Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Ngasere45

Senior Member
Dec 31, 2022
149
566
Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Ukinambia ni sehemu ya Tanzania nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar?

2. Kwanini ni ngumu ajira za Zanzibar kuhusisha Watanganyika?

3. Kwanini Zanzibar wana rais wao na bendera yao?

4. Kwanini wana taasisi zao zinazojitegemea kama mahakama, bunge, tume ya uchaguzi nk?

5. Kwanini timu za Zanzibar zinaiwakilisha Zanzibar kama nchi kwenye mashindano mbalimbali ya CECAFA, CAF kwa ngazi ya vilabu?

6. Kwanini taasisi zao zinaendeshwa tofauti kabisa na Tanzania, mfano Zanzibar watu wanatibiwa bure kwa hospitali za serikali, gharama za umeme ni nafuu sana nk?

Ukinambia Zanzibar ni nchi huru nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini haina amiri jeshi mkuu kwa maana ya kwamba haina jeshi linalojitegemea (Standing Army)?

2. Kwanini Zanzibar haiwezi kukopa katika taasisi yoyote ya kimataifa isipokuwa ikopewe na Tanzania bara na kama Tanzania bara wakikataa ndio habari ya kukopa inaishia hapo?

3. Kwanini haina sarafu yake yenyewe?

Mtazamo wangu: Muungano una mapungufu mengi.

Huwezi kuwa na Nchi ambayo kuna wakati inakuwa nchi kamili na kuna wakati inakuwa sehemu ya nchi nyingine.

Nadhani ni muda sahihi wa muungano huu kurekebishwa na tuwe na serikali 3 yaani

1: Serikali ya kwanza ni serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo itasimamia mambo yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar.

2: Serikali ya pili ni serikali ya Tanganyika ambayo itasimamia mambo yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanganyika.

3: Serikali ya tatu ni serikali ya muungano ambayo itasimamia mambo yote ya muungano tu kwa pande zote mbili.

Ama tuachiwe nchi yetu tujitegemee wenyewe ila ndugu zetu Watanganyika hawayataki yote haya badala yake wanataka kuendelea kuiona Zanzibar ikidhalilika na kuendelea kuwa masikini katika Muungano huu usiokuwa na usawa wala haki ndani yake.

Inavyoonekana ni kuwa Nyerere alitaka kuwalaghai Wazanzibari mwisho wa siku akajikuta anatengeneza muungano usioeleweka na sasa madhara yake yapo dhahiri.

Hoja ya usalama kwangu haina mashiko! Kama Watanganyika wameweza kuilinda mipaka yao yote dhidi ya nchi korofi zinazowazunguka watashindwaje kujilinda dhidi ya Zanzibar?

Huu ni ukoloni uliopevuka tena ukoloni wa mtu mweusi ni mbaya sana

Wallah sijawahi kuwaona CCM hata mmoja kutetea maslahi ya Zanzibar katika Muungano

2025 asikae mtu ndani ili tuiondoe CCM madarakani na inshaallah Allah ataleta rehma zake

Heshima ya Zanzibar itarudi inshaallah kimataifa na tutambulika kwa jina la taifa letu la Zanzibar popote pale duniani inshaallah.
 
Zanzibar wanaifilisi Tanganyika. Chao Chao Chetu Chao.

Sasa hivi kuna wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri ambao ni wazanzibar huku Tanganyika.

Watanganyika bongo lala. Wazanzibar wanatutawala watu milioni 60 wao wapo milioni 3
 
Sijawahi ona hii, yani nchi kama Tanganyika yenye kila aina ya rasilimali ika ibe au kuchukua kitu Zanzibar ili ijiendeshe?
Tuwekee bayana kuna rasilimali gani zanzibar zaidi ya fukwe za bahari na minazi?
 
Tanganyika inainyonya zanzibar kiuchumi na Kisiasa. halafu bado watanganyika ndio wanaolalamika
 
Back
Top Bottom