zaidi ya nyeti kuna mengi yenye upendeleo Kuhusu Zanzibar Ila watu wake wasihisi kubanwa ijapokuwa wanataka zaidi yahayo.
 

Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,463
2,000
Wapo wanaotumia kisingizio kwamba Zanizbar ina eneo dogo kwahiyo wabara wasipewe umiliki wa ardhi ila huku bara wazanzibar wapewe umiliki wa maeneo kwasababu bara ni eneo kubwa.

Sioni mantiki ya hizi sababu, sisi tunachokitaka kama wao wanaweza kumiliki popote basi na mtu wa bara aweze kuwe na Uhuru wa kumliki ardhi sehemu yoyote either Tanganyika or Zanzibar, bila kuuangalia idadi ya watu na eneo la sehemu, ndio matunda ya Muungano au wewe unataka Muungano iwe faida kwao lakini kwa Mtanganyika ni hasara, Sifa ya kumliki ardhi iwe tu wewe ni Mtanzania na unaruhusiwa kumliki sehemu yoyote ndani ya Tanzania bila kikwazo. kuhusu bei ni swala la eneo husika mfano Masaki /Osterbay kiwanja ni Bei kubwa kuliko kigamboni lakini mfuko ikiwa inasoma unanunua. Tofauti na Zanzibar ambako hairusiwi Mtanganyika kisheria kumliki ardhi.
Mkuu, basi Pemba yote ile ni ya kwako ichukue.

Au unataka upewe Unguja?

NB: Nimeongea hivyo baada ya wewe kusema kwamba kuwazuia watu milioni hamsini kukakalia kaeneo kadogo kama Zanzibar ni hoja isiyo na mashiko.
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
3,222
2,000
Ardhi ya huku (bara) ni kubwa mno, acha tu tutumie sote. Watu wenyewe wako milioni moja na nusu, hawawezi kutumalizia "hiyo ardhi yetu".

Khaa, nchi hii...
hakuna alierusiwa kumiliki ardhi kwa mwenzake kwenye muungano isipokua kwenye mambo ya uwekezaji tu.

Shida inapokuja ni wazanzibari kupewa umiliki wa ardhi nje ya matumizi ya uwekezaji.
 

Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,463
2,000
hakuna alierusiwa kumiliki ardhi kwa mwenzake kwenye muungano isipokua kwenye mambo ya uwekezaji tu.

Shida inapokuja ni wazanzibari kupewa umiliki wa ardhi nje ya matumizi ya uwekezaji.
Kwaiyo msingi wa hoja yako ni kwanini Wazanzibari wanamiliki ardhi Bara kwa sababu zisizokua ni uwekezaji, si ndio ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom