STORY: Miss Tanzania

STORY: Miss Tanzania

MISS TANZANIA
SEHEMU YA 42
MTUNZI 😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Patrick amewahi kuwa na mahusiano na Savanna…?!!!.” Kila alipowaza jambo hili aliendelea kumuumia sana kichwa.
“Ninakubaliana na maneno ya George kwa sababu Patrick huwezi kumweleza chochote kuhusu Savanna akakuelewa.Anamuamini Savanna kupita kiasi.Vile vile hainiingii akilini hata kidogo katika ulimwengu wa sasa mtu akajitolea kuifanya kazi hii ngumu ya kisheria bila kulipwa chochote.Savanna amefanya hivi kwa sababu ana agenda yake ya siri.I’m so confused” akawaza Happy
“lakini pamoja na kuwa na agenda ya siri,Patrick ataendelea kuwa wangu peke yangu.Sintamruhusu Savanna amchukue Patrick toka katika mikono yangu.I’ve sacrificed a lot for Patrick and I wont loose him this time.Nitapambana naye” akawaza Happy

ENDELEA…………..

“Loniki,tayari nimekwisha wafahamu wahusika wakuu wanaotakiwa kushughulikiwa.Huyu mwanamke ,Happy ndiye nitakayeanza naye na siku ya kesho lazima nimpate” akasema Khumalo huku akipuliza moshi wa sigara hewani.Walikuwa katika ofisi ya Linah baada ya kutoka mahakamani.
“Nitashukuru sana kama zoezi hili litakwenda haraka kwani itanisaidia hata mimi kurejea haraka Uingereza.Nimeapa sintaondoka Tanzania hadi Patrick na Happy na wengine wote ambao wamesababaisha kifo cha Happy wawe tayari wamekwishalipa..Jioni ya leo nitakupatia kiasi cha shilingi million arobaini na zitakazobaki kumi nitakupatia baada ya kazi hii kukamilika.Kama kazi itakwenda vizuri basi ninaweza hata kukuongeza zaidi.Kwangu mimi pesa si tatizo hata kidogo.” Akasema Loniki.Khumalo akaaga na kuondoka zake kwa miadi ya kuonana jioni ili aweze kupatiwa mzigo wake wa shilingi millioni arobaini.
“Ninamuamini sana Khumalo.Anaongea taratibu lakini siku zote huwa anamaanisha anachokisema.Kama ameahidi kwamba kesho atampata Happy basi amini atafanya hivyo” akasema Linah baada ya Khumalo kuondoka
“Nitashukuru sana .Leo roho yangu imechafuka mno baada ya kumuona Patrick mahakamani tena akitabasamu kana kwamba hana hatia.Sitaki kuisubiri haki ya mahakama ambayo pengine isipatikane.Nitamlipia Vero kwa namna ninayojua mwenyewe.Natamani hata sasa hivi nisikie kamba Patrick na Happy wamefariki dunia.Sikufichi Linah ,moyo wangu utakuwa na amani pale tu Patrick na Happy watakapoacha kuivuta hewa hii safi na sintafumba macho mpaka nitakapohakikisha kwamba wameondoka duniani” akasema Loniki halafu akaagana na Linah kwa miadi ya kukutana jioni ili wamkabidhi Khumalo mzigo wake.
Baada ya kutoka ofisini kwa Linah,Loniki akarejea nyumbani na kumkuta mdogo wake Saraha tayari amekwisha fika na anaongea na mama yake.Loniki akasalimiana na mama yake bila kumsemesha lolote Sarah
“Mbona Sarah humsalimu? Mmekwisha onana? Akauliza mama yao
“Mama sijisikii hata kumpa salamu yangu huyu mwanao.Sioni kama anastahili salamu yangu.” Akasema Loniki kwa dharau
“Sihitaji salamu yako Lonny.” Akasema Sarah huku akitabasamu
“Sarah kwa nini unamjibu hivyo dada yako? Akafoka mama yao
“Mama kamwe sintakubali au kuvumilia dharau za Loniki.Siko tayari kumnyenyekea Loniki na kumsikiliza kwa kila anachokiongea kwa sababu tu anaishi Ulaya.” Akasema Sarah na kwa hasira akaelekea katika gari lake na kuondoka akiwaacha mama yake na Loniki wakishangaa
“Mama huyu mwanao amenichefua sana .Sikutegema kabisa kumuona akiwa hivi.Haonyeshi uchungu wowote ule wa kufiwa na mdogo wake na badala yake anadiriki hata kushirikiana na wauaji wa mdogo wake.Mama siko tayari kuvumilia upuuzi kama huu anaoufanya Sarah.Ngoja nimalize mambo yangu nitamfundisha adabu” akasema Loniki
“Hata mimi sijafurahishwa kabisa na tabia ya Sarah na hasa ya kuchangamana na familia ya Patrick,ambao wametupa mateso haya yote.Kwa uchungu nilionao sijui hata nifanye nini” akasema mama yake Loniki
“Usijali mama,haki lazima ipatikane.Lazima Patrick na wale wote waliosababisha kifo cha mdogo wangu walipe.Sintarejea Uingereza hadi nihakikishe kwamba wote walimuua mdogo wangu wamelipa”
“ Kwa kweli kwa uchungu ninaousikia hata mimi natamani sana waliomuua mwanangu nao walipe uovu wao.Walitenda kitendo cha kinyama sana.Wamemuua mwanangu bila kosa lolote..Ouh Vero ..!!!!” akashindwa kuendelea akaanza kulia.Loniki ambaye naye macho yake yalijaa machozi akamkumbatia mama yake
“Basi usilie mama Haki lazima ipatikane.” Akasema Loniki
“Ahsante mwanangu ,ila naomba wewe na Sarah msigombane kwani sina uwezo wa kuhimili maumivu mengine tena .”
“Hatutagombana mama .Tutarekebishana tu “akasema Loniki

* * * *

Saa kumi na moja za jioni Happy aliamka .Toka aliporejea akitokea mahakamani alikuwa amelala.Kutokana na mawazo mengi aliyokuwa nayo aliamua kumeza vidonge vya usingizi na kulala kwa muda mrefu namna hiyo.Mambo aliyoambiwa na George yalimchanganya sana na alishindwa afanye nini.Kichwa kilikuwa kinamgonga kupita kiasi. Akainuka na kukaa kitandani.
“For the first time I feel dead.Kwa mambo aliyoniambia George ninajihisi kama mfu.Siamini kama Patrick na Savanna waliwahi kuwa wapenzi.Na ninavyohisi kuna kila dalili kwamba bado wanaendelea na mahusiano yao kwa siri kwani walikuwa na mahusiano hata kipindi kile ambacho Patrick alikuwa na Vero.Hii nina maana Patrick hakuwa mwaminifu kwa mchumba wake.Alimsaliti Vero. Na kama aliweza kumsaliti Vero hatashindwa kufanya hivyo hata kwangu.Ouh My God..why always me ? akawaza Happy halafu akaanza kuzunguka zunguka mle chumbani.
“Ninampenda Patrick na nimejitolea kila kitu kwa ajili yake.Lazima nipambane nihakikishe kwamba Savanna hapati nafasi hiyo anayoitaka.Siwezi kukubali ndoto zangu nyingi na za muda mrefu za kuwa na Patrick zipotee hivi hivi.Nilipendana na Patrick kabla hajakutana na Savanna kwa hiyo Patrick ni wangu peke yangu.I’ve made so many sacrifices just to be with him,so I cant let all that be for nothing,I must fight” akawaza Happy halafu akachukua simu na kumpigia Pendo akamuomba amtengenezee juisi ya embe.Baada ya kumaliza kuongea na Pendo akazitafuta namba za simu za Savanna akataka kumpigia lakini akasita .Akavuta pumzi ndefu na kutafakari kwa sekunde kadhaa na mwishowe akakakata shauri
“Lazima nimpigie.Siwezi kumpa Savanna nafasi ya kumpata Patrick.” Akawaza Happy halafu akabonyeza kitufe cha kupigia simu na simu ikaanza kuita.
“Hallow Happy.habari yako?” akasema Savanna baada ya kupokea simu
“Habari yangu nzuri Savanna.” Akajibu Happy
“Happy mbona sauti yako inaonyesha kama vile hauko sawa? Una tatizo lolote Happy? Akauliza Savanna
“Savanna we need to talk” akasema Happy na kumstua kidogo Savanna
“To talk?
“yes Savanna”
“Talk about what?
“About what I’ve discovered today”
“Ok Happy ngoja niegeshe gari hapa pembeni tuongee vizuri.Nitakupigia baada ya muda mfupi” akasema Savanna na kukata simu
“Leo lazima nimeueleze ukweli na utakuwa mwisho wake kuisimamia kesi ya Patrick.Niko tayari hata kukodisha mawakili kumi lakini si kuwa na wakili mmoja aliyevaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni simba.”Akawaza Happy huku simu yake ikiwa mkononi akisubiri Savanna ampigie.Baada ya dakika tano simu yake ikaita.Alikuwa ni Savanna
“Happy tayari nimeegesha gari.Jambo gani unalotaka kunieleza?
“Savanna kuna jambo ambalo ninataka kulifahamu toka kwako.Wewe na Patrick mlifahamiana lini?
“Kwa nini unauliza hivyo Happy ?
“Just answer my question Savanna” akajibu Happy huku sauti yake ikionyesha kutokuwa na masihara.Kimya cha sekunde kadhaa kikapita halafu Savanna akajibu
“Mimi na Patrick tulikutana miaka kadhaa iliyopita,sikumbuki ilikuwa katika mazingira gani”
“Mahusnao yenu baada ya kukutana yalikuwaje?
“Happy mbona unauliza maswali ya namna hiyo? Kuna matatizo gani?
“Savanna naomba unijibu maswali yangu” akasema Happy
“Patrick ni rafiki yangu wa muda mrefu.” Akajibu Savanna kwa ufupi
“Savanna usinidanganye.Tayari ninaufahamu ukweli halisi kuhusu wewe na Patrick.”
“Mimi na Patrick ..!!!!” Savanna akastuka
“Ndiyo.wewe na Patrick”
“Unafahamu ukweli gani kuhusu mimi na Patrick? Akauliza Savanna
“Ninafahamu kila kitu”
“Kila kitu gani Happy?
“Wewe na Patrick mliwahi kuwa wapenzi na bado mnaendelea na mahusiano yenu kwa siri na lengo la wewe kuamua kujitolea kumtetea Patrick mahakamani ni moja ya malengo yako ya kutaka kurudiana tena na Patrick “
“ouh My gosh …!!!!” Savanna akastuka
“Umezipata wapi hito taarifa? Akauliza Savanna
“Sina haja ya kukwambia nimezipata wapi .Ninachotaka kujua toka kwako je ni kweli ? akauliza Happy
“Happy nisikilize vizuri sana mdogo wangu.Tuko katika wakati mgumu wa kuhakikisha kwamba Patrick anashinda kesi kwa maana hiyo haya mambo unayoniuliza hayana msingi wowote kwa sasa.Naomba tuyaache hadi hapo tutakapomaliza haya mambo ya mahakamani na ndipo tutapata muda mzuri wa kuulizana maswali kama hayo” akasema Savanna
“Savanna mambo haya hayana umuhimu kwako lakini kwangu mimi ni muhimu sana.Tafadhali naomba unijibu” akasema Happy
“Happy kwa nini hutaki kunielewa? Nimekwisha kwambia siko tayari kukujibu maswali yako ya kipuuzi kwa muda huu” akasema Savanna kwa sauti ya ukali kidogo
“Savanna wewe ndiye hutaki kunielewa.Nimekuuliza swali rahisi sana Kwa nini hutaki kunipa jibu?
“Nenda kwa aliyekupa taarifa hizo yeye ndiye atakaye kuthibitishia kama ni kweli au si kweli.Mimi sina muda huo wa kupoteza.Tena Happy ninakuomba kama huna jambo la maana la kuongea nami,tafadhali naomba usinipigie simu.Nina mambo mengi ya kushughulikia kesi uliyoisababisha wewe mwenyewe” akasema Savanna
“Savanna hapo ulipo katika kidole chako unayo ile pete uliyopewa na Patrick? Akauliza Happy.Savanna akavuta pumzi ndefu na kusema
“Ninayo”
“kwa nini alikupa pete hiyo? Na kwa nini hujawahi kuivua kidoleni mwako? Kitu kingine ni kwa nini umekorofishana na mumeo George baada ya kuanza kujihusisha na kesi ya Patrick?” akauliza Happy.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa,Savanna akatamani kukata simu lakini akaamua andelee kuongea na Happy
“Happy unahitaji nini toka kwangu?
“Umekubaliana nami kwamba kila nilichokiongea hapa ni ukweli mtupu? Akasema Happy.Savanna akakasirika sana.
“Unahitaji kuujua ukweli,sasa ngoja nikwambie ukweli” akasema Savanna kwa hasira
“Ni kweli mimi na Patrick ni wapenzi.Unataka ukweli gani zaidi ya huo? akasema Savanna na kumpandisha hasira Happy
“Malaya mkubwa wewe.Siku zote hizi umekuwa ukijifanya ni mtu mwema kumbe una lako jambo.Nyoka mkubwa we” akafoka Happy
“Happy naomba usinitukane.Wewe ni binti mdogo sana wa kutukanana na mimi.Tena naomba iwe ni mara yako ya mwanzo na mwisho kuniita mimi Malaya.Una jeuri ya kuufungua mdomo wako na kunitukana sasa hivi wakati kwa uwezo wangu umekuwa huru?.Hivi sasa ulitakiwa uwe gerezani na mimi na Parick tungekuwa huru tunajinafasi kwa raha zetu.Happy narudia tena kukuonya kwamba kuwa makini na kauli zako.Mimi ni mtu mzuri sana lakini hubadilika na kuwa mbaya pale ninapokorofishwa.” Akasema Savanna kwa ukali
“Savanna naomba usinitishe.Kwa taarifa yako sikuogopi hata kid……………!!!!” Happy akastuka baada ya kumuona Pendo akiwa amesimama mlangoni akiwa na sura yenye mshangao na mkononi akiwa na glasi ya juisi.
“Kwa muda gani umekuwepo mlangoni? Happy akamuuliza Pendo
“Nimefika muda huu” akajibu Pendo
“Ok weka hiyo Juisi hapo mezani na uondoke” akasema Happy na pendo akatoka mle chumbani.
“Savanna,narudia tena kukwambia kwamba usitubutu tena kunitolea vitisho.Sikuogopi na huwezi kunifanya lolote.Nakuonya kuanzia sasa achana na hiyo kesi ya Patrick.Mimi nitagharamia kumtafuta wakili mpya wa kumtetea Patrick” akasema Happy na kumfanya Savanna acheke kwa dharau.
“Happy huna uwezo wa kuniamrisha mimi nisimtetee Patrick.Wewe ni mtu mdogo sana kwa Patrick.Kama huamini basi nenda kamweleze Patrick kwamba hutaki nijihusishe tena na kesi yake na usikie jibu atakalokupa na hapo ndipo utakapoamini kwamba wewe ni mtu mdogo sana kwake na huna nguvu wala uwezo wa kuamua chochote kuhusiana na maisha yake” akasema Savanna na kuzidi kumpandisha hasira Happy
“Savanna kama hutajitoa katika kesi hii hadi kesho ba………………..” Kabla Happy hajamaliza kusema alichotaka kukisema Savanna akamzuia.
“Utanifanya nini?
“Nitapambana nawe.Sintakubali unichukulie mpenzi wangu.Nitapambana nawe hadi mwisho.Patrick nimetoka naye mbali sana na sintaruhusu fisadi kama wewe kuyaingilia mapenzi yetu.” Akasema Happy kwa ukali
“Huna lolote la kunifanya Happy.Nakuonea huruma sana Happy hujui unachokiongea.Kuwa makini na kauli zako.Kama unajiona una uwezo wa kupambana na mimi nakuruhusu ujaribu..” akasema Savanna na kukata simu.Happy jasho lilikuwa linamtiririka.Mishipa ilikuwa imemtoka usoni kwa hasira alizokuwa nazo.
“Aaaaaggggghhhh..!!!!!!!!!!!!!!!!!!” akasema Happy kwa hasira na kuanza kutupa tupa vitu hovyo mle chumbani
“Savanna siwezi kukupa nafasi,nitapambana nawe kwa kila namna nitakayoweza.Siko tayari kumpoteza Patrick” akasema Happy kwa hasira huku machozi yakimtoka

* * * *

Zaidi ya dakika tano zimekwishakwenda tangu Savanna amalize kuongea na Happy simuni.Alikuwa ameegemea kiti chake akiwa na hasira kali.
“Bastard ..!!!!!!!” akasema Kwa ghadhabu huku akiipiga mikono yake katika usukani wa gari.
“Happy mbona anataka kukivuruga kichwa changu? Amefahamuje kama nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Patrick?Amefahamuje kama nilikorofishana na George sababu ikiwa ni Patrick?Ameitaja hadi pete hii aliyonipa Patrick” Akawaza Savanna halafu akainua mkono wake wa kushoto akaitazama pete ya dhahabu yenye kung’aa iliyokuwa na maandishi P&S,akatabasamu
“Ni kweli pete hii tulipeana na Patrick ishara ya kupendana hadi kifo.Patrick ni kila kitu kwangu na sintamuacha kamwe” akawaza Savanna halafu akaibusu ile pete
“Nimepata jibu.taarifa hizi zote atakuwa amepewa na George.Ni yeye pekee anayefahamu kila kitu kuhusiana na kinachoendelea kati yangu na Patrick.Aliahidi kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kamba mimi na Patrick hatuwi pamoja tena.Hata hivyo anajidanganya na hawezi kamwe kuizuia mipango yangu.Hata kama ikitokea bahati mbaya nikashindwa kufanikisha mipango yangu ya kuwa na Patrick tena,itakuwa vyema kama nitaishi maisha yangu yaliyobakia bila ya kuwa na mwenzi kuliko kuwa na mtu kama George.Nimekwisha mtoa katika akili yangu na juhudi zake zote za kutaka kuhakikisha kwamba anavuruga mipango yangu kwa matazamio ya kurudiana naye tena ,hazitazaa matunda.Tena ngoja nimuonye asijaribu kupambana na mimi” akawaza Savanna na kuzitafuta namba za George akapiga
“Hallow mpenzi wangu.habari yako.Missing you like crazy my angel…” akasema George mara tu alipopokea simu.Savanna akasonya kwa hasira
“Savanna my love usich………………” kabla hajaendelea Savanna akamkatisha
“Sikiliza George tena naomba unisikilize kwa makini.Sijakupigia simu kutaka kuusikiliza upuuzi wako.Ninataka kukueleza jambo moja tu.Hongera sana,juhudi zako nimeziona.Yote uliyomwambia Happy nimeyasikia.Pamoja na hayo naomba nikwambie kitu kimoja,stay away from me,far away from my life,forget that I exist.Naomba unifute kabisa katika akili yako na usitegemee kwamba siku moja mimi na wewe tutakuwa wapenzi .It’s over George.Huna nafasi tena kwangu.I don’t love you and I never loved you.Ni heri nikaolewa na shetani kuliko kuwa na mtu kama wewe” akasema Savanna
“Savanna..!!!” George akataka kutamka neno lakini Savanna akamzuia.
“Subiri nimalize George.” Akasema Savanna kwa ukali
“Ninakuonya George kwamba usijaribu kushindana na mimi .Kama unahitaji kunifahamu vizuri basi endelea kufuatilia maisha yangu.” Akafoka Savanna na kukata simu.
“Si George ,Happy wala mtu yeyote anayeweza kunizuia kuwa na Patrick.I’ll do everything ,I mean everything to be with Patrick again” akawaza Savanna na kuwasha gari akaendelea na safari yake
“Hii ni vita na inanibidi kupambana.Patrick ni mwanaume ninayempenda na nitahakikisha ninashinda vita hii ya kumgombania.Najua akili yake iko kwa Happy lakini nitafanya kila linalowezekana ili kuiharibu taswira ya Happy kichwani mwake.” Akawaza Savanna .
Mara tu alipomaliza kuongea na Savanna simuni,George akampigia simu Happy.Uso wake ulikuwa umejikunja kwa hasira.
“Hallo naongea na Happy ? akauliza George baada ya simu yake kupokelewa
“Ndiyo George.Happy hapa ninaongea’
“Happy umefanya nini? Kwa nini umemueleza Savanna yale mambo niliyokueleza? Tulikubaliana iwe ni siri yetu mimi na wewe.Kwa nini umekiuka makubaliano yetu? Akasema George kwa ukali
“George nimeshindwa kuvumilia.Patrick ni mtu wangu na nimeshindwa kuvumilia kuona kuna mtu mwingine akiwa katika jitihada za kutaka kumchukua.Nimeamua kumueleza ukweli Savanna ili aachane kabisa na mipango yake.” Akasema Happy
“Happy umekosea sana.Umefanya kosa kubwa sana.Umeharibu kila kitu.Umeniharibia kabisa mimi .Savanna ndiye mwanamke ninayempenda kuliko wote na kwa maneno uliyomwambia umezidi kumuweka mbali nami zaidi.Sikutegemea kama ungeweza kufanya jambo la kijinga kama hili…Unadhani kwa kumweleza ukweli Savanna utamzuia aachane na Patrick? Unajidanganya Happy umezidi kujiweka katika sehemu mbaya na usipoangalia hata huyo Patrick utabaki unamsikia tu.Kwa nini ukakurupuka bila kuuliza Happy???Nilikuona ni mtu mwenye akili kumbe ni mjinga kiasi hiki…..”
Happy hakumpa nafasi George ya kuendelea kuongea akakata simu.
“ Stupid !!!....” akasema kwa hasira

TUKUTANE SEHEMU IJAYO.......
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 43
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT: 0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“George nimeshindwa kuvumilia.Patrick ni mtu wangu na nimeshindwa kuvumilia kuona kuna mtu mwingine akiwa katika jitihada za kutaka kumchukua.Nimeamua kumueleza ukweli Savanna ili aachane kabisa na mipango yake.” Akasema Happy
“Happy umekosea sana.Umefanya kosa kubwa sana.Umeharibu kila kitu.Umeniharibia kabisa mimi .Savanna ndiye mwanamke ninayempenda kuliko wote na kwa maneno uliyomwambia umezidi kumuweka mbali nami zaidi.Sikutegemea kama ungeweza kufanya jambo la kijinga kama hili…Unadhani kwa kumweleza ukweli Savanna utamzuia aachane na Patrick? Unajidanganya Happy umezidi kujiweka katika sehemu mbaya na usipoangalia hata huyo Patrick utabaki unamsikia tu.Kwa nini ukakurupuka bila kuuliza Happy???Nilikuona ni mtu mwenye akili kumbe ni mjinga kiasi hiki…..”
Happy hakumpa nafasi George ya kuendelea kuongea akakata simu.
“ Stupid !!!....” akasema kwa hasira

ENDELEA…………………..

“Its gonna take a lot to drag me away from you.
There ‘s nothing that 100 men or more could ever do
Just like the rain down in Africa
Its gonna take some time but I know you’re worth fighting for
I’d fight for you
Eh ba bam ba eh eh ba bam baeh
I’d fight for you
Eh ba bam ba eh eh ba bam ba eh
I’ d fight for you
Let’s go
Friends are cool
But we both know
They don’t wanna see us together
Don’t wanna lose what I live for
I’m with willing to do whatever
Cause I don’t wanna see you cry
Give our love another chance
I bet we get it right this time
As long as youre prepared to fight,prepared to fight
I don’t wanna live another day
Without your body next to me
I’m not gonna let them break us down
Cause baby I know now,know now

If you got someone that’s worth fighting for .let no body hold you down.
Let me hear say whoa—oh – oh--oh
And if you you found someone that’s worth dying for
The one you cant live without
let me hear say whoa –oh—whoa

Wimbo huu ulioimbwa na Jason De Rulo ndio uliokuwa ukisika chumbani kwa Happy asubuhi hii..Kuonyesha ni namna gani wimbo ule ulivyokuwa umemgusa Happy alikuwa akiimba akienda sambamba na mashairi haya yenye ujumbe mzito.
Saa ya ukutani ilionyesha ni saa mbili na dakika kumi na nane za asubuhi.Happy bado alikuwa mbele ya kioo kikubwa cha meza yake iliyosheheni vipodozi vya kila aina.Siku hii ya leo alidamka mapema sana na aliutumia muda mrefu katika kujiandaa.Baada ya kuhakikisha kwamba amejipodoa vya kutosha akaenda katika kioo kikubwa cha kujitazamia mwili mzima ,akajitazama na kutabasamu
“Sipendi kujisifu lakini mimi ni mzuri.Yule Kunguru Savanna,hafikii hata robo ya uzuri wangu.” Akawaza Happy huku akiendelea kujitazama katika kioo.Siku hii ya leo alikuwa amevaa suruali ya jeans ya rangi nyeupe iliyomkaa vyema aliyoiambatanisha na shati jeupe lenye nakshi za kuvutia.Chini alivaa viatu virefu vyeupe.Hakika kama ungefanikiwa kumuona Happy siku hii ya leo ungekubali kwamba alistahili kuwa mrembo wa Taifa.
Akiwa katika harakati za kutaka kutoka mle chumbani mara mlango wa chumba chake ukafunguliwa na akaingia mama yake.
“Wow ! mama .!Shikamoo.”
“Marahaba mwanangu ,unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri mama”.
“Happy una haraka sana?
“Ndiyo mama..kuna tatizo lolote?
“Kuna jambo nilitaka kuongea nawe”
“Mama kuna mahala ninawahi lakini nitarejea baada ya muda mfupi. Tutakuja kuongea nikirudi mama” akasema Happy na kuchukua mkoba wake mweupe na kutoka mle chumbani akaingia katika gari lake na kuondoka.Hakutaka kumueleza mtu yeyote alikokuwa anaelekea.
“Its gonna take a lot to drag me away from you.
There‘s nothing that 100 men or more could ever do
Just like the rain down in Africa
Its gonna take some time but I know you’re worth fighting for”
Mashairi ya wimbo huu alioupenda Happy yalimfanya atikise kichwa huku akifuatilizia na kuimba taratibu.Alikuwa akiutumia mkono wake wa kushoto kuendesha gari huku mkono wake wa kulia akiwa ameuegemeza dirishani.Alikuwa analivuka daraja la kigamboni kuelekea Uwangwa prison kuonana na Patrick
“Nimewahi sana leo.Natumai muda huu Savanna bado hajafika.Naomba Mungu iwe hivyo na mimi nifike kabla yake.Nataka atakapofika akute tayari nimekwisha ongea na Patrick na kuanzia leo asimame kuisimamia kesi ya Parick.Ni Patrick pekee mwenye uwezo wa kumsimamisha Savanna asiendelee kumtetea.Nina imani atakubaliana na hoja zangu kwa sababu mimi ndiye mwanamke pekee anayenipenda na nimejaa katika akili yake.Nitakuwa tayari kulipa kiasi chochote cha pesa kwa wakili mwingine ili aendelee kumtetea Patrick mahakamani na si Savanna.” Akawaza Happy huku gari likienda kwa kasi kubwa.
Saa nne kasoro dakika saba ilimkuta Happy katika gereza la Uwangwa.Alisalimiana na askari kadhaa waliokuwepo mapokezi.Tayari walikwisha anza kumfahamu hivyo alishughulikiwa haraka haraka kukamilisha taratibu za kuonana na mahabusu wake .Siku hii ya leo alimkuta askari mmoja aliyemsaidia na kumpeleka katika sehemu ya tofauti na ile iliyozoeleka ambayo hutumiwa na kila mtu ajaye kumuona mahabusu.Sehemu hii aliyopelekwa Happy ilikuwa nzuri na ilifaa hata kwa maongezi ya faragha.Baada ya dakika kama kumi hivi Patrick akaletwa na alipogonganisha macho yake na Happy akaachia tabasamu kubwa.
“Ouh my angel..!!!” akasema Patrick
“Patrick..!!!” akasema Happy kwa furaha huku akiinuka kitini na kumkumbatia.
“Mama una dakika thelathini za kuongea na mtu wako” akasema askari aliyekuwa ameambatana na Patrick
“Ahsante sana” akasema Happy kisha akakumbatiana na Patrick.
“Nimefurahi sana kukuona malaika wangu” akasema Patrick kwa furaha halafu akaipeleka mikono yake yote miwili kichwani kwa Happy wakaangaliana kwa sekunde kadhaa halafu wakapeana busu zito na kukumbatiana tena
“Ouh my angel,I was dying to see you” akasema Patrick huku akiketi kitini.
“Patrick my love,before coming here I felt like I was dead but now I feel alive “ akasema Happy
“Ouh Happy usihofu kitu malaika wangu.Mimi ni mzima ninaendelea vizuri sana.Nitashinda hii kesi na nitakuwa huru tena” akasema Patrick
Happy akatabasamu na kuufungua mfuko aliokuwa amekuja nao uliokuwa umesheheni vitu mbali mbali alivyokuwa amemchukulia mpenzi wake.
“Ahsante sana mpenzi wangu kwa kunijali” akasema Patrick.Happy hakujibu kitu akatabasamu.Kimya kifupi kikapita wakati Patrick akiendelea kunywa juisi aliyoletewa na Happy
“Jana ulifika mahakamani? Akauliza Patrick
“Ndiyo nilifika na nilikuwamo katika chumba cha mashtaka .Usingeweza kuniona kwa sababu nilikuwa nimekaa mwisho kabisa.Hata hivyo nilitoka wakati wanasheria wakivutana baada ya kugundua kwamba kuna watu walikuwa wakinitazama vibaya sana.Nahisi watakuwa ni ndugu zako au wa Vero.Sikutaka kuwakwaza ikanilazimu kutoka nje.” Akasema Happy
“Pole sana Happy.Najua kwa wakati huu baadhi ya ndugu zangu na familia nzima hawatakuangalia kwa jicho zuri wakiamini kwamba wewe ndiye chanzo cha haya yoye.Kaza moyo na usiwajali .Elekeza akili yako katika ndoto yetu ya kuwa pamoja.Kesi hii nitashinda na nitakuwa huru na ndoto yetu ya siku nyingi ya kuwa pamoja itatimia.Ninamuamini Savanna,ana uwezo na uzoefu mkubwa katika kusimamia kesi kama hizi na amenihakikishia kwamba lazima atashinda kesi hii” akasema Patrick .Happy aliposikia jina la Savanna likitajwa na kumwagiwa sifa akabadilika ghafla na kuinama chini.Patrick akaendelea kunywa juisi .
“Patrick..!!” akaita Happy
“Yes my angel “ akaitika Patrick.Happy akamtazama usoni kwa sekunde kadhaa na kusema
“Umefahamiana lini na Savanna?
“Savanna ni rafiki yangu wa muda mrefu.Tumefahamiana miaka mingi iliyopita”
“Ouh Okk.! “ akajibu Happy.Patrick akamuangalia Happy usoni na kugundua Hakuwa sawa.
“Happy kuna kitu gani kinakusumbua leo mpenzi wangu? Nakuona kama hauko sawa.Halafu kwa nini umeniuliza kuhusiana na Savanna?
“Usihofu Patrick.Mimi niko sawa kabisa na sina tatizo lolote.Nilihitaji tu kumfahamu Savanna vizuri”
“Happy whats going on? Akauliza Patrick.Happy akainama chini kwa sekunde kadhaa na kisha akainua kichwa na kusema
“Patrick I know you love me”
“Yes I I love you so much”
“As much as you love me you’ll never lie to me” akasema Happy na kuzidi kumshangaza Patrick
“Happy una tatizo gani leo? Akauliza Patrick
“Patrick wewe na Savanna mmewahi kuwa wapenzi? Akauliza Happy.Patrick aliyekuwa ameshika boksi la juisi akastuka na kuliweka mezani akamtazama Happy
“Happy are you ok today?
“I’m ok Patrick.Just answer my question” Patrick akaendelea kumtazama Happy halafu akasema
“Hapana .Mimi na Savanna ni marafiki na hatujawahi kuwa wapenzi”.
Patrick akavuta pumzi ndefu baada ya kumpa Happy jibu lile.Kimya cha sekunde kadhaa kikapita wakabaki wanatazamana.
“Are you sure Patrick?
“Yes I’m sure.Happy kuna kitu gani kinakusumbua leo?
Happy akatoa kitambaa na kujifuta jasho.
“I know down deep in your heart you know exactly that you are lying to me.” Akasema Happy.Patrick akahisi kuchanganyikiwa.
“Happy nimekwambia ukweli mtupu na siwezi kukudanganya malaika wangu”
“Patrick muda niliopewa ni mdogo sana na si lengo langu kuanza kubishana nawe.Ninaomba tu ufahamu kwamba ninaufahamu ukweli wote kwamba wewe na Savanna mliwahi kuwa wapenzi wakati ukiwa na Veronika na mlitengana baada ya Savanna kumpata bwana aitwaye George.Is that true? Akasema Happy.Patrick midomo ilikuwa inamtetemeka.
“Unakumbuka tukiwa Arusha niliwahi kukuhoji kuhusu yale maneno P&S yaliyoko katika pete yako na ukaniambia kwamba hayana maana yoyote? Ukweli ni kwamba maneno yale yanamaanisha Patrick na Savan.Maneno haya yapo pia katika pete na mkufu wa Savanna.” Akasema Happy.Patrick jasho lilikuwa linamtoka
“Savanna bado anakupenda sana na kwa taarifa yako ana mpango wa kuitumia kesi hii kuwa chanzo cha wewe na yeye kurudiana na kuwa wapenzi tena na ndiyo maana amejitolea hata kuifanya kazi hii ya uwakili bure kabisa.Hii ni sababu iliyosababisha aachane na mumewe akiamini kwamba atarudiana na wewe”
Patrick jasho liliendelea kumtiririka.Happy akainuka ,akamfuta jasho kwa kitambaa chake.
“Happy mambo haya yote umeyatoa wapi? Nani aliy………………..” akataka kuuliza Patrick lakini Happy akamzuia
“Patrick hakuna haja ya kuanza kupoteza muda wa kuelezana mambo haya nimeyajua vipi.Kitu pekee ambacho unapaswa kukifahamu na kukizingatia ni kwamba wewe ndiye maisha yangu ,furaha yangu,pumzi yangu na kila kitu changu.Ninakupenda Patrick zaidi ya ninavyoweza kueleza.Usihofu kuhusu haya niliyokueleza,nilitaka tu ufahamu kwamba ulifanya kosa kuwa na mahusiano ya siri wakati ukiwa na Veronika.Sina hakika kama unaweza ukanifanyia mimi jambo kama hilo kwa sababu endapo nikigundua kwamba una mahusiano nje ya uhusiano wetu ,Patrick I swer I‘m gonna kill you and kill myself.You are mine alone.Anyway tuachane na hayo ni mambo yaliyopita na hayana nafasi kwa sasa.Ila kuna jambo moja ninaloliomba toka kwako”
“Jambo gani hilo Happy?
“I want Savanna out of this case.”
Patrick alihisi kama kuishiwa nguvu ,akabaki anamtazama Happy asijue aseme nini.
“Happy…..!!” Patrick akataka kusema kitu lakini Happy akamzuia
“Patrick you are my angel,my everything.Uko hapa ndani kwa sababu yangu,kwa sababu ya upendo wako kwangu.Patrick hicho ni kitu pekee ninachokuomba mpenzi wangu.Nataka Savanna aachane kabisa na kesi hii .Mimi niko tayari kumtafuta wakili mwingine mahiri ambaye ataendelea kukutetea mahakamani lakini si Savanna.Siko tayari kukupoteza Patrick.” akasema Happy.Patrick akainama akatafakari na kusema
“Happy napenda nichukue nafasi hii kwanza kukuomba msamaha kwanza kwa kusema uongo pale uliponiuliza kama niliwahi kuwa na mahusiano na Savanna.Ni kweli niliwahi kuwa na mahusiano na Savanna lakini tulisitisha mahusiano yetu pale yeye alipompata George.Toka wakati huo tumeendelea kuwa marafiki wa kawaida.Tumekuwa tukisaidiana katika mambo mengi na ndiyo maana hata katika kesi hii Savanna ananisimamia kama rafiki na mtu wake wa karibu na si kama mpenzi wake.Savanna ni mwanasheria aliyebobea na mzoefu katika kesi kubwa kama hizi.Amekuwa akisimamamia kesi kubwa kubwa na hajawahi kushindwa.Tafadhali nakuomba uniamini Happy kwamba hakuna kinachoendelea kati yangu na Savanna kwa sasa zaidi ya urafiki wa kawaida.Nakuomba Savanna uniamini kwamba ni Savanna pekee ambaye anaweza kuniweka huru.Naomba tusimuondoe katika kesi hii” akasema Patrick kwa sauti ndogo
“Patrick nakuelewa na sina tatizo na uwezo wa Savanna..Najua unamuamini sana na ni wakili mzoefu na mbobezi wa sheria.Ninachotaka kukiepuka mimi ni kupigana vita ya pili kati yangu na Savanna.Wewe ni mwanaume wangu wa pekee na niko tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili yako na ndiyo maana nimeamua kuachana na kila kitu kwa ajili yako kwa hiyo atakapotokea mwanamke ambaye atatishia usalama wa penzi langu nawe lazima nipambane naye.Sitaki kupambana na Savanna na ndiyo maana ninataka umuondoe katika kesi hii.Mimi niko tayari kulipa gharama za wakili hata zaidi ya mmoja.Najua Savanna anakupenda na yeye atafanya kila linalowezekana ili aweze kunitenganisha nawe.tafadhali Patrick naomba unikubalie jambo hili moja tu.” Akasema Happy
“ Happy nimekuelewa unachokisema na mimi niko radhi kufanya chochote kile kwa ajili yako na ndiyo maana niko hapa gerezani muda huu.Pamoja na yote uliyonieleza bado sijaona sababu ya msingi yakumuondoa Savanna katika kesi yangu.Naomba Happy muache Savanna aendelee kunisimamia mahakamani”
“Patrick umejitolea kuibeba adhabu yangu kwa sababu ya upendo wako mkubwa kwangu.Sina cha kuweza kukulipa kulingana na thamani ya upendo wako kwangu.Please Patrick allow me to do at least one thing for you.Allow me to hire another lawyer for you to replace Savanna.” Happy akaendelea kusisitiza
“Happy najitahidi sana kupingana na nafsi yangu kuhusiana na suala hilo unalolitaka.Najitahidi kutaka kukubaliana nawe lakini bado moyo wangu unakataa kabisa.Najua una lengo zuri la kutaka kunisaidia lakini sina hakika kama uamuzi wa kumuondoa Savanna ni uamuzi unaofaa kwa sasa.Nahitaji kutoka humu gerezani,nahitaji kushinda kesi ili niwezi kuitimiza ndoto yangu ya kuwa nawe na hilo litawezekana tu kama Savanna ataendelea kuisimamia kesi hii.Endapo tutaamua vinginevyo basi ndoto zangu zote za kuwa nawe zitapotea kwa sababu nitapotelea gerezani”
“Patrick huwezi kupotelea gerezani.I give you my word.Nitamtafuta wakili mahiri kabisa na hata zaidi ya mmoja kama itahitajika.” Happy akaendelea kuusimamia msimamo wake bila kutetereka.Patrick akainama akafikiri kidogo na kusema
“Happy hilo ni jambo lisilowezekana hata kidogo.” Happy machozi yakamlenga
“You are still in love with her,right? Akauliza Happy
“Si hivyo unavyofikiri Happy “
“Nijibu Patrick.Bado unampenda Savanna? Kwa sababu yake hauko tayari hata kunisikiliza mimi mpenzi wako” akasema Happy huku machozi yakimtoka na mara mlango ukafunguliwa na wote wakapigwa na butwaa baada ya kumuona mtu aliyesimama mlangoni.Alikuwa ni Savanna.Nyuma yake alikuwepo Andrew ,rafiki mkubwa wa Patrick ,Alois kaka wa Patrick aliyeongozana na mke wake na pamoja nao alikuwepo mama yake Patrick.
Happy akahisi mwili wote unamtetemeka.Akakosa neno la kusema.Savanna akawaongoza watu aliokuja nao wakaingia mle chumbani.Mama yake Patrick nusura aanguke kwa mstuko baada ya kuingia mle chumbani na kugonganisha macho yake na Happy
“Wewe ..!!!” akasema kwa sauti yenye mshangao.Hakuwa ametegemea kama angekutana na Happy mahala pale.Happy alikuwa anatetemeka kwa woga namna alivyokuwa anaangaliwa kwa jicho la chuki.
“Shikam…….” Happy akataka kumsalimu mama yake Patrick lakini kabla hajamaliza salamu yake akazuiwa.
“Haraka sana toka nje” akasema kwa ukali mama yake Patrick.
“Mama ..!!! Patrick akataka kusema jambo lakini naye akazuiwa
Kwa Haraka Happy akauchukua mkoba wake uliokuwa kitini .Machozi yalikuwa yanamtoka akaanza kupiga hatua kuondoka.
“Na iwe ni mara ya mwanzo na ya mwisho kufika hapa.Sitaki kukuona tena karibu na mwanangu shetani wewe.Kila mara unapokaa karibu na mwanangu lazima jambo baya limfike.Una laana wewe mtoto na ndiyo maana mambo mabaya yanakukuta kila wakati.” Akasema kwa ukali mama yake Patrick
“Basi mama imetosha.Usiongee sana utasababisha matatizo mengine” akasema Alois
“Na wewe Patrick naomba ukae mbali kabisa na huyu mwanamke.Sitaki kuona ukiwa karibu naye.Yeye ndiye chanzo cha haya matatizo yote” Akaendelea kufoka mama yake Patrick.
“Patrick nimekuletea wageni” akasema Savanna baada ya hali kutulia mle chumbani
Patrick akasalimiana na mama yake pamoja na ndugu zake.Waliongea mambo mengi na kumpa moyo kuhusiana na kesi inayomkabili.Baada ya maongezi yao yaliyochukua zaidi ya nusu saa wakaaga na kuondoka.Ni Savanna pekee aliyebaki.
“Patrick unajisikiaje leo kwa kuonana tena na ndugu zako na hasa mama? Akauliza Savanna
“Nimefurahi sana kuonana nao tena,nimefarijika sana.Ahsante Savanna kwa kuwaleta.Pamoja na ujio wao lakini bado kichwa changu hakiko sawa” akasema Patrick.Savanna akamuangalia kwa makini na kusema
“Its because of her,right? Amekwambia nini Happy?
Patrick akafikiri kidogo na kusema
“Tayari anafahamu kwamba mimi na wewe tuliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.”
“Hata mimi alinipigia simu jana na kunieleza kuhusu suala hilo na sikuweza kukataa kwa sababu alikwisha elezwa kila kitu na George.Happy alinitukana sana na kusema kwamba atahakikisha ninaondolewa katika kesi yako.Nadhani hilo ni jambo mojawapo lililomleta kwako asubuhi hii.She wanted me out,right?
“Ni kweli Savanna.Happy alinitaka nikuondoe katika kesi yangu na nitafute mawakili wengine”
“wewe umemjibu nini?
“Siwezi kufanya jambo la kipuuzi kama hilo.” Akasema Patrick
“Kwa nini hujamsikiliza mpenzi wako Patrick.Kwa nini hujamtimizia alichokuomba? Akauliza Savanna
“kwa sababu nakuamini Savanna.Umejitolea kunitetea na ninaamini kwamba nitashinda kesi.Hakuna mtu anayeweza kunishauri nikutoe katika kesi hii.”
Savanna akatabasamu baada ya kauli ile ya Patrick.
“Nilikwambia Happy,mipango yako kamwe haitaweza kufanikiwa.Nilikuonya kwamba Patrick hawezi akakusikiliza .Na huu ni mwanzo tu.Ulitaka mapambano na mimi na sasa utaiona nguvu yangu “ akawaza Savanna
“So is that true? akauliza Patrick
“Is what true?
“kwamba umeachana na George.
“Yah..its true.” Savanna akajibu
“Samahani Patrick kwa kutokufahamisha kuhusu jambo hili kwa sababu halikuwa na umuhimu wowote”
“Sababu gani iliyopelekea mkaachana? Akauliza Patrick
“George alinitaka niachane na kesi yako.Aliogopa kwamba kesi hii ingeweza kutuweka karibu muda mwingi kwa hiyo akahofu kwamba pengine tunaweza kujikuta tukirejesha mahusiano yetu ya zamani.Sikuwa tayari kuachana na kesi yako kama alivyotaka George kwa hiyo tukaachana.Patrick niko tayari hata kutengana na dunia nzima lakini si kukuacha katika kipindi hiki kigumu.Hakuna mtu yeyote chini ya jua zaidi yako wewe mwenyewe anayeweza kunizuia nisikutetee.” Akasema Savanna
“Ahsante sana Savanna kwa kunithamini namna hii.Sina kitu cha kukulipa kwa wema wako huu mkubwa.Tafadhali fanya kila linalowezekana ili uweze kuniondoa katika kesi hii”
“Patrick usihofu.Nitafanya kila linalowezekana na kukuweka huru.naomba uniamini.I’ll fight till you get free.I give you my word” akasema Savanna na kumfanya Patrick atabasamu
“Ahsante sana Savanna” akasema Patrick

TUKUTANE SEHEMU IJAYO...........
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 44
MTUNZI😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“George alinitaka niachane na kesi yako.Aliogopa kwamba kesi hii ingeweza kutuweka karibu muda mwingi kwa hiyo akahofu kwamba pengine tunaweza kujikuta tukirejesha mahusiano yetu ya zamani.Sikuwa tayari kuachana na kesi yako kama alivyotaka George kwa hiyo tukaachana.Patrick niko tayari hata kutengana na dunia nzima lakini si kukuacha katika kipindi hiki kigumu.Hakuna mtu yeyote chini ya jua zaidi yako wewe mwenyewe anayeweza kunizuia nisikutetee.” Akasema Savanna
“Ahsante sana Savanna kwa kunithamini namna hii.Sina kitu cha kukulipa kwa wema wako huu mkubwa.Tafadhali fanya kila linalowezekana ili uweze kuniondoa katika kesi hii”
“Patrick usihofu.Nitafanya kila linalowezekana na kukuweka huru.naomba uniamini.I’ll fight till you get free.I give you my word” akasema Savanna na kumfanya Patrick atabasamu
“Ahsante sana Savanna” akasema Patrick

ENDELEA……….

Ilimchukua Happy zaidi ya dakika kumi kutulia na kuwasha gari.Mikono yake ilikuwa inamtetemeka. Kitambaa chake cha mkononi kilikuwa kimeloa machozi.Hatimaye akawasha gari na kuondoka maeneo yale ya mahakamani.
“Na iwe ni mara ya mwanzo na ya mwisho kufika hapa.Sitaki kukuona tena karibu na mwanangu shetani wewe.Kila mara unapokaa karibu na mwanangu lazima jambo baya limfike.Una laana wewe mtoto na ndiyo maana mambo mabaya yanakukuta kila wakati”
Maneno haya ya mama yake Patrick,yalikuwa yanajirudia kichwani kwa Happy na kumfanya aangushe machozi huku akiendesha gari.
“Kwa mara ya kwanza ninajuta ni kwa nini nilionana tena na Patrick.Nadhani ingekuwa vyema kama Patrick asingejitokeza tena katika maisha yangu.Nilikuwa na maisha yangu mazuri na yenye furaha na Mike.Sikutegema hata siku moja kama siku moja ningekuja kuwa na wakati mgumu namna hii.Toka nilipoonana na Patrick maisha yangu yamebadilika ghafla.Ndoto zangu zote za maisha nilizokuwa nazo zimepotea.Mateso na maumivu ya moyo hayaishi.Nimekuwa ni mtu wa kulia kila siku.maisha yangu yamepoteza mwelekeo” akawaza Happy huku akipunguza mwendo wa gari na kufuta machozi
“Una laana wewe mtoto na ndiyo maana mambo mabaya yanakukuta kila wakati.”
Maneno ya mama yake Patrick yakazidi kujirudia kichwani mwa Happy
“Inawezekana ni kweli nina laana na ndiyo maana mambo yangu hayafanikiwa.lakini ni kwa nini hunikuta nikiwa na Patrick pekee? Miaka hii yote niliyokuwa na Mike sijawahi kuangusha hata chozi”.Happy akajiuliza na kushindwa kupata jibu.Sura ya mama yake Patrick akimtazama kwa macho makali yaliyojaa chuki ikamjia kichwani.
“Kila nikiikumbuka sura ya Yule mama mwili unatetemeka.Macho yake yalionyesha dhahiri ni namna gani anavyonichukia.Nimeogopa sana na sijui nitawezaje tena kuonana na Patrick .Kwa sasa itanibidi nijitahidi kwa kila namna nitakavyoweza kuikwepa familia ya Patrick kwani kwao mimi ni adui wao namba moja” Happy alikuwa amezama katika mawazo mazito.Alikuwa analivuka daraja la Kigamboni.
Wakati akiendelea na safari yake huku kichwa chake kikiwa kizito kwa mawazo mengi aliyokuwa nayo,mita kama mia moja hivi nyuma yake gari mbili zilikuwa zinakuja kwa kasi.Gari zile zilionekana kana kwamba zilikuwa zinafukuzana.Happy aliziangalia kupitia kioo cha pembeni lakini hakuzitilia maanani.Gari zile zikafika usawa wa gari la Happy na zote mbili zikawa kama zinataka kupishana kwa wakati mmoja.Gari lililotaka kupitwa likasogea karibu sana na gari la Happy kitendo kilichomstua na kabla hajafanya chochote gari lake likakwaruzwa ubavuni.Happy akataharuki na kufunga breki ya ghafla .Kwa bahati nzuri hakuwa katika mwendo mkali.Gari lililomkwaruza ubavuni nalo likasimama mbele yake.Happy akashuka kwa hasira na kutazama gari lake lilivyokwaruzwa.Kwa hasira akaelekea katika gari lililomkwaruza ambalo lilisimama mita chache toka aliposimamisha gari lake.Milango ya gari lile ikafunguliwa na wakashuka watu watatu mwanadada mmoja na wanaume wawili.
“You people don’t you know how to drive?? !!....” akafoka Happy
“Samahani sana dada.Hatukutegemea kama tungeweza kukukwaruza.Nilikuwa najaribu kumkwepa Yule jamaa” akasema mmoja wa wale jamaa huku akimuelekezea jamaa mmoja aliyevaa suruali nyeusi na fulana nyeupe aliyekuwa akiwaelekea
“Nasema hivi,sitaki kesi wala mjadala wowote.Nahitaji gari langu likatengenezwe.” Akaendelea kufoka Happy
“Usihofu madam,wenye makosa ni sisi na tunaomba tugharamie matengenezo ya gari lako na hata kukupatia gari lingine la kutembelea wakati gari lako linatengezwa mahala lilipokwaruzwa”
“Nimesema sihitaji kitu chochote ninachotaka ni gari langu litengenezwe haraka sana” akaendelea kufoka Happy Muda huo huo jamaa mmoja mnene akiongozana na vijana wawili akafika eneo la tukio”
“Dada samahani sana kwa tatizo lililotokea,naomba tusipoteze wakati,tuelekee gereji gari lako likatengenezwe” akasema yula jamaa mnene.Happy akaanza kupiga hatua kurejea katika gari lake lakini Yule jamaa akamzuia
“Hapana panda gari hili” Happy akageuka kwa hasira .Hakuamini macho yake kwa alichokiona.Alikuwa anatazamana na midomo miwili ya bastora.Kijasho kikamtoka,mwili mzima ukamtetemeka.
“Taratibu bila ubishi ingia ndani ya gari hili.Usitulazimishe tutumie nguvu” akaamuru Yule jamaa.Huku akitetemeka Happy akajikaza na kuuliza
“What’s going on here? What’s the meaning of this?
“Get in the car ,now !! akafoka Yule jamaa mnene.Bado miguu ya Happy ilikuwa mizito sana kunyanyuka.Hakuamini kilichotokea aliona ni kama njozi.
Kwa haraka mwanadada aliyekuwa ameongozana na watu wale akamfuata Happy na kumnong’oneza kitu sikioni halafu akamshika mkono na kumuingiza katika gari lile aliloamriwa kupanda.Haraka haraka wakarejea katika magari yao na kijana mmoja akaenda katika gari la Happy.Magari yakawashwa na kuondoka eneo lile.Kitendo kile hakikuchukua zaidi ya dakika kumi.

* * * *

Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuwaona watu wale waliokuwamo garini.Hakuwafahamu na wala hakufahamu lengo la wao kumtaka aongozane nao.Mapigo ya moyo wake yalikuwa yanaenda kwa kasi ya ajabu na jasho jingi lilimtiririka na kuloanisha shati lake jepesi.
“Mungu wangu mambo gani haya yananitokea tena ? Watu hawa ni akina nani na wanataka nini kwangu? Happy akawaza huku machozi yakimtoka.
“Jamani mnanipeleka wapi? Naombeni msinidhuru tafadhali.Nitawapa kiasi chochote cha pesa mtakachokihitaji” Akalia Happy
“Shut up !!! akafoka jamaa aliyekuwa amekaa pembeni yake.Happy alikuwa amewekwa kati kati ,mikononi alifungwa pingu.Gari lilikuwa linakwenda kwa kasi kubwa na kabla ya kulimaliza daraja la kigamboni jamaa mmoja aliyekuwa amekaa mbele pembeni ya dereva akapokea simu na kuongea kwa takribani dakika mbili halafu akawageukia wale waliokuwa wamekaa kiti cha nyuma ,akawafanyia ishara Fulani na kwa haraka wale jamaa wakamfunga Happy kitamba cheusi usoni na hakuweza kuona chochote tena.Bado aliendelea kulia akiomba aachiwe huru lakini hakuna mtu hata mmoja aliyemjali na kumsikiliza.gari lilianza kukata mitaa ya jiji .Happy hakuweza kutambua ni wapi walikokuwa wanaelekea .
Katika gari iliyokuwa imetangulia mbele,kijana mmoja mwembamba mrefu alikuwa anatabasamu kwa furaha wakati akiongea na simu.Alipomaliza kuzungumza na simu akamgeukia dereva wake
“Sasa ngoja nimpigie simu Loniki nimtaarifu kwamba mtu wake tayari tumekwisha mtia mikononi.” Akasema na kuzitafuta namba za simu la Loniki na kumpigia
“Hallow Khumalo” akasema Loniki baada ya kupokea simu
“Hallo Loniki ,habari yako.Uko wapi mida hii?
“Kwa sasa niko saluni natengeneza kucha”
“Lonny nimekupigia simu kukutaarifu kwamba Happy tayari tumemtia mikononi mwetu na hivi sasa tunaelekea mahala kazi itakapofanyikia.Nitakutaarifu baadae ni wapi tumempeleka ili ushuhudie namna atakavyofanyiwa”
“Wow !! that’s wonderful.Thats good news” akasema Loniki kwa furaha
“One more thing lonny,hatutakiwi kumuweka mafichoni kwa muda mrefu sana.Kila kitu kinatakiwa kifanyike usiku wa leo na halafu tumuache huru.Ukumbuke vile vile kuja na kiasi cha pesa kilichobakia.Jambo la mwisho vijana wanataka uwaongeze shilingi million ishirini ili waweze kuendelea kutoa ushirikiano katika kazi iliyobaki.Kwa kweli vijana wamefanya kazi kubwa na ya kitaalamu sana kiasi kwamba tumemchukua Happy bila ya rabsha wala mtu yeyote kugundua kwa maana hiyo basi vijana wanahitaji motisha ili waendelee kuwa na ari ya kazi.”
“Twenty million more …!!!!???. Loniki akastuka
“yes Lonny vijana wanataka uwaongeze kiasi hicho”
“Khumalo hatukupatana hivyo na wala hatukukubaliana kuongeza kiasi chochote cha pesa zaidi ya kile cha million hamsini tulichopatana.Hizo million ishirini unazozisema nitazipata wapi sasa hivi? Its a lot of money” akasema Loniki
“Sikiliza Lonny.tusiendelee kubishana kuhusu suala hilo.Ulitupa kazi ya kufanya tumekwisha ifanya tayari lakini kutokana na ugumu wa kazi yenyewe vijana wanataka uwaongeze kiasi hicho cha pesa ili kazi yako ikamilike.Najua hauko tayari kuona kazi hii kubwa ikiharibika,kwa hiyo jitahidi upate kiasi hicho cha pesa na tutakapoonana jioni ya leo utukabidhi.”
“Khumalo that’s unfair” akasema Loniki
“Lonny find that money.Mpaka jioni ya leo kama hutakuwa umezipata ,nitamuachia Happy” akasema Khumalo na kukata simu.Uso wake ukapambwa na tabasamu kubwa.Bado akiwa na simu yake mkononi akazitafuta namba za Linah na kumpigia
“Hallow Linah” akasema Khumalo
“Khumalo vipi maendeleo?
“Kila kitu kinakwenda vizuri.Tayari Happy tunaye na kwa sasa tunampeleka mafichoni.Nimempigia simu Lonny na kumwambia kwamba aongeze milioni ishirini na kama akishindwa kuzipata fedha hizo hadi jioni ya leo basi nitamuachia Happy.Nina uhakika atakupigia simu , na kama akifanya hivyo na wewe endelea kumsisititiza ili aweze kuzitafuta hizo fedha.”
“Good job Khumalo.Its time now to make easy money.Kama nilivyokwambia kwamba Lonny ana pesa na nina hakika mpaka jioni ya leo atakuwa amezipata hizo fedha.Hakukuwa na tatizo lolote wakati wa kumkamata Happy?
“Hapana Linah.Tulimchukua kirahisi mno na ni tukio ambalo lilichukua chini ya dakika kumi na hakuna nguvu iliyotumika zaidi ya gari lake kupata mikwaruzo kidogo”
“Vizuri sana khumalo.Nitakuja jioni na Lonny”
“Sawa Linah .Nitamtuma kijana ambaye atakuja kuwachukua jioni na kuwaleta mahala tutakapompeleka Happy”
“Ok Khumalo.Lakini naomba msimuumize Happy.Namuonea huruma sana huyo binti hana kosa lolote”
“Usijali kuhusu hilo.Hakuna mtu atakayempiga hata kofi moja.Atapatiwa kila kitu na hata mimi mwenywe sijisikii vizuri kwa kitendo hiki lakini kwa kuwa kazi hii ina hela nzuri imenilazimu kuifanya tu.See you later Linah.” Akasema Khumalo na kukata simu
“hahahaaaaa..!!! thats why I love Dar es salaam.Its easy to make money in here” akasema Khumalo nakuendelea kucheka halafu akatoa sigara yake akaiwasha na kuvuta.


* * * *



Mara tu alipomaliza kuongea na Khumalo simuni ,Loniki alihisi kuchanganyikiwa.Haraka haraka akapanda gari na kurejea nyumbani.Alipofika nyumbani akamvuta pembeni mama yake aliyekuwa amekaa na kundi la akina mama waliokuja kumpa pole.
“ Loniki vipi,mbona uko hivyo? Akauliza mama yake
“Mama nina shida”
“Shida gani Lonny?
“Mama nina shida ya pesa”
“Pesa !! mama yake akaonyesha mshangao.Hakuwahi kumsikia hata siku moja Loniki akiwa na shida ya pesa
“Unahitaji kiasi gani cha pesa? Akauliza mama yake
“Nahitaji million ishirini”
“Millioni shirini !!!! mama yake akastuka
“Ndiyo mama”
“Pesa zote hizo za nini Loniki?
“Nina shida nazo kubwa na ya haraka kwa leo.Nimeongea na mume wangu na ameniahidi kunitumia pesa hizo kesho toka London.Kama una kiasi hicho cha pesa naomba uniazime na kesho nitakurejeshea.”
Mama yake akabaki anamuangalia loniki kwa mshangao.
“Mama mbona unanitazama hivyo?
“Nimestushwa na kiasi hicho kikubwa cha pesa.lakini hebu niambie Loniki unataka kuzipeleka wapi fedha zote hizo?
“Mama nina shida nazo sana kwa leo.” Akasema Loniki.Mama yake akafikiri kidogo na kusema
“Kwa sasa bado sijajua nina kiasi gani cha pesa ndani kwani Vero ndiye aliyekuwa meneja wangu.Twende ndani nikaangalie nina kiasi gani “ akasema mama yake na wakaelekea chumbani kwake ,akafungua kabati na kutoa vitita vya pesa wakaanza kuhesabu.
“Millioni kumi na tatu” akasema mama yake wakatazamana
“Bado million saba” akasema Loniki
“Tutatoa wapi hizo zilizobaki? Akauliza mama yake
“Mimi sijui mama.Jaribu kufanya maarifa.” Akasema Loniki
“Jaribu kuongea na mdogo wako Sarah anaweza akakupatia kiasi hicho cha pesa”
“Hapana mama siwezi kufanya hivyo.Tena ninaomba usimweleze chochote kile kuhusiana na pesa hizi.Kama unataka kuazima kwa Sarah,azima kama wewe na asifahamu kama unanipa mimi.” Akasema Lonny.mama yake akachukua simu na kumpigia Sarah.
“Hallow mama” akasema sarah
“Sarah nina shida kidogo mwanangu”
“Shida gani mama?
“Nina shida ya pesa “
Sarah akacheka kidogo aliposikia mama yake anashida ya pesa.
“Mbona unacheka Sarah?
“Ni mara yangu ya kwanza kukusikia ukisema una shida ya pesa”
“Kweli Sarah nina shida ya pesa lakini nitakurejeshea kesho”
“Unahitaji shilingi ngapi mama?
“nahitaji million saba”
“Millioni Saba? !!!!..Sarah akastuka
“Ndiyo sarah.Ninahitaji pesa hizo kwa haraka.Kama unazo naomba uniazime na kesho nitakurejeshea.”
Sarah akavuta pumzi ndefu na kimya kifupi kikapita
“Sarah unaweza ukanisaidia kiasi hicho cha pesa?
“Mama unataka kutumia kwa kazi gani fedha zote hizo?
“Nina mizigo yangu imekwama nataka nikaikomboe.Kesho nitakwenda benki na kukurejeshea pesa zako”
Sarah akafikiri kidogo na kusema
“mama naomba unipe masaa mawili,nitakuletea fedha hizo nyumbani”
“Ahsante sana Sarah” akajibu mama yake na kukata simu
“Sarah atatupatia fedha hizo.Lakini hakikisha kwamba kesho tumepata fedha za kumrudishia ndugu yako”
“Usijali mama kesho nitatumiwa fedha na tutazirejesha fedha za Sarah,ila nakuomba sana Sarah asifahamu lolote kama fedha hizo unanipa mimi.”
“Usihofu Loniki sintamwambia kitu”
“Haya ahsante mama.Niko chumbani kwangu” akasema Loniki na kuinuka akaelekea chumbani kwake.
Baada ya kuingia chumbani kwake akampigia simu Linah na kumuomba amfahamishe Khumalo kwamba tayari amekwisha pata kiasi cha pesa alichokuwa anakihitaji na atampelekea jioni ya siku hiyo kama alivyokuwa ameagiza

* * * *

Bado kitambaa kilikuwa machoni kwa Happy na hakuweza kuona chochote.Hakutambua walikuwa wapi lakini alichojua ni kwamba alikuwa wamefika mahala fulani na gari likasimama.Milango ya gari ikafunguliwa na wale watu wakashuka na kumshusha naye pia.Hakujua alikokuwa anaelekea lakini alihisi kama vile alikuwa anashushwa ngazi.Mara wakafika mahala wakasimama na watu wale wakajadili jambo halafu akasikia milango inafungwa na kitambaa kikatolewa machoni.Happy akajikuta katika chumba kikubwa chenye samani za kuvutia.Kulikuwa na kitanda kikubwa kizuri chenye nakshi,kilichotandikwa mashuka mazuri,.Kulikuwa pia na kabati kubwa la nguo na meza kubwa iliyosheheni vipodozi.Kulikuwa vile vile na runinga kubwa na sofa nzuri za kupendeza..hali ya hewa ilikuwa ni ya ubaridi uliotokana na kiyoyozi.
Happy alikitazama chumba kile halafu akageuza shingo yake na kumgeukia mwanadada aliyesimama mbele yake.
“Mmenileta wapi? Mnataka nini toka kwangu? Nani kawatuma mnilete huku? Happy akauliza maswali mfululizo.Mwanadada yule akatabasamu na kusema
“Usihofu Happy.Hapa uko salama na hakuna tatizo lolote.Jisikie huru na wala usiogope chochote.”
“mnataka nini kwangu? Nani kawatuma mnikamate na kuja kunifungia humu? Niambieni mnataka kiasi gani cha pesa? Familia yangu itatoa” akasema Happy huku machozi yakimtoka
“Relax Happy.Huna haja ya kutoa machozi.Sisi hatuna haja na pesa zako na wala hatujakuleta hapa kukudhuru au kuitaka familia yako itupe pesa” akasema Yule mwanadada
“Kama hamna shida na pesa,kwa nini basi mmeniteka nyara?
“Tumekuleta hapa ,kuna mtu anataka kuongea na wewe”
“Mtu anataka kuongea na mimi? Thats crazy.!!!! Kwa nini mtu huyo asinitafute nikaongea naye hadi awatumie ninyi mniteke na kunileta hapa?
“Happy darling,why don’t you take some rest first? Tumekuandalia kitanda kizuri.Feel at home.Anything you need let me know” akasema Yule mwanadada halafu akainuka sofani na kuufungua mlango mmoja
“Kuna bafu hapa.Ingia uoge ujisikie vizuri.Katika kabati kuna nguo nzuri utabadilisha baada ya kuoga”
“Nimesema sitaki kitu chochote,nataka mniache huru niende zangu.” Akasema Happy kwa ukali
“Huna haja ya kukasirika Happy.Mara tu mtu anayetaka kuongea nawe akifika tutakuacha huru.By the way ninaitwa Rosa” akasema Yule mwanadada.Happy akamtazama kwa hasira halafu akajitupa kitandani
“Mambo gani haya yananitokea mimi? Mbona mikosi inaniandama namna hii? Kabla ya suala moja kumalizika linaibuka lingine.why always me?” akawaza Happy huku machozi yakimtoka
“Watu hawa walionileta hapa ni akina nani ? Huyo mtu anayetaka kuongea na mimi ni nani? Anataka nini kwangu? Ouh Mungu wangu tafadhali naomba unisaidie” akawaza Happy na mara mlango ukafunguliwa na jamaa mmoja mnene akaingia akiwa na sinia la chakula.Happy akamkumbuka alikuwa ni mmoja wa watu waliomteka.Taratibu mtu yule akamsogelea Happy pale kitandani
“How do you feel Happy? Akasema Yule jamaa huku akiliweka sinia lile juu ya meza ndogo
“what do you want from me? Who are you people? Akauliza Happy kwa ukali
“Usihofu Happy.Sisi si watu wabaya na wala hatuna lengo baya nawe.Just relax and eat”
“Sintakula chochote hadi huyo mtu aliyewatuma mniteke na kunileta hapa aje anieleze sababu ya kunileta na kunifungia humu.”Yule jamaa akamtazama Happy usoni halafu akatoka nje.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO.........
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 45
MTUNZI😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Watu hawa walionileta hapa ni akina nani ? Huyo mtu anayetaka kuongea na mimi ni nani? Anataka nini kwangu? Ouh Mungu wangu tafadhali naomba unisaidie” akawaza Happy na mara mlango ukafunguliwa na jamaa mmoja mnene akaingia akiwa na sinia la chakula.Happy akamkumbuka alikuwa ni mmoja wa watu waliomteka.Taratibu mtu yule akamsogelea Happy pale kitandani
“How do you feel Happy? Akasema Yule jamaa huku akiliweka sinia lile juu ya meza ndogo
“what do you want from me? Who are you people? Akauliza Happy kwa ukali
“Usihofu Happy.Sisi si watu wabaya na wala hatuna lengo baya nawe.Just relax and eat”
“Sintakula chochote hadi huyo mtu aliyewatuma mniteke na kunileta hapa aje anieleze sababu ya kunileta na kunifungia humu.”Yule jamaa akamtazama Happy usoni halafu akatoka nje.

ENDELEA…………..

Sarah aliwasili nyumbani kwako baada ya masaa mawili kama alivyokuwa ameahidi.Katika mkoba wake kulikuwa na kiasi cha shilingi millioni saba alizokuwa ameomba mama yake.Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mama yake kumuomba msaada wa kiasi kikubwa cha pesa kwa hiyo alifanya kila aliloweza hadi akazipata fedha hizo.
Baada ya kushuka garini moja kwa moja akaelekea sehemu alikokuwa mama yake halafu wakaelekea chumbani akamkabidhi fedha zile
“Mama mzigo huu hapa.Nimelazimika kuzichukua katika akaunti ya mume wangu kwa hiyo kama ulivyoahidi kuzirejesha kesho naomba iwe hivyo” akasema Sarah
“Ahsante sana Sarah.Kesho nitakurejeshea fedha zote”
“Sawa mama,lakini mbona hujaniambia fedha hizo ni kwa ajili ya nini? Umepatwa na tatizo gani?
“Usijali sarah.Ni suala la kawaida katika biashasra zangu” akasema mama yake.Sarah hakutaka maongezi mengi akatoka mle chumbani lakini wakati akitoka akagongana na Loniki ambaye naye alikuwa anaelekea chumbani kwa mama yake.Sarah akapatwa na wasi wasi.
“Whats going on here? kuna kitu gani kinaendelea kati ya mama na Loniki.? Sarah akajiuliza maswali lakini hakutaka kuwafuatilia akaendelea na shughuli zake.Baada ya kama dakika ishirini toka Loniki aingie mle chumbani mwa mama yake mlango ukafunguliwa na wote wawili wakatoka.Sarah akamfuata mama yake
“mama kitu gani kinaendelea kati yako na Loniki?Mna mipango gani ya siri?
“Hakuna kitu chochte kibaya Sara.Kuna masuala Fulani yanayohusiana na biashara zangu ambayo Loniki anakwenda kuyashughulikia.”
“Ni masuala gani hayo mama? Naomba unieleze.”
“Ni masuala yangu ya kibiashara. Mbona maswali yanakuwa mengi Sarah?
“mama nina haki ya kufahamu tatizo lako kama mwanao.Kinachonishangaza ni kwamba miaka hii yote Loniki hakuwepo na tuliokuwa tukikusaidia katika masuala yako mbali mbali ya kibiashara ni mimi na Vero sasa iweje leo uniache mimi na umtumie Lonny?
“Sarah si kila kitu kuhusiana na biashara zangu unapaswa kukifahamu.” Akasema mama yake
“Mama nimetoa pesa zangu nyingi katika tatizo hilo kwa hiyo nina haki ya kujua zinakwenda wapi”
“Sarah inatosha sasa.Nimechoshwa na maswali yako.Umenipa pesa subiri kesho nitakurejeshea pesa zako” Akasema kwa ukali mama yake na kuanza kuondoka lakini Sarah akamuita
“Samahani mama kama nimekuudhi lakini nimekuuliza kwa nia njema tu ya kutaka kufahamu kama una tatizo lolote.Siku zote nimekuwa rafiki yako na hujawahi hata siku moja kunificha tatizo linalokusumbua.Vile vile hata siku moja hujawahi kuniomba pesa na ninafahamu unazo pesa za kutosha toka katika miradi yako .Kitendo hicho kimenistua sana na ndiyo maana nahitaji kufahamu endapo kuna matatizo katika biashara ili kwa pamoja tuone namna ya kuweza kuyaondoa”
“Sarah ahsante sana kwa msaada wako.Kwa sasa tatizo lenyewe limekwisha na endapo nitahitaji msaada zaidi nitakueleza.” Akasema mama yake na kuondoka.Hakutaka tena maongezi na Sarah
“lazima nifahamu Lonny anazipeleka wapi zile pesa.Sina hakika kama mama ana shida ya pesa.Biashara zake zinamuingizia mamilioni ya pesa na hawezi kuwa na shida na millioni saba.Lazima kuna kitu kinaendelea hapa ambacho mama hataki kukiweka wazi.Hata macho yake yanaonyesha kabisa kuna jambo analificha.Taa ya tahadhali inaanza kuwaka kichwani,inaonekana Lonny ameanza kutekeleza mpango wake wa kulipiza kisasi.” Akawaza Sarah

* * * *

Saa kumina mbili za jioni gari aina ya Toyota Surf lenye rangi nyeusi likawasili katika jumba moja la kifahari lenye rangi nyeupe lilizungukwa na miti na maua mazuri
Linah na Loniki wakashuka katika ile gari .Wakiongozwa na kijana aliyetumwa kwenda kuwachukua wakaingia ndani ya jumba lile kubwa la kifahari.Walikaribishwa katika sebule kubwa na nzuri sana na baada ya dakika tano akajitokeza Khumalo.
“Karibuni sana” akasema khumalo huku akiwapa mikono
“Hii ni moja ya makazi yangu pia na mara nyingi hupenda kuja kupumzika huku.Ni watu wachache sana wanaopafahamu mahala hapa? Akasema Khumalo huku akitabasamu na kupuliza moshi wa sigara hewani
“Hongera ,umejitahidi sana Khumalo” akasema Linah
“Ahsante sana” akajibu Khumalo halafu kikapita kimya kifupi ,Khumalo akasema
“Miss Tanzania tuko naye hapa na anaendelea vizuri”
“Kazi nzuri sana Khumalo.Hakukuwa na rabsha zozote wakati wa kumchukua? Akauliza Loniki
“Hapana Loniki.Hakukuwa na tatizo lolote.Tukio hilo limefanywa kitaalamu sana.Natumai umekuja na ule mzigo kamili kama tulivyoongea” akasema Khumalo
“Ndiyo Khumalo.Nimekuja kamili” akasema Loniki na kuufungua mkoba wake akatoa mabunda ya noti akayaweka mezani.
“million thelathini.” Akasema Loniki.Khumalo akayashika mabunda yake akatabasamu
“Mtu wangu yuko wapi? Akauliza Loniki
“Usihofu Loniki.Utamuona tu” akasema Khumalo halafu akayakusanya mabunda yale ya noti akaondoka nayo na baada ya dakika tano akarejea na kuwaomba Linah na Loniki wamfuate.Waliongozana hadi katika chumba kimoja kikubwa kilichokuwa na mitambo mingi.Kilionekana ni kama studio.Kulikuwa na kompyuta nyingi na runinga kubwa ukutani.
“Nipatie namba nane” Khumalo akamwambia kijana aliyekuwamo mle ndani na baada ya sekunde kadhaa kupitia ile runinga kubwa Happy akaonekana akiwa amekaa kitandani.Loniki akasonya na kukunja uso kwa hasira
“Unaweza kuniruhusu nikaonana naye ana kwa ana?
“Hapana Lonny.Hutakiwi kuonana naye ana kwa ana.si vizuri kwa usalama wetu.Nadhani tusiendelee kupoteza muda ni wakati wa kuianza kazi sasa”.Akasema Khumalo,Loniki akatikisa kichwa kuitikia lakini ilionyesha dhahiri kamba alikubali kwa shingo upande.Lengo lake lilikuwa ni kuonana ana kwa ana na Happy
“Ninyi mtashuhudia kila kinachoendelea kupitia hii runinga ambayo imeunganishwa na kamera zilizoko katika chumba alimo Happy.Mtashuhudia kila kitu” akasema Khumalo halafu akatoka mle chumbani.Bado Loniki aliendelea kumtazama Happy kwa hasira

Mlango wa chumba alimowekwa Happy ukafunguliwa na Khumalo akaingia.Happy ambaye alikuwa amejiinamia akainua uso wake baada ya kusikia mlango unafunguliwa.Akakutana na sura iliyomstua na kumfanya aismame
“Its you ..!!!” akasema Happy kwa mshangao
“Hallo Happy..!! akasema Khumalo huku akitabasamu.
“Kumbe ni wewe !!!.Nakukumbuka sana.Ulikuwepo mahakamani juzi na ulikuwa unaniangalia kwa jicho baya.Who are you? ..Happy akasema kwa hasira
Khumalo akatabasamu na kuizima sigara aliyokuwa anaivuta
“Calm down my love.Huna haja ya kuhamaki namna hiyo.Unajisikiaje Happy? Mbona hujala chakula? Akasema Khumalo na kuketi sofani.Happy bado aliendelea kumuangalia kwa hasira
“Niambie ni kwa nini umewatuma watu wako waniteke na kunifungia humu? Unataka nini toka kwangu?
“Happy naomba ukae,kuwa na amani na wala usiwe na hasira.Nimekuleta hapa nina maongezi nawe mafupi lakini ya muhimu sana.Baada ya kumaliza maongezi nawe nitakuruhusu uende zako” akasema Khumalo kwa upole
“Unataka kuongea nami nini na kwa nini usinitafute katika njia za kawaida hadi uniteke nyara? Akauliza Happy
“Happy ni saa moja za jioni sasa na nina imani familia yako tayari imeanza kuwa na wasi wasi juu yako kwa hiyo naomba tusipotee muda .Nisikilize kile kilichonifanya nikulete hapa halafu nitakuacha uende zako” akasema Khumalo na kauli ile ikamfanya Happy atulie.
“Naitwa Job.Mimi ni mfanya biashara wa kimataifa.Nafikiri ni mara yako ya pili kuniona.Baada ya kujitambulisha kwako ,napenda nichukue nafasi hii kukuomba samahani kwa usumbufu wote ulioupata.Nafahamu ulikuwa na shughuli zako nyingi tu na zote zimevurugika kwa kukuleta hapa.Kuna mtu ambaye alitaka uwepo hapa kwa sababu anazojua yeye mwenyewe lakini kwa bahati mbaya hutaweza kumuona mtu huyo kwani jukumu zima la kuongea nawe amenikabidhi mimi.” Akasema Khumalo na kukaa kimya akamuangalia Happy
“ Ni nani huyo aliyekutuma unikamate? Ni Savanna? Akauliza Happy kwa hasira.Khumalo hakujibu kitu akamuangalia Happy kwa makini usoni na kusema
“Happy nafahanmu uko katika wakati mgumu hivi sasa kutokana na mfululizo wa matukio lakini kuna swali moja tu ninalotaka kukuuliza.” Khumalo akatulia halafu kwa sauti ndogo akauliza
“Do you love Patrick?
Happy akamtazama Khumalo kwa mshangao na kusema
“yes I do love him”
“How much do you love him?
“More than my life” akajibu Happy kwa ufupi
“Good.Nafurahi kusikia hivyo” akasema Khumalo
“Jibu lako ninanifanya niamini kwamba uko radhi kufanya jambo lolote kwa ajili yake?
Happy akamuangalia Khumalo machoni halafu akasema
“Ndiyo .”
“nafurahi sana kusikia hivyo.Ni watu wachache sana ambao wanaweza kuyatoa maisha yao kwa ajili ya wale wawapendao.” Akasema Khumalo akakaa kimya kwa muda halafu akasema
“Patrick alikuwa na mpenzi wake aitwaye Veronika.walipendana sana na walikuwa katika hatua za mwishoni ili wafunge pingu za maisha na kuishi maisha yenye raha,lakini ulipojitokeza wewe mipango yao yote ikavurugika. Patrick alibadilika na kusitisha kila kitu kuhusiana na ndoa yake na Vero.Watu wengi sana waliumia.Vero alipatwa na uchungu mwingi na hatimaye alifariki dunia.Ni pigo kubwa kwa ndugu zake,rafiki zake na wale wote waliompenda.Matukio haya yote yaliyotokea yanadhihirisha wazi ni namna gani wewe na Patrick mnavyopendana.Ninadiriki kusema kwamba wewe na Patrick mmeumbwa ili muwe pamoja.Penzi lenu ni zito na la kweli na hakuna wa kuwatenganisha katika hii dunia” akasema Khumalo .Happy bado aliendelea kumshangaa asielewe alikuwa anamaanisha nini kwa maneno yale.Kumalo akaendelea
“Awali ulinihakikishia kwamba uko tayari kufanya jambo lolote kwa ajili ya Patrick.Vizuri sana Happy.Nitapenda nilitibitishe hilo siku ya leo” akasema Khumalo
“Sijakuelewa unamaanisha nini.Naona unaongea maneno mengi sana na sikuelewi unahitaji nini toka kwangu.Kama unahitaji pesa niambie unahitaji kiasi gani nikupatie ili niondoke zangu” akasema Happy
“Happy naomba unisikilize tena unisikilize kwa makini sana.Hatuna haja na pesa zako ,mtu aliyetutuma tukulete hapa ametupa pesa nyingi sana ,a lot of money .Kwa hiyo hatuna shida na senti yako hata moja.” Akasema Khumalo
“Hivi tunavyoongea “ akaendelea Khumalo
“Kuna mtu ambaye ni mfanyakazi wa idara ya magereza anayefanya kazi katika gereza alimo Patrick,yuko tayari na chakula chenye sumu ambacho anasubiri kumpa Patrick na baada ya dakika kumi tu atakuwa amekufa.Anachosubiri ni maelekezo yangu tu.Just one call and Patrick dies” akasema Khumalo
“whaaattt…!!!!!!!!!!.Happy akastuka na kusimama akamuangalia Khumalo kwa hasira
“Najua umestuka sana kusikia kwamba Patrick yuko hatarini kuuawa.Najua Patrick ndiye mwanaume wa maisha yako na endapo atafariki basi ndoto zako zote za kuwa na maisha yenye furaha pamoja naye zitayeyuka.Maisha yako yataharibika na juhudi zako zote ulizozifanya katika kulijenga penzi lako na Patrick zitakuwa ni kazi bure.Maisha ya Patrick ,mwanaume umpendaye yako mikononi mwako hivi sasa.Wewe ndiye utakayeamua hatima ya maisha yake kwa sasa endapo aendelee kuishi au afariki dunia kwa sumu.” Akasema Khumalo.Happy akatetetemeka .Khumalo hakuonyesha kama anafanya masihara
“Please Job,don’t ever hurt Patrick.Hakuna anayefahamu umuhimu wake kwangu.Patrick ndiye maisha yangu,ndiye furaha yangu,ndiye kila kitu kwangu.Siwezi kuishi bila yeye.Tafadhali naomba msimfanye jambo lolote la kumdhuru.Nambieni mtu aliyewatuma amewapa shilingi ngapi? Nitawapa mara mbili yake” akasema Happy huku akilia
“Happy sisi kwa maelekezo tuliyopewa na mtu aliyetutuma tukulete hapa ,hatutamgusa Patrick na wewe utaachiwa huru endapo utakubali kufanya anavyotaka yeye.”
“Huyo mtu anataka nini toka kwangu? Nimemkosea nini? Naomba niongee naye mimi mwenyewe anieleze nilichomkosea” akasema Happy
“Hapana Happy.Huwezi kuongea naye.You’ll talk to me” akasema Khumalo
“Ok Niambie unataka nini? Huyo mtu wenu anataka nini toka kwangu kama malipo ya kutomdhuru Patrick?
“Ni kitu kidogo sana ambacho kiko ndani ya uwezo wako.Kabla sijakwambia nini unatakiwa kufanya hebu kwanza angali picha hizi namna mtu aliyekula sumu hii tunayotaka kumpa Patrick anavyokufa” akasema Khumalo na kwenda katika runinga akachomeka kifaa kidogo cha kuhifadhi kumbu kumbu na kukiwasha.Picha zikaanza kuonekana
“Ukimaliza kuangalia kama utakuwa tayari kumuokoa Patrick utabonyeza kitufe hiki chekundu.Hii ni kengele ambayo itaniashiria kwamba uko tayari na mimi nitakuja mara moja.You have twenty minutes to decide” akasema Khumalo na kutoka.Happy akabaki peke yake mle chumbani akitazama picha zile za kutisha

* * * *

Baada ya kutoka katika chumba alichokuwamo Happy ,chumba ambacho kilijengwa chini ya ardhi,Khumalo akapanda moja kwa moja hadi katika chumba walimo Linah na Loniki walikokuwa wakifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea kule chini kupitia runinga kubwa.
“Nimemuacha aangalie picha zile na nina hakika baada ya kumaliza kuzitazama lazima ataniita.Anampenda Patrick sana na hawezi kukubali Patrick adhurike.” Akasema Khumalo
“Bado roho yangu haina amani kabisa Khumalo.Nilichokuwa nakitaka ni kuona mida hii Happy akiwa katika mateso makali sana.” Akasema Loniki
“Relax Lonny.Hii ni mbinu ya kumfanya Happy akubali kufanya mapenzi yeye mwenywe kwa hiari yake na vijana wetu na ili filamu zitakapotoka isionekane kwamba kuna nguvu ilitumika.Ninakuhakikishia Lonny ,kama lengo lako ni kutaka Happy ateseke basi ndani ya muda mfupi ujao atapata mateso makali sana na kwa namna jina lale litakavyochafuka nina hakika lazima atachukua jukumu la kujimaliza .Filamu hiyo tutaisambaza katika mitandao ya ngono duniani,katika mitandano ya kijamii,katika simu na kila sehemu ambayo tutaweza kuitumia kumchafua Happy.Atateseka kwa maisha yake yote yaliyobaki hapa duniani.” Akasema Khumalo
Lonny bado aliendelea kumtazama Happy kwa hasira kupitia runinga ile.
“Usisahau vile vile kwamba picha zitakazopigwa ,Happy akifanya mapenzi na vijana wetu atafikishiwa pia Patrick gerezani.I swear to you Lonny,kwa namna Patrick anavyompenda Happy I’m sure he will drop dead” akasema Khumalo huku akicheka
“Kwa mtu mwenye jina kubwa kama la Happy kuingia katika kashfa kubwa ya ngono ni habari ambayo haitaweza kufutika kwa urahisi katika vinywa vya watanzania.Ni historia ambayo itadumu kwa vizazi hadi vizazi na atakayeteseka si Happy pekee bali hata familia yake ka ujumla na zaidi sana Patrick” Akasema Khumalo huku akipuliza moshi mwingi hewani
“Damn you Happy !!.Laiti ningekuwa na uwezo wa kufika katika chumba ulimo ,ningekuua mimi mwenyewe kwa mikono yangu.Natamani hata niutafune moyo wako.Wewe ni sababu ya mdogo wangu kufariki dunia.I swear I’ll make your life a living hell before you die” akawaza Lonny huku akiendelea kumtazama Happy kwa hasira kupitia Runinga


* * * *

Familia yote ya mzee Kibaho ilikwisha rejea nyumbani na walikuwa wanajiandaa kupata mlo wa usiku.Ni Happy pekee ambaye hakuwa ameonekana .Toka amerejea nyumbani,mzee Kibaho hakuwa ameonana na mwanae kipenzi Happy.
“Happy ameshindaje? Yuko wapi? Akauliza mzee Kibaho
“Bado hajarejea toka alipoondoka asubuhi.” Akajibu mama yake Happy
“Toka alipoondoka asubuhi?? Akashangaa mzee Kibaho
“Ndiyo.Aliondoka hapa nyumbani asubuhi na alisema kwamba hatakawia kurudi lakini nashangaa mpaka mida hii hajarajea”
“Alikuaga anakwenda wapi?
“Hakusema anakwenda wapi lakini ilionekana alikuwa na haraka na mahala alikokuwa anakwenda”
Mzee Kibaho akainuka na kwenda chumbani kwa Happy kuhakikisha kama ni kweli Happy hayupo.Akarudi sebuleni na kuchukua simu yake akapiga namba za simu za Happy lakini simu haikuwa inapatikana.
“Si kawaida ya Happy kuzima simu.” Akasema kwa wasi wasi mzee Kibaho huku akijaribu tena na tena kupiga simu ya Happy lakini jibu likawa ni lile lile namba anayopiga haipatikani.
“Margreth,Happy hakukueleza mahala anakoelekea leo? Akauliza mzee Kibaho baada ya Margreth kuingia pale sebuleni
“Hapana baba .Jana nilichelewa sana kurudi na sikuweza kuonana naye na leo asubuhi nimeondoka mapema mno na yeye akiwa bado amelala.Nilimtafuta katika simu yake mchana lakini simu yake haikuwa ikipatikana”
Mzee Kibaho akamuita Pendo mfanyakazi wa ndani
“Pendo wewe ndiye uliyekuwa na Happy jana mahakamani.Kuna jambo lolote alikueleza kuhusu mahala alikokusudia kwenda leo?
“Hapana baba hakunieleza chochote.Ninachokumbuka ni kwamba kabla hatujaondoka pale mahakamani alitokea kijana mmoja akaongea kitu na dada halafu tukaondoka naye hadi katika baa Fulani wao wakashuka mimi nikabaki ndani ya gari.Walikuwa na maongezi muhimu lakini sikujua walikuwa wanaongea nini.Baada ya muda mfupi dada akarejea garini kwa kasi akauinamia usukani akaanza kulia.Nilimuuliza alikuwa analia nini lakini hakunijibu kitu,akawasha gari tukaondoka.Jioni mida ya saa kumi na moja akanipigia simu akaniomba nimtengenezee juisi ya maembe.Nilipompelekea chumbani kwake nilimkuta akiongea na simu na kuna mtu alikuwa kama anajibizana naye.Walikuwa ni kama wanazozana.Nakumbuka nilimsikia akitaja jina la Savanna katika maongezi yao”
“ Savanna !!..akastuka mzee Kibaho
“Ninayo namba ya simu ya Savanna ngoja tumpigie pengine anaweza kufahamu mahala alipo Happy” akasema Margreth
“Nipe niongee naye” akasema mzee Kibaho
“hallo Margreth” akasema Savanna baada ya kupokea simu
“Hallow Savanna.Mimi ni mzee Kibaho baba yake na Happy”
“Ouh shikamoo mzee.”
“marahaba Savanna.Samahani kwa kukusumbua usiku huu.Tumekuwa na wasi wasi kuhusu Happy.Hajaonekana toka alipoondoka nyumbani asubuhi ya leo na hata katika simu hapatikani.Umeonana naye kwa siku ya leo?
“Ndiyo baba.Happy nilionana naye asubuhi .Tulikutana gerezani alikuja kumtembelea Patrick.Mimi nilimkuta tayari amekwisha fika na inaonekana aliwahi mapema sana.Hatukupata wasaa wa kuongea zaidi ya kusalimiana kwa sababu nilikuwa nimeongozana na familia ya Patrick.” Akasema Savanna.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu
“Ahsante sana Savanna,.Endapo ikitokea ukawasiliana naye basi tutaarifu mara moja”
“Sawa baba nitafanya hivyo.” Akajibu Savanna na kukata simu
“Kwa mujibu wa maelezo ya Savanna,Happy alikwenda gerezani asubuhi ya leo kuonana na Patrick.” Akasema mzee Kibaho baada ya kumaliza kuongea na Savanna simuni
“Atakuwa ameelekea wapi? Akauliza mama yake
“Alipoondoka asubuhi alinihakikishia kamba hatakawia kurudi.Na hata mavazi yake hayakuonyesha kama alikuwa na safari ya kuelekea mbali.Alivaa mavazi ya kawaida”
“Kama ni hivyo atakuwa wapi? Akauliza Magreth na kisha wakaanza kupiga simu kwa watu mbalimbali kumuulizia Happy lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa amemuona Happy
“Msiwe na wasi wasi.Happy ni mtu mzima na anafahamu kitu anachokifanya.Inawezekana amepatwa na dharura kama mnavyofahamu kwa siku za hivi karibuni amakuwa na mambo mengi .Tuendeleeni kumsubiri na nina hakika atarejea muda si mrefu” mzee Kibaho akawapa moyo familia yake lakini hata yeye alikuwa na wasi wasi mwingi moyoni kutokana na mfululizo wa matukio yaliyomuandama binti yake

TUKUTANE SEHEMU IJAYO..........
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 46
MTUNZI 😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Msiwe na wasi wasi.Happy ni mtu mzima na anafahamu kitu anachokifanya.Inawezekana amepatwa na dharura kama mnavyofahamu kwa siku za hivi karibuni amakuwa na mambo mengi .Tuendeleeni kumsubiri na nina hakika atarejea muda si mrefu” mzee Kibaho akawapa moyo familia yake lakini hata yeye alikuwa na wasi wasi mwingi moyoni kutokana na mfululizo wa matukio yaliyomuandama binti yake

ENDELEA……………….

Mlio wa kengele ukasikika katika chumba walichokuwamo akina Khumalo.
“kazi imeanza.” Akasema Khumalo na kuondoka kuelekea katika chumba alichokuwamo Happy
“Hallo Happy” akasema Khumalo
“Stop it..Please stop it” akalia Happy huku akiyafunika macho yake kwa viganja vya mikono ili asiendelee kuzitazama picha zile za kutisha
“Umeona Happy? Umeona namna sumu hii inavyowatesa watu kabla hawajafa?
“ Please Job ,dont do that to Patrick.I beg you don’t hurt Patrick” akalia Happy
“Kwa hiyo umeamua nini? Uko tayari kufanya kile tunachotaka kwa ajili ya kuokoa uhai wa Patrick? Akauliza Khumalo
“I’m ready.Please don’t hurt Patrick.I’m ready to do anything to save him”
“Vizuri sana.Watu kama wewe ni wachache sana.Hata mimi namuonea wivu Patrick kwani amempata mwanamke anayempenda kwa dhati.”
“Tafadhali sema mnataka niwafanyie nini? Akasema Happy huku akifuta machozi.Khumalo akainuka pale sofani alipokuwa amekaa akamsogelea Happy
“Stop crying Happy.Usilie tena.” Akasema Khumalo halafu akanyamaza kidogo akamtazama Happy usoni na kusema
“ Aliyenituma nikulete hapa alitoa sharti moja tu ambalo ukilitekeleza utaokoa maisha ya Patrick na wewe utakuwa huru.Anao vijana wake wawili wanaokupenda sana na anataka ufanye nao mapenzi.”
“ What !!!!????...Happy akastuka na kumtazama Khumalo kama ameona mzuka
“Hilo ndilo sharti pekee alilolitoa mtu aliyekuleta hapa.Ni juu yako kukubali au kukataa.Kama hautakuwa tayari sisi tutakuacha uende zako lakini nakuhakikishia kwamba wakati wewe ukitoka ndani ya jumba hili,mtu umpendaye kuliko wote duniani atakuwa atakuwa tayari amelala usingizi wa milele.” Akasema Khumalo na kuzidi kumtisha Happy.
“ Ni nani huyo shetani ambaye amenileta hapa? Ni nani huyo asiyekuwa na hata chembe ya ubinadamu? Nimemkosea kitu gani hadi aamue kunitenda namna hii ? akasema Happy huku akilia kwa uchungu
“Happy ni juu yako kuamua .Kilio na matusi kamwe havitakusaidia na muda wetu unazidi kwenda.Ninakupa tena dakika kumi nyingine za kuamua “ akasema Khumalo na kupiga hatua kutoka mle chumbani
“Ouh My God !!!! akalia Happy.Alihisi kuchanganyikiwa
“whats happening to me? Ni kweli nina laana? Kwa nini ninaandamwa na mikosi kama hii kila siku? Huyu mtu aliyenileta hapa ni nani na kwa nini atake kunidhalilisha namna hii? Happy akazidi kulia
“Huyu mtu aliyenileta hapa lengo lake ni moja tu ,kunidhalilisha. Nini kitatokea kama nitakataa kufanya anavyotaka? Je ni kweli Patrick yuko katika hatari ya kuuawa? Sina hakika kama suala hili ni la kweli.Huyu mtu lengo lake ni kuudhalilisha utu wangu.Ninaanza kuhisi mtu huyu atakuwa ni Savanna kwani ndiye mtu niliyelumbana naye jana na tukatoleana vitisho.Pengine ameamua kunionyesha uwezo wake kwa kuniteka na kunileta hapa ili nidhalilike.Siwezi kukubali hata kidogo kuwapa nafasi ya kuuchezea mwili wangu.Ni bora waniue kuliko kuwapa nafasi ya kunichezea.” Akawaza Happy lakini mara akastuka
“What if its true and Patrick is going to die? Inawezekana pengine watu hawa wakawa wanasema kweli ..Am I ready to let Patrick die? I’m confused..!!! Happy akahisi kuchanganyikiwa
“Patrick amejitolea mengi kwa ajili yangu na hata hivi sasa anasota gerezani kwa ajili yangu.Kwa nini na mimi nishindwe kusimama imara kuutetea uhai wake? Kwa maana hiyo itanilazimu kukubaliana na matakwa yao ya kufanya mapenzi na watu wawili? Ouh Jamani akili yangu naona haifanyi kazi tena.Sijui nifanye nini” akawaza Happy na mara mlango ukafunguliwa Khumalo akaingia.Safari hii macho yake yalionekana mekundu na yasiyo na masihara hata kidogo.Happy akaingiwa na woga.Mwili ukamtetemeka
Happy dakika kumi zimekwisha na ninadhani tayari umekwisha fanya maamuzi” Akasema Khumalo huku akimuangalia Happy kwa macho makali sana.
Happy mwili ulimtetemeka na hakujua aseme nini
“Inaoneka bado hujaamua lolote.I’m so sorry Happy.” Khumalo akasema kwa masikitiko halafu akatoa simu yake na akabonyeza namba na kupiga
“Hallow Josh,amekataa kutoa ushirikiano endelea na mpango wetu,mpe Patrick chakula” akasema Kumalo halafu akamuangalia Happy kwa masikitiko
“I’m so sorry Happy.Muda mfupi toka sasa Patrick hatakuwa nasi tena.”
“Stop it !!!!!..Please stop it !!!!...” akapiga kelele Happy
“Please stop it.Dont kill Patrick.Niko tayari kufanya mnavyotaka.” Akasema Happy.Khumalo akamtazama kwa makini machoni halafu akatoa simu yake na kupiga
“Hallow Josh,subiri kwanza.Sitisha kwanza hilo zoezi” akasema Khumalo na kukata simu
“Happy nadhani sasa umeamua kumuokoa Patrick”
“Niko tayari kufanya lolote ili msimdhuru Patrick”
“Vizuri sana” akasema Khumalo huku akitabasamu
“Please don’t hurt Patrick.Hastshili mateso yoyote.Kama ni mateso naomba mnitese mimi”
“Hatukutesi Happy.Fanya kama ulivyoamriwa na utakuwa huru na hakuna mtu atakayemgusa Patrick” akasema Khumalo
“Niko tayari kufanya mnavyotaka lakini kwa sharti moja tu.Mtu huyo ambaye mnataka afanye mapenzi na mimi lazima atumia kinga”
“Usihofu kuhusu hilo Happy.Tunazingatia sana usalama wa afya yako.Jiandae Happy,baada ya muda watakuja vijana wawili unachotakiwa ni kuonyesha ushirikiano na jitahidi kuwaridhisha vijana hao.Baada ya hapo tutakuruhusu uende zako” akasema Khumalo halafu akatoka mle chumbani akimuacha Happy ameinama akilia
“Mpango mzima umekamilika .Mtashuhudia kila kitu muda si mrefu.Ninawahakikishia kwamba hili ni pigo kubwa kwa Happy” akasema Khumalo baada ya kurejea katika chumba walichokuwamo akina Linah
Baada ya dakika zipatazo kumi hivi,Khumalo akiwa ameongozana na vijana wawili waliojazia miili yao na wenye vifua vipana,wakaingia katika chumba alichokuwamo Happy.Vijana wale walikuwa wamezificha nyuso zao ili wasitambulike. Happy alipowaona akaogopa na kuanza kulia.
“Naombeni mnihurumie jamani.Nimewakosea nini hadi mnifanyie hivyo? Akalia Happy lakini Khumalo wala vijana wake hawakumsikiliza
“Happy nyamaza kulia.Futa machozi yako na tukamilishe zoezi letu ili tukurejeshe nyumbani kwenu.Nina imani familia yako ina wasi wasi mwingi sana sasa hivi” akasema Khumalo huku akiwasha taa kubwa iliyokuwamo mle chumbani na kukifanya chumba kiwe na mwanga mkali
“Happy kumbuka makubaliano yetu kwamba unatakiwa uonyeshe ushirikiano na uwaridhishe vijana wangu .Tumeelewana Happy? akasema Khumalo
“Ndiyo “ akajibu Happy
“Vizuri sana” akasema Khumalo na kutoka mle chumbani .Jamaa mmoja kati ya wale vijana walioletwa na Khumalo akamfuata Happy akaketi karibu yake na kumfuta machozi
“Fanya kama alivyokuamuru mkuu wetu.Endapo utaenda kinyume na matakwa yake anaweza akabadilika na akibadilika huwa ni mtu mbaya sana” akasema yule jamaa huku akianza kumtomasa Happy
“Please don’t hurt me “ akasema Happy
“Hautaumia mrembo.You’ll feel like you are in heaven” akasema jamaa mwingine
“Ninafanya hivi kwa ajili ya Patrick, kwa ajili ya kumlinda yeye “akawaza Happy halafu kijana mmoja akaanza kufungua vifungo vya lile shati lake dogo alilokuwa amevaa
“Leave me alone…Nitafanya mwenyewe” akafoka Happy na kumsukuma Yule jamaa halafu akasimama na kuanza kufungua vifungo vya shati lake huku machozi yakimtoka
“Mtu anayenifanyia kitendo hiki ni nani? Nimemkosea kitugani? akawaza Happy
Khumalo,Linah na Loniki walikuwa wameyaelekeza macho yao katika runinga ile kubwa mbele yao wakiangalia namna zoezi linavyoendelea.Baada ya kama dakika tano za mabishano kati ya Happy na wale vijana hatimaye vijana wale wenye nguvu walifanikiwa kumuangusha Happy kitandani na kuanza kumuingilia kwa zamu.Happy alilia sana wakati vijana wale wakiendelea na udhalimu wao juu ya mwili wake.Zoezi liliendelea huku likiendelea kurekodiwa pamoja na kupigwa picha.
Zoezi lilichukua zaidi ya dakika ishirini .Vijana wale walimaliza kazi waliyopewa huku wakihema kwa nguvu sana.Taratibu waliondoka mle chumbani na kumuacha Happy akiwa analia.
“kazi tayari” akasema Khumalo huku akitabasamu
“Ina maana kazi ndo imeishia hapa? Akauliza Loniki kwa mshangao
“Pesa zote hizi nilizotoa ni kwa ajili ya kazi hii ?
“Ndiyo Loniki.Lengo lako ni kumuadhibu Happy,? Akasema Khumalo
“Ndiyo” akajibu Happy
“Kama lengo lilikuwa hilo basi kazi imekwisha kwa leo na subiri kwa hatua itakayofuata.Kesho asubuhi nchi nzima itatikisika kwa taarifa hii.Ni skendo ambayo haijawahi kutokea hapa nchini” akasema Khumalo
“Kwa hiyo nini kitafuata baada ya hapa? Akauliza Loniki
“Niachie mimi kila kitu.Kesho asubuhi usiache kufuatilia vyombo vya habari,magazeti ya udaku na mitandao ya kijamii.Taarifa itakayokuwa inatawala ni ya picha za ngono za Happy” akajibu Khumalo.
Baada ya maongezi kadhaa na Khumalo Linah akamshika mkono rafiki yake Loniki wakaelekea katika gari ambalo liliwarudisha hadi ofisini kwa Linah ambako Loniki alichukua gari lake na kurejea nyumbani
Baada ya Loniki na Linah kuondoka ,Khumalo akaelekea katika chumba alimo Happy,akaufungua mlango na kuingia ndani.Happy alikuwa amelala kitandani akilia.Khumalo akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akapuliza dawa ya usingizi na kutoka mle chumbani
Baada ya dakika kumi na tano kupita toka Khumalo aipulize dawa ile katika chumba alichokuwamo Happy,Khumalo akarejea akiwa na vijana wake na kumkuta tayari Happy amelala fofofo hajitambui.Wakamuinua na kumpakia katika gari lake na kuondoka naye
“Kazi ya kwanza imekwisha.Kazi iliyobaki ni kuzisambaza picha na video.Naamini hadi kesho asubuhi zoezi hili litakuwa limekamilika na hatutakuwa na deni tena kwa Loniki“ akawaza Khumalo akiwa na vijana wake wakimrejesha Happy nyumbani kwao.Khumalo ndiye aliyekuwa ametangulia mbele na gari lake halafu gari la Happy lililokuwa linaendeshwa na kijana mwingine likafuata nyuma.Tayari Khumalo alikuwa anafahamu mahala anakoishi Happy kwani alikwisha mfanyia uchunguzi wa kutosha.
Saa saba kasoro za usiku waliwasili nyumbani kwa akina Happy.Kwa haraka haraka vijana wale wa Khumalo wakashuka katika gari la Happy.Kabla ya kushuka walimuwekea kitu fulani puani na kumzindua toka usingizini .Akapiga chafya mfululizo.Kwa haraka vijana wale wakaingia katika gari la Khumalo na kuondoka kwa kasi maeneo yale.
Mlio wa magari nje ya nyumba yake,ulimstua mzee Kibaho ambaye alikuwa macho mpaka mida hii akimsubiri mwanae arejee.Akatoka chumbani kwake na kwenda getini.Mbwa walikuwa wanabweka.Akachungulia nje kupitia uwazi mdogo na kuliona gari la Happy.Haraka haraka akafungua geti na kuliendea gari.Akachungulia ndani ya gari na kumuona Happy akiwa amelala kitini.Akapigwa na butwaa kwa hali aliyokuwa nayo .Happy alikuwa amelegea na mwili wake haukuwa na nguvu hata kidogo.Kwa haraka akamtoa mwanae garini na kumpeleka ndani na familia nzima ikaamka .Kila mtu alistushwa na hali aliyokuwa nayo Happy.Haraka haraka akaanza kupatiwa huduma ya kwanza.Hakuna aliyefahamu nini kimemsibu hata akawa katika hali ile.Ilikuwa ni hali ya kusikitisha sana.Daktari wa familia aliitwa akafika kwa haraka kuja kumuangalia Happy,akampima na kisha akampatia dawa na kumtaka akapumzike hadi asubuhi atakapopata majibu ya vipimo alivyochukua.

*******************

Kumekucha Tanzania.Ni saa moja za asubuhi, jijini Dar es salaam barabara zimesheheni watu na magari wote walikuwa wanaelekea katika shughuli mbalimbali za kila siku za uzalishaji mali.Katika vibanda na katika sehemu mbali mbali za kuuzia magazeti,kulikuwa na makundi ya watu waliokuwa wakihitaji magazeti ili kufahamu kulichoandikwamo asubuhi hii.Katika baadhi ya vituo vya kuuzia magazeti kulitokea ugomvi wa watu wakigombea magazeti kitu ambacho ni nadra sana kushuhudiwa.
Gazeti lililozusha mjadala asubuhi hii na kuwafanya watu wajazane katika vibanda vya kuuzia magazeti na wengine kufikia hata hatua ya kurushiana makonde ni gazeti la Mitikisiko,gazeti maarufu kwa kuandika habari za udaku na hasa zile zinazowahusu watu maarufu ndani na nje ya nchi.Siku hii ya leo gazeti hili lilipambwa na kichwa cha habari kilichobeba habari iliyozua gumzo nchini.
“HAIJAWAHI KUTOKEA” hiki kilikuwa ni kichwa cha habari kilichoandikwa kwa maandishi makubwa na chini yake kulikuwa na vichwa vingine vidogo vidogo.
“NI VIGUMU KUAMINI LAKINI KWELI”
“HUU NDIO UCHAFU WA MISS TANZANIA”
Vichwa hivi vya habari vilisindikizwa na picha kubwa ya Happy Kibaho,akiwa mtupu huku sehemu ya kifuani na chini ya kiuno zikiwa zimezibwa kwa rangi nyeusi.Picha nyingine ilimuonyesha Happy akiwa amelala kitandani akiwa na wanaume wawili waliozifunika nyuso zao ambao ilionyesha wazi walikuwa katika harakati za kufanya mapenzi.
“Mlimbwende aliyenyakua taji kubwa la urembo hapa nchini la miss Tanzania ambaye siku chache zilizopita amelivua taji hilo kutokana na kashfa ya kujihusisha katika ugomvi wa kumgombania mwanaume,na kusababisha kifo cha msichana aitwaye Veronika ,ameingia katika aibu kubwa baada ya picha na video yake ya ngono kuvuja” Haya yalikuwa ni maelezo ya utangulizi ya habari hii kubwa na kulifanya gazeti la Mitikisiko kuongoza katika mauzo kwa siku hii.Taarifa ile iliendelea katika ukurusa wa tatu huku ikipambwa na picha zinazomuonyesha Happy akiwa mtupu huku akifanya mapenzi na wanaume wawili waliozifunika nyuso zao katika mitindo tofauti tofauti..Ilikuwa ni aibu nzito isiyoelezeka .
Katika tovuti mbali mbali na mitandao ya kijamii,tayari video na picha za Happy vilianza kusambaa kwa kasi kubwa na kuwa gumzo mtandaoni.Watu walikuwa wanatumiana video na picha hizo za Happy akifanya ngono na wanaume wawili hadi katika simu za mikononi.Kutokana na kukua kwa teknolojia ya upashanaji habari ndani ya masaa machache tayari habari kuhusu Happy ilikwisha sambaa karibu nchi nzima.
Mlango mdogo katika geti la kuingilia nyumbani kwa akina Happy ulikuwa wazi,hivyo kumfanya mama Joseph jirani wa akina Happy,apite kama mshale na kuingia ndani huku akihema akiwa na gazeti mkononi
“Mama Happy ..!!! akaita mama Joseph .Alikuwa anahema huku jasho likimtoka.Mama yake Happy ambaye alikuwa katika kazi za usafi wa nyumba asubuhi hii,akaja kwa kasi baada ya kusikia sauti ya mama Joseph.
“Mama Joseph kuna tatizo gani? akauliza mama Happy kwa mshangao
“Mama Happy njoo huku” akasema mama Joseph huku akimvuta mama Happy kuelekea sebuleni.
“Mama Happy umeshapata taarifa?
“Taarifa gani mama Joseph? Mama yake Happy akazidi kushangaa
“Ina maana hakuna hata mtu mmoja aliyekupigia simu kukueleza nini kimetokea leo?
“mama Joseph mbona unanichanganya? Nini kimetokea?
“Soma gazeti hili” akasema mama Joseph huku akimpa mama Happy gazeti lile alilokuwa amelishika mkononi.Mara tu mama Happy alipolitupia macho akaanguka na kupoteza fahamu
Mama joseph akapiga ukulele mkubwa uliomstua mzee Kibaho aliyekuwa chumbani na kumfanya atoke haraka na kuelekea sebuleni kuangalia kumetokea nini.Alistuka baada ya kumkuta mkewe akiwa ameanguka chini akiwa hana fahamu
“Nini kimetokea? Akauliza mzee Kibaho huku akimuinamia mkewe.Mama Joseph hakuweza kujibu chochote alikuwa anatetemeka huku machozi yakimtoka.Haraka haraka mzee KIbaho akaanza kumpatia mke wake huduma ya kwanza.
Kelele zile za mama Joseph,zilimstua pia Happy .Alizisikia kelele zile akiwa usingizini na mwanzoni alidhani labda alikuwa ndotoni lakini alipofumbua macho aliendelea kuzisikia.Akaogopa pengine kuna jambo baya limetokea pale nyumbani kwao. Kichwa kilikuwa kizito na mwili wake ulimuuma sana.Alisikia maumivu makali sana sehemu za kinenani lakini akajikaza na kuinuka na kukaa kitandani.Akafikiri kidogo halafu akavaa nguo na kutoka mle chumbani na kuelekea sebuleni ambako ndiko kelele zilikokuwa zinatokea.Alistuka baada ya kumuona mama yake akiwa amelala chini hana fahamu.Baba yake alikuwa anahangaika kumsaidia ili aweze kurejewa na fahamu.
Mama Joseph na mfanyakzi wa ndani Pendo walikuwa wanalia kwa uchungu.Mara tu mama Joseph alipomuona Happy ameingia pale sebuleni akazidi kulia.Happy akatamani ajue kilichokuwa kimetokea na kumpelekea mama yake apoteze fahamu,akamfuata mama Joseph na kumuomba anyamaze ili aweze kumueleza nini kilichotokea
“Mama mdogo kuna nini? Nini kimetokea hapa? ..akauliza Happy kwa sauti dhaifu lakini mama Joseph hakujibu kitu na badala yake akamuonyeshea ishara alichukue lile gazeti lilikokuwa limeanguka chini.Taratibu Happy akainama na kuliokota ,akalikodolea macho.Mwili wote ukamtetemeka alipokuwa analisoma.Alikuwa ni kama mtu aliyeliona jitu la kutisha.Mara gazeti lile likaanguka chini na uso wa Happy ukajaa machozi .Taratibu bila kuongea na mtu yeyote akageuka na kutembea kwa kasi kuelekea chumbani kwake.
Mama Joseph aliyekuwa anamuangalia Happy kwa makini ,akaogopa sana kutokana na mstuko alioupata Happy.Akamfuata mzee Kibaho na kumuomba amfuate Happy
“Kuna nini? Happy amefanya nini? Akauliza mzee Kibaho huku akiendelea na jitihada zake za kumpatia huduma ya kwanza mke wake ili aweze kurejewa na fahamu
Mama joseph akaliokota gazeti lililoanguka chini na kumpatia mzee Kibaho
“Hili ndilo chanzo cha haya yote” akasema mama Joseph
Mzee Kibaho akaanza kulipitia lile gazeti na mara akahisi mikono yake ikimtetemeka.
“Ouh My God !!!” akasema mzee Kibaho na kwa haraka akainuka na akaelekea chumbani kwa Happy.Mlango wa Chumba cha Happy ulikuwa umefungwa.Akagonga lakini hakukuwa na dalili zozote za kuwepo mtu ndani.Akachungulia katika tundu la funguo na kuiona funguo ikiwa ndani.
“Happy fungua mlango..Fungua mlango mwanangu …” akasema mzee Kibaho lakini hakusikia dalili zozote za kuwepo mtu mle chumbani.Kwa kasi akakimbia kuelekea chumbani kwake akachukua ufunguo wa akiba na kuja kuufungua mlango akaingia ndani
“Ouh Mungu wangu ..!!!!!..Mzee Kibaho nusura aanguke kwa alichokiona mle ndani.Happy alikuwa amelala kitandani huku mapovu yakimtoka mdomoni.
“Happy..!! Happy.!!! Happy.!!!!!...akapiga ukelele mzee Kibaho huku akimtikisa Happy lakini hakuwa na fahamu hata kidogo,alikuwa anakoroma.
“Ouh Mungu wangu !!” akasema mzee Kibaho baada ya kuiona chupa ndogo yenye dawa ya kuulia panya ikiwa mezani.Haraka haraka akamuinua Happy na kukimbia naye hadi garini.Mama Joseph na Pendo wakapiga ukeleel mkubwa baada ya kuishuhudia hali ile ya Happy.Mzee Kibaho hakuwajali akawasha gari lake na kwa kasi ya aina yake akaondoka pale nyumbani huku akipishana na majirani waliokuwa wakiingia kwa kasi mle ndani baada ya kusikia kilio cha mama Joseph na Pendo.
“Please God.dont let my daughter die, Please save her” mzee Kibaho ambaye kwa mbali macho yake yalilengwa na machozi ,alikuwa akiyarudia maneno haya mara kwa mara wakati akiendesha gari kwa kasi kuelekea hospitali.Kila sekunde zilivyozidi kusonga mbele ndivyo hali ya Happy ilivyozidi kubadilika na kupoteza matumaini.Alikuwa anakoroma na povu jingi likiendelea kumtoka
Geti la hospitali ya Brahmaputra inayomilikiwa na daktari bingwa Makhresh Patel lilikuwa wazi .Gari la mzee Kibaho lilikuwa likija kwa kwendo wa kazi huku likiwa limewasha taa zote.Watu waliokuwa wamesimama karibu na geti walikimbia baada ya kuliona gari lile namba lilivyokuwa likija.
Namna gari lile lilivyoingia hospitali na sauti za matairi yakilalama kutokana na breki kali aliyofungwa,iliwafanya madaktari na wauguzi watoke nje na kushuhudia nini kilichotokea.Mzee Kibaho akashuka na kukimbia na kuwataarifu wauguzi kwamba kulikuwa na mgonjwa mahututi ndani ya gari.Kwa kasi ya aina yake,wauguzi wakampakia Happy katika kitanda na kumkimbiza katika chumba cha wagonjwa mahututi.Mzee Kibaho akaombwa asubiri nje.Bado mwili wake ulikuwa unamtetemeka kupita kiasi.Aliogopa sana.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO....
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 47
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT: 0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Namna gari lile lilivyoingia hospitali na sauti za matairi yakilalama kutokana na breki kali aliyofungwa,iliwafanya madaktari na wauguzi watoke nje na kushuhudia nini kilichotokea.Mzee Kibaho akashuka na kukimbia na kuwataarifu wauguzi kwamba kulikuwa na mgonjwa mahututi ndani ya gari.Kwa kasi ya aina yake,wauguzi wakampakia Happy katika kitanda na kumkimbiza katika chumba cha wagonjwa mahututi.Mzee Kibaho akaombwa asubiri nje.Bado mwili wake ulikuwa unamtetemeka kupita kiasi.Aliogopa sana.

ENDELEA…………

“Please my Lord,don’t let my daughter die” akazidi kuomba mzee Kibaho.na mara simu yake ikaita.Alikuwa ni Margreth.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu kabla ya kuipokea simu ile halafu akabonyeza kitufe cha kupokelea.
“Hallo Margreth” akasema mzee Kibaho
“baba uko hospitali gani?
“ niko hapa Brahmaputra hospital.Uko wapi Margreth?
“Nimefika hapa nyumbani sasa hivi nikaambiwa kuhusu hali ya Happy.Dady tell me please how’s she? Akauliza Margreth
“Tayari amepokelewa hapa na ameingizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.Madaktari wamesimamisha shughuli zote na wanajitahidi kuokoa maisha yake.”
“Unaonaje hali yake? Akauliza Margreth
“Margreth siwezi kusema chochote kwa sasa”
“sawa baba,nakuja sasa hivi huko hospitali” akasema Margreth
“Maggie mama yako anaendeleaje?
“Mama hali yake naye si nzuri hata kidogo.Amezinduka na kuzirai tena.Dokta Salome Yule jirani yetu yuko hapa anaendelea kumuhudumia.” Akasema Margreth.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu na kukata simu
“Whats happening to my family? Ee Mungu naomba unipe nguvu ya kuweza kuyakabili matatizo haya makubwa yanayoikabili familia yangu kwa sasa.Naomba umsaidie mwanangu Happy aweze kupona” Mzee Kibaho alikuwa anaomba kimoyo moyo.Hakuweza kutulia sehemu moja.Alikuwa ni kama mtu aliyechanganyikiwa.
Margreth aliwasili Brahmaputra hospital na moja kwa moja akaelekea mahala alikokuwa baba yake.Macho yalikuwa mekundu kwa kulia
“baba kuna taarifa yoyote tayari umepata kuhusiana na Happy? akauliza Margreth
“Hakuna taarifa yoyote mpaka hivi sasa.Bado madaktari wanaendelea kumshughulikia.” Akasema mzee Kibaho.Jibu lile likazidi kumtoa machozi Margreth.Baba yake akamsogelea na kumkumbatia
“Please Margreth be strong.We need to be strong for Happy” akasema mzee Kibaho huku naye sauti yake ikionyesha kutetemeka
“Dady why could Happy do such a thing to us? Kwa nini aamue kunywa sumu? Akasema Margreth huku akilia
“I don’t know Maggie,I don’t know”
“Inauma sana baba.Sijawahi kuumia kama nilivyoumia leo.Hapa nilipo ninahisi moyo wangu unakatwa vipande vipande.Baba ninampenda sana Happy na sijui nitafanya nini kama hataweza kupona.Sijui kama nitaweza kuishi bila yeye” Margreth akaendelea kulia
“Tunatakiwa tujikite katika maombi tumuombee.Mungu atasikia vilio vyetu na atamponya Happy.I know Happy is strong and she’s going to fight this .She’ll fight for us and for all those who love her.” Akasema mzee Kibaho huku naye macho yake yakiwa na machozi.Margreth akatoa kijikaratasi toka katika mkoba wake na kumpatia baba yake
“Kikaratasi hiki kimekutwa chumbani kwa Happy.Ni ujumbe aliouacha”akasema Margreth.Mzee Kibaho akakunjua kikaratasi kile na kuanza kukisoma
“wakati mnausoma waraka huu tayari nitakuwa nimekwisha ondokewa na uhai.Nimechukua maamuzi haya magumu kutokana na kuchoshwa na aina ya maisha ninayoishi sasa.Mambo mengi yamenitokea ndani ya kipindi kifupi sana na nimeyavumilia yote lakini kwa hili lililotokea leo limenifadhaisha mno .Kwa ufupi tu ni kwamba jana nilitekwa na watu nisiowafahamu wakanipeleka mahala na wakanilazimisha kuyafanya haya mliyoyaona katika magazeti,kwa ajili ya kuokoa uhai wa Patrick.Sitaki kuliongeala sana suala hili lakini naomba mnifikishie ujumbe kwa Patrick kwamba nimekufa na yeye akiwa ni mwanaume pekee ninayempenda na sintaacha kumpenda hata huko niendako.Nilikubali kufanya haya kwa ajili ya kumuokoa yeye asiuawe.Nawapenda wote na ninawaomba mnisamehe kwa jambo hili ambalo najua litawaumiza sana lakini sina namna nyingine ya kuniondoa katika aibu hii kubwa zaidi ya kujitoa uhai…Kwa herini nyote”
Mzee Kibaho alishindwa kuyazuia machozi kumtoka baada ya kumaliza kuusoma ujumbe ule wa Happy
“Ee Mungu najua unaweza na haushindwi na lolote,nakuomba umponye binti yangu Happy.Mimi na familia yangu bado tunamuhitaji sana.Ni wewe tu ambaye unaweza kumuokoa toka kifoni kwa sasa.Naomba usikilize maombi ya familia yangu na Happy aweze kupona” Mzee Kibaho akaomba kimya kimya huku akijifuta machozi kwa kitambaa
Taarifa za Happy kutaka kukatisha uhai wake kwa kunywa sumu zilianza kusambaa kwa kasi baina ya ndugu na marafiki wa karibu wa familia.Wengi walianza kufika pale hospitali ili kujua kilichokuwa kinaendelea.
“Nilijua tu lazima kuna sababu iliyomfanya Happy afanye kitendo kile.Sikuamini kabisa kama Happy ambaye nimemlea na kumkuza katika maadili anaweza akatenda kitendo kama hiki cha kujidhalilisha kwa hiari yake.Ni nani huyo ambaye amemfanyia mwanangu unyama na udhalilishaji huu mkubwa? Huu ni udhalilishaji uliovuka mipaka.Happy ameshindwa kuvumilia na ndiyo maana akaamua kuchukua maamuzi haya aliyoyachukua.” Akawaza mzee Kibaho
“Aliyefanya jambo hili na kumdhalilisha mwanangu lazima atakuwa na lengo la kulipiza kisasi.Ninaanza kuhisi kwamba pengine jambo hili linahusiana na kifo cha Veronika kwa sababu kwa nini jambo hili litokee sasa? Lazima uchunguzi ufanyike na wale wote waliohusika na udhalilishaji huu walipe uovu wao.Lazima watu hawa wapatikane kwa namna yoyote ile.Nitahakikisha watu hawa wanakamatwa na hata kwa kuwatumia wapelelezi binafsi nitafanya hivyo.Niko tayari kutumia kiasi chochote cha fedha ili kuwasaka watu hawa waliomfanyia mwanangu jambo hili.” Akawaza mzee Kibaho.

* * * *

Mlio wa simu ukamstua Loniki toka usingizini.Akanyoosha mkono na kuichukua .Mpigaji alikuwa ni Linah
“Hallo Linah” akasema Loniki akiwa bado na usingizi
“Lonny bado umelala?
“Simu yako ndiyo iliyonistua.Jana niliporudi nilikunywa sana mvinyo na ndiyo ulionipelekea kulala namna hii” akasema Loniki
“Lonny umepata habari?
“Habari gani tena wakati wewe ndiyo mtu wa kwanza kuongea naye leo?
“Dah ! mambo tayari yameanza”
“mambo gani tena Linah?
“Leo jiji zima limeamshwa na habari moja tu.Habari ya Happy”
“Tayari habari yake imeshatoka? Akauliza Loniki na kuinuka akakaa
“Chezea Khumalo wewe .! akasema Linah huku akicheka.
“Khumalo amekwishamaliza kila kitu na hivi nikwambiavyo gazeti la Mitikisiko limekwisha na halipatikani tena mtaani.Katika mitandao ya kijami,taarifa inayozunguka hivi sasa ni hii ya Happy.Kila mtandao zimetapakaa picha na video ya Happy”
“Dah ! nashukuru sana kama kazi imekamilika.Nadhani hivi sasa kama Happy atakuwa amezipata taarifa hizi atakuwa katika maumivu makali sana kama niliyonayo mimi .Baada ya kummaliza Happy sasa tutahamia kwa Patrick” akasema Loniki.
“Lazima nihakikishe wale wote walioudhulumu uhai wa mdogo wangu wanalipa.They all must pay.This is just the beginning…” akasema Loniki
“Lonny nina imani ushauri huu alioutoa Khumalo ni wa busara sana kwani endapo Happy ataziona picha zile ni wazi ataumia mno .Ni picha zenye kudhalilisha sana.”
“Kweli kabisa Linah.Ninaanza kukubaliana na Khumalo kwamba unaweza usimuue mtu moja kwa moja lakini ukampa mateso makali ya moyo na akateseka katika maisha yake yote.Kwa mfano Happy,kwa sasa maisha yake hayatakuwa sawa tena.Tayari ameingia katika kashfa nzito na hii itamtesa katika maisha yake yote yaliyobaki.Pamoja na hayo Linah kuna jambo nataka kukuuliza”
“Uliza Lonny”
“Khumalo ni mtu wa namna gani? Anajishughulisha na nini? Na kile chumba alichowekwa Happy kina kazi gani hadi kikafungwa kamera za kisasa namna ile?
Linah akavuta pumzi ndefu halafu akasema
“Kwa kuwa wewe ni rafiki yangu nitakueleza lakini naomba mtu mwingine yeyote asifahamu.Khumalo anajishughulisha na biashara nyingi haramu ikiwamo ya madawa ya kulevya na hata shughuli kama hii uliyompa na wakati mwingine hata ujambazi wa silaha huwa anahusika pia.Kwa sasa ameamua kujikita zaidi katika biashara ya madawa ya kulevya ambayo ndiyo inayomuingizia fedha nyingi sana.Ukiacha biashara hiyo ya dawa za kulevya,hukitumia kile chumba alichowekwa Happy kwa ajili ya kurekodi filamu za ngono ambazo huziuza katika nchi za ulaya na Amerika na kujipatia fedha nyingi.Huwatafuta mabinti wazuri wa kiafrika na kuwalipa pesa nyingi halafu huwarekodi wakifanya ngono.Hii ndiyo kazi ya chumba kile.Lonny tutaongea zaidi baadae kwa sasa kuna mahala ninawahi” akasema Linah
“Ok Linah.Nitakuja ofisini kwako baadae.Ahsante kwa taarifa” akasema Lonny na kukata simu
“Ouh gosh !!Sasa moyo wangu unaanza kupata amani.I cant imagine how painfull Happy is right now.Picha ndo kwanza linaanza.Nitahakikisha wale wote waliohusika kusababisha kifo cha Vero wanalipa.Japokuwa ni gharama kubwa lakini nitajitahidi kufanya kila niwezavyo hadi nihakikishe nimemilipia kisasi mdogo wangu.” Akawaza Loniki huku akitoka mle chumbani

* * * *

Akiwa bado katika mapumziko huku akiendelea na shughuli zake za usafi asubuhi hii,Sarah hakuwa na habari juu ya kilichokuwa kinaendelea hadi pale jirani yake alipoingia akiwa na gazeti mkononi na kumstua.
“Shoga yangu huyu si miss Tanzania aliyevunja uchumba wa Vero? Akasema shoga yake Sarah huku akimpa Sarah lile gazeti.Sarah akafuta maji mkononi na kulichukua gazeti lile
“Ouh My God ..!!! “ akasema Sarah kwa mshangao.Taarifa ile ilimstua mno.Mikono yake ilikuwa inamtetemeka.
“Hakika malipo ni hapa hapa duniani.Amemzuia mwenzake asiolewe halafu kumbe huu ndio uchafu anaoufanya.Dah ! ameumbuka sana” akasema Yule shoga yake Sarah
“Hapana..!!..Hii si sahihi.Sidhani kama Happy anaweza akafanya kitendo kama hiki.Lazima hapa kuna namna iliyofanyika ili kumzalilisha .Lazima kuna mkono wa mtu hapa na kama ndiyo hivyo mtu huyo si mwingine atakuwa ni Loniki.Ni yeye peke mwenye chuki na Happy na aliweka dhamira ya kulipiza kisasi na ninadhani hii ni moja ya mipango yake.” Akawaza Sarah.
“Mbona uko kimya Sarah? Akauliza Yule shoga yake
“Nimestushwa sana na taarifa hii.” Akasema Sarah na kuingia ndani akachukua funguo za gari lake na kuondoka kwa kasi
“Nina hakika mkubwa Loniki anahusika kwa kiasi kikubwa na jambo hili la udhalilishaji.Lazima leo hii niufahamu ukweli.Kwa nini anataka kuendeleza uhasama usiokuwa na faida yoyote kwetu? Hapana siwezi kukubali jambo hili liendelee” akawaza Linah
“Ninahisi hata zile fedha ambazo mama aliniomba jana na kisha akampatia Lonny,alikuwa anazihitaji kwa ajili ya kutekeleza mipango yake hii miovu.Ninahisi hata mama naye atakuwa anahusika kwa namna fulani na jambo hili.Kuna kitu atakuwa anafahamu kuhusiana na mipango ya Lonny ya kulipiza kisasi.Kama ni kweli Lonny atakuwa amehusika katika kumdhalilisha Happy namna hii ,kamwe sintaweza kumsamehe .” akawaza Sarah
Mama yake sarah alikuwa amekaa nje ya nyumba yake na pembeni yake kulikuwa na meza ndogo iliyokuwa na chupa kubwa ya chai.Alistuka alipomuona Sarah akiingia pale ndani akiwa na uso uliojaa hasira
“Mama shikamoo” akasema Sarah
“Marahaba Sarah.Mbona hivyo? Kwema huko utokako?
“Kwema mama” akajibu Sarah halafu akalitoa gazeti lile la mitikisiko na kumpatia mama yake
“mama hebu niambie unafahamu chochote kuhusiana na jambo hili?
Mama yake akalichukua gazeti lile akalitazama na kustuka sana
“Ouh Mungu wangu..!!
“Hii ni kashfa kubwa sana”
“kweli mama ni kashfa kubwa mno.Nina hakika Loniki anahusika na jambo hili” akasema Sarah
“Loniki .!! mama yake akashangaa
“Ndiyo mama .”akasema Sarah
“Hapana Sarah.Loniki hawezi kuhusika na jambo kama hili”
“Mama humjui vizuri Loniki.Nina hakika lazima atakuwa anahusika na jambo hili.Aliapa kwamba atalipiza kisasi kwa Happy na wale wote waliohusika na kifo cha Vero.”
“Hapana Sarah.Sikubaliani nawe kwa hilo .Ni kweli Lonny ameumizwa sana na kifo cha vero lakini sidhani kama atakuwa anahusika kwa namna yoyote na jambo hili.Hii ni tabia ya Happy mwenyewe .Amemdhulumu mwanangu na haya ndiyo yanayomkuta sasa.”
“mama pesa ulizoniomba jana zilikuwa za kazi gani?
“Sarah naomba usitake kuyafahamu mambo yangu binafsi.Kama umeifuata pesa yako nitakurejeshea baadae kama nilivyokwambia” akasema mama yake kwa ukali
“mama sijaja hapa kufuata fedha.Nimekuja kutak…………….” Sarah akastuka baada ya Loniki kutokea ghafla
“Mbona kuna mabishano hapa? Akauliza Loniki huku akiangaliana na Sarah kwa macho makali
“Niambie uhusiki katika jambo hili ?” akasema Sarah huku akimpa Loniki gazeti ambaye alilichukua akalipitia kisha akaangua kicheko kikubwa.
“Haya ndiyo malipo ya udhalimu wake.Yeye na yule mshenzi wake Patrick walimdhulumu Vero uhai wake.Ona sasa alivyoumbuliwa na magazeti..” Akasema Loniki huku akicheka.Sarah akamtazama kwa hasira
“Mbona unanitazama hivyo Sarah? Hufurahi kwa kilichompata mtu aliyemuua mdogo wako?
“Kwa nini nifurahi? Happy si adui yangu na wala sintajenga uadui naye hata mara moja.Hata kama alihusika na kifo cha vero ,lazima niuheshimu utu wake.Kitendo cha kumdhalilisha namna hii hakivumiliki hata kidogo.”
“ Nilijua tu.Huna uchungu wowote kwa kifo cha Vero na ndiyo maana kila mara umekuwa upande wa Patrick na Happy.naomba nikufahamishe kwamba Happy anastahili kudhalilika namna hii.Anastahili kuumia kama tulivyoumia sisi kwa kufiwa na mdogo wetu.Huu ni mwanzo tu na bado ataumia sana.Mengi bado yatamkuta yeye na huyo shetani mwenzake Patrick”
Sarah alishindwa kumvumilia dada yake akamsogelea karibu
“Loniki wewe ni ndugu yangu wa damu lakini ninakuonya kwamba nitafanya uchunguzi wangu na endapo nitagundua kwamba unahusika kwa namna yoyote ile na jambo hili .I swear in heaven and earth I will never forgive you.”
“Utanifanya nini? Akauliza Loniki kwa ukali
“Utafahamu wakati utakapofika.”
“Go to hell sarah.Tena nakuomba uuchunge sana mdomo wako usije ukakuponza.Mimi si mtu wa kunyooshewa kidole kama unavyofanya.Kama ni mapambano niko tayari kupambana nawe na siogopi hata kama wewe ni ndugu yangu.Ninaweza nikakufanyia kitu kibaya sana na usiamini Sarah.”
Ilimlazimu mama yao kuingilia kati na kuwaamua wanae wale ambao walikuwa wanatoleana maneno makali.Sarah hakutaka tena kukaa pale nyumbani akapanda gari na kuondoka zake kwa hasira

* * * *

Savanna hakuwa mpenzi sana wa kusoma magazeti.Hii ilitokana na kuwa na kazi nyingi kiasi cha kukosa muda wa kupitia habari magazetini.Akiwa ofisini kwake akikamilisha baadhi ya kazi zake za kila siku asubuhi kabla ya kuelekea gereza la Uwangwa kuonana na Patrick,mara mmoja wa watumishi wa ofisi yake akaingia akiwa na gazeti mkononi.
“Savanna ,najua hupendi kusoma magazeti lakini naomba uchukue dakika chache upitie gazeti hili” akasema Edson mmoja wa mawakili wanaomtetea Patrick
“Edson toka lini umeniona nikipata muda wa kusoma magazeti? Ninataka kuelekea gerezani kuonanana na Patrick halafu nije niendelee na shughuli zangu nyingine” akasema Savanna
“Naomba usome Savanna.” Akasisitiza Edson na kuliweka gazeti lile mezani.Savanna akavutiwa na kichwa cha habari akalichukua ili alisome na ghafla akalitupa mezani
“Ouh My Gosh !!!... akasema Savanna kwa mstuko
“Bado siamini.Happy anaweza akafanya uchafu wa namna hii kweli? Happy huyu ninayemfahamu mimi? No..!! thats not true..!!!” akasema Savanna
“Ni kweli Savanna.Ukiacha picha hizi kuna video yake pia ambayo imesambaa mitandaoni.” Akasema Edson huku akiisogelea kompyuta ya Savanna akaifungua video ile ya Happy .Savanna akaitazama video ile na kujikuta mdomo wazi.
“Ouh gosh !! ..Ni vigumu kuamini.Happy kweli anaweza akafanya mambo ya aibu namna hii? Akasema Savanna na kujikuta akiishiwa nguvu miguuni,akakaa kitini.
“Usishangae Savanna.Siku hizi umezuka mtindo wa mabinti hasa hawa maarufu kujirekodi wakifanya ngono au kupiga picha za utupu kisha huzihifadhi kwa ajili ya kumbu kumbu zao wenyewe lakini ikitokea zikashindwa kuhifadhiwa vizuri na zikaingia katika mikono ya watu wabaya ,huziuza kwa waandishi wa habari kwa fedha nyingi ambao hutengeneza mamilioni ya fedha katika magazeti yao kwa kuichapisha habari hiyo” akasema Edson.Savanna akainama akafikiri halafu akachukua simu yake na kumpigia Margreth.
“Hallow “ akasema Margreth baada ya kupokea simu.Savanna akastushwa kidogo na sauti ya Margreth
“Margreth,sauti yako inaonyesha kama unalia.Unaumwa? akauliza Savanna .Margreth akashindwa kukizuia kilio chake akalia kwa nguvu
“Margreth nini kimetokea? Please tell me”
“Its…..it’s….” Margregth akashindwa kuongea akaangua kilio tena
‘Margreth nini kimetokea? Tafadhali naomba unieleze”
“Its Happy….!!
“Happy kafanya nini?
“Amekunywa sumu” Margreth akajibu halafu kikapita kimya cha sekunde kadhaa.Savanna akabaki mdomo wazi akashindwa aseme nini.Akameza fundo la mate na kusema
“Margreth tafadhali naomba uniambie ukweli”
“Ni kweli Savanna.Happy amekunywa sumu “
“So how’s She? Where ae you now?
“Niko hapa Brahmaputra hospital.She’s in critical condition fighting for her life “
“Ouh gosh ! ,nakuja sasa hivi” akasema Savanna na kukata simu kisha akachukua mkoba wake na kutoka kwa kasi hadi katika gari lake na kuondoka kuelekea hospitali.
“haya mambo mbona yanazidi kuchanganya? Jana nimepigiwa simu Happy haonekani lakini leo hii amekunywa sumu.Kitu gani kinaendelea hapa? Akawaza Savanna akiwa katika mwendo mkali kueleka hospitali
“Masikini Patrick,sipati picha atakuwa katika hali gani mara atakapozipata taarifa hizi.Sifahamu atachukua maamuzi gani lakini nafahamu lazima ataumia sana.” Akawaza Savanna
Baada ya kuwasili Brahmaputra hospital Savanna akakutana na familia ya Happy
“Shikamoo baba”
“Marahaba Savanna hujambo?
“Sijambo baba. Poleni sana” akasema Savanna halafu akamuomba mzee Kibaho wakaongee pembeni
“Nini kimetokea ? Happy anaendeleaje? Akauliza Savanna.Mzee Kibaho akakohoa kidogo halafu akasema
“Unakumbuka nilikupigia simu jana usiku nikitaka kufahamu kama unaweza ukafahamu lolote kuhusu mahala aliko Happy kwani hadi wakati ule ninakupigia hakuwa amerejea na hata simu yake haikuwa inapatikana kitu ambacho si kawaida yake.” Akasema mzee Kibaho
“Nakumbuka baba.Happy nilikutana naye jana asubuhi gerezani akiwa na Patrick.Nilipoingia nikiwa nimeongozana na familia ya Patrick yeye akaondoka na hatukupata muda wa kuongea.Nini kilitokea? Alikuwa wapi? Akauliza Savanna
“Mida ya kama saa nane hivi za usiku nilisikia muungurumo wa gari nje ya nyuma.Nilipotoka nje ya nyumba nilikuta gari la Happy na yeye akiwa ndani yake lakini akiwa hoi hajitambui.Hatukujua nini kilimpata kwa sababu alionekana ni kama mtu aliyelewa.Tulimuita dokta wa familia akaja mara moja na kumpatia huduma na alipopata nafuu akatuomba tumuache akapumzike.Hakutueleza alikuwa wapi na wala nini kilimpata.Asubuhi ya leo nilisikia mtu akilia sebuleni nikaenda kutazama nini kimetokea nikamkuta mke wangu akiwa amezirai.Wakati tukimpatia huduma ili azinduke akatokea Happy na kuliokota gazeti lililokuwa limeanguka chini.Ghafla akalitupa na kuelekea chumbani kwake.Nililitazama gazeti lile nikastuka sana.Nilimfuata Happy chumbani kwake lakini mlango ulikuwa umefungwa,ikanilazimu kuchukua ufunguo wa akiba nikaufungua mlango na kumkuta Happy akiwa hana fahamu na povu jingi likimtoka mdomoni.Alikunywa sumu ya kuulia panya.Nimemkimbiza hapa hospitali na toka nilipomfikisha hapa madaktari wanaendelea kumshughulikia.Shughuli zote hapa hospitali zimesimama kwa muda madaktari wote wanaendelea kumuhudumia Happy.Vile vile Happy aliacha ujumbe huu” mzee Kibaho akampatia Savanna ujumbe ule aliouacha Happy.Savanna akaupitia ujumbe ule na kisha akatoa kitambaa mfukoni na kuyafuta machozi
“Nilijua tu ,Happy hawezi kufanya jambo kama lile kwa hiari yake mwenyewe.Nilijua tu lazima jambo hili lina mkono wa mtu.Ni nani huyo ambaye anaweza kuwa amefanya unyama wa namna hii? Akasema Savanna
“Hakuna ajuaye ni nani muhusika wa jambo hili.Anayefahamu ni Happy pekee.Tuombe Mungu apone na atufahamishe ni nani hawa waliomfanyia kitendo hiki.Lazima wafikishwe katika mkono wa sheria“ akasema mzee Kibaho
“Ni kweli baba watu hawa waliohusika na udhalilishaji huu lazima walipe uovu wao.lazima wafikishwe katika vyombo vya sheria.” Akasema Savanna halafu kikapita kimya kifupi
“Savanna wewe ni wakili”
“Ndiyo baba”
“Naomba ushauri wako wa kisheria kuhusu kitendo hiki cha Happy.Hiki kitendo alichokifanya Happy cha kutaka kujiua ni kosa kisheria?
“Ni kweli baba,hiki ni kitendo cha kijinai.Kwa mujibu wa sheria ya kanuni za adhabu sura ya ishirini na mbili kifungu cha 217 kinachosema mtu yeyote anayejaribu kujiua ana hatia ya kosa.Iwapo suala hili litafuatiliwa na vyombo husika Happy anaweza kukabiliwa na adhabu
“Ouh My Gosh ..!!! what am I going to do ? akasema kwa masikitiko mzee Kibaho.Savanna akamtazama mzee Yule kisha akasema
“Baba kuna jambo ambalo tunatakiwa kulifanya kwa sasa”
“Jambo gani hilo savan?
“Kwanza nataka kufahamu kama suala hili limekwisha ripotiwa katika vyombo vya usalama.”
“Hapana Savanna.Suala hili halijaripotiwa sehemu yoyote ile na tunaofahamu ni sisi familia yake pamoja na ndugu wachache pamoja na majirani”
“Vizuri sana.Tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kulifanya suala hili kuwa siri kubwa na kuhakikisha hakuna mwandishi wa habari anayezipata taarifa hizi.Ongea na uongozi wa hospitali hii ili hata kama ikitokea watahojiwa na vyombo vya habari au usalama wasiweke wazi kwamba Happy alijaribu kujiua kwa kunywa sumu.Baada ya hapo itabidi tufanye jambo la haraka sana kwa Happy”
“Jambo gani hilo? Akauliza mzee KIbaho
“Najua hautalipenda lakini hakuna jinsi ninabidi lifanyike tu”
“Niambie Savanna.Niko tayari kufanya lolote hivi sasa kwa ajili ya Happy” akasema mzee KIbaho.Savanna akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“I wapo Mungu atamsaidia akapona We have to take her away from here as quick as possible”
Mzee Kibaho akastuka kwa maneno yale ya Savanna

TUKUTANE SEHEMU IJAYO.......
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 48
MTRUNZI.PATRICK.CK
CONTACT:0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Jambo gani hilo? Akauliza mzee KIbaho
“Najua hautalipenda lakini hakuna jinsi ninabidi lifanyike tu”
“Niambie Savanna.Niko tayari kufanya lolote hivi sasa kwa ajili ya Happy” akasema mzee KIbaho.Savanna akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“I wapo Mungu atamsaidia akapona We have to take her away from here as quick as possible”
Mzee Kibaho akastuka kwa maneno yale ya Savanna

ENDELEA……………..

“Baba najua umestuka sana kwa maneno haya lakini naomba uniamini haya nikwambiayo kwamba endapo Mungu atamjalia Happy uzima,tunatakiwa kumuondoa Happy hapa nchini haraka sana”
“Kwa nini unashauri hivyo ? Akauliza mzee Kibaho
“Jambo hili lililotokea si jambo dogo kama unavyoliona na hadi hivi sasa tayari limemuathiri Happy kwa kiasi kikubwa.Taswira yake katika jamii imeharibiwa na habari hii ya leo.Kwa maana hiyo basi anatakiwa kupata sehemu tulivu yenye uangalizi makini ili aweze kupatiwa msaada wa kisaikolojia na akili yake iweze kutulia.Kuendelea kumweka hapa ni kumuongezea maumivu na kutaendelea kuhatarisha usalama wake.Vile vile kumuondoa hapa kutasaidia kumuepushia mashtaka ya kijinai.Najua hili si suala jepesi lakini inatubidi tushirikiane sote kwa faida ya Happy” akasema Savanna.Mzee Kibaho akavuta pumzi ndefu .Alionekana kama amechanganyikiwa
“I don’t know what I’m going to do” akaongea peke yake.Baada ya dakika mbili za tafakari akamgeukia Savanna
“Savanna mawazo yako naona yana msingi sana.Nina mdogo wangu anaishi Mtwara.Nadhani itakuwa vyema kama nitampeleka kule akakae kwa muda”
“Hapana baba.Mtwara bado ni Tanzania.Happy anatakiwa aende mahala ambako hakuna mtu anayemfahamu mahala ambako atapata msaada wa kisaikolojia na kumsaidia kurejea katika hali yake ya kawaida.Hapa nchini Happy ana jina kubwa na anafahamika kila kona”
“Savanna suala hili linahitaji muda wa kutosha kulifanyia maandalizi.Inabidi nikae na familia yangu baada ya kujua maendeleo ya Happy na kwa pamoja tujadili suala hili ndipo tufikie maamuzi “ akasema mzee Kibaho huku akionekana ni mwenye mawazo mengi sana
“Mzee wangu nakubaliana na wazo la kukaa na kufanya maamuzi kama familia .Pamoja na hilo naomba na mimi nitoe mchango wangu.Iwapo mwenyezi Mungu atamjalia Happy uzima na iwapo mtakubaliana na mawazo yangu basi ninapendekeza Happy asafirishwe kwenda Kigali Rwanda.Mimi nitagharamia gharama zote za safari.Nitakodisha ndege binafsi hadi Kigali.Pale Kigali nina rafiki yangu aitwaye Christine umuhiza ambaye ndiye atakayemuhudumia Happy kwa kipindi chote atakachokuwa pale.Vile vile ninafahamiana na mmiliki wa hoteli moja iitwayo Reonald Hotel.Ni hoteli mpya na kubwa pale Kigali yenye hadhi ya nyota tano.Nitafanya mpango ili Happy aweze kukaa hotelini hapo kwa muda wote atakaouhitaji akiwa katika chumba chenye hadhi ya rais.Christine atamtafutia daktari ambaye atamsaidia kumtibu na vile vile tutamtafutia daktari wa masuala ya kisaikolojia “ akasema Savanna.Mzee Kibaho aliyekuwa anamsikiliza kwa makini akakohoa kidogo na kusema
“Savanna mimi binafsi nimeumizwa sana na jambo hili na kwa mantiki hiyo basi niko tayari kufanya jambo lolote lile ambalo litakuwa na msaada kwa Happy.Sipingani hata kidogo na wazo lako la kumpeleka Happy nje ya nchi.Ninachotaka kufahamu ni iwapo Happy ataondoka hapa nchini kwa ajili ya kumsaidia kwanza kumuepusha na aibu hii na pili kumuepusha na mkono wa sheria kwa kosa la kujaribu kujiua, nini itakuwa hatima ya watu waliomtenda hivi? Sitakuwa na amani hadi nihakikishe kwamba watu waliomfanyia mwanangu kitendo hiki cha kinyama wamekamatwa ,wamefikishwa katika mkono wa sheria na wameadhibiwa kutokana na kitendo walichokifanya.Lakini ninajiuliza maswali mengi hilo litawezekana vipi wakati Happy akiwa nje ya nchi? Nataka jina la mwanangu lisafishwe .Nataka umma wa watanzania wafahamu nini kilitokea na kwamba mwanangu hawezi kufanya kitendo kama kile kwa ridhaa yake.” Akasema mzee Kibaho
“Baba hayo yote unayoyasema ni ya msingi sana lakini tukumbuke kwamba ni Happy pekee ambaye anawafahamu watu hao na ambaye anaweza akatusaidia kuwatambua watu hao na anaweza akafanya hivyo pale ambapo akili yake itakuwa imetulia .Mimi binafsi nakuahidi ushirikiano wangu wa dhati katika suala hili na mara tu watakapogundulika watu hawa nakuahidi kwamba kesi hiyo nitaisimamia mimi mwenyewe na kuhakikisha kwamba wanapata adhabu kali sana”
Kabla mzee Kibaho hajasema chochote,akatokea Margreth na kumtaarifu baba yake kwamba anahitajika na daktari.Kwa haraka wote watatu wakaongozana kuelekea katika ofisi ya daktari

“karibuni sana” akasema daktari mkuu wa hospitali hii ambaye ana asili ya India lakini anakifahamu vizuri sana Kiswahili
“Poleni sana kwa matatizo” akasema daktari.Wote watatu nyoyo zao zilikuwa zinawadunda wakisubiri taarifa ya daktari
“Jamani nimewaiteni hapa ili kuwapeni taarifa kuhusiana na maendeleo ya mgonjwa wenu.Kwa ujumla ni kwamba Happy alikuwa amekunywa dawa ya kuulia wadudu ambayo ni sumu katika mwili wa binadamu.Ninakushukuru sana mzee wangu kwa jitihada zako za kumfikisha mapema hapa hospitaloi kabla sumu ile haijasababisha madhara makubwa mwilini.Tulimpokea Happy akiwa katika hali mbaya na tumefanya kila jitihada ili kumuondoa katika hali ya hatari ya kupoteza maisha.Tunapaswa kumshukuru sana Mungu kwani tumefanikiwa katika hilo.Kwetu sisi tunaona ni kama muujiza kutokana na hali aliyokuwa nayo Happy.Tumefanikiwa kuiondoa sumu iliyoko mwilini mwake kwa kutumia mtambo wetu maalum ambao ni mpya kabisa wa kuondoa sumu ya aina yoyote mwilini.Kwa sasa ninaweza kutamka kwamba Happy hayuko tena katika ile hatari ya kupoteza maisha na endapo litatokea jambo kama hilo basi itakuwa ni kwa mapenzi ya Mungu lakini napenda kuwahakikishia kwamba tumemuondoa katika hatari hiyo.” Akasema daktari na wote watatu wakashusha pumzi .Mzee Kibaho akajifuta jasho lililokuwa linamtiririka kwa wingi
“Zoezi linaloendelea kwa sasa ni kuipitisha damu yake katika mtambo maalum wa kuchuja sumu ili kuweza kujiridhisha zaidi kwamba hakuna kiasi chochote cha sumu kitakachobaki mwilini mwake.Kwa hiyo nawasihi ndugu zangu,ondoeni wasi wasi mliokuwa nao.Happy yuko salama na anaendelea vizuri.Zoezi hili litakapomalizika tutamuondoa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kumpeleka katika sehemu ya uangalizi maalum ili kuangalia maendeleo yake.”
“Ouh Thanx God” akasema mzee Kibaho huku akiinua mikono yake juu kumshukuru Mungu
“Daktari zoezi hilo la uchujaji wa sumu litachukua muda gani? Akauliza Savanna
“Ni muda wa masaa manne”
“Mzee wangu nini hasa kilichopeleka binti mdogo kama huyu kutaka kukatisha uhai wake? Nini kimemsibu ili tuone namna ya kumpatia msaada wa kisaikolojia na asiweze kurudia tena kufanya kitendo cha hatari kama hiki? akauliza daktari.Mzee Kibaho akakohoa kidogo na kusema
“Happy ni binti yangu wa kwanza.Hivi karibuni alifanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania.Baada ya kulinyakua taji hilo ndipo matatizo yalipoanza.Yote haya yamesababishwa na mgogoro wa kimapenzi uliopekeka msichana aliyekuwa akizozana naye kufariki dunia.Leo asubuhi katika gazeti moja la udaku kumechanpishwa picha za Happy za faragha.Ni picha zenye kuumiza sana na zote hizi ni njama za wabaya wake za kutaka kumchafua.Jambo hilo ndilo lililopelekea aamue kujaribu kukatisha uhai wake kwa kunywa sumu.” Akasema mzee Kibaho
“Poleni sana.Hii inaonyesha ni jinsi gani dunia ilivyobadilika hivi sasa.watu wamekosa huruma na wako tayari kufanya jambo lolote lile kwa manufaa yao bila kupima athari zinazoweza kujitokeza.Poleni sana ,lakini kitu ninachoweza kuwaambia ni kwamba Happy anahitaji msaada wa kisaikolojia.Hapa tunao madaktari wazuri sana wa masuala haya ya akili.Tunacho kitengo hicho hapa cha kuasadia watu wenye matatizo kama ya Happy.Ninawashauri kwamba baadaya hali yake kuwa nzuri basi tuendelee kumpatia msaada wa kisaikolojia hapa hapa hospitalini kwetu” akasema daktari
“Nakubaliana nawe daktari kwani inaonyesha wazi kwamba binti yangu ameathirika kisaikolojia na anahitaji msaada .Lakini kuna jambo ninataka kukuomba.Kwa mujibu wa sheria ,kitendo hiki alichokifanya Happy ni kosa la kijinai kwa hiyo kuna uwezekano endapo vyombo vya kisheria vikazipata taarifa hizi vikamfungulia mashitaka,kwa hiyo tunakuomba daktari ,jambo hili libaki kuwa siri na asifahamu mtu mwingine yeyote yule awe ni mwandishi wa habari au afisa wa polisi.Unaweza ukaandika ugonjwa mwingine wowote lakini si sumu.Jambo la pili ambalo tumekusudia kulifanya kwa haraka ni kumuhamishi Happy nje ya nchi haraka iwezekanavyo.mahala ambako hakuna mtu yeyote anayemfahamu.Nadhani hii itakuwa ni njia nzuri sana ya kumsaidia kumuondoa katika mazingira haya na wakati huo huo tukiendelea kumpatia msaada wa kisaikolojia.” Akasema mzee Kibaho
“Kwanza kabisa kuhusiana na kutoa taarifa kuwa vyombo vya habari na vile vya usalama,msiwe na hofu.Nitawasaidia katika hilo.Pili kuhusiana na suala la kumpeleka Happy nje ya nchi ni suala zuri sana lakini nina wasi wasi kidogo.Happy anahitaji bado kuwa katika uangalizi wa madaktari.Kama ni kumuondoa hapa nchini basi itawabidi msubiri kidogo hadi hapo hali yake itakapoboreka kabisa.”
“Inaweza kuchukua muda gani daktari? Akauliza Savanna
“Inaweza kuchukua zaidi ya wiki moja”
“Daktari tunahitaji kumuondoa Happy nchini leo hii.”
“Kwa leo haitawezekana kumsafirisha Happy” akasema Daktari
“Daktari naomba ufanye kila linalowezekana ili tuweze kumuondoa Happy hapa nchini siku ya leo” akaendelea kusisitiza Savanna
Daktari akafikiri kidogo na kusema
“Kama mkihitaji hivyo basi ni lazima pawepo makubaliano maalum”
“makubaliano gani hayo? Akauliza Savanna
“Baada ya zoezi la kuchuja sumu kukamilika mgonjwa anatakiwa apumzike kabla ya zoezi lingine lolote kufanyika.Endapo mtahitaji kumsafirisha Happy kwa siku ya leo,itawalazimu kumsafirisha na mmoja wa madaktari wetu kitu ambacho kitawaongezea gharama zaidi kwa hiyo nawashauri mngesubiri hadi hapo Happy atakapokuwa amepata nafuu ndipo mumsafirishe”
“Daktari hilo ulilolisema si tatizo kwetu hata kidogo kwani tunatumia ndege ya kukodi.Tunaelekea jijini Kigali Rwanda.Usijali kuhusu gharama.Tutakulipa pesa zote zitakazotakiwa ikiwa ni pamoja na kumuhudumia daktari huyo hadi hapo Happy atakapopata nafuu.” Akasema Savanna
“Kama mko tayari kwa hilo mimi sina shida yoyote.Kwa sasa naombeni mnipe nafasi nikakutane na jopo la madkatari wangu ili kwa pamoja tuweze kushauriana namna bora ya kuweza kulifanikisha jambo hili” akasema daktari.
“Usijali daktari.Sisi pia ngoja tukajiandae kwa safari.Naomba hesabu ya gharama zote unitumie kwa kupitia namba hizi hapa” akasema Savanna huku akimpatia daktari kadi yake yenye namba za simu halafu wakatoka mle ofisini.
“Baba mpango huu wa kumpeleka Happy Kigali umetoka wapi? Mbona hakuna aliyekuwa anafahamu kama kuna mpango kama huu? Akauliza Margreth baada ya kutoka ofisini kwa daktari
“Margreth samahani kwa kulisikia jambo hili kabla ya kutaarifiwa.Ni kwamba Savanna alikuja na wazo hili la kutaka kumuhamisha Happy na kumpeleka nje ya nchi ili kumuweka mbali na mazingira haya.Endapo ataendelea kukaa hapa wakati tayari jina lake limekwisha chafuka ataendelea kuumia zaidi.Ni bora ikiwa atakwenda kukaa mbali na hapa,mhala ambako hafahamiki kabisa.Hii itamsaidia sana kumsahaulisha kilichotokea”
“Ni mpango mzuri baba lakini maandalizi yanakwendaje manake nimemsikia Savanna akisema kamba Happy atapelekwa Kigali.Imekuwa ghafla sana na nina wasi wasi kama kuna maandalizi yoyote yaliyofanyika”
“Margreth,usihofu chochote kuhusiana na jambo hilo.Pale Kigali kuna hoteli moja kubwa ya nyota tano ambayo mmiliki wake tunafahamiana vyema na ndipo Happy atakapofikia na kukaa yeye na watu atakaoambatana nao hadi hapo hali yake itakapokuwa nzuri.Kuhusu usafiri nitagharamia mimi ,nitakodisha ndege hadi Kigali “

* * * *

Saa tano na dakika ishirini za usiku familia ya Happy ikaruhusiwa kuingia katika chumba alichokuwa amelazwa Happy.Tayari alikwisha amka toka saa mbili za usiku lakini madaktari hawakuruhusu aonane na mtu yeyote hadi hapo atakapokuwa amerejewa na fahamu zake kamili
Mara tu alipoiona familia yake ikiingia mle chumbani wakiongozwa na baba yake mzee Kibaho Happy alishindwa kujizuia akaanza kulia.
“Ouh Happy mwanangu” akasema mama yake huku akiinama na kumkumbatia wote wawili wakilia.
“Mungu ahsante kwa kumponya mwanangu” akasema mama yake Happy. Happy akasalimiana na baba yake mzee Kibaho na halafu mdogo wake Margreth na ghafla akastuka baada ya kugonganisha macho na Savanna
“Pole sana Happy” akasema Savanna.Happy akashindwa ajibu nini,donge kubwa likamkaba kooni.Savanna alilitambua hilo akatoka nje ya kile chumba.
“what is she doing here? Baba kwa nini umemleta Savanna hapa? Akauliza Happy
“Usijali Happy,Savanna tuko naye kutwa nzima ya leo tukishughulikia suala hili.Amekuwa ni msaada mkubwa kwetu katika wakati huu mgumu tulionao.Ametupa ushirikiano mkubwa sana.” Akasema mzee Kibaho
“Dady I don’t want to see her here.That woman is a devil.She’s a monster” akasema Happy kwa hasira juku akiendelea kulia.
“Its ok Happy It’s ok.Nyamaza usiendelee kulia mwanangu” akasema mzee Kibaho huku akimfuta Happy machozi
“Dady why you saved me? Akauliza Happy
“Happy naomba usahau kilichotokea.Kitu pekee kwa sasa ni kumshukuru Mungu kwa kukuponya .Sisi kama familia ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba unakuwa salama.Tunakupenda sana na hakuna mtu yeyote anayeweza akakubali upoteze maisha” akasema mzee Kibaho halafu.Happy akainua mkono akafuta machozi.
“Baba ungeniacha nife.Nimechoka na maisha haya.I’m real tired with this kind of life.Nili……………….” kabla hajaendelea baba yake akamuwekea kidole mdomoni
“Shhhhhhhhh..!!!!..Happy usiseme hivyo.Sahau kilichotokea .Hii ni mitihani ya maisha na ambayo hatuna budi kuishinda.Happy tunakupenda sana zaidi ya unavyoweza kufikiri”
“Najua kwamba mnanipenda sana lakini kwa aibu hii niliyowapa najiona sistahili hata kuitwa mwanenu.Nime………………” Happy akashindwa kuendelea akaangua kilio
“Happy usilie mwanangu.Tunakupenda sana na siku zote tutakuwa pamoja nawe katika kila jambo.Tuko pamoja katika suala hili na ndiyo maana tumeamua kukuhamisha hapa nchini usiku huu na kukupeleka sehemu ambayo utaweza kupumzika na kusahau kilichotokea,sehemu ambayo hakuna mtu yeyote anayekufahamu”
“Mnataka kunipeleka wapi baba?
“Tumeamua kwanza uende ukapumzike Kigali Rwanda wakati tukiangalia sehemu nyingine ambayo itakufaa zaidi.Tayari kila kitu kimekwisha andaliwa kwa msaada mkubwa wa Savanna ambaye ndiye aliyefanikisha mipango yote ya safari ikiwa ni pamoja na kuandaa hoteli ambayo utafikia kule Kigali na hata kuwalipa madkatari wote watakaokuwa wakikuhudumia katika kipindi hiki chote utakachokuwa kIgali.Tumefikia uamuzi huu wa kukuondoa hapa nchini ili kukusaida usiweze kuumia zaidi kutokana na maneno ya watu na vyombo vya habari.Iwapo utaendelea kukaa hapa utakuwa ukiumia zaidi kila siku” akasema mzee Kibaho
“Please dady take me out of here right now” akasema Happy huku akitoa machozi.
“Usijali Happy.Kila kitu kimekwisha andaliwa na tuchosubiri ni taratibu za hapa hospitali .Lakini kabla hatujaondoka hapa kuna jambo ninataka kukuuliza” akasema mzee Kibaho halafu akamtazama mwanae na kusema
“Unawafahamu au kuwa na hisia ni nani aliyekufanyia hivi?
Happy akafumba macho kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“Its not important anymore dady.Just take me out of here”
“Happy waliofanya unyama huu wanatakiwa wafikishwe katika vyombo vya sheria.Huu ni ukatili mkubwa sana ambao hauvumiliki.Tafadhali tusaidie tuweze kuwafahamu watu hao.Mimi na Savanna tutashirikiana na kuhakikisha kwamba wale wote waliotenda hivi wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria”
“Dady not now.Please take out of here” Happy akaendelea kuushikilia msimamo wake.Mzee Kibaho akatoka ndani ya kile chumba akakutana na Savanna.
“Savanna naomba usimjali Happy.Twende tukashughulikie masuala ya hapa hospitali ili tuweze kuruhusiwa kuondoka.” Akasema mzee Kibaho
“Kitu gani kinaendelea baina yako na Happy? Akauliza mzee Kibaho wakati wakishuka ngazi
“Its something stupid.Tulipishana maneno.Kuna mtu ambaye alimpelekea Happy maneno ambayo yalimfanya akasirike na kuja juu na mimi nikashindwa kudhibiti hasira zangu na tukajikuta tukitamkiana maneno makali.” Akasema Savanna
“Ninaweza kufahamu ni jambo gani hilo lililosababisha wewe na Happy mtupiane maneno? Akauliza mzee Kibaho
“Si jambo la msingi sana na sioni sababu ya kukwambia.Ni mambo ya wanawake tu na tutayamaliza” akasema savanna
Hatimaye ruhusa ya Happy kuondoka ikatolewa na akapatiwa daktari mmoja ambaye angeongozana naye kuelekea Kigali Rwanda ambaye angeendelea kumuhudumia hadi hapo hali yake itakapokuwa nzuri.Wote waliingia katika gari moja na safari ya kuelekea uwanja wa ndege ikaanza.Walikuwa makini sana kuhakikisha kwamba hawafuatiliwi na mwandishi yeyote wa habari kwani suala hili lilikuwa ni siri kubwa ya familia.Safari ilikuwa ya kimya kimya na hakuna aliyekuwa anaongea ndani ya gari.Waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na ,mizigo ya Happy ikashushwa garini.Kilikuwa ni kipindi kigumu sana hasa kwa mama yake Happy.Alimkumbatia mwanae huku wote machozi yakiwatoka.
“Mom I’m going to miss you” akasema Happy
“Happy sina cha kusema zaidi ya kukuombea kwa Mungu akutangulie huko uendako.Uwe salama kila siku “ akasema mama yake Happy huku machozi yakimtoka
“Nitakuwa salama mama” akasema Happy halafu akamuacha mama yake na kumfuata Margreth.
“Be safe there and get well soon” akasema Margreth
Happy hakusema kitu ,macho yake yalikuwa yamefunikwa na machozi
“Its time to go Happy” akasema mzee Kibaho kwa sauti ndogo
“Baba Happy” akaita mama yake Happy.Mzee Kibaho akageuka
“Tafadhali hakikisha Happy anakuwa salama”
Mzee Kibaho hakujibu kitu zaidi ya kutingisha kichwa ishara ya kukubaliana na kile alichokisema mke wake halafu akamshika mkono Happy na kumuomgoza kuelekea ndani ya uwanja kwa ajili ya kukamilisha taratibu za hapo uwanjani kabla ya kuruhusiwa kuondoka

TUKUTANE SEHEMU IJAYO.....
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 49
MTUNZI : PATRICK.CK
CONTACT: 0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Its time to go Happy” akasema mzee Kibaho kwa sauti ndogo
“Baba Happy” akaita mama yake Happy.Mzee Kibaho akageuka
“Tafadhali hakikisha Happy anakuwa salama”
Mzee Kibaho hakujibu kitu zaidi ya kutingisha kichwa ishara ya kukubaliana na kile alichokisema mke wake halafu akamshika mkono Happy na kumuomgoza kuelekea ndani ya uwanja kwa ajili ya kukamilisha taratibu za hapo uwanjani kabla ya kuruhusiwa kuondoka

ENDELEA…………………..

Waliwaisli salama katika uwanja a ndege wa kimataifa wa Kigali.Christine Umuhiza alikuwepo uwanjani kuwapokea wageni wake na kisha wakaelekea moja kwa moja Reonaldo hotel,moja ya hoteli mpya na kubwa jijini Kigali
Tayari kila kitu kilikwisha andaliwa na Happy akapewa chumba chenye hadhi ya rais yaani presidential suit kama alivyokuwa ameahidi Savanna.Mzee Kibaho ambaye ambaye naye alikuwa ameambatana na mwanae naye alipewa chumba kizuri sana kwa ajili ya kupumzika kwa siku zote atakazokaa hapo Kigali,daktari aliyeambatana nao pia alipewa chumba cha hadhi ya juu kabisa.
“Happy,nilipendekeza ufikie katika hoteli hii kwa sababu ni nzuri na huduma zake ni nzuri na za kimataifa.Jitahidi kupumzika kwa kadiri utakavyoweza na kwa muda wowote utakaohitaji.Mmiliki wa hoteli hii ni rafiki yangu sana na anafahamu uwepo wako hapa na gharama zote ni juu yangu .Endapo kutakuwa na tatizo lolote wasiliana nami moja kwa moja.Christine atakusaidia kumpata daktari bingwa wa magonjwa ya akili ambaye atakuwa akifika hapa kila siku na atakusaidia kisaikolojia ili uweze kurejea katika hali yako ya kawaida.”Akasema Savanna halafu akamtazama Happy aliyekuwa amejilaza kitandani.
“Happy najua tulipisha kauli na kutoleana maneno makali.Tafadhali naomba tusahau yale yote yaliyopita na tuangalie mambo ya mbele.Binafsi nimeumizwa mno na jambo hili kama walivyoumia wale wote wanaokupenda na ndiyo maana nimejitolea kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu ili kuhakikisha unarudi katika hali yako ya kawaida na kwa pamoja tuhakikishe wale wote waliohusika na kitendo hiki wanatafutwa kwa gharama zozote na kufikishwa mbele ya sheria” akasema Savanna.Bado Happy alikuwa anamuangalia kwa macho makali yaliyojaa machozi
“Happy mimi naenda kupumzika nyumbani kwa Christine.Nitakuja kukuaga asubuhi kabla ya kurejea Dar es salaam” akasema Savanna baada ya kugundua kwamba Happy hakuwa tayari kuongea naye kwa usiku ule .Akaufungua mlango na kutoka mle chumbani

* * * *

Kumekucha Kigali,kijua tayari kimechomoza na shughuli mbali mbali za uzalishaji mali zilikuwa zinaendelea kama ilivyo ada.Saa mbili za asubuhi Chistine na Savanna wakawasili hotelini.Wa kwanza kuonana naye alikuwa ni mzee Kibaho ambaye alikwisha amka na kufanya mazoezi ya viungo katika ukumbi mkubwa wa mazoezi uliopo katika hoteli ile.
“Happy ameamkaje? Akauliza Savanna
“Nimeongea naye kwa simu asubuhi ya leo ,amesema anaendelea vizuri ,lakini kwa mujibu wa daktari ni kwamba itamchukua siku kadhaa kurejea katika hali yake ya kawaida” akajibu mzee Kibaho
“usijali baba.Nina hakika baada ya muda hali yake itakuwa nzuri na maisha yataendelea kama kawaida.” Akasema Savanna halafu akaenda kuonana na daktari aliyemuhakikishia kwamba hali ya Happy ilikuwa inaendelea vizuri.Baada ya hapo akaelekea katika chumba cha Happy akabonyeza kengele ya mlangoni.Dakika kama mbili zilipita bila majibu yoyote .Akaanza kuingiwa na wasi wasi.Akabonyeza tena kengele na baada ya kama dakika mbili tena akasikia kitasa cha mlango kikinyongwa na mlango ukafunguliwa.Akagonganisha macho na Happy ambaye bado yalikuwa yamemvimba kutokana na kulia sana.Happy hakusema kitu akarejea kitandani kwake akaketi.Savanna naye akaingia mle chumbai na kusimama pembeni ya meza kubwa ya chakula.
“Happy unaendeleaje? Akauliza Savanna lakini Happy hakumjibu kitu.
“Happy nafahamu hukupenda kuniona hapa.Nafahamu ndani ya moyo wako mimi ni mmoja wa wale watu unaowachukia sana hivi sasa.Unapaswa kunichukia hasa baada ya maneno yale makali tuliyotoleana.Sote tulitoleana maneno makali kutokana na hasira tulizokuwa nazo.Sina mengi sana ya kusema lakini naomba utambue kwamba nimeguswa sana na jambo hili na kama rafiki na mwanamke mwenzako,niko pamoja nawe katika wakati huu mgumu” akasema Savanna halafu akanyamza kidogo akamtazama Happy na kuendelea
“Happy nimekuja kukuaga.Muda mfupi ujao ninarejea Dare s salaam.Ningependa kuwa nawe hapa kwa muda mrefu zaidi lakini bado ninakabiliwa na majukumu mengine mengi.Mzee Kibaho na daktari ,wataendelea kufuatilia hali yako kwa karibu na watatufahamisha kila hatua na endapo kutakuwa na tatizo lolote basi tutasaidiana namna ya kulitatua.Kitu pekee ambacho nitaka kukushauri ni kwamba ,japokuwa ni vigumu sana lakini naomba ujaribu kusahau kilichotokea na uruhusu maisha yaendelee.Happy nakufahamu wewe ni mwanamke jasiri sana naomba tafadhali usikubali kushindwa katika hili.Usimpe nafasi mtu,au kikundi cha watu kukufanya ukate tamaa na ushindwe kutimiza ndoto zako.” Savanna akanyamaza na kumtazama Happy ambaye macho yake yalikuwa yemejaa machozi
“Hapa hotelini utaishi kwa muda wowote utakaoutaka,utapatiwa kitu chochote utakachohitaji.Endapo kutakuwa na tatizo lolote naomba unipigie simu yangu moja kwa moja.Mwisho naomba ufahamu kwamba kuna maelfu ya watu wanaokupenda na mashabiki wako wanaokusubiri upone na siku moja urejee tena Tanzania.Get well soon Happy “ akasema Savanna huku naye akilengwa na machozi halafu akageuka na kuanza kupiga hatua kuondoka
“Savanna subiri kidogo” akasema Happy.Savanna ambaye alikuwa ameukaribia mlango akasimama na kugeuka.Happy akainuka pale kitandani akamfuata
“Savanna naomba unisamehe kwa yale yote niliyokutenda.Ni kweli siku ile tulipopishana maneno nilikuwa na hasira sana lakini naomba unisamehe.Kabla hujaondoka,naomba toka ndani ya moyo wangu niseme kwamba ahsante sana kwa yote.Wema huu ulionitendea ni mkubwa na sina hakika kama nitaweza kuurejesha.Pamoja na shukrani zangu kuna jambo moja nataka kukuweka wazi”akasema Happy akamtazama Savanna kwa makini halafu akasema
“Savanna sintarejea tena Tanzania.I’ve left Tanzania for good.Its my country but I hate Tanzania so much.Kwa sababu hiyo basi naomba nimkabidhi Patrick katika mikono yako.Ninamuacha mikononi mwako kwa sababu ninaamini unampenda na utahakikisha anakuwa mwenye furaha siku zote katika maisha yake.Please take good care of him .He’s all yours now.Kokote nitakakokuwa nitajua kwamba Patrick ana furaha kwa sababu yuko katika mikono salama.” Akasema Happy huku machozi yakimtoka
“Tafadhali Happy usiseme maneno hayo” akasema Savanna kwa mshangao
“Savanna naomba ufanye kama nilivyokuomba.Huu ni uamuzi wangu na nimeamua kuchukua maamuzi haya magumu kutokana na hali halisi ilivyo na ukweli ulio wazi kwamba mimi na Patrick hatutaweza kuwa pamoja japokuwa tunapendana kwa mioyo yetu yote.Pamoja na hayo naomba unihakikishie jambo moja.”
“Jambo gani Happy?
“Naomba unihakikishie kwamba Patrick atashinda kesi na atakuwa huru na kwamba hautamwambia mahala niliko.Can you promise me that?
Savanna akamwangalia Happy usoni na kusema
“Patrick will be free.I give you my word” akasema Savanna
“Thank you Savanna.Thank you so much.You can go now” akasema Happy huku uso wake ukiwa umeloa machozi
“Thank you so much Happy.” Akasema Savanna huku naye machozi yakimtoka na kumkumbatia Happy halafu akatoka mle chumbani

* * * *

“The war is over now.Patrick is mine and he’s mine alone.” Akawaza Savanna akiwa katika ndege akirejea Dar es salaam.Uso wake ulikuwa umepambwa kwa tabasamu pana
“Sijafurahia kilichomtokea Happy japokuwa sote tulikuwa katika vita ya kumgombania Patrick lakini kufa kufaana.Namuonea huruma sana Happy japokuwa kwa upande wa pili nimejawa na furaha kwa yeye kuamua kuachana na Patrick.” Akawaza Savanna
“Lakini ni nani hawa waliomfanya udhalilishaji huu mkubwa? Ninaanza kujenga picha kwamba waliofanya kitendo hiki walikuwa na lengo moja tu la kumdhalilisha Happy.Nashawishika kuamini kwamba yeyote aliyefanya jambo kama hili alikuwa na lengo la kulipiza kisasi.Ninalazimika kuamini pia kwamba lazima tukio hili litakua na uhusiano fulani na kifo cha vero.Nasikitika kwamba hatutaweza kuwapata watu hawa kwa sababu Happy hayupo tena Tanzania na hana mpango wa kurejea tena wala wa kuwatafuta watu hawa. ”
Savanna alikuwa na furaha sana kwani aliamini ile ndoto yake ya kuwa na Patrick sasa inakwenda kutimia

*****************

Saa tatu za asubuhi gari moja dogo jeupe likaingia katika gereza la Uwangwa.Kijana mmoja mfupi mnene aliyevaa suti ya kijivu iliyomkaa vyema akashuka toka ndani ya gari lile na kuelekea sehemu ya mapokezi ambako alijitambulisha kama mgeni wa Apolinary.Moja kwa moja akapelekwa katika ofisi ya Apolinary mmoja kati ya maafisa wa gereza hili
“karibu sana kijana” akasema Apolinary ,mzee mmoja mnene mweupe
“Ahsante sana mzee.” Akajibu Yule kijana huku akiketi kitini na bila kuchelewa akaitoa bahasha ya khaki toka mfukoni na kupatia mzee Apolinary ambaye aliifungua na kukutana na bunda kubwa la noti mpya kabisa nyekundu
“Sina haja ya kuhesabu,nadhani ni millioni tatu kamili.”
“Ndiyo mzee,ni tatu kamili”
“namuamini sana Khumalo.Ahadi zake huwa za kweli.” Akasema Apolinary huku akizifungia fedha zile katika kabati lake na kuchukua fimbo yake akamuomba Yule kijana amfuate.Apolinary alienda hadi katika ofisi moja inayohusiana na masuala ya mahabusu akaongea na askari mmoja aliyekuwamo mle ofisini kisha akainua simu akapiga na muda si mrefu wakatokea askari wawili ambao akaongea nao jambo fulani halafu wakaongozana na mzee Apolinary pamoja na yule kijana wake.Waliingia katika chumba kimoja kidogo kilichokuwa na viti viwili.
“Nickson, Patrick ataletwa hapa muda si mrefu na utaongea naye” akasema Apolinary halafu akawatuma wale askari wawili wakamlete Patrick.Baada ya kama dakika saba hivi Patrick akaletwa
“Patrick kuna mtu amekuja kukutembelea.” Akasema Apolinary halafu akawafanyia ishara askari wale watoke mle chumbani na kuwaacha Patrick na yule kijana Nickson
“Nickson una dakika kumi tu za kuongea na Patrick” akasema Apolinary naye akatoka nje
“Watatumia dakika kumi tu halafu mumrudishe Patrick mahabusu” Apolinary aliwaambia wale askari waliokuwa wamesimama nje ya kile chumba
“Patrick pole sana.Nadhani ni mara ya kwanza mimi na wewe tunaonana.Bila kupoteza muda naomba nijitambulishe “ akasema Nickson na kutulia kidogo halafu akaendelea
“Ninaitwa Nickson.Ni mfanyabiashara.Nimekuja hapa kukuletea taarifa ambazo si nzuri na nina imani hautazifurahia lakini kama mwanaume nakusihi ukaze moyo.” Akasema Nickson na kumfanya Patrick apatwe na wasi wasi
“Nickson sina hakika kama tumewahi kuonana mahali.Ni taarifa gani hizo ambazo si nzuri kwangu? Akauliza Patrick
“Patrick ninafahamu mahusiano yako na Happy Kibaho.Ninafahamu kwamba ulivunja mahusiano yako ya awali kwa ajili yake.Ninasikitika kukutaarifu kwamba pamoja na mapenzi yote uliyomuonyesha Happy lakini yeye ameshindwa kuwa mwaminifu kwako na hasa katika kipindi hiki ambacho uko gerezani” akasema Nickson na kumfanya Patrick azidi kuwa na wasi wasi
“Happy amefanya nini? Akauliza Patrick kwa wasi wasi.Nickson hakuongea kitu akaingiza mkono katika koti lake na kutoa bahasha akaisogeza karibu na Patrick
“Fungua uangalie” akasema Nickson.Patrick akaichukua bahasha ile na kuifungua.Ndani ya bahasha ile kulikuwa na picha akazitoa.Picha ya kwanza ikamstua na kuzifanya picha nyingine zote alizokuwa amezishika mkononi zianguke mezani.Akaitazama picha ile aliyokuwa ameishika mkononi.Mikono ilikuwa inamtetemeka huku kijasho kikianza kumchuruzika.Akaiweka picha ile chini na kuchukua picha nyingine akaiangalia.Macho yake yakaanza kutoa machozi.Akajikaza na kuanza kuzipitia picha zile moja baada ya nyingine.Kabla hajamaliza kuzitazama akamtazama Nickson kwa macho makali sana
“Nani amekutuma uniletee picha hizi? Akauliza Patrick huku machozi yakimtoka.Akainama tena akaziangalia picha zile.
“Ouh my gosh !! Happy !!!.Siamini .Siamini kama Happy anaweza akanifanyia hivi.” Akasema Patrick na kufuta machozi.Ghafla kwa nguvu akainuka ,akaisukuma ile meza na kumkaba Nickson
“Niambie nani amekutuma uniletee picha hizi?
Patashika kubwa likaibuka mle ndani na mara askari waliokuwa nje ya kile chumba wakaingia haraka na kumkamata Patrick kisha wakamuamuru Nickson aondoke haraka sana.Kwa haraka Nickson akazikusanya zile picha akaziweka mfukoni na kutoka mle chumbani huku Patrick akiwa ameshikiliwa na askari.Ghafla Patrick akamsukuma kwa nguvu askari aliyekuwa amemshikilia na kwa kasi ya aina yake akamvaa askari aliyekuwa amesimama pembeni ya mlango na kutaka kunyang’anya bunduki.Kuliibuka kizaazaa kikubwa .Patrick na Yule askari walikuwa wananyang’anyana silaha.Yule askari aliyekuwa amesukumwa na kuanguka chini akakiona kitendo kile na kuinuka haraka akamtandika teke kali la mbavuni na kumfanya Patrick aachie bunduki ile aliyokuwa akiing’ang’ania na kutoa yowe.Bila kujali maumivu aliyoyapata kwa teke lile akainuka tena kwa kasi na kutaka kumvamia askari tena yule mwenye silaha lakini askari Yule e alikiona kitendo kile na kwa nguvu akampiga na kitako cha bunduki akaanguka na kupoteza fahamu.Kwa kutumia simu ya upepo wakatoa taarifa kwa viongozi ambao walifika mara moja kushuhudia kilichotokea na kuamuru Patrick apelekwe katika hospitali ya gereza kwa matibabu wakati uchunguzi wa tukio lile ukiendelea.Patrick akatolewa mle chumbani na kukimbizwa katika hospitali ya gereza kwa ajili ya matibabu


* * * *

Savanna aliwasili salama jijini Dar es salaam,kutoka pale uwanjani alikodisha teksi iliyompeleka hadi nyumbani kwake.
“ Kitu cha kwanza ninachotakiwa kukifanya siku ya leo ni kwenda kuonana na Alois na kumuomba wasimueleze kitu chochote Patrick kuhusiana na tukio lile la Happy.Inatakiwa itafutwe namna nzuri ya kumfahamisha Patrick juu ya tukio hili kwani endapo tukikurupuka kumweleza tunaweza kusababisha mambo mengine.” Akawaza Savanna akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake
“Namuonea huruma sana Patrick.Matatizo aliyonayo ni makubwa sana.Amempoteza Vero,baba yake na sasa amejitumbukiza katika kesi kubwa ya mauaji na kabla haijajulikana hatima yake linaibuka tena suala hili la Happy.Ninatakiwa nifanye kila niwezalo ili kuhakikisha ninamtoa Patrick gerezani “akaendelea kuwaza Savanna
Alifika nyumbani kwake akaoga na kuvaa suruali nyeupe ya jeans na shati jekundu .Alipendeza vilivyo kama ilivyo kawaida yake.Kabla hajatoka akampigia simu Alois kaka yake Patrick na kumuomba waonane,kisha akaingia katika gari lake akaondoka .
“Nayaona maisha yangu kama yamejaa nuru na furaha hivi sasa na yote hii ni kwa sababu nina uhakika wa kuishi maisha yangu yote nikiwa na mwanaume nimpendaye kuliko wote duniani.” Akawaza Savanna akiwa njiani kuelekea nyumbani kwa wazazi wa Patrick kuonana na Alois kaka wa Patrick
Alipofika alipokelewa na Alois na baada ya maongezi machache akamkaribisha sebuleni
“Unaendeleaje Alois?
“Ninaendelea vizuri Savanna.Tumekwishaizoea hali hii.Nashukuru Mungu hata mama naye anaendelea vizuri hivi sasa” Akasema Alois
“Nashukuru kusikia hivyo”
“Vipi kuhusu wewe Savanna unaendeleaje? Kesi inakwendaje?
“Mimi ninaendelea vizuri sana Alois na kuhusu kesi hakuna haja ya kuwa na wasi wasi kila kitu kinakwenda vizuri .Nawaomba muondoe shaka kabisa kuhusu kesi hii kwani ni lazima tushinde.” Akasema Savanna na kumfanya Alois atabasamu
“Ahsante sana Savanna kwa kuzidi kutupa matumaini.Umekuwa mfariji wetu na tegemeo letu katika suala hili la Patrick.Umemsaidia sana hata mama kutokuwa na wasi wasi na mwanae.Nikupe siri moja mama anampenda sana Patrick.”akasema Alois halafu kikapita kimya kifupi
“karibu sana Savanna” akasema Alois
“Alois mimi si mkaaji sana nimepita hapa mara moja ili tujadili kwa pamoja jambo hili lililotokea.” Akasema Savanna
“Jambo gani Savanna? Hili la Patrick?
“Ni kuhusu Happy.Nadhani umeisikia kashfa iliyompata”
“Ndiyo.Alinipigia simu Andrew jana na kunifahamisha.Niliitazama video yake katika mtandao sikuamini kama ni kweli Happy ameweza kufanya kitendo cha aibu kama kile.Nimefadhaika sana kwa sababu yule msichana ndiye chanzo cha Patrick kusota gerezani hivi sasa.Ni aibu kubwa mno na hata mama nimemficha sijamweleza chochote” akasema Alois
“Nakubaliana nawe Alois.Kitendo kile ni cha aibu sana na hakivumiliki.Kikubwa kilichonileta hapa ni kukuomba kwamba Patrick asifahamishwe kwa sasa.Endapo akifahamu alichokifanya Happy itamsababishia matatizo makubwa sana kwani kchwa chake kwa sasa kimebeba mambo mengi ”
“Savanna bila hata kuomba lakini naomba nikuhakikishie kwamba si mimi wala mtu yeyote katika familia yetu angeweza kumweleza Patrick kitu chochote kuhusiana na uchafu uliofanywa na Happy.Ni kitendo cha aibu sana na kisichovumilika.Moyo wangu umeumia hasa nikimuangalia mdogo wangu anavyoteseka gerezani kwa ajili ya huyu huyu msichana”
“Ahsante sana Alois kwa busara hiyo.Basi ni hilo pekee lililonileta hapa.Naomba uniruhusu niondoke nikaendelee na majukumu mengine.” Akasema Savanna
“Nashukuru sana Savanna kwa kuja kututembelea bahati mbaya mama amelala alikuwa na hamu sana ya kukuona”
“Mpe salamu zangu.Nitakuwa nikija hapa mara kwa mara kumsalimu” akasema Savanna kisha akainuka na kuondoka.
“Kwa sasa ni safari ya moja kwa moja kueleka Uwangwa .kabla sijafanya chochote lazima niaonane kwanza na Patrick.Sijamtia machoni kwa siku nzima ya jana” akawaza Savanna

* * * *

Ilimchukua dakika arobaini kuwasili katika gereza la Uwangwa.Kijua kilikuwa kikali sana siku hii.Kisha shuka garini akaelekea moja kwa moja mapokezi kama ilivyo kawaida yake na pale alipewa taarifa kwamba akaonane na mkuu wa gereza.Alistushwa sana na taarifa ile.Alijaribu kudadisi ili kufahamu nini kilichotokea hadi ikamlazimu akaonane na mkuu wa gereza kabla ya kuonana na Patrick lakini hakuna aliyekuwa tayari kumweleza chochote.
Huku akiwa na uso uliojaa wasi wasi Savanna akatembea kwa kasi kuelekea katika ofisi ya mkuu wa gereza.Alijitambulisha kwa katibu muhtasi wa mkuu wa gereza ambaye alimpigia simu mkuu wake na kisha akamruhusu Savanna aingie ofisini.
“karibu Savanna” akasema mkuu wa gereza.
“Nashukuru sana mkuu” akasema Savanna.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa
“Mkuu nimekuja kuonana na mteja wangu lakini nimestushwa kidogo kwa kuambiwa kwamba unahitaji kuniona kabla ya kuonana na mteja wangu” akasema Savanna
“Ni kweli Savanna.Nilitoa maagizo hayo.Kuna jambo limetokea leo kuhusiana na mteja wako” akasema mkuu wa gereza na kumfanya Savanna astuke
“jambo gani limetokea tena?
“Leo asubuhi kuna mtu ambaye alikuja kuonana na Patrick.Kwa mujibu wa askari waliokuwepo eneo la tukio,mtu huyo alikuwa na bahasha yenye picha ambazo alimpa Patrick azitazame.Hatujui picha hizo ni za nani na kwa nini mtu huyo alimpa Patrick lakini inasemekana baada tu ya Patrick kuziona picha hizo alibadilika na kuwa kama mtu aliyechanganyikiwa.Alimkaba mtu Yule aliyempeleka zile picha na akazua tafrani kubwa.Askari ambao walikuwa nje waliingilia kati ugomvi huo na kumdhibiti Patrick lakini alifanya kitu cha ajabu sana kwani alimvamia askari na kutaka kumnyang’anya silaha.Hatuelewi alikusudia kufanya nini na ile bunduki lakini nina hakika angefanikiwa kuipata silaha ile angeleta maafa makubwa.Askari walifanikiwa kumdhibiti na kumsababishia jereha kidogo kichwani na hivi sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika zahanati ya gereza”
“Ouh my gosh !! akasema Savanna huku ameshika kichwa kwa mikono.
“Kuna taarifa zozote za maendeleo yake?
“Kwa taarifa nilizozipata toka kwa madaktari muda si mrefu ni kwamba Patrick anaendelea vizuri.”
“Ouh Mungu wangu ..!!” akasema Savanna.Suala lile lilikuwa limestua sana.
“Savanna suala hili la Patrick ni suala zito sana na endapo litafika katika vyombo vya sheria litakuwa na athari kubwa sana kwa Patrick na hata kwa uongozi wa gereza.Kwa heshima yako suala hili litaishia hapa hapa na halitaenda sehemu yoyote lakini hata hivyo inabidi tuchukue hatua za kuzuia jambo kama hili lisijitokeze tena.Tumeamua kudhibiti watu wanaokuja kumtembelea Patrick.Kuanzia hivi sasa watakaoruhusiwa kuonana naye ni wewe pamoja na familia yake pekee.Hakuna mtu mwingine yeyote atakayeruhusiwa kumuona.Hii ni kwa ajili ya usalama wa Patrick vile vile kwani hatujui katika watu wanaokuja kumtazama ni yupi atakuwa adui yake”
“Nashukuru sana mkuu wa msaada wako huu mkubwa.Nitaongea na Patrick na kumsihi asithubutu kufanya kitendo cha hatari namna hiyo tena.Ninaweza kuruhusiwa kuonana naye?
“Twende tuongozane na mimi nikaangalie maendeleo yake.” Akasema mkuu wa gereza huku akiinuka akatoka mle ofisini
“Nahisi mwili wote ni kama umekufa ganzi.Ni nani huyu aliyemletea Patrick picha? Najua ni lazima zitakuwa ni picha za Happy.Ninaanza kujenga hisia kwamba jambo hili si la mtu mmoja bali linahusisha kikundi cha watu na wana ajenda yao ya siri kufanya hivi na ajenda yao kubwa ni kuuharibu uhusiano wa Patrick na Happy.Kwa mujibu wa barua ile aliyoindika Happy ni kwamba alitekwa na kundi la watu waliomlazimisha kufanya ngono na kisha kumpiga picha za utupu na kuzisambaza.Kuna ulazima wa kuwafahamu watu hawa wenye roho za kikatili namna hii” akawaza Savanna wakati wakielekea katika zahanati ya gereza kumuangalia Patrick
Mkuu wa gereza na Savanna waliingia katika ofisi ya mganga mkuu wa gereza ambaye aliwapa taarifa za maendeleo ya Patrick na kisha kuwapeleka katika chumba alichokuwa amelazwa Patrick
“Tumemchoma sindano ya usingizi nadhani baada ya masaa mawili au matatu ataamka.” Akasema daktari.Patrick alikuwa amelala usingizi mzito sana pale kitandani na sehemu ya juu ya jicho lake alikuwa na jeraha.Mkono wake wa kushoto ulikuwa umefungwa pingu.Savanna akashindwa kuvumilia kumuona Patrick katika hali ile akaangusha machozi
“Tafadhali mkuu naombeni mumfungue hiyo pingu.Hatakwenda sehemu yoyote.Hawezi kukimbia”
“Hii pingu amefungwa kwa ajili ya usalama.Alipoamka mara ya kwanza alionekana ni kama mtu aliyechanganyikiwa.Alitaka kukimbia akazuiwa hivyo tumeona ni bora kama tukimfunga pingu ili asiweze kutoka hapa kitandani akasema daktari
“Savanna wewe unaweza kwenda kupumzika.Mteja wako yuko katika uangalizi makini .Endapo kutakuwa na tatizo lolote tutakutaarifu” akasema mkuu wa gereza.
“Ahsante sana mkuu ,lakini naomba niendelee kukaa hapa hadi hapo atakapoamka ili niweze kuongea naye hata maneno mawili na nimsihi atulie asifanye jambo lolote la hatari.tafadhali mkuu naomba uniruhusu kwa hilo” akaomba Savanna
Mkuu wa gereza akainama akafikiri kwa muda kisha akasema
“Sawa Savanna,kama unahitaji kujiridhisha zaidi na maendeleo ya mteja wako basi hakuna shaka.Kuna mgahawa wa gereza unaweza kwenda kukaa pale na pindi atakapoamka tutakutaarifu.” Akasema mkuu wa gereza halafu wakatoka .Savanna akakabidhiwa askari aliyempeleka hadi katika mgahawa wa maofisa wa gereza.
“Sintawataarifu familia yake kwa sasa hadi hapo nitakapohakikisha anaendelea vizuri.Nikiwaeleza sasa hivi kwamba mtoto wao amepatwa na matatizo tena ninaweza kuwasabishia matatizo mengine katika wakati huu mgumu walionao” akawaza Savanna

TUKUTANE SEHEMU IJAYO.......
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 50
MTUNZI😛ATRICK.CK
CONTACT:0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Mkuu wa gereza akainama akafikiri kwa muda kisha akasema
“Sawa Savanna,kama unahitaji kujiridhisha zaidi na maendeleo ya mteja wako basi hakuna shaka.Kuna mgahawa wa gereza unaweza kwenda kukaa pale na pindi atakapoamka tutakutaarifu.” Akasema mkuu wa gereza halafu wakatoka .Savanna akakabidhiwa askari aliyempeleka hadi katika mgahawa wa maofisa wa gereza.
“Sintawataarifu familia yake kwa sasa hadi hapo nitakapohakikisha anaendelea vizuri.Nikiwaeleza sasa hivi kwamba mtoto wao amepatwa na matatizo tena ninaweza kuwasabishia matatizo mengine katika wakati huu mgumu walionao” akawaza Savanna

ENDELEA……………….

Ni mtu mmoja tu aliyekuwa anasubiriwa atoke ndani ili safari ya kuelekea makaburini ianze.Siku hii ya leo familia ya Vero waliamua kwenda kulitembelea kaburi la Vero ambalo tayari lilikuwa limemalizwa kutengenezwa.Kazi iliyokuwa ikifanyika ilikuwa ni kuweka vigae pamoja na marembo mengine na kulifanya lipendeze mno
Familia yote ilikwisha kusanyika na aliyekuwa anasubiriwa ni mama yao.Wote walikuwa wamepanda katika gari moja.
“She’s taking too long” akasema Loniki
“Labda anasal…….” Shangazi yao akataka kusema kitu lakini kabla hajamaliza mtu waliyekuwa wanamsubiri akatokea na safari ikaanza
Kabla hawajafunga mlango simu ya Loniki ikaita.Akaitoa mfukoni na kutazama mpigaji alikuwa ni Linah
“Hallow Linah
“Lonny umeamkaje dear?
“Nimeamka salama Linah.”
“Uko wapi mida hii? Bado umelala?
“Hapana Linah.Niko na familia tunajiandaa kwenda kutembelea kaburi la Vero.Mafundi tayari wamemaliza matengenezo”
“Lonny kama ningekuwa na muda ningekuja kuungana nanyi lakini nimebanwa sana leo”
“usijali sana Linah.Vipi kuna habari gani mpya?
“Khumalo kanipigia simu sasa hivi na kunitaarifu kwamba tayari Patrick ameziona zile picha”
“Ouh gosh ..!! what happened? Akauliza Loniki kwa furaha huku akishuka garini ili aweze kuongea vizuri na Linah bila ya mtu kusikia maongezi yao
“kwa mujibu wa taarifa ya kijana aliyezipeleka picha hizo ni kwamba mara tu Patrick alipozitama alibadilika na kuwa kama mtu aliyepandwa na uchizi.Alimvamia kijana huyo na kutaka kufahamu aliyemtuma ampelekee picha hizo kwa bahati nzuri kulikuwa na askari karibu hivyo hakuweza kumdhuru.Baada ya askari kumshikilia Patrick asiendelee kuleta fujo ,alimrukia askari aliyekuwa na bunduki na kutaka kumnyang’anya silaha jambo lililowalazimu askari kumtembezea kipigo kikali sana.Hivi sasa nasikia hali yake ni mbaya na amelazwa katika hospitali ya gereza”
“Ouh gosh ! that’s great news to hear this morning.Sipati picha ingekuaje kama angefanikiwa kuinyakua hiyo bunduki.Nadhani lengo lake lilikuwa kujiua.Hahaha haaa I think the plan is working .Patrick and Happy are both in great pain right now” akasema Loniki huku akitabasamu kwa furaha
“Si hilo tu Lonny kuna taarifa nyingine pia imevuja kwamba Happy alitaka kujiua kwa kunywa sumu baada ya kuziona picha zile.Taarifa zinaseama kwamba baada ya kunywa sumu alikimbizwa katika hospitali ya Brahmaputra lakini uongozi wa hospitali ile umekanusha taarifa hizo.Taarifa mpya iliyopatikana toka vyanzo vya karibu vya Khumalo ni kwamba mpaka muda huu Happy hajulikani alipo.Waandishi wa wa habari wamekuwa wakimtafuta kwa mahojiano lakini hawajui yuko wapi na simu yake haipatikani tena na hata familia yake haiko tayari kusema mtoto wao yuko wapi” akasema Linah
“hahaaa aahahaa haaa!! Loniki akacheka kwa furaha na mara honi ya gari ikapigwa
“Linah wananipigia honi.Tutaongea baadae.Ahsante kwa taarifa” akasema Linah akakata simu na kukimbilia garini
“mambo ndo kwanza yanaanza Patrick.I’ll make your life a living hell.You and your girl must pay for what you did to Vero” akawaza Loniki
“Natumai kwa muda huu Patrick na Happy watakuwa katika mateso makubwa sana.Niliahidi kulipiza kisasi kwa kifo cha mdogo wangu na nitafanya hivyo.Huu ni mwanzo tu” akawaza Loniki
Safari ilikuwa ya kimya kimya hadi walipofika makaburini.Wakashuka garini na kuelekea katika kaburi la Vero.Lilikuwa kaburi linalopendeza na lililojengwa kwa ustadi mkubwa.Mama yake Vero akashindwa kuyazuia machozi kumtoka tena.Akakaa juu ya kaburi la binti yake aliyempenda sana na kuanza kulia
“Masikini binti yangu,wamekukatili uhai wako.Hukustahili kuondoka na kuniacha peke yangu mapema namna hii.Ninaomba usiku na mchana wale wote waliokukatili mwanangu na kunisababishia mateso haya makali wapate adhabu kali inayowastahili” akalia mama yake Vero.Loniki akamsogelea na kukaa pembeni yake
“Usilie mama,wote waliohusika na kifo cha Vero watapata adhabu inayowastahili na tayari yamekwisha anza kuwapata makubwa.Wataumia na kuteseka kama sisi tunavyoumia na kuteseka” akasema Loniki
Sarah ambaye anaye alikuwa amesimama karibu na kaburi akastuka baada ya kusikia maneno ya Loniki.
“mama ,kitu peke kinachoweza kukupa amani ya moyo ni kumuachia Mungu suala hili na si kuwaombea mabaya wahusika wa tukio hili.Kwa kuwaombea mabaya unakwenda kinyume na maandiko yanayotukumbusha kwamba tuwapende wabaya wetu na tuwaombee neema na Baraka .Ni Mungu pekee ndiye atakayewaadhibu” akasema Sarah
“Sarah najitahidi sana kufanya hivyo lakini ninashindwa.Kila nikifikiria namna mwanangu alivyokufa najikuta nikiwa na hasira na hamu ya kutaka kuwaona wale wote waliofanya kitendo kile wakipata adhabu kali.”
“Usiseme hivyo mama.Unat……” akasem Sarah lakini Loniki akaingilia kati
“Mama usimsikilize huyu.Siku zote yeye amekuwa upande wa Patrick.Hana uchungu wowote na kifo cha mdogo wake.Mama mimi ndio niko pamoja nawe.Wote waliosababisha kifo cha Vero lazima wapate adhabu kali”
Sarah na Loniki wakaangaliana kwa macho makali sana.Ikamlazmu mama yao kuingilia kati
“Haya inatosha sasa.Tuwekeni maua tuondoke” akasema mama yao halafu akachukua maua akayaweka juu ya kaburi na kupiga magoti,akasali kimya kimya na kusogea pembeni kuwapa nafasi wengine.Kila mmoja aliyekuja hapo aliweka shada la maua na kusali sala fupi
“Vero mdogo wangu,natumai huko uliko unaniona mida hii.Niliahidi kulipa kisasi kwa wale wote waliokufanyia unyama ule mkubwa na kukukatili maisha yako .Tayari nimeanza kuitekeleza ahadi yangu na wahusika wameanza kulipa.Si kazi rahisi lakini nakuahidi nitaifanya hadi nihakikishe Patrick na mwenzake wamelipa” akasema Loniki kwa sauti ndogo akiwa amepiga magoti katika kaburi la Vero.Zoezi lilipokamilika wakaingia garini na kuondoka kuelekea nyumbani

* * * *

Mlio wa simu ukamstua Savanna toka katika mawazo mengi.Ilikuwa ni simu toka kwa mkuu wa gereza
“hallo mkuu” akasema Savanna
“Savanna nimetaarifiwa kwamba tayari Patrick ameamka,unaweza kwenda kumuona sasa”
“Ahsante sana mkuu” akasema Savanna huku akiinuka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika zahanati ya gereza
“Mungu msaidie Patrick katika kipindi hiki kigumu alichonacho.” Akaomba Savanna wakati akipanda ngazi kuingia zahanati.Alionana na daktari ambaye alimpeleka moja kwa moja katika chumba alicholazwa Patrick
Mara tu Patrick alipomuona Savanna akainuka na kukaa kitandani.Savanna akamuendea na kumkumbatia
“Ouh Patrick,pole sana” akasema Savanna
“Savanna nashukuru umekuja” akasema Patrick kwa sauti ndogo yenye kukwama kwama.
“Patrick unajisikiaje sasa hivi?
“I’m dead Savanna.I feel dead” akasema Patrick
“Patrick usiseme hivyo”
“Savanna I want to die.namba uwaambie wanifungue hii pingu nife.I want to die.Sioni tena sababu ya kuendelea kuishi“
“Patrick tafadhali naomba unisikilize”
“Savanna believe me I’m dead.Ninahisi maumivu makali ya moyo.Nahisi kama kuna kitu kikali kinaukata moyo wangu vipande vipande..Ninasikia maumivu makali ambayo siwezi kuyaelezea” akasema Patrick
“Patrick nini kimetokea? Akauliza Savanna
“Savanna Happy yuko wapi? Happy ameniua.Ameniua bila kosa kama alivyomuua Vero.Nimemkosea nini mpaka anifanyie unyama wa namna hii? Upendo wote huu niliomuonyesha iweje leo hii anifanyie namna hii? It was all a lie.There was no us,there was no love ,it was all lies.Please let me die” akasema Patrick kwa uchungu
“Patrick tafad…………….” kabla Savanna hajamaliza alichotaka kukisema Patrick akapaaza sauti
“Waambie wanifungue.I want to die..!!!!!!!!!!!!!!!!”
Savanna akaogopa na kuwaita madaktari ambao walimkamata na kumchoma sindano ya usingizi
“Savanna unaweza kwenda nyumbani saas.Patrick bado akili yake haijatulia.Tutaendelea kumuangalia na kama kutakuwa na tatizo lolote tutakufahamisha” daktari akamshauri Savanna ambaye alikubali na kuondoka kuelekea nyumbani kwake.Hakutaka tena kufanya kazi yoyote kwa siku ile.kili yake yote ilikuwa inamuwaza Patrick.

* * * *

Ni siku ya pili sasa toka Parick alpolazwa katika hospitali ya gereza.Hali yake ilikuwa imeimarika tofauti na siku zilizotangulia
“Halloo Patrick “ akasema Savanna aliyekuja kumsalimu asubuhi hii
“Savanna.Karibu sana” akasema Patrick huku akijilazimisha kutabasamu
“Ahsante Patrick,unaendeleaje?
“Namshukuru Mungu leo sijambo.Naendelea vizuri sana.Madaktari wamenisaidia sana kunirejesha katika hali ya kawaida” Akajibu Patrick ambaye siku hii hakuwa amefungwa pingu kama siku zilizotangulia.
“Nashukuru sana kama unaendelea vizuri” akasema Savanna huku akiifungua chupa ya chai aliyokuja nayo na kummiminia Patrick chai katika kikombe
“mama na ndugu zangu wote hawajambo? Akauliza Patrick
“wote wazima na wanaendelea vizuri .Ninapita kila siku kuwasalimu na kumpa mama maneno ya matumaini.Mama anafarijika sana kila anionapo.Utanisamehe kwa kuwa sijawaambia chochote kuhusiana na wewe kulazwa hapa hospitali.Niliogopa kumuongezea mama matatizo hasa katika wakati huu ambao hali yake imeanza kuimarika.”
“Ulifanya vizuri sana Savanna kutokuwaeleza chochote.Wamekwisha umia vya kutoka kwa sababu yangu na sitaki waendelee kuumia zaidi.Nataka niendelee kuteseka mimi mwenyewe.” Akasema Patrick
“Savanna nakushukuru sana .Sipati nena la kuelezea shukrani zangu .You are my true friend.Umekuwa na mimi toka dakika ya kwanza na hadi leo hii haujaniacha hata siku moja.Savanna you have a special place in my heart.Sikujua kama siku moja wewe ndiye ungekuja kuwa mkombozi wangu.Watu niliowaamini na kuyatoa maisha yangu kwa ajili yao leo hii hawako tena na mimi,wamenisaliti na kuniacha peke yangu.Rafiki yangu Andrew,Happy…” Patrick akainama akazama katikam awazo halafu akainua kichwa na kusema
“Savanna naomba unisaidie ili niweze kutoka humu gerezani kwani sioni tena sababu ya mimi kuendelea kukaa humu gerezani.Nimempoteza Vero msichana aliyenipenda kwa moyo wake wote kwa ajili ya mtu ambaye haoni thamani yangu kwake.I was so wrong” Akasema Patrick kwa uchungu.
“Patrick usijilaumu sana kwani hukutegemea kama yangetokea haya yaliyotokea.Pamoja na kuondoka kwa Vero lakini kaa ukijua kwamba bado kuna watu wengi wanaokupenda na kukuombea usiku na mchana ili uweze kutoka salama gerezani na kuendelea na maisha yako.Familia yako,Happy na m………” kabla hajamaliza sentensi yake Patrick akasema kwa ukali
“Savanna tafadhali naomba usilitamke jina la huyo Malaya mbele yangu tena.Hilo ni jina ambalo sitaki kulisikia tena katika masikio yangu.Nilimpenda sana nikampa mwili na moyo wangu,nilikuwa tayari kuachana na kila kitu kwa ajili yake lakini kwa alichonifanyia sidhani kama nitakuja kumsamehe Happy.Savanna nimeumia sana.Sikuona sababu ya kuendelea tena kuishi siku ile niliponyeshwa picha za uchafu wake.” Akasema kwa uchungu Patrick
“Sijui nimweleze ukweli kuhusu suala hili? Lakini hapana,siwezi kufanya hivyo.Tayari amekwisha mtoa Happy akilini mwake na hii ni nafasi yangu sasa.Nataka Patrick awe wangu na inanibidi kuitumia vyema nafasi hii niliyoipata.Sintamweleza lolote kuhusiana na Happy” Akawaza Savanna
“Patrick pole sana.Hata mimi nilistuka sana nilipoziona picha za Happy katika gazeti na mitandao.Niliogopa sana hata kukwambia kwani nilijua ungeumia mno.” Akasema Savanna
“Usijali Savanna.Kuna watu walioguswa sana na kitendo kile na wakaniletea picha zile ili niangalie uchafu alioufanya mtu niliyemkabidhi moyo wangu.Siwafahamu watu hawa lakini nawashukuru sana kwa kunisaidia kutambua kwamba mtu niliyedhani ni kondoo ,alikuwa ni chui.Sikutegemea kama Happy angeweza kutenda kitendo kichafu na cha kujidhalilisha kama kile.Ninachoweza kukuomba kwa sasa ,nisaidie niweze kutoka humu gerezani na nianze upya maisha yangu.tafadhali Savanna usiniache nikafungwa kwa sababu ya mtu ambaye haioni thamani yangu kwake.”
“Patrick usijali kuhusu hilo.Kama nilivyokwisha kuahidi na ninavyoendelea kukuahidi ni kwamba nitafanya kila niwezalo ili uweze kushinda kesi hii.Bado hujachelewa kuyaanza upya ,maisha yako.Siku zote fahamu kwamba umezungukwa na watu wanaokupenda na kukujali kwa hiyo usijione mpweke.I’m right here for you any time you need a friend” akasema Savanna..

**********************


Dr Consolata bugama bingwa wa magonjwa ya akili,aliagana na mgonjwa wake akapanda gari lake na kuondoka pale Reonaldo hoteli.Happy alilitazama gari lile hadi lilipotoka kabisa katika lango la hoteli ile ya kifahari jijini Kigali.Akatabasamu na kuelekea katika sehemu ya kupumzikia
Ni siku ya tisa sasa toka alipokuja katika jiji hili la Kigali.Hali yake ilikuwa inaimarika siku hadi siku.Kwa msaada mkubwa anaoupata toka kwa daktari aliyeambatana naye toka Dar es salaam pamoja na Dr Consolata bingwa wa magonjwa ya akili katika hospitali kuu ya Kigali hali yake ilikuwa ya kuridhisha sana.
“Namshukuru sana Mungu kwa huruma yake hivi sasa ninaendelea vizuri.Sikutegema kama hali yangu ingekuwa namna hii.Mungu ni mwema sana na bado ananipenda na ndiyo maana hakuruhusu nife kwa sumu.Nawashukuru sana madkatari wangu kwa jitihada zao za kuhakikisha kwamba ninarejea katika hali yangu ya kawaida.Dr Consolata amejitahidi sana kuhakikisha kwamba akili yangu inarejea katika hali yake ya kawaida.Namshukuru sana pia Christine.Huyu dada amekuwa ni mtu wangu wa karibu na kila mara ninapohitaji mtu wa kuongea naye yeye amekuwa tayari kufanya hivyo.Siwezi kuusahau uongozi na wafanyakazi wa hoteli hii .They are all wonderfull people.Ni wakarimu na wote wananipenda sana.Ninahudumiwa kama mtoto wa rais.Ninapenda sana kuendelea kuishi hapa.Nimepapenda Kigali.I feel so Happy and safe around here” akawaza Happy huku akitabasamu
“Ouh gosh ! siwezi kumsahau Savanna.Japokuwa moyo wangu unastuka kila ninapoikumbuka sura yake lakini sina budi kumshukru kwa msaada mkubwa alionipatia.Najua hata wazo la kuondoka Tanzania na kuja Kigakli ni yeye ndiye aliyelitoa na kulisimamia kwa nguvu zote na likafanikiwa.Amenisaidia mno kuniondoa katika aibu na fedheha niliyoipata.Niko nje ya Tanzania sasa,ninashukru sana kwa sababu aibu niliyoipata ni kubwa na ambayo inanifanya nisitake tena kurudi Tanzania.Inaniuma sana kuiacha nchi yangu na kumuacha Patrick mwanaume wa maisha yangu niliyempigania kwa kila namna niliyoweza lakini kwa hili lililotokea nimeinua mikono.Sina namna nyingine zaidi ya kukubali kushindwa na kumuacha Patrick mikononi mwa Savanna.Najua atakuwa katika mikono salama.Mimi na Patrick hatuwezi kuwa pamoja tena.Huu ni ukweli ambao hatuwezi kuukwepa.” Akawaza Happy na sura yake ikaanza kubadilika na kuwa ya huzuni kidogo
“ Najaribu kumuhusisha Savanna na tukio lile la kutekwa kwangu lakini sioni kama ana uhusika wowote katika jambo lile.Kama si yeye nani basi anaweza kuwa nyuma ya tukio lile? Picha niliyoipata ni kwamba watu walionitenda vile lengo lao lilikuwa ni kunidhalilisha na kuhakikisha kwamba kwa namna yoyote ile ninaachana na Patrick.Laiti ningejua kwamba lengo lao ni hilo nisingekubali kufanyiwa udhalilishaji ule mkubwa.Anyway namuachia Mungu yeye ndiye atakayenilipia kwa mambo yote niliyofanyiwa.” Akaendelea kuwaza Happy
“Najua maisha yangu hayatakuwa na furaha tena na ninajua kwamba sintampata mwanaume kama Patrick katika maisha yangu yaliyobaki lakini ni vyema endapo nitakwenda kuishi mbali kabisa naye,mbali na Tanzania .Sitaki kukaa karibu naye kwani itanifanya niendelee kulipigania penzi letu na kadiri ninavyoendela kuupigania uhusiano wetu ndivyo mambo mabaya yanavyozidi kunitokea.Nimekwisha msababishia Patrick maumivu mengi ya moyo na sitaki aendelee kuumia zaidi.Nadhani uamuzi huu wa kutorejea tena Tanzania ni uamuzi wa busara sana ingawa najua Patrick ataumia mno na kunichukia.Ataniona kama ni msaliti na nilifanya kitendo kile kwa makusudi.Hakuna siri siku hizi hata kama yuko gerezani lazima atazipata taarifa zangu na nina hakika ataamini kwamba hii ndiyo tabia yangu.Ouh gosh ! ni mateso makali sana ya moyo atakayoyapata..” Akawaza Happy halafu akainuka na kuanza kuzunguka bustanini
“Dr Consolata amekuwa akijitahidi sana kuhakikisha ninasahau yaliyopita .Sipaswi kuendelea kuyafikiria yaliyopita.Ninachotakiwa kufanya kwa sasa ni kufikiri kuhusu maisha yangu ya mbele yatakuwaje.” akawaza Happy huku akiendelea kuzunguka zunguka mle bustanini
“Nimeipenda sana Rwanda .Ni nchi nzuri na ningefurahi mno kama ningeishi katika nchi hii kwa maisha yangu yote yaliyobakia.Lakini siwezi kufanya hivyo.Lazima niondoke Rwanda.Natakiwa kwenda kuishi mbali kabisa na Tanzania ikiwezekana nje kabisa ya Afrika.Nataka nikaishi mahala ambako nitaishi bila kuonana na mtu yeyote wa kutoka Tanzania.Kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza akanisaidia katika hili. Ni Mike pekee.Najua niliutia moyo wake jeraha kubwa ambalo si rahisi kupona haraka ,niliuvunja vunja moyo wake pale nilipoamua kuachana naye na kurudiana na Patrick.Najutia nafsini kwangu kwa kitendo kile.It needs more than a man to forgive me for what I did.Japokuwa kabla hajaondoka Tanzania alinihakikishia kwamba amenisamehe lakini sina hakika kama ataweza kukisahau kitendo kile nilichomfanyia.”
Happy akasimama baada ya picha ya Mike akiondoka Tanzania chini ya ulinzi mkali kumjia kichwani.
“Ouh Gosh ! forgive me Mike” akasema Happy huku akisikia uchungu mwingi moyoni
“Sina hakika kama Mike anaweza kuwa tayari kunisaidia au hata kunisikiliza lakini sitakiwi kukata tamaa.Natakiwa kujaribu kumuomba anisaidie.Endapo atakataa kunipa msaada ninaoutaka nitatafuta namna nyingine ya kufanya.Nitamuomba hata Savanna anisaidie.Kitu pekee ninachokiami na kinachonipa msukumo wa kutaka kuwasiliana na Mike ni kwamba Mike ananipenda kwa moyo wake wote.” Akawaza Happy na kuupeleka mkono sehemu ulipo moyo wake ambao ulikuwa unadunda kwa kasi kubwa.
“lazima niwasiliane naye na nimuombe anisadie.Lazima niondoke hapa Kigali na kwenda mbali.Namuonea huruma sana baba yangu .Amekuwa nami kwa kipindi kirefu toka matatizo haya yalipoanza na yeye ndiye amekuwa msaada mkubwa kwangu.Ni wakati sasa wa yeye kupumzika na kuendelea kufanya shughuli zake za kimaendeleo.Ninajisikia furaha sana kuwa na baba kama huyu.He’s the best father in the world.” Akawaza Happy na kutabasamu
“Ngoja sasa nikampigie simu Mike.” Akawaza Happy na kuelekea chumbani kwake.Alipoingia chumbani kwake akasimama mbele ya meza iliyokuwa na simu akaitazama simu ile na kuvuta pumzi ndefu.
“I’m so scared” akasema kwa sauti ndogo.Kwa takribani dakika tatu alisimama akiitazama simu ile.Alihisi kama mikono yake ikimtetemeka kila alipojaribu kutaka kuichukua simu ile na kupiga
“Mungu wangu tafadhali naomba unisaidie.Nahitaji kufanya hivi.Nahitaji kuongea na Mike” akasema Happy kwa sauti ndogo.Baada ya tafakari akaamua kupiga.Alizifahamu namba za simu ya mkononi ya Mike na akaziandika huku mapigo ya moyo wake yakienda kwa kasi kubwa.Akauweka mkono wa simu sikioni na simu ikaanza kuita.Baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti ikimwambia
“Mike hayuko katika nafasi ya kupokea simu kwa sasa tafadhali acha ujumbe wako baada ya mlio.” Happy akavuta pumzi ndefu na mara baada ya mlio kusikika akasema
“Hallow Mike,ni mimi Happy.Naomba upatapo uumbe huu,unipigie simu.Kwa sasa niko Kigali Rwanda,Reonaldo hoteli presidential suit number two.Please call me back Mike.I real need to talk to you” Happy aliyasema maneno haya huku machozi yakimtoka.Akauweka mkono wa simu chini ,akapangusa machozi na kwenda kuketi sofani
“Please Help me Mike” akasema kwa sauti ndogo
Baada ya dakika tano kupita simu ikaita.Akainuka na kwenda mezani akasimama na kusita kuipokea.Simu ikaendela kuita na mwishowe akaamua kuipokea.
“hallo “ akasema Happy
“Hallow Happy.Mike hapa nongea” Ikajibu sauti ya upande wa pili.Mikono ya Happy ikaloa jasho.Kwa sekunde kadhaa alihisi kama sauti yake ikigoma kutoka
“Hallow Mike” akasema Happy kwa sauti yenye kitetemeshi
“Hallow Happy.Unaendeleaje? Nimeupata ujumbe wako muda si mrefu.Habari ya Tanzania?
“habari ya Tanzania nzuri ila kwa sasa niko Kigali Rwanda”
“Sawa Happy.Nashukuru sana kwa kunikumbuka .Patrick anaendeleaje?
Swali lile likamchoma sana Happy akahisi kama miguu inaisha nguvu
“ Anaendelea vizuri” akajibu kwa ufupi
“Happy una tatizo gani? Naisikia sauti yako kama haiko sawa.Ninakufahamu vyema wakati una tatizo”
Happy akakaa kimya akahisi kama midomo yake inashindwa kufunguka
“ Happy una tatizo gani? Akauliza tena Mike
Happy akakohoa kidogo na kusema
“Mike ni kweli nina tatizo na ninahitaji msaada wako” kimya kifupi kikapita Mike akasema
“Una tatizo gani Happy?
“Mike siwezi kukueleza katika simu ni tatizo kubwa.Najua kwa sasa mimi ni mtu ambaye hupendi kuniona na hata kuisikia sauti yangu kutok…………”
“No ! No ! Happy.Usifikiri hivyo” mike akamkatisha Happy
“Ni kweli Mike.Hata mimi mwenyewe nafsi yangu inanisuta sana kwa kitendo nilichokufanyia lakini pamoja na hayo yote yaliyotokea sina mtu mwingine ninayeweza kumkimbilia kuomba msaada kwa sasa.Mike najua ndani kabisa mwa moyo wako bado nina nafasi japokuwa ndogo sana.Ninakuomba kama rafiki unisaidie” akasema Happy huku machozi yakimtoka.Kupitia spika za simu Happy akamsikia Mike akivuta pumzi ndefu na kusema
“Happy,napenda niwe wazi kwako kwamba kilichotokea baina yetu kiliniumiza sana.Nilipata jeraha ambalo halitaweza kutibika.Ulipoamua kuniacha niliumia sana.hadi hivi sasa bado ninaamini kilichotokea ni kama ndoto na ndiyo maana nilipoupata ujumbe wako nimekupigia simu mara moja.” Akasema Mike na kunyamaza .Maneno yale yakamuumiza sana Happy na kuzidi kumtoa machozi.Mike akaendelea
“Happy kama nilivyosema siku ile nilipokuja kukuaga kwamba mimi tayari nimekusamehe na wala sina kinyogo chochote nawe.Kwangu mimi ,wewe bado ni mtu muhimu sana na rafiki wa pekee kabisa. Niko tayari kukupa msaada wowote na kwa wakati wowote.Naomba unieleze unahitaji msaada gani Happy? Akasema Mike .Happy ambaye kifua chake kilikuwa kimeloa machozi akasema
“Mike kwa sasa nimekwama hapa Kigali na lengo langu kubwa ni kuondoka hapa. Nataka kuja Marekani lakini sina namna ya kuondoka hapa.Naomba unisaidie ili niondoke hapa kuja Marekani.Nahitaji kuwa mbali na Tanzania.Tafadhali Mike nahitaji sana msaada wako sasa kuliko wakati wowote katika maisha yangu.Tafadhali naomba unisaidie Mike” Happy akaomba.Sauti yake ilitia huruma sana na ilionyesha dhahiri ni jinsi gani alivyokuwa akihitaji msaada wa Mike
Mike akavuta pumzi ndefu ,kikapita kimya cha dakika moja halafu akasema
“Nimekuelewa Happy.Nitakusaidia.Siwezi kukuacha wakati wa matatizo.Nitakusaidia Happy.Ninachohitaji kufahamu ni kama nyaraka zako zote za kusafiria unazo?
“Ndiyo Mike.Nyaraka zote ninazo hapa”
“Sawa Happy.Usijali nitakusaidia .Nitakupigia simu jioni ya leo kukufahamisha mchakato mzima ulivyo”
“Ouh Mike nakushukuru sana kwa kukubali kunisaidia” akasema Happy huku uso wake ukichanua kwa tabasamu
“Ni wajibu wangu kukusaidia Happy na nitafanya hivyo.Nitaongea nawe tena jioni ya leo kwa kirefu zaidi”
“Ahsante Mike” akasema Happy na kukata simu
“Ouh Gosh ! Siamini kabisa kama Mike amekubali knisaidia. Nasikia aibu sana kumuomba msaada Mike lakini kwa wakati huu nimekwama na ni yeye pekee anayeweza kunisaidia.Ninaamini Marekani nitaweza kuishi kwa amani bila bughudha.Ouh Mungu wangu naomba unisaidie ili Mike asiweze kubadili mawazo yake.” Akawaza Happy
Wakati Happy akiwa katika lindi la mawazo lililochanganyika na furaha mara kengele ya mlangoni ikalia. Haraka akajipangusa machozi na kuelekea mlangoni.Alikuwa ni baba yake mzee Kibaho aliyetoka kuvinjari mitaa ya jiji hili la Kigali
“Ouh Dady..!!” akasema Happy na kumkumbatia baba yake.
“I missed you dady” akasema Happy.Baba yake akamtazama kwa makini usoni
“Ulikuwa unalia? akauliza mzee Kibaho .Happy akakaa kimya
“Happy una tatizo gani? Siku zote nimekuwa nikikwambia kwamba kama una tatizo lolote usisite kuniambia”
“Ni kweli baba nilikuwa nalia lakini machozi ya furaha.
“Machozi ya furaha?
“Ndiyo baba”
“Umefurahi nini leo?
“Dady kwanza kabisa napenda sana nikushukuru kwa upendo wako mkubwa kwangu.Dady umekuwa nami katika matatizo yangu.Hujawahi kuniacha hata sekunde moja toka nilipoanza kuandamwa na matatizo.You are the best dady in the whole world.I’m proud to be your daughter.” Akasema Happy na kumfanya mzee Kibaho atabasamu
“dady umekuwa nami hata katika nyakati zile ambazo hakuna mwingine aliyethubutu.Kazi uliyoifanya ni kubwa na ninadhani ni wakati wako sasa wa kupumzika”
“Happy unazidi kunichanganya.Hata siku moja sijawahi kuchoka wala sintachoka kuwa nawe kwani ni jukumu langu kuhakikisha kwamba siku zote binti zangu wanakuwa na furaha.”
“Nafahamu hilo dady na ndiyo maana nasema kwamba wewe ni baba wa kutiliwa mfano duniani.Nimesema kwamba ni wakati wako wa kupumzika kwa sababu nimeamua kuondoka Kigali
“Unaondoka Kigali? Mzee Kibaho akashangaa
“Ndiyo dady.Kigali ni mji mzuri na ninapapenda sana na ningependa kama maisha yangu yote yaliyobaki ningeishi hapa lakini kuwepo kwangu hapa kutaendelea kunikumbusha tukio lile.Baada ya kufikiri sana nimeamua ili niweze kulisahau kabisa tukio lile basi niende kuishi mbali na nyumbani,mahala ambako sifahamiki na sintaweza kukutana na mtu yeyote anayenifahamu.Nataka niyaanze maisha yangu mapya.Nataka nisahau yale yote yaliyonipata japokuwa najua si kazi rahisi lakini nitajilazimisha kufanya hivyo .Maisha yangu mapya nataka kwenda kuyaanza mbali kabisa mahala ambako ni familia yangu pekee watapafahamu”
“Happy nashukuru sana kwa maamuzi hayo.Siku zote hilo limekuwa ni wazo langu kwamba ukaanze maisha mbali kabisa na nyumbani ikiwezekana nje ya afrika.Ni wapi umefikiria kwenda ili tuanze mchakato wa Safari.?
“Ouh dady.Huna haja ya kusumbuka.Tayari nimekwisha pata msaada .Nitakwenda kuishi Marekani”
“marekani?
“Ndiyo baba”
“marekani yuko Mike na ukumbuke bado atakuwa na hasira kwa mambo yaliyomtokea Tanzania.Nina wasi wasi anaweza akakufanyia kitu kibaya cha kulipiza kisasi”
“hapana baba.Huwezi kuamini kwamba Mike ndiye anayenisaidia mimi katika mchakato huu wa kurejea Marekani”
“Happy…!!!!” akastuka mzee Kibaho
“Usiogope baba.Tayari nimekwisha ongea naye na ameniahidi kunisaidia.”
Mzee Kibaho akamtazama mwanae kwa makini na kusema
“Do you trust him?
“Yes dady ! I trust him.Mike ananipenda sana na hawezi kukataa kunisaidia”
“Najua Mike bado anakupenda na anaweza kuwa amekubali kukusaidia kwa matumaini kwamba mtarejesha mahusiano yenu.Naomba nisikie toka kwako je bado unampenda Mike na uko tayari kurudana naye?Vipi kuhusu Patrick?..akauliza mzee Kibaho.Haoppy akafikiri kidogo na kusema
“I don’t know dady… I real don’t know what going to happen there.Kuhusu Patrick I think its right time now that I let him go.Matatizo niliyoyapata katika kipindi hiki kifupi nilichokutana naye yametosha na sintaweza kuvumilia zaidi.Dady nimekuwa ni mtu wa kulia kila siku kutokana na majanga yasiyokwisha.Inauma kusema lakini ni ukweli ulio wazi kwamba mimi na Patrick hatuwezi kuwa pamoja tena.NI vyema kama tutatengana kwa sasa.Ninaumia sana kwa kuamua kuondoka na kumuacha Patrick gerezani kwa kosa nililolisababisha mimi lakini sina namna ya kufanya siwezi tena kurejea Tanzania.Nina hakika Savanna atahakikisha kamba hafungwi gerezani.Savanna amenihakikishia kwamba Patrick atakuwa huru na ataendelea na maisha yake.Patrick told me to put a trust in her and I trust her. It hurt so much dady.All these years I’ve been dreaming that some day I’ll be married to Patrick but now I have to forget him.”” akasema Happy huku machozi yakimtoka.Kikapita kimya kirefu mzee Kibaho akasema
“Nakubaliana nawe Happy ni kweli yawezekana wewe na Patrick haikupangwa muwe pamoja.Ni vyema kama utakwenda kuishi mbali naye na kujitahidi kumsahau.Vipi kuhusu wale wanaharamu waliokufanyia udhalilishaji ule? Uko tayari kuliongelea suala hilo kwa sasa?
“No dady .I’m not ready.Thats the part of my life I’m trying to forget”
“Ok Happy usijali.Utaliongelea suala hilo pale utakapokuwa tayari”
Happy akainuka pale alipokuwa amekaa akaenda dirishani akatazama nje kisha akasema
“I’ll never be ok without Patrick.But then I have to live my life without him.It hurt so much dady……” Happy akashindwa kujizuia akazidi kulia

TUKUTANE SEHEMU IJAYO..........
 
MISS TANZANIA
SEHEMU YA 51
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT: 0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“No dady .I’m not ready.Thats the part of my life I’m trying to forget”
“Ok Happy usijali.Utaliongelea suala hilo pale utakapokuwa tayari”
Happy akainuka pale alipokuwa amekaa akaenda dirishani akatazama nje kisha akasema
“I’ll never be ok without Patrick.But then I have to live my life without him.It hurt so much dady……” Happy akashindwa kujizuia akazidi kulia

ENDELEA………………..

Tayari kiza kimetanda jijini Dar es salaam,ndani ya mkahawa mmoja maarufu sana jijini Dar es salaam,watu watatu,wanawake wawili na mwanaume mmoja walikuwa wameizunguka meza iliyokuwa imesheni vinywaji vikali
Mwanamke mmoja aliyekuwa na sigara mkononi akapuliza moshi mwingi hewani na kusema
“Khumalo tumekuja kama ulivyotutaka tuonane jioni ya leo” akasema Yule mwananmke na kuchukua glasi yake ya mvingo akapiga funda kubwa.Khumalo akawatazama wanawake wale kisha akasema
“Loniki na Linah ,nimewaiteni hapa ili kuwapeni taarifa ya maendeleo kuhusiana na kazi mliyonikabidhi.Kama mnavyokumbuka ,makubaliano yetu yalikuwa ni kuwashughulikia watu wawili waliohusika katika kifo cha ndugu yenu,.Watu hawa ni Patrick na Happy.Kwa mujibu wa Loniki ulitaka watu hawa wauawe lakini nilikushauri kwamba suala la kuua mmoja wao kati ya Hapy au Patrick kwa wakati huu lingeweza kuleta utata mkubwa na lingeonekana kabisa ni tukio la kulipiza kisasi.Nashukuru mlikubaliana na ushauri wangu na na kazi ya kwanza ikafanyika. Happy alishughulikiwa na nyote mkishuhudia.Ninathubutu kusema kwamba tulifanikiwa sana lengo letu kwa Happy kwani toka picha zile na video kutolewa Happy amepotea na hajulikani alipo.Vijana wangu wamekuwa wakimtafuta lakini hakuna anayefahamu mahala alipo.Kuna tetesi vile vile kwamba alijaribu kujiua kwa kunywa sumu lakini hakuna aliyepatikana kulithibitisha hilo kwani hospitali ile aliyotibiwa wamegoma kata kata kuthibitisha taarifa hizo.Kuhusu Patrick tulifanikiwa kumpekekea picha za Happy na alipoziona nusura apandwe na uchizi.Nina hakika kwamba tumefanikiwa kuyavunja mahusiano ya watu hawa na hivi sasa watu hawa wote wawili watakuwa katika mateso makubwa sana.Happy akiteseka kwa picha zile na Patrick akiteseka kwa kumuona mpenzi wake akifanya jambo kama lile. Jana usiku nilipokea simu toka kwa Linah akiniambia kwamba Loniki bado hajaridhishwa na jambo tulilolifanya na anataka Patrick na Happy wauawe.” Khumalo akanyamaza kidogo akanywa mvinyo na kuendelea
“Loniki naomba niwe wazi kwako kwamba suala la kumuua Patrick kwa sasa limekuwa gumu kidogo kwa sababu ulinzi umeimarishwa sana pale gerezani toka alipopelekewa picha zile za Happy na akazua tafrani kubwa.Kwa sasa wanaoruhusiwa kuonana naye ni mawakili na familia yake tu.Ninashauri kwamba suala hili la kumuua Patrick au tulivutie subira kwanza ili tuweze kutafuta namna bora kabisa ya kuweza kuutekeleza mpango huu.Endapo tutataka kulazimisha jambo hili linaweza kutuletea matatizo”
Kauli ile ya Khumalo haikuonekena kumfurahisha Loniki
“Ouh gosh..!!” akasema Loniki na kukaa kimya
“Mbona umestuka Lonny? Akauliza Khumalo
“Damn you Khumalo ! laiti ungejua ni namna gani ninavyosubiri usiku na mchana kuona watu hawa wakifutika toka katika uso wa dunia usingetamka maneno hayo uliyoyatamka”
“Nahafahamu Loniki,lakini naomba ufahamu kwamba mimi ndiye uliyenikabidhi kazi na ndiye ninayefahamu ugumu wa kazi yenyewe.Hii si kazi ya kuiendea haraka.”
“Khumalo naomba usianze kuniletea hadithi zako.I’ve paid you a lot of money for this job ,so do your job..I want Patrick and Savanna dead !! ..” akasema Loniki kwa ukali.Khumalo akamtazama,akainua glasi na kupiga funda moja na kusema
“Lonny,naomba ufahamu kwamba nilikubali kuifanya kazi hii kwa heshima ya Linah.Naomba vile vile ufahamu kwamba kazi hii nimeifanya kama msaada tu kwa sababu kazi kama hii mimi huifanya kwa milioni mia mbili na zaidi.Nimekwambia haya yote ili ufahamu kwamba sijaifanya kazi hii kwa pesa. Na endapo ukihitaji fedha zako unaweza ukaniambia nikakurejeshea na ukatafuta watu wengine wa kukufanyia kazi yako” akasema Khumalo.
“Jamani naomba tusifike huko.Loniki naomba umsikilize Khumalo anavyosema.Ushauri wake mimi binafsi naona ni mzuri tu.Tujipe muda ili tuweze kujipanga vizuri zaidi kwani hata kazi iliyofanyika ni kubwa na inatia matumaini.Patrick na Happy wote kwa pamoja wameumia sana na nina hakika hawatakuwa pamoja tena “ akasema Linah
“ Linah hujui ni namna gani nilivyokuwa nahitaji kuona Patrick na Happy wameuawa kabla sijarejea London.Kamwe moyo wangu hautakuwa na amani kumuona Patrick akiendelea kuvuta hewa hii safi wakati mdogo wangu akioza kaburini”
“Usihofu Lonny.Hata kama hautakuwepo mimi nitakuwepo kuusimamia mpango huu.Unaweza ukawa Uingereza lakini tukafanya kila kitu sisi tuliobaki huku.Ninakuahidi mimi binafsi nitashirikiana na Khumalo kwamba nitahakikisha lazima Patrick na Happy wanauwa na tunalipa kisasi kwa kifo cha Vero “ akasema Linah na kauli ile ikampa moyo Loniki na kumfanya akubaliane naye japo kwa shingo upande.

MIEZI SITA

Ni siku iliyotawaliwa na kijua kikali kama ilivyo kawaida ya jiji la Dar.Pilika pilika katika jiji hili lenye shughuli nyingi ziliendelea kama kawaida.Katika mahakama ya kisutu kulikuwa na idadi kubwa ya watu tofauti na ilivyozoeleka.Ongezeko hili wa watu lilitokana na minong’ono iliyokuwa imeanza kusambaa kwamba huenda Patrick ambaye anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia,angepatiwa dhamana siku ya leo baada ya taratibu zote kukamilika.Kwa muda wa miezi sita sasa toka Patrick alipoanza kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusababisha mauaji,kesi hii imekuwa ikipewa umuhimu mkubwa sana na vyombo vya habari na hasa kutokana na miss Tanzania Happy Kibaho kutajwa kuhusika katika ugomvi uliosababisha kifo cha Vero.Kutokana na kutangazwa sana na vyombo vya habari watu wengi walikuwa wanaifuatilia ili kujua nini hatima yake.
Wengi wa watu waliofika walitegemea kumuona miss Tanzania aliyevua taji lake Happy Kibaho akiwa mahakamani.Toka picha na video yake ya utupu kuchapishwa na kusambaa mtandaoni Happy alipotea ghafla na hakuna aliyefahamu mahala alipo hivyo wengi walitegemea pengine angeweza kuonekana mahakamani siku ya leo.
Hatimaye kama ilivyokuwa imetegemewa na wengi,saa saba za mchana Patrick alipatiwa dhamana baada ya masharti yote yanayohitajika kutimizwa.Kilikuwa ni kipindi cha furaha sana hasa kwa familia yake,ndugu jamaa na marafiki.Ilikuwa ni kama ndoto pale Patrick aliposhikwa mkono na Savanna na kuthibitishiwa kwamba yuko huru kuondoka.Hakuamini macho yake.
“Savanna thank you very much.” Hilo ndilo neno pekee aliloweza kulitamka Patrick kwa wakili huyu mahiri ambaye amekuwa akimtetea katika kesi hii.Patrick akasalimiana pia na mawakili wengine ambao kwa pamoja wanaunda jopo la mawakili wanaomtetea na kisha taratibu huku akiwa ameongozana na Savanna wakatoka nje ya jengo la mahakama ambako aliendelea kusalimiana na watu mbali mbali mbali waliofika mahakamani.Wakati akiendelea kusalimiana na watu mbali mbali ,ghafla akastuka baada ya kuiona sura yenye tabasamu ya mwanadada mrembo na kuufanya moyo wake kuanza kudunda kwa kasi.Alikuwa anatazamana na Sarah dada yake Vero.Kwa sura Sarah na Vero walikuwa wanafanana sana kiasi kwamba ungeweza kudhani ni mapacha
Sarah ambaye alikuwa anatabasamu na kumkumbusha Patrick lile tabasamu alilolizoea la Vero akamsogelea na kumkumbatia.
“Pole sana Patrick.Usijali Mungu atakusaidia na mambo haya yatakwisha.” Akasema Sarah na kumshangaza sana Patrick ambaye alikosa neno la kusema midomo yake ilikuwa inamtetemeka.Hakutegema kama Sarah angeweza kuongea naye kistaarabu namna ile hasa baada ya kusababisha kifo cha mdogo wake.
“Sarah nashukuru sana” Patrick akasema.Sarah akatabasamu na kusema
“Patrick tutaongea siku nyingine kwa sasa unahitaji mapumziko.” Akasema Sarah halafu wakaagana akaondoka zake.Baada ya Patrick kusalimiana na watu wengi waliokuja kumpa pole siku hii ya leo,Savanna akamshika mkono na kumuongoza hadi katika gari lake na ndugu wengine nao wakaingia katika magari yao na kuondoka pale mahakamani.Patrick alikuwa amegeuza shingo yake akiangalia nje na mara akavuta pumzi ndefu
“Ouh my gosh ..!!! “ akasema Patrick akionekana kustushwa na kitu Fulani
“Patrick whats wrong? Akauliza Savanna
“Bado naona ni kama muujiza vile leo nimerejea tena uraiani.Sipati neno la kukushukuru Savanna.Ni Mungu pekee ndiye atakayekulipa” akasema Patrick
“Ouh Patrick plase don’t say anything.Ni wajibu wangu kufanya hivi na huna sababu ya kunishukuru” akasema Savanna huku akitabasamu
“Unanipeleka wapi,nyumbani kwangu au kwa mama? Akauliza Parick
“Patrick ,haitakua vizuri kama ukienda nyumbani kwako kwa sasa.Nyumba ile ina kumbukumbu nyingi ambazo zitakukumbusha historia ya wewe na Vero ambayo unajitahidi kuisahau.Nyumbani kwa mama nako kuna kumbukumbu nyingi ambazo zitakukumbusha kuhusu baba.Unatakiwa kwanza kuwa tayari kukabiliana na hayo yote.Nashauri kwanza upate mapumziko halafu tutakwenda nyumbani kwa mama lakini kwa sasa utakwenda kuishi kwangu .Nimekuandalia chumba maalum.Pale utapata kila kitu unachokihitaji hadi hapo utakapojisikia kuwa tayari kurejea kwako” akasema Savanna.Patrick akatabasamu
“Nilipenda sana kufika nyumbani kwa mama siku ya leo.Najua hata yeye pia ana hamu kubwa ya kuniona”
“Nyumbani kwa mama utakwenda lakini kwanza unatakiwa ukaoge,upate chakula,upumzike kidogo halafu ndipo uwe tayari kuonana na mama”
“Ok Savanna.Wewe ndiye kiongozi wangu kwa sasa.Siwezi kukupinga kwa lolote” akasema Patrick huku akicheka na kumfanya Savanna naye acheke
“Simu hii hapa mpigie Alois na umtaarifu kwamba utakwenda nyumbani kwa mama jioni ya leo” akasema Savanna.Patrick akaichukua simu ile na kumpigia Alois akamtaarifu kwamba atakwenda kuonana nao jioni.

* * * *

Geti la rangi nyeupe likafunguliwa na gari aina ya Range rover vogue likaingia katika jumba la kifahari lenye rangi nyeupe.Milango ikafunguliwa akashuka Savanna na Patrick
“Karibu nyumbani Patrick” akasema Savanna
“Ahsante sana Savanna.Una nyumba nzuri sana” akasema Patrick huku akitabasamu.Waliingia ndani ya sebule kubwa
“Jisikie nyumbani Patrick” akasema Savanna
“Nashukuru sana Savanna.Nyumba yako nzuri mno” akasema Patrick huku akitabasamu.Mtumishi wa ndani akafika na kuwahudumia vinywaji.
Baada ya maongezi kidogo,Savanna akampeleka Patrick katika chumba maalum kilichoandaliwa kwa ajili yake
“Patrick, hiki ndicho chumba chako.Nimekiandaa maalum kwa ajili yako..Utaishi hapa hadi hapo utakapojisikia kurejea katika makazi yako.Nimejaribu kuweka karibu kila kitu unachokipenda.Katika kabati kuna nguo nilizokuandalia na sina hakika kama nimekosea vipimo” akasema Savanna na wote wakacheka halafu Savanna akamuacha Patrick na kwenda chumbani kwake .
Patrick aliingia bafuni na kabla ya kuoga akasimama kwanza na kuzama katika mawazo
“Hatimaye nimekuwa huru tena.Naona ni kama ndoto lakini huu ndio ukweli nimerudi tena nyumbani baada ya kusota gerezani kwa muda wa miezi sita.Ama kweli maisha yanaweza kubadilika ndani ya sekunde moja kama yalivyobadilika kwangu.Sikuwahi kuota kma maisha yangu yangebadilika namna hii” akawaza Patrick na mara sura ya Vero ikamjia kichwani
“Sura hii ya Vero itaendela kuniandama kwa muda mrefu sana na kuifuta sura hii kichwani kwangu itanichukau muda pia” akawaza Patrick
Baada ya kuoga akajumuika na Savanna wakapata chakula pamoja halafu akarejea chumbani kwake kupumzika.
“Ni muda mrefu sijalala katika sehemu nzuri kama hii.I missed this life a lot.Shukrani za pekee zimwendee Savanna ambaye amepambana na kuhakikisha ninapata dhamana.Savanna ni mwanamke wa shoka.Nina deni kubwa kwake.Amenionyesha kwamba yeye ni rafiki wa kweli kuliko hata wale niliowaamini kwa moyo wangu wote.Ni Mungu peke atakaye mlipa Savanna kwa wema wake huu mkubwa” akawaza Patrick
“Kwa sasa natakiwa kujipanga kwa ajili ya kuanza upya maisha yangu.Nimepoteza kila kitu.Nimepoteza kazi,nimewapoteza wapendwa wangu Vero na Happy , hata Andrew rafiki yangu mkubwa naye ameniacha na sina taarifa zake tena. Sijilaumu sana kwa kilichotokea bali napaswa kutuliza akili na kujipanga upya.Bado sijachelewa kuyapanga na kuyajenga upya maisha yangu bila ya wale niliowapenda .Tukio lililotokea limenifundisha mambo mengi sana na safari hii sitaki kurudia makosa.Nakiri nilifanya kosa kubwa kuachana na Vero.Sikupaswa kufanya vile.Vero alikuwa ni mwanamke aliyenipenda kwa moyo wake wote na siku zote alikuwa tayari kwa lolote kwa ajili yangu.Nilimpuuza,nikaupuuza upendo wake kwangu na kuamini kwamba Happy ndiye mwanamke ambaye nimepangiwa niwe naye katika maisha.Nilijidanganya sana.Mimi na Happy katu hatuwezi kuwa pamoja.Tumekwisha jaribu na imeshindikana na tayari nimemfahamu Happy ni nani.Nashukuru nimeweza kumuondoa moyoni mwangu na amebaki ni katika historia ya maisha yangu lakini moyo wangu haudundi tena kwa ajili yake.Alichokifanya kimenifanya nimvue thamani kabisa na hana nafasi tena moyoni mwangu” Akawaza Patrick halafu akafumba macho na kulala
Saa moja za jioni akiwa ameongozana na Savanna akawasili nyumbani kwa wazazi wake ambako baadhi ya ndugu walikuwa wamekusanyika ili kumpa pole kwa masahibu yaliyomkuta.Wote walijawa na furaha kubwa kwa Patrick kurejea tena nyumbani.Chakula kizuri kiliandaliwa,wakala na kunywa na ilipofika saa tano za usiku Patrick na Savanna wakaondoka kurejea nyumbani kwa Savanna ambako Patrick aliwekewa makazi yake ya muda

* * * *

Saa nne za asubuhi siku iliyofuata iliwakuta Patrick na familia yake katika kaburi la baba yao.Alois ndiye aliyeongoza sala fupi ya kumuombea marehemu baba yao halafu ukafuata wakati wa kuweka shada za maua.Patrick aliyekuwa amevalia suti nyeusi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuweka shada la maua juu ya kaburi la baba yake.Akaliweka karibu kabisa na msalaba halafu akapiga magoti na kuliinamia kaburi
“Baba kokote uliko hivi sasa naomba unisamehe sana kwa mambo niliyoyafanya na kusababisha kifo chako.Sikutegemea kama maamuzi yangu yangetufikisha hapa.Ninasikia uchungu mkubwa sana ambao si rahisi kuuelezea.Baba nahitaji msamaha wako ili niweze kuondokana na mateso haya makubwa niliyonayo na nianze maisha mapya.Siku zote nitakuombea kwa Mungu ili aipumzishe roho yako mahala pema peponi Amina”
Baada ya kumaliza maombi yale mafupi ya kimya kimya akainuka na kuwapa nafasi ndugu zake wengine nao waweke shada zao za maua.Zoezi lile lilipokamilika Patrick na Savanna wakaingia garini na kuondoka kuendelea na ratiba nyingine ya siku hiyo.
“Kinachofuata sasa hivi kwa mujibu ratiba yetu tunaelekea katika kaburi la Vero” akasema Savanna
Walifika makaburini na Savanna akamuongoza Patrick hadi katika kaburi la Vero.
Hapa ndipo alipozikwa Vero” akasema Savanna.Patrick akaweka shada lake la maua na kuliinamia kaburi na machozi mengi yakamtoka.Savanna akasogea mbali kidogo na kumpa Patrick nafasi ya kuwa peke yake katika kaburi la aliyewahi kuwa mchumba wake.
“Anatia huruma sana Parick lakini hii ndiyo hali halisi ambayo lazima akabiliane nayo.” Akawaza Savanna
Baada ya dakika kumi za Parick kuliinamia kaburi la Vero akainuka.Macho yake yalikuwa mekundu na uso wake ulijaa machozi.Savanna akamsogelea na kumpa kitambaa
“its ok Patrick,Don’t cry anymore” akasema Savanna Patrick akafuta machozi.Akaendelea kulitazama kaburi lile kwa uchungu
“rest in peace Vero.You’ll always be in my heart” akasema Patrick halafu wakaondoka .

Toka makaburini ,Patrck na Savanna wakaendelea na safari yao hadi nyumbani kwa Patrick.Walinzi toka katika kampuni binafsi ya ulinzi ya Chem Chem security waliendelea kuilinda nyumba ya Patrick kwa kipindi chote ambacho Patrick alikuwa gerezani
“Welcome home Patrick” akasema Savanna huku akitabasamu.Patrick alishindwa kuzuia furaha yake alipoishuhudia nyumba yake namna ilivyokuwa imependeza.Ilikuwa imepakwa rangi nzuri nyeupe na kupandwa maua mengi kuizunguka.
“wow !! its incredible…!!!” akasema Patrick kwa furaha
“Nyumba yote ni salama.Imeendelea kulindwa na kampuni hii ya ulinzi kwa kipindi chote ulichokuwa gerezani.Niliingia nao mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuilinda nyumba yako na tayari fedha zote nimekwisha zilipa.Vile vile nyumba yote imepakwa rangi kwa nje.It looks beautiful,isn’t it?
“Savanna sijui hata niseme nini.Sijui nikushukuruje.The house looks so beautiful.Sikutegemea kama ningeikuta nyumba yangu katika hali hii.Ahsante sana Savanna kwa kunitunzia nyumba yangu.” Akasema kwa furaha Patrick na kuufungua mlango mkubwa akaingia ndani.Patrick alionekana kama anaiogopa nyumba yake.Hakutaka kugusa kitu chochote mle sebuleni.Walitoka sebuleni wakazunguka katika baadhi ya vyumba na hatimaye wakaingia katika chumba cha kulala cha Patrick.Mara tu walipoingia Patrick akastuka sana baada ya kuziona picha mbili kubwa zilizowekwa ukutani.Ilikuwa ni picha yake na Veronika.Alisimama kwa sekunde kadhaa akizikodolea macho picha zile kubwa
Juu ya kitanda kulikuwa na nguo za vero ambazo alizivua na kuziweka kitandani mchana wa siku ile ya kufariki kwake.Patrick akakumbuka dakika za mwisho akiwa na Vero mle chumbani.Vero alikuwa akimkumbatia kwa mahaba mazito.Alikumbuka namna walivyofanya mapenzi kwa mara ya mwisho na walipanga kuendelea tena jioni yake lakini Vero hakurejea tena katika chumba kile
“That’s the day I’ll never forget in my life.It’s the day that I made the biggest mistake of my life.Niliipoteza dhahabu ya thamani kubwa kwa mng’ao wa jiwe” akawaza Patrick huku machozi yakimlenga
“Savanna I need to be alone for a while” akasema Patrick na Savanna akatoka mle chumbani,Patrick akaufunga mlango halafu akapanda kitandani na kuzikumbatia nguo za Vero huku akilia
“Please forgive me Vero,forgive me“ akasema Patrick huku machozi yakimtoka.Alilia sana kisha akainuka na kwenda katika meza ya vipodozi iliyokuwa imesheni vipodozi vya kila aina alivyokuwa anatumia Vero.Akalifungua kabati kubwa na kuzikuta nguo nyingi za Vero ,akaanza kuitoa nguo moja baada ya nyingine na kuziweka kitandani.Kila nguo aliyoishika ilimkumbusha nyakati zile za furaha alizokuwa nazo akiwa na Vero.Alivikusanya vitu vyote vya Vero na kuviweka katika masanduku mawili makubwa
“Natakiwa kuvirudisha vitu hivi kwa ndugu zake.Kuendelea kuviweka hapa vitanifanya nishindwe kumsahau Vero na kuendelea na maisha yangu.Nitamtafuta Sarah na kumpatia vitu hivi vya mdogo wake” akawaza Patrick
“Itanichukua muda mrefu kurejea tena katika nyumba hii.Kwa sasa itanilazimu kuendelea kuishi nyumbani kwa Savanna.Ninahisi furaha na amini nikiwa pale.Savanna ananijali sana na anajitahidi kwa kila namna niweze kurejea katika maisha yangu ya kawaida.She’s a wonderfull woman” Patrick akatabasamu halafu akatoka na kuelekea sebuleni aliko Savanna.
“Savanna itanichukua muda sana kuweza kumsahau Vero .Kuna kumbu kumbu nyingi humu ndani zinazonikumbusha mbali na hasa dakika za mwisho nilizokuwa na Vero.Laiti ningejua kama ile ilikuwa ni siku ya mwisho ya Vero basi nisingefanya vile nilivyofanya.” Akasema Patrick
“Pole Patrick.Mambo haya yote yatakwisha japokuwa ni ngumu na itachukua muda kumsahau Vero lakini naomba ujitahidi kwa kila namna kuizoea hali hii na kuiona ya kawaida”
“Nitajitahidi Savanna.I’ll be ok” akasema Patrick halafu wakazungukia nyumba yake yote na walipomaliza wakaingia garini na kuondoka kurejea katika makazi ya Savanna

TUKUTANE SEHEMU IJAYO......................
 
Back
Top Bottom