LEGE
JF-Expert Member
- Oct 14, 2011
- 5,122
- 9,222
- Thread starter
- #41
ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA Hatimaye kesi ya kusababisha kifo inayomkabili Patrick ikatajwa kwa mara ya kwanza .Mshitakiwa katika kesi hiyo ambaye ni Patrick akasomewa shitaka la kusababisha kifo cha Veronika na hakutakiwa kujibu chochote.Kesi ikapangwa kutajwa tena baada ya wiki tatu na mshitakiwa akaamriwa kupelekwa mahabusu katika gereza jipya la Uwangwa kigamboni. "Usihofu Patrick .Kesi hii tunaifuatilia kwa umakini mkubwa .Niko pamoja nawe katika kila dakika.Naomba uondoe hofu na uniamini " .Akasema Savanna akimpa moyo Patrick wakati akisubiri kupanda katika basi maalum la kubebea mahabusu na kupelekwa gerezani. "Nakuamini Savanna na sina shaka hata kidogo na wewe.Ulifanikiwa kuonana na Happy? akauliza Patrick "Happy sijaonana naye .Nadhani hajafika mahakamani siku ya leo" akasema Savanna. "Una mawasiliano yake" akauliza Patrick "Nina namba za simu za mdogo wake Margreth.Nitampigia baadae nifahamu maendeleo yake" akasema Savanna .Muda huo huo akaingia mmoja wa mawakili wanaounda jopo la kumtetea Patrick akamuomba Savanna waongozane kuna suala la kisheria linalohitaji ufumbuzi wa haraka.Savanna akaagana na Patrick kwa ahadi ya kwenda kumtembelea gerezani kesho yake. "kwa nini Happy hajafika mahakamani? Ana matatizo gani?Pengine ameshindwa kufika akiogopa macho ya watu?" akawaza Patrick baada ya Savanna kuondoka. "Mama ,ndugu zangu na marafiki nimewaona mahakamani .Wote wamekuja kunifariji na kunipa moyo.Japokuwa nimewaudhi na kuwaumiza sana kwa mambo niliyoyafanya lakini bado wananipenda na wamekuja kunionyesha kwamba bado tuko pamoja.Ni familia ya Happy pekee ambayo haijafika mahakamani.Napatwa na wasi wasi nini kimetokea? I love Happy and I trust her with my life.." akawaza Patrick na mara sura ya Veronika ikamjia kichwani akafumba macho na kuuma meno. "Maskini Veronika sina taarifa atazikwa lini.Laiti nigekuwa na uwezo ningehudhuria mazishi yake lakini siwezi tena.Niko mikononi mwa sheria.Pumzika kwa amani vero.Utabaki ndani ya moyo wangu daima.Nitazikumbuka zile nyakati zote za furaha tulizowahi kuwa nazo katika mapenzi yetu. Daima nitaukumbuka upendo wako,ukarimu na ucheshi wako.Natambua ulinipenda kwa moyo wako wote.Kama siku moja nitabahatika kutoka gerezani nitalitafuta kaburi lako na kuweka maua meupe uliyokuwa unayapenda sana enzi za uhai wako,lakini kama nitahukumiwa kunyongwa au kufungwa maisha basi tutakutana mbinguni kwa baba.Pumzika kwa amani Veronika sikutegema kabisa kama mambo yangekuwa namna hii." akawaza Patrick huku akijizuia asidondoshe machozi. Saa nane za mchana Patrick akapakiwa katika basi maalum la kubebea mahabusu na safari ya kuelekea gereza la Uwangwa ikaanza.Taratibu basi likaanza kuondoka.Kupitia dirishani Patrick akaweza kumuona mama yake ambaye alikuwa amekaa chini kutokana na kuishiwa nguvu,kaka yake Alois akiwa na mkewe,rafiki yake Andrew akiwa na mchumba wake Vick pamoja na ndugu wengine,na marafiki.Wengi walikuwa na nyuso za huzuni kubwa na wengie walishindwa kujizuia kutokwa na machozi. Patrick akawapungia mkono na taratibu basi likaondoka maeneo ya mahakama kuelekea mahabusu katika gereza la Uwangwa ambako anakwenda kuanza maisha mapya
ENDELEA NA SEHEMU YA PILI………… Gari moja aina ya Lexus lenye rangi nyeusi lilikuwa limeegeshwa katika mahakama ya kisutu.Hakuna mtu aliyekuwa ameitilia maanani gari ile wala kuifuatilia.Ndani ya gari ile yenye vioo vyeusi walikuwemo wasichana wawili waliokuwa wamekaa kimya.Mmoja wao alikuwa akitokwa na machozi “Happy nyamaza kulia.You have to remain strong.Kulia hakutakusaidia chochote na wala hakutabadili hali halisi ya mambo.Ukumbuke vile vile kwamba tears is the sign of defeat.Usikubali kushindwa Happy.Simama imara na kumpa nguvu Patrick .Simama katika maamuzi yako.” Margreth akampa dada yake maneno ya faraja. “Margreth najitahidi sana kujipa moyo na ujasiri lakini najikuta nikishindwa.Kila nikifikiria kuhusu tukio lile najikuta nikiangusha machozi.Nasikia uchungu mkubwa moyoni.namuonea huruma Patrick na wakati huo huo sijui nifanye kitu gani..ouh Patrick..!!!!..Amebeba jukumu zito sana .Amejitwisha mzigo wangu.Ni mimi ndiye niliyestahili kuwepo mahakamaini mida hii na si yeye lakini kwa upendo wake usio na kifani amejitolea kuubeba mzigo huu nilioustahili.Sijui nitaulipaje upendo huu mkubwa alionionyesha Patrick.I’m confused !!” akasema Happy.Margreth akamtazama halafu akamshika bega “Happy huna haja ya kuendelea kulia .Unachotakiwa kufanya kwa sasa ni kukubaliana na kilichotokea na kujipanga kuikabili hali hii na kuona namna tutakavyoweza kumsaidia Patrick ambaye amefanya kitendo ambacho mimi nakiita ni cha kijasiri sana na ameyatoa maisha yake kwa ajili yako.Jukumu lako kwa sasa ni kumpa kila aina ya ushirikiano unaohitajika na kuhakikisha kwamba anashinda kesi.Kwa hiyo Happy nakushauri uwe jasiri sana na ujasiri wako ndicho kitu pekee cha kumpa Patrick nguvu ya kuhimili kukaa gerezani.” Akasema Margreth “Margreth, si kwamba nashindwa kuwa jasiri ,lakini kuna nyakati ninajikuta nikiwa dhaifu sana hasa kila nikikumbuka mambo yaliyotokea.Things happened so fast.Sikutegemea kama mambo yangefika hapa yalipofika.” “Huna haja ya kujilaumu Happy.Yaliyotokea yametokea na na kuna usemi usemao kwamba kila jambo hutokea kwa sababu.Ninaamini hata suala hili limetokea kwa sababu maalum pia.Jiulize ni kwa nini jambo hili limetokea sasa? Muda ambao zilibaki siku chache Patrick afunge ndoa na Vero? Huoni kwamba hapa kuna sababu kubwa ya nyie kukutana tena na mambo yakawa hivi yalivyokuwa ?.Happy kama kweli moyo wako unampenda Patrick na kama ndiye mwanaume wa maisha yako tafadhali simama imara katika msimamo wako huo.This is for your own life and your own happiness.” Akasema Margreth “Nimekuelewa Maggy.Naomba nikuhakikishie kwamba ninampenda Patrick na ndiye mwanaume pekee wa maisha yangu .Sintaubadili msimamo wangu,I’ll fight for him.Nitas………..” Happy akanyamaza ghafla akaelekeza macho yake nje.Gari mbili za polisi zilikuwa zinaingia pale mahakamani na nyuma yake kulikuwa na basi la kijani ambalo ni maalum kwa kubebea mahabusu na kuwaleta mahakamani.Happy alibaki ameyakodolea macho magari yale.Alikosa neno la kusema. “Nadhani mahabusu ndio wanaletwa mahakamani” akasema Margreth. Happy bado aliendelea kuyakodolea macho magari yale hadi yaliposimama.Mapigo ya moyo wake yalibadilika na kuanza kwenda kwa kasi kubwa na machozi yakamtoka. “Usilie Happy.Nilifahamu kwamba utaumia sana na ndiyo maana nikakuzuia usije mahakamani siku ya leo.Twende tuondoke maeneo haya.Turudi nyumbani ukapumzike” akasema Margreth “No Maggy,let me stay here.I need to be here .I’m supposed to be here” akasema Happy.Katika mashavu yake ilionekana michirizi ya machozi yakitiririka.Baada ya dakika kama mbili hivi akainamisha kichwa “I’m so stupid !!!..so stupid !!!!....” akasema Happy kwa uchungu huku akikipiga piga kichwa chake. “Calm down Happy…..!!!!” akasema Margreth “Maggy,I’m so stupid” akasema tena Happy kwa sauti ya masikitiko “I’m so stupid Margreth..Mtu aliyeyatoa maisha yake kwa ajili yangu yuko mahakamani lakini ninashindwa kuingia mle ndani na kumuonyesha kwamba niko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake.Nashindwa kuonyesha ushirikiano.I’m real so stupid.” Akasema Happy “You are not stupid Happy.Nakufahamu vizuri dada yangu.You are strong woman.You’ve been and you are always so strong so don’t become weak now.Huu ni wakati unaotakiwa kuwa na ujasiri wa hali ya juu sana.” Akasema Margreth.Happy akafuta machozi akauangalia mlango wa kuingilia mahakamani akakishika kitasa cha mlango wa gari. “Maggy,I cant be such a stupid.Happy isn’t that coward.Naingia mahakamani” akasema Happy huku akiufungua mlango wa gari tayari kwa kushuka.Margreth akamzuia. “Hapana Happy huwezi kushuka.” “Kwa nini Maggy? Kwa nini nisiingie mahakamani? Patrick atajisikiaje asiponiona mahakamani leo? Please Maggy let me go” “Happy,nafahamu umuhimu na ulazima wa wewe kuwepo mahakamani lakini siku ya leo sidhani kama itakuwa vyema uingie mle ndani.Kuna watu wengi leo na hasa waandishi wa habari ambao wanategemea kukuona mahakamani ili wakupige picha na kuzipamba kurasa zao za mbele.Nakushauri siku ya leo usiingie mahakamani badala yake unatakiwa kwenda kumtembelea Patrick gerezani kila mara na hapo ndipo utakapopata nguvu na ujasiri wa kuweza kuikabili hali hii na ndipo utakapoweza hata kuhudhuria mahakamani.Endapo utaingia mle ndani utashindwa kujizuia na utaangua kilio.Utazidi kuumia” Happy akabaki kimya kwa muda wa kama dakika tatu hivi akitafakari “Nahisi kuchanganyikiwa Margreth.Sijui nifanye nini “ akasema Happy “twende tuondoke hapa.Twende turudi nyumbani ukapumzike” “Nadhani hilo ni jambo la msingi kwa sasa.Nirudishe nyumbani nikapumzishe kichwa changu” akasema Happy na Margreth akawasha gari wakaondoka kurejea nyumbani. “Usife moyo Happy ,mambo haya yatakwisha.Tuzidi kumuomba Mungu” Margreth akampa moyo dada yake wakiwa njiani kurejea nyumbani. “Hii ni mara ya pili sasa Patrick anaingia gerezani kwa ajili yangu.Mara ya kwanza aliua bila kukusudia wakati akiniokoa nisidhalilishwe na genge la wahuni.Safari hii ni mimi ndiye niliyesababisha kifo lakini bado ameamua kuubeba mzigo huu wote wa mauaji na sijui hatima yake itakuwa nini.Huu ni upendo wa ajabu sana ambao sijawahi kuuona katika zama hizi.Sielewi ni kwa nini Patrick ananipenda namna hii kiasi cha kufanya haya anayoyafanya .Huu ni zaidi ya upendo ambao hauelezeki kwa maneno.Huyu ndiye mwanaume wa maisha yangu Nitampenda hadi mwisho wa uhai wangu.” Akawaza Happy akiwa amejiinamia. “Nina deni kubwa sana kwa Patrick.Nimefanya kosa kubwa kutokuoenekana mahakamani siku ya leo.Sijui atakuwa amejisikiaje kwa kutoniona mahakamani .Najua alitegemea sana kuniona na ingemfariji sana kuona kwamba tuko pamoja katika wakati huu mgumu.Sintakubali suala kama hili lijitokeze tena.Kuanzia sasa sintaogopa mtu yeyote Yule.Nitasimama imara na Patrick hadi dakika ya mwisho.” Bado Happy aliendelea kuwa na mawazo mengi sana.Safari yao ilikuwa inaendelea kimya kimya. Hatimaye wakafika nyumbani .Mtumishi wa ndani akawafungulia geti wakaingia.Mara tu walipoingia ndani Happy akapatwa na mstuko mwingine baada ya kuliona gari moja dogo jeupe lenye namba za kibalozi likiwa limeegeshwa mle ndani.Mapigo ya moyo yakabadilika na kuanza kumwenda mbio . “Ouh Gosh ! Its Mike.” Akasema Happy huku uso wake ukiwa umebadilika. “Sitaki kuonana na naye kwa sasa.Nitafanya nini Margreth? “Usiogope Happy.Huna haja ya kumkimbia Mike.Onana naye ana kwa ana.” Akasema Margreth. “I’m not ready Margreth .I’m not ready to face him yet” ( siko tayari Margreth.Siko tayari kuonana naye ana kwa ana” “Hakuna namna nyingine ya kufanya Happy zaidi ya kuonana na Mike.Nadhani ni wakati muafaka sasa kwa Mike kuufahamu ukweli halisi.He loves you and he deserve to know the truth”( anakupenda na ana haki ya kuufahamu ukweli” “Not now Margreth.Siko tayari kuongea lolote na Mike kwa sasa” “Ok Happy kama kama hauko tayari kuongea naye lolote kwa saa siwezi kukulazimisha kufanya hivyo lakini hata hivyo twende ndani ukasalimiane naye halafu uende chumbani kwako.Mimi nitaongea naye na kumuelewesha kwamba akusubiri hadi hapo utakapokuwa tayari kuzungumza naye” akasema Margreth.Happy akavuta pumzi ndefu na kuufungua mlango wa gari akashuka. Margreth ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia sebuleni akifuatiwa na Happy.Pale sebuleni alikuwepo mama yao pamoja na Mike.Mara tu Margreth na Happy walipoingia Mike akasimama na sura yake ikaonyesha tabasamu kwa mbali. “Hallo Happy” Mike akamsalimu. “Hallo Mike” Happy akajibu huku akiwa amekiinamisha kichwa chake chini.Mike akamsogelea na kutaka kumshika mkono lakini Happy akausogeza mkono wake ili Mike asiushike. “Unajisikiaje Happy.” Akauliza Mike “Naendelea vizuri .” akajibu Happy “Nafurahi kusikia hivyo.Nimekuwa na wasi wasi mwingi sana juu ya maendeleo yako Happy.Nashindw…” Mike hakumaliza alichotaka kukisema Happy akamkatisha “Mike tutaongea siku nyingine.Nimechoka sana naomba uniruhusu nikapumzike.tafadhali sana naomba unisamehe Mike” akaomba Happy halafu akaanza kutembea kuelekea chumbani kwake. “Happy !!!....akaita Mike.Sura yake ilionyesha huzuni kubwa. “Mike let her go.She need some rest” akasema Margreth. “Margreth ninaumia sana nikimuona Happy akiwa katika hali hii.Sijawahi kumuona hata mara moja Happy akiwa hivi” “Mike !“ akaita Margreth halafu akamsogelea karibu.Mike akageuka na kumtazama “Happy anapita katika kipindi kigumu sana hivi sasa.Ni kipindi kigumu kupita vyote alivyowahi kupitia.Anahitaji kupewa muda wa kutosha wa kutuliza akili yake.Kwa muda huu hataweza kuongea lolote.Nakushauri Mike vuta subira hadi hapo atakapokuwa tayari ametulia na mtakaa mtaongea” akasema Margreth.Mama yake aliyekuwa amesimama karibu yao akakohoa kidogo na kusema “Mike maneno ya Margreth ni ya msingi sana.Happy anahitaji muda wa kupumzisha akili yake.Mambo mengi mazito yamemtokea katika kipindi kifupi kwa hiyo bado anahitaji kuirejesha akili yake katika hali ya kawaida.Nakuomba Mike umvumilie mwenzio hadi hapo atakapokuwa tayari” Mike akainama chini akafikiri kwa muda kisha akasema “Nimesafiri toka Marekani mpaka hapa kwa lengo moja tu la kuwa karibu na Happy katika wakati ambao niliamini alikuwa ananihitaji sana.Nafahamu katika wakati mgumu kama huu Happy anahitaji mtu wa karibu wa kumfariji na kumfanya awe na furaha ndani ya moyo wake.Nashangaa sana kwa Happy kutokuonyesha dalili za kunihitaji katika wakati huu wa matatizo.Inaonekana kama vile ananikwepa” Akasema Mike kwa sauti ya masikitiko. “Mike ninafahamu kwamba unampenda sana Happy na ndiyo maana umesafiri safari hii ndefu kwa lengo la kuwa naye katika matatizo yaliyompata.Ushauri wangu kwako ni kwamba muache Happy apumzike kwa siku ya leo na kesho kama atakuwa yuko vizuri basi mtakaa na kuongea kuhusiana na kinachoendelea hivi sasa.” Akasema mama yake Happy.Mike akainamisha kichwa akafikiri kwa muda halafu akainua kichwa na kusema “Nimekuelewa mama.Nitamuacha Happy apumzike.Nitakuja tena kesho kumtembelea na kujua maendeleo yake.Naomba endapo kutatokea mabadiliko yoyote katika hali yake basi mnitaarifu mara moja ili kwa pamoja tusaidiane namna ya kufanya” Akasema Mike kisha wakaagana akaondoka Margreth akamsindikiza “Margreth,moyo wangu umeumia sana kwa hali ya Happy.Mpaka hapa niko gizani na sielewi chochote kuhusiana na kilichotokea na kumpelekea Happy awe katika hali hii.Margreth unaweza ukanifahamisha japo kwa muhtasari ni kitu gani kilichotokea na kumfanya Happy awe katika hali hii? Kuna huyu mtu aitwaye Patrick ambaye Happy aliwasiliana naye tukiwa kule hotelini tukipata chakula cha mchana na Happy akabadilika ghafla ni nani? Akauliza Mike “Mike sina maelezo yoyote ambayo yanaweza kukutosheleza kwa sasa.Kama mama alivyokushauri msubiri Happy atulize akili yake na atakueleza kila kitu kilichomsibu yeye mwenyewe.”akasema Margreth.Mike akamtazama usoni kwa makini na kumuuliza tena “Kitu gani kinaendelea hapa Margreth? Kuna jambo naona unalifahamu lakini hutaki kunieleza.Unazidi kunipa wasi wasi.Naomba kama kuna kitu unakifahamu kinachomsumbua Happy nieleze ili kwa pamoja tuweze kukitafutia ufumbuzi.” “Mike kama nilivyokwambia kwamba sina chochote cha kukwambia.Mwenye maelezo yote na anayeweza kukueleza kwa ufasasa na kwa kina juu ya kilichompata na kinachomsumbua ni Happy mwenyewe.Kwa hiyo naomba umsubiri yeye mwenyewe hadi hapo atakapokuwa tayari” akasema Margreth. “Nimekuelewa Margreth.Nitakuja tena kesho kumuangalia Happy” akasema Mike na kuingia garini akaondoka. * * * * Basi la kubeba mahabusu likiwa linaongozwa na magari mawili ya polisi liliendelea kuikata mitaa ya jiji hili la Dar es salaam likielekea maeneo ya Kigamboni.Patrick alikuwa mmoja wa mahabusu kumi waliokuwamo katika basi hili,wote walikabiliwa na kesi za mauaji.Wakati wote wa safari macho yake yalikuwa nje akitazama majengo mazuri ya jiji hili pamoja na pilika mbali mbali za kila siku “ Patrick gerezani tena “ akasema kwa sauti ndogo na kisha akainama chini “Sikutegemea kama mambo yangekuwa namna hii.Sikutegemea kama suala hili lingenirejesha tena gerezani” akaendelea kuwaza Patrick huku gari likienda kwa kasi. “Kuna nyakati najiuliza ni kwa nini Happy ametokea tena kwa wakati huu? Baada ya kupita kwa miaka mingi iweje ajitokeze sasa? Yote haya yaliyotokea yametokea kwa sababu ya kuonekana kwake tena.Endapo asingetokea kwa wakati huu yasingetokea haya yote” Akawaza Patrick halafu akainua kichwa akatazama nje “Kuna kitu kimoja ambacho kinanifanya niamini kwamba kutokea kwa Happy katika wakati huu ni kwa sababu maalum.Ilipangwa iwe hivi.Japokuwa vikwazo ni vingi lakini ni ukweli usiopingika kwamba mimi na Happy tumepangiwa tuwe pamoja na kamwe hatuwezi kutenganishwa.Vero hakuwa amepaumbwa kwa ajili yangu na ndiyo maana yametokea haya yaliyotokea.Ninaamini hivyo kwa sababu ya upendo mkubwa uliopo kati yangu na Happy.Licha ya kutengana kwa miaka mingi lakini tumeonana tena na kujikuta tukiwa bado tunapendana tena kwa kiwango kikubwa sana na ndiyo maana kwa pamoja mioyo yetu ilikuwa tayari hata kuachana na wapenzi wetu wa sasa kwa lengo moja tu la kuwa pamoja tena.Lakini pamoja na hayo yote bado kuna kitu kinachotutenganisha mimi na Happy.Hata hivyo kwa vyovyote vile itakavyokuwa sintabadili msimamo wangu.Nitasimama katika maamuzi yangu.Happy ndiye mwanamke pekee ambaye ninamuhitaji katika maisha yangu.Niko tayari kwa lolote lile hata kama ni kuhatarisha maisha yangu kwa ajili yake.Sitaki kuuficha ulimwengu juu ya mapenzi yangu mazito kwa Happy.Kwa wale wanaofahamu nini maana ya mapenzi ya kweli wataungana nami na kusimama upande wangu lakini wale wasioelewa maana ya penzi la kweli watanichukia ,watanibeza na kunilaani.Nitaubeba mzigo wa lawama ,chuki na laana zote nitakazopewa kwa sababu ya upendo wangu kwa Happy ulionipelekea nikafanya maamuzi haya niliyoyafanya.” Akawaza Patrick na mara sura ya Happy ikamjia kichwani, akatabasamu “ I love you Happy and I will always love you my angel”( Nakupenda Happy na nitakupenda daima malaika wangu) akasema kimoyomoyo.Kwa sasa gari lilikuwa linalivuka daraja kuelekea Kigamboni liliko gereza kubwa la Uwangwa gereza ambalo hutumika kuwahifadhi watu wenye kesi kubwa kubwa hasa za mauaji.Kupitia dirishani Patrick aliweza kushuhudia namna watu walivyokuwa wakiendelea na shughuli zao za kiuchumi baharini. “Mida hii nilipaswa niwe kazini nikiendelea na shughuli zangu kama watu wengine lakini niko garini naelekea gerezani.Mipango na malengo yangu yote ya maisha vimepotea.Sijilaumu kwa kilichotokea kwa sababu naamini ilipangwa iwe hivi.Nimefanya haya yote kwa sababu ya mwanamke ninayempenda kuliko wote duniani” akawaza Patrick na kuendelea kutazama nje huku gari likiendelea na safari yake kwa kasi. “Nasikitika sana kwa kifo cha Vero.Sikutegemea kama suala hili lingesababisha Vero apoteze uhai wake.Inauma sana lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuusikia moyo wangu na kuufuata.Moyo wangu umeniambia kwamba Happy ndiye mwanamke wa maisha yangu na siku zote moyo wangu huwa haunidanganyi.Hata hivyo kifo cha Vero kimeniumiza sana.Tukio hili ni moja kati ya matukio ambayo hayatafutika katika historia ya maisha yangu hadi naingia kaburini.” Akawaza Patrick.Sura ya Vero ikamjia akainamana na kufuta machozi. “Bado nazikumbuka zile nyakati zetu za furaha enzi za uhai wake.Tulipendana sana na sikutegemea hata kidogo kwamba mwisho wetu ungekuwa namna hii.Inaniuma sana na siku zote nitaendelea kumkumbuika .Vero ni mwanamke ambaye nimetoka naye mbali toka nikiwa gerezani Songea.Alinisaidia sana wakati ule nikiwa gerezani .Alinifanya nisiyaone magumu maisha ya gereza.Hata wakati ule nilipoamini kwamba Happy amenisaliti bado Vero alisimama nami ,akanifariji na kunifanya nitake kuishi tena.Baada ya kutoka gerezani alijitahdi kwa kila alivyoweza kuhakikisha kwamba ninayaanza upya maisha yangu.Amekuwa na mchango mkubwa sana katika kuyajenga upya maisha yangu na ninaweza kusema kwamba ni mmoja kati ya watu waliochangia sana mimi kufika hapa nilipofika.Siku zote yeye ndiye alikuwa mfariji wangu,mshauri wangu na msimamizi wangu katika kila jambo ninalolifanya.Sina shaka na upendo wake kwangu.Vero alinipenda kwa moyo wake wote na alikuwa tayari kufanya lolote na kwa wakati wowote kwa ajili yangu.Nini kimetokea hadi yakatokea haya yaliyotokea?!!!...” Patrick akainama chini kichwa chake kilijaa mawazo na macho yake yalikuwa na machozi. “ Nilimpenda sana Vero lakini Kosa moja tu alilolifanya ni kutunga ule uongo na kunitenganisha na Happy.Alifanya hivi bila kufahamu kwamba mimi na Happy ni watu ambao hakuna awezaye kututenganisha zaidi ya Mungu pekee.Tunapendana kwa dhati ya mioyo yetu na tayari mioyo yetu imekwisha ungana.Ouh Vero …..!!!!!” Patrick alisikia maumivu ya moyo kana kwamba kuna kisu kikali kinaukata.Wakati huo gari lilikuwa linamalizia kulivuka daraja la Kigamboni. “Kwa nini Happy hajatokea mahakamani leo? Nilitegemea kumuona akiwa miongoni mwa watu waliokuja kusikiliza kesi yangu ikitajwa.Ningefarijika sana kama ningeiona sura yake.Inawezekana hakutokea mahakamani kwa sababu kuna jambo limemsibu.Inawezekana akawa ni mgonjwa.Ninamfahamu vizuri Happy asingeweza kukosa mahakamani leo lazima kuna jambo linamsumbua .Au inawezekana akawa anakwepa macho ya watu na waandishi wa habari ambao wengi walitegemea kumuona mahakamani leo.Maskini Happy ameingia katika matatizo makubwa.Tayari alikuwa na maisha yake mazuri yaliyotulia,alikuwa na machumba wake anayempenda, alikuwa na ndoto nyingi za maisha yake lakini baada tu ya kukutana na mimi ndoto zake zote zimepotea.Nasikitika sana kwa jambo hili.Hana muda mrefu toka amelitwaa taji la Miss Tanzania lakini katika kipindi hiki kifupi tayari amekwisha tengeneza vichwa vya habari kwa kuhusika kwake na tukio la kifo cha Vero.Sifa yake kama mrembo wa Taifa imepotea na kwa mara nyingine historia imejirudia kwa warembo wanaovishwa taji hili la kuingia katika kashfa .Simlaumu Happy kwa alichokifanya .Alikuwa akilipigania penzi lake la kweli .Alimsukuma Vero kwa lengo la kuniokoa mimi kwani ni wazi Vero alikuwa na kila dalili za kufanya tukio baya” Bado Patrick aliendelea kuwaza mambo mengi kuhusiana na tukio lile lililopelekea kifo cha Vero na yeye kukabiliwa na kesi ile ya kusababisha kifo.Kwa sasa gari lile la mahabusu lilikwisha ishika njia ya kuelekea gerezani. “Japokuwa kuna watu ambao hawakubaliani moja kwa moja na maamuzi yangu ya kumtoa Happy katika kesi hii ambayo ilikuwa imkabili yeye na mzigo wote kuubeba mimi,bado sijutii kufanya hivyo hata kidogo kwa sababu hata siku moja sintakubali mwanamke nimpendaye aingie gerezani.Niko tayari kwa adhabu ya aina yoyote ile lakini si kumuona Happy akiteseka gerezani.Nitaipokea adhabu hiyo kwa mikono miwili kwa sababu nitakuwa nimeibeba adhabu ambayo alistahili kuibeba mwanamke ninayempenda kuliko wanawake wote duniani.” Gari lilipunguza mwendo na kusimama.Akachungulia nje walikuwa wamesimama katika geti la kwanza la kuingilia hapo gerezani. “Nakumbuka Savanna hakukubaliana nami kabisa katika uamuzi wangu huu wa kumtoa Happy katika kesi hii na jukumu lote kulibeba mimi.Nalikumbuka swali aliloniuliza kama je Happy naye yuko tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili yangu kama mimi nilivyofanya kwake? Patrick akanyanyua kichwa akatazama nje.Gari liliruhusiwa kupita na kuendelea na safari ya kuelekea gerezani. “Swali kama Happy yuko tayari kufanya kama nilivyofanya mimi ni swali gumu sana kulipatia jawabu lakini sina shaka na Happy.Japokuwa siwezi kuusemea moyo wake lakini nina uhakika kwamba anaweza akafanya lolote kwa ajili yangu kama alivyokubali kuuvunja uhusiano wake na mchumba wake kwa lengo moja tu la kuwa nami.Ninaamini ananipenda kwa dhati ya moyo wake .Patrick akawaza,akainua kichwa akatazama juu halafu akaninama tena chini. “Sijui hali ya baba ikoje huko hospitali.Nimewaumiza watu wengi kwa maamuzi yangu.Kwanza ni familia yangu.Baba hali yake si nzuri hata kidogo.Ndugu zangu,marafiki wameumizwa sana na kitendo hiki cha kuuvunja uchumba wangu na Vero.Familia ya vero nayo imeumizwa sana kwanza kwa kuuvunja uchumba na mtoto wao na pili kwa kusababisha kifo cha binti yao.Ninaamini kamwe hawataweza kunisamehe kwa jambo hili.Familia ya Happy pia imeumizwa sana na jambo hili.Mtoto wao ameingia katika kashfa nzito ya kusababisha mauaji wakati wa ugomvi wa kimapenzi.Jina lake limechafuka.Hawakutegemea hata siku moja mtoto wao waliyemlea katika maadili aingie katika kashfa kubwa kama hii.Yote haya yamesababishwa na mimi.Mchumba wa Happy aitwaye Mike sifahamu atakuwa katika hali gani akiufahamu ukweli kwani sina hakika kama tayari Happy amekwisha muweka wazi kwamba uhusiano kati yao umefika mwisho.kwa ujumla nimeumiza watu wengi sana.Rafiki zangu walijitolea michango mingi mikubwa ili kuhakikisha kwamba harusi yangu inakuwa ya kihistoria .Wote hawa wameumizwa kwa kiwango cha juu kabisa na nina hakika itawachukua muda mrefu sana kunisamehe lakini pamoja na hayo sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuchukua maamuzi haya magumu niliyoyachukua kwa ajili ya kuipigania furaha ya maisha yangu.Siku zote yanapofanyika maamuzi magumu lazima wawepo watu watakaoathirika na maamuzi hayo na ndiyo maana yakaitwa ni maamuzi magumu.Natakiwa nisimame katika maamuzi yangu na nionyeshe msimamo japokuwa si kazi rahisi hata kidogo na inahitaji ujasiri mkubwa sana lakini hata hivyo lazima nifanye hivyo.Haya ni maisha yangu na ninachokipigania hapa ni furaha ya maisha yangu.Pumzika kwa amani Vero.Nitakukumbuka siku zote za maisha yangu na nina hakika huko uliko utanisamehe” Akawaza Patrick na kuyafuta machozi. Tayari gari lilikwisha fika gerezani.Mlango ukafunguliwa na mahabusu wote wakashushwa garini na kuingizwa gerezani * * * * Akionekana ni mwenye haraka Savanna akawaaga mawakili wenzake ambao kwa pamoja wanamtetea Patrick kisha akaingia katika gari lake ,akaliweka lundo la vitabu na nyaraka katika kiti cha pembeni akaufunga mkanda akawasha gari na kuondoka maeneo ya mahakamani. “Nitaisimamia kesi hii hadi nihakikishe Patrick anashinda.Ni kesi ambayo haiwezi kunisumbua hata kidogo.Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba Patrick hafungwi.Patrick ni mtu wa muhimu sana kwangu .Nakumbuka wakati tukiwa bado na mahusiano ya kimapenzi alinipa penzi la kiwango cha juu mno na kumfanya awe ni mwanaume wa pekee kabisa kwangu.Anajua kupenda ,anajali,na anafahamu mwanamke anahitaji nini toka kwa mwanaume.Nathubutu kusema kwamba sijaona wa mfano wake.Japokuwa tulisitisha mahusiano yetu baada ya mimi kumpata George lakini mpaka leo hii sijaweza kumsahau hata kidogo.Kuna nyakati nikiwa nafanya mapenzi na George ninahisi kama ninaiona sura ya Patrick na mara kadhaa nimewahi kujisahau na kulitamka jina la Patrick kutokana na kuhisi uwepo wake karibu yangu.Wakati mwingine ili nipate hisia za kimapenzi lazima niivute taswira ya Patrick ndipo ninasisimka.Bado nampenda na sijafanikiwa kumtoa moyoni mwangu.Huu ni wakati wangu wa kumrudisha Patrick kwangu na kitu kikubwa kitakachonifanya nimrejeshe kwangu ni namna nitakavyomjali na kumpigania katika wakati huu mgumu .Anahitaji mtu wa kuwa naye karibu katika kipindi hiki na mtu huyo lazima niwe mimi.Nitakuwa naye karibu nitamfariji,na mwishowe atakuwa wangu tena.” Akawaza Savanna akiwa garini. “Kwa nini Happy hajatokea mahakamani leo? Sina hakika kama anampenda Patrick kiasi cha kuweza kuyatoa maisha yake kama Patrick alivyofanya..Nikitoka hospitali nitakwenda kujua nini kimemsibu na kwa nini hakufika mahakamani siku ya leo.Nimeanza kuwa na wasi wasi sana na huyu Happy na nina imani baada ya muda si mrefu Patrick atakijutia kitendo chake cha kuubeba mzigo alioustahili Happy ambaye ameshindwa hata kufika mahakamani kuonyesha kwamba anajali.” Akawaza Savanna Ilimchukua Savanna takribani saa moja kufika katika hospitali kuu ya magonjwa ya moyo alikolazwa baba yake Patrick.Akashuka garini na kutembea kwa kasi kuelekea katika vyumba vya wagonjwa walio katika uangalizi maalum.Kwa mbali akamuona Alois kaka yake Patrick akiwa nje akamsogelea.Alois alipomuona Savanna akakatisha maongezi na mtu aliyekuwa akiongea naye simuni. “Hallo mheshimiwa “ Alois akamsalimu Savanna.Huku akitabasamu Savanna akasema “Ouh Alois niite Savanna inatosha sana.”akasema Savanna “Karibu sana Savanna.” “Ahsante Alois” akajibu Savanna halafu kikapita kimya kifupi “Alois tulionana kule mahakamani lakini hatukupata wasaa wa kuzungumza lolote .Pilika pilika zilikuwa nyingi sana.” Akasema savanna. “Usijali Savanna,hata mimi niliona namna ulivyokuwa na shughuli nyingi.Ninafahamu ugumu uliopo katika kusimamia kesi kubwa kama hizi na ndiyo maana sikutaka kukusumbua.Hata hivyo Savanna naomba nikushukuru sana kwa kuamua kulibeba jukumu hili la kumtetea Patrick katika kesi hii ngumu” akasema Alois “Ahsante Alois.Kesi inayomkabili Patrick ni kesi ngumu sana ,ni kesi ya mauaji lakini nitajitahidi kufanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba Patrick anashinda kesi hii” “Savanna,sisi kama familia tuko pamoja nawe na tuko tayari kulipa gharama zozote zile zinazohitajika katika kesi hii.” “Patrick ni mtu wangu wa karibu sana na nimeamua kuifanya kazi hii bila malipo yoyote yale.Kitu pekee nitakachokihitaji toka kwenu kama familia ni kumpa Patrick ushirikiano mkubwa katika wakati huu.Mambo yote yaliyotokea na kusababisha tofauti katika familia naomba muyaweke pembeni kwa wakati huu.Kwa pamoja tutashinda jambo hili” akasema Savanna “Usihofu kuhusu hilo Savanna.Patrick ni ndugu yetu na pamoja na yote aliyoyafanya lakini hatutaweza kumuacha.Tutatoa kila aina ya ushirikiano unaohitajika .Vipi kuhusu Yule binti Happy,mbona sijamuona mahakamani leo? Akauliza Alois “Hata mimi sifahamu ni kwa nini hajatokea mahakamani leo” “Savanna,sielewi ni kwa nini kila mara Patrick anapokuwa na huyu Happy lazima jambo baya limfike.Mara ya kwanza aliwahi kufungwa gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia akiwa na huyu huyu Happy.Safari hii amefanya tena kosa lile lile la mauaji akiwa na huyu huyu Happy.Ninahisi msichana huyu ana mkosi na ndiyo maana kila mara lazima mambo mabaya yamfike Patrick.Kitu kingine,sielewi ni kwa nini ameibuka katika wakati huu ambao tayari maisha ya Patrick yametulia na alikuwa anakaribia kufunga ndoa na Vero.Kuibuka kwake kumeharibu kila kitu ikiwamo na maisha ya Patrick.Vero amefariki na Patrick anakabiliwa na mashtaka ya mauaji..Ninamchukia sana Happy na sitaki hata kuonana naye uso kwa uso kwani ninaweza kughafirika na kufanya jambo baya linaloweza kuniletea matatizo.Naomba Mungu aniepushe kabisa nisikutane na Yule mwanamke uso kwa uso na hasa katika siku hizi za karibuni.” Akasema Alois kwa hasira. “Alois,mambo haya yamekwisha tokea na hatupaswi kulaumiana kwa sasa.Tunachotakiwa kukifanya ni kukabiliana na hali halisi iliyojitokeza.Si Patrick wala Happy aliyetegemea wala kupanga kwamba kingetokea kifo cha Vero.Hakuna aliyejua kama mambo haya yangefika hapa yalipofika.” “Nakubaliana nawe Savanna lakini moyo wangu unauma sana kwa jinsi huyu Happy alivyomuweka ndugu yangu katika matatizo makubwa.Sina hakika kama nitaweza kumsamehe .Si mimi tu bali hata familia yote kwa ujumla.Yeye ndiye chanzo cha haya yote.Ametusababishia jeraha kubwa ambalo litachukua muda sana kupona” akasema Alois “Alois huna haja ya kumchukia Happy.Kama nilivyokueleza kwamba si Patrick wala Happy aliyetegemea kama jambo kama hili litatokea na kufika hapa yalipofika.Tuachane na hayo,nimekuja kujua hali ya mzee anaendeleaje? “Hali ya mzee si nzuri hata kidogo.Baada tu ya kutoka mahakamani tulitaarifiwa kwamba hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya.Muda mfupi uliopita amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.Kwa ufupi hali yake bado si nzuri hata kidogo.Hapa tunasubiri madaktari watueleze nini kinaendelea.Tunafikiria hata kufanya mpango wa kumpeleka nje ya nchi lakini endapo italazimika kufanya hivyo.Mama na ndugu wengine wako kule ndani mimi nimechomoka mara moja kwa ajili ya kuja kupiga simu.” Akasema Alois “Dah ! Poleni sana Alois.” Akasema Savanna halafu kikapita kimya kifupi Savanna akasema “Alois kwa kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ni taarifa ya madaktari kuhusiana na maendeleo ya mzee,mimi naona niondoke nikaendelee na shughuli nyingine.Utanifahamisha kuhusu maendeleo yake” Akasema Savanna na kubadilisha namba za simu na alois. “Usihofu Savanna,lolote litakalotokea nitakutaarifu mara moja” akasema Alois kisha wakaagana na Savanna akaondoka. “Kwa namna nilivyoiona sura ya Alois ,inaonyesha hali ya baba yake katu si nzuri.Mungu amsaidie mzee Yule apone haraka kwa sababu endapo ikatokea akafariki dunia mambo yatazidi kuwa mabaya sana kwa Patrick.” Akawaza Savanna wakati akiligeuza gari lake na kuondoka maeneo ya hospitali. “Kwa sasa ngoja nikaonane na Happy nifahamu nini sababu iliyomfanya ashindwe kufika mahakamani siku ya leo.Nilikuwa namtazama Alois machoni wakati akiongea kuhusiana na namna anavyomchukia Happy,hakuwa akitania hata kidogo.Ni wazi anamchukia mno Happy toka moyoni.Suala hili linazidi kuchukua sura mpya kila uchao.Kwa hivi sasa mambo haya yatahamia katika famila.Chuki kubwa itajengeka baina ya familia hizi .Familia ya Happy katu haitaweza kutazamana na familia ya Patrick na ile ya Vero katu hawatakuja kuelewana na ile ya Patrick.Dah.!!....” akawaza Savanna na mara simu yake ikaita.Akatazama mpigaji alikuwa ni George “I’m sorry George,siwezi kupokea simu yako kwa sasa.” Akasema Savanna na kuirusha simu pembeni.Simu ikaendelea kuita lakini hakusumbuka hata kuitazama tena. “George aliniudhi sana kiasi kwamba sihitaji hata kuiona sura yake tena .Kwa sasa akili yangu yote nimeielekeza katika kitu kimoja tu.Kumsaidia Patrick ashinde kesi.Pamoja na kushinda kesi hii lakini nina kazi nyingine ngumu ya kumrudisha Patrick katika himaya yangu tena.Yeye ni mwanaume pekee ambaye aliwahi kunifikisha mawinguni kwa raha alizokuwa akinipa.Naapa pamoja na ugumu wote uliopo nitamrejesha kwangu.Najua moyo wake umekufa ukaoza kwa Happy lakini hii hainipi shida hata kidogo.Nitafanya kila niwezalo kumrejesha kwangu tena” akawaza Savanna * * * Mlio wa kengere ya getini ulimfanya Margreth ainuke sofani na kwenda kuangalia mtu aliyekuwa akigonga.Hakuamini alipokutana na msichana mmoja mrembo na wakili maarufu,Savanna “Dada Savanna !!..shikamoo” akasema Margreth “Marahaba Margreth.Habari yako? “Habari yangu nzuri dada ” Akasema Margreth huku akilifungua geti na Savanna akaingiza gari ndani “Karibu sana dada Savanna,karibu ndani” akasema Margreth akimuongoza Savanna kuelekea ndani “Pole na matatizo dada ” akasema Margreth huku akimuwekea Savanna kinywaji mezani “Nimekwisha poa Margreth.Poleni nanyi pia.Matatizo haya ni yetu sote.” “Ahsante dada Savanna.” Akajibu Margreth halafu kikapita kimya kifupi.Savanna akasema “Happy anaendeleaje? Sijamuona leo mahakamani.Patrick alipatwa na wasi wasi sana na akaniomba nifike nijue kilichomsibu” akasema Savanna “Dada Savanna hali ya Happy si nzuri hata kidogo na ndiyo maana hata leo alishindwa kuingia mahakamani japokuwa alikuwepo pale mahakamani.Nadhani itakuwa vyema kama nitakupeleka chumbani kwake ukaongee naye wewe mwenyewe.” Akasema Margreth na kumuongoza Savanna kuelekea chumbani kwa Happy “Karibu sana Savanna” akasema Happy akiwa amekaa kitandani.Macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba kwa kulia.Nywele zake ndefu na nzuri zilikuwa zimetawanyika.Kwa ujumla alitia huruma sana mnyange huyu wa Taifa. “Pole sana Happy” akasema Savanna “Nimekwisha poa Savanna” “Happy mimi si mkaaji sana,nimepita mara moja kujua hali yako baada ya kutokuona mahakani leo .Patrick alipatwa na wasi wasi mwingi na akanituma nifike nijue hali yako na kama kuna jambo limekusibu” akasema Savanna “Savanna nilifika mahakamani leo lakini nilishindwa kuingia ndani ya mahakama” akasema Happy “Kwa nini Happy? Akauliza Savanna “Niliogopa kukutana na macho ya watu pamoja na waandishi wa habari.Niliogopa vile vile kukutana na ndugu za Patrick ambao sijui wangenitazamaje kwani moja kwa moja wanafahamu kwamba mimi ndiye chanzo cha matatizo yote yanayomkuta mtoto wao.Najua Patrick atakuwa na mawazo mengi sana kwa kutoniona mahakamani leo .I’m so stupid Savanna….I’m so stupid “ akasema Happy kwa masikitiko.Savanna akamtazama kwa makini na kusema “Sikiliza Happy,huu si wakati wa kujilaumu kwa kilichotokea.Si wewe wala Patrick aliyetegemea mambo haya kufika hapa yalipofika.Yaliyotokea yameshatokea na hatupaswi kushughulika nayo ila tunachopaswa kushughulika nacho kwa sasa ni athari zilizotokana na kilichotokea.Patrick kwa upande wake tayari amekubaliana na kilichotokea na ndiyo maana ameamua kulibeba jukumu zima ambalo ulistahili ulibebe wewe,kwa hiyo basi nakushauri na wewe usimame imara na usimamie kile kilichowapelekea mkafika hapa mlipofika kwa ujasiri mkubwa.Ikabili jamii na usiogope kitu chochote kile.Usiogope kwamba utaonekanaje kwa kuivaa kofia hii ya Miss Tanzania.Kofia hii ni ya kupita tu kwa maana hiyo usiogope kupigwa picha ukiwa mahakamani ukisikiliza kesi ya Patrick.Kuanzia sasa futa machozi na usimame imara.Kumbuka utakuwa ni mmoja wa watu watakaosimama mahakamani kutoa ushahidi wao kwa hiyo jitahidi kuanzia sasa uwe jasiri” Maneno yale ya Savanna yalimuingia Happy vilivyo.Akainama akatafakari “Tumeelewana Happy ? akauliza Savanna “Savanna nakushukuru sana kwanza kwa kuja kunitembelea.Ujio wako na maneno yako machache yenye nguvu vimenifanya nipate nguvu mpya.Nakuahidi sintalia tena.Nitasimama imara kumtetea Patrick.Siku zote nitakuwa karibu yake na kumpa moyo kwa sababu ameubeba mzigo mzito ulionistahili mimi.Nimefanya kosa kubwa sana kutokuingia mahamani leo .Savanna naomba uniombee msamaha kwa Patrick kwa kitendo hiki.Nilikuwa dhaifu sana kukabiliana na hali halisi” akasema Happy huku kwa mbali machozi yakimlenga. “Usijali Happy,nitamuelewesha Patrick na atakuelewa ,ila kumbuka kuyafanyia kazi hayo niliyokwambia..Patrick needs you now more than ever.Anahitaji ushirikiano wetu sote kwa wakati huu .Kila mmoja kwa upande wake anatakiwa aonyeshe ushir…………………….” Savanna akanyamaza ghafla kutokana na mlio wa simu yake.Akaitoa na kutazama mpigaji alikuwa ni Alois kaka yake Patrick.Savanna akamtazama Happy usoni huku simu yake ikiendelea kuita. “It’s Alois “ akasema Savanna kwa sauti ndogo “Pokea usikie anataka kukueleza kitu gani.” Akasema Happy.Savanna akavuta pumzi ndefu halafu akabonyeza kitufe cha kupokelea simu. “Hallo Alois “ akasema Savanna baada ya kupokea simu.Baada ya sekunde kadhaa taratibu Savanna akajikuta akishusha mkono wenye simu chini.Sura yake ilikuwa imebadilika ghafla. “Ouh My God !! “ akasema Savanna na kuzidi kumuogopesha Happy “Savanna kuna tatizo gani? Akauliza Happy ambaye alistushwa sana na mabadiliko yale ya ghafla ya Savanna aliyekuwa amesimama huku mkono wake wa kulia ukiwa kifuani . “Savanna kuna tatizo gani? Mbona umebadilika ghafla.Kuna taarifa gani toka kwa Alois? Is Patrick ok? Akauliza Happy. “Baba yake Patrick amefariki” akasema Savanna.Happy akaishiwa nguvu akajikuta akikaa kitandani. “Ouh Mungu wangu ,mambo haya yanazidi kuwa makubwa kila siku” akasema Happy kwa wasi wasi Savanna akiwa bado chumbani kwa Happy simu yake ikaita tena.Safari hii alikuwa ni Andrew. “Hallo Andrew..!!” akasema Savanna baada ya kupokea simu “Savanna kuna taarifa mbaya imenifikia sasa hivi.baba yake Patrick amefariki dunia.” Akasema Andrew. “Hata mimi nimezipata taarifa hizo muda si mrefu .Alois amenipigia kunitaarifu kuhusu msiba huo.kwa sasa uko wapi? “Niko ofisini kwangu lakini baada ya kupata taarifa hizi ninaelekea hospitali kupata uhakika zaidi na kujua nini kinachoendelea” “Sawa Andrew hata mimi nakuja huko hospitali” akasema Savanna na kukata simu halafu akamfuata Happy pale kitandani. “Happy naomba tafadhali usihuzunike sana wala kupata mstuko kwa jambo hili.Tulia na muombe Mungu akupe nguvu ya kuweza kuhimili mambo haya na yote yatakayokuja kwani hatujui nini kitatokea huko mbeleni.Hiki ni kipindi kigumu sana kwako ,kwa Patrick na kwetu sote.Endapo utakuwa na tatizo lolote lile nipigie simu haraka sana nitakusaidia.Kwa sasa ngoja nielekee hospitali ili kujua kinachoendelea huko.Akasema Savanna. “Ahsante sana Savanna.Nashukuru kwa kuja kunitembelea na kunipa moyo.Nitazidi kumuomba Mungu anipe nguvu na kwa pamoja tuweze kukipita kipindi hiki kigumu sana.Kuhusu kifo hiki cha baba yake Patrick nimeshindwa nifanye nini,siwezi kulia wala kufanya lolote.Yote namuachia Mungu” akasema Happy kwa majonzi “Usilie tena Happy.Kuwa jasiri .Mkabidhi Mungu matatizo yako yote naye atakushindia” akasema Savanna “Savanna siwezi kukusindikiza.Miguu yangu haina nguvu hata ya kuinuka “Akasema Happy ,akaagana na Savanna akatoka mle chumbani akaelekea sebuleni ambako alimkuta Margreth “Margreth ,tafadhali naomba uwe karibu sana na Happy ,anapitia kipindi kigumu sana hivi sasa na anahitaji uangalizi wa karibu mno.Tumepata taarifa mpya muda si mrefu baba yake Patrick amefariki dunia kwa shinikizo la damu.Taarifa hii imemstua sana Happy kwa hiyo naomba uwe karibu naye sana kumpa moyo.” Akasema Savanna.Margreth naye alistushwa sana na taarifa ile ya kifo cha baba yake Patrick.Baada ya maongezi mafupi na Margreth,Savanna akaondoka kuelekea hospitali. “mambo yanazidi kuwa mambo.Suala hili limewaumiza watu wengi hadi hivi sasa.Sifahamu hatima yake ni nini kwani nina hakika chuki inazidi kuongezeka miongoni mwa familia hizi hasa baada ya kifo cha baba yake Patrick leo.Familia ya Patrick itaongeza chuki dhidi ya Happy kwa madai kwamba yeye ndiye chanzo cha haya yote yaliyotokea..Namuonea huruma sana Happy,yuko katika wakati mgumu mno.Patrick naye sijui atazipokeaje taarifa hizi za kifo cha baba yake.Najua ataumia mno” Akawaza Savanna akiwa njiani kuelekea hospitali kuu ya magonjwa ya moyo ili kukutana na ndugu za Patrick “Bado sijapata taarifa zozote kuhusiana na msiba wa Veronika.Najua Patrick angependa afahamu kinachoendelea kule.Kuna wakati hata mimi najikuta nikiogopa kila nikifikiria jinsi Patrick, Happy pamoja na familia zao walivyo katika wakati mgumu.” Akawaza Savanna * * * “Nilimuonya Patrick mapema sana kuhusiana na athari za jambo hili lakini alinipuuza na akaendelea na harakati zake za kuurejesha uhusiano wake na Happy.Nilifahamu mambo kama haya yangeweza kujitokeza kwa sababu uhusiano wake na Vero tayari ulikwisha kuwa mkubwa na kuota mizizi.Patrick hakutaka kunisikiliza.Laiti angenisikia mambo haya yote yasingetokea” akasema Andrew kwa masikitiko akiwa amesimama na Savanna pale katika hospitali kuu ya moyo.Vilio vya akina mama vilitawala eneo hili.Ilikuwa ni hali ya simanzi kubwa. “Andrew huu si wakati wa kulaumiana kwa kilichotokea.Hakuna kati yao aliyefahamu kama mambo haya yangefika hapa yalipofika.” Akasema savanna “ Savanna sikufichi mimi ni mmoja wa watu walioumizwa sana na kitendo hiki alichokifanya Patrick cha kuachana na Vero.Siwezi kuelezea nimeumia kiasi gani lakini naomba ufahamu kwamba nimeumizwa mno.Patrick ni rafiki yangu mkubwa sana lakini kwa hili alilolifanya nitazidi kumlaumu kila siku na pengine baada ya mambo haya kumalizika itanilazimu kuangalia upya kama nitaweza tena kuendelea na urafiki naye.Amekuwa ni mtu asiyetaka ushauri wa mtu yeyote yule .Nilimshauri sana na kumuonya kuhusiana na Yule mwanamke Happy lakini hakunisikia.Yote haya yamesababishwa na Happy. Kama asingejitokeza kwa wakati huu tusingekuwa katika matatizo haya tuliyomo sasa hivi.Namchukia sana Happy.Ninamchukia sana..!!!” akasema Andrew. “Andrew,sote tumeumizwa na kitendo cha Patrick kuachana na Vero lakini hatupaswi kuelekeza lawama zote kwa Patrick au kwa Happy.Sote tunafanya makosa hapa duniani na sioni sababu ya kila mmoja kuelekeza chuki zake kwa Happy.Kila mtu ninayekutana naye anasema anamchukia Happy nani atakayesimama na kumtetea ? Nani yuko tayari kumsikiliza? Tusiwe wepesi wa kuhukumu namna hii.Hata yeye hakujua kama mambo haya yangetokea.Nawaombeni msimchukie Happy” Akasema Savanna halafu kikapita kimya kifupi “Vipi una taarifa zozote kuhusiana na msiba wa Vero? “Nilipanga niende leo ili kujua taratibu za mazishi zikoje.Nilitegemea pengine kungekuwa na ujumbe wa watu toka kwa familia ya akina Patrick kwenda kuwakilisha katika mazishi na kupeleka salamu za pole lakini kutokana na jambo lililojitokeza la kifo cha mzee sidhani kama hilo litawezekana tena.” Akasema Andrew “Andrew kuna ulazima wa kutuma wajumbe kwenda kwa akina Vero kwani tayari familia hizi zilikwisha unganishwa na upendo uliokuwepo baina ya watoto wao.Hivi sasa kumetokea aina fulani ya chuki iliyoanza kujengeka miongoni mwa familia hizi mbili.Tusiache hilo litokee Andrew.We have to do something” akasema Savanna “Tutafanya nini Savanna? Mambo haya ni ya kifamilia na hatupaswi kuingilia ugomvi wa familia hizi mbili.” “Andrew,Patrick ni mtu wetu wa karibu kwa maana hiyo hatupaswi kuwa waoga ,tunachotakiwa kufanya ni kuishawishi familia yake wakubali kutuma ujumbe kwa akina Happy ili kwenda kuwaunga mkono na kupeleka salamu za pole,hii itasaidia sana katika kupunguza chuki na uhasama vilivyoanza kujengeka kutokana na tukio hili .Alois yuko wapi? Akauliza Savanna.Andrew akayaelekeza macho yake katika kundi la akina mama waliokuwa wakilia huku madaktari na wauguzi wakiendelea na jitihada za kuwanyamazisha kwani eneo lile halikuhitaji kelele. “Inasikitisha sana “ akasema Savanna “Inauma Savanna.Bado nitaendelea kumlaumu sana Patrick kwani yeye ndiye chanzo cha haya yote.Amesababisha maumivu kwa watu wengi.” Akasema Andrew.Magari matatu yakasogezwa karibu na akina mama wale waliokuwa wakilia,wakaombwa waingie katika magari yale na kuondolewa pale hospitali.Alois ambaye alikuwapo karibu na magari yale aliwaona Andrew na Savanna akawafuata “Pole sana Alois “ wakasema kwa pamoja “Ahsanteni sana.Ni kazi ya Mungu ambayo hakuna mwanadamu anayeweza kuipinga.Tunapaswa kushukuru kwa kila jambo kwani yeye ndiye mwenye kutoa na kutwaa” akasema Alois “kwa kweli hali ya mzee haikuwa nzuri hata kidogo .Tulikuwa na mpango wa kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi lakini madaktari walinihakikishia kwamba hali ya mzee haikuwa na tumaini la kupona kwani hata kama angepelekwa nje ya nchi uwezekano wa kupona ulikuwa mdogo sana.” Akasema Alois “Poleni sana Alois.Inauma sana jamani.” Akasema Savanna kwa huzuni.Kikapita kimya cha muda mfupi “Kwa hiyo nini kinaendelea hapa kwa sasa? Akauliza Andrew “Kwa sasa kinachoendelea ni maandalizi ya shughuli za msiba pale nyumbani kwa mzee.Tunasubiri baada ya ndugu kukusanyika wote tutakaa na kupanga taratibu zote za mazishi .Mpaka sasa bado tunaendelea kusambaza taarifa hizi kwa ndugu jamaa na marafiki walioko hapa jijini na walio nje ya Dar es salaam.” Akasema Alois “Alois kuna jambo nilitaka kulifahamu .Vipi kuhusiana na msiba wa Vero kuna taarifa zozote mmezipata? Kuna mtu yeyote ambaye ataiwakilisha familia yenu kule? Akauliza Savanna “Kusema kweli bado sina taarifa zozote kuhusiana na kinachoendelea katika msiba wa Vero na wala bado hatujatuma mtu yeyote kwenda kutuwakilisha kule.Toka lilipotokea tukio hili kumekuwa na mvurugano mkubwa sana.Ahsante sana kwa kunikumbusha kuhusu jambo hili Savanna kwani japokuwa hata sisi tumefiwa na mzee lakini kuna ulazima mkubwa wa kutuma uwakilishi katika msiba wa Vero kwani halitakuwa jambo la busara endapo hatutatuma mtu yeyote kwenda kutuwakilisha.” Akasema Alois