Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Kizungumkuti! - 42

Na Bishop Hiluka

ILIPOISHIA

Carlos na kampani yake walikuwa kimya pale sebuleni wakinywa na kutafakari, na juu ya meza ndogo zilizokuwa mbele yao kulikuwa na mizinga mitatu mikubwa ya mvinyo na bilauri kadhaa. Hii ilikuwa ni kama sherehe ndogo baada kwa kufanikiwa kufikisha mzigo salama licha ya hekaheka za kupita huku na kule, barabara hizi na zile katika safari ya mzunguko ambao ingekuwa vigumu sana mtu yeyote kuelewa walielekea wapi endapo angejaribu kuwafuatilia.

Kwa kifupi ni kwamba, baada ya kutoka pale Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba gari lao aina ya Ford Transit lenye nembo ya NeoVision Security liliifuata barabara ya Bibi Titi Mohammed na kwenda moja kwa moja hadi makutano ya barabra ile na barabara ya mtaa wa Nkrumah.

Hapo Carlos aliongeza kasi ya mwendo wa gari huku akipiga king’ora kuyataka magari mengine yakae kando huku akikatisha katikati ya majengo ya ghorofa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), yaliyokuwa katika pande zote mbili za barabara ile ya Nkrumah.

Endelea...

Alipoivuka reli katika eneo la Goldstar alikunja na kuingia kushoto akiifuata barabara ya mtaa wa Lugoda, wakapita katikati ya majengo makubwa yalikuwa na ofisi mbalimbali na kwenda kutokea katika barabara ya mtaa wa Gerezani iliyokuwa ikitokea Posta, na hapo akakunja na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara ile ya Gerezani.

Aliendelea kupiga king’ora kuyataka magari mengine yakae kando huku akiyapita kwa mwendo wa kasi na kuufika mzunguko wa barabara za Gerezani iliyotokea Kariakoo kwenda Posta na ile ya Bandari iliyoelekea Kurasini. Aliifuata barabara ya Bandari na mwendo wake haukuwa wa kubahatisha hata kidogo.

Akalivuka daraja ambalo chini yake kulikuwa na njia za treni kuelekea bandarini, hakupunguza mwendo hadi alipofika katika mzunguko ulioziunganisha barabara za Bandari, Kilwa na Mandela. Na hapo akazunguka na kuifuata barabara ya Kilwa.

Alizidi kusonga mbele zaidi hadi alipoivuka baa maarufu ya Pentagon mbele kidogo akaachana na barabara ya Kilwa na kuingia katika mtaa mmoja kushoto kwake, kisha akaivuka Meshack Automotive Solutions halafu akakata tena kushoto akiingia ndani zaidi katika eneo la Mivinjeni, kisha alikwenda kuliegesha gari lake chini ya kivuli cha miti mikubwa katika eneo lile la Mivinjeni.

Kwa muda ule eneo lile halikuwa na pilika pilika zozote, hivyo kitendo bila kuchelewa, wote walishuka haraka kutoka kwenye lile gari huku Kabwe akilishusha lile begi lenye fedha kisha wakaingia kwenye gari jingine la kifahari aina ya Toyota Alphard jeupe lililokuwa likiwasubiri pale.

Ndani ya lile gari aina ya Toyota Alphard kulikuwa na mtu mmoja tu, dereva ambaye ni Jacky, aliyekuwa ameketi nyuma ya usukani kwa utulivu.

Muda ule ule Liston alitumia utaalamu wake wa hali ya juu wa uhandishi wa umeme, kukorofisha mfumo wa umeme wa lile gari aina ya Ford Transit, na hapo gari likashika moto.

Kisha aliingia haraka kwenye lile Toyota Alphard lililoanza kuondoka taratibu, alipoingia tu likaondoka kwa mwendo wa kasi kutoka eneo lile kabla hata watu hawajang’amua nini kilichokuwa kikiendelea pale. Kitendo kile kilifanyika ndani ya muda mfupi sana sawa kitendo cha kufumba jicho na kufumbua.

Jacky alikuwa makini sana na kazi yake na alikuwa amevaa soksi maalumu za mikononi (gloves). Wakati wanatokomea mtaani waliliacha lile gari aina ya Ford Transit likiteketea kwa moto na hivyo kuvuta makundi ya watu kushuhudia na wengine wakijaribu kuuzima ule moto, na hivyo hakuna aliyeweza kuwafuatilia.

Kutoka pale walielekea moja kwa moja Mtoni Kijichi na kufika kwenye lile jumba, Carlos akabonyeza remote maalumu ya kufungua geti kubwa jeusi mbele ya lile jumba na mara lile geti likaanza kufunguka, walipoingia ndani lile geti likajifunga.

Jacky alikwenda moja kwa moja kwenye chumba maalumu kilichokuwa kinatumika kama ofisi maalumu na maktaba ya siri kilichofanana na kile kilichojengwa kwenye ile nyumba ya Segerea, alikuwa anaburuza lile begi lenye magurudumu lililojaa fedha.

Chumba hiki kilikuwa na ulinzi wa uhakika na ili kuingia mle ndani ilikuwa ni lazima ubofye namba fulani za siri zilizokuwa kwenye kisanduku kidogo chenye namba pembeni ya mlango.

Jacky alipoufikia mlango wa chumba kile, ambao juu yake kulikuwa na taa nyekundu ikiwaka alibonyeza namba nne za siri kwenye kile kisanduku kilichokuwa pembeni ya mlango kisha akaweka dole gumba la mkono wake wa kulia katika sehemu maalumu iliyokuwa ikiwaka taa ya kijani.

Thank you, Jackline, you’re welcome…” sauti maalumu kwenye spika ndogo pembeni ya mlango ikasikika ikimkaribisha Jacky huku ikiambatana na maandishi “Welcome Jackline” na mara mlango ule ukafunguka.

Jacky aliliingiza lile begi na kulihifadhi kwenye kabati maalumu na kutoka kwenda kujiunga na watu wengine waliokuwa wameketi sebuleni wakijipongeza kwa mvinyo. Kabwe alinyanyua bilauri yake na kugida pombe yote iliyokuwemo kwa mkupuo mmoja, kisha aliikita ile bilauri mezani huku akisisimkwa mwili, alionekana kuwa mwenye haraka ya jambo fulani.

“Kwa hiyo, kamanda, inakuwaje sasa?” Kabwe alimuuliza Carlos huku akimkazia macho.

“Kuhusu nini?” Carlos alimuuliza Kabwe kwa mshangao huku akimtazama kwa makini.

“Kuhusu pesa, baba’ke… tupe chetu tusepe kwani tunasubiri nini hapa?” Kabwe alijibu huku akifinya macho yake kutokana na ulevi ulioanza kumwingia.

“Naomba tusifanye papara ya kugawana fedha, tusubiri kwanza kwa siku mbili tuone hali itakuwaje,” Carlos aliongea kwa sauti ya utulivu huku akiwatazama watu wote na kuupeleka mche wake wa sigara mdomoni.

Kabwe alikunja sura yake na kutingisha kichwa kwa nguvu akionesha kukataa na wakati huo huo hasira zilikwisha anza kumpanda.

“Aah, hiyo sasa noma, kamanda…” Kabwe alisema na kugeuka kuwatazama Kisu na Liston, “Au siyo wanangu! Eti tusubiri siku mbili, huu si ndiyo mwanzo wa kuingizwa cha kike! Siku mbili tusubiri nini, pingu?”

“Hatusubiri pingu, wala hakuna mtu yeyote mwenye kutaka kuwaingiza cha kike, kwanza siku mbili wala siyo nyingi, na kama mambo yatakuwa shwari tukutane kule kwenye nyumba ya Segerea ili kila mtu achukue chake. Kwani tatizo liko wapi?” Carlos alisema kwa sauti tulivu huku akiwatazama mmoja baada ya mwingine.

Kabwe alizidi kutingisha kichwa chake kukataa, aliwatazama Kisu na Liston kwa kitambo, kisha akamgeukia tena Carlos.

“Unajua mkubwa, hii shughuli haikuwa mchezo, na wewe unajua hilo,” Kabwe aliongea kwa hamaki huku akiwa amekunja sura yake iliyotengeneza ndita usoni.

“Najua sana, ndiyo maana nilihitaji kupata watu wa aina yenu ili kuifanya,” Carlos alisema kwa sauti tulivu akionesha kukubaliana na maneno ya Kabwe.

“Sasa kama unajua hivyo, ni lazima ujue vile vile kwamba tumejitolea roho zetu ili tutengeneze fedha itusaidie kwenye maisha yetu, au siyo, kamanda?”

“Sawa sawa!”

“Sasa fedha yenyewe si ndo hii tuliyoipata? We tukatie chetu tuondoke ili kila mtu ajue ustaarabu wake, kwani kero iko wapi?” Kabwe alizidi kusisitiza apewe mgawo wake huku akionekana kukosa uvumilivu.

Hata hivyo, muda wote wakati Kabwe akiongea, Kisu alikuwa akitabasamu tu bila kusema chochote na Liston alikuwa kimya kabisa akisikiliza kwa makini jinsi ambavyo Carlos na Kabwe walivyokuwa wakilumbana, ingawa wote kila mmoja alikuwa na yake rohoni.

“Tatizo lako Kabwe hunifahamu vizuri, mbona hushangai Kisu na Liston hawana presha? Sina kawaida ya kumdhulumu mtu, nimeshafanya nao kazi kibao za fedha nyingi kuliko hata hii na nikawapa chao bila usumbufu,” Carlos alisema na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku akijaribu kuidhibiti hasira.

“Kabwe, Listoni na Kisu ni watu watatu tofauti na kila mmoja ana changamoto zake, huenda wao wameshiba lakini mimi nina njaa. Ninahitaji fedha ili kutatua matatizo yangu na kama sijakosea tulikubaliana kulipana mara baada ya kazi, na kazi yenyewe ndo hii imeshafanyika kwa ufanisi mkubwa, sijui haya mengine ya kusubiri siku mbili yanatoka wapi, mkubwa!” Kabwe alisema huku akirusha mikono yake juu kwa hasira.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 43

“Okay, naomba unisikilize, niko tayari kuwapa ninyi wawili, wewe na Liston fedha kiasi za kutumia siku hizi mbili wakati tukisubiri, na kama mambo yakiwa shwari tukutane kule Segerea keshokutwa saa kumi na mbili jioni ili kila mmoja achukue chake, au vipi!” Carlos alisema kwa utulivu huku akimkazia macho Kabwe.

“Kwa nini tupewe sisi wawili tu, kwani Kisu hayumo kwenye listi?” Kabwe aliuliza kwa mshangao.

“Makubaliano yangu na Kisu ninyi hayawahusu na wala si kazi yenu kujua namlipaje,” Carlos alisema kwa utulivu huku akijitahidi kuidhibiti hasira yake.

Baada ya kauli ile kikapita kitambo kifupi cha ukimya huku Kabwe na Liston wakiangaliana kama waliokuwa wanauliza mambo ambayo hawakupenda Carlos ajue. Kisha Kabwe alibetua mabega yake juu na kugeuka kumtazama Carlos. “Kwa hiyo leo utakata shilingi ngapi, boss?”

“Nitakupeni shilingi laki tano kila mmoja, lakini hii fedha wala haimo kabisa kwenye mgao, naitoa tu kama offer kutoka mfukoni mwangu,” Carlos alisema huku akigeuza shingo yake kumtazama Jacky, ambaye muda wote alikuwa ameketi kimya kwenye kona moja ya ile sebule akiwa makini sana.

Kabwe na Liston waliangaliana tena kisha kikapita kitambo kingine kifupi cha ukimya. Liston alishusha apumzi za ndani kwa ndani na kumpiga ukope Kabwe kama ishara ya kumtaka akubali wachukue zile fedha.

“Poa, boss, basi leta hizo fedha sisi tujikatae,” Kabwe alisema huku akichukua chupa ya mvinyo na kujimiminia kwenye bilauri, kisha akapiga funda kubwa la mvinyo na kusisimkwa.

Carlos aliinuka na kupanda ngazi kuelekea ghorofani huku akisindikizwa na macho ya watu wote pale sebuleni, na baada ya muda mfupi aliteremka ngazi akiwa ameshika mabunda mawili ya noti nyekundu nyekundu na kuwarushia Kabwe na Liston, kila mtu na la kwake.

Kila mmoja alizidaka zile fedha, Kabwe alionekana kukenua meno yake kwa furaha, kisha alimkonyeza Liston akimpa ishara ya kuondoka.

“Sasa tunaondokaje, boss?” Kabwe alimuuliza Carlos huku akiwa tayari amesimama wima kwa ajili ya kuondoka.

Carlos aligeuza shingo yake kumtazama Jacky na kumpa ishara fulani, Jacky aliinuka na kuelekea juu haraka na baada ya dakika kama kumi hivi alirudi akiwa amevaa sketi fupi ya rangi nyeusi yenye miraba myeupe, blauzi nyeupe ya mikono mirefu na viatu vya kamba. Mkononi alikuwa ameshika ufunguo wa gari.

Ile sketi ilikuwa imenasa vyema kwenye tumbo lake dogo na kiuno chembamba lakini imara kilichoshikilia minofu laini ya mapaja yake makubwa na kuifichua hazina iliyotukuka ya miguu yake mizuri.

Alipotokea tu harufu nzuri ya marashi ghali aina ya Clive yenye kuhamasisha ngono aliyokuwa amejipulizia mwilini ilitamalaki pale sebuleni na kuzifanya pua za watu wote pale sebuleni kupata uhai mpya. Jacky aliwatazama Kabwe na Liston na kuwapa ishara kuwa wamfuate, na hapo wote watatu wakaanza kutoka nje huku wakiwaacha Kisu na Carlos bado wameketi.

Walipotoka waliingia ndani ya gari la Jacky aina ya Range Rover Sport L494 jeupe, Jacky akabonyeza remote na mara lile geti kubwa la nyumba likafunguka na kuruhusu gari litoke nje.

“Sijui niwapeleke wapi, mabwana?” Jacky aliwauliza mara tu alipotoka nje ya lile jumba la kifahari. Kabwe na Liston waliangalia katika namna ya kuulizana.

“Kama unaweza tupeleke Kinondoni, vinginevyo unaweza kutuacha pale Viwanja vya Sabasaba,” Kabwe aliyekuwa ameketi siti ya mbele kushoto kwa dereva alijibu huku akiachia tabasamu.

Jacky aliingiza gia na kuliondoa gari kwa mwendo wa kasi, magurudumu ya gari yalichuna ardhi wakati lilipokuwa likiingia katika barabara ya mtaa na baada ya mwendo mfupi likaingia katika barabara ya Kilwa. Hapo Jacky akaongeza mwendo na gari likaserereka.

Katika barabara ile ya Kilwa muda wote Kabwe alionekana kumtupia jicho la wizi Jacky huku akiyaangalia mapaja yake yaliyonona kwa matamanio. Baada ya mwendo wa kitambo fulani Kabwe akaonekana kushindwa kuvumilia, akajikohoza kidogo ili kusafisha koo lake, kitendo kilichomfanya Jacky ageuze shingo yake kumtazama kwa makini.

“Shem, kwa kweli nimeshindwa kuvumilia, naomba nikiri tu kuwa wewe ni mrembo mno, sijawahi kumuona msichana mrembo kama wewe…” Kabwe alisema huku akipitisha ulimi wake kulamba midomo yake iliyoanza kukauka.

“Mtu yeyote bila kujali kama ana ndoa anaweza kujikuta akichanganyikiwa na uzuri wako na pengine kutelekeza ndoa yake wallahi,” aliongeza na kuangua kicheko hafifu. Jacky alimtazama na kutabasamu pasipo kusema neno.

“Yaani wewe ni mzuri mpaka nahisi kuumwa, kwa jinsi nilivyo na wivu kama ungekuwa mke wangu nisingekubali kukuruhusu kuongea na mwanaume yeyote achilia mbali kuwasindikiza wakware kama sisi, nisingekubali hata iweje!” Kabwe alisema tena na kumfanya Liston aangue kicheko hafifu.

“Si utani! Hata mimi nisingekubali,” Liston aliunga mkono.

“Umeona eeh! Yaani mtoto amenoga mno utadhani ameteremshwa kutoka mbinguni, au pengine alikusudiwa kuumbwa malaika ila akaletwa duniani kimakosa!” Kabwe alisema kwa utani huku akigeuza shingo yake kumtazama Liston aliyekuwa ametulia kwenye siti ya nyuma.

“Hmm!” Jacky aliguna huku akiachia tabasamu laini. Hakusema neno lolote bali alibaki anawatupia jicho Kabwe na Liston huku akiendelea kuendessha gari kwa umakini mkubwa.

I wish ningekuwa Carlos na wewe ndiye mke wangu, japo hata kwa nusu saa tu,” Kabwe alisema huku akishusha pumzi.

“Mbona wazuri wapo wengi tu, shem, juhudi zako tu,” Jacky alisema huku akiendelea kutabasamu, na mara wakawa wamefika katika eneo la Sabasaba, Jacky aliliegesha gari lake karibu na kituo cha daladala cha Sabasaba, Kabwe na Liston wakashuka.

Jacky akaanza kuliondoa gari lake taratibu akielekea mbele nia yake ilikuwa kuchukua uelekeo wa kurudi Mtoni Kijichi baada ya kufika kwenye mzunguko wa barabara mbele kidogo ya viwanja vya Sabasaba, mara akaliona gari aina ya Toyota Lexus RX la rangi nyeusi likija nyuma yake kwa mwendo wa kasi.

Jacky alipunguza mwendo ili kulipisha lile gari lipite lakini lile gari lilipokuwa likimpita ghafla likapunguza kidogo mwendo huku magurudumu yake yakiserereka kwenye barabara ya lami na baadaye gari likaanza kwenda sambasamba na gari la Jacky. Ikabidi Jacky ageuze shingo yake kumtazama dereva wa lile gari kwa jicho la wasiwasi kidogo.

Bishop jamani endelea
 
Daaah... Ahsante sana Askofu..

Halafu naona kama siku hizi umepunguza ujazo..!? Au sababu ya utamu kunoga!??
Hapana, ni kwa sababu nilikuwa naumwa, na sasa tumeanza vikao vya kupitisha bajeti kabla haijapelekwa kwenye kamati za bunge na baadaye bungeni. Nikitulia nitazimwaga hadi mpatwe kizungumkuti... 😀😀😀
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom