Kizungumkuti! - 34
Na Bishop Hiluka
ILIPOISHIA
“Jana au leo kabla hapajapambazuka?” Yusuf aliuliza mkewe huku akivuta picha, ingekuwaje endapo angevamiwa na vibaka!
“Kweli, ni leo,” Mama Jasmine alijisahihisha na kuendelea, “Siku nyingine rudia kususa halafu ulale tena hapo nje utaipata habari yake.”
Mama Jasmine alisema na kuanza kusogea kwenye meza ndogo iliyokuwa pembeni ya kitanda akitaka kuchukua kitambaa chake cha kufunika nywele, lakini kabla hajakichukua, Yusuf alimvuta na kumtupia kitandani, naye akajitupa juu yake. Mama Jasmine alilala chali.
Endelea...
Kitendo kile kilimwamsha Jasmine, aliinuka akakaa kitako pale kitandani huku akiwatazama wazazi wake kwa macho ya udadisi. Mama Jasmine alimsukuma Yusuf na kuinuka haraka, akachukua mswaki wa Jasmine na kuutia dawa, kisha akamteremsha Jasmine kutoka pale kitandani.
“Haya, twende ukapige mswaki, mtoto mzuri,” Mama Jasmine alisema huku akimpiga ukope Yusuf, akatoka na Jasmine hadi uwani, akachukua kikombe na kuchota maji yaliyokuwa ndani ya jaba na kumpa.
“Haya, kaa hapa upige mswaki vizuri na ukimaliza lazima nikukague, usiondoke hadi nije, sawa?” Mama Jasmine alimwambia Jasmine huku akianza kupiga hatua kuingia ndani, alipofika mlangoni aligeuka kumtupia jicho na kumuona akianza kujishughulisha na meno yake.
Jasmine alikuwa amechuchumaa kwenye ukingo wa ukuta wa ule ua akajitahidi kuchokonoa mswaki wake huku na huko kinywani kwake, kwani alijua baada ya kumaliza kupiga mswaki kulikuwa na ukaguzi.
Mama Jasmine aliingia chumbani ambako alimkuta Yusuf akiwa bado anamsubiri kwa hamu, alikwenda kuketi kitandani kando ya Yusuf huku akimtazama kwa aibu na hapo Yusuf akamdaka na kumsukumia kitandani. Mama Jasmine alijiangusha chali huku akiitandaza mikono kama aliyekuwa akiwambwa msalabani.
Yusuf alikuja juu yake huku mikono yake akiitandaza kuishikilia mikono ya mkewe na nyuso zao zikatazamana kwa ukaribu. Mama Jasmine alifumba macho yake kuyakwepa macho ya Yusuf, na taratibu wakajikuta wakianza kuhamia katika dunia nyingine kabisa, dunia ya mahaba… kuanzia hapo hapakuwa na kitu kingine zaidi ya kupeana mahaba mazito mazito.
Walipomaliza Yusuf alijifunga taulo kisha wote walielekea bafuni kwa ajili ya kuoga. Walipotoka nje Mama Jasmine alimkuta Jasmine akiwa bado amekaa pale pale upenuni mwa ua wa ile nyumba alipomwacha akisubiri kukaguliwa.
“Umemaliza?” Mama Jasmine alimuuliza mwanawe huku akimkazia macho. Jasmine alikubali kwa kichwa huku akikenyua meno yake kumuonesha mama yake.
“Haya nenda kanisubiri ndani kwenye makochi, nikitoka kuoga nakuja kukukagua kama umesugua vizuri,” Mama Jasmine alimwambia Jasmine huku akichota maji kwenye lile jaba na kuyajaza kwenye ndoo ya kuogea, kisha akayapeleka bafuni ambako mumewe Yusuf alikuwa amesimama anasubiri. Mama Jasmine alioga haraka haraka na kutoka akimwacha Yusuf anaendelea kuoga taratibu, yeye alikuwa akimuwahi Jasmine.
Baada ya kumaliza kuoga Yusuf aliingia ndani na kuzikuta nguo zake zikiwa tayari zimenyooshwa vizuri na kuwekwa sehemu maalumu tayari kwa kuvaliwa. Alijiandaa na kuvaa huku moyoni akiwa amefurahi sana, hasa baada ya kuonekana kuwa mkewe alikuwa amemsamehe kabisa.
Yusuf alipomaliza zoezi lile la kujiandaa alimuaga mkewe kwa kumbusu kwenye paji la uso, kisha akambusu mwanawe Jasmine na kutoka, akaelekea kituo cha daladala cha Bungoni huku akipiga mluzi wa ushindi.
* * * * *
Saa ya ukutani sebuleni nyumbani kwa Carlos na Jacky ilisomeka kuwa saa sita na robo mchana. Katika ile sebuleni kulikuwa na wanaume wanne waliokuwa wameketi wakijadiliana hili na lile huku maongezoi yao yakisindikizwa na pombe kali.
Juu ya meza kulionekana chupa kadhaa kubwa pombe aina ya
whisky,
Grant na mvinyo mwekundu wa Kifaransa wa
Navette de Marseille na bilauri ndefu nne.
Kwenye kochi dogo la sofa Carlos alikuwa ameketi akizungumza na vijana wawili waliokuwa wameketi kwenye kochi kubwa lililokuwa mkabala na lile aliloketi.
Vijana hao ni Kabwe, ambacho kilikuwa kifupi cha majina ya Kassim Bwenzi. Huyu alikuwa na kimo cha wastani na mweusi kama Mjaluo akiwa na misuli imara ya mikononi iliyotuna kikamilifu kwa namna kuonesha kuwa alikuwa na kawaida ya kufanya mazoezi ya nguvu yasiyokuwa na kikomo.
Kabwe alikuwa amevaa fulana nyeupe iliyombana na kulionesha vyema umbo lake lililojengeka kwa misuli na alivaa suruali ya jeans ya rangi ya bluu na buti ngumu aina ya
‘safari boot’ za rangi ya hudhurungi.
Kichwani alivaa kofia aina ya kapelo ya rangi nyekundu iliyokuwa imetuama vizuri kwenye upara wake uliokuwa unawaka na usiokuwa na unywele hata mmoja.
Japokuwa alikuwa mzungumzaji mzuri na mwenye kujua mambo mengi lakini Kabwe hakupata nafasi ya kupata elimu bora kutokana na hali ya ufukara uliopindukia wa famili yake, alilelewa na mama pekee na alikuwa na ndugu zake wengine watano, huku baba yao akiwatelekeza na kwenda kusikojulikana wakati Kabwe akiwa na miaka saba tu.
Kuanzia hapo walijikuta wakiishi maisha ya ufukara uliopindukia, na hata hayo madarasa manne ya shule ya msingi ambayo Kabwe alisoma aliyapata kwa taabu sana.
Wakati akisoma ilimlazimu Kabwe na ndugu zake kwenda shuleni wakiwa na njaa, wakashinda huko na njaa na waliporudi nyumbani walilazimika kumsaidia mama yao aliyekuwa mlemavu kutafuta chakula kwa kufanya kazi za vibarua, ndipo Kabwe akajionea upuuzi kuendelea na shule. Akaachana na shule, akawa anarandaranda mitaani na watoto wengine wa mtaani.
Hapo ndipo alipoanza kujifunza uporaji madukani na mitaani ili kujipatia riziki, na ndipo pia alipoanza kujenga mzuka wa kujisikia kuua. Alianza polepole kwa kunyonga shingo za kuku na kuwatazama wakipaparika kwa maumivu makali hadi kufa. Kisha akahamia kwenye kuvizia paka akijifanya Manyaunyau, aliwakamata na kuwatenganisha miili yao na vichwa. Ukatili huu uliuburudisha sana moyo wa Kabwe.
Alipofikisha umri wa miaka ishirini Kabwe alikwisha toa roho tatu za watu waliokuwa wameingia katika anga zake.
Kijana mwingine aliyekaa pamoja na Kabwe aliitwa Liston George, huyu alikuwa mrefu na mweupe kiasi, mwenye umbo kakamavu kama wachezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani. Alikuwa amevalia shati jeupe la mistari ya rangi ya bluu la mikono mirefu, suruali ya jeans ya rangi nyeusi na raba nyeusi.
Macho yake yalikuwa makubwa na mekundu yenye uchovu lakini yaliyokuwa na kila dalili ya kuonya na muda wote alikuwa akimtazama Carlos huku tabasamu jepesi likijitokeza taratibu usoni mwake.
Itaendelea...
Cc
Shunie the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater,
Bigjahman moneytalk marybaby,
nipo2,
ram,
kisukari,
Smart911,
Madame S,
carbamazepine,
Astelia,
culture gal ,
Prisoner of hope,
kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes,
Kudo, swahiba92,
ludist,
Toyota escudo,
Clkey,
macson3,
Thad,
boga la kiangazi,
macson3,
Smart911,
Richard irakunda,
skfull,
popie,
Krizy Beat,
hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY HALELUYA MOSHI Clkey