Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Kizungumkuti! - 68

Na Bishop Hiluka

ILIPOISHIA

“Nzuri tu, karibuni,” Dk Masha aliitikia huku akimpa ASP Komba mkono, kisha akamsalimia Sajenti Mapambano na wote wakaketi kwenye viti. Walipoketi tu Dk Masha alivuta droo ndogo ya meza yake na kutoa humo kitabu kidogo cha kumbukumbu.

“Kitu pekee nilichokipata kutoka kwenye mfuko wa suruali ya marehemu ni hiki kitabu chake cha kumbukumbu,” Dk Masha alisema huku akinyoosha mkono wake kumpa ASP Komba kile kitabu.

ASP Komba alikipokea kile kitabu cha kumbukumbu, maarufu kama Diary na kukigeuza geuza huku akikiangalia kwa umakini. Kilikuwa kitabu kidogo cha rangi ya bluu.

“Pia kuna karatasi zingine mbili tatu, labda zitaweza kuwasaidia,” Dk Masha alisema tena huku akichukua zile karatasi na kunyoosha mkono wake kumpa ASP Komba.

Endelea...

ASP Komba alizipokea zile karatasi na kuzitupia jicho mara moja kisha akayarudisha macho yake kwenye kile kitabu cha kumbukumbu. Akakifungua na macho yake yakatua kwenye ukurasa wa kwanza tu ambapo alikutana na jina la mmiliki wa kile kitabu, “Carlos Mwamba” likiambatana na taarifa zingine binafsi ikiwemo mawasiliano yake.
ASP Komba akaonesha kushtuka kidogo kwa kuwa alimfahamu vyema Carlos Mwamba, ni wiki chache tu zilizokuwa zimepita walikutana wakaongea na Carlos Mwamba alimuahidi kuwa alitaka kulisaidia Jeshi la Polisi kiasi cha shilingi milioni 100 katika operesheni zake mbalimbali.
ASP Komba alishusha pumzi kisha akaanza kuangalia kurasa mbili tatu na hapo macho yake yakatua kwenye karatasi mbili zilizokuwa zimepachikwa kwenye ukurasa mmoja wa kile kitabu cha kumbukumbu.
ASP Komba alizitoa zile karatasi na kuzitazama kwa umakini, karatasi moja ilikuwa ni nakala kivuli (photocopy) ya hundi ya The Jacarandah Group iliyokuwa na saini na karatasi nyingine ilikuwa imeandikwa namba kadhaa za simu.
ASP Komba alizitazama zile namba kwa umakini mkubwa na kugundua kuwa namba mbili kati ya zile zilikuwa ni namba alizokuwa ameziona kwenye simu ya Yusuf, moja ikiwa ni namba ya Joram Mbezi, ambayo pale ilipewa jina la Kisu na namba ya Belinda Jackson, ambayo pale ilipewa jina la beloved coordinator.
Pia katika orodha ile kulikuwa na namba aliyoifahamu kuwa ni ya Yusuf na namba nyingine mbili ambazo hakuweza kuzifahamu. ASP Komba alijikuta akiachia tabasamu pana ambalo baadaye lilitengeneza kicheko hafifu na hivyo kuwafanya Dk Masha na Sajenti Mapambano wapate shauku ya kutaka kujua kilichokuwa kimeandikwa kwenye zile karatasi.
“Vipi, afande, kuna lolote umegundua?” Dk Masha alimuuliza ASP Komba kwa shauku huku akijitahidi kurefusha shingo yake ili ajionee kilichokuwemo kwenye zile karatasi.
“Huwezi kuamini, umenisaidia sana, dokta… nilikuwa nina hamu kubwa sana ya kukutana na huyu mtu,” ASP Komba alisema huku akiendelea kutabasamu.
“Nani, huyu marehemu?” Dk Masha alimuuliza ASP Komba kwa mshangao.
“Naam! Lakini tayari kajihukumu mwenyewe…” ASP Komba alisema na kusita kidogo, kisha kama aliyegutuka akauliza, “Na hali ya yule binti aliyekuwa na marehemu ikoje?”
“Yule binti kama atavuka kesho jioni basi ataweza kuongea,” Dk Masha alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.
ASP Komba aliinuka kutoka kwenye kiti chake huku akiendelea kutabasamu kisha akampa ishara fulani Sajenti Mapambano ambaye pia aliinuka, wakamuaga Dk Masha.
“Nakushukuru sana, dokta, huwezi kujua ni kwa kiasi gani umeifanya kazi yangu kuwa rahisi mno, nitakutembelea kesho au keshokutwa kutegemea na hali ya yule binti itakavyokuwa, maana nina hamu kubwa ya kutaka kuongea naye.”
“Karibuni sana,” Dk Masha alijibu huku akiinuka kutoka kwenye kiti chake na kuwasindikiza ASP Komba na Sajenti Mapambano. Wakatoka nje na kuelekea walikokuwa wameegesha gari lao.
Waliingia kwenye gari lao na dereva akaliondoa, waliamua kurudi ofisini. Walipofika ofisini ASP Komba aliketi kwenye kiti chake, akaanza kupitia maandishi yaliyokuwa yameandikwa kwenye kile kitabu cha kumbukumbu cha Carlos Mwamba, ukurasa mmoja baada ya mwingine.
Kuna wakati alijikuta akisisimkwa mwili wake kutokana na kusoma mipango ya hatari iliyokuwa imeandikwa kwenye kile kitabu cha kumbukumbu ikionesha tarehe ya kutekeleza mipango ile na aina ya watu ambao wangetumika kufanikisha mipango ile.
ASP Komba hakuamini kabisa kile alichokuwa akikisoma kwenye kile kitabu cha kumbukumbu cha Carlos Mwamba, mtu aliyekuwa rafiki yake, yeye na mkewe Jackline Mgaya Mwamba. Siku zote ASP Komba aliamini kuwa Carlos ni mfanyabiashara mwenye mafanikio na raia mwema aliyependa kusaidia wengine kwa hali na mali, kumbe ni mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo!
Hadi wakati ule ASP Komba alikuwa bado akikkikodolea macho kile kitabu cha kumbukumbu akiwa haamini kama ni kweli Carlos Mwamba alikuwa nyuma ya uhalifu ule, akaamua kuingiza jina la Carlos Mwamba kwenye ile kompyuta maalumu ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu iliyokuwa pale ofisini ili kutafuta taarifa zake.
Alipoingiza tu lile jina zilikuja taarifa nyingi zilizoonesha kuwa Carlos Mwamba alikuwa mfanyabiashara wa madini mwenye mafanikio makubwa akimiliki kampuni mbili, Mwamba Mines iliyojihusisha na biashara ya madini na Jaco Investment (ikiwa ni kifupi cha Jackline na Carlos) iliyokuwa ikihusika na ujenzi wa majumba (estates), na hakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu.
Taarifa zile zilibainisha kuwa jina lake kamili aliitwa Carlos Michael Mwamba, mzaliwa wa jijni Mwanza, umri wake ulikuwa miaka arobaini na mbili, alikuwa na mke Jackline Mgaya Mwamba na aliwahi kupata mafunzo na kuhitimu Shahada ya Kwanza ya System Analysis and Design katika Chuo Kikuu cha Oxford Uingereza na baadaye alifanya mafunzo ya shahada ya uzamili katika masuala ya takwimu (Statistics) huku huko Oxford nchini Uingereza…
ASP Komba alishusha pumzi ndefu huku akimtazama msaidizi wake, Sajenti Mapambano, kisha akakohoa kidogo kusafisha koo lake huku akizitazama kwa makini picha kadhaa za Carlos zilizokuwa zimeambatana na taarifa ile.
“Niseme wazi, taarifa hizi zimenishtua sana, sikutegemea kama Carlos Mwamba anaweza kuwa ndiye Master Planner aliye nyuma ya uhalifu huu!” ASP Komba alisema huku akishusha pumzi.
Kisha alitoa paketi ya sigara na kuiweka kwenye pembe ya mdomo wake na kuchukua kiberiti kutoka mfukoni, akawasha ile sigara kwenye pembe ya mdomo wake na kusimama, akaelekea dirishani.
Alisimama pale dirishani na kutazama nje kupitia ukuta msafi wa kioo cha dirisha akiyatazama mandhari ya jiji la Dar es Salaam yaliyokuwa yakipendeza katika muda ule wa alasiri. Hata hivyo, hakuwa na tashwishwi yoyote katika sura yake.
Alivuta sigara yake kwa utulivu huku akiutoa moshi mwingi na kuutazama kwa makini kisha akapiga mkupuo mwingine mkubwa wa moshi na alipoitoa sigara mdomoni akapuliza moshi wake pembeni huku akiutazama kabla ya macho yake kuweka kituo kwenye magari machache yaliyokuwa yameegeshwa katika sehemu maalumu ya kuegesha magari yaliyokuwa na kesi au matatizo katika lile jengo la polisi.
Alilitazama gari la Carlos Mwamba aina ya BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati lililokuwa limeharibika vibaya baada ya kupata ajali kule kwenye daraja la Mto Msimbazi katika eneo la Vingunguti.
Wakati akiwa bado amesimama pale dirishani akitazama chini mara mlango wa kile chumba ukagongwa na kufunguliwa, ASP Komba na Sajenti Mapambano wakageuza shingo zao kutazama kule mlangoni na kumuona askari mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo akiingia na kutembea kwa ukakamavu hadi pale dirishani kisha akasimama karibu na ASP Komba na kupiga saluti ya ukakamavu.
“Afande, kuna mtu mmoja amepiga simu akijitambulisha kama raia mwema anayeishi Tabata Segerea, amesema kuwa amesikia mzozo mkali kwenye nyumba ya jirani yake anayeitwa Carlos Mwamba kuhusiana na mgao wa fedha,” yule askari mwenye cheo cha Koplo alisema.
Maneno yale yakawafanya ASP Komba na Sajenti Mapambano waangaliane kwa makini. Kikatokea kitambo kifupi cha ukimya, kisha ASP Komba akashusha pumzi za ndani kwa ndani.

Itaendelea...

Cc the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
wakuonewa huruma tu nimke wayusuph na mtoto wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kizungumkuti! - 71

Na Bishop Hiluka

ILIPOISHIA

Yusuf alitaka kusema neno lakini akasita, na hapo machozi yakaanza kumlenga lenga machoni. Kikapita kitambo kifupi cha ukimya huku Yusuf akifuta machozi, “Tuli… tulikutana hotelini,” hatimaye alisema huku akifuta machozi.
“Mlikutana katika hoteli gani?” ASP Komba alizidi kumsaili Yusuf.
“Kwanza tulikutana Southern Sun na baadaye tukakutana Amariah Hotel,” Yusuf alijibu kwa unyonge.
ASP Komba alivuta droo ndogo na kutoa picha kadhaa za Carlos na Jacky alizokuwa amezipakua kutoka kwenye mtandao, kisha akachukua picha ya Jacky na kumuonesha Yusuf, “Belinda Jackson ndiyo huyu, siyo?”
Yusuf aliitazama ile picha ya Jacky kwa kitambo kirefu pasipo kusema neno lolote huku midomo yake ikimtetemeka kwa hofu. Machozi yalizidi kumlenga lenga machoni.
“Nijibu, huyu ndiye Belinda Jackson, siyo?”
“Ndiyo, afande,” Yusuf alijibu kwa unyonge.

Endelea...

“Kwa hiyo, ni rafiki yako, siyo?” ASP Komba alizidi kumbana Yusuf huku akizidi kumkazia macho. Yusuf alisita tena, akamwangalia ASP Komba kwa wasiwasi.
“Siyo sana, afande,” Yusuf alisema kwa sauti ya unyonge.
“Si sana, eh? Ulijua kama alikuwa amekuongopea jina na wala haitwi Belinda Jackson?”
Yusuf akaonekana kushtuka sana na kumtazama ASP Komba kwa mshangao. Hata hivyo, hakujibu bali alibaki kimya mdomo ukiwa wazi kwa mshangao.
“Je, ulijua kama ana mume?” ASP Komba alimuuliza tena huku akimkazia macho.
“Sikupata kumuona!”
“Jibu swali langu, sijakuuliza kama ulipata kumuona… Ulijua kama ana mume?”
“Aliniambia kuwa hajaolewa,” Yusuf alisema huku akitaka kulia.
“Alikwambia hajaolewa… na ukamuamini na kufanya naye urafiki?” ASP Komba aliuliza huku akitingisha kichwa chake kwa huzuni.
“Siyo sana, afande. Si nimekuambia?” Yusuf alisema huku akifuta machozi.
ASP Komba alimtazama Yusuf kwa umakini kwa kitambo kirefu, kisha akatingisha kichwa chake na kuvuta jalada la kesi lililokuwa mbele yake. Alilifungua lile jalada na kutoa nakala kivuli ya hundi ya benki ya kampuni ya The Jacarandah Group iliyokuwa na saini, akaiwekea mbele ya Yusuf.
“Hii ulimpa nani? Carlos Mwamba au Jackline Mgaya ambaye wewe unamfahamu kwa jina la Belinda Jackson?” ASP Komba alimuuliza Yusuf huku akiisogeza ile nakala kivuli ya hundi karibu zaidi ya Yusuf.
Yusuf alinywea sana mara alipoiona ile nakala kivuli ya hundi ya benki ya kampuni ya The Jacarandah Group iliyokuwa na saini, alianza kutetemeka, machozi yakaanza kumwagika machoni utadhani milizamu iliyopasuka. ASP Komba aliendelea kumkazia macho pasipo kupepesa.
“Ulimpa nani, mbona hujibu?” ASP Komba alimuuliza kwa ukali.
“Lakini, afande…” Yusuf alitaka kujitetea lakini ASP Komba alimkatisha kwa sauti ya ukali.
“Hutaki kujibu, eh?”
“Nilimpa Belinda,” Yusuf alisema huku akifuta machozi. ASP Komba alibetua kichwa chake huku akiachia tabasamu, lakini akiwa bado amemkazia macho Yusuf bila kupepesa.
“Je, unamjua Jasmine Kombo?” ASP Komba alimtupia Yusuf swali jingine. Yusuf alimtazama ASP Komba kwa unyonge na kufuta machozi yaliyoendelea kumtoka kwa fujo na kutitirika mashavuni.
“Kwa kweli huyo simjui kabisa!” Yusuf alisema kwa huzuni huku akiinamisha kichwa chake chini kwa majonzi.
“Hukupata hata kumsikia?”
“Hata mara moja.”
ASP Komba aliichukua ile nakala kivuli ya hundi na kuirudisha kwenye lile faili, kisha alipaza sauti yake kumwita Sajenti Mapambano, na mara aliingia Sajenti Mapambano na kusimama mbele yake kwa ukakamavu.
“Mrudishe huyu rumande,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano huku akiinuka na akusimama dirishani.
Sajenti Mapambano alimchukua Yusuf na kutoka naye nje ya kile chumba cha mahojiano. ASP Komba alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuingiza mkono wake kwenye mfuko wa gwanda lake na kutoa pakiti ya sigara kisha akatoa sigara moja na kuibana kwenye pembe ya mdomo wake, akaiwasha na kuanza kuvuta taratibu huku akitafakari kuhusu kazi iliyokuwa mbele yake.
* * * * *
Saa kumi na mbili jioni katika eneo la Tabata Segerea katika mtaa wa majumba ya kifahari ya watu wenye ukwasi mkubwa, vilio na nyimbo mbalimbali za maombolezo vilikuwa vikisikika kutoka ndani ya nyumba kubwa ya kifahari ya Jacky na Carlos.
Muda ule taarifa za msiba mzito wa Carlos zilikuwa zimeenea kila mahali na watu wengi waliomfahamu na hata wale waliokuwa wakimsikia tu walifika pale kuomboleza kifo kile cha ajali.
Ndani ya lile jumba la kifahari Jacky alikuwa analia kwa uchungu mkubwa kilio cha kwikwi akiwa pale sebuleni huku akiwa amezungukwa na waombolezaji kadhaa wanawake, wengi wakiwa rafiki na jamaa zake wa karibu.
Pamoja na maombolezo hayo bado hakukuwa na taarifa rasmi zilizokuwa zimetolewa kuhusiana na nini sababu ya ajali iliyosababisha kifo cha Carlos. Salamu za rambirambi zilikuwa zikimiminika kutoka kila pembe ya nchi, watu mbalimbali waliomfahamu au kufanya biashara na Carlos walikuwa wakimpa pole Jacky kwa kufiwa na mumewe Carlos.
Na kwa watu waliokuwa wamefika pale kwenye msiba kila mmoja alijaribu kuuliza hili na lile ili kupata uhakika kama kweli ajali iliyosababisha kifo cha Carlos ilitokana na kuwakimbia polisi, kama ilivyokuwa imeelezwa kwenye taarifa zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao.
Makachero wa polisi, Haji Adam, Sebastian Masesa na Koplo Victor Shirima, waliokuwa wamevaa mavazi ya kiraia walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa katika eneo lile wakiomboleza msiba ule mzito uliogusa nyoyo za watu wengi. Hata hivyo, wao hawakuwepo pale kama waombolezaji bali walikuwepo pale kwa kazi maalumu waliyokuwa wamepewa na ASP Komba.
Kila aliyekuwepo katika eneo lile la msiba kama hakuwa katika sura ya huzuni basi alikuwa kazungukwa na maswali mengi yasiyo na majibu. Eneo la nje katika barabara ya mtaa ule kulikuwa na magari kadhaa ya kila aina ya ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wamefika kuomboleza msiba ule na kumpa pole Jacky kwa kifo cha mumewe Carlos Mwamba.
Ki ukweli kifo cha Carlos kilikuwa pigo kubwa kwa vijana wa eneo lile na kileta simanzi nzito, ulikuwa ni msiba wa mtu mashuhuri sana katika eneo lile ambaye alikuwa akisaidia watu na alijitoa kwa hali na mali, na kila mtu aliyefika pale kwenye msiba alionesha kuguswa kwa namna moja au nyingine kwa jinsi Carlos alivyokuwa akijitoa kusaidia watu, alikuwa mcheshi aliyeopenda kucheka na kila mtu na mkarimu ambaye mfano wake ulikuwa haujapata kuonekana katika eneo lile.
“Ama kweli wema hawadumu!” kijana mmoja aliyekuwa ameketi nje ya fensi ya ile nyumba yenye msiba, chini ya mti mkubwa wa kivuli akiwa na vijana wenzake alisikika akisema kwa kauli ya kukata tamaa huku akivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.
* * * * *
Saa moja na nusu ya asubuhi ilimkuta ASP Komba akiwa bado ameketi kwenye kiti chake ofisini mwake akiyapitia baadhi ya makaratasi aliyokuwa akiyafanyia kazi, kuhusiana na upelelezi wa wizi wa mabilioni ya fedha katika Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba, jijini Dar es Salaam. Alikuwa ameketi pale tangu saa kumi na mbili na nusu akijaribu kuhakikisha anakamilisha kazi ile haraka. Muda ule alikuwa amevaa nguo za kiraia.
Simu yake ya mkononi iliyokuwa mbele yake juu ya meza iliaza kuita kwa fujo, ASP Komba akaitupia jicho mara moja tu na kuiona namba ngeni, akaipuuza. Alikuwa ametingwa na kazi ngumu mbele yake na kitendo cha kupokea simu kingemchelewesha kwani alitaka akamilishe ile kazi haraka iwezekanavyo ili kesi ipelekwe mahakamani.

Itaendelea...

Cc the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
 
Kizungumkuti! - 72

Na Bishop Hiluka

Simu yake ya mkononi iliyokuwa mbele yake juu ya meza iliaza kuita kwa fujo, ASP Komba akaitupia jicho mara moja tu na kuiona namba ngeni, akaipuuza. Alikuwa ametingwa na kazi ngumu mbele yake na kitendo cha kupokea simu kingemchelewesha kwani alitaka akamilishe ile kazi haraka iwezekanavyo ili kesi ipelekwe mahakamani.

Endelea...

Ile simu iliendelea kuita hadi ikakatika, kisha ikaanza kuita tena kwa muda mrefu na kumfanya ASP Komba ayaondoshe macho yake kutoka kwenye yale makaratasi, akainyakua ile simu kwa hasira.
“ASP Komba… nani mwenzangu?” ASP Komba huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.
“Dk Masha hapa. Habari za saa hizi, afande,” sauti ya Dk Masha ilisikika wazi ikiongea kutoka upande wa pili wa ile simu.
“Ooh, dokta! Habari ni nzuri tu, za huko?”
“Nzuri kabisa. Mbona simu imeita weeee…”
“Ah, nilidhani napigiwa simu na jamaa fulani hivi wanataka mchango wa harusi. Enhe mnaendeleaje huko?” ASP Komba alisema huku uso wake ukichanua tabasamu.
“Tunaendelea vyema.”
“Vipi hali ya yule binti?”
“Hali yake inazidi kuimarika. Enhe jana ilikuwaje ndugu yangu?” Dk Masha alimuuliza ASP Komba.
“Vipi?”
“Nimekutafuta sana kwenye simu yako ya mkononi sikukupata.”
“Ni kweli, niliizima kabisa simu kukwepa kero.”
“Kero ipi tena?”
“Nilikuwa napigiwa simu nyingi kuulizwa maswali ambayo sikuwa na majibu yake, na mengine yalionesha kuingilia utaratibu wangu wa kazi.”
“Basi nilitaka kukutaarifu kuwa yule binti kwa sasa yuko fit, ukipata nafasi mchana baada ya madaktari kupita round unaweza kuja kuongea naye,” Dk Masha alisema na kumfanya ASP Komba aachie tabasamu.
Okay, ninashukuru kwa taarifa, dokta.” ASP Komba alisema na kushusha pumzi. Simu ikakatwa.
ASP Komba aliinuka kutoka pale kwenye kiti chake, akaingiza mkono wake kwenye mfuko wa suruali yake na kutoa pakiti ya sigara kisha akatoa sigara moja na kuibana kwenye pembe ya mdomo wake, akaiwasha na kuanza kuvuta taratibu huku akitafakari.
Baada ya kitambo kirefu aliamua kutoka ndani ya ile ofisi yake kisha akashuka ngazi na kuelekea kule chini, kwenye mahabusu, akamkuta Yusuf akiwa amekaa akiwa amejikunyata kwa huzuni jirani na uzio wa nondo. ASP Komba alimtazama Yusuf, akatingisha kichwa polepole.
“Afande, vipi sasa kuhusu dhamana yangu?” Yusuf alimuuliza ASP Komba mara baada ya kumuona.
“Nani aliyekuambia unaweza kuwekewa dhamana? Unashirikiana na majambazi waliokubuhu, halafu upewe dhamana?”
Yusuf alibaki kimya akiwa anamtumbulia macho ASP Komba, uso wake ulisawajika na alionesha kupoteza kabisa matumaini ya kutoka. ASP Komba alitoka na kumwita Koplo Victor, “Twende zetu hoteli ya Southern Sun na baadaye Amariah,” alimwambia. Wakatoka nje ya lile jengo la kituo kikuu cha polisi na kuliende gari lao.
Muda ule ule Mama Jasmine akiwa ameambatana na mwanamke mmoja mtu mzima walifika na kuingia ndani ya lile jengo, walifika pale kaunta ya polisi na kusimama huku wakimwangalia ofisa mmoja wa polisi mwenye cheo cha sajenti. Mama Jasmine alikuwa amekuja na chai.
“Wewe ndiye uliyetakiwa kumletea chai huyu… Yusuf?” yule ofisa wa polisi mwenye cheo cha sajenti aliyekuwa pale kaunta alimuuliza Mama Jasmine baada ya kujitambulisha.
“Ndiyo.”
“Ni ndugu yako?”
“Mume wangu.”
“Fungua hiyo chai, mimina kidogo unywe!”
Mama jasmine alifanya kama alivyoambiwa na yule ofisa wa polisi mwenye cheo cha sajenti, akaonja na kitafunwa alichokuwa ameleta na baada ya yule askari kuridhika akamfuata Yusuf na kumpa ile chai.
* * * * *
Saa sita za mchana, katika wodi moja ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Amana, Jasmine alikuwa amejilaza kitandani kwenye foronya laini na mto wa kuegemeza kichwa. Alikuwa na majeraha kwenye kichwa chake na kwenye mkono wake wa kushoto.
Muda ule Jasmine alikuwa anaongea na jamaa zake wawili waliokuwa wamefika pale hospitalini kumletea chakula na kumjulia hali. Dk Masha aliingia akiwa ameongozana na ASP Komba, ambaye hakuwa amevaa mavazi rasmi ya kazi, wakatembea taratibu hadi kwenye kitanda alichokuwa amelazwa Jasmine.
“Vipi, unajisikiaje sasa?” Dk Masha alimuuliza Jasmine huku akiachia tabasamu pana usoni kwake.
“Kidogo afadhali, ila kichwa ndiyo bado kinaniuma,” Jasmine alimwambia Dk Masha huku akipeleka mkono wake kichwani.
“Usijali… utapata nafuu na kupona kabisa,” Dk Masha alimwambia Jasmine huku akigeuza shingo yake kumtazama ASP Komba. Wakatazama kwa kitambo fulani huku Dk Masha akishusha pumzi za ndani kwa ndani.
“Sasa Jasmine, nimekuja na mgeni ambaye atajitambulisha, anahitaji kupata maelezo fulani kutoka kwako,” Dk Masha alisema kwa sauti tulivu huku akiachia tabasamu.
Jasmine alishtuka sana na kumtumbulia macho ASP Komba kwa wasiwasi. Alimtazama kama aliyekuwa akimfananisha, “Kwema lakini?” Jasmine aliuliza huku akizidi kumkazia macho ASP Komba.
“Usihofu, hapa uko kwenye mikono salama kabisa, binti,” Dk Masha alimwambia Jasmine huku akigeuza shingo yake kumtazama tena ASP Komba.
Okay! I wish you a good success, let me go back to the office,” (Nakutakia mafanikio mema, ngoja mimi nirudi ofisini) Dk Masha alimwambia ASP Komba na kuondoka bila kusubiri jibu lake huku akimwacha ASP Komba akiwa amesimama akimtazama Jasmine kwa makini. Jasmine na rafiki zake waliendelea kumtazama ASP Komba kwa wasiwasi.
“Unajisikiaje sasa, Jasmine?” ASP Komba alimuuliza Jasmine huku akiwatupia macho wale jamaa zake.
“Sijambo kiasi, nashukuru Mungu kwa kuwa bado naongea.”
“Pole sana!”
“Asante, lakini mimi sikufahamu, sijui mwenzangu nani?” Jasmine alimuuliza ASP Komba huku akitabasamu.
“Naitwa Ibrahim Komba, mimi ni ofisa wa polisi na ninatokeaa kituo kikuu cha polisi,” ASP Komba alimwambia Jasmine huku akiachia tabasamu pana usoni kwake.
Jasmine alibadilika ghafla na kunywea, uso wake ulisawajika na muda ule ule aliwatazama wale jamaa zake na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani. “Sawa… karibu,” aliitikia kwa unyonge.
“Asante sana… nadhani ndugu zako wangetupisha kidogo, nahitaji kuongea na wewe,” ASP Komba alimwambia Jasmine kwa sauti tulivu ya chini.
Jasmine alisita kidogo na kuwatupia jicho wale jamaa zake, kisha alimtazama ASP Komba na kukunja sura yake. “Kuongea na mimi kuhusu nini?” alimuuliza ASP Komba huku akimkazia macho.
“Mambo mawili matatu. Wala usiwe na wasiwasi, binti.”
“Mungu wangu! Mambo gani tena jamani?” Jasmine alilalama huku akiwatupia jicho wale jamaa zake.
ASP Komba aliwageukia wale jamaa wa Jasmine na kuongea kwa sauti tulivu ya kirafiki, “Samahani, naomba mtupe nafasi kidogo, nahitaji kuongea na ndugu yenu.”
Wale wanawake waliinuka kwa unyonge bila kuhoji chochote na kutoka nje huku wakimtazama Jasmine kwa wasiwasi. ASP Komba alimkazia macho Jasmine akimtazama kwa umakini.
“Jasmine, wewe ni mfanyakazi wa The Jacarandah Group, ile kampuni iliyoibiwa mabilioni ya fedha hivi karibuni, sawa?” ASP Komba alimuuliza Jasmine huku akiendelea kumkazia macho pasipo kupepesa.
“Sawa,” Jasmine alijibu bila kusita.
“Lini uliacha kwenda kazini?” ASP Komba aliuliza huku akiketi kando ya kitanda.
“Mi sijaacha kwenda kazini, nani kakwambia kuwa mimi siendi kazini?” Jasmine alisema huku akikunja sura yake.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 73

“Sijaambiwa na mtu yeyote,” ASP Komba alijibu huku akiachia tabasamu.
“Kumbe umejuaje?”
“Jasmine, najua ni vigumu sana, lakini ningependa ujibu maswali yangu bila kuhoji chochote. Tumeelewana?” ASP Komba alisema kwa sauti tulivu.
“Yaani miye ninyamaze tu?” Jasmine alisema na kugeuka pembeni huku akiwa amenuna.
“Hujanielewa, sijasema wewe unyamaze tu. Nasema jibu maswali yangu bila kunihoji chochote, tumeelewana?”
“Haya,” Jasmine alijibu huku akiwa bado kaangalia pembeni.
“Tunaanza mwanzo, tangu lini hujaenda kazini?”
“Nimeshakujibu, sijaacha kwenda kazini.”
“Hata siku moja?”
“Ndiyo, hata siku moja.”
“Unaweza kukumbuka ni lini fedha za kampuni yenu ziliibwa benki?”
“Hata sikumbuki, kwani wakati wizi huo unatokea mimi nilikuwa nyumbani naumwa,” Jasmine alisema huku akimtupia jicho kali ASP Komba.
“Ulikuwa ukiumwa nini?”
“Malaria.”
“Umeugua siku ngapi?”
“Siku tatu.”
“Ulitoa taarifa kwa mwajiri wako?”
“Sikuweza, nilizidiwa sana.”
“Kwa nini usimtume mtu akatoe taarifa, au hata kupiga simu?”
“Nimtume nani, kila mtu ana shughuli zake,” Jasmine alisema huku akinyanyua juu mabega yake juu.
“Na hawa ndugu zako niliowakuta hapa?” ASP Komba alimuuliza huku akimkazia macho.
“Wale siyo ndugu zangu, ni majirani tu.”
“Na kwa nini usipige simu, kwani huna simu?” ASP Komba alizidi kumuuliza Jasmine huku akiwa amemkazia macho bila kupepesa.
“Simu yangu imeharibika, ndiyo nilikuwa natarajia kununua simu nyingine hivi karibuni nikipata mshahara,” Jasmine alijaribu kujitetea.
“Ulimfahamu vipi marehemu Carlos Mwamba?” ASP Komba alimuuliza swali ambalo lilionekana kumshtua kidogo Jasmine.
“Alikuwa rafiki wa marehemu baba yangu, kwani amekufa?” Jasmine alijibu na kuuliza swali hapo hapo huku akiinamisha uso wake na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.
“Ndiyo amekufa. Kwa maana hiyo, alikuwa rafiki wa baba yako ndiyo maana akaamua kukutumia kufanikisha wizi wa hundi kutoka ofisini kwenu, Uongo?” ASP Komba alisema huku akiwa amekunja sura yake akimkazia macho Jasmine.
Jasmine alishtuka sana, moyo wake ukashikwa na mfadhaiko huku ukianza kwenda mbio isivyo kawaida. Kwa sekunde chache aliyasahau maumivu yake na jasho jepesi likaanza kumtoka sehemu mbalimbali za mwili wake, akamtazama ASP Komba huku akitetemeka kwa mbali.
“Hebu nieleze ukweli, Jasmine, na ole wako ukijaribu kuficha… ujue Carlos Mwamba hayupo lakini wewe upo… hivyo kukana ni kujichongea,” ASP Komba alisema na kunyamaza kidogo huku akizidi kumtazama Jasmine kwa makini.
“Ni wewe uliyempa ile hundi Carlos Mwamba?” ASP Komba alimuuliza Jasmine kwa sauti tulivu. Jasmine alionekana kunywea sana, alimtazama ASP Komba kwa chuki pasipo kujibu lile swali.
“Jibu swali langu, Jasmine,” ASP Komba aliuliza huku akizidi kumkazia macho.
“Ndiyo,” Jasmine alijibu kwa sauti ya unyonge huku akitazama kando.
“Uliipata vipi?”
“Kitabu cha hundi huwa kipo mezani kwa bosi, na mimi huwa naingia ofisini kwake kila siku,” Jasmine alisema huku machozi yakimlenga lenga machoni.
“Carlos Mwamba alikuahidi kukupa kiasi gani cha fedha akifanikiwa?”
“Shilingi milioni mia moja.”
“Ooh… kwa hiyo wewe sasa hivi ni milionea, siyo? Nadhani tayari amekwisha kupa!”
“Bado, ndiyo alikuwa amenifuata ili akanipe, bahati mbaya tena ikatokea ajali,” Jasmine alisema kwa huzuni huku akifuta machozi yaliyoanza kumtoka.
ASP Komba alimtazama Jasmine kwa kitambo kirefu, huruma ikaanza kumwingia lakini hakutaka kuiruhusu iingilie majukumu yake ya kazi, hivyo alitingisha kichwa chake taratibu huku akimtazama Jasmine kwa makini.
Mara simu yake ikaanza kuita, ASP Komba aliitazama ile simu kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani, kisha akamtaka radhi Jasmine na kutoka nje haraka.
ASP Komba alifika nje ya lile jengo la wodi ya wanawake akamkuta Sajenti Mapambano akiwa amesimama na muuguzi mmoja wakiongea. Wakazungumza mawili matatu kwa kitambo kifupi, kisha ASP Komba akaelekea ofisini kwa Dk Masha kumuaga akiahidi kurudi baadaye.
Alipotoka wakaongozana hadi kwenye gari lao aina ya Nissan Patrol la rangi nyeusi lililokuwa na maandishi ya POLISI ubavuni, wakaingia ndani ya lile gari na kuondoka haraka.
* * * * *
Jua la saa saba mchana lilishaanza kuchukua nafasi yake juu ya anga, hali ambayo waswahili waliita jua la utosi, na hivyo kuifanya hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam kuwa ya joto sana. Katika barabara ya Mandela kulionekana foleni ya magari, na miongoni mwa magari yale lilionekana gari polisi aina ya Nissan Patrol la rangi nyeusi lililokuwa na maandishi ya POLISI ubavuni liikuwa katika mwendo wa kasi.
Ndani ya gari lile kulikuwa na watu watatu, dereva wa gari lile, Koplo Victor Shirima, ASP Komba aliyekuwa ameketi kwenye siti ya mbele kushoto kwa dereva na Sajenti Mapambano aliyeketi siti ya nyuma.
Sajenti Mapambano alikuwa akimweleza ASP Komba kuhusiana na taarifa mpya za kipelelezi alizozipata kutoka nyumbani kwa marehemu Carlos Mwamba.
Gari lile la polisi lilipofika katika eneo la taa za barabarani za kuongozea magari katika eneo la Tabata liliiacha ile barabara ya Mandela na kukunja kushoto likiingia katika barabara iliyokuwa ikielekea Tabata.
Kuanzia pale maongezi ndani ya lile gari yalikatika ghafla na kila mmoja alikuwa kimya akitafakari kuhusu kazi ile iliyokuwa mbele yao.
ASP Komba aliangaza macho yake kuangalia nje akiyatazama magari mbalimbali waliyopishana nayo katika mitaa ile ya Tabata huku kichwani akiwaza kuhusu hatma ya mshikemshike wa kila siku wa kukimbizana na wahalifu. Alishangaa kwa nini watu hawakutaka kuacha uhalifu na kusihi maisha mema ya kumcha Mungu, huku akijiuliza hali kama ile itaisha lini!
Alijikuta akizikumbuka ndoto zake za ujanani alipokuwa akiota kuja kuwa na mafanikio makubwa kwa kucheza soka, kwani alipokuwa shuleni alikuwa mcheza soka mahili sana na alisifiwa na kila mtu, na wakati mwingine alikuwa na ndoto ya kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa nchini.
Hata siku moja hakuwahi kuota kuja kuwa ofisa wa polisi, na ilitokea tu siku moja pale alipokuwa katika kumalizia masomo yake pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alijikuta akishawishiwa na hatimaye kuvutiwa kuchukua fomu akiomba kujiunga na Jeshi la Polisi.
ASP Komba alizidi kuwaza hili na lile na mara akajikuta akikumbuka siku zake za mwanzo kabisa baada ya kufuzu mafunzo yake ya upolisi katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi (MPA).
Alikumbuka baada ya kumaliza mafunzo ya uaskari kituo chake cha kwanza cha kazi kilikuwa mkoani Mwanza na baada ya kuripoti pale Mwanza, haikupita hata miezi sita kukatokea mapambano makali sana kati ya polisi na majambazi sugu waliokuwa wamejificha katika mapango ya milima ya Utemini, yaliyochukua zaidi ya saa 12.
Wakati ule hayo yakitokea ASP Komba alikuwa bado hajapewa cheo chochote, na baada ya mapambano yale polisi walishinda na majambazi wale wakakutwa na silaha nzito za kivita walizokuwa wamezificha mapangoni.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 74

Pia ASP Komba aliyakumbuka makovu mawili ya risasi yaliyokuwa kwenye paja lake la mguu wa kulia na kovu jingine la kisu lililokuwa kwenye bega lake ambayo alikuwa ameyapata kwenye harakati mbalimbali za kupambana na uhalifu mkubwa. Alijikuta akimeza funda kubwa la mate kuzitowesha kumbukumbu zile mbaya.
Mawazo yake yaliporudi tena mle ndani ya gari alishtuka kuona kuwa tayari walikuwa wamefika eneo walilokuwa wakienda, kwani walikuwa wakipita katika barabara tulivu ya mtaa wenye majumba ya kifahari yaliyozungukwa na miti mirefu ya kivuli na kuta zenye usalama wa uhakika.
Hawakuchukua muda wakawa wamefika katika nyumba ya kifahari aliyokuwa akiishi Carlos Mwamba na mkewe Jackline Mgaya. ASP Komba na Sajenti Mapambano walishuhudia magari mengi ya kifahari na mengine ya kawaida yaliyokuwa yameegeshwa kwenye barabara yote ya mtaa ule.
Pia kulikuwa na watu wengi waliofika pale kuomboleza msiba na kumpa pole Jacky kwa kifo cha mumewe Carlos waliokuwa wameketi kwa utulivu kwenye maturubai maalumu yaliyokuwa yamefungwa kwenye eneo kubwa la wazi mbele ya ile nyumba.
Muda ule sauti ya nyimbo za maombolezo kutoka kwenye spika kubwa zilizokuwa zimesambazwa katika eneo lote ziliendelea kusikika katika eneo lile, nje na ndani ya nyumba ile, huku watu wakizidi kufika pale kuomboleza msiba ule mkubwa wa mtu mashuhuri.
Koplo Victor alipunguza mwendo wa gari huku akiyatembeza macho yake huku na kule akitafuta sehemu nzuri ya kuegesha gari lao na baada ya muda mfupi hatimaye akawa amepata sehemu nzuri na kuliegesha lile gari.
ASP Komba na Sajenti Mapambano waliteremka kutoka kwenye lile gari na kuanza kutembea taratibu wakirudi nyuma kuifuata ile nyumba, kisha wakaanza kukatiza wakipenya penya katikati ya watu waliokuwa wamejaa eneo lile ili kuingia ndani ya ile nyumba. Baadhi ya waombolezaji waliokuwepo eneo lile waliwatazama kwa wasiwasi huku wakiwapisha.
Walifanikiwa kupenya na kulifikia geti kubwa jeusi, kisha wakaingia ndani ya uzio wa lile jumba la kifahari na baadaye wakafanikiwa kuingia sebuleni na kukaribishwa. Walikwenda moja kwa moja hadi alipokuwa ameketi Jacky akiwa analia taratibu kilio cha kwikwi pale sebuleni huku akifarijiwa na ndugu, jamaa na rafiki zake.
Pale sebuleni pia walikuwepo ndugu wengine kama wifi zake, shemeji zake, wakwe zake na wazazi wake ambao wote kwa pamoja waliendelea kuomboleza msiba ule wa mpendwa wao.
Jacky aliinua uso wake na kuwaona wale maofisa wa polisi, akashtuka sana na kupunguza kulia. Aliwatazama kwa umakini na kufuta machozi yake huku akijitahidi kutengeneza sura ya kirafiki. ASP Komba na Sajenti Mapambano walimsogelea huku wakionesha huzuni yao.
“Pole sana kwa msiba,” ASP Komba alimwambia Jacky kwa sauti tulivu ya chini huku akichuchumaa na kumpa mkono.
“Asante, kazi ya Mungu,” Jacky alijitahidi kujibu huku akionesha unyonge na kujiweka vizuri pale sakafuni alipokuwa ameketi huku akimpisha ASP Komba apate nafasi ya kuketi. Sajenti Mapambano naye alimsalimia na kuketi kando.
Wale watu wengine waliokuwa wakiomboleza na wengine waliokuwa wakimfariji Jacky waliwatazama ASP Komba na Sajenti Mapambano kwa umakini huku wakiwa na maswali kibao kichwani. ASP Komba alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiwatazama wale kina mama waombolezaji.
“Jacky, kwanza nichukue nafasi hii kukupa pole sana… mimi naitwa Ibrahim Komba na mwenzangu hapa ni Venance Mapambano, nadhani sisi siyo wageni kwako kwani tumeshawahi kukutana mara kadhaa…” ASP Komba alijitambulisha kwa Jacky kwa sauti tulivu ya chini.
Jacky alibetua kichwa chake kukubali huku akishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani, “Nawafahamu vizuri sana, wala hamna haja ya kujitambulisha kwanu” alisema huku akiinamisha sura yake kutazama chini.
Okay, basi tuna sababu muhimu sana ya kuja hapa kuongea na wewe. Tunajua uko kwenye msiba mkubwa sana kwa kuondokewa na mume wako mpenzi, lakini tutahitaji nafasi kidogo ili kukuuliza maswali mawili matatu kama hutojali,” ASP Komba alimwambia Jacky kwa sauti tulivu ya chini.
Jacky aliwatupia jicho ndugu na jamaa zake kwa wasiwasi waliofika kwenye msiba kumfariji kisha akamtazama ASP Komba akionekana kusita kidogo, kisha alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiminya midomo yake.
“Usijali, tunaweza kwenda kuongea chemba kidogo ili tusiingilie shughuli za watu wengine,” ASP Komba alimweleza Jacky huku akiinuka. Jacky aliweatupia tena jicho wale ndugu na jamaa zake kisha akainuka na kuwaongoza ASP Komba na sajenti Mapambano hadi eneo moja chini ya mti wa kivuli lililoonekana tulivu kwenye ile fensi ya nyumba.
Eneo lile kulikuwa na vijana wameketi wakibishana kuhusiana na nani mkali kati ya Messi na Cristiano Ronaldo. Jacky aliwaomba wale vijana wapishe kidogo kwani alihitaji kuongea na wale maofisa wa polisi. Wale vijana waliinuka na kuondoka eneo lile mmoja mmoja huku wakiwaacha wale maofisa wa polisi na Jacky wakiwasindika kwa macho.
“Karibuni, sijui mnasemaje maana sijajua sababu ya ujio wenu,” Jacky alimwambia ASP Komba mara baada ya kuachwa peke yao huku akijiweka sawa kwenye kiti chake.
“Ni kuhusu wizi wa bilioni moja na milioni mia tatu zilizoibiwa katika Benki ya Biashara juzi, sisi polisi tunaamini kuwa wewe na mumeo mmehusika,” ASP Komba alimwambia Jacky kwa sauti tulivu huku akimkazia macho.
“Mimi na mume wangu!” Jacky aliuliza akijifaanya kushangaa sana.
“Ndiyo, wewe na mumeo Carlos Mwamba. Nadhani unamfahamu Yusuf Akida, yule mfanyakazi wa benki iliyoibiwa pesa!” ASP Komba alimuuliza Jacky huku akiendelea kumkazia macho.
Jacky alimwangalia ASP Komba kwa kitambo kifupi akionekana kufikiria kidogo. “Nimepata kumuona mara kadhaa pale pale benki, mimi ni mteja wao.”
“Je, una uhusiano naye?”
“Sina uhusiano naye wowote!”
“Unajua unachokisema?”
“Nakijua sana,” Jacky alisema huku akimtazama ASP Komba kwa jicho la chuki.
“Aliipataje namba yako ya simu?” ASP Komba aliuliza akiwa amemkazia macho Jacky bila kuyapepesa.
“Nina uhakika kuwa hana namba yangu ya simu.”
“Si hii namba uliyosajili kama Jackline Mgaya, bali namba yako kama Belinda Jackson, iliyowekwa mfumo maalumu wa ulinzi…” ASP Komba aliendelea kumuuliza huku akimkazia macho.
“Sina namba yoyote iliyowekwa mfumo wa ulinzi na wala simfahamu huyo mtu mnayemwita Belinda Jackson.”

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 75

“Mbona tunafahamu kuwa hilo ni jina ambalo Yusuf alikuwa akikuita, je alilipata wapi?”
“Sijui, mi sijamwambia aniite hivyo.”
“Kama hukumwambia yeye alilijuaje?”
“N’tajuaje, labda kamuulize mwenyewe,” Jacky alijibu kijeuri huku akigeuza shingo yake kuangalia kando, alikunja sura yake kwa hasira.
“Nimeshamuuliza, kasema wewe ulijitambulisha kwake kwa jina hilo na ulimpa ile namba ili muwasiliane. Na kanieleza mengi, mengine ambayo sidhani hata kama marehemu mumeo aliyafahamu,” ASP Komba alimwambia Jacky huku akimtazama kwa tabasamu.
“Sasa hayo yana uhusiano gani na haya?” Jacky alimuuliza ASP Komba huku akitazama pembeni kuyakwepa macho yake.
“Yana uhusiano wa karibu sana, kama ulivyo wewe na Yusuf Akida,” ASP Komba alisema na kutoa kitabu kidogo cha kumbukumbu za kila siku cha Carlos Mwamba.
“Unakikumbuka hiki kitabu?” ASP Komba alimuuliza Jacky huku kamkazia macho. Jacky alikiangalia kile kitabu cha kumbukumbu mara moja tu na kuonekana kunywea. Alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akitazama kando, alihisi kijasho chembamba kikianza kumtoka mwilini.
“Ndiyo, cha marehemu mume wangu,” Jacky alisema kwa unyonge.
ASP Komba alikifungua kile kitabu na kuitoa ile nakala kivuli ya hundi ya The Jacarandah Group iliyokuwa na saini, akamuonesha Jacky huku akiendelea kumkazia macho. “Yusuf alimpa nani hii nakala, wewe au marehemu Carlos Mwamba?”
Jacky aliitazama ile nakala kivuli ya hundi ya The Jacarandah Group iliyokuwa na saini na kuinamisha uso wake chini.
“Nataka kujua, Yusuf alimpa nani hii nakala ya hundi?” ASP Komba alimuuliza tena Jacky, safari hii kwa ukali kidogo. Jacky alinyanyua uso wake uliosheheni maumivu na kumtazama ASP Komba kwa huzuni, michirizi ya machozi ilikuwa inaonekana kwenye mashavu yake.
“Jamani, bora mniuwe tu nikapumzike kama mume wangu. Shida yote ya nini?” Jacky alilalama huku akifuta machozi. ASP Komba aliendelea kumkazia macho bila kupepesa.
“Alimpa nani? Naomba ujibu swali langu,” ASP Komba aliuliza kwa ukali huku akisisitiza.
“Alimpa mume wangu,” Jacky alijibu kwa unyonge.
“Mbona yeye anadai alikupa wewe?”
“Alimpa mume wangu, kwa nini niongope?”
Okay, na hawa wahuni wawili wanaokuja kuja hapa nyumbani kwako kudai mgao wao wa fedha ni kina nani?” ASP Komba alimuuliza Jacky huku akimtupia jicho Sajenti Mapambano.
“Carlos ndiye aliyekuwa akijuana nao.”
“Wewe huwajui?”
“Siwajui.”
ASP Komba alimtazama Jacky kwa umakini kwa kitambo kirefu na kutingisha kichwa chake. “Huwajui, eh? Okay, fedha mlizoiba kule Benki ya Biashara mmezificha wapi?”
Jacky alibaki kimya akiwatumbulia macho wale maofisa wa polisi. Mara akawaona Kabwe na Liston wakaingia kwenye ule uzio wa ile nyumba huku wakiangaza macho yao kutazama huku na kule huku wakitembea kwa ubabe wakionekana kuwa na hasira.
Walitaka kuingia lakini wakasita baada ya kumuona Jacky akiwa ameketi na wanaume wawili chini ya kivuli cha mti, wakamfuata. Walifika pale na kuketi bila hata kukaribishwa huku wakiwakazia macho ASP Komba na Sajenti Mapambano.
“Habari zenu wakubwa?” Kabwe aliwasalimia ASP Komba na Sajenti Mapambano huku akiwatazama kwa dharau.
“Nzuri, za kwenu?” Jacky peke yake aliitikia ile salamu. ASP Komba na Sajenti Mapambano walibaki kimya huku wakiwatazama kwa umakini.
“Poa. Poleni kwa msiba,” Kabwe alijibu na kugeuka kumtazama ASP Komba, “Habari yako braza?” alimsalimia huku akimkazia macho.
“Nzuri!” ASP Komba alijibu kwa sauti tulivu huku akimtazama Kabwe kwa umakini zaidi. Kisha kikazuka kimya cha kitambo fulani huku wakiangaliana kwa makini. Kisha Liston na Kabwe wakaangaliana na Kabwe alionekana kumkonyeza Liston.
“Jamani, sisi tuna mazungumzo na huyu bibie hapa, tunaomba mtupishe kidogo, au kama vipi twende naye pembeni tukatete kidogo,” Kabwe aliwaambia ASP Komba na Sajenti Mapambano huku akiuma mdomo wake wa chini.
“Zungumzeni tu hapa hapa hamna taabu, au vipi mwenzangu?” ASP Komba aliwaambia huku akigeuka kumtazama Sajenti Mapambano na kuachia tabasamu la kifedhuli.
“Sawa kabisa, wazungumze tu, hata sijui wasiwasi wao ni nini?” Sajenti Mapambano alionekana kuafiki huku akiwaangalia Kabwe na Liston kwa umakini zaidi.
“Aa, noma hiyo washkaji. Haya ni mambo yetu na bibie nyinyi yanawahusu nini? Kama mmekuja kwenye msiba basi fateni ya msiba haya mengine hayawahusu, sawa?” Kabwe alisema kwa sauti ya kibabe huku akiwatazama ASP Komba na Sajenti Mapambano kwa umakini, tayari alikuwa ameanza kupandwa na hasira zisizoelezeka.
“Kama mambo yenu ni ya siri, basi kasubirini kwanza kule ili sisi tumalize maongezi yetu. Lakini hapa hatoki mtu. Mnalazimisha nini wakati watu wengine wamekaa huko pembeni, au mnadhani wao hawataki kuongea na bibie,” ASP Komba alisema huku taratibu akizilamba kingo za mdomo wake kwa ulimi.
Liston alionekana kupandwa zaidi na hasira, alimtazama ASP Komba kwa hasira huku akionekana kutaka kuanzisha matata muda wowote. Kabwe alishtukia na kumtuliza.
“Achana nao mafala hawa…” Kabwe alimwambia Liston huku akionekana kuwapuuza ASP Komba na Sajenti Mapambano, kisha akaongeza. “Oya shem, fanya mambo tuondoke isiwe taabu hapa.”
“Ndiyo ishakuwa taabu. Hawa mnaowaona hapa ni maofisa wa polisi kutoka kituo kikuu cha polisi,” Jacky alimwambia Kabwe kwa sauti tulivu.
Liston na Kabwe walitazamana kisha wakawatupia macho ASP Komba na Sajenti Mapambano huku wakiwatazama kwa makini na hatimaye wakamgeukia tena Jacky.
“Hebu acha kutuwekea mkwara wa kitoto, unataka kutuchezea picha sisi. Hadhulumiwi mtu hapa,” Kabwe alisema huku akimnyooshea kidole Jacky kwa hasira.
“Wala hakuna anayetaka kuwachezea picha, mnataka au hamtaki lakini huo ndiyo ukweli wenyewe…” Jacky alimwambia Kabwe huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.
Muda ule ule kabwe aliinuka ghafla kwa pasipo kutegemea alichomoa bastola yake iliyokuwa imehifadhiwa kiunoni. Aliikamata vyema ile bastola na kuielekezea kwenye kichwa cha Jacky huku akionekana kugadhabika sana. Muda ule midomo yake ilikuwa ikimtetemeka kwa hasira.

Mambo yamezidi kupamba moto, kila mahali ni kizungumkuti tu, na sasa ASP Komba na Sajenti Mapambano wameingia katika anga za Kabwe na Liston, ambao wanahisi kutaka kudhulumiwa. Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia stori hii ya kusisimua...
 
Kweli ni kizungumkuti....ngoja tuone kinachofuata.

Asante Bishop.

Kabwa na liston sijui wapoje ndio shida ya kufanya dili na wahuni
Hahaha, ila hapo wamejileta wenyewe kwa kina Komba. Jacky anaweza akawakana na kuendelea kukomaa kuwaambia hao polisi kua shows zote alikua anajua Carlos. Hapo kilichobaki Jacky angeenda kumwaga pesa hoteli alizoenda kulala na yusuf ushahidi ukafutwe

the Legend☆
 
Ila nimempenda Jacky mafia mkavu kama sio yeye
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom