Stress za kuolewa/kuoa sio kwa wadada tu!

Stress za kuolewa/kuoa sio kwa wadada tu!

Stress za mwanaume halisi ni kushindwa kuchagua yupi kati ya Lundo la wanawake alionao ili aoe....


Wanaume Juu

Sent From My Nokia Ya Tochi
Kukosa kipato, pesa na uwezo wa kuendesha familia hakuwezi kumfanya mwanaume kuwa na stress??
 
Mwanaume huwezi kuoa hujui mke utamlisha vipi, kumbuka kwenye kuoa kuna maswala ya kifamilia , pande 3, hiyo mliyoiunganisha, familia yako wewe mwanaume na familia ya mwanamke

Mwanaume akishakuwa na uwakika wa hayo mambo juu hapo huwa hana pressure kubwa ya kuoa.

Kwetu sisi wanawake tunasubiri mwanaume akutongoze halafu aamue mwenyewe, akuoe au akutumie km tissue.

Kwa hiyo sisi wanawake tunapressure kubwa kuliko wanaume kwasababu hata huyo mchumba uliyenaye huna uwakika kama atakuoa au la. Ndio maana siku hizi mwanamke akishamuelewa mwanaume anajibebea mimba fastar kwa sababu anajua mwanaume anakwambia subiri mwisho wa siku unaachwa anaolewa mwingine.
Aiseee uko sahihi
 
Hilo lipo wazi kabisa. Hata tukiachana na sababu binafsi/intra-personal facts kuna sababu za kijamii zitakazomletea stress.

Kwa jamii zetu Ndoa sio jambo la mtu bali ni jambo la jamii. Leo hii Daby nikichelewa kuoa wazazi, ndugu na jamii yote lazima iniangalie kwa jicho lingine. Hii ni stress tosha.

Mwanaume mtu mzima asiye na mke wala watoto kwa Jamii zetu ni mhuni hata kama hauambiwi ila akilini mwao ndiyo hivyo. Utajipa moyo kwamba unamind maisha yako ila kiuhalisia huwezi kujiengua kwenye mawazo ya jamii yako.


Sema sasa Eli79 wanawake wa jamii zetu wanaihitaji Ndoa zaidi ya tunavyoihitaji sisi. Hili lipo wazi. Ila stress hadi kwetu zipo.
Thanx mkuu for your well-though insights.
 
Kwa mtazamo wangu kwa sisi wanawake ndoa inakuja wenyewe, huwezi ukakurupuka asubuhi ukamwambia mwanaume nataka unioe, kwahiyo ndoa ni jambo la subraa kutoka kwa mwenyezi mungu, vivyo hivyo na mwanaume japo yeye atatongozaa .
Ingawa ndo mnatukataa haaaaaa
 
Stress unazo wewe domo zege na usieona wanawake wa kuoa,.. Usijarib kulinganisha wewe ulivo na wengine pia wako kama wewe hulka ya kipumbavu kabisa,.....

Sent from my SM-G950FD using JamiiForums mobile app
 
Hapa ni mwendo wa prof Jay na AY tu...kitu 13 hukooo uchumba wenye ukurutu kama sio sugu
 
Hiyo ni mifano tu ya vigezo kuonesha ni jinsi gani unavyoweza kuwa na madem kadhaa na usiridhike nao wote..

Makalio na Sura ni kunogesha tu jumamosi yetu. Huwezi kuoa kwa vigezo hivyo. I'm smart enough to be aware of that.
By the way I'm 24 big bro. No offense taken.
Wow!! 24yrs, dogo you still have the whole world ahead of you.
 
Stress za kuolewa/kuoa zinamkuta mtu yeyote, kutegemeana na ndoto au mipango yake. Maybe mtu amepanga kuwa nikifika age/stage fulani lazima niwe na A, B, C, so hiyo age/stage ikifika na hajakamilisha ndoto yake ndo mtu anaanza kuwa na stress. Au tu mtu anahitaji sana ndoa at the moment afu haoni mtu wa kufunga naye ndoa, ndo wengine desperation inapoanza bila kujali ni me/ke

Nafikiri kinachofanya wanawake tuwe desperate sana ni kale kamfumo kalikotuaminisha kuwa mwanamke hujakamilika bila ndoa . So pamoja na yote unayoyafanya/kuachieve as long as hujaolewa, jamii haitoacha kukuuliza maswali. So wengi wetu wanafall kuwa victims wa society, wanakuwa desperate sana kuolewa. Nilishawahi kukaa na binti, she was just 22 ila ni desperate kuliko shangazi yake hapa.

Kingine ni kwa vile tu wanawake tuna biological clock. Ukishafika age fulani fulani si salama sana kuzaa watoto. But at the very same time wapo wanaume ambao pia wanataka kuwa na familia mapema ili wazae mapema na walee watoto wao. Msemo wa kwamba mwanaume hata akiwa 50 anazaa ni kweli ila nafikiri wengi inawakuta tu kwa sababu fulani zilizo nje ya uwezo wao. Ila kwamba mwanaume anapanga kabisa kuwa nitazaa 1st born nikiwa 50 mmmmh. So wapo wanaume pia ikifika age fulani anaanza kuwa desperate as anaona muda unampita mkono na hana familia

Na ukweli ni kwamba tukakutana na wanaume desperate wengi tu. Kuna muda na sisi japo tunahitaji ndoa lakini udesperate wa mtu unakuogopesha hadi ndoa huitaki tena lol. Mtu mmekutana ndani ya mwezi anataka muanze process za ndoa, me hapana kwa kweli weee.

IMO, kuwa desperate ( na kitu chochote not necessarily ndoa) ni choice, ni sign ya kuwa "UNGRATEFUL". Unaconcentrate sana na usivyonavyo, unasahau kucount your blessings ndo maana unapanic. Maandiko yanasema "Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo yote mtazidishiwa". So why are you stressing yaself ? Don't you believe in God's perfect time darlin?. Plus hakuna kitu kibaya kama kufanya maamuzi ya maisha yako ukiwa desperate. No wonder ndoa zetu nyingi ni za misukosuko, mtu hakuolewa/kuoa kwa sababu anajua ndoa ni nini na anajua ni nini wito wake katika ndoa, alifunga ndoa simply because muda umeenda or jamii inamnyooshea sana vidole au anataka azae watoto mapema. Decision yoyote ya maisha yako ifanyike muda ambao umerelax, while things are flowing naturally. Nikianza kuhesabu ambavyo sina kwenye maisha yangu, ni vingi mweeh but I chose to stick with my blessings, na huwezi kunikuta nina stress unless niwe naumwa (hahha Mungu nisamehe tu muda ninaoumwaga lol, Afya yangu, mtaji wangu). Weekend njema
Well said mamaa sina cha kuongeza baadae njoo uchukue choda..na ulivyonisusa sasa
 
Well said mamaa sina cha kuongeza baadae njoo uchukue choda..na ulivyonisusa sasa
Hahaha fanya kunitumia hela ya soda, weekend leo. Ufanye kunishtua my ndugu, kuna vitu nilivuruga so no where to be seen
 
Ee unakuta huyu ana tabia nzuri lakini tako hana, mwingine ana tako ila sura mweeeh.. Huyu ana sura na tako ila tabia mbayaa.. Yaani ni stress tupu braza angu[emoji24]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] hapo ndo changamoto mnachagua sana

Me nakubaliana na mtoa mada mkishafikisha 30 mtaanza kupunguza vigezo
 
hahahaa
field marshall nakuona
Waiii...nipo huku mtaani na vijana walioa ila wameshabwagana...wengine wameo ila ndo hivyo wako kama Mabachelor tuu..kutwa vijiweni, clubs, hawajielewi...ina maana hawakuwa mature kuoa...walikuwa na stress kwa kuona wengine..


Woooooooi...sina muda
 
Ukiona mwanamke hana wa kumtoa kutu jua hajataka wanaume wapo kibao
Tatizo wanaume wanaweza wakawa wanapita na kuondoka tu, mwisho wa siku ndoa ikaota mbawa moja kwa moja.

Sifa ya mwanamke mwema ni kukataa wanaume wanaokuja kwa ajili ya kumtoa kutu. Lakini kwa wanaume ni kinyune chake.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom