Stori gani uliwahi kusimuliwa kuhusu mchezaji wa mpira kumbe 'kamba'?

Marehemu mambosasa kutolewa/kutishiwa jambia ili aachie goli kwenye mechi ya nusu fainali klabu bingwa afrika kati ya simba na mehlal kubla nchini misri mwaka 1974 (hii sijawahi kuamini mpaka kesho,, ni kweli hiyo mechi ilichezwa, lakini hili tukio hili la kutolewa jambia sina uhakika nalo. ) 🤣

Pele kukutana na golikipa anadaka sana penati, akalegeza kamba za viatu, wakati anaenda kupiga, akafanya kama anapiga kiatu kikatoka kisha akapiga mpira, kipa akadaka kiatu na mpira kujaa wavuni. 😂
 
Timu ya taifa ya China ilibadilisha kikosi chote mpaka kipa wakati wa mapumziko

Golikipa wa Colombia anadaka mpira Kwa miguu

Robto Kalosi mashuti yake mabeki wanakwepa sababu makali Sana

Fegurson Bigi Jii yake huwa haiishi utamu ni maalum tu Kwa Ajili yake anatengenezewa yeye tu

Hii ya goalkeeper wa Colombia ina ukweli kidogo, huyo kipa alikuja na staili inaitwa butterfly katika kupangua mashuti.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Timu ya taifa ya China ilibadilisha kikosi chote mpaka kipa wakati wa mapumziko

Golikipa wa Colombia anadaka mpira Kwa miguu

Robto Kalosi mashuti yake mabeki wanakwepa sababu makali Sana

Fegurson Bigi Jii yake huwa haiishi utamu ni maalum tu Kwa Ajili yake anatengenezewa yeye tu

🤣🤣🤣🤣🤣
Hili la China kweli lilisemwa sana in 80s kuwa wanabadilisha wachezaji wote half to time.
 
Kulikuwa na story mchezaji fulani wa brasil anapiga penalt usawa wa kipa na lazima kipa akwepe maama shuti ni kali sana asipokwepa anaingia nao wavuni.... Nimemsahau jina ila ni no 6
Hahaha! atakuwa Roberto Carlos!

Sema alikuwa na mashuti makali kweli sio mchezo.
 
Nadhani unamaanisha roberto carlos. huyu jamaa wakiwa wanacheza nadhani kombe la dunia Brazil vs ujerumani ilipatikana faulo nje ya kumi na nane golikipa akiwa oliver kahn.

Wakati akina rivaldo wamejipanga na mabeki wa ujerumani akawa anawaonyesha ishara ya kusogea kwa mkono sasa akina rivaldo wakadhani anawapanga wakawa wanasogea tu.

Ikabidi anyoshe mkono juu ishara ya kuomba refa amvumilie akaenda akamnong'oneza kitu rivaldo nae akamwambia cafu wakatoka mstarinj baada ya kutoka akawaambia wachezaji wa ujerumanj kwa ishara wasogee kuziba huo mwanya.

Jamaa alirudi nyuma kama hatua kumi alipiga shuti usawa wa nyasj za uwanja wakati anapiga wachezaji wa ujerumani wakaruka mpira ukapita chinj ya miguu yao ukamlenga golikipa oliver kahn.

Na akafung sasa muulize oliver kahn mpira ulipitia wapi na ulimlenga.
Ila nakumbuka kama alipiga pembeni sio kama waliuruka mpira Bali ulizunguka ndo likaenda kua Goli moja matata Sana ..
By the way mi shabiki wa kudumu wa Brazil lakini nilikua nampenda Sana Oliver khan kwangu anabaki kua kipa Bora wa muda wote akifatiwa na Tony silver
 
Timu ya taifa ya India waliingia kombe la dunia wakagoma kucheza huku wamevaa viatu wakatolewa
China ilipigwa marufuku kucheza kombe la dunia kwa sababu baada ya half time walibadili wachezaji wote 11. Kisa na maana ni vile wanafanana
 
Roberto Carlos alifungiwa kutumia mguu wake wa kulia kwasababu alivyokua mtoto alibiga shuti kipa aliedaka akafa hapohapo
 
Kulikuwa na story mchezaji fulani wa brasil anapiga penalt usawa wa kipa na lazima kipa akwepe maama shuti ni kali sana asipokwepa anaingia nao wavuni.... Nimemsahau jina ila ni no 6
Ni kweli siyo uongo mashuti ya Carlos walikuaga wanayakwepa angalia hata youtube utaona, uongo ni ile kuwa Carlos aliwahi kupiga shuti kipa aliedaka akafa
 
Ni kweli siyo uongo mashuti ya Carlos walikuaga wanayakwepa angalia hata youtube utaona, uongo ni ile kuwa Carlos aliwahi kupiga shuti kipa aliedaka akafa
Hatari sana! Brasil ilikuaga ya moto miaka ya 1998 sijui siku hizi wana nini watu laini laini kama Neymer
 
Hatari sana! Brasil ilikuaga ya moto miaka ya 1998 sijui siku hizi wana nini watu laini laini kama Neymer
Noma sana ilikua Brazil ya wazee wa kazi Carlos akipiga free kick wanakwepa kanzia mabeki hadi kipa wao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom