Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Kizungumkuti! - 37

Na Bishop Hiluka

ILIPOISHIA

“Belinda, umeichanganya akili yangu kiasi kwamba najihisi kuwa nataka kuwa mwendawazimu kwa ajili yako…” Yusuf alisema huku akihema kwa nguvu na muda mfupi uliofuata Jacky na Yusuf walikuwa juu ya kitanda kikubwa wakiwa wamemezwa na ulimwengu mwingine kabisa, wa sinema ya mapenzi na mahaba mazito yenye kila aina ya kionjo cha kumtoa nyoka pangoni.

Kwa wakati ule hawakukumbuka kingine chochote isipokuwa kuivunja amri ya sita, huku mapenzi yakionekana kunoga kwa namna yake na miguno ya mahaba ikahanikiza kila mahali mle ndani.

Katika purukshani zile mito ya kujiegemeza pale kitandani iliangukia sakafuni, mmoja huku na mwingine kule lakini hakuna aliyejishughulisha kuiokota. Shuka lilikuwa limevurugwa ovyo wakati wazinzi wale walipokuwa wakivingirishana kwa sarakasi za aina yake pale kitandani.

Takribani muda wa saa moja ulipoyeyuka wote wawili walikuwa hoi huku kila mmoja akionekana kutosheka na mwenzake. Jacky alikuwa wa kwanza kuamka na kuketi kwenye ukingo wa kile kitanda huku akiwa mtupu kama alivyozaliwa.

Endelea...

Alijiegemeza ukutani na kutazama juu ya dari kwa muda mrefu kiasi cha kuyavuta macho ya Yusuf pale kitandani na yeye ageuke na kutazama kule juu ya dari.

What is it, my love?” (Kuna nini, mpenzi?) Yusuf alimuuliza Jacky huku akizifikicha chuchu zake, tukio ambao lilionekana kuamsha upya hisia za Jacky na hapo akageuka na kumtazama Yusuf pale kitandani huku akiachia tabasamu kabambe.

Nothing, my love, I was just thinking why we’d not stay here until tomorrow morning like the other day so that we’d enjoy our love more,” (Hakuna chochote mpenzi, nilikuwa nafikiria tu kwa nini tusingelala hapa hapa hadi kesho asubuhi kama siku ile ili tufurahie zaidi penzi letu) Jacky aliongea huku akikipapasa kifua cha Yusuf.

You know, darling, I still have things to keep in track at home, and I’d also want for something like that to happen, and not just for one day but for a whole week so that when we get out of here everyone is dog-tired. You probably told me in advance so that I’d prepare,” (Unajua bado nina mambo ya kuweka sawa nyumbani, nami natamani sana jambo kama hilo litokee, tena si kwa siku moja tu bali wiki nzima ili tukitoka kila mmoja yuko hoi. Pengine ungeniambia mapema ningeweza kujiandaa) Yusuf aliongea kwa utulivu na kutabasamu huku taratibu akizungusha mkono wake kushika kiuno cha Jacky.

What preparations?” (Kujiandaa kwa lipi?) Jacky aliuliza huku akimtazama Yusuf machoni.

How to explain to my wife so that she’d understand me, you know I don't want to get into another difficulties and now I have to be more smart,” (Namna ya kuongopa kwa mke wangu ili anielewe, unajua sitaki tena kuingia kwenye mtafaruku mwingine na sasa natakiwa kuwa mjanja zaidi) Yusuf aliongea kwa sauti tulivu ya kubembeleza huku akionekana kuzama kwenye tafakuri fupi.

Jacky aliachia tabasamu ambalo machoni kwa Yusuf lilikuwa tabasamu lenye bashasha na la upendo lakini nafsini mwa Jacky lilikuwa limeficha kitu ndani yake. Ki ukweli ilikuwa vigumu sana kumuelewa Jacky.

Kisha kilifuata kitambo kirefu cha ukimya, Yusuf alizama kwenye tafakari na wakati huohuo Jacky alibaki akimtazama kwa utulivu kisha akavunja ukimya.

Yes, where is my work?” (Enhe, kazi yangu iko wapi?)

It’s there, however, it was not an easy thing, my love,” (Ipo, hata hivyo, halikuwa jambo rahisi, mpenzi) Yusuf aliongea huku akimtazama Jacky usoni.

What do you mean? Did you do or did you not?” (Una maana gani? Kazi umeifanya au hujaifanya?) Jacky aliuliza huku sauti yake ikionekana kuingiwa na kitetemeshi.

Your work has been done, done very well,” (Kazi yako imefanyika, tena vizuri sana) Yusuf aliongea kwa utulivu huku taratibu akipeleka mkono wake na kukipapasa kiuno cha Jacky.

Where is it?” (Iko wapi?) Jacky aliuliza huku akionekana kuwa na shauku. Yusuf hakutia neno badala yake taratibu aligeuza kichwa chake kuutazama ule mkoba wa ngozi uliokuwa pembeni ya kile kitanda. Kitendo kile kikamfanya Jacky na yeye ageuke na kuutazama ule mkoba huku tabasamu jepesi likichanua usoni mwake.

Jacky aliutazama ule mkoba kwa hamasa kubwa kama uliokuwa na kito cha thamani ya juu sana, hata hivyo hakuupeleka mkono wake kuuchukua ule mkoba badala yake akawa ni kama aliyekuwa anataka kushuka pale kitandani ili aufuate. Lakini Yusuf aliwahi kumzuia kwa kumshika mkono huku uso wake ukiwa mbali na mzaha kisha akamuuliza Jacky.

So, what are the plans?” (Kwa hiyo, mipango ikoje?) Yusuf alimuuliza Jacky huku akimtazama moja kwa moja machoni.

Everything is on the line,” (Kila kitu kipo kwenye mstari) Jacky alijibu kwa mkato.

Yusuf alimtazama Jacky kwa udadisi kabla ya kumuuliza tena. “Who coordinates all the plans?” (Ni nani anayeratibu mipango yote?).

I am coordinating it myself, why are you worried with me?” (Ninairatibu mimi mwenyewe, kwani vipi una mashaka na mimi?) Jacky alijibu kwa kifupi na kuuliza huku akimkazia macho Yusuf.

Yusuf alitingisha kichwa chake huku akikunja uso wake, kisha aliinamisha kichwa chake akionekana kufikiria kidogo. Kilipita kitambo kifupi cha ukimya, kisha Yusuf aliinua uso wake kumtazama Jacky.

Are you sure that the whole plan will succeed and I will not be affected?” (Una hakika kuwa mpango mzima utafanikiwa na mimi sitashtukiwa?) Yusuf alimuuliza Jacky akiwa bado amekunja uso wake na kutengeneza matuta madogo madogo usoni.

I’ve never failed in this kind of plan, tomorrow I’ll tell you how the whole game how will be played,” (Sijawahi kushindwa katika mipango ya aina hii, kesho nitakueleza jinsi mchezo mzima utakavyochezwa) Jacky alisema huku akiangua kicheko hafifu cha mahaba, kisha aliinama na kumbusu Yusuf mdomoni halafu taratibu akajitoa pale kitandani na kuelekea bafuni.

Akiwa na hakika kuwa macho ya Yusuf yalikuwa nyuma yake yakisimsindikiza, Jacky alitembea kwa maringo kama twiga anayekatisha barabara ya mbugani huku mtikisiko wa umbo lake lisilositiriwa na nguo yoyote ukitengeneza taswira nzuri ya kuvutia machoni.

Yusuf alimtazama kwa hamasa huku akionekana kupendezwa na mjongeo ule hadi pale Jacky alipoingia bafuni. Dakika chache baadaye Jacky alirudi kutoka kule bafuni na kuchukua nguo zake, alianza kuzivaa huku akionekana mwenye haraka.

Yusuf akiwa pale kitandani alimtazama Jacky kwa utulivu huku akitabasamu kisha akajisogeza pembeni na kuupeleka mkono wake kuuchukua ule mkoba wa ngozi.

Jacky hakuonekana sana kumtilia maanani badala yake alivaa haraka haraka na alipomaliza alisogea kwenye kioo kikubwa cha kabati la mle chumbani na kuanza kujiweka sawa.

Alipomaliza kujiweka sawa na kuonekana kama Diana Mulenga kutoka Zambia, aligeuka kumtazama Yusuf huku akitabasamu. Yusuf aliufungua ule mkoba wake na kutoa bahasha moja ndogo ya khaki, kisha alinyoosha mkono wake kumpa Jacky.

Jacky aliichukua ile bahasha na kuichana kisha alitoa karatasi nyeupe iliyokuwa na maandishi.

Aliyatuliza macho yake kuiangalia kwa makini ile nakala ya hundi ya The Jacarandaha Group, na kadiri alivyozidi kuiangalia ile karatasi ndivyo tabasamu lake lilivyokuwa likichanua usoni. Muda wote huo Yusuf alikuwa bado ameketi pale kitandani akiwa kimya huku akimtazama Jacky kwa tabasamu.

Jacky aliporidhika aliirudisha ile karatasi kwenye bahasha na kuitia ile bahasha kwenye mkoba wake wa kike. Kisha aliinama akambusu Yusuf mdomoni kwa bashasha.

Itaendelea...

Cc Shunie the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, kuku mweus, Thad, hearly, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY HALELUYA MOSHI Clkey
 
Ahsante sana Bishop kwa kutuletea Kizungumkuti. Vipi unaendeleaje Kiafya?
 
Kizungumkuti! - 38

Na Bishop Hiluka

Jacky aliichukua ile bahasha na kuichana kisha alitoa karatasi nyeupe iliyokuwa na maandishi.

Aliyatuliza macho yake kuiangalia kwa makini ile nakala ya hundi ya The Jacarandaha Group, na kadiri alivyozidi kuiangalia ile karatasi ndivyo tabasamu lake lilivyokuwa likichanua usoni. Muda wote huo Yusuf alikuwa bado ameketi pale kitandani akiwa kimya huku akimtazama Jacky kwa tabasamu.

Jacky aliporidhika aliirudisha ile karatasi kwenye bahasha na kuitia ile bahasha kwenye mkoba wake wa kike. Kisha aliinama akambusu Yusuf mdomoni kwa bashasha.

Endelea...

Thank you, my love. See you next time,” (Asante mpenzi. Tutaonana wakati mwingine) Jacky alisema na kutoka nje bila kusubiri neno lolote kutoka kwa Yusuf.

* * * * *

Mvua kubwa iliyonyesha kwa saa zaidi ya tano usiku uliokuwa umetangulia, ikiwaudhi hawa na kuwafurahisha wale, ikiharibu hiki na kutengeneza kile, hatimaye ilianuka ghafla asubuhi ya siku iliyofuata na kuliachia jua lenye kupunga la asubuhi likichomoza kutoka ndani ya mawingu na kuifanya miale yake kuleta uhai mpya duniani.

Mvua hiyo ilikuwa imesababisha kijibaridi cha kukera asubuhi ile, hasa kwa jiji la Dar es Salaam lililozoeleka kwa joto kali lisilo la kawaida, watu mbalimbali walionekana mitaani na barabarani wakiwa wamevalia majaketi na wengine walibeba miavuli midogo midogo kama tahadhari.

Saa mbili na nusu za asubuhi ya siku ile, katika barabara ya Lumumba eneo la Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, gari dogo aina ya Toyota Corona la rangi nyeupe lililokuwa likitumika kama taksi-bubu lilisimama kando ya Benki ya Biashara.

Benki ya Biashara tawi la Barabara ya Lumumba lilikuwa kubwa na lenye wateja wengi, ambapo wengi wao walikuwa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa waliomiliki malori yaliyokwenda nje ya nchi na wamiliki wa majengo ya ghorofa na apartments katika maeneo ya Upanga, Kariakoo, Ilala na maeneo mengine yenye shughuli nyingi za kibiashara.

Jengo la Benki ya Biashara halikuwa na ulinzi wa kiwango cha usalama kamili, labda kwa sababu kulikuwa na kamera nyingi za ulinzi kila sehemu na tangu lifunguliwe hapajawahi kutokea tukio lolote la ujambazi. Au pengine ni kwa sababu waliwaamini sana walinzi wao kutoka Kampuni ya Ulinzi ya K5 Group.

Nje ya lile jengo kulikuwa na walinzi wawili vijana waliokuwa wamevalia sare maalumu za Kampuni ya Ulinzi ya K5 Group na walikuwa wameshika silaha.

“Usizime gari,” Jacky alimwambia dereva wa lile gari dogo aina ya Toyota Corona lililomleta huku akimtazama ndani ya miwani yake myeusi aliyovaa.

Yule dereva alikubali kwa kubetua kichwa pasipo kuhoji chochote, kwani pesa ilikuwa inaongea, alishalipwa shilingi elfu hamsini za kumleta Jacky pale benki na kumsubiria ili kumpeleka Mtoni Kijichi alikoacha gari lake. Dereva alibaki kwenye usukani akiwa mtulivu

Jacky alishuka kutoka kwenye lile gari na kuanza kupiga hatua kwa madaha kuelekea ndani ya ile benki huku akiuning’iniza begani mkoba wake wa ngozi aliokuja nao. Alikuwa amevaa suti maridadi ya kike ya rangi ya kijivu na miwani mikubwa myeusi iliyofunika macho yake.

Alipoingia ndani ya ile benki alikuta wateja wachache waliokuwa wamewahi asubuhi ile ya saa mbili na nusu, Jacky alijiunga katika mstari uliokuwa na watu wanne katika dirisha la Yusuf, macho yake yalikuwa yakimtazama Yusuf kwa makini, ambaye muda ule alikuwa kwenye kaunta yake, nyuma ya kompyuta akihudumia wateja waliofika muda ule.

Hata hivyo, Yusuf alikuwa akitiririkwa na jasho jingi ingawa mle ndani kulikuwa na viyoyozi vilivyotoa ubaridi mkali. Yusuf alimuona Jacky na kujikausha huku akiendelea kuwahudumia wale wateja waliokuwepo.

Ilipofika zamu yake, Jacky alichukua karatasi za benki na kuandika kiasi cha fedha shilingi laki tano alichotaka kukiingiza kwenye akaunti yake, kisha akatoa zile fedha kutoka kwenye mkoba wake na kuziweka kwenye kaunta mbele ya Yusuf huku akimnong’oneza kuwa kila kitu kingekwenda kama walivyopanga. Alipomaliza mchakato mzima wa kuweka fedha akatoka haraka akimwacha Yusuf bado anatiririkwa na jasho.

Alipotoka nje ya lile jengo la benki akatoa simu yake na kutuma ujumbe mfupi kwa Carlos, kisha aliingia kwenye ile taksi-bubu aliyokuja nayo na mara gari likaondoka huku likipishana na gari la bluu aina ya Ford Transit lililokuwa na vioo vya giza vilivyomzuia mtu kuona ndani. Gari lile lilifika na kuegeshwa mbele ya ile benki.

Lilikuwa ni gari lililotengenezwa maalumu kwa ajili ya kusafirisha fedha nyingi kutoka sehemu moja kwenda nyingine chini ya ulinzi madhubuti na lilikuwa na nembo ya NeoVision Security, ambayo ilikuwa kampuni ya ulinzi iliyolinda mali za The Jacarandah Group.

Lile gari ndilo lililokuwa likifika pale Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba mara kwa mara kwa ajili ya kuleta au kuja kuchukua fedha.

Hata hivyo, lile gari aina ya Ford Transit lililofika hapo benki siku hiyo halikuwa lile gari la siku zote la NeoVision Security lililokuwa likitumika kusafirisha fedha bali hili liliibwa na kubandikwa stika za NeoVision Security kwa kazi moja tu ya kubeba fedha kutoka Benki ya Biashara tawi la Barabara ya Lumumba hadi mahali palipokusudiwa, basi.

Kutokana na utaalamu uliotumika kuandaa stika zenye nembo za NeoVision Security na aina ya gari lenyewe isingekuwa rahisi hata kwa walinzi na wafanyakazi wa kampuni husika kung’amua kuwa lile halikuwa gari lao, kwani liliweza kufanana kwa kila kitu kwa zaidi ya asilimia tisini, hadi namba za gari.

Ndani ya lile gari kulikuwa na watu wanne. Carlos ndiye aliyekuwa dereva wa lile gari, na kwa kuwa alikuwa mwangalifu sana kutopenda kuhusishwa na tukio lolote la kihalifu, kama alivyo kwa sura yake ya kawaida, alikuwa amevaa glovu maalumu mikononi na kubandika sharubu nyembamba, sharafu zilizo na mchanganyiko wa mvi moja moja na msitu mdogo wa ndevu.

Pia alijitumbukiza ndani ya jaketi zito lililomuhifadhi vizuri na kuvaa miwani mikubwa myeusi huku akitulia kwenye usukani kama dereva mtiifu na mwoga kwa bosi wake aliyesubiri kupewa maelekezo.

Kwenye siti ya mbele ya abiria upande wa kushoto wa dereva, Kisu alikuwa ameketi akiwa mtulivu, alivaa suti maridadi na miwani mikubwa myeusi iliyoyaficha macho yake.

Kwenye siti za nyuma za lile gari waliketi Liston aliyekuwa ameshika bunduki aina ya rifle na Kabwe aliyekuwa ametulia. Wote wawili walikuwa wamevaa sare ya ulinzi wa kampuni ya NeoVision Security.

“Kazi kwenu,” Carlos alimwambia Kisu huku akigeuza shingo yake kuwatazama Kabwe na Liston kwa makini, na hapo Kisu aligeuka kuwatazama Kabwe na Liston na kuwaashiria kushuka kutoka kwenye lile gari.

Wote watatu walishuka na Kabwe alizunguka nyuma na kufungua mlango wa lile gari kisha alitoa begi kubwa la magurudumu na kusimama kikakamavu.

Kisu, Kabwe na Liston walianza kupiga hatua za kikakamavu kuelekea ndani ya lile jengo la Benki ya Biashara, Kisu alitangulia mbele huku akifuatwa nyuma na Liston aliyetembea kikakamavu na Kabwe aliyekuwa anaburuza begi kubwa lenye magurudumu.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 39

Mara walipoingia tu mle ndani ya ile benki walikuta msongamano wa watu uliokuwa umeongezeka kidogo muda huo na kuwa mkubwa. Watu walikuwa wamepanga foleni kwenye mistari minyoofu kufuata huduma kwenye kauta kadhaa zilizokuwa na wafanyakazi wa benki waliokuwa wamependeza katika sare zao za kazi.

Ilichukua sekunde tatu tu kwa Kisu kumtambua Yusuf ambaye alikuwa amesimama nyuma ya kaunta yake, kama kawaida akiwahudumia wateja waliokuwa wamefika pale benki. Kisu alimfahamu Yusuf kwa kuwa alikuwa ameoneshwa picha zake na Jacky zilizopigwa kwa siri bila Yusuf mwenyewe kufahamu.

Kisu alipoingia hakutaka kupanga foleni, bali waliuvuka mstari wa wateja wengine waliokuwa wamepanga foleni na moja kwa moja alikwenda hadi kwenye dirisha la kaunta alipokuwa amesimama Yusuf. Wateja waliokuwa wamepanga foleni ndani ya ile benki waligeuka kumtazama Kisu na kampani yake kwa mshangao.

Yusuf alimuona Kisu na kampani yake walivyokuwa wakija pale alipokuwa amesimama na kuhisi mwili wake ulikuwa ukiishiwa nguvu, akiwaangalia kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio isivyo kawaida.

Kisu alipofika pale kaunta alisimama katikati ya kaunta, huku akikingwa huku na huku na walinzi wake Liston na Kabwe. Kabwe alikuwa ameshikilia lile begi la magurudumu.

Kisu alitoa ile hundi na kuiweka kwenye meza ya ile kaunta mbele ya Yusuf kwa kujiamini kisha aliwatupia jicho wafanyakazi wengine wa ile benki na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

Wale wafanyakazi wengine katika kaunta zingine waligeuka kumtazama Kisu na kampani yake kwa makini huku dhahiri wakionekana kushindwa kuwaelewa. Hata hivyo, Kisu aliwasalimia kwa ishara ya mkono na wote wakaitikia kwa kubetua vichwa vyao huku wakiachia tabasamu la makaribisho na kisha waligeuka na kuendelea na hamsini zao.

Baadhi ya wale wafanyakazi walikuwa wakichambua taarifa za fedha kutoka kwenye nyaraka mbalimbali huku wakifanya uhakiki wa taarifa za fedha kwenye kompyuta zao. Wengine walikuwa wakisaini hundi mbalimbali, wakipokea na kutoa fedha taslimu kwa wateja waliokuwa wamefika pale benki kwa ajili ya kutoa au kuweka fedha zao.

Yusuf aliichukua ile hundi na kuitazama kwa makini, alionekana kushtushwa sana akiwa haamini macho yake. Alizitazama zile saini kwenye ile hundi na kushindwa kutofautisha saini halali na bandia.

Akiwa bado kwenye mshangao ule alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuwataka radhi wateja wengine ili awatoe kwanza kina Kisu. Alimtazama Kisu mara moja na kugonga mhuri kwenye ile hundi, kisha alitia saini yake.

Mambo yote yalikwenda chap chap kwani Yusuf alimaliza haraka kuingiza taarifa za kibenki kwenye kompyuta yake na bila kupoteza muda alikwenda ofisini kwa meneja wa tawi na baada ya taratibu zote kukamilika alitoka na kuwaeleza kina Kisu wamfuate kwenye chumba maalumu, ambacho waliingia na lile begi ili kwenda kuchukua fedha.

Iliwachukua takriban dakika ishirini kumaliza na baadaye walitoka mle chumbani, wakaanza kuzitupa hatua zao kikakamavu lakini kwa utulivu wakiliacha lile eneo la kaunta. Wateja waliokuwa mle ndani ya benki walibaki wameduwaa huku macho yao yakiwasindikiza kina Kisu hadi pale walipopotea kabisa mbele ya macho yao.

Walipotoka nje, haraka waliingia ndani ya lile gari lao lililokuwa nje ya jengo la benki likiunguruma taratibu kwa kuwa lilikuwa halijazimwa injini.

Carlos aliyekuwa nyuma ya usukani ndani ya lile gari aina ya Ford Transit aliliondoa lile gari kwa mwendo wa kasi mara tu watu wote walipoingia ndani ya gari na kufunga milango. Magurudumu ya gari yalisugua lami na hivyo cheche ndogo za moto zilitokea wakati gari lile lilipokuwa likiingia kwenye barabara ya Lumumba na kutokomea.

Mbele kidogo lilikata kona na kuingia mtaa wa Mkunguni kwa mwendo wa kasi, na wakati likiingia katika mtaa wa Mkunguni, gari jingine aina ya Range Rover SV Autobiography LWB la rangi nyeusi lililokuwa linatokea Barabara ya Morogoro lilifika katika lile jengo la ile Benki ya Biashara na kuegeshwa pale pale lilipotoka gari aina ya Ford Transit.

Ndani ya lile gari aina ya Range Rover SV Autobiography LWB lililofika pale benki kulikuwa na watu watatu, dereva mtu mzima aliyekuwa amevaa shati la draft la mikono mirefu, na kwenye siti ya mbele ya abiria alikuwa ameketi mwanamume mmoja mrefu chotara wa Kigiriki, Nassos Chatzopoulos na katika siti ya nyuma aliketi mwanamume mwingine wa Kiafrika aliyeitwa Cosmas Gama.

Nassos na Cosmas waliteremka kutoka kwenye lile gari na kuelekea ndani ya ile benki huku dereva akiliondoa lile gari na kwenda kuliegesha sehemu maalumu ya maegesho ya magari pale kwenye eneo la benki.

Nassos Chatzopoulos alikuwa mrefu na mweupe mwenye macho makali na mikono imara, mtu asiye na maneno mengi lakini alikuwa mcheshi. Umri wake wa miaka hamsini na ushee bado ulikuwa haujatosha kabisa kuzipokonya nguvu zake mwilini.

Alikuwa amevaa suruali ya rangi ya bluu ya jeans, buti ngumu za ngozi miguuni, fulana ya rangi nyeupe iliyokuwa na picha ya bendera ya Ugiriki kifuani na koti la rangi ya bluu.

Cosmas Gama alikuwa na kimo cha wastani, mnene na rangi ya ngozi yake ilikuwa maji ya kunde. Alikuwa amevaa suti ghali ya rangi ya kijivu, viatu vya ngozi vya rangi nyeusi na miwani.

Walipoingia ndani ya ile benki, Yusuf aliwaona na kushtuka sana. Alijikuta akigwaya sana huku koo lake likikauka ghafla na ubaridi wa hofu ulianza kumtambaa mwilini mwake. Yusuf alimwangalia Nassos aliyekuwa ameambatana na Gama kwa wasiwasi mkubwa na asijue ni nini kilichokuwa kimemleta pale siku hiyo.

Wakiwa hawana wasiwasi, Nassos na Gama walikwenda moja kwa moja hadi pale kaunta alipokuwa amesimama Yusuf kwa kuwa kulikuwa na watu wachache waliokuwa wamesimama kwenye lile dirisha tofauti na kaunta zingine zilizokuwa na foleni ndefu.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 40

Yusuf alikodoa macho yake kumtazama Nassos huku akili yake ikiwa imeanza kupoteza utulivu na wakati huo huo mapigo ya moyo wake yaliongezeka kasi mara dufu, hofu ilikuwa imemwingia na kumtambaa mwili mzima. Alihisi kama vile mkojo ulitaka kumtoka pasipo hiyari yake mwenyewe.

Good morning, Mr Akida?” (Habari za asubuhi, bwana Akida?) Nassos alimsalimia Yusuf kwa bashasha zote huku akichia tabasamu.

I’m fine, you’re welcome,” (Sijambo, karibuni) Yusuf aliitikia huku akijitahidi kuchangamka ingawa uso wake ulikuwa umesawajika sana.

Thank you very much… we got a new accountant who will replace Japhet Lutego who went to Sweden…” (Asante sana… tumempata mhasibu mpya ambaye atashika nafasi ya Japhet Lutego aliyekwenda Sweden…) Nassos alimwambia Yusuf katika hali ya kumtambulisha Cosmas Gama.

He is the one who will be coming here to deposit and withdraw money on behalf of the Jacarandah Group,” (Huyu ndiye atakayekuwa akifika hapa kuweka na kuchukua pesa kwa niaba ya kampuni ya Jacarandah Group) Nassos alisema na kuongeza, “His name is Cosmas Gama.” (Jina lake anaitwa Cosmas Gama).

Kwa utambulisho ule mfupi Yusuf alibetua kichwa chake kukubali huku akimtazama Cosmas Gama kwa tabasamu pana la kibiashsara.

I am glad to know you, Mr Gama, you’re mostly welcome, sir,” (Nafurahi kukufahamu, bwana Gama, karibu sana, bwana mkubwa) Yusuf alisema huku akijitahidi sana kuifanya sauti yake ionekane tulivu.

I am also grateful to know you, Mr…” (Nami nashukuru pia kukufahamu, bwana…) Cosmas Gama alisema na kusita kidogo huku akimtupia jicho Nassos.

“Akida… Yusuf Akida,” Nassos alisema na kuongeza, “Now, Yusuf, I want you to print a bank statement so that we know the amount of money available to the bank so far and we compare it with the calculation I have in the office. I remember recently I put three checks with a total amount of three billion and four hundred million shillings and then we took out only four hundred million shillings. Let me have that statement so that Gama knows where to start.”

(Sasa, Yusuf, nataka utuchapishie taarifa za kibenki ili tujue kiasi cha fedha kilichopo benki mpaka sasa na tulinganishe na hesabu niliyonayo ofisini. Nakumbuka majuzi niliweka hundi tatu zenye jumla ya shilingi bilioni tatu na milioni mia nne na baadaye tulitoa shilingi milioni mia nne tu. Hebu nipatie hesabu ya kiasi kilichopo ili Gama ajue anaanzia wapi).

Yusuf alishtuka sana na kunywea, alimtumbulia macho Nassos kwa wasiwasi huku mapigo ya moyo wake yakizidisha kasi yake. Alihisi kama vile anataka kuzimia kwa sababu ya shinikizo la juu la damu lililomkabili ghafla.

Nguvu zilianza kumuishia mwilini na alitamani kukaa. Mara kikazuka kitambo kifupi cha ukimya wa aina yake kilichomshtua Nassos, ambaye alimkodolea macho Yusuf kwa mshangao, hata hivyo, Yusuf alijishtukia na kuigeukia kompyuta yake kisha akaanza kutafuta taarifa za kampuni hiyo.

Alibofya kitufe fulani kwenye kibonyezo cha ile kompyuta na mara moja zilikuja taarifa za wateja mbalimbali wa ile benki, kisha alibonyeza herufi ‘J’, mara yakatokea majina kadhaa ya kampuni na wateja yaliyoanza na herufi ‘J’.

Hapo alitumia kipanya kushusha chini zile taarifa na hakuchukua hata sekunde tano akawa ameliona jina la The Jacarandah Group, kisha alibonyeza kwenye lile jina na hapo taarifa za kibenki kuhusu akaunti ya The Jacarandah Group zikaonekana kwenye kioo cha ile kompyuta.

Yusuf alizitazama zile taarifa kwa kitambo huku akionekana kusita sana, kisha alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku akimtupia jicho Nassos na kupiga moyo konde, akaamuru taarifa zile zichapwe kwenye karatasi kupitia mashine maalumu ya kuchapa kwa kubofya kitufe fulani katika kibonyezeo cha kompyuta yake.

Baada ya taarifa zile za kibenki kuhusu akaunti ya The Jacarandah Group kuchapwa kwenye karatasi, Yusuf alizichukua zile karatasi na kuzitupia jicho haraka haraka huku akimpa Salim, mapigo ya moyo wake yalizidi kwenda kasi isivyo kawaida, japo alikuwa akijipa ujasiri moyoni mwake kuwa kila kitu kitakwenda sawa.

Nassos alizipokeaa zile karatasi na kuzitazama kwa makini, kisha pale pale alitoa karatasi alizokuwa nazo na kuanza kulinganisha hesabu zake na zile zilizokuwa kwenye zile karatasi alizopewa na Yusuf.

Muda wote Yusuf alikuwa kimya akimtumbulia macho Nassos huku mazingira ya pale kaunta yakiwa ya utulivu mno kwa dakika nzima. Baada ya kuzilinganisha zile hesabu na kugundua kasoro, Nassos alishtuka sana na kumtazama Yusuf kwa umakini mkubwa.

I don’t understand at all!” (Sielewi kabisa!) Nassos alimwambia Yusuf huku akimkazia macho na kumuonesha zile karatasi alizompa.

Yusuf alimkodolea macho Nassos akiwa hajui la kusema, hofu ilikuwa imemtambaa mwili mzima na muda ule akili yake ilikuwa haifanyi kazi yake sawasawa, alihisi ubaridi mwepesi ukiipiga ngozi yake na nywele zake zikimsimama.

I don't understand! Your statement indicates a deficit of one billion and three hundred million, how?” (Sielewi kabisa! Hizi hesabu zenu zinaonesha upungufu wa shilingi bilioni moja na milioni mia tatu, kwa vipi?) Nassos aling’aka huku akimrushia Yusuf zile karatasi alizompa. Tayari alikwisha kuwa mwekundu kwa ghadhabu iliyoanza kumpanda.

Yusuf alikuwa anatetemeka huku akimwangalia Nassos kwa woga kana kwamba alikuwa amemuona malaika mtoa roho. Alihisi donge fulani hivi la fadhaa likizidi kumkaba na kusimama kwenye koo lake kwa muda mrefu huku joto kali likianza kuibuka ndani yake.

Our calculations have no defects, sir, perhaps you have forgotten that today you have taken some money,” (Hesabu zetu hazina kasoro yoyote ile, bwana mkubwa, labda ninyi mmesahau kuwa leo mmechukua fedha zingine) Yusuf alisema kwa sauti yenye kitetemeshi huku akijitahidi kuifanya ionekane ya kawaida.

What money? No one from our office came here today or yesterday to put or take money. What do you want to tell me?” (Fedha gani? Hakuja mtu yeyote kutoka ofisini kwetu leo hii wala jana kuweka ama kuchukua fedha. Unataka kuniambia nini?) Nassos alisema kwa hasira huku akirusha mikono yake hewani. Ni wazi Nassos alikuwa ameghadhabika sana na sauti yake ilikuwa kali zaidi na iliyojaa ghadhabu.

Yusuf alianza kulihisi joto kali likimtambaa mwilini mwake na kumfanya ahangaike zaidi. Kila alilotaka kusema alihisi kama lisingeweza kumwepusha na ghadhabu ya yule Mgiriki. Nassos aliendelea kuongea, lakini safari hii sauti yake ilikuwa ni kama alikuwa anataka kupiga kelele.

Prove to me, who came here today from our company to take money?” (Nithibitishie, ni nani aliyekuja leo kutoka kwenye kampuni yetu kuchukua pesa?) Nassos alimuuliza Yusuf kwa ghadhabu huku akiwa amemkazia macho yaliyokuwa yakiwaka kwa ghadhabu.

Muda ule wote wafanyakazi wengine wa ile benki pamoja na wateja walibaki kimya wakiwatazama kwa mshangao Nassos na Yusuf waliokuwa wakilumbana, ni dhahiri walionekana kushindwa kuelewa kilichokuwa kinaendelea pale.

Three people came here, and two were wearing your company’s NeoVision Security uniform. And the checks they came with is here,” (Walikuja hapa watu watatu, tena wawili walikuwa wamevaa sare za kampuni yenu ya NeoVision Security. Na hundi waliyokuja nayo ni hii hapa) Yusuf alisema kwa kujitetea huku akimwonesha Nassos ile hundi.

Mambo yamekuwa mambo, Je, nini kitaendelea? Yusuf atapona na ghadhabu ya Mgiriki mwenye kampuni ya The Jacarandah Group? Endelea kufuatilia simulizi hii, ama kweeli ni KIZUNGUMKUTI...
 
Delila (Jack) katika ubora wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi ipo...ngoja tutege alarm, tuone kifuatacho.

Asante sana Bishop.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kizungumkuti! - 39

Na Bishop Hiluka

“Kazi kwenu,” Carlos alimwambia Kisu huku akigeuza shingo yake kuwatazama Kabwe na Liston kwa makini, na hapo Kisu aligeuka kuwatazama Kabwe na Liston na kuwaashiria kushuka kutoka kwenye lile gari.

Wote watatu walishuka na Kabwe alizunguka nyuma na kufungua mlango wa lile gari kisha alitoa begi kubwa la magurudumu na kusimama kikakamavu.

Kisu, Kabwe na Liston walianza kupiga hatua za kikakamavu kuelekea ndani ya lile jengo la Benki ya Biashara, Kisu alitangulia mbele huku akifuatwa nyuma na Liston aliyetembea kikakamavu na Kabwe aliyekuwa anaburuza begi kubwa lenye magurudumu.

Endelea...

Mara walipoingia tu mle ndani ya ile benki walikuta msongamano wa watu uliokuwa umeongezeka kidogo muda huo na kuwa mkubwa. Watu walikuwa wamepanga foleni kwenye mistari minyoofu kufuata huduma kwenye kauta kadhaa zilizokuwa na wafanyakazi wa benki waliokuwa wamependeza katika sare zao za kazi.

Ilichukua sekunde tatu tu kwa Kisu kumtambua Yusuf ambaye alikuwa amesimama nyuma ya kaunta yake, kama kawaida akiwahudumia wateja waliokuwa wamefika pale benki. Kisu alimfahamu Yusuf kwa kuwa alikuwa ameoneshwa picha zake na Jacky zilizopigwa kwa siri bila Yusuf mwenyewe kufahamu.

Kisu alipoingia hakutaka kupanga foleni, bali waliuvuka mstari wa wateja wengine waliokuwa wamepanga foleni na moja kwa moja alikwenda hadi kwenye dirisha la kaunta alipokuwa amesimama Yusuf. Wateja waliokuwa wamepanga foleni ndani ya ile benki waligeuka kumtazama Kisu na kampani yake kwa mshangao.

Yusuf alimuona Kisu na kampani yake walivyokuwa wakija pale alipokuwa amesimama na kuhisi mwili wake ulikuwa ukiishiwa nguvu, akiwaangalia kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio isivyo kawaida.

Kisu alipofika pale kaunta alisimama katikati ya kaunta, huku akikingwa huku na huku na walinzi wake Liston na Kabwe. Kabwe alikuwa ameshikilia lile begi la magurudumu.

Kisu alitoa ile hundi na kuiweka kwenye meza ya ile kaunta mbele ya Yusuf kwa kujiamini kisha aliwatupia jicho wafanyakazi wengine wa ile benki na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

Wale wafanyakazi wengine katika kaunta zingine waligeuka kumtazama Kisu na kampani yake kwa makini huku dhahiri wakionekana kushindwa kuwaelewa. Hata hivyo, Kisu aliwasalimia kwa ishara ya mkono na wote wakaitikia kwa kubetua vichwa vyao huku wakiachia tabasamu la makaribisho na kisha waligeuka na kuendelea na hamsini zao.

Baadhi ya wale wafanyakazi walikuwa wakichambua taarifa za fedha kutoka kwenye nyaraka mbalimbali huku wakifanya uhakiki wa taarifa za fedha kwenye kompyuta zao. Wengine walikuwa wakisaini hundi mbalimbali, wakipokea na kutoa fedha taslimu kwa wateja waliokuwa wamefika pale benki kwa ajili ya kutoa au kuweka fedha zao.

Yusuf aliichukua ile hundi na kuitazama kwa makini, alionekana kushtushwa sana akiwa haamini macho yake. Alizitazama zile saini kwenye ile hundi na kushindwa kutofautisha saini halali na bandia.

Akiwa bado kwenye mshangao ule alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuwataka radhi wateja wengine ili awatoe kwanza kina Kisu. Alimtazama Kisu mara moja na kugonga mhuri kwenye ile hundi, kisha alitia saini yake.

Mambo yote yalikwenda chap chap kwani Yusuf alimaliza haraka kuingiza taarifa za kibenki kwenye kompyuta yake na bila kupoteza muda alikwenda ofisini kwa meneja wa tawi na baada ya taratibu zote kukamilika alitoka na kuwaeleza kina Kisu wamfuate kwenye chumba maalumu, ambacho waliingia na lile begi ili kwenda kuchukua fedha.

Iliwachukua takriban dakika ishirini kumaliza na baadaye walitoka mle chumbani, wakaanza kuzitupa hatua zao kikakamavu lakini kwa utulivu wakiliacha lile eneo la kaunta. Wateja waliokuwa mle ndani ya benki walibaki wameduwaa huku macho yao yakiwasindikiza kina Kisu hadi pale walipopotea kabisa mbele ya macho yao.

Walipotoka nje, haraka waliingia ndani ya lile gari lao lililokuwa nje ya jengo la benki likiunguruma taratibu kwa kuwa lilikuwa halijazimwa injini.

Carlos aliyekuwa nyuma ya usukani ndani ya lile gari aina ya Ford Transit aliliondoa lile gari kwa mwendo wa kasi mara tu watu wote walipoingia ndani ya gari na kufunga milango. Magurudumu ya gari yalisugua lami na hivyo cheche ndogo za moto zilitokea wakati gari lile lilipokuwa likiingia kwenye barabara ya Lumumba na kutokomea.

Mbele kidogo lilikata kona na kuingia mtaa wa Mkunguni kwa mwendo wa kasi, na wakati likiingia katika mtaa wa Mkunguni, gari jingine aina ya Range Rover SV Autobiography LWB la rangi nyeusi lililokuwa linatokea Barabara ya Morogoro lilifika katika lile jengo la ile Benki ya Biashara na kuegeshwa pale pale lilipotoka gari aina ya Ford Transit.

Ndani ya lile gari aina ya Range Rover SV Autobiography LWB lililofika pale benki kulikuwa na watu watatu, dereva mtu mzima aliyekuwa amevaa shati la draft la mikono mirefu, na kwenye siti ya mbele ya abiria alikuwa ameketi mwanamume mmoja mrefu chotara wa Kigiriki, Nassos Chatzopoulos na katika siti ya nyuma aliketi mwanamume mwingine wa Kiafrika aliyeitwa Cosmas Gama.

Nassos na Cosmas waliteremka kutoka kwenye lile gari na kuelekea ndani ya ile benki huku dereva akiliondoa lile gari na kwenda kuliegesha sehemu maalumu ya maegesho ya magari pale kwenye eneo la benki.

Nassos Chatzopoulos alikuwa mrefu na mweupe mwenye macho makali na mikono imara, mtu asiye na maneno mengi lakini alikuwa mcheshi. Umri wake wa miaka hamsini na ushee bado ulikuwa haujatosha kabisa kuzipokonya nguvu zake mwilini.

Alikuwa amevaa suruali ya rangi ya bluu ya jeans, buti ngumu za ngozi miguuni, fulana ya rangi nyeupe iliyokuwa na picha ya bendera ya Ugiriki kifuani na koti la rangi ya bluu.

Cosmas Gama alikuwa na kimo cha wastani, mnene na rangi ya ngozi yake ilikuwa maji ya kunde. Alikuwa amevaa suti ghali ya rangi ya kijivu, viatu vya ngozi vya rangi nyeusi na miwani.

Walipoingia ndani ya ile benki, Yusuf aliwaona na kushtuka sana. Alijikuta akigwaya sana huku koo lake likikauka ghafla na ubaridi wa hofu ulianza kumtambaa mwilini mwake. Yusuf alimwangalia Nassos aliyekuwa ameambatana na Gama kwa wasiwasi mkubwa na asijue ni nini kilichokuwa kimemleta pale siku hiyo.

Wakiwa hawana wasiwasi, Nassos na Gama walikwenda moja kwa moja hadi pale kaunta alipokuwa amesimama Yusuf kwa kuwa kulikuwa na watu wachache waliokuwa wamesimama kwenye lile dirisha tofauti na kaunta zingine zilizokuwa na foleni ndefu.

Itaendelea...
Yusuph muoga kama mm yaani huyu uoga wake utamletea matatizo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom