Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Kizungumkuti! - 49

Na Bishop Hiluka

ILIPOISHIA

Alisoma ujumbe kwa umakini huku akizinakiri baadhi ya namba za simu zilizokuwa zimetumika kutuma ule ujumbe na kuandika taarifa fulani kwenye kitabu chake kidogo na alipomaliza kuandika aliinua uso wake kumtazama Nassos huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

You’re welcome,” (Karibu sana) ASP Komba alimkaribisha Nassos kana kwamba ndiyo alikuwa amemuona kwa mara ya kwanza.

Thank you, officer,” (Ahsante, afande) Nassos alijibu huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

Do you know Swahili?” (Unajua Kiswahili?) ASP Komba alimuuliza huku akimtulizia macho.

Yes, but a little, officer,” (Ndiyo, lakini kidogo, afande) Nassos alijibu kwa kujiamini.

Are you the chief executive director of The Jacarandah Group, right?” (Wewe ndiye mkurugenzi mtendaji wa The Jacarandah Group, sawa?) ASP Komba alimuuliza Nassos huku akiwa amemtulizia macho yake usoni pasipo kupepesa.

Yes, officer,” (Ndiyo, afande) Nassos alisema huku akilamba midomo yake iliyoanza kukauka.

Endelea...

I’ve information that you went to the Commercial Bank four days ago to put a large amount of money, and the next day you took a certain amount of money… Do you remember the amount of money you took that day?” (Ninazo taarifa kwamba ulifika pale Benki ya Biashara siku nne zilizopita kuweka kiasi kikubwa cha pesa, kisha kesho yake ukatoa kiasi fulani cha pesa… Je, unakumbuka idadi ya pesa ulizochukua siku hiyo?)

I took only four hundred million shillings, officer.” (Nilichukua shilingi milioni mia nne tu, afande).

Since that day you’ve never signed in any check from your office?” (Tangu siku ile hujatia tena saini katika hundi yoyote ya ofisini kwenu?)

Not yet!” (Bado!)

ASP Komba aliminya midomo yake na kushusha pumzi za ndani kwa ndani akionekana kutafakari kidogo, kisha alinyoosha mkono wake kumpa Nassos ile hundi.

Can you look well and identify for those signatures?” (Unaweza kuziangalia vizuri na kuzitambua hizo saini hapo?) ASP Komba alisema huku kamkazia macho Nassos. Nassos aliipokea ile hundi na kuitazama kwa makini, alitingisha kichwa chake kwa huzuni huku akishusha pumzi ndefu.

I’m very shocked, this one is my very signature, but I did not sign in this check!” (Imenishangaza sana, afande, hii moja ni saini yangu kabisa, lakini mimi sikutia saini kwenye hundi hii!) Nassos alisema kwa masikitiko huku akimrudishia ASP Komba ile hundi.

And who’s this other sign?” (Na hii saini nyingine ni ya nani?) ASP Komba aliuliza.

It belongs to my accountant, Japhet Lutego, but I'm sure he didn't sign this check,” (Ni ya aliyekuwa mhasibu wangu, Japhet Lutego, lakini nina uhakika pia yeye hakusaini hundi hii) Nassos alisema kwa kujiamini.

Why are you sure that he was not the one who signed?” (Kwa nini una uhakika kuwa si mhasibu wako aliyesaini?)

Because he has traveled to Sweden since last week, and if he’d have been involved in this scandal he’d have not left before this robbery. He’d have possibly waited for his portion.” (Kwa sababu amesafiri tangu wiki iliyopita kwenda masomoni Sweden, na angekuwa ameshiriki kwenye kashfa hii asingeondoka kabla wizi huu mkubwa haujafanyika. Kwa vyovyote angesubiri mgawo wake).

How do you know, maybe he decided to travel before this robbery just to complicate the evidence that he was involved and he might ask them to send his portion there where he went?” (Unajuaje, pengine aliamua kusafiri kabla ya wizi huu ili kupoteza ushahidi kuwa alishiriki na huenda aliomba atumiwe mgawo wake huko huko alikokwenda?) ASP Komba aliuliza tena huku akikunja sura yake.

Nassos alikunja sura yake kutafakari kidogo, kikapita kitambo kifupi cha ukimya kisha alitingisha kichwa chake kukataa.

I don't think so… anyway, I don't know,” (Sidhani… hata hivyo, siwezi kujua) Nassos alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

Kilipita tena kitambo kifupi cha ukimya, ASP Komba alimtazama Nassos kwa huku akitafakari, kisha alikohoa kidogo kusafisha koo lake. “Tell me, who exactly is keeping your check book?” (Hebu niambie, ni nani hasa anayetunza kitabu cha hundi ofisini kwenu?)

It's me!” (Ni mimi!) Nassos alijibu.

Do you lock it or leave with it?” (Huwa unakifungia kabatini au unaondoka nacho?)

I don't lock it or leave with it, it's always on my table…” (Sikifungii wala siondoki nacho, mara nyingi huwa kipo juu ya meza yangu…)

Who enters your office regularly?” (Ni nani anayeingia ofisini kwako mara kwa mara?)

I don't allow people to go into my office, and if a person needs a loan we have a system that he or she’d meet my accountant and then all procedures are followed…” (Huwa siruhusu watu kuingia ofisini kwangu, na kama mtu anahitaji mkopo tuna utaratibu kwamba aonane na mhasibu wangu na kisha taratibu zote hufuatwa…) Nassos alisema kwa utulivu.

Kikapita tena kitambo kifupi cha ukimya, Nassos alikuwa ameinamisha kichwa chake akitafakari kidogo, mara alionekana kugutuka na kuinua uso wake kumtazama ASP Komba.

ASP Komba ambaye muda wote alikuwa akimtazama Nassos kwa makini aliingiwa na shauku baada ya kumuona Nassos akigutuka na kumkazia macho.

Is there anything you want to share with me?” (Kuna kitu unataka kunishirikisha?) ASP Komba aliuliza kwa shauku.

I remember, there is only one person who is free to enter my office at any time, but I don't think if she can be involved with a big deal like this…” (Nimekumbuka, kuna mtu mmoja tu ambaye huwa yuko huru kuingia ofisini kwangu saa yoyote, lakini sidhani kama anaweza kuhusika na njama kubwa kiasi hiki…) Nassos alisema huku akikunja sura yake.

Who is she?” (Ni nani?) ASP Komba aliuliza tena kwa shauku.

Her name is Jasmine Kombo. She deals with the cleanliness of my office.” (Anaitwa Jasmine Kombo. Yeye hushughulikia usafi wa ofisi yangu.)

ASP Komba aliinamisha uso wake kwenye notebook yake na kuandika maelezo mafupi huku akilipigia mstari jina la Jasmine, kisha akamkazia macho Nassos.

How long have you worked with Jasmine?” (Umefanya kazi na Jasmine kwa muda gani sasa?)

This is the fifth year now,” (Huu mwaka wa tano sasa) Nassos alijibu baada ya kufikiria kidogo.

Can I have an interrogation with her?” (Naweza kumpata ili nimhoji?)

I wonder, today is the third day she has not come to work and I’ve no information, I don't know what has happened to her!” (Nashangaa, leo ni siku ya tatu hajafika kazini na sina taarifa zake, sijui amepatwa na nini!) Nassos alisema huku akinyanyua juu mabega yake juu kuonesha kuwa hajui.

Maelezo ya Nassos yakamfanya ASP Komba aweke kituo na kumtazama Nassos kwa macho yaliyoonesha kuhisi jambo lisilo la kawaida. Aligeuza kichwa chake kumtazama Sajenti Mapambano, kisha aliyarudisha tena macho yake kwa Nassos.

Your employee has not come to work without notice for three days and you’re not worried even to look for her! Don't you see this is not normal?” (Mfanyakazi wako hajatokea kazini pasipo taarifa kwa siku tatu na wala hujahangaika kumtafuta! Huoni kama hili si jambo la kawaida?) ASP Komba aliuliza huku akivuta sigara yake kwa mara mwisho na kuupuliza moshi pembeni.

Itaendelea...
 
Habari za Jumamosi, ni siku nyingine tena tunakutana ndani ya dunia yenye KIZUNGUMKUTI, hapa kuna Carlos na Jacky, kule kuna Kabwe, Liston na Kisu, na huku kuna Yusuf, Jacob na bila kuwasahau ASP Komba na Sajenti Mapambano, halafu kwa mbaali nawaona warembo Diana na Zuhura a.k.a Mama Jasmine...

CC the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
Nishawahi siti mkuu

the Legend☆
 
Kizungumkuti! - 50

Kisha alikitupa chini kile kipisi cha sigara kilichokuwa mbioni kuunguza vidole vyake na kukizima kwa kukikanyaga na buti lake.

I was really very busy and I didn't think anything wrong would happen.” (Kwa kweli nilitingwa sana na sikufikiria kama jambo lolote baya lingeweza kutokea.)

Do you know where Jasmine lives?” (Je, unajua Jasmine anaishi wapi?) ASP Komba aliuliza tena huku akiwa ameyatuliza macho yake kwenye uso wa Nassos.

No, but there is one employee who knows her location, unfortunately today she is off until tomorrow,” (Hapana, ila yupo mfanyakazi mmoja ambaye anafahamu nyumbani kwake, bahati mbaya leo hayupo kazini hadi kesho) Nassos alisema baada ya kufikiria kidogo.

What’s her name?” (Anaitwa nani?)

Zena Chande. They’re great friends.” (Zena Chande. Ni marafiki wakubwa).

Okay, you can go, I’ll call you whenever I get new information or need help from you.” (Sawa, unaweza kwenda, nitakupigia simu kila nitakapopata taarifa mpya au nikihitaji msaada kutoka kwako).

No problem, officer, I’m available at any time,” (Hakuna neno, afande, napatikana muda wowote) Nassos alisema huku akiinuka na kunyoosha mkono wake kumpa ASP Komba. Wakaagana kisha Nassos akatoka akiwaacha ASP Komba na Sajenti Mapambano wakiangaliana.

“Hapa kuna mchezo umechezwa ofisini kwake bila yeye kujua, nina wasiwasi na watu wawili, kama siyo mhasibu wake basi ni yule binti Jasmine,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano.

“Kwa Jasmine sidhani, ila kwa yule mhasibu inawezekana, maana aliyefanya wizi huu siyo mtu wa kawaida, he must be a professional bank criminal,” Sajenti Mapambano alisema na kumfanya ASP Komba abetue kichwa chake kukubaliana naye.

“Nadhani baadaye tukizitazama kwa umakini mkubwa zile clip za video kutoka kwenye kamera za usalama zilizoko ndani nan je ya lile jengo la benki tutaweza kugundua kitu zaidi, I’m very sure tutaweza kubaini kitu,” Sajenti Mapambano alisisitiza.

ASP Komba alibetua kichwa chake kukubaliana na maneno ya Sajenti Mapambano huku akizama kwenye tafakari, kisha kama aliyegutuka akamkazia macho Sajenti Mapambano.

“Sasa nenda kamlete yule meneja wa tawi la benki ulikofanyika wizi,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano huku akitoa pakiti ya sigara kisha akatoa sigara moja na kuibana kwenye pembe ya mdomo wake.

Sajenti Mapambano aliinuka na kutoka nje huku akimwacha ASP Komba anajiwashia ile sigara na kuanza kuvuta taratibu huku akitoa moshi na kuutazama kwa makini.

* * * * *

Saa nane na robo mchana Jacky alikuwa amejilaza kwenye sofa kubwa la sebuleni nyumbani kwake Segerea, alikuwa peke yake, kimya kabisa, akijaribu kutafakari hili na lile pasipo kupata majibu. Ni dhahiri kuwa kusambaa haraka kwa taarifa zile za wizi wa mabilioni katika Benki ya Biashara zilikuwa zimemshtua kidogo.

Hakuwa ametarajia kabisa kama taarifa za wizi ule zingeweza kujulikana katika muda mfupi sana kiasi kile, na wala hakujua ni nani aliyekuwa amefichua kuhusu wizi ule. Kilichomtia hofu zaidi Jacky ni suala la kukamatwa kwa Yusuf, aliamini kuwa endapo maofisa wa polisi wangembana kidogo tu wasingepata taabu kuupata ukweli kwani angetapika siri zote akidhani kusema ukweli kungemfanya apunguziwe adhabu.

Kutokana na mshtuko aliokuwa ameupata baada ya kuona clip za video kwenye makundi kadhaa ya WhatsApp, Jacky hakujua alifikaje pale nyumbani kwake, alichokumbuka ni kuwa alijibwaga pale kwenye sofa kubwa sebuleni baada ya kuegesha gari lake kwenye eneo maalumu la maegesho. Hii ilikuwa ni baada ya kuachana na Jacob pale Uhasibu.

Carlos hakuwepo nyumbani na wala Jacky hakuwa amemjulisha kuwa hangerejea kule kwenye nyumba ya Mtoni Kijichi. Jacky alitulia pale kwenye sofa akitafakari, mara akakumbuka jambo na kuanza kuitafuta ile kadi aliyokuwa amepewa na Jacob.

Baada ya kuitafuta kwa sekunde kadhaa hatimaye aliipata kwenye mkoba wake na kuzinakiri namba za simu ya Jacob kisha akapiga na kuiweka simu sikioni. Aliisikia simu ikiita upande wa pili na baada ya kitambo kifupi ikapokelewa.

Hello!” sauti nzito ya Jacob ilisikika ikizungumza kutokea upande wa pili wa simu. Kimya! Jacky alitaka kuitikia lakini akasita huku akijiuliza aseme nini, maana hadi muda ule alipoamua kumpigia Jacob simu hakujua alitaka kumweleza nini. Zikapita sekunde kadhaa bila ile simu kujibiwa, Jacob akaonekana kushangaa kidogo huku akiitazama simu yake kwa wasiwasi.

Hello! Who is this?” (Halo! Nani mwenzangu?) Jacob aliuliza kwa wasiwasi baada ya kusikia sauti ya mtu upande wa pili wa simu akivuta pumzi ndefu.

Hello, Jacob, it’s me Jacky…” (Halo, Jacob, ni mimi Jacky…) Jacky alisema kwa sauti ya unyonge sana iliyoonesha kumshangaza kidogo Jacob.

Ooh Jackline, tell me my love! Are you okay?” (Oo Jackline, niambie mpenzi! Vipi uko sawa?) Jacob aliuliza kwa sauti yenye wasiwasi kidogo baada ya kuhisi Jacky hakuwa sawa.

I’m alright… I need to talk to you, where are you?” (Niko sawa… nahitaji kuongea na wewe, sijui uko wapi?) Jacky alimuuliza Jacob kwa sauti yenye wasiwasi kidogo.

Is there any problem? You sound so strange today. It seems like you’re nervous! What’s wrong my love?” (Vipi kuna tatizo? Sauti yako inaashiria kuwa hauko sawa leo. Ni kama vile una wasiwasi! Vipi kuna tatizo, mpenzi?) Jacob aliuliza maswali mfululizo kwa wasiwasi kidogo baada ya kuhisi sauti ya Jacky haikuwa sawa.

I’m not tense, but I missed you a lot. Today I've noticed that I still love you… and I’m sure that now my happiness will be back,” (Sina wasiwasi, lakini nilikukumbuka sana. Leo ndiyo nimetambua kuwa bado nakupenda… na nina uhakika kuwa sasa furaha yangu sasa itarudi) Jacky alisema huku akishusha pimzi za ndani kwa ndani.

Oh, I'm glad to hear that you still love me…” (Ooh, nafurahi kusikia kuwa bado unanipenda…) Jacob alisema huku sauti yake ikionesha wazi jinsi alivyofurahi, hata hivyo Jacky alimkatiza kabla hajamaliza kuongea.

I need to see you, Jacob,” (Nahitaji kukuona, Jacob) Jacky alisema kwa sauti ya chini.

“Kwa sasa haitawezekana, nawasaidia polisi kushughulikia masuala fulani kuhusiana na wizi uliotokea leo benki, when I finish it, I will let you know, my love, maana hata mimi nimekumiss sana,” Jacob alisema.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 51

“Wizi katika benki?“ Jacky alimuuliza Jacob kwa mshangao kana kwamba alikuwa hajui kilichofanyika.

Yes, Kuna wizi mkubwa wa mabilioni umetokea leo asubuhi katika Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba, and very unfortunate my friend has been linked to the theft and he is now in police custody,” (…na bahati mbaya sana rafiki yangu wa karibu amehusishwa na wizi huo na sasa yupo mahabusu ya polisi) Jacob alisema na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani.

Which friend of yours?” (Rafiki yako yupi?) Jacky aliuliza huku akibana pumzi zake, kisha akakunja sura yake na kufumba macho.

You can't know him, his name is Yusuf Akida, we were together at Tambaza Secondary School and later at IFM…” (Huwezi kumfahamu, anaitwa Yusuf Akida nilisoma naye Tambaza Secondary School na baadaye IFM…)

Jacky alihisi kuishiwa na nguvu, mwili wake ulilegea na pumzi zikampaa kisha jasho jepesi likaanza kumtoka sehemu mbalimbali za mwili wake, woga wa aina yake ulianza kumtambaa mwilini na mapigo ya moyo wake yalibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida! Kikapita kitambo fulani cha ukimya.

Jackline, are you there?” (Jackile, upo kwenye simu?) sauti ya Jacob ndiyo iliyomzindua Jacky.

“Oh… yes… my love,” (Oh… ndiyo… mpenzi) Jacky aliongea kwa kusita sita huku akiwa na mashaka, “So, how do you handle police issues?” (Kwa hiyo, wewe unashughulikiaje masuala kipolisi?)

The Police Officers have come to our company and ask us to help them explore a some phone numbers they are in doubt, that had been contacted with Yusuf, so I have them here at the office,” (Maofisa wa polisi wamekuja kwenye kampuni yetu na kuomba tuwasaidie kuzichunguza namba fulani za simu wanazozitilia shaka zilizokuwa zikiwasiliana na Yusuf, hivyo niko nao hapa ofisini) Jacob alisema na kumfanya Jacky kuhisi kizunguzungu. Kilipita kitambo kirefu cha ukimya kilichomshangaza Jacob.

Hello!…” Jacob alianza kusema lakini Jacky akadakia.

Jacob, I'm very sorry to bother you but I've called you because I have a little problem and I need your help,” (Jacob, samahani sana kwa kukusumbua lakini nimekupigia simu kwa sababu nina tatizo kidogo na ninahitaji sana msaada wako) Jacky alisema huku akishusha pumzi ndefu kama mtu aliyekuwa ametoka kwenye mashindano ya mbio ndefu.

What problem do you have, my love?” (Una tatizo gani, mpenzi?) Jacob aliuliza kwa wasiwasi kidogo.

I can't tell you on the phone, if you have time even now we can meet each other wherever you tell me.” (Sintoweza kukueleza katika simu, kama una muda hata sasa hivi tunaweza kuonana popote utakaponiambia).

“As I told you now it’s not possible, I’ll call you later when I leave the office and tell you where we’ll meet, or what do you say, my love?” (Kama nilivyokueleza kwa sasa haiwezekani, nitakupigia simu baadaye nikishatoka ofisini nikuelekeze wapi tutaweza kukutana, au unasemaje, mpenzi?) Jacob alimuuliza Jacky baada ya kufikiri kidogo.

Okay, I’ll wait for your phone call, please it is very important,” (Okay, nitasubiri simu yako, ni muhimu sana tafadhali) Jacky alisema na kukata simu huku akionesha kukata tamaa, kisha alimeza funda la mate kutowesha koo lake lililoanza kukauka.

Alitafakari kwa sekunde chache akijaribu kuhisi jinsi ambavyo Yusuf alikuwa akitetemeka mbele ya maofisa wa polisi hata kueleza kila kitu alichoulizwa, hata hivyo, Jacky alijipa moyo kuwa polisi asingeweza kuhusishwa na wizi ule kwa kuwa namba aliyokuwa akiitumia haikusajiliwa kwa jina lake halisi, pili Yusuf alimfahamu kama Belinda na hakujua aliishi wapi, na mwisho namba aliyoitumia kuwasiliana na Yusuf aliiwekea uzio kiasi kwamba mtu yeyote asiyebobea katika teknolojia asingeweza kubaini ilikuwa ikipigwa kutokea wapi.

Baada ya kitambo fulani cha kuwaza hili na lile, Jacky alikumbuka kumpigia simu Carlos na kumtaarifu kuhusu yote aliyoyasikia kutoka kwa Jacob, kisha akamweleza kuwa alitarajia kutoka baadaye na huenda angechelewa kurudi nyumbani kwa kuwa ilikuwa ni lazima afuatilie taarifa zote muhimu kuhusiana na upelelezi wa polisi kwenye lile sakata la wizi wa fedha benki.

* * * * *

Jacob alipomaliza kuongea na Jacky aliingia ndani ya ofisi ya Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni ya simu aliyokuwa akiifanyia kazi, alikuwa ametoka nje ya ofisi mara moja kusikiliza ile simu, kwani muda wote alikuwa akitarajia simu kutoka kwa mke na ndugu wa Yusuf waliotaka kujua maendeleo ya dhamana baada ya mkasa ule.

Aliporudi mle ndani alitulia akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wao wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa kampuni aliyekuwa akitoa maelezo kuhusiana na mawasiliano kati ya Yusuf na namba zilizotiliwa shaka.

Hii ilikuwa ni baada ya ASP Komba na Sajenti Mapambano kwenda Makao Makuu ya kampuni ile kubwa ya simu nchini. Ingeweza kuwa rahisi kwa ASP kuzipiga namba zile za simu alizozitilia shaka baada ya kuzipata kutoka kwenye simu ya Yusuf lakini aliamua kufuatilia suala lile mwenyewe katika Ofisi za Makao Makuu ya kampuni ya simu.

Ilikuwa ni nusu saa iliyokuwa imepita ambapo ASP Komba na Sajenti Mapambano walifika kwenye Mapokezi ya ofisi hizo wakiwa wamevaa kiraia, wakasubiri mhudumu amalizane na bwana mmoja, mtu mzima wa Kiasia, kisha wakamfuata. Mhudumu alipowaona aliachia tabasamu pana la makaribisho.

“Karibuni, nikusaidieni nini?” alisema yule mhudumu wa Mapokezi huku akiendelea kutabasamu.

“Tunaomba kumwona Mkurugenzi, tafadhali,” ASP Komba alimweleza yule mhudumu huku naye akiachia tabasamu la kirafiki.

“Mkurugenzi?” yule mhudumu aliuliza kwa mshangao.

“Ndiyo.” ASP Komba alimjibu yule mhudumu huku akimkazia macho. Yule mhudumu alinyamaza kidogo, akapitisha ulimi chini ya mdomo wake wa chini, “Yupi mmojawapo, maana wapo watatu,” aliuliza huku akimtulizia macho ASP Komba.

“Yeyote tu kati yao.”

“Kwani shida yenu ni nini hasa? Kwani hamuwezi kusaidiwa na watu wengine?”

“Kama nani?”

“Inategemea na uzito wa shida yenu.”

ASP Komba aliona mahojiano yangeweza kuchukua muda mrefu, hivyo alitoa kitambulisho chake, akamwekea yule mhudumu mbele ya macho yake.

“Ni masuala ya kazi, dada’angu,” ASP Komba alisema huku akimkazia macho yule mhudumu. Yule mhudumu alipitisha tena ulimi chini ya mdomo safari hii haraka haraka, kisha akameza funda la mate kutowesha koo lake lililoanza kukauka.

“Ngojeni nikupelekeni kwa Mkurugenzi wa Masoko bwana Jacob Haule, nadhani mtaelewana,” yule mhudumu wa Mapokezi alimwambia ASP Komba, ambaye alionekana kushtuka kidogo.

“Ooh, sawa nadhani hata huyo ataweza kutusaidia. Hivi ofisi yake bado iko pale pale ghorofa ya pili, mlango wa tatu, au siyo?” ASP Komba alisema hyuku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Ndiyo, kumbe umeshawahi kufika ofisini kwake. Basi nendeni tu, nitamjulisha sekretari wake.”

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 52

“Asante, dada,” ASP Komba alisema huku akikirudisha kitambulisho chake mfukoni kisha wakazifuata ngazi za kuelekea juu. Walizikwea zile ngazi hadi ghorofa ya pili, wakaufikia mlango wa ofisi ya Jacob iliyokuwa mkono wa kushoto mara baada ya kumaliza kupanda ngazi za kuingia ghorofa ya pili kwenye korido pana. ASP Komba aliusukuma mlango, wakaingia.

Walipoingia walimkuta katibu wa Jacob, msichana mmoja mrembo ambaye alikuwa ameinamisha uso wake kwenye kompyuta akiandaa taarifa fulani za kiofisi. Walipoingia tu yule msichana aliinua uso wake akawatazama. Ilionekana kuwa tabasamu kwa wateja ilikuwa ni kama sheria kwa wafanyakazi wa kampuni ile ya simu, yule msichana naye aliachia tabasamu bashasha.

“Karibuni sana,” alisema yule msichana huku akiinuka kutoka kwenye kiti chake kwa adabu.

“Asante, binti, Habari za kazi?” ASP Komba alisema huku akiufunga mlango baada ya Sajenti Mapambano kuingia, kisha akamsogelea yule msichana huku akiachia tabasamu.

“Nzuri, shikamoo,” yule msichana aliwasalimia kwa adabu huku akiwatazama kwa makini.

“Marhaba,” wale maofisa wa polisi waliitikia kwa pamoja.

“Huyu bwana tumemkuta?” ASP Komba alimuuliza huku akiendelea kutabasamu.

“Ndiyo, yupo… subirini kidogo,” yule msichana alisema huku akienda kugonga kwenye mlango wa Jacob mara moja tu kisha akaingia akiwaacha wale maofisa wa polisi bado wamesimama. Kule ndani alimkuta Jacob na kumweleza ujio wa ASP Komba na Sajenti Mapambano.

Jacob alitoka mara moja na kuwakaribisha ASP Komba na Sajenti Mapambano huku akionesha wasiwasi kidogo.

We are sorry to come here without information, we need your help,” (Samahani kwa kukuvamia hapa bila taarifa, tunahitaji msaada wako) ASP Komba alisema huku akimtulizia macho yake Jacob.

It’s okay, you’re welcome,” (Haina shida, karibuni) Jacob alisema huku akiwakaribisha ofisini kwake. Wote watatu waliingia ofisini kwa Jacob.

Ilikuwa ni ofisi nzuri na pana yenye mazingira ya nadhifu na yaliyovutia kwa mpangilio wa samani za kisasa, ikiwa na zulia jekundu sakafuni na meza ndefu ya ofisini yenye viti vinne. Viti viwili upande wa kushoto na viti viwili upande wa kulia.

Juu ya meza ile ya ofisini kulikuwa na vitabu na majalada machache yaliyopangwa kwa ustadi pembeni ya kibao kidogo kilichochongwa vizuri kwa maandishi ya kutanabaisha cheo cha Mkurugenzi wa Masoko pamoja na kidau cha wino na mhuri wa ofisi.

Upande wa kulia wa ofisi ile kulikuwa na picha kubwa ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na picha nyingine ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikiwa zimetundikwa ukutani. Upande wa kushoto kulikuwa na rafu kubwa ya mbao iliyosanifiwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Ndani ya rafu ile kulipangwa vitabu na majalada mbalimbali na mbele ya ofisi ile ukutani kulikuwa na ramani kubwa ya nchi ya Tanzania iliyoonesha mtandao wa kampuni ile ya simu ulivyoenea nchi nzima.

Jacob aliketi kwa utulivu nyuma ya meza yake kubwa ya ofisini mwisho wa ofisi ile upande wa kushoto akiwa katika uso wa kusawajika kidogo, kisha kwa utulivu akawakaribisha ASP Komba na Sajenti Mapambano waketi kwenye kochi moja la sofa lililokuwa likitazamana na ile meza yake mle ndani.

.

ASP Komba na Sajenti Mapambano waliketi huku macho ya Jacob yakiwatazama kwa udadisi kidogo jinsi walivyokuwa wakiketi kwenye viti. Jacob hakujua kilichokuwa kimewaleta wale maofisa wa polisi pale ofisini kwake, hasa kwa kuwa hakuwa akielewana vizuri na ASP Komba kutokana na Diana.

ASP Komba na Jacob Haule walikuwa marafiki wakubwa utotoni na walisoma darasa moja katika shule ya msingi huko kwao Songea mkoani Ruvuma, lakini urafiki wao ulikuja kuingia doa walipokutana jijini dar es Salaam na ASP Komba kuamua kumuoa Diana wakati akijua fika kuwa alikuwa mpenzi wa Jacob.

Jacob alimtazama ASP Komba akalazimisha tabasamu huku akijaribu kukumbuka kilichokuwa kimetokea saa takriban tatu zilizokuwa zimepita kule kituo cha polisi alipokwenda kutaka kumwekea dhamana Yusuf.

Alikumbuka jinsi ASP Komba alivyomkatalia katakata huku akitingisha kichwa chake kwa nguvu.

“Nani aliyekuambia unaweza kumwekewa dhamana mtu aliyeshirikiana na wezi wakubwa kuiba mabilioni ya fedha benki? Huyu hatoki hapa, si leo wala kesho hadi upelelezi utakapokamilika,” ASP Komba alimweleza Jacob akiwa amekunja sura yake kana kwamba walikuwa hawafahamiani.

“Bwana Komba, mbona maneno mengi, niambie tu moja, kwa hiyo dhamana hamtaki?” Jacob alimwuliza ASP Komba huku akimtulizia macho usoni.

“Hakuna dhamana,” ASP Komba alijibu kwa kifupi huku akiendelea na shughuli zake.

“Kwa nini?” Jacob aliuliza akitaka kujua.

“Kwa nini!” ASP Komba naye alimwuliza Jacob huku akimshangaa.

“Ndiyo, kwa nini? Dhamana ni haki ya kila mtu… Hata kama angekuwa mwuaji,” Jacob alisema kwa sauti tulivu huku akiendelea kumtulizia macho ASP Komba.

“Unanifundisha kazi ndugu yangu, ee?” ASP Komba alisema huku akiyasogeza makaratasi pembeni, akasimama…

______

“Sasa bwana Haule…” sauti ya ASP Komba ilimzindua Jacob kutoka kwenye mawazo yake, akamtazama ASP Komba kwa makini na kuachia tabasamu.

“Nimeshangazwa na ujio wako hapa ofisini, nilikuwa najaribvu kujiuliza sijui kampuni hii tumewakosea nini ndugu zetu wa polisi?” Jacob alisema na kuwafanya waangue kicheko hafifu!

“Wala hamjatukosea lolote, Bwana Haule, usiwe na wasiwasi, kuna jambo muhimu sana lililotulazimisha tuje kwenu kuomba msaada…” ASP Komba alisema huku akijiweka vizuri kwenye sofa. Jacob naye akajiweka vema kitini huku akimtazama kwa makini.

“Kwanza samahani kwa majibu yangu ya asubuhi ulipotaka kumwekea dhamana yule mfanyakazi wa benki, unajua wakati mwingine tunakuwa kwenye tension za…” ASP Komba alianza kusema lakini Jacob alimkatisha.

“Usijali, naelewa… Sasa kabla sijakuuliza ni msaada upi unahitaji, uniambie mpatiwe kinywaji gani?” Jacob alisema kwa sauti tulivu huku macho yake yakiwa hayabanduki kwa ASP Komba.

ASP Komba aliachia tabasamu pana lililomgusa Jacob, “Tunashukuru sana, lakini kwa sasa hatuna kiu ya kinywaji chochote, labda sijui mwenzangu hapa. Sitaki nimsemee…” ASP Komba alisema huku akigeuza shingo yake kumtazama Sajenti Mapambano, ambaye alitingisha kichwa taratibu kukataa.

“Sawa. Basi twende moja kwa moja kwenye hilo lililokuleteni,” Jacob alimweleza ASP Komba huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

ASP Komba alimweleza Jacob msaada waliokuwa wakiuhitaji katika ofisi ile, Jacob akaona suala lile halikuhusiana na ofisi yake, hivyo akawachukua hadi kwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni ile.

Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni, Zuberi Mwalimu, hakuwa mtu mzima sana, alikuwa na miaka arobaini na mitano hivi, mwenye macho maangavu, uso wa duara na nywele ndogo ndogo alizokuwa amezinyoa mtindo wa low cut.

“Karibuni sana,” Zuberi Mwalimu aliwakaribisha huku akinyoosha mkono wake kwa ASP Komba na baadaye kwa Sajenti Mapambano. Walisalimiana kwa furaha, kisha Jacob akamweleza sababu ya ujio wa wale maofisa wa polisi pale ofisini kwao.

Tukutane kesho ili kuyajua yanayoendelea kwenye dunia ya Kizungumkuti...
 
Habari za Jumamosi, ni siku nyingine tena tunakutana ndani ya dunia yenye KIZUNGUMKUTI, hapa kuna Carlos na Jacky, kule kuna Kabwe, Liston na Kisu, na huku kuna Yusuf, Jacob na bila kuwasahau ASP Komba na Sajenti Mapambano, halafu kwa mbaali nawaona warembo Diana na Zuhura a.k.a Mama Jasmine...

CC the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
Mzee baba tupo pa1
 
Waleteee.. Niko ugenini najua sitakua mpweke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kizungumkuti! - 52

Na Bishop Hiluka

“Ni masuala ya kazi, dada’angu,” ASP Komba alisema huku akimkazia macho yule mhudumu. Yule mhudumu alipitisha tena ulimi chini ya mdomo safari hii haraka haraka, kisha akameza funda la mate kutowesha koo lake lililoanza kukauka.

“Ngojeni nikupelekeni kwa Mkurugenzi wa Masoko bwana Jacob Haule, nadhani mtaelewana,” yule mhudumu wa Mapokezi alimwambia ASP Komba, ambaye alionekana kushtuka kidogo.

“Ooh, sawa nadhani hata huyo ataweza kutusaidia. Hivi ofisi yake bado iko pale pale ghorofa ya pili, mlango wa tatu, au siyo?” ASP Komba alisema hyuku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Ndiyo, kumbe umeshawahi kufika ofisini kwake. Basi nendeni tu, nitamjulisha sekretari wake.”

Endelea...

“Asante, dada,” ASP Komba alisema huku akikirudisha kitambulisho chake mfukoni kisha wakazifuata ngazi za kuelekea juu. Walizikwea zile ngazi hadi ghorofa ya pili, wakaufikia mlango wa ofisi ya Jacob iliyokuwa mkono wa kushoto mara baada ya kumaliza kupanda ngazi za kuingia ghorofa ya pili kwenye korido pana. ASP Komba aliusukuma mlango, wakaingia.

Walipoingia walimkuta katibu wa Jacob, msichana mmoja mrembo ambaye alikuwa ameinamisha uso wake kwenye kompyuta akiandaa taarifa fulani za kiofisi. Walipoingia tu yule msichana aliinua uso wake akawatazama. Ilionekana kuwa tabasamu kwa wateja ilikuwa ni kama sheria kwa wafanyakazi wa kampuni ile ya simu, yule msichana naye aliachia tabasamu bashasha.

“Karibuni sana,” alisema yule msichana huku akiinuka kutoka kwenye kiti chake kwa adabu.

“Asante, binti, Habari za kazi?” ASP Komba alisema huku akiufunga mlango baada ya Sajenti Mapambano kuingia, kisha akamsogelea yule msichana huku akiachia tabasamu.

“Nzuri, shikamoo,” yule msichana aliwasalimia kwa adabu huku akiwatazama kwa makini.

“Marhaba,” wale maofisa wa polisi waliitikia kwa pamoja.

“Huyu bwana tumemkuta?” ASP Komba alimuuliza huku akiendelea kutabasamu.

“Ndiyo, yupo… subirini kidogo,” yule msichana alisema huku akienda kugonga kwenye mlango wa Jacob mara moja tu kisha akaingia akiwaacha wale maofisa wa polisi bado wamesimama. Kule ndani alimkuta Jacob na kumweleza ujio wa ASP Komba na Sajenti Mapambano.

Jacob alitoka mara moja na kuwakaribisha ASP Komba na Sajenti Mapambano huku akionesha wasiwasi kidogo.

We are sorry to come here without information, we need your help,” (Samahani kwa kukuvamia hapa bila taarifa, tunahitaji msaada wako) ASP Komba alisema huku akimtulizia macho yake Jacob.

It’s okay, you’re welcome,” (Haina shida, karibuni) Jacob alisema huku akiwakaribisha ofisini kwake. Wote watatu waliingia ofisini kwa Jacob.

Ilikuwa ni ofisi nzuri na pana yenye mazingira ya nadhifu na yaliyovutia kwa mpangilio wa samani za kisasa, ikiwa na zulia jekundu sakafuni na meza ndefu ya ofisini yenye viti vinne. Viti viwili upande wa kushoto na viti viwili upande wa kulia.

Juu ya meza ile ya ofisini kulikuwa na vitabu na majalada machache yaliyopangwa kwa ustadi pembeni ya kibao kidogo kilichochongwa vizuri kwa maandishi ya kutanabaisha cheo cha Mkurugenzi wa Masoko pamoja na kidau cha wino na mhuri wa ofisi.

Upande wa kulia wa ofisi ile kulikuwa na picha kubwa ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na picha nyingine ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikiwa zimetundikwa ukutani. Upande wa kushoto kulikuwa na rafu kubwa ya mbao iliyosanifiwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Ndani ya rafu ile kulipangwa vitabu na majalada mbalimbali na mbele ya ofisi ile ukutani kulikuwa na ramani kubwa ya nchi ya Tanzania iliyoonesha mtandao wa kampuni ile ya simu ulivyoenea nchi nzima.

Jacob aliketi kwa utulivu nyuma ya meza yake kubwa ya ofisini mwisho wa ofisi ile upande wa kushoto akiwa katika uso wa kusawajika kidogo, kisha kwa utulivu akawakaribisha ASP Komba na Sajenti Mapambano waketi kwenye kochi moja la sofa lililokuwa likitazamana na ile meza yake mle ndani.

.

ASP Komba na Sajenti Mapambano waliketi huku macho ya Jacob yakiwatazama kwa udadisi kidogo jinsi walivyokuwa wakiketi kwenye viti. Jacob hakujua kilichokuwa kimewaleta wale maofisa wa polisi pale ofisini kwake, hasa kwa kuwa hakuwa akielewana vizuri na ASP Komba kutokana na Diana.

ASP Komba na Jacob Haule walikuwa marafiki wakubwa utotoni na walisoma darasa moja katika shule ya msingi huko kwao Songea mkoani Ruvuma, lakini urafiki wao ulikuja kuingia doa walipokutana jijini dar es Salaam na ASP Komba kuamua kumuoa Diana wakati akijua fika kuwa alikuwa mpenzi wa Jacob.

Jacob alimtazama ASP Komba akalazimisha tabasamu huku akijaribu kukumbuka kilichokuwa kimetokea saa takriban tatu zilizokuwa zimepita kule kituo cha polisi alipokwenda kutaka kumwekea dhamana Yusuf.

Alikumbuka jinsi ASP Komba alivyomkatalia katakata huku akitingisha kichwa chake kwa nguvu.

“Nani aliyekuambia unaweza kumwekewa dhamana mtu aliyeshirikiana na wezi wakubwa kuiba mabilioni ya fedha benki? Huyu hatoki hapa, si leo wala kesho hadi upelelezi utakapokamilika,” ASP Komba alimweleza Jacob akiwa amekunja sura yake kana kwamba walikuwa hawafahamiani.

“Bwana Komba, mbona maneno mengi, niambie tu moja, kwa hiyo dhamana hamtaki?” Jacob alimwuliza ASP Komba huku akimtulizia macho usoni.

“Hakuna dhamana,” ASP Komba alijibu kwa kifupi huku akiendelea na shughuli zake.

“Kwa nini?” Jacob aliuliza akitaka kujua.

“Kwa nini!” ASP Komba naye alimwuliza Jacob huku akimshangaa.

“Ndiyo, kwa nini? Dhamana ni haki ya kila mtu… Hata kama angekuwa mwuaji,” Jacob alisema kwa sauti tulivu huku akiendelea kumtulizia macho ASP Komba.

“Unanifundisha kazi ndugu yangu, ee?” ASP Komba alisema huku akiyasogeza makaratasi pembeni, akasimama…

______

“Sasa bwana Haule…” sauti ya ASP Komba ilimzindua Jacob kutoka kwenye mawazo yake, akamtazama ASP Komba kwa makini na kuachia tabasamu.

“Nimeshangazwa na ujio wako hapa ofisini, nilikuwa najaribvu kujiuliza sijui kampuni hii tumewakosea nini ndugu zetu wa polisi?” Jacob alisema na kuwafanya waangue kicheko hafifu!

“Wala hamjatukosea lolote, Bwana Haule, usiwe na wasiwasi, kuna jambo muhimu sana lililotulazimisha tuje kwenu kuomba msaada…” ASP Komba alisema huku akijiweka vizuri kwenye sofa. Jacob naye akajiweka vema kitini huku akimtazama kwa makini.

“Kwanza samahani kwa majibu yangu ya asubuhi ulipotaka kumwekea dhamana yule mfanyakazi wa benki, unajua wakati mwingine tunakuwa kwenye tension za…” ASP Komba alianza kusema lakini Jacob alimkatisha.

“Usijali, naelewa… Sasa kabla sijakuuliza ni msaada upi unahitaji, uniambie mpatiwe kinywaji gani?” Jacob alisema kwa sauti tulivu huku macho yake yakiwa hayabanduki kwa ASP Komba.

ASP Komba aliachia tabasamu pana lililomgusa Jacob, “Tunashukuru sana, lakini kwa sasa hatuna kiu ya kinywaji chochote, labda sijui mwenzangu hapa. Sitaki nimsemee…” ASP Komba alisema huku akigeuza shingo yake kumtazama Sajenti Mapambano, ambaye alitingisha kichwa taratibu kukataa.

“Sawa. Basi twende moja kwa moja kwenye hilo lililokuleteni,” Jacob alimweleza ASP Komba huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

ASP Komba alimweleza Jacob msaada waliokuwa wakiuhitaji katika ofisi ile, Jacob akaona suala lile halikuhusiana na ofisi yake, hivyo akawachukua hadi kwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni ile.

Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni, Zuberi Mwalimu, hakuwa mtu mzima sana, alikuwa na miaka arobaini na mitano hivi, mwenye macho maangavu, uso wa duara na nywele ndogo ndogo alizokuwa amezinyoa mtindo wa low cut.

“Karibuni sana,” Zuberi Mwalimu aliwakaribisha huku akinyoosha mkono wake kwa ASP Komba na baadaye kwa Sajenti Mapambano. Walisalimiana kwa furaha, kisha Jacob akamweleza sababu ya ujio wa wale maofisa wa polisi pale ofisini kwao.

Tukutane kesho ili kuyajua yanayoendelea kwenye dunia ya Kizungumkuti...
Shukrani sana Mr kizungumkuti...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kizungumkuti! - 53

Na Bishop Hiluka

ILIPOISHIA

“Sawa. Basi twende moja kwa moja kwenye hilo lililokuleteni,” Jacob alimweleza ASP Komba huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

ASP Komba alimweleza Jacob msaada waliokuwa wakiuhitaji katika ofisi ile, Jacob akaona suala lile halikuhusiana na ofisi yake, hivyo akawachukua hadi kwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni ile.

Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni, Zuberi Mwalimu, hakuwa mtu mzima sana, alikuwa na miaka arobaini na mitano hivi, mwenye macho maangavu, uso wa duara na nywele ndogo ndogo alizokuwa amezinyoa mtindo wa low cut.

“Karibuni sana,” Zuberi Mwalimu aliwakaribisha huku akinyoosha mkono wake kwa ASP Komba na baadaye kwa Sajenti Mapambano. Walisalimiana kwa furaha, kisha Jacob akamweleza sababu ya ujio wa wale maofisa wa polisi pale ofisini kwao.

Endelea...

Baada ya maelezo yale yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano aliinua simu, akamwita Jonas Maganga, mtaalamu wa masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambaye alikuwa tegemea kubwa katika kampuni ile, baada ya kuondoka kwa Jackline Mgaya.

Ndani ya dakika mbili Jonas alikuwa amefika katika ofisi ya bosi wake Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuitika ule wito. Alikuwa kijana mrefu wa wastani na hakuwa na umri wa zaidi ya miaka thelathini.

Alikuwa amevaa shati jeupe la mikono mirefu na juu yake alivaa koti jeusi lililokuwa na mistari myeupe, na saa ya mkononi. Chini alivaa suruali ya kadeti ya rangi ya kaki na buti ngumu za ngozi miguuni.

Yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano alimweleza yule kijana kilichowaleta pale wale maofisa wa polisi na kumpa zile namba nne ambazo ASP Komba na Sajenti Mapambano walikuwa wamezitilia shaka kutoka katika simu ya Yusuf.

“Jonas, tafadhali fuatilia hizi namba kwenye kompyuta na utupatie taarifa zote muhimu za wateja wenye kumiliki namba hizi, ikiwemo majina yao, namba za vitambulisho vyao walivyotumia kusajili, locations zao, na namba zote ambazo zimekuwa zikiwasiliana na namba hizi kwa tarehe husika na saa… sijui itakuchukua muda gani kuifanya kazi hii, maana taarifa hii inatakiwa haraka sana,” yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano alimwambia Jonas huku akimkazia macho.

Jonas aliipokea ile karatasi yenye zile namba akaziangalia zile namba kwa kitambo nkifupi huku akifikiria kidogo, “Wala haitachukua muda, boss. Yote hayo yamo kwenye Kompyuta.”

“Kama nusu saa?” yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano aliuliza kwa shauku.

“Haifiki, ni kama dakika kumi hadi kumi na tano tu zinanitosha kuimaliza kazi.”

“Ooh, basi itakuwa vyema!” yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano alisema huku akitabasamu.

Jonas aliwatupia jicho ASP Komba na Sajenti Mapambano haraka haraka na kuachia tabasamu kisha alitoka haraka huku macho ya wale maofisa wa polisi yakimfuata hadi alipotoka kabisa na kuufunga mlango wa ile ofisi.

“Huyu kijana ndiye tegemeo letu hapa ofisini kwa sasa, kwa kweli anastahili makubwa zaidi… hamtaamini jinsi atakavyoifanya kazi hii kwa uharaka sana na kuleta majibu chanya,” yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano aliwaambia wale maofisa wa polisi baada ya Jonas kuondoka.

“Anaonekana tu kwa jinsi anavyojiamini,” ASP Komba alisema akionekana kuafiki.

“Je, mnadhani hii inaweza kuwa njia sahihi ya kuwakamata hao wezi? Na kama hawakutumia mawasiliano ya simu…” yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano alimuuliza ASP Komba huku akimkazia macho lakini ASP Komba alimkatisha kabla hata hajamaliza kuongea.

“Kwetu, hilo si suala la kudhani, tumekwisha fanya kazi nyingi na ngumu za uhalifu hatari zaidi wa mtandaoni na kufanikiwa. Vyovyote iwavyo lazima tuwatie mbaroni tu,” ASP Komba alisema katika namna ya kujigamba huku akimtupia jicho Jacob.

Kisha yule Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano aliamua kubadilisha maongezi, na baada ya takriban dakika kumi na tano Jonas alirejea ofisini kwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano akiwa ameshika karatasi kadhaa zilizokuwa zimechapwa kwa maandishi ya kompyuta zikiwa na taarifa zote muhimu zilizohitajika.

Alipoingia alizikkabidhi karatasi zile kwa Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Yule Mkurugenzi alizipokea zile karatasi na kuanza kuzipitia papo hapo huku uso wake ukichanua kwa tabasamu dogo la kuridhika na alichokiona. Kisha alimkabishi ASP Komba.

“Naona kijana amefanya kazi nzuri sana, kila ulichohitaji kuhusu hizo namba kimo humo, hebu zipitie kwanza hapa hapa ujiridhishe kabla hujaondoka ili uone kama bado kuna chochote ungependa kutafutiwa.”

ASP Komba na Sajenti Mapambano walizipitia zile karatasi haraka haraka kwa kupokezana kisha ASP Komba alisimama kutoka kwenye kiti alichoketi na kumpa mkono yule Mkurugenzi kumshukuru huku akionesha furaha yake.

“Naona mtaalamu kafanya kazi kubwa na nzuri sana, tunashukuru kwa kweli,” ASP Komba alisema kwa furaha huku akimpa mkono kwa pongezi Jonas.

“Hata hivyo, kuna namba moja kati ya hizo imenisumbua kidogo, ilikuwa imewekewa mfumo maalumu wa kiulinzi,” Jonas alimwambia ASP Komba huku akimtazama kwa makini.

“Una maana gani unaposema mfumo maalumu wa kiulinzi?” ASP Komba alimwuliza Jonas huku akimtulizia macho yake.

“Inaonekana wazi mtumiaji wa namba hiyo ni mtaalamu aliyebobea sana kwenye masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano na ana ufahamu mkubwa sana wa masuala ya kompyuta, aliiwekea namba yake programu maalumu ambayo inamuwezesha mtumiaji wa namba hiyo kutojulikana mahali alipo na ameweza hata kuzuia mawasiliano yake yasiingiliwe na watu wengine, na pia aliifanya namba hiyo kutumika katika simu yake tu.”

“Duh, natumai umefanikiwa kuiondoa hiyo programu ya kiulinzi, siyo?” ASP alimuuliza Jonas kwa shauku huku akimtulizia macho kwa makini.

“Ndiyo, nimeweza kuiondoa programu hiyo japo imenipa shida kidogo, sasa mtaweza kuona jinsi anavyoweza kuwasiliana na watu wengine ingawa mahali alipo wakati anawasiliana na watu bado inaweza kuwa shida,” Jonas alisema huku akishusha pumzi ndefu.

“Hata hivyo, umetusaidia sana… enhe, ni namba ipi kati ya hizi?” ASP Komba alimuuliza Jonas kwa shauku huku akimsogezea zile karatasi.

“Ni hii hapa!” Jonas alisema huku akimwonesha ASP Komba ile namba baada ya kuzitazama zile namba kwa makini.

Itaendelea...

CC the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY IFRS
 
Kizungumkuti! - 54

Na Bishop Hiluka

“Ndiyo, nimeweza kuiondoa programu hiyo japo imenipa shida kidogo, sasa mtaweza kuona jinsi anavyoweza kuwasiliana na watu wengine ingawa mahali alipo wakati anawasiliana na watu bado inaweza kuwa shida,” Jonas alisema huku akishusha pumzi ndefu.

“Hata hivyo, umetusaidia sana… enhe, ni namba ipi kati ya hizi?” ASP Komba alimuuliza Jonas kwa shauku huku akimsogezea zile karatasi.

“Ni hii hapa!” Jonas alisema huku akimwonesha ASP Komba ile namba baada ya kuzitazama zile namba kwa makini.

Endelea...

ASP Komba alibetua kichwa chake huku akiiwekea alama ile namba, “Asante sana, na hii ndiyo namba tutakayoanza nayo katika uchunguzi wetu tukifika tu ofisini,” alisema huku akimtupia jicho Sajenti Mapambano.

“Kazi ya kwanza ambayo tutaweza kuifanya ni kuichunguza kwa umakini zaidi hii namba ya simu yenye programu maalumu ya mfumo wa kiulinzi ili tufahamu Yusuf alikuwa akiwasiliana na nani kwa siri. Nina hakika lazima kuna sababu iliyomfanya mtumiaji wa namba hii kuamua kuificha namba yake hii isionekane na mtu yeyote,” ASP Komba alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Ninatumaini kila kitu kipo sawa, kama kutakuwa na chochote sitasita kuja tena hapa kutaka msaada, tafadhali msinichoke tu,” ASP Komba alimwambia Jacob huku akitabasamu, kisha akampa mkono Jacob.

“Ndugu yangu, tusameheane kwa yote, nadhani umeyaona mazingira ya kazi zetu jinsi yalivyo magumu,” ASP Komba alisema huku akimpa mkono.

“Usijali,” Jacob alisema kwa kifupi huku akiuma mdomo wake wa chini na kushusha pumzi.

Wakaagana kisha ASP Komba na Sajenti Mapambano wakatoka nje ya ile ofisi. Walitembea kwa utulivu huku mawazo mengi yakipita kichwani kwa ASP Komba na walipozifikia zile ngazi wakaanza kuzishuka taratibu na baada ya muda mfupi hatimaye wakawa wamefika eneo la chini la lile jengo na hatimaye wakatokea eneo la Mapokezi. ASP akaona ni vyema wapiti kwanza pale Mapokezi ili kwenda kuaga

“Vipi mmefanikiwa?” yule mhudumu wa Mapokezi alimwuliza ASP Komba huku akitabasamu mara baada ya kuwaona.

“Sana! Wala hatuna cha kulalamikia,” ASP Komba alisema kwa utani huku akiachia tabasamu.

“Haya, karibuni tena,” yule mhudumu alisema huku akiangua kicheko hafifu.

“Nitarudi mara tu nikimaliza kazi hii, lakini safari hii sitakwenda tena ghorofa ya pili bali nitaishia hapa hapa Mapokezi,” ASP Komba alisema kwa utani na wote watatu wakacheka.

* * * * *

Everything is in position now,” ASP Komba alimwambia Sajenti Mapambano huku akiziangalia taarifa nyeti kwenye kompyuta maalumu ya ofisi iliyokuwa mbele yao ikiwa imeunganishwa na mfumo maalumu wa kiintelijensia uliowawezesha kupata taarifa mbalimbali za kiintelijensia kwa ajili ya kubaini mambo mbalimbali ya uhalifu wa kimtandao.

ASP Komba na Sajenti Mapambano walikuwa wameketi ndani ya chumba cha ofisi ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu katika jengo la Kituo Kikuu cha polisi Dar es Salaam, maarufu kama Central Police.

Chumba cha ofisi ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu kilikuwa kikubwa kilichokuwa upande wa kushoto kabisa mara baada ya kumaliza kupanda ngazi za kuingia katika ghorofa ya tatu kwenye korido pana, kilikuwa hatua chache baada ya kuzipita ofisi za Idara ya Intelijensia ya Jinai na ile ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali.

Kilikuwa chumba kipana na sakafu ya ofisi ile ilifunikwa kwa zulia maridadi jekundu huku katikati ya lile zulia likiwa na nembo kubwa ya Jeshi la Polisi la Tanzania. Chumba kile kilikuwa na meza ndefu ya mikutano iliyozungukwa na viti kumi na mbilii. Viti vitano upande wa kushoto, viti vingine vitano upande wa kulia, kiti kimoja mwanzoni mwa ile meza na kiti kimoja kilikuwa mwisho wa meza.

Upande wa kushoto wa chumba kile kulikuwa na picha kubwa tatu, ya kwanza ilikuwa ni ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, picha ya pili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na picha ya tatu ilikuwa ya Inspekta Jenerali wa Polisi, sote zikiwa zimewekwa kwenye fremu maalumu za vioo na kutundikwa ukutani.

Mbele ya kile chumba ukutani kulikuwa na ramani mbili kubwa. Ramani moja ya nchi ya Tanzania na ramani ya pili ya Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Upande wa kulia kulikuwa na rafu kubwa ya mbao iliyosanifiwa kwa ustadi wa hali ya juu. Ndani ya rafu ile kulipangwa vitabu na majarida mbalimbali.

Kulikuwa na meza kubwa mbili za ofisini zenye majalada mengi juu yake. Bendera ndogo nne zilionekana juu ya zile meza, mbili zikiwa bendera za Taifa na nyingine mbili zilikuwa bendera za Jeshi la Polisi. Vitabu kadhaa vya Katiba ya Tanzania, kidau cha wino, mhuri na kichupa kidogo chenye wino mweupe wa kufutia maandishi.

Nyuma ya meza zile kulikuwa na viti vikubwa vya ofisini vyenye foronya laini na kwenye kiti kimojawapo nyuma ya meza moja yenye kompyuta aina ya IMac alikuwa ameketi ASP Komba na Sajenti mapambano alikuwa amesimama kando yake wakifuatilia taarifa kwenye ile kompyuta.

Pembeni ya ile meza ya ofisini chini yake kulikuwa na mashine ndogo ya kidijitali ya kurudufu, mashine maalumu ya kuchapa barua na nyraka za kiofisi, mashine ya picha na mashine moja ya nukushi.

Upande wa kulia wa ile meza aliyokuwa ameketi ASP Komba kulikuwa na kabati kubwa nadhifu la chuma lenye droo sita. Pia ukutani kulitundikwa saa kubwa ya mshale na pembeni ya saa ile kulikuwa kalenda moja kubwa. Na kando yake kwenye ukuta juu ya rafu kubwa kulikuwa na runinga bapa iliyounganishwa na chaneli tofauti za kimataifa iliyokuwa imetundikwa ukutani.

Kulikuwa na seti moja ya makochi mazuri ya ngozi laini ya sofa yaliyoizunguka meza ya kioo yenye umbo duara na chini ya meza ile kulikuwa na magazeti na majarida kadhaa tofauti na kando ya makochi yale kulikuwa na rafu kubwa ya vitabu na majalada yaliyopangwa kwa ustadi wa hali ya juu. Kulikuwa na kiyoyozi kikubwa mle ndani kilichokuwa kikisambaza hewa safi.

Ki ujumla ofisi ile ilikuwa ya kistaarabu sana yenye samani za kisasa na iliyopangiliwa vizuri na muonekano wake uliendana kabisa na ule kipelelezi wa makosa ya jinai.

ASP Komba alikuwa katika uso wa kusawajika kidogo huku akiwa ameegemea kiti chake. Alikuwa kimya kabisa akiziangalia zile taarifa kwa makini walizokuwa wamepewa kule kwenye ofisi za kampuni kubwa ya simu na kujaribu kulinganisha na taarifa walizokuwa wakizipitia kwenye ile kompyuta. Sajenti Mapambano alisimama akipitia taarifa zile kwa utulivu.

Sajenti Mapambano alibofya kitufe fulani kwenye ile kompyuta na kuanza kupandisha maandishi akitafuta taarifa fulani kisha akaingiza taarifa za namba waliyokuwa wakiichunguza, akaipachika katika kifaa fulani kidogo mithili ya mkebe na kuanza kuibonyeza ile kompyuta. Mara akaguna

This is very strange! Inawezekanaje hii namba yenye mfumo wa ulinzi ikawa imetumika kuwasiliana na watu wawili pekee yake!” Sajenti Mapambano alisema kwa mshangao huku akikodolea macho kwenye ile kompyuta.

ASP Komba alimtazama kwa makini kisha akaziangalia zile taarifa na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku naye akionesha kushangaa.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 55

“Ni kweli, imewasiliana na watu wawili tu! Kwa mujibu wa taarifa za kampuni ya simu namba hizo ni za Yusuf na nyingine ni ya mtu anayeitwa Joram Mbezi. Inaonesha huyu mwenye namba hii na hawa watu wamekuwa wakiwasiliana zaidi katika wiki hizi mbili za mwisho kabla ya kutokea kwa wizi wa mabilioni pale benki,” ASP Komba alisema huku akizikodolea macho zile namba.

“Na kwa mujibu wa taarifa kutoka kampuni ya simu namba hii inamilikiwa na mtu anayeitwa Belinda Jackson,” Sajenti Mapambano alisema huku akizitazama zile karatasi walizozitoa kampuni ya simu, kisha akabonyeza kifute fulani kwenye ile kompyuta na baada ya dakika kama tatu hivi akasimama na kuvuta pumzi ndefu.

“Inabidi kupata taarifa za hawa watu wawili, Belinda Jackson na Joram Mbezi ili tuwajue ni kina nani hasa kabla hatujawaunganisha kwenye hili tukio la wizi, nadhani tunaweza kufuatilia taarifa zao kwenye mtandao wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Nida, na ule wa kiintelijensia wa Jeshi la Polisi,” ASP Komba alisema huku akiminya midomo yake.

Sajenti Mapambano alibofya kwenye ile kompyuta na kuingia kwenye mtandao maalumu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ambao ulikuwa umeunganishwa na ile kompyuta ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu.

Baada ya kuperuzi kwa dakika kadhaa na kupata taarifa kamili za Joram Mbezi, Sajenti Mapambano aliingia kwenye mtandao mwingine wa kiintelijensia na kutafuta taarifa zaidi za Joram Mbezi ili kuona kama amewahi kuhusishwa na matukio yoyote ya uhalifu, mara akaonekana kushtuka kidogo.

Alisimama akafikicha macho yake na kuzitazama tena zile taarifa akiwa haamini macho yake.

“Joram Mbezi, mfanyabiashara wa kuuza madini ya rubi, tanzanite na mengineyo, anaishi eneo la Sinza jijini Dar es Salaam na ana umri wa miaka takriban hamsini. Historia yake imekuwa yenye utata kidogo kwa kuwa amewahi kuhusishwa mara kadhaa na matukio ya uhalifu katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania…” Sajenti Mapambano alisema huku akisoma zile taarifa kutoka katika ile kompyuta ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Kanda Maalumu.

“Ila huyu Belinda Jackson inaonekana habari zake zinakanganya sana inawezekana ni mtu hatari mno kuliko tunavyoweza kudhani kwani taarifa zinadai kuwa alikuwa daktari bingwa wa afya ya akili katika Hospitali ya Milembe mkoani Dodoma na alifariki miaka mitatu iliyopita. Inashangaza kuona kuwa hii namba yake imesajiliwa miezi mitatu tu iliyopita na imetumika zaidi wiki mbili za mwisho kabla ya tukio la wizi pale benki…” Sajenti Mapambano alisema huku akimtazama ASP Komba. Wakatazamana kwa kitambo kifupi, kila mmoja akijaribu kutafakari kwa kina.

“Kwa hiyo maana yake ni kwamba marehemu Belinda aliisajili hii namba wakati tayari akiwa marehemu kwa takriban miaka mitatu!” ASP Komba aliuliza kwa mshangao huku akihisi uwepo wa kitu kisichokuwa cha kawaida kwenye ile namba.

“Hapa ndipo penye utata wenyewe, nadhani kuna namna hapa, ndiyo maana hii namba ikawekewa mfumo wa siri wa kiulinzi ili mtu huyu asiweze kufuatiliwa katika mawasiliano yake na hawa watu wawili, Yusuf Akida na Joram Mbezi. Inawezekana kabisa kwa kumbana Yusuf tutaweza kumtambua huyu mtu anayejiita Belinda, na huenda akawa na laini nyingine za siri ambazo huzitumia kuwasiliana na watu wengine zaidi,” Sajenti Mapambano alisema na kuanza kutafuta taarifa zaidi.

ASP Komba alichoka kabisa, aliamua kusimama na kuelekea kwenye dirisha, kwa dakika kadhaa alitulia pale dirishani huku akitazama nje kupitia ukuta msafi wa kioo cha lile dirisha, aliyatazama magari mbalimbali yaliyokuwa yakipita barabarani huku akionekana kuyachunguza kwa utulivu, mikono yake alikuwa ameiegemeza pale dirishani.

Kisha macho yake yakahamia kutazama pale chini ya lile jengo kulipokuwa na magari machache yaliyoegeshwa katika sehemu ya maegesho ya magari ya lile jengo. Na hapo akaliona gari aina ya Toyota Lexus RX la rangi nyeusi likiegeshwa sehemu ile. Lile gari ASP Komba alilitambua mara moja kuwa lilikuwa gari la Jacob.

* * * * *

Ilikuwa saa kumi na mbili na nusu wakati Jacky alipokuwa akiingia katika sebule kubwa yenye masofa mazuri nyumbani kwa Jacob.

It’s a nice place, I really liked your home,” (Ni sehemu nzuri, nimepapenda sana nyumbani kwako) Jacky alimwambia Jacob wakati akiingia katika sebule ile kubwa huku akiitazama kwa makini. Sakafuni kulikuwa na zulia zuri la rangi nyekundu huku katikati ya sebule ile kukiwa na meza fupi ya kioo yenye umbo la yai.

Upande wa kushoto wa ile sebule kwenye kona kulikuwa na runinga pana iliyofungwa ukutani huku chini yake kukiwa na meza fupi nyeusi yenye sistimu ya muziki, deki ya Dvd, kingamuzi cha DStv na vinyago vya Kimakonde vilivyokuwa vimepangwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Upande wa kulia wa ile sebule kwenye kona nyingine kulikuwa na meza fupi ya mapambo. Kutoka pale alipokuwa amesimama Jacky upande wa kulia kulikuwa na mlango mkubwa wa sebule ile katikati ya madirisha mapana ya vioo yaliyofunikwa kwa mapazia marefu. Ulikuwa ni mlango wa kuelekea kwenye vyumba vya kulala vya ile nyumba.

Nyumba ya Jacob ilikuwa nzuri na kubwa ya kisasa iliyozungukwa na miti mizuri ya vivuli na sehemu za wazi zenye bustani nzuri ya maua na nyasi za kijani kibichi zilizokatiwa vizuri.

Nyumba ile ilikuwa na ukuta mfupi kuizunguka wenye nakshi za hapa na pale kiasi cha kumruhusu mtembea kwa miguu kuweza kuona mle ndani kwa shida kidogo. Mbele ya ile nyumba kulikuwa na geti kubwa jeusi na kando ya lile geti kulikuwa na kitufe cha kengele.

Ilikuwa ni nyumba kubwa ya kisasa ya ghorofa moja iliyokuwa na madirisha makubwa ya kisasa ya vioo na baraza kubwa mbele yake.

Nje ya nyumba ile upande wa kulia kulikuwa na banda la wazi la kuegeshea magari na alipochunguza akaona kuwa kulikuwa na magari awili ya kifahari aina ya Mercedes Benz E-class limousine jeusi lenye milango sita na gari aina ya Toyota Lexus RX la rangi nyeusi.

Sehemu nyingine ya mandhari ya nyumba ile ilizungukwa na miti mirefu na mikubwa ya kivuli, hata hivyo matawi makubwa ya miti ile yalikuwa yametengeneza vichaka vilivyosababisha kiza fulani.

Sehemu ya mbele ya ile nyumba ilikuwa imezungukwa na bustani nzuri ya maua ya kupendeza yaliyotoa harufu nzuri na katikati ya bustani ile kulitengenezwa njia nzuri ya kutembea kwa miguu kwa vitofali vidogo vilivyokuwa vinavutia.

“Sijui unatumia kinywaji gani?” Jacob alimwuliza Jacky huku akimtazama kwa makini.

“Mvinyo mwepesi tafadhali,” Jacky alisema, na hapo Jacob akainuka na kuelekea kwenye jokofu kubwa la vinywaji.na kurudi na chupa ya mvinyo, akamimina katika bilauri mbili, moja akampatia Jacky na nyingine akabaki nayo mwenyewe, kisha waligongesha zile bilauri kutakiana afya njema huku Jacob akiachia tabasamu pana.

Itaendelea...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom