MISS TANZANIA
SEHEMU YA 60
MTUNZI: PATRICK.CK
CONTACT:0764294499
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Alimaliza kuisoma barua ile na kuirudia tena kwa mara ya pili halafu akaikunja na kuiweka mfukoni
“Anasemaje Happy? Akauliza Savanna.Patrick hakujibu kitu akaitoa barua ile na kumpatia
“utasoma mwenyewe alichokiandika”
Savanna hakuisoma barua ile kwa kuwa alikuwa anaendesha gari akaiweka pembeni kwa lengo la kuisoma baadae
ENDELEA……………..
Toka mahakamani Patrick na Loniki wakaelekea moja kwa moja makaburini ambako Patrick alitaka kuweka maua katika kaburi la Vero .Waliegesha gari na kushuka wakaelekea lilipo kaburi la Vero.Akiwa na maua mkononi,Patrick akasimama mbele ya kaburi la Vero.Akalitazama kaburi lile kwa makini halafu akapiga magoti na kuyaweka maua aliyokuja nayo.
Savanna alijisogeza pembeni na kumuacha Patrick peke yake pale kaburini
“He needs to be alone” akawaza Savanna na kusogea pembeni
Wakati Patrick akiwa amepiga magoti katika kaburi la Veronika,gari walilokuwamo Linah na Loniki nalo likawasili.Walikuwa wakiwafuata kwa nyuma akina Patrick.Loniki akaitoa bastora yake akaishika mkononi
“Stay in the car” akasema Loniki na kuufungua mlango lakini kabla hajashusha mguu chini akasikia sauti za watu wakiimba wakielekea kule makaburini
“Whats that ? You hear something? Akauliza Loniki
“Nasikia kama sauti za nyimbo” akajibu Linah mara ukatokea msafara wa watu waliokuwa wanakuja kuzika
“ouh gosh !! akasema Loniki kwa ghadhabu
“Mpango wote umeharibika”
“Damn ..!!!..akazidi kulalama Loniki.Msafara ule wa magari ukazidi kukaribia ,Loniki akafunga mlango wa gari.
Sauti zile za watu wakiimba zikamstua pia Patrick,akasitisha maombi yake na kuinuka
“Twende tuondoke Savanna” akasema Patrick wakaingia katika gari laona kuondoka pale makaburini.Loniki na Linah wakaendela kuwafuatilia kwa nyuma
“ Kama si watu hawa kunivuruga ningemtundika risasi Patick juu ya kaburi la mdogo wangu.Ana bahati sana lakini kabla jua halijazama jioni ya leo lazima niitoe roho yake” akasema Lonki.Linah hakujibu kitu alikuwa anatetemeka kwa ndani.Hakujua angewezaje kumuokoa Patrick kwani Loniki alikwisha dhamiria kufanya mauaji
Toka makaburini Patrick na Savanna wakaelekea moja kwa moja nyumbani .Patrick alikuwa na kazi kubwa ya kupokea simu nyingi nyingi za pongezi toka kwa watu mbalimbali kwa kesi ile kumalizika
“Itanichukua siku nzima ya leo kupokea salamu mbali mbali toka kwa watu.Nimefarijika sana kwa pongezi na pole nyingi toka kwa watu mbalimbali” akasema Patrick kwa furaha
“Bado pongezi zangu mimi” akasema Savanna na wote wakacheka .Waliendelea na safari yao bila kufahamu kwamba walikuwa wanafuatiliwa na akina Loniki
Walifika nyumbani kwao na kusimamisha gari nje ya geti wakisubiri geti lifunguliwe.
“Nahisi wamekuja nyumbani kwao.This is the time” akasema Loniki
Linah akasimamisha gari nyuma ya gari la akina Patrick waliokuwa wanasubiri kufunguliwa geti.
“Wait for me here.Dont do anything stupid to ruin my plan.” akasema Loniki halafu akaichukua bastora yake akaificha kiunoni na kuchomoa funguo ya gari akashuka.Akapiga hatua chache na kulifikia gari la akina Patrick.Akagonga kioo cha mbele upande aliokaa Patrick ambaye aligeuza kichwa na kupatwa na mstuko mkubwa.Aliitambua sura ya mtu aliyekuwa amesimama nje ya gari.
“Loniki ..!!! akasema Patrick kwa mshangao.Hakuwa ametegemea kumuona Loniki sehemu ile na kwa wakati ule.Ni muda mrefu hajawahi kuonana na Loniki.Savanna naye akageuka na kumtazama Loniki.Mara moja akaikumbuka sura ile.Alikumbuka kuiona sura ile katika msiba wa Vero.
“What is she doing here ? akajiuliza Loniki.
Patrick akafungua mlango wa gari na kushuka huku sura yake ikionyesha wasi wasi
“Hallow Patrick.How are you? Ite been a while “ akasema Loniki huku akilazimisha kutabasamu
“Kweli ni muda mrefu sana hatujaonana Loniki.Karibu sana” akasema Patrick.
Geti lilifunguliwa na Savanna akaliingiza gari ndani.Alipatwa na wasi wasi mwingi kuhusiana na ujio ule wa ghafla wa Loniki
“Karibu ndani Loniki” akasema Patrick na kumuongoza Loniki kuelekea ndani
“Ahsante sana” akajibu Loniki na kumfuata Patrick kuelekea ndani
“wow ! Patrick una nyumba nzuri sana.Hongera” akasema Loniki
“ahsante sana “ akajibu Patrick.Bado aliendelea kuwa na wasi wasi kuhusiana na ujio ule wa ghafla wa Loniki
“Hallow I’m Savanna” Savanna akamsalimu Loniki
“Ouh I’m glad to meet you Savanna.You are Patrick’s lawyer right?
“Yes ! “ akajibu Savanna
“Naitwa Loniki.Ni dada wa Veronika.Nimepita hapa mara moja kuwasalimu na kutoa pongezi zangu kwa Patrick na kuongea naye machache ili tuyamalize yaliyopita na tuanze maisha mapya.” Akasema Loniki na kumfanya Patrick atabasamu
Mara tu alipohakikisha kwamba Loniki ameingia ndani na akina Patrick,Linah akachukua simu yake akaiwasha na kuzitafuta namba za simu za Sarah
“ouh my God naomba nimpate Sarah.” Akawaza Linah huku akibonyeza kitufe cha kupigia simu na simu ikaanza kuita.Iliita mara ya kwanza na kukatika bila kupokelewa. Akapiga tena
“Ouh C’mon Sarah pick up the phone” akasema Linah na mara simu ikapokelewa.
“Hallow Linah.Umepotelea wapi?Nimekutafuta mahakamani sijakuona.Nini kinaendelea ? Mbona hatujawasiliana tena?
Huku akihema kwa nguvu Linah akasema
“Sikiliza Sarah hatuna muda wa kupoteza tena.Loniki yuko hapa nyumbani anakoishi Patrick na Savanna.Ana bastora ameificha na akina Patrick hawajui chochote.She’s going to kill Patrick.Tafadhali fanya kila unaloweza ufike hapa mara moja ila nakuomba tafadhali usipite polisi.Ukija na polisi mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi.Tafadhali Sarah fanya haraka” akasema Lnah
“Ouh Mungu wangu ! hebu nielekeze mahala nyumba hiyo ilipo” akasema Sarah huku mwili ukimtetemeka.Linah akamuelekeza mahala nyumba ya Savanna ilipo
“Ahsante Linah nakuja sasa hivi.Na wewe unafanya nini hapo? Kwanini usikimbie kuyanusuru maisha yako?
“Natamani sana nikimbie lakini funguo ya gari anayo yeye na amenifungia ndani ya gari”
“C’mon Linah fanya unavyoweza na uondoke humo ndani ya gari.Lazima Loniki atakuua tu.”
“Siwezi kuondoka Sarah.Nataka nijue kila kinachoendelea hapa.” Akasema Linah
“Sawa Linah ninakuja hapo sasa hivi” akajibu Saraha na kukata simu.Akageuza gari na kuanza safari ya kuelekea mahala alikoelekezwa
Akiwa njiani kuelekea nyumbani kwa Savanna akachukua simu na kumpigia shangazi yake
“Shangazi naomba unisikilize vizuri.Muda huu Loniki yuko nyumbani kwa Patrick .Amekwenda kwa lengo la kumuua na sekunde yoyote kuanzia sasa anaweza akafanya hivyo.Ana bastora ameificha .Shangazi tunatakiwa tumzuie asifanye unyama huo anaotaka kuufanya”
“Hebu nielekeze mahala huko aliko Loniki,mbona anataka kutuletea matatizo mengine makubwa? Akasema shangazi yake kwa mstuko
Sarah akamuelekeza shangazi yake mahala nyumba ya Savanna ilipo.Mara tu alipomaliza kuongea na Sarah simuni mama yake Loniki ambaye alikuwa pembeni yake akamkazia macho na kumuuliza
“Nini kimetokea? Kuna tatizo gani?
“Loniki amekwenda nyumbani kwa Patrick .Anataka kumuua ana bastora”
Mama yake akastuka na kupata nguvu za ghafla akainuka na kuelekea chumbani kwake akafungua kabati lake kubwa la nguo na mara moyo wake ukaanza kwenda mbio
“Ouh Mungu wangu ! Loniki amechukua bastora iliyokuwa humu”
Baada ya kuongea na shangazi yake,Sarah akazitafuta namba za simu za Alois na kumpigia akamfahamisha juu ya tukio hilo
“Please Alois we have to save Patrick.Loniki ana silaha na muda wowote anaweza akamuua ” akasisitiza Sarah
“Sarah nakuja huko sasa hivi” akajibu Alois
* * * *
“Habari za siku nyingi Loniki? Akasema Patrick
“habari nzuri Patrick.Ni muda mrefu sana hatujaonana.Nimerudi juzi na kilichonirudisha ni kuhudhuria siku ya leo”.akasema Loniki halafu kimya kifupi kikatanda
“Patrick mimi si mkaaji sana.Nimeona kabla sijarudi London nipite hapa nikusalimu na kukupa pole kwa matatizo yaliyokupata.Pamoja na hayo….” Lonik akainuka na kuwatazama Patrick na Savanna
“Pamoja na hayo nimekuja pia kukuaga Patrick”
“Are you leaving so soon? Akauliza Patrick
“Yah ! soon I’ll be going but today its you who is going.Patrick I’vecome to kill you” akasema Loniki na kwa kasi ya aina yake akatoa bastora yake na kuwalenga Patrick na Savanna
“Loniki ..!! Unafanya nini? Akauliza Patrick kwa mstuko
“shut up !! akafoka Loniki kwa ukali
Patrick na Savanna wakaangaliana kwa woga.Wote walikuwa wanatetemeka .Macho ya Loniki hayakuonyesha masihara hata kidogo.
“Ouh Mungu wangu mambo gani haya yananitokea? Please help me God.Ee Mungu umekuwa unaniokoa katika kila ovu,naomba usiniache katika hili pia.” Patrick akaomba kimoyo moyo huku mwili ukitetemeka
Mara mtumishi wa ndani akaingia pale sebuleni kwa kasi na sinia la vinywaji bila kujua kilichokuwa kinaendelea,ghafla akastuka baada ya kumuona Loniki amewaelekezea Patrick na Savanna bastora ,sinia la vinywaji likamponyoka na kuanguka chini.Loniki akamgeukia
“Ukijaribu kukimbia nakupiga risasi.Kaa pale na ufanye vile nitakavyokuamuru” Loniki akamwambia kwa ukali yule mtumishi wa ndani ambaye alikuwa anatetemeka.
“Pigeni magoti wote” akaamuru Loniki.
“Loniki please don’t kill us.Nitakupa kiasi chochote cha pesa unachohitaji ….!! “ akasema Savanna huku akitetemeka .Machozi mengi yalikuwa yanamtoka
“Shut up !!..akafoka Loniki na kumtazama Yule mfanyakazi wa ndani
“wewe ! Kata ule waya wa umeme na uwafunge hawa mikono kwa nyuma.!! Loniki akamuamuru yule mfanyakazi ambaye kwa woga aliokuwa nao aliitekeleza amri ile kwa haraka.Akawafunga Patrick na Savanna mikono kwa nyuma kwa kutumia waya
“Loniki tafadali naomba usitudhuru.Tumekukosea kitu gani hadi utufanye hivi?” akaomba Patrick.Kauli ile ikaonyesha uzidi kumpandisha hasira Loniki
“Huna haya mshenzi wewe.Ulimuua mdogo wangu bila kosa.Niliapa kulipa kisasi kwa wale wote walioukatili uhai wa mdogo wangu.I loved her so much.Ni kwa sababu ya mapenzi yangu kwake ndiyo maana niliweka ahadi ya kulipa kisasi.Kifo chake kiliniuma sana.How could you kill her like that? Don’t you have a soul you bastard? She loved you with all her heart and in return you killed her.I cant let you walk again.Ndani ya sekunde kadhaa zijazo utaungana naye mbele za haki mshenzi wewe” akasema Loniki na kumtemea Patrick mate usoni.
“Loniki Patrick hakufanya lolote.Hakumua Veronika.Ngoja nkwambie ukw……” akasema Savanna lakini kabla hajamaliza sentensi yake ukasikika mlio wa risasi.Wote wakaanguka na kulala chini.Taratibu Patrick akafumbua macho ,pembeni yake alikuwa amelala Savanna na damu nyingi zikimtoka
“Savanna !! Savanna !! Savannaaaaa..!!!!! “ akaita Patrick huku akilia
“Hiyo ndiyo adhabu yako kuku wewe.Wewe ndiye uliyeishawishi Mahakama imuachie huru huyu mshenzi.Hii ndiyo hukumu yako” akasema Loniki huku akiusogelea mwili wa Savanna pale chini na kuupiga teke.Patrick alikuwa amelala sakafuni mikono yake imefungwa kwa nyuma hivyo hakuweza kufanya lolote.Pembeni yake mwanamke aliyempenda sana alikuwa amelalia dimbwi la damu.
“shetani wewe !! how could you do this? I’m going to kill you !! “ Patrick akasema ghadhabu.
“Usihofu Patrick.In few minutes you’ll join her” akasema Loniki
Mlio ule wa risasi ulimstua sana Linah aliyekuwa amefungiwa garini
“Ouh Mungu wangu tayari Lonny amemuua Patrick” akasema Linah na kuchukua simu yake akampigia Sarah
“Saraha umefika wapi?
“Tayari nimefika maeneo haya.Ndani ya dakika moja nitakuwa nimewasili hapo nyumbani”
“Hurry up ! Tayari risasi moja imelia ndani”
“Ouh my God ! ..akasema Sarah na kuongeza mwendo wa gari.Mikono yake ilikuwa inamtetemeka.
“Nilisikia uchungu sana kwa kifo cha Vero.Hakuna mtu niliyempenda kama yeye.Nataka ukamjibu ni kwa nini ulimsaliti? Kabla hujamuua aliumia sana moyo wake kwa usaliti uliomfanyia. Mateso na maumivu ya moyo aliyoyapata siku ile nataka uyapate nawe leo hii. You’ll die in agony ..! akasema Loniki
“Lonny ..!! Unafanya nini? Akasema kwa sauti Sarah.Loniki akastuka mno baada ya kumuona Sarah pale.Hasira zikampanda mara dufu
“Lonny please ! naomba tafadhali usimuue Patrick..Dont……!!!! akasema Sarah lakini Loniki akamkatisha
“imekuwa vizuri umekuja mwenyewe ushuhudie namna ninavyo mlipia Vero kisasi.Nataka ushuhudie namna Patrick anavyokufa kwa maumivu” akasema Loniki kwa hasira huku mkono wake ukimtetemeka.
“Loniki tafadhali usimuue Patrick.Please I beg you my sister don’t do that..!!! akaomba Sarah huku akipiga magoti
“Sarah sikutambui tena kama ndugu yangu.I don’t know you anymore.Kwa kitendo chako cha kushirikiana na huyu nguruwe wewe si ndugu yangu.Nakukana duniani na ahera.Nina kuchukia sana na baada ya Patrick itakuwa ni zamu yako wewe na Linah…She betrayed me…!!!!
Bila kusita Loniki akaachia risasi kumuelekea Patrick akaanguka chini pembeni ya Savanna.Mlio ule wa risasi ukawastua Linah na Sarah ambao walianguka chini.Baada ya sekunde kadhaa Sarah aliyekuwa anatetemeka mwili akainua kichwa.Hakuamini alichokiona.Patrick alikuwa ameanguka pembeni ya Savanna akiwa katika dimbwi la damu
“Ouh Mungu wangu ..Lonny umemuua Patrick.Umemuua Patrick.Lonny !!! “ akapiga ukelele Sarah na kuinuka akaanza kupiga hatua kumfuata Loniki.
“Sarah simama hapo hapo,usipige hata hatua moja.” Akasema Loniki kwa ukali
“Are you going to shoot me? Akasema Sarah huku akitembea kumuendea Loniki
“Sarah tafadhali naomba usipige hatua hata moja.I’ll shoot you..!!!!! akasema Loniki kwa ukali
“Sarah usijaribu kumsogelea atakupiga risasi ,anamaanisha anachokisema“ Linah aliyekuwa amejibanza pembeni ya mlango akamuonya Sarah
“Shoot me Lonny.Kama mimi si ndugu yako nipige risasi” akasema Sarah huku akipiga hatua kumuendea Patrick aliyekuwa amelala pale sakafuni
“Sarah don’t force me to kill you.Stay where you are” akasema tena Loniki kwa ukali
“Shoot me ..!!! akasema Sarah huku akiunyanyua mguu wake lakini kabla hajaushusha chini ukasikia tena mlio wa risasi.Sarah akaanguka chini.Alikuwa anavuja damu nyingi.Loniki akaushusha chini mkono wake uliokuwa na bastora.Alikuwa anatetemeka
“gosh !! nimemuua ndugu yangu..!! akasema Loniki na kuitupa chini bastora yake akamkimbilia Sarah aliyekuwa amelala chini damu nyingi ikimtoka
“Sarah..! Sarah..!!! Saraaaahhhh….!! Akaita Loniki kwa sauti kubwa huku akilia.Alimuinua mdogo wake na kumuweka magotini pake huku akilia kwa nguvu.
“Sarah !’m sorry ..!!!..I’m sorry sarah ..!! …Please forgive me ..!! ..Loniki aliendelea kulia kwa nguvu.Pembeni ya mlango Linah alikuwa ameanguka na kuzirai
Mara katika mlango mkubwa wa sebuleni akaingia Aloisi akiwa ameongozana na askari waliokuwa wamevalia fulana za kujikinga na risasi.Sebule yote ilikuwa imetapakaa damu.Watu watatu walikuwa wamelalia damu.Loniki bado aliendelea kulia kwa nguvu.Askari polisi wakaiokota bastora ile ya Loniki aliyokuwa ameitupa pembeni.
Magari mawili ya wagonjwa yakafika haraka sana .Patrick,Savanna,Sarah,Linah na msichana wa kazi wakapakiwa katika magari na kukimbizwa hospitali.Eneo lote lilitawaliwa na vilio wakati miili inatolewa ndani.Loniki alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa.Alikuwa anaongea maneno mfululizo yasiyoeleweka.Polisi walifanya uchunguzi wao wa kina ndani ya ile nyumba na wakiwa katika harakati za uchunguzi mara akawasili mama yake Loniki lakini mara tu alipokutana na umati mkubwa wa watu pale nje akaanguka na kupoteza fahamu.
Baada ya kukamlisha uchunghuzi wao askari polisi wakaondoak na Loniki ambaye bado alionean kama my aliyechanganyikiwa.
* * * *
St Patrick hospital moja ya hospitali kubwa na mpya jijini Dar ambayo hivi karibuni serikali imeitangaza kuwa hospitali ya rufaa iligeuka uwanja wa heka heka baada ya majeruhi wa shambulio la risasi kufikishwa pale hospitalini.Haraka haraka walikimbiza katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa ajili ya kuokoa maisha yao.Madaktari wote mabingwa wa upasuaji wakaitwa mara moja ili kuongeza nguvu katika kuokoa maisha ya majeruhi wale.
Vipimo vya awali vilibaini kwamba Savanna tayari amekwisha fariki dunia kabla ya kufikishwa pale hospitali.Patrick na Sarah ambao walionekana kuwa hai wakakimbizwa katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa dharura.Katika chumba kingine cha wagonjwa wa dharura ,Linah na mfanyakazi wa ndani wa Savanna walikuwa wanaendelea vizuri baada ya kuzimia kutokana na mstuko walioupata.Tayari walikuwa chini ya uangalizi wa polisi kwani ni watu pekee ambao walilishuhudia tukio zima lilivyotokea.
Taarifa za kutokea shambulio la risasi nyumbani kwa wakili maarufu Savanna Francis Kito zilisambaa kwa kasi na kusababisha idadi kubwa ya watu kumiminika St Patrick hospital ili kuhakikisha kuhusu taarifa hizo.Walinzi waliokuwepo getini walizuia watu kuingia hospitalini hapo isipokuwa wale wagonjwa wa dharura
Alois akiwa njiani kuelekea hospitali alipatwa na wazo la kuwapigia nyumbani kwao na kuwafahamisha kilichotokea.Akapunguza mwendo wa gari na kumpigia simu mama yake.
“Hallo Alois mbona umeondoka ghafla na hujaniaga unaelekea wapi?Tunahitaji chupa tatu za shampeni pamoja na bia za kopo.Naomba wakati unarudi ununue vitu hivyo uje navyo.” Akasema mama yale.Alois akavuta pumzi ndefu na kufikiri kwa muda
“Alois umesikia “ akauliza tena mama yake
“mama .!! akaita Alois
“Nini Alois? Kama hutaweza niambie ili nimtume mtu mwingne”
“Si hivyo ,mama ila kuna tatizo limetokea”
“Tatizo gani tena?
“mama hakutakuwa na sherehe yoyote tena” akasema Alois
“Alois mbona unanistua? Kwa nini kusiwe na sherehe?
“Patrick amepatwa na matatizo”
“matatizo ?? mama yake akashangaa
“Ndiyo mama”
“Matatizo gani? Akauliza mama yake kwa wasi wasi.Alois akavuta pumzi ndefu na kusema
“Patrick amepigwa risasi….”
“Ouh Mun………..” kabla hajamliza sentensi yake akaanguka ghafla na kupoteza fahamu
“mama .!! mama..!! mama..!!!!’ akaita Alois lakini hakujibiwa.Akaogopa na kukata simu akampigia mke wake akamuomba amuangalie mama yake.
“mama ameanguka ghafla na amepoteza fahamu.Hatujui tatizo ni nini lakini alionekana alikuwa anaongea na simu kwani simu yake imeanguka pembeni na imesambaratika.Uko wapi Alois? Akasema Sesilia mke wa Alois
“Sikiliza mke wangu” akasema alois
“Kuanzia sasa hivi sitisheni shughuli zote kuhusiana na sherehe mliyokuwa mnaiandaa.Hakutakuwa na sherehe tena.Kitu kingine nakuomba uendeshe gari na mumpeleke mama haraka katika hospitali ya karibu kwa Dr Khan ili apatiwe matibabu ya haraka”
“Alois wewe uko wapi? Akauliza Sesi kwa wasi wasi
“Siwezi kuja huko nyumbani sasa hivi.Kuna jambo limetokea nitakutaarifu baadae.Ukishafika hospitali tafadhali nipigie simu” akasema Alois na kukata simu.Mwili bado uliendelea kumtetemeka
“Mambo gani haya yanatupata katika familia yetu? Hata kabla machungu ya kuondokewa na baba hayajapoa ,tunapatwa na tatizo lingine.Ouh Mungu naomba umponye Patrick.Tafadhali usimchukue kwa wakati huu” akaomba Alois.
Mara tu alipofika hospitali alijitambulisha mapokezi na kuomba kuonana na daktari ili aweze kupatiwa taarifa za maendeleo ya mgonjwa wake lakini alitaarifiwa kwamba kwa muda ule asingeweza kumuona daktari kwa kuwa walikuwa katika chumba cha upasuaji wakijaribu kuokoa maisha ya Patrick na Sarah.Alois akapelekwa katika sehemu ya mapumziko katika ofisi ya mganga mkuu akimsubiri amalize upasuaji .Akiwa amepumzika katika sofa jeusi lililokuwa nje ya ofisi ya mganga mkuu simu yake ikaita.Alikuwa ni mke wake.
“Hallow Secy .Tayari mmefika hospitali?
“Ndiyo Alois tumefika lakini kuna tatizo lingine limejitokeza.Dr Khan amempima akagundua kwamba tatizo la mama ni zaidi ya kupoteza fahamu kwa hiyo ametuandikia tumpeleke katika hospitali ya rufaa ya jeshi pale wana wataalamu wazuri na vifaa na wanaweza wakabaini kwa haraka tatizo la mama.Hivi sasa tuko njiani tunaelekea huko hospitali”
“Ouh Mungu wangu ! kwa hiyo Dr Khan hajasema lolote kwamba linaweza kuwa ni tatizo gani?
“Hapana hajasema lolote isipokuwa ametuandikia makaratasi ya kwenda nayo huko na sijui kaandika nini”
“Unaionaje hali ya mama?
“hali yake haina mabadiliko yoyote”
“Uko na nani hapo karibu?
“Niko na ndugu wengine hapa .Wewe uko wapi? Njoo Alois hali hii mimi inaniogopesha sana” akasema Secilia
“Sesilia naomba uwe na ujasiri hasa kwa wakati huu .Mimi nitakuja lakini kwa sasa niko sehemu fulani.Ukifika hospitali nitaarifu kuna jambo nitakuelezea lakini nataka wakati uko peke yako”
“Alois nini kinaendelea?”
“Nitakwambia baadae.Ukifika hospitali nijulishe” akasema Alois na kukata simu.Jasho lilikuwa linamtiririka
TUKUTANE SEHEMU IJAYO.......