Suala la ardhi halimo kwenye Muungano, Zanzibar wapo makini kulinda ardhi yao lakini wametuzidi akili kuimiliki ardhi ya bara

Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
60,612
2,000
hakuna alierusiwa kumiliki ardhi kwa mwenzake kwenye muungano isipokua kwenye mambo ya uwekezaji tu.

Shida inapokuja ni wazanzibari kupewa umiliki wa ardhi nje ya matumizi ya uwekezaji.
Binafsi huu muungano huwa siutaki kabisa maana wazanzibar wana haki zote huku bara lakini sisi hatuna haki kwao ni kama watalii wengine
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
60,612
2,000

Bepari2020

JF-Expert Member
Nov 7, 2020
974
1,000
Mkivunja muungano mtaishi nchi gani? Tanzania ni hiyo mmeichoka na Tanganyika haipo tena. Sasa nyie machogo wenye chuki na Zanzibar mtakuwa raia wa nchi gani?
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,017
2,000
Kwenye katiba ya Tanzania hakuna sehemu iliyohusisha ardhi kwenye muungano, Ardhi ya Tanzania bara ni kwajili ya raia wake na ardhi ya Zanzibar ni ya raia wake, Pongezi nyingi ziende kwa wazanzibari maana hawana mchezo kwenye kulitekeleza hili kwa kulinda ardhi yao iwe kwajili yao, Lakini sasa huku bara hatupo siriazi (serious) kutekeleza hili jukumu maana wazanzibari wanapewa umiliki wa ardhi huku katiba imeweka wazi kabisa hairusiwi, kiuhalisia tukubali kwamba Wazanzibar wametuzidi akili.

Mtu wa bara ukienda huko Zanzibar hata uwe na pesa vipi utapigwa stop, ukilazimisha kuimiliki kijanja janja basi utakuwa umevunja Sheria kwa kujua au kutojua , wakienda mahakamani huna haki ya kumiliki hio ardhi na hutolipwa fidia yoyote

Ajabu ni kwamba Kigamboni karibu yote, Temeke, Buguruni, Wazanzibar wanamiliki ardhi bila bugudha. Msingi wa hoja yangu ni kwanini Wazanzibari wanamiliki ardhi Bara kwa sababu zisizokua ni uwekezaji?

Kimsingi Tanganyika imekuwa kama shamba la bibi au yatima, haina mwenyewe wala mtetezi.

kuna kila sababu ya kuona kwamba Zanzibar "wametuzidi akili", Sizungumzii akili za kukariri darasani what is physics, ni akili ya kawaida kabisa ambayo mtu inabidi awe nayo, kwa kiingereza huitwa "common sense"

View attachment 2041966
Siku ya muungano ulichanganywa udongo toka Zanziba na Tanganyika. Hii ina maana.
 
sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
3,222
2,000
Huu muungano fake uvunjwe haraka sn
Kuna vitu vingine tunalalamika sana wakati vipo wazi lakini sisi tunashindwa kufatilia,

Binafsi nawapongeza wazanzibar p kwa kuwa na uchungu na nchi yao wanafata makubaliano ya muungano hawampi mtu wa bara ardhi yao,

hata sisi huku hairusiwi kuwapa lakini tumekuwa wavivu sana kufata haya makubaliano, kiasi kwamba kuna fikra zimejengeka kuona kana kwamba wao wanarusiwa kumiliki huku ila sisi haturusiwi kumiliki kwao lakini kiukweli sheria ipo wazi hakuna muungano kwenye ardhi.

Huenda tymezidiwa akili tu, maana kila kitu kipo wazi sasa kwanini tushindwe utekelezaji??
 
Tressa

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
807
1,000
Yeah 😂😂😂,si wabara wako busy kutukanana na wanadhani sifa.wazenji kamateni fursa kabisa.
 
Thaconfession

JF-Expert Member
Jun 16, 2021
232
500
Ardhi ya huku (bara) ni kubwa mno, acha tu tutumie sote. Watu wenyewe wako milioni moja na nusu, hawawezi kutumalizia "hiyo ardhi yetu".

Khaa, nchi hii.
Mkitukanwa kwamba akili zenu zinawaza usawa wa pua zenu mnakasirika, ardhi haiongezeki, idadi ya watu inaongeseka, hivi unawaza miaka 100 ijayo uwiano wa ardhi na idadi ya watu itakuwaje?

Pili kinachosemwa hapa sio kingine ila matakwa ya kikatiba na kisheria, kwanini inaheshimiwa upande mmoja tu?
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
60,612
2,000
Kuna vitu vingine tunalalamika sana wakati vipo wazi lakini sisi tunashindwa kufatilia,

Binafsi nawapongeza wazanzibar p kwa kuwa na uchungu na nchi yao wanafata makubaliano ya muungano hawampi mtu wa bara ardhi yao,

hata sisi huku hairusiwi kuwapa lakini tumekuwa wavivu sana kufata haya makubaliano, kiasi kwamba kuna fikra zimejengeka kuona kana kwamba wao wanarusiwa kumiliki huku ila sisi haturusiwi kumiliki kwao lakini kiukweli sheria ipo wazi hakuna muungano kwenye ardhi.

Huenda tymezidiwa akili tu, maana kila kitu kipo wazi sasa kwanini tushindwe utekelezaji??
Hata ajira wamejazana kwenye sekta zote lakini hakuna mbara kule kwao kaajiriwa zaidi ya polisi wachache
 
nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
2,948
2,000
Kwenye katiba ya Tanzania hakuna sehemu iliyohusisha ardhi kwenye muungano, Ardhi ya Tanzania bara ni kwajili ya raia wake na ardhi ya Zanzibar ni ya raia wake.

Hatuna budi kuwapongeza wazanzibari maana hawana mchezo kwenye kulitekeleza hili kwa kulinda ardhi yao iwe kwajili yao, Lakini sasa huku bara ni kama vile tuna upofu katika kusimamia haki yetu kwasababu katiba imeshaweka wazi hii ardhi ni ya raia wa bara pekee lakini cha ajabu wazanzibari wanapewa umiliki wa ardhi, ndugu zangu hata nisiwafiche, hapa tukubali tu kwamba Wazanzibari wametuzidi akili.

Mtu wa bara ukienda huko Zanzibar hata uwe na pesa vipi utapigwa stop, ukilazimisha kuimiliki kijanja janja basi utakuwa umevunja Sheria kwa kujua au kutojua , wakienda mahakamani huna haki ya kumiliki hio ardhi na hutolipwa fidia yoyote

Ajabu ni kwamba Kigamboni karibu yote, Temeke, Buguruni, Wazanzibar wanamiliki ardhi bila bugudha. Msingi wa hoja yangu ni kwanini Wazanzibari wanamiliki ardhi Bara kwa sababu zisizokua ni uwekezaji?

Kimsingi Tanganyika imekuwa kama shamba la bibi au yatima, haina mwenyewe wala mtetezi.

kuna kila sababu ya kuona kwamba Zanzibar "wametuzidi akili", Sizungumzii akili za kukariri darasani what is physics, ni akili ya kawaida kabisa ambayo mtu inabidi awe nayo, kwa kiingereza huitwa "common sense"

View attachment 2041966
Ccm inailea kama yai Zanzibar

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Montserrat

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
7,293
2,000
Kwenye katiba ya Tanzania hakuna sehemu iliyohusisha ardhi kwenye muungano, Ardhi ya Tanzania bara ni kwajili ya raia wake na ardhi ya Zanzibar ni ya raia wake.

Hatuna budi kuwapongeza wazanzibari maana hawana mchezo kwenye kulitekeleza hili kwa kulinda ardhi yao iwe kwajili yao, Lakini sasa huku bara ni kama vile tuna upofu katika kusimamia haki yetu kwasababu katiba imeshaweka wazi hii ardhi ni ya raia wa bara pekee lakini cha ajabu wazanzibari wanapewa umiliki wa ardhi, ndugu zangu hata nisiwafiche, hapa tukubali tu kwamba Wazanzibari wametuzidi akili, Wenzetu hawatoi ardhi yao kirahisi rahisi aisee, hio sahau.

Mtu wa bara ukienda huko Zanzibar hata uwe na pesa vipi utapigwa stop, ukiona unamilikishwa kirahisbi rahisi jua ya kwamba umekutana na wajanja wa kipemba, watakufojia hadi hati za ardhi feki ilimradi uingie kingi, utatapeliwa pesa zako mchana kweupe, siku unaanza shughuli zako ndipo unakuja kugundua umetapeliwa.

Ajabu ni kwamba Kigamboni karibu yote, Temeke, Buguruni, Wazanzibar wanamiliki ardhi bila bugudha. Msingi wa hoja yangu ni kwanini Wazanzibari wanamiliki ardhi Bara licha ya kwamba katiba hata ya sasa ipo wazi haiwaruhusu ?

Kimsingi Tanganyika imekuwa kama shamba la bibi au yatima, haina mwenyewe wala mtetezi.

kuna kila sababu ya kuona kwamba Zanzibar "wametuzidi akili", Sizungumzii akili za kukariri darasani what is physics, ni akili ya kawaida kabisa ambayo mtu inabidi awe nayo, kwa kiingereza huitwa "common sense"

View attachment 2041966

Nope, hawajatuzidi akili, ipo siku
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,869
2,000
Zanzibar kisiwa
Ardhi yao ndogo
Wangeruhusu wabara wamiliki ardhi
Mpaka sasa kungekwisha

Ova
Kama ni hivyo basi kila mtu akamiliki kule kwao, Wazanzibar wakamiliki ardhi Zanzibar na Watanganyika wamiliki ardhi Tanganyika. Kila mtu asimiliki kwa mwenzie
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom